“Akawaambia mfano wale walioalikwa, alipoona
jinsi walivyochagua viti vya mbele; akisema, Ukialikwa na mtu arusini, usiketi
katika kiti cha mbele; isiwe kwamba amealikwa mtu mwenye kustahiwa kuliko wewe,
akaja yule aliyewaalika wewe na yeye, na kukuambia, Mpishe huyu! Ndipo
utakapoanza kwa haya (AIBU) kushika mahali pa nyuma. Bali ukialikwa, nenda
ukaketi mahali pa nyuma, ili ajapo yule aliyekualika akuambie, Rafiki yangu, njoo
huku mbele zaidi; ndipo utakapokuwa na utukufu mbele ya wote walioketi pamoja
nawe. Kwa maana kila ajikwezaye
atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.”
Utangulizi:
Maandiko matakatifu
yanatufundisha namna bora ya kuishi katika ulimwengu huu, na kupata mafanikio,
moja ya njia iliyo bora zaidi ya kuishi maisha ya furaha na amani ni pamoja na
kuishi maisha ya unyenyekevu, pamoja na kuwaheshimu watu wengine au watu wote,
Maandiko yanasema katika.
Wafilipi
2:3 “Msitende
neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu
na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.”
Yesu Kristo katika kufundisha
kwake alipenda sana kutumia mifano ya aina mbalimbali kwaajili ya kufundisha
watu kuhusu ufalme wa Mungu, na ili watu waweze kuelewa alitumia story pamoja
na matukio mbalimbali halisi yaliyotokea kuwafundisha watu maisha na ufahamu
kuhusu utendaji wa Mungu na tabia zake ili waweze kuishi kwa amani, Ingawa Yesu
alitumia mifano lakini mifano hii ilibeba maana kubwa sana na za kweli kuhusu maisha.
Katika kifungu cha Maandiko
tunayosoma leo, Katika Luka 14, Yesu alikuwa amealikwa katika chakula cha jioni
na moja ya maafisa wakubwa sana wa Mafarisayo, Watu wengine wengi sana
walikuwepo au walialikwa pia, kulikuwa na watu muhimu wengi sana wastahiki na
pia watu wengine wengi waliokuwa na nyadhifa mbalimbali na wale ambao bila shaka walijifikiri kuwa ni
wa muhimu sana, walipokuwa wakiingia Yesu alikuwa akifuatilia kila kilichokuwa
kinaendelea, wengi walikwenda kukaa moja kwa moja kwenye viti maalumu vya Meza
kuu, hatujui nini kilitokea lakini Yesu alipata somo la kuwafundisha wanafunzi
wake, kwa kile kilichotokea kwani
tunaweza kukiona japokuwa mwandishi hakukigusia wazi inawezekana wengi
walikwenda kukaa mahali ambapo huenda hapakuwa pameandaliwa kwa ajili yao na hivyo haikuwa sahihi kwao kukaa, na
inawezekana baadaye walihamisha na kupelekwa katika viti vya kawaida na
hawakujisikia vizuri, (Zamani hakukuwa
na utaratibu wa kuweka majina mezani, Lakini aliyepanga viti na meza yaani
mwenyeji ndiye aliyekuwa na jibu moyoni kuwa nani anastahili kukaa wapi). Yesu
anatumia tukio hili kutufundisha jinsi njia ya unyenyekevu ilivyo ya muhimu
sana katika maisha yetu ya kila siku na zaidi sana katika ufalme wa Mungu.
Kuna nukuu nyingi sana duniani
zinazotufundisha kuhusu umuhimu wa unyenyekevu na hapa nimechagua chache:-
Mtakatifu Augustino alisema “it was Pride
that Changed the Angels to be devils and its humility that makes man as Angels”
yaani “Ni kiburi kilichowafanya malaika
kuwa pepo na ni unyenyekevu unaowafanya wanadamu kuwa kama malaika”
Thomas Merton
alisema “Pride
makes us artificial and humility makes us really” kwamba “kiburi hutufanya kuwa fake na unyenyekevu
hutufanya kuwa halisi”
Rev. Innocent
Kamote “Many
ways may let people down, but have never ever seen humility letting someone
down” “njia nyingi zinaweza kuwaangusha watu chini lakini sijawahi ona
unyenyekevu ukiwaangusha mtu chini”
Unaweza kuona Yesu anataka tuelewe
kanuni za ufalme wa Mungu na kanuni za maisha haya, ni wazi kuwa mgeni hajui
kuwa anapaswa kukaa katika kiti gani, ni lazima asubiri kukaribisha mwenyeji
ndiye anayejua, Katika ufalme wa Mungu mwenyeji wetu ni Yesu, ni uhusiano wetu
na mwenyeji wetu ndio utakaoamua kuwa ni kiti gani tutakalia, wako wengine
wanajifikiri kuwa ni bora, kutokana na Dini zao, au madhehebu yao, au elimu
zao, au kabila zao, au familia wanayotokea, au mkoa, au kutokana na huduma
aliyo nayo, au kwa sababu anatumiwa sana na Mungu kufanya miujiza mikubwa, mtu
anaweza akapiga hesabu zake kichwani mwake akajidhani kuwa yeye ni wa muhimu kuliko wengine, Ni mwenyeji wetu
Yesu ndiye ana mamlaka ya kuhamisha watu viti, anaweza kukuambia ndugu kakae
mbele au anaweza kukuambia ndugu kakaye nyuma!
Mwanafunzi anapokwenda shuleni,
anakuwa amekuja kujifunza, amekuja kukaa chjini ya walimu amekuja kufuata
maelekezo, amekuja kufuata program zote za shule, na hivyo wanafunzi wa aina hii hukubali kukaa
chini ya walimu kwa unyenyekevu na kukubali kufundishika, wanakaa chini
wanajifunza na kutafuta majibu ya maswala husika huku wakitii kila
wanachoagizwa, Mwanafunzi yeyote ambaye anajidhani kuwa yuko smatter kuliko mwalimu
wake, huwa na kiburi hawawezi kukubali kufuata maelekezo ya walimu wao wala
program za shule na hatimaye matokeo yataeleza baadaye who is more smatter?
Yesu Kristo alikuwa ni mwana wa
Mungu, lakini aliishi maisha ya unyenyekevu, alikuwa mtii alikubali kuelekezwa
na alihukumiwa na alikubali kutii mpango wa Mungu na kumtii hata katika mauti
ya msalaba ambayo ni mauti ya aibu sana kutokana na uwezo wake mkubwa wa
unyenyekevu Mungu amemuadhimisha mno.
Wafilipi 2:4-11 “Kila mtu asiangalie mambo yake
mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Iweni na nia iyo hiyo ndani
yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna
namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha
kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa,
akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu,
alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena
Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;ili kwa jina
la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini
ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu
Baba”
Ili Mungu atuinue na kutuheshimu
katika kanuni za ufalme wa Mungu njia ya kuwa wa muhimu sana ni kujishusha
sana, njia ya kupanda juu sana ni kuwa mnyenyekevu sana ukikumbuka kuwa kuwa
mnyenyekevu hakumaanishi kuwa wewe ni mjinga bali ni hekima ya Mungu ya hali ya
juu ni njia ambayo Yesu aliichagua katika maisha na akatuachia kielelezo
tuifuate kwani ina mafanikio makubwa sana.
Zaburi 138: 6 “Ingawa Bwana yuko juu, amwona
mnyenyekevu, Naye amjua mwenye kujivuna tokea mbali.”
Mithali 18:12 “Kabla ya uharibifu moyo wa
mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.”
Warumi 12:16 “Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi.
Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe
watu wa kujivunia akili.”
Aidha Yesu alikuwa anataka
tujifunze kuwaheshimu wengine na kutambua uweza wa wengine, mwaka 18th
April 1980 ilikuwa nisiku ya Zimbabwe kupata uhuru wake kutoka kwa Muingereza,
katika siku hiyo walialikwa wageni maarufu kabisa duniani akiwemo Rais maarufu
wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, pamoja na mambo mengine, Zimbabwe
ilimualika Mwanamziki maarufu wa muziki wa Regge duniani
Robert Nesta "Bob"
Marley (6 Februari 1945 - 11 Mei 1981) yaye alikuwa mwimbaji na mwanamuziki muhimu kutoka nchini Jamaika. Alivuma
hasa kunako miaka ya 1970 na 1980. Ambaye ameweza kuifanya staili ya muziki wa reggae kuwa
maarufu sana duniani. Muziki wake mwingi ulikuwa unazungumzia dini ya Rastafari
ambayo yeye alikuwa anaifuata. Kuna baadhi ya nyimbo zake zinahusu masuala ya
dini na zingine siasa.
Katika wakati wa kusalimiana
Mwalimu Julius Nyerere alipopeana mkono na mwanamuzik Bob Marley hakuwa
amependezwa naye kwani alionekana kuwa mtu rafu asiyekata nyele zake na kama
mvuta bangi hivi, lakini katika wakati Mwanamuziki huyo alipotumbuiza ndipo
mwalimu Nyerere alipokwenda kumkumbatia na kumkubali mwanamziki huyo kutokana
na nyimbo zake nzuri zenye kuhamasisha fikra za kiukombozi wimbo mojawapo
muhimu ulikuwa ni pamoja na wimbo kuhusu Zimbabwe ambao ulikuwa na maneno yenye
hamasa ya hali ya juu, yaliyodhihirisha kuwa Bob alikuwa msanii mahiri mwana mapinduzi aliyeipenda afrika kwa dhati kutoka Moyoni.
Every man
gotta right to decide his own destiny
And in this judgment there is no partiality
So arm in arms, with arms
We'll fight this little struggle
'Cause that's the only way
We can overcome our little trouble
And in this judgment there is no partiality
So arm in arms, with arms
We'll fight this little struggle
'Cause that's the only way
We can overcome our little trouble
No more
internal power struggle
We come together to overcome the little trouble
Soon we'll find out who is the real revolutionary
'Cause I don't want my people to be contrary
We come together to overcome the little trouble
Soon we'll find out who is the real revolutionary
'Cause I don't want my people to be contrary
To divide
and rule could only tear us apart
In everyman chest, there beats a heart
So soon we'll find out who is the real revolutionary
And I don't want my people to be tricked by mercenaries
In everyman chest, there beats a heart
So soon we'll find out who is the real revolutionary
And I don't want my people to be tricked by mercenaries
Maneno haya na uwezo mkubwa alioonyesha mwanamuziki huyo ulimfanya
Mwalimu Julius Nyerere amualike Bob Marley kuitembelea Tanzania lakini kabla ya
kuitembelea Tanzania Bob alifariki kwa ugunjwa wa Kansa ambapo May 11 1981
alifariki Dunia, Bob alipowasili Zimbabwe alitumia ndege ya Boeing 777 na
vyombo vyake vya music vilikuwa na uzito wa tani 21.
Kila mwanadamu Dunainai ana kitu cha ziada ndani yake na kwa sababuhiyo
tunapaswa kuwaheshimu wenzetu na kutambua kuwa wana umuhimu mkubwa duniani
kulinga ana nafasi zao
Rev. Innocent Kamote.
Mkuu wa wajenzi mwenye hekima.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni