Habakuki 3:19 “YEHOVA, aliye Bwana, ni nguvu zangu, Yeye huifanya MIGUU
YANGU KUWA KAMA YA KULUNGU, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.”
Utangulizi:
Leo hii tutachukua muda
kutafakari kwa kina na upana ma urefu kuhusu mnyama mwingine anayesifiwa sana
katika maandiko anayejulikana kama “KULUNGU” tunapojifunza kuhusu mnyama huyu
utaweza kugundua kweli nyingine za kibiblia ambazo zinaanika upendo wa Mungu
kwetu.
Katika tamaduni za mashariki ya
kati Kulungu au kwa kiarabu Ayyalah (maana yake Mbuzi pori) ni
mnayama anayetumika kuelezea symbol ya Mamlaka ya kiroho, pia ni myama ambaye
pembe zake zinauwezo wa kukua na kuvunjika au kuanguka kisha kuota nyingine ni
alama ya “kuanza upya”au “kuzaliwa upya” regenereation na ni
alama ya Huruma na kujitoa au kujali kwa Mungu dhidi ya watoto wake yaani wana
wa Mungu.
Tutajifunza somo hili kwa
kuangalia vipengele vitatu vya muhimu vifuatavyo:-
·
Ufahamu kuhusu “KULUNGU”
·
Sifa kuu za Kulungu
·
Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya Kulungu!
Huifanya miguu yangu kuwa kama ya Kulungu!
Ufahamu kuhusu Kulungu.
Kulungu ni mnyama aina ya jamii
ya swala ambae kwa kiingereza anaitwa “Deer”
kwa jina la kisayansi huitwa “Cervidae”
nimnyama mwenye uwezo wa kuishi kati ya miaka 15-25 mnyama huyu amesifiwa kuwa
na mbio na miguu mwepesi, katika
maandiko kwa vile anauwezo wa kukimbia kati ya speed 60-80 km/h yaani mbio kati
ya kilomita sitini mpaka themanini kwa saa, pia ni mnyama hodari katika uwezo
wa kuruka na kukwepa vihunzi vya aina mbalimbali, anauwezo wa kukimbia katika
nyika na kuruka kwa madaha kutokana na wepesi wa miguu yake, na kwa vile Mungu
amemuumba Kulungu kuwa mwepesi na mwenye uwezo wa kutokomea kwa haraka Adui
zake hukata tamaa katika kumfuatilia, kwani ni vigumu kumpata na anaweza kupita
katika eneo lolote ambalo kwa wanyama wengine linaweza kuwa ni lenye kuleta
changamoto.
Kulungu au ayyala wanapenda sana
kuishi milimani na kwenye majabali wawapo nyikani au mwituni hii humsaidia
kuweza kuona maadui kwa mbali, lakini pia katika majabali huwa anakuwa mwepesi
zaidi kuliko katika matope, Daudi alikuwa na ujuzi kuhusu Kulungu kwa vile
aliishi nao katika milima yao wakati akimkimbia Sauli, ISamuel 24:2, "Ndipo Sauli akatwaa watu elfu waliochaguliwa katika Israeli wote, akaenda kumtafuta Daudi na watu wake juu ya majabali ya mbuzi-mwitu."
Aidha kulungu aliwekwa katika
orodha ya wanyama safi wasio najisi Kumbukumbu 14:4-5. “Wanyama
mtakaokula ni hawa ng'ombe, na kondoo, na mbuzi, kulungu, na paa, na kongoni,
na mbuzi wa mwitu, na paa mweupe, na pofu, na mbuzi wa mlima;”
Adui zake wakubwa ni Simba, Dubu
na Chui, ambao humwinda na kumfanya kuwa kitoweo, kwa ujumla ni mnyama mzuri
sana na pia kama ukipata nafasi ya kula nyama yake ni tamu sana ayala hufananishwa
na mke mzuri wa halali.
Sifa kuu za Kulungu.
Kulungu ni mnyama wa nane Duniani kwa mbio
1.
Baada
ya mnyama aina ya chui au cheter ambaye ana uwezo wa kukimbia kwa kasi zaidi ya 110-120 km/h mnyama anayefuata kwa nafasi ya nane katika mbio ni Kulungu 60-80 km/h sawa sekunde 0.016 kwa kilomita moja. Kwa msingi huo sifa kubwa ya
mnyama huyu ni wepesi Inyakati 12:8 “Na wa
Wagadi wakajitenga kumfuata Daudi ngomeni huko nyikani, waume mashujaa, watu
waliozoea vita, walioweza kutumia ngao na mkuki; ambao nyuso zao zilikuwa kama
nyuso za simba, nao walikuwa WEPESI
kama kulungu juu ya milima;
Habakuki 3:19 “YEHOVA,
aliye Bwana, ni nguvu zangu, Yeye huifanya MIGUU
YANGU KUWA KAMA YA KULUNGU, Naye ataniendesha katika mahali pangu
palipoinuka.”
2Samuel 2:18 “Na wana
watatu wa Seruya walikuwako huko, Yoabu, na Abishai, na Asaheli; na Asaheli
alikuwa MWEPESI WA MIGUU KAMA KULUNGU.”
2.
Kulungu
ni mnyama mzuri sana na hivyo sifa zake hufananishwa na mwanamke mrembo wa wakati wa ujana, Mithali
5:18-19 “Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe
umfurahie mke wa ujana wako. Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Maziwa yake
yakutoshe sikuzote; Na kwa upendo wake ushangilie daima.”
3.
Kulungu
hupenda kukaa juu, ni mnyama mwangalifu sana kwaajili ya kujikinga na maadui na
kujilinda wakati wote huhakikisha usalama wake na maisha yake ni ya muhimu
sana Zaburi
18:33 “MIGUU
YANGU ANAIFANYA KUWA YA KULUNGU, Na
kunisimamisha mahali pangu pa juu.”
4.
Kulungu
wanajua kufurahi wakati wanapokuwa na amani, wana ujuzi wa kuruka ruka kwa
furaha Isaya 35:6 “Ndipo mtu aliye kilema
ataruka-ruka kama kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba; maana katika nyika
maji yatabubujika; na vijito jangwani.”
5.
Kulungu
wanapenda sana maji, alisema mtaalamu mmoja njia pekee ya kuwavutia Kulungu, au
ayala ni kuwapatia maji ya kunywa, Zaburi 42:1-5
“Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo
hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu. Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU,
Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu? Machozi yangu
yamekuwa chakula changu mchana na usiku, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko
wapi Mungu wako. Nayakumbuka hayo nikiweka wazi nafsi yangu ndani yangu, Jinsi
nilivyokuwa nikienda na mkutano, Na kuwaongoza nyumbani kwa Mungu, Kwa sauti ya
furaha na kusifu, mkutano wa sikukuu. Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na
kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya
ya uso wangu, Na Mungu wangu”
Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu!
Ni muhimu kufahamu kuwa Nabii Habakuki alinukuu maneno ya mfalme Daudi
Habakuki 3: 19 ““YEHOVA, aliye Bwana, ni nguvu
zangu, Yeye huifanya MIGUU YANGU KUWA KAMA YA KULUNGU, Naye ataniendesha katika
mahali pangu palipoinuka.”
Inafanana na Zaburi 18:31-40 “Maana ni nani
aliye Mungu ila Bwana? Ni nani aliye mwamba ila Mungu wetu? Mungu ndiye
anifungaye mshipi wa nguvu, Naye anaifanya kamilifu njia yangu. Miguu yangu
anaifanya kuwa ya kulungu, Na kunisimamisha mahali pangu pa juu. Ananifundisha mikono yangu vita, Mikono yangu
ikaupinda upinde wa shaba. Nawe umenipa ngao ya wokovu wako, Mkono wako wa
kuume umenitegemeza, Na unyenyekevu wako umenikuza. Umezifanyizia nafasi hatua
zangu, Na miguu yangu haikuteleza. Nitawafuatia adui zangu na kuwapata, Wala
sitarudi nyuma hata wakomeshwe. Nitawapiga-piga wasiweze kusimama, Wataanguka
chini ya miguu yangu. Nawe hunifunga mshipi wa nguvu kwa vita, Hunitiishia
chini yangu walioniondokea. Naam, adui zangu umewafanya wanipe visogo, Nao
walionichukia nimewakatilia mbali.”
Mwandishi wa Zaburi Pamoja na
Nabii Habakuki wanarudia umuhimu wa mtu anayemtegemea Mungu
1. Kwamba
ukimtegemea Mungu yeye anageuka kuwa chanzo cha nguvu zako, anakufanya kuwa
mwepesi dhidi ya adui zako, anakuweka juu Mahali palipoinuka ili uweze kuwaona
na kuwasanifu
2. Anaifanya
njia yako kuwa kamilifu, anakusaidia usijikwae anakuwekea wepesi, ananyoosha
mapito yako miguu yako inakuwa mwepesi kukwepa vohuzi vya kila aina ya adui,
3. Anakuweka
mahali pa juu, palipoinuka anazungumzia ushindi, heshima katika jamii, anakupa
uwezo wa kuona vikwazo na kuvikwepa anakupa uwezo wa kuzijua hila za adui na
kuzizima au kuzikimbia anakupa namna ya kwenda bila kupata madhara, utakuwa
unapita juu ya hatari na unaziangalia kwa chini na adui zako ni ngumu kukupata.
4. Bwana
na akupe neema ya kuifanya Miguu yako kuwa kama ya Kulungu katika jina la Yesu
Kristo. Bwana na akufanyie wepesi katika kila unalolifanya mwaka huu mpya,
Bwana na akupe wepesi dhidi ya adui zako, bwana ana akupe njia na kukuweka
mahali pa juu
Kulungu ni alama
ya:-
·
Usafi/utakatifu – utaishi kwa mafanikio bila
kulaumiwa na mtu utajikinga na maadui zako
·
Ibada/kiu na njaa ya haki/uhitaji wa Mungu -
Mungu ndiye tegemeo lako tamani kudumisha uhusiano na Mungu
·
Ulinzi wa Mungu, miguu yao haitelezi, Mungu
atakulinda usijikwae usianguke katika mitego ya adui
·
Mapenzi – Onyesha kumjali na kumuheshimu kila
mmoja
·
Furaha – shetani hupenda sana uwe na huzuni
Furaha ya bwana ndio nguvu zetu usihuzunike furahi katika bwana siku zote
·
Wepesi katika kazi, katika kukwepa mitego ya
adui – Mungu akufanyie wepesi katika kila ulifanyalo
·
Kukaa katika amani na salama./mahali palipoinuka.
– Mungu akupe akili ya kujihadhari na maadui zako
·
Mungu akupe pembe mpya, njia mpya na mbinu mpya
unapokuwa umechoshwa na maswala ya zamani, usiangalia nyuma songa mbele.
Na Mkuu wa
wajenzi mwenye Hekima.
Rev. Innocent
Kamote.
Maoni 25 :
Nimependa kuusu kulungu..nimesoma Leo Ila kwa nimesoma na hii nimeelewa zaidi nashkulu Mungu awazidishe
Ooh thank you made me aware
Barikiwa sana Mtumishi.Nime elewa hii maana ya Kulungu ktk biblia
Ubarikiwe mtumishi Kwa udadavuzi huu wa mnyama huyu kibiblia ndiyo maana biblia ni msitu mnene nimeongeza maarifa Leo.
Barikiwa sana mtumishi wa Mungu, hakika nimejifunza jambo kubwa sana
Barikiwa Sana mtumishi kwa kunifumbua kuhusu mnyama huyo nilikuwa cjui anything kuhusu kulungu
Ubarikiwe sana na Bwana Yesu Kristo kwa ufafanuzi mzuri kuhusu kululunga, nimebarikiwa na nimejifunza.
Asante kwa maarifa haya nimepata vingi 🙏
New knowledge in my head🤌 nimependa Kaka a FOOD OF THOUGHT
Nilitamani kujua nimejua
Nilitamani kujua nimejua
Nimejifunza kitu kikubwa sana. U barikiwe
Hakika,ninamtukuza Mungu kwaajili yenu,nilihitaji ufahamu huu kwa majira haya,Mungu mwema awape hatua zaidi
Kwa kweli nimependa ufafanuzi huu
Nimejifunza mengi Sanaa mungu anifanyie wepesi Nitshill kama kulungu
Somo zuri sana
Nimeelewa kwa undani maana ya Kulungu, umeongezea na picha, basi umefanya vema sana; Neema ya Mungu ikufunike kwa huu ufunuo, Mungu wa Mbinguni ashukuliwe kwaajili yako, Amina
Nimeelew ubarikiwe sana
Nimeelewa sasa ubarikiweee
Ameni barikiwa mno
Asante sana Kwa somo zuri Namuomba Mungu anifanye niwe na sifa njema kama kulungu
Hasante kwa kwa tafsiri ya jina kulungu
Asante sana Kwa mafundisho yaliyosheheni maandiko matakatifu
Barikiwa Sana mtumishi
MUNGU akubariki sana mtumishi kwa somo zuri ambayo limeongeza kitu kingine leo katika uelewa wangu wa maandiko na somo la biblia asante sana kwa kazi nzuri barikiwa
Mungu akubariki, Umenifungua macho kuhusu hili ni somo zuri sana sana na maana
Chapisha Maoni