Jumatano, 13 Novemba 2019

Mtu wa Kwenu akipungukiwa na Hekima!


Yakobo 1:5 “Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.”


Utangulizi:
Neno la Mungu linasisitiza sana umuhimu na ubora wa kuwa na Hekima, Kitabu cha Mithali na Muhubiri vimekazia tena na tena vikitoa ushauri, na kuelezea umuhimu wa Hekima na vikisisitiza kuwa ni muhimukwetu kuhakikisha kuwa tunamiliki hekima kwa gharama yoyote ile

Mithali 4:7 “Bora hekima, basi jipatie hekima; Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.”

Wenye hekima wanahitajika kila Mahali, Nyakati za kanisa la kwanza walijua wazi kuwa wakiwepo watu wenye hekima, uko uwezo wa kutatua changamoto za aina mbalimbali zinazolikabili kanisa na dunia kwa ujumla, Wenye hekima walihitajika katika kanisa kwaajili ya kutatua changamoto za aina mbalimbali

1Wakoritho 6:5 “Nasema hayo nipate kuwatahayarisha. Je! Ndivyo, kwamba kwenu hakuna hata mtu mmoja mwenye hekima, awezaye kukata maneno ya ndugu zake?
Matendo 6:1-3 “Hata siku zile wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manung'uniko ya Wayahudi wa Kiyunani juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika huduma ya kila siku. Wale Thenashara wakawaita jamii ya wanafunzi, wakasema, Haipendezi sisi kuliacha neno la Mungu na kuhudumu mezani. Basi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, wenye kujawa na Roho, na hekima, ili tuwaweke juu ya jambo hili;
Mfalme Sulemani pamoja na utajiri na fahari kubwa sana aliyo nayo alikuwa na ufahamu kuwa Hekima ni ya thamani kuliko rubi nay a kuwa hakuna jambo linaweza kulinganishwa na Hekima

Mithali 8:11 “Maana hekima ni bora kuliko marijani; Wala vyote vinavyotamanika havilingani nayo.”
Kwa nini Maandiko yanatuisistiza sana juu ya kuhitaji Hekima

1.      Itatusaidia kujua mema na mabaya katika mtazamo wa Mungu na hivyo itatupa furaha na amani Mithali 3:13-16 “Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu. Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi. Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye. Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto.

2.      Itatusaidia kutatua matatizo yenye utata na kuyapatia ufumbuzi au kuamua vema 1Wafalme 3:16-28 “Ndipo wanawake wawili, makahaba, walimwendea mfalme, wakasimama mbele yake. Na mwanamke mmoja akasema, Ee bwana wangu, mimi na mwanamke huyu tunakaa katika nyumba moja; nami nalizaa nilipokuwa pamoja naye nyumbani. Kisha, siku ya tatu baada ya kuzaa kwangu, ikawa mwanamke huyu naye akazaa; na sisi tulikuwa pamoja; hapakuwa na mtu mwingine pamoja nasi nyumbani, isipokuwa sisi wawili tu. Na mtoto wa mwanamke huyu akafa usiku, maana alimlalia. Akaondoka kati ya usiku, akamwondoa mtoto wangu ubavuni pangu, mimi mjakazi wako nilipokuwa usingizini, akamweka kifuani pake, na mtoto wake mwenyewe, aliyekuwa amekufa, akamweka kifuani pangu. Nilipoondoka asubuhi nimnyonyeshe mtoto wangu, kumbe? Amekufa. Hata asubuhi nilipomtazama sana, kumbe! Siye mtoto wangu niliyemzaa. Ndipo yule mwanamke wa pili akasema, Sivyo hivyo; bali mtoto wangu ndiye aliye hai, na mtoto wako ndiye aliyekufa. Na mwenzake akasema, Sivyo hivyo; bali mtoto wako ndiye aliyekufa, na mtoto wangu ndiye aliye hai. Ndivyo walivyosema mbele ya mfalme. Ndipo mfalme akasema, Huyu anasema, Mtoto wangu yu hai, na mtoto wako amekufa. Na huyu anasema, Sivyo hivyo; bali mtoto aliyekufa ni wako, na mtoto aliye hai ni wangu. Mfalme akasema, Nileteeni upanga. Wakaleta upanga mbele ya mfalme. Mfalme akasema, Mkate mtoto aliye hai vipande viwili, kampe huyu nusu, na huyu nusu. Ndipo mwanamke yule, ambaye mtoto aliye hai ni wake, akamwambia mfalme kwa maana moyoni mwake alimwonea mtoto wake huruma, akasema, Ee bwana wangu, mpe huyu mtoto aliye hai, wala usimwue kamwe. Lakini yule mwingine akasema, Asiwe wangu wala wako; na akatwe. Ndipo mfalme akajibu, akasema, Mpe huyu wa kwanza mtoto aliye hai, maana yeye ndiye mama yake. Na Israeli wote wakapata habari za hukumu ile aliyoihukumu mfalme wakamwogopa mfalme; maana waliona ya kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake, ili afanye hukumu.

3.      Itatusaidia kujibu mafumbo na maswali Magumu 1Wafalme 10:1-3 “Na malkia wa Sheba aliposikia habari za Sulemani juu ya jina la Bwana, alikuja ili amjaribu kwa maswali ya fumbo. Akaingia Yerusalemu na wafuasi wengi sana, na ngamia wachukuao manukato, na dhahabu nyingi sana, na vito vya thamani; alipomfikilia Sulemani, akazungumza naye mambo yote aliyokuwa nayo moyoni. Naye Sulemani akamfumbulia maswali yake yote; wala hakukuwa na neno alilofichiwa mfalme asimwambie.


Napenda tafasiri ya biblia ya kiingereza ya Amplified Bible mahali hapa inasema “SHE  CAME TO TEST HIM WITH HARD QUESTIONS” yaani alikuja kumjaribu kwa maswali Magumu, Lakini Sulemani aliyatatu yote mpaka yaliyofichika nyuma yake.

Wakati huu tunapopitia mitihani, pamoja na majaribu ya aina mbalimbali hapa duniani, ni wazi kuwa tunahitaji Hekima,Yakobo aliyesema tuombe Hekima alikuwa ni moja ya watu muhimu waliotatua matatizo mangi katika nyakati za kanisa la Kwanza,Hekima kubwa ya Mungu ikionekana kukaa juu yake, kwa msingi huo ni kama anatupa majibu yaliyo wazi kuwa ni namna gani tunaweza kuipata Hekima, Yeye anasema ni lazima tuombe, kwamba tukiomba, Mungu hana kizuizi, hawezi kuzuilia hilo, hawezi kukunyima atakupatia, Hekima hii sio ile ya Darasani hii ni Hekima inayoshuka kutoka Mbinguni. Hekima hii itakufaa,katika maeneo mengi ya maisha kuleta suluhu wakati wa mahitaji. Uongezewe neema.

Na Mkuu wa wajenzi mwenye hekima.
Rev. Innocent Kamote
0718990796

Hakuna maoni: