Mwezi juni 6-20 mwaka huu nilipata neema ya kutembelea Marekani, ambalo ni moja ya Mataifa makubwa na Yenye Kuheshimika sana Duniani, katika siku chache nilizokuweko huko katika program iliyoitwa Vision Trip makusudi yetu makubwa ilikuwa ni kujifunza Maswala Mbalimbali na kasha kuja na kuyatumia yale yatakayoweza kutuletea maendeleo makubwakatika taifa letu, Mimi na wanafunzi wangu tuliotembelea huko tulikuwa tunataka kujua chanzo cha Maendeleo ya wenzetu na kisha tutumie ujuzi huo kuendeleza Taifa Letu kama viongozi wa sasa na wa baadaye
Moja
ya maswala Muhimu yaliyosababisha taifa hili kuendelea ni pamoja na kupata
neema ya kuwa na Viongozi Bora! Msingi mkubwa wa Taifa hili uliwekwa na rais wa
Kwanza Mzee George Washington mzee huyu alikuwa anamcha Mungu na Hivyo Mungu
aliwekwa mbele katika taifa hili na ndio msingi wa maendeleo makubwa kwenye
taifa hili, hata hivyo leo nataka kumzungumzia
moja ya viongozi muhimu sana ambaye anawekwa katika orodha ya Maraisi
wakubwa sana wa Marekani wanaoheshimika the Greatest Presidents of United
States Huyu si mwingine bali ni Abraham Lincoln
Abraham Lincoln
Nilianza
kuhisi umuhimu wa Rais huyu wa Marekani hata kabla sijaingia Marekani kwenyewe
kwani tulipokuwa tumeomba Visa na kufanikiwa kuipata nilitamani kuona Visa ya
kimarekani ikoje kwa vile upatikanaji wake nimtihani nilipochungilia visa hiyo
haraka sana niliona Jengo muhimu sana lenye kuashiria makao makuu ya serikali
ya Marekani US Capitol na picha ya Rais huyo wa zamani wa Marekani, licha ya
kuwamo katika mamlaka hayo ya utoaji visa pia Lincon anaonekana katika baadhi
ya fedha za Kimarekani Dollar
Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima Rev Innocent Kamote akiwa Marekani, Jijini Washington nyuma ni sanamu ya Abraham Lincoln moja ya maraisi wanaoheshimika sana Nchini humo
Na
tulipofika Marekani pale Washington moja ya maeneo tuliyotembezwa ilikuwa ni
pamoja na Hekalu kubwa lijulikanalo kama Abraham Lincoln Memorial nikataka kujua undani wa Rais huyu na kwa
nini anatukuzwa sana na kusifiwa? Licha ya kutembelea Makumbusho yake pia
nilifika eneo alikouawa na Kupigwa risasi nilikuta watu wengi wanatembelea hapo
who is Abraham Lincoln Huyu jamaa ni nani
Abraham
Lincoln Ni rais wa 16 wa Marekani, alilitumikia taifa hilo mwezi March 1861
mpaka alipouawa April 1865, rais huyu aliongoza Marekani katika wakati mgumu
kwani kulikuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilimwaga damu za wengi,
Majimbo saba ya kusini walitangaza kujitenga mara moja mara baada ya kuapishwa
kwa Lincoln wakijua kuwa angekomesha shughuli za watumwa, pamoja na kuwa
aliongoza katika kipindi kifupi sana Rais huyu alifanikiwa kulijenga Taifa hili
Kimaadili, hivyo wamarekani walikuwa na kiwango cha juu sana cha maadili wakati
wake, aliimarisha umoja wa Majimbo yote ya marekani, aliimarisha Katiba na
kumaliza kabisa migogoro ya kisiasa iliyokuweko kwa kufanya hivyo alifanikiwa
sana katika kujenga umoja wa kitaifa wa Taifa la Marekani unayoiona Leo.
Moja
ya Maswala yaliyompa heshima mkubwa huyo pia ni pamoja na kukomesha Biashara ya
Utumwa na ubaguzi Amerika alisema “hatuwezi kuwa na uhuru wa kweli katika taifa
ambalo wengine ni Mabwana na wengine ni watumwa” Hatuwezi kuwana taifa ambalo
wengine wanafurahia uhuru huku wengine wakiwa ni watumwa!”
Licha
ya kupngwa na baadhi ya watu waliokuwa wakiwatumia watumwa kwa faida zao,
Lincoln ni chanzo kikuu cha kuimarika kwa Uchumi wa wamarekani walio nao leo
ndani ya kipindi kifupi alichoonngoza, aliimarisha sekta ya Viwanda,
aliimarisha Mabenki, alijenga Mifereji ya kupita chini kwa chini, alijenga reli
na kuimarisha ukusanyaji wa kodi, Lincoln alikataa pia kupigana vita au kusaini
vita kati ya Marekani na Mexico mnamo mwaka 1846.
Abraham Lincoln
Alizaliwa
mwala 1809 na kuuawa mwaka 1865, alitokea katika Familia masikini nay a kawaida sana Babu yake Samuel
Lincoln alihamia kutoka Uingereza, Baba yake aliitwa Thomas Lincolin Abraham
Lincoln hakuweza kupata hata elimu ya awali katika familia yake na hivyo
alijiendeleza mwenyewe kwa kufanya kazi na kujisomesha, alisoma kwa kutumia taa
ya mafuta ya taa, al;ijiendeleza na kufanikiwa kuwa mwanasheria na baadaye
kujiunga na siasa nyumba aliyoishi na familia yao mwanzoni ilikuwa ya mbao na
yenye chumba kimoja tu, alipojiunga na siasa Lincoln alikuwa na Ushawishi
mkubwa sana kiasi ambacho ukimsikiliza akizungumza unakubali kuwa yaya ni
kiongozi, alikuwa na uwezo wa kujenga hojana mwenye uwezo mkubwa sana wa
Ushawishi, Familia yao ilihamia huko Illinois Jimbo analotokea rais wa Sasa wa
Marekani Barak Obama, alipofanikiwa kuwa rais aliondoka Illinois kuelekea
Washington akitumia Treni jambo ambalo limewahi kuigizwa na Kiongozi wa sasa wa
Marekani.
Nikiwa mahali alipopigwa risasi na nyumba aliyofia Abraham Lincoln angalia kibao juu ya kichwa changu hapo juu
sasa waweza kukiona kwa ukaribu House where Lincolin Died yaani Nyumba ambayo Lincolin alifia
Aliingia
madarakani akiwa haeshimiki sana lakini amepokea Heshima kubwa na nyingi sana
baada ya kuuawa kwake, Pamoja na Lincolin kuwa mwanademocrasia mkubwa katika
unenaji alikuwa na Madaraka makubwa kuliko raisi yeyote wa marekani
aliyepatakuweko kiasi ambacho kimaamuzi ni kama alikuwa Dikteta. Nanaheshimika
sana kwa kiwango ambacho jamii kubwa hutembelea Makumbusho yake wakiwemo
wayahudi, waasia na watu wa mataifa Mengineyo
Lincolin
aliuawa kwa kupigwa risasi na wanaosadikiwa kuwa wapinzani wake hususani wa
sera ya kukataa kumiliki watumwa wa majimbo ya kusini, aliyemuua alijulikana
kwa jina la John Wilkes Booth tarehe 14 April 1865 siku ya Ijumaa kuu wakati
alipokuwa ametembelea Ford Theatre Washington Booth alikuwa amechukizwa
alipomsikia Lincoln akizungumza na alikuwa amakusudia kumteka lakini
aliposhindwa aliamua kumuua, wakati wa Pasaka hata hivyo lincolin alifariki
asubuhi yake Tarehe 15 April 1865 saa moja na dakika 20. Siku ya kuuawa kwake
mapema alikuwa na Mawaziri wake na aliwaeleza ndoto yake aliyoiota usiku na
wakaitafasiri kuwa ni ya ushindi dhidi ya Sherman na kuwa vita hiyo imefikia
mwisho, siku hiyo Rais Lincoln alionekana mwenye furaha kuliko kawaida hata
waliomuona walisema haijawahi kuonekana akiwa na Furaha kiwango hicho Lincoln
alizikwa nyumbani kwake Springfield kwa Hesmika kubwa za kijeshi, Katika Maraisi
wa Marekani hakuna Rais amabaye amaewahi kuandikwa nn maandishi mengi sana Kama
ilivyo kwa Abraham Lincolin
Mambo ya kujifunza:
1. Kiongozi bora haitaji miaka mingi
sana ili aweze kufanya mambo mazuri Lincoln aliweza kufanya mambo mengi mazuri
huku akiwa na kipindi kidogo cha uongozi
2. Kuweko kwa matatizo hakuzuii
shughuli za maendeleo Lincolin aliweza kuleta maendeleo licha ya kuweko na
vikwazo na kuwa na wakati mgumu ni vema viongozi wa afrika tukakubali kuwa
Mbaazi zikikosa Mvua husingizia jua, kwa Lincoln changamoto alizokuwa nazo
hazikuzuia yeye kusababsha maendeleo
3. Nguzo ya maadili ni nguzo muhimu
sana kwaajili ya kujenga ufanisi wa kazi
4. Taifa lisilokusanya kodi au kutoa
mianya ya misamaha ya kodi na ubadhirifu kuendelea kwake ni menemene tekeli na
peresi
5. Viongozi wasiojali matumizi
mabaya ya mali za umma matumizi mabaya ya Magari ya serikali watajifunza kwa
Lincoln aliyeamua kwenda ikulu akitumia treni
6. Mwisho nimejifunza kuwa kama
Tukiwatumikia watu kwa moyo wetu wote bila kujali ni vikwazo gani tunakutananavyo
nkatika maisha yetu ama upinzani toka kwa maadui heshima itatufuata siku zote
za maisha yetu hata tujapokufa tutakuwa tungali tunaishi Lincoln anakumbukwa na
kuhesimiwa na watu Milele