1Samuel 16:10-11 “Yese akawapitisha wanawe
saba mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, Bwana hakuwachagua hawa. Kisha
Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, Amesalia
mdogo wao, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma
watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja huku.”
Utangulizi:
Je wewe umewahi kukataliwa?
Umewahi Kurukwa? Umewahi kufanya kazi kwa bidii sana mahali na kwa moyo wako
wote lakini hakuna mtu aliyetambua mchango wako, na hatimaye ukawa unapuuziwa
tu? Daudi alikuwa mmojawao! Yeye alikuwa
ni kijana wa mwisho kati ya vijana nane wa Mzee Yese, ambaye alikuwa ni Mkulima
na mfugaji kutoka kabila la Yuda huko Bethelehemu, lakini kijana huyu aliyekuwa
mchunga kondoo alipuuzwa tu, hakujaliwa alirukwa, hakuehesabika kuwa ni kitu! Mungu
alipomuagiza Nabii Samuel kwenda kumpaka mafuta mfalme ajaye wa Israel kwa Mzee
aitwaye Yese, kila kijana wa Yese alisogezwa mbele ya Samuel katika ibada
maalumu ya kumtia mafuta mfalme ajae vijana saba wote waliletwa kwa nini kwa
sababu nadhani Karibu wote walikuwa na sifa zinazofaa kwa wao kuwa wafalme na
wanadamu walikubali nadhani hata Samuel aliweza kufikiri wazi kuwa mpakwa
mafuta angekuwepo pale bila shaka ona !
1Samuel 16:1-3 “Bwana akamwambia Samweli,
Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli? Ijaze
pembe yako mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana
nimejipatia mfalme katika wanawe. Samweli akasema, Nawezaje kwenda? Sauli
akipata habari, ataniua. Basi Bwana akasema, Chukua ndama pamoja nawe, ukaseme,
Nimekuja ili kumtolea Bwana dhabihu. Ukamwite Yese aje kwenye dhabihu, nami
nitakuonyesha utakayotenda; nawe utamtia mafuta yule nitakayemtaja kwako.”
1Samuel 16:4-10 “Samweli akafanya hayo
aliyosema Bwana, akaenda Bethlehemu. Wakaja wazee wa mji kumlaki, wakitetemeka,
nao wakasema, Je! Umekuja kwa amani? Naye akasema, Naam, kwa amani; nimekuja
kumtolea Bwana dhabihu; jitakaseni; njoni pamoja nami kwenye dhabihu.
Akawatakasa Yese na wanawe, akawaita kwenye dhabihu. Ikawa walipokuja,
alimtazama Eliabu, akasema, Yakini masihi wa BWANA yupo hapa mbele zake. Lakini
Bwana akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa
maana mimi nimemkataa. Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana
wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo. Ndipo Yese akamwita
Abinadabu, akampitisha mbele ya Samweli. Naye akasema, Bwana hakumchagua huyu.
Ndipo Yese akampitisha Shama. Naye akasema, wala Bwana hakumchagua huyu. Yese
akawapitisha wanawe saba mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, Bwana
hakuwachagua hawa.”
Unaweza kuona kwa vipimo vya
kibinadamu wote waloisogezwa ilifikiriwa kuwa wanafaa lakini hata hivyo kwa
bahati mbaya Mungu hakuwa amewakusudia hao
Mungu alimuonya Samuel kuwa yeye haaangalii kama wanadamu wanavyoangalia
yeye ana mtazamo tofauti na wanadamu kwani yeye anaona tangu moyoni na
hazingatii mtazamo wa nje peke yake!
1Samuel 16:7 “Lakini Bwana akamwambia
Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi
nimemkataa. Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama
sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo.”
Unaona aliyekusudiwa
alidharauliwa, hakuwa ameonekana kuwa na sifa za kimaongozi, hakuna mtu
aliyewajua watoto hawa kwa ukaribu kama
baba na kwa mawazo ya baba mzazi Yese alikuwa anaelewa vizuri sana
watoto wenye kufaa kuongoza Israel pengine mapendekezo yake kwa Samuel na hata
Kwa Mungu tukinena kiwazimu Yese alikuwa sahihi, yeye ni mzazi hivyo anajua ,
aliyebaki alikuwa ni mchungaji wa kondoo na kwa nyakati zile wachungaji wa
kondoo na mifugo hawakudhaniwa kuwa ni watu safi, walikuwa wachafu ni watu wa
porini na ni ngumu kumualika mtu kama huyo kwenye sherehe ya ibada kubwa mbele
ya nabii aliyeheshimika sana Samuel hivyo zilikuwepo kila sababu za kumruka au
kurukwa kwa kijana yule hii inaweza kumtokea mtu awaye yote miaka ya zamani
kufaulu darasa la saba halikuwa jambo rahisi watu wengi sana walirukwa, kwenda
kidato cha tano pia halikuwa jambo rahisi kama ilivyo leo na watu wengi
walirukwa, wenginehawakwenda hata vyuo vya kawaida walirukwa lakini wengi
katika hao Mungu amewatumia kuwa msaada mkubwa kwa taifa letu na makanisani
pia, hapa simaanishi kuwa vyeti vya kitaaluma havina maana hapana hata kidogo
Mungu alikuwa amemuandaa Daudi kwa namna vyingine hukohuko Porini kuwa kijana
jasiri mwenye kuhurumia kondoo ambaye angeweza pia kuwa na huruma kwa kondoo wa
Israel Mungu huwaandaa watumishi wake kwa muda mrefu na wa kutosha ili waweze
kuja kuwa wenye kufaa kwa utumishi aliowakusudia ilimchukua Mungu miaka 80
kumuandaa Musa, Miaka 30 kumuandaa Yohana kwa huduma ya miezi sita tu Paulo
mtume miaka 14 kwaajili ya injili ! Daudi naye alikuwa anaandaliwa kipekee na
Mungu na alikuwa amehitimu shule hiyo ambayo hakuwa amemsimulia mtu na sasa
Mungu anamuona mtu huyu kuwa anafaa lakini kwa vipimo vya kibinadamu anaonekana
kuwa hafai
Wewe ndiye mtu yule !
Kurukwa na wanadamu sio sababu ya Mungu kutokukutumia,
Mungu anamtazamo wake mwingine tofauti sana, Hekima yake ni tofauti sana na
Hekima ya kibinadamu, Mungu huchagua vitu vinyonye, vyenye mapungufu, vilivyodarauliwa
na au kukataliwa katika hekima ya wanadamu ili avitumie kwa utukufu wake ona
1Wakorintho 1:25-29 “Kwa sababu upumbavu wa
Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya
wanadamu. Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye
hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; bali
Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu
alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; tena Mungu
alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo
haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; mwenye mwili awaye yote asije
akajisifu mbele za Mungu.”
Je wewe umewahi kurukwa? Umewahi
kupotezewa? Umewahi kuonekana mbele za watu kuwa hufai hii ilitokea kwa Daudi
mwana wa Yese na inawezekana pia ukawa unakubali moyoni mwako kuwa wewe sio
mkubwa, wewe sio kama kaka zako, wao wana ujuzi mkubwa wao ni safi wewe ni
mchunga mbuzi tu unaweza kujiweka katika daraja lolote la chini unalolitaka na
watu pia wanaweza kukuweka katika mzani huo
lakini Mungu anakuita leo na anataka uchangamke kwa sababu wewe ndiye
mtu yule wewe ndiye uliyechaguliwa wewe ndiye mtumishi wake wewe ndiye mtu yule ambaye Mungu ameona moyo
wako na ndiye mtumishi wake
aliyekuchagua!
Matendo 13:22-23 “Na alipokwisha kumwondoa
huyo, akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona
Daudi, mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayefanya mapenzi yangu
yote. Katika uzao wake mtu huyo Mungu amewaletea Israeli Mwokozi, yaani, Yesu,
kama alivyoahidi;”
Unaona Mungu alimuona Daudi tena
alipendezwa naye na ni kupitia yeye na katika uzao wake Mungu alimleta Yesu
Krito Bwana na Mwokozi wetu Duniani,
Kama Mungu aliweza kumtumia Daudi mchunga kondoo wa kawaida kabisa Mungu
hashindwi kukutumia wewe! Iwe unajidharau au iwe umedharaulika au umerukwa!
Wakati watu wanakutazama kwa
jeuri, na kukuona kama hufai katika eneo hili au lile Yeye aliyekuumba anajua
wapi unafiti kwa sababu ndiye aliyekuumba anakujua kuliko baba yako mzazi,
anakujua kuliko manabii, anajua namna alivyokuandaa anajua uwanja wako wa
mafunzo ya vita ulikuwa wapi na hivyo ni yeye ndiye anayependezwa nawe hata kama wanadamu wanakukataa na kukuona
haufai Mungu aliyekuumba anauona moyo wako naye anapendezwa nawe ona :-
Isaya 49:6-10 “naam, asema hivi, Ni neno
dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuziinua kabila za Yakobo, na kuwarejeza
watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa,
upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia. Bwana, mkombozi wa Israeli,
Mtakatifu wake, amwambia hivi yeye anayedharauliwa na wanadamu; yeye
anayechukiwa na taifa hili; yeye aliye mtumishi wao watawalao; Wafalme wataona,
watasimama; wakuu nao watasujudu; kwa sababu ya Bwana aliye mwaminifu,
Mtakatifu wa Israeli aliyekuchagua Bwana asema hivi, Wakati uliokubalika
nimekujibu, na siku ya wokovu nimekusaidia; nami nitakuhifadhi, nitakutoa uwe
agano la watu hawa, ili kuiinua nchi hii, na kuwarithisha urithi uliokuwa
ukiwa; kuwaambia waliofungwa, Haya, tokeni; na hao walio katika giza,
Jionyesheni. Watajilisha katika njia, na juu ya majabali watapata malisho.
Hawataona njaa, wala hawataona kiu; hari haitawapiga, wala jua; kwa maana yeye
aliyewarehemu atawatangulia, naam, karibu na chemchemi za maji atawaongoza.”
Mungu yuko tayari kumuinua
mtumishi wake anayedharauliwa na wanadamu, anayechukiwa na kumfanya kuwa nuru
kubwa sana kwa mataifa yote na hivi ndivyo alivyomfanyia Daudi ambaye kweli
alidharauliwa lakini sasa ni mwenye sifa kubwa saba duniani, sio yeye tu Hata
kristo alikataliwa na kudharauliwa lakini sasa jina la Yesu ni msaada mkubwa
kwa watu wote duniani, hiki ndicho Mungu anachiokikusudia kwako wewe unayesioma
ujumbe huu na unayepitia changamoto kama hii!
Leo hii hakuna mtu maarufu sana
katika Israel Kama Daudi, Bendera ya Israel ina nyota ya buluu katikati inaitwa
nyota ya Daudi amekuwa ni kiongozi maarufu sana hata Yesu aliitwa mwana wa
Daudi, alitumiwa na Mungu alikuwa na sifa za kiungu, alimsifu Mungu katika
maisha yake, hakufanya jambo bila kumuuliza Mungu, alijaa neno, alikuwa mwenye
msamaha, aliwapenda maadui, alipigana vita vingi vya bwana, alipokosea kama
wanadamu alitubu, alijinyeneykeza kwa Mungu na Mungu alimtumia katika watu
ambao Mungu anajivunia kuwa anapendezwa nao Daudi alikuwa ni mmoja wao, Mungu
anakuamini anajua utatenda kwa busara naye atakuinua juu nawe utakuwa juu sana
Isaya 52:13 “Tazama, mtumishi wangu
atatenda kwa busara, atatukuzwa, na kuinuliwa juu, naye atakuwa juu sana”
Kama ilivyo kwa Daudi Endelea
kuwa hodari, jifunze njia za Mungu, mwamini Mungu jiungamanishe na Mungu katika
dua na sala na maombi Na Mungu yule nimwabuduye kwa dhamiri safi atakutokea na kuifuta aibu yako na kukuweka panapo nafasi
na kukuinua juu sana kama yeye mwenyewe alivyokuandaa kwa utukufu wake !
Na Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima. !
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni