Yeremia 6:16 “Bwana asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize
habari za mapito ya zamani, I wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo,
nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, Hatutaki kwenda
katika njia hiyo.”
“Kama Jamii yoyote itapoteza Historia, maana yake imepoteza Muelekeo”
Rev Innocent Kamote Mkuu wa wajenzi mwenye hekima
Utangulizi.
Ni muhimu kufahamu kuwa Maisha
yetu hayawezi kuwa na furaha ya kweli kama mara kwa mara hatutajifunza kutokana
na Historia, Historia ni mwalimu mkubwa sana wa kutusaidia kujua tunatoka wapi
na tuko wapi na tunakwenda wapi, “Kama jamii yoyote itapoteza Historia, maana
yake itapoteza muelekeo” Na mkuu wa wajenzi mwenye Hekima, Kwa msingi huo kuna
umuhimu wa kujifunza kutokana na Historia, semi kadhaa za Kihistoria
zinatusaidia kujua umuhimu wake
·
Historia sio mzigo katika kumbukumbu zetu bali
ni Mwangaza wa Nafsi zetu lord Acton- History is not a burden on the memory but
an illumination of the soul – Lord Action.
·
Mtu asiyejali Historia ni sawa na Kiziwi ni sawa
na kipofu – Aldof Hittler The man who
has no sense of history, is like a man who has no ears or eyes. Adolf Hitler
·
Baada ya kufanya makosa au kuteseka, na kupoteza
muelekeo Mtu mwenye akili huangalia nyayo zake – Napoleon - After making a
mistake or suffering a misfortune, the man of genius always gets back on his
feet. Napoleon
·
Tunasoma kutokakatika Historia kile ambacho
Hatujakisoma katika Historia – Desmond Tutu - We learn from history that we
don’t learn from history! Desmond Tutu
·
Raia wenzangu, Hatuwezi kuiepuka Historia
Abrahamu Lincoln - Fellow citizens, we cannot escape history. Abraham Lincoln
Kama tunavyoweza kuona hapo juu,
umuhimu wa Historia ni wazi kuwa neno la Mungu pia limeandikwa kwa makusudi ya
kutukumbusha na kutufundisha kutokana na Historia Biblia inasema hivi :-
1Wakoritho 10:1-11 “Kwa maana, ndugu
zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu;
wote wakapita kati ya bahari; wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na
katika bahari; wote wakala chakula kile kile cha roho; wote wakanywa kinywaji
kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba
ule ulikuwa ni Kristo. Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao;
maana waliangamizwa jangwani. Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi
sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.Wala msiwe
waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi
kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze.Wala msifanye uasherati, kama wengine
wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu. Wala
tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka.Wala
msinung'unike, kama wengine wao walivyonung'unika, wakaharibiwa na mharabu.
Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya
sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.”
Kumbe kila mmoja anaweza kujifunza kitu kutokana na Historia.
Katika kifungu cha maandiko
Yeremia 6:16 Mungu anatoa wito kwa wana wa Israel, yaani wayahudi kuuliza kwa
habari za mapito ya zamani, yaani katika wakati huu kulikuwa na ukengeufu
mkubwa na mmomonyoko mkubwa wa uadilifum watu walikuwa wakifuata njia zao
wenyewe na hivyo walipoteza raha na amani ya kweli, Taifa, Kanisa, Jamii na
kila mmoja anapaswa kuangalia njia zake na kujifunza kutokana na Historian a
kuangalia njia za Zamani na kujikagua kama tuko sahihi au lah nini kimepoteza
furaha tuliyokuwa nayo, ka sababu gani tupo hapo tulipo? Kwa nini hilo au lile linatokea?
Nabii Yeremia alitumwa na Mungu kuwakubusha wayahudi kuifuata njia ile ili
waweze kufanikiwa
Yeremia 7:22-23 “Maana sikusema na
baba zenu, wala sikuwaamuru kwa habari za sadaka za kuteketezwa na dhabihu,
siku ile nilipowatoa katika nchi ya Misri; lakini naliwaamuru neno hili,
nikisema, Sikilizeni sauti yangu, nami nitakuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu
wangu; mkaende katika njia ile yote nitakayowaamuru mpate kufanikiwa.”
Unaweza kuona iko njia ya
mafanikio ambayo Mungu aliwaonyesha Israel Tangu zamani lakini wao walikuwa
wamekaidi kuifuata na hivyo maisha yao yalijaa taabu na kukosa raha na
amani, Hakuna namna yoyote ambayo
tunaweza kuwa na amani ya kweli endapo tutakuwa nje ya njia ya kweli au kama
tumeiacha njia ya Mungu, Kama Mungu anatupenda kwa dhati anachokifanya ni
kuwatuma watumishi wake manabii wake kutukumbusha kurudi katika njia, Mungu
anataka watu wake wajifunze kutokana na Historia Israel walipofanya vema na
kuzishika nzjia za Mungu Mungu aliwarudia na kuwa pamoja nao, lakini walipofanya
mabaya Mungu aliwaacha na walipata tabu sana
Sisemi kwamba kila taabu
inasababishwa na kuacha njia ya Mungu hapana lakini kuna raha kupitia taabu
huku ukiwa na Mungu, na kuna utungu mkubwa kupitia taabu huku ukiwa umemuacha
Mungu, Katika nyakati hizi tulizo nazo pia Mungu ametupa njia ya kuifuata
Yohana 14:6 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na
uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”
Linapotokea jambo
Gumu la kuumiza na kukatisha tamaa ni muhimu kuangalia Habari ya mapito ya
zamani, baba zetu na watakatifu waliotutangulia walifanya nini? Wao
walimtegemea Mungu hawakuzitegemea akili zao wenyewe, walimuweka Mungu mbele,
walimfamya Mungu kuwa kinga yao, walimfanya yeye kuwa mtetezi wao, walimfanya
kuwa ngao yao, walimfanya kuwa tumaini lao, walimgeukia yeye na kwa sababu hiyo
walipata raha nafsini mwao, Historia inaonyesha kuwa Yesu hajawahi kumuangusha
mtu aliyemtegemea
Mathayo 11:28-29 “Njoni kwangu, ninyi
nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira
yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi
mtapata raha nafsini mwenu;”
Yesu amewahakikishia raha wale
wote wanaoshikamana naye, Hakuna namna unaweza kujikwamua katika jambo lolote
bila ya Yesu, Taifa jamii na kanisa kama tunataka kufanikiwa basi tunapaswa
kuangalia njia zetu kama tumekengeuka tukajifunze habari za mapito ya zamani na
kuangalia kwamba tunaenenda sawasawa au hapana? Tumfanye Yesu kuwa tegemeo
letu, ngao yetu, kimbilio letu, mwamba wetu, tumaini letu na tukimtegemea yeye
na kutii maelekezo yake tutapata raha nafisni mwetu,
Tenzi namba 16 Kumtegemea Mwokozi kwangu tamu kabisa…………..
Na Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni