Zaburi 16:10 “Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu, wala hutamtoa Mtakatifu wako aone Uharibifu”
Zaburi ya 16 ni moja ya Zaburi
ambazo mtunzi wake Ni Daudi, Katika zaburi hii kuna Ufunuo mkubwa sana ambao ni
Matokeo ya kumuamini Mungu tuwapo Duniani, Mwandishi anaonekana Kumtegemea
Mungu katika maisha yake, Kama mnitakavyoelezea Baadaye kwa kina.
Kabla sijazama ndani sana katika
kuchambua aya hii, ni Muhimu kufahamu kuwa Mtume Petro aliutumia Mstari huu
kuzungumzia habari za Kufufuka kwa Masihi Matendo
2:25-31 “25. Maana Daudi ataja habari zake, Nalimwona Bwana mbele yangu siku zote,
Kwa kuwa yuko upande wa mkono wangu wa kuume, nisitikisike. 26. Kwa hiyo moyo
wangu ukapendezewa, ulimi wangu ukafurahi; Tena mwili wangu nao utakaa katika
matumaini. 27. Kwa maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu; Wala hutamtoa
Mtakatifu wako aone uharibifu. 28. Umenijuvisha njia za uzima; Utanijaza furaha
kwa uso wako. 29. Waume, ndugu zangu,
mniwie radhi, niseme kwa ujasiri mbele yenu habari za baba yetu mkuu, Daudi, ya
kuwa alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hata leo. 30. Basi kwa kuwa
ni nabii, akijua ya kuwa Mungu amemwapia kwa kiapo, ya kwamba katika uzao wa
viuno vyake atamketisha mmoja katika kiti chake cha enzi; 31. yeye mwenyewe akitangulia
kuyaona haya, alitaja habari za kufufuka kwake Kristo, ya kwamba roho yake
haikuachwa kuzimu, wala mwili wake haukuona uharibifu.” Paulo Mtume pia aliutumia mstari huu
kumuhusu Masihi yaani Bwana wetu Yesu na Kufufuka Kwake Matendo 13:34-37 “34. Tena ya kuwa alimfufua katika wafu, asipate kurudia
uharibifu, amenena hivi, Nitawapa ninyi mambo matakatifu ya Daudi yaliyo amini.
35. Kwa hiyo anena na pengine, Hutamwachia Mtakatifu wako kuona uharibifu, 36.
Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake,
alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu. 37. Bali huyu
aliyefufuliwa na Mungu hakuona uharibifu.”
Ni wazi kabisa Zaburi hii ilikuwa inahusu kufufuka kwa
Yesu Kristo kwa sababu kuna maneno makuu mawili yanayotumika katika Mstari huu
wa Msingi “Maana hutakuachia KUZIMU nafsi yangu, wala hutamtoa
Mtakatifu wako aone UHARIBIFU”
Neno Kuzimu katika Lugha ya kiibrania ni Sheol na kiyunani ni Hades ambayo yalimaanisha Kaburini au
sehemu Fulani katika ulimwengu wa waliokufa, Na neno Uharibifu lilimaanisha KUOZA.
Pichani ni Mwili wa Mtakatifu John Neumann, aliyefariki Dunia Mwaka 1860 huko Philadelphia akiwa na umri wa mika 48. Mwili wake baadaye uligunduliwa kuwa haukuharibika, Alikuwa ni Askofu wa Kwanza wa Marekani kutangazwa kuwa Mtakatifu, mwili wake umehifadhiwa katika jeneza la kioo katika madhabahu isiyofunikwa Katika kanisa la Mtakatifu Petro Mtume huko 5th and Girard Streets in the Northern Liberties section of Philadelphia.
Yesu Kristo Bwana wetu
aliishi maisha Matakatifu bila ya dhambi, aliposulubiwa aliwekwa Kaburini na
kabla hajaoza Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, kwa hoiyo lugha hutakuachia
kuzimu nafsi yangu ina maana hutaiacha nafsi yangu Kaburini, na neno wala
Mtakatifu wako kuona uharibifu maana yake wala mtakatifu wako Kuoza
Yesu alifufuka kutoka
kwa wafu Yu hai, Paulo mtume na Petro walitafasiri vema kabisa kwa sababu jambo
hili lilizungumzwa na Daudinkama Nabii, lakini Daudi alipokufa alizikwa na
hakutoka Kaburini na mwili wake ulioza kama ilivyokuwa kwa manabii wengine kwa
hiyo ilikuwa ni sahii kabisa kwa Petro na Paulo kuona unabii huu unamhusu Yesu
Kristo
Hata hivyo Pamoja na
hayo Leo nataka twende mbele zaidi, kwa kulitumia andiko hili kwetu sisi Daudi
hata kama alikuwa ni nabii na alizungumza kinabii Kuhusu Yesu Kristo lakini zaburi nzima inatufunulia Imani na
ujasiri aliokuwa nao Daudi na ambao unaweza kumuhusu kila mmoja wetu.
Zaburi 16: 1-2 “1. Mungu, unihifadhi mimi, Kwa maana nakukimbilia Wewe. 2.
Nimemwambia Bwana, Ndiwe Bwana wangu; Sina wema ila utokao kwako.”
Yalikuwa
ni maombi ya Daudi yakiomba Hifadhi kwa Mungu kwa sababu amemkimbilia Yeye,
Daudi alimfanya Mungu kuwa ndiye Bwana hata pamoja na kujitambua kuwa hakuwa na
wema wa kutosha lakini alijikinga kwa Mwenyezi Mungu na kumtegemea yeye,
inawezekana ulikuwa wakati mgumu na wakati wa mapito mbalimbali lakini
aliendelea kutambua kuwa Mungu ndie kimbilio lake na msaada uonekanao tele
wakati wa Mateso Zaburi 46:1.
Zaburi 16:3-4 Daudi alionyesha kuwapenda watu wanaishi maisha ya
utakatifu na kumtumikia Mungu, huku akitabiri kuongezeka kwa huzuni za watu
wasiomuabudu Mungu wa kweli na kuabudu miungi mingine , Daudi alichukizwa zaidi
na watu waliokuwa wakiabudu miungu na kutoa sadaka za damu kwa miungu hiyo
alikiri kutokuwataja hata majina yako vinywani mwake Isaya 57:5, watu walitoa
watoto wao sadaka kwa miungu Daudi alichukizwa nao sana hakufurahishwa na
Ushirikina hata kidogo
Zaburi 16:5-9 Daudi anaonyesha kuwa yeye Kwake Bwana ndiye fungu
lake yaani amemchagua Bwana, kama ni uamuzi wa kuchagua Basi yeye angelimchagua
Bwana Mungu ameshika kura ya Daudi, anaamini kumchagua Bwana ni kuangukia
mahali pema, ni urithi Mzuri, kuliko kawaida na kuwa atamhimidi Bwana, aliyempa
shauri na kumfundisha amemweka Bwana mbele Daima na hataondoshwa moyo wake
unamfurahia bwana na kumtumaini.
Matokeo ya Imani ya Daudi.
- · Daudi aliamini katika kumtegemea Mungu
- · Aliamini na kuwapenda watu wanaomtumikia Mungu badala ya kuchukizwa nao
- · Alimchagua Bwana na kumfanya kuwa fungu lake na alikataa kushiriki ibada zisizofaa wala kutoa sadaka za kuua watoto na kutoa Damu yake alipingana na ushirikina
- · Aliamini kuwa akifanya hayo atapata furaha kuu hata kama atakuwa katika hali ya kifo, Mungu hatakubali au kumuacha afe na akifa Mungu hatakubali kumuacha aone uharibifu yaani aoze!
Hutamtoa Mtakatifu wako aone
Uharibifu! Zaburi ya 16:10-11
Hatujui kuwa daudi alikuwa na
ufahamu gani kuhusu maisha baada ya kufa, lakini ni lazima tuamini na kukaa
katika kumuamini Mungu kama Daudi, Daudi kwa kusema Maneno hayo alimaanisha
Lazima Mungu atamfufua tu, Biblia iko wazi kuwa iko siku miili ya watakatifu
itafufuka Isaya 26:19 “Wafu
wakowataishi” Daniel 12:2-3 “wengi
wa hao waliolala katika Mavumbi wataamka” Yesu alieleza wazi kuwa kuna maisha
baada ya kufa Marko 12:26-27 Biblia
inasema hivi “26.
Na kwa habari ya wafu ya kwamba wafufuliwa, hamjasoma katika kitabu cha Musa,
Sura ya Kijiti, jinsi Mungu alivyomwambia, akisema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu,
na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? 27.
Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Hivyo mwapotea sana.” Ni wazi kuwa Yesu alifufuka yeye alikuwa ni
Malimbuko tu ni alama ya kuwa kila amuaminiye yeye atamfufua Yohana 11:23-25, Biblia inasema hivi “23. Yesu akamwambia,
Ndugu yako atafufuka. 24. Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika
ufufuo siku ya mwisho. 25. Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima.
Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi” Unaona Daudi hakuwa anazungumzia Ufufuo wa
Yesu Kristo Pekee Yesu Kristo ni Ufufuo na Uzima maana yake ndiye anayefufua na
ndiye atakayefufu, Daudi alikuwa akizungumzia imani yake kuwa atafufuliwa hata
kama ameoza lakini iko siku Mungu atamuinua tena, Daudi pia alikuwa
anazungumzia ufufuo wa kila mmoja wetu kuwa sisi sote tutafufuka Yesu
atakapokuja tena na kama atakukuta unaishi huku unamuamini basi hutakufa kabisa.
Hutamtoa Mtakatifu wako
aone uharibifu ni
muhimu kufahamu pia kuwa uharibifu sio kifo pekee Bilia inaeleza kuwa mwivi
haji ila aibe kuchinja na kuharibu, Yohana
10:10 hivyo muharibifu ni Shetani, Kama tutamutmaini Mungu na kuachana na
ushirikina, na kumfanya yeye kuwa fungu letu ni wazi kuwa Mungu atatulinda
hatutaona uharibifu wa aina yoyote katika maisha yetu, Mashambani, Biashara,
Ndoa, Uchumba, kazini, afya magonjwa
mabaya, mimba kuharibika, mashambulizi
ya kishetani, Umasikini na udhaifu katika taifa letu, tukimtumaini Mungu
atatupa neema na uzee mwema na tutaondoka Duniani kwa wakati tukiwa tumeshiba
miaka, na Mungu akitukuzwa sana na maisha yetu. Mungu akupe neema usione
uharibifu katika jina la yesu Kristo amen
Na Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni