Mstari wa Msingi: Kutoka 6:5-8 “Na zaidi ya hayo, nimesikia kuugua kwao wana wa
Israeli, ambao Wamisri wanawatumikisha, nami nimelikumbuka agano langu. Basi
waambie wana wa Israeli, Mimi ni YEHOVA, nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya MIZIGO
ya Wamisri, nami nitawaokoa na UTUMWA wao, nami NITAWAKOMBOA kwa mkono
ulionyoshwa, na kwa HUKUMU KUBWA; nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa
Mungu kwenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ni YEHOVA, Mungu wenu, niwatoaye mtoke
chini ya mizigo ya Wamisri. Nami nitawaleta hata nchi ile ambayo naliinua mkono
wangu, niwape Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo; nitawapa iwe urithi wenu; Mimi ni
YEHOVA”
Utangulizi:
Hivi karibuni wakristo nchini
wataungana na wakristo wengine kote duniani kuadhimisha sikukuu ya pasaka,
katika wakati huu ni muhimu kujikumbusha kuwa Pasaka inayoadhimishwa na
wakristo, inaadhimishwa katika wakati ambapo Wayahudi nao huadhimisha Pasaka
yao, wako wakikumbuka kuokolewa kwao Katika Inchi ya misri na sisi tukikumbuka
na kuadhimisha kusulubiwa kufa na kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo pale
Msalabani, Hata hivyo ni muhimu kufahamu kuwa Pasaka zote kwa ujumla
zinazungumzia Jambo moja la ukombozi na zote zinaashiria nguvu ya ukombozi
kupitia damu ya mwana kondoo, na Damu hiyo ni ya Kondoo Halisi ambaye ni Yesu
Kristo.
Kutoka 12;12-13 “Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami
nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa
mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA. Na
ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami
nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu,
nitakapoipiga nchi ya Misri.”
Pasaka zote ile ya Wayahudi na
ile ya Yesu Kristo zote zinauhusiano na Damu, Damu wakati wa agano la kale
ilitumika kama ishara ya ukombozi na wakati wa agano jipya ni damu halisi ya
Yesu Kristo damu hii ina nguvu ya ukombozi kama ilivyokuwa ile ya Mwana kondoo
wa pasaka na nguvu hii ndio huitwa nguvu ya Pasaka kwa mujibu wa Rabbi Avraham
Brandwein Damu ya Pasaka ina nguvu kuu nne za ukombozi zinazotajwa katika Kutoka 6:6-7 ambao ndio mstari wa
Msingi
1. Kutuondoa chini ya Mzigo – Mzigo ni
kila aina ya usumbufu unaotuelemea wa Ulimwengu huu, ni maumivu na mateso ya
kila aina ambayo yametusonga na kutosononesha ni kila aina ya kifungo cha
ibilisi na nguvu za yule adui zinazo tuonea Yesu Kristo anataka kila mmoja
anayelemewa na mizigo kumwendea yeye Mathayo
11:28 “Njoni
kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.”
2. Kutuokoa katika utumwa – Israel
walikuwa utumwani Misri na wakristo walikuwa chini ya butumwa wa dhambi na
Shetani Kazi ya Bwana Yesu Kristo ni kutuweka huru kutoka huko na kufanya kuwa
wana wa Mungu, Kazi aliyoifanya Yesu Pale msalabani ilikuwa na kusudi la
kutukomboa kutoka katika kila aina ya utumwa Wagalatia 4:4-7 “Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe
ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, kusudi awakomboe hao waliokuwa
chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana. Na kwa kuwa ninyi
mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani,
Baba. Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u
mrithi kwa Mungu”
3. Kutukomboa kwa Mkono ulioonyooshwa –
kukomboa kitu maana yake ni kulipa gharama zinazohusika ili kukirejesha
kwamuhusika halisia, kitaalamu Mungu alituumba kwa kusudi lake lakini Shetani
alitutumikisha na kutuweka chini ya utumwa wa dhambi na chini yake yesu alikuja
apate kutukomboa kutoka katika utumwa wa dhambi Warumi 6:17-18 “ Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa
watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni
utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki. Lakini
Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa
mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake; na mlipokwisha
kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki.”
4.
Kutufanya
kuwa watu wake urejesho - Yeremia 30:122
“Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha
zako, asema Bwana, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni,
ambao hapana mtu autakaye. Bwana asema hivi, Tazama, nitarudisha tena hema za
Yakobo zilizohamishwa, na kuyahurumia makao yake; nao mji huo utajengwa juu ya
magofu yake wenyewe, nalo jumba litakaliwa, kama ilivyokuwa desturi yake. Tena
kwao itasikiwa shukrani, na sauti yao wachangamkao; nami nitawazidisha, wala
hawatakuwa wachache; tena nitawatukuza, wala hawatakuwa wanyonge. Watoto wao
nao watakuwa kama zamani, na kusanyiko lao litathibitika mbele zangu, nami
nitawaadhibu wote wawaoneao. Na mkuu wao atakuwa mtu wa kwao wenyewe, naye
mwenye kuwatawala atakuwa mtu wa jamaa yao; nami nitamkaribisha, naye
atanikaribia; maana ni nani aliye na moyo wa kuthubutu kunikaribia? Asema
Bwana. Nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu.”
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni