Jumanne, 26 Januari 2016

UJUMBE: KUVIKWA UWEZO UTOKAO JUU



Luka 24:49 “Na tazama nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu lakini kaeni humu mjini, Hata MVIKWE uwezo utokao juu”
Leo nataka kuzungumzia Jambo la Muhimu sana kuhusu Ujazo wa Roho Mtakatifu  ambalo kwa kawaiada wahubiri wengi pamoja na kanisa huwa hawalizungumzii, wanapofundisha kuhusu Roho mtakatifu au alama zinazotumika kumuelezea au kuelezea kazi za Roho mtakatifu, na alama hii  au kielelezo hini kinatokana na neon “MVIKWE” Neno hilo ukilichunguza kwa makini lina uhusiano na tendo la kuvaa au kuvikwa ambapo ndani yake kuna neon vazi

Ni muhimu kama wanafunzi wa Biblia kujiuliza kwa nini Yesu anaunganisha tendo la kumpokea au kujazwa nguvu za Roho Mtakatifu na neon kuvikwa au vazi? Hii ni Lugha ya kinabii, kwa Kawaida Biblia inapozungumzia kuhusu Vazi, inazungumzia kuhusu Heshima au Mamlaka ni hesima gani na mamlaka gani ni muhimu kuelewa!

Mara baada ya Adam na Hawa kufanya dhambi, utakumbuka mara moja walipoteza heshima na mamlaka na kupungukiwa na utukufu wa Mungu na hivyo walijitambua na kujiona kuwa wako UCHI
Mwanzo 3:10,21.

Lugha za kinabii katika maandiko zinatufundisha kuwa Vazi lina uhusiano mkubwa sana HESHIMA ama  kuipata au Kuipoteza:
Biblia imejaa mifano kadhaa inayoonyesha Lugha ya KInabii kuhusu Vazi

Mfano
1.       Yusufu alitengenezewa Vazi maalumu na Baba yake kama alama ya heshima na kibali kutoka kwa baba yake  Mwanzo 37:1-3
2.        Vazi hilo lilipata mashambulizi na kuonyesha kuwa ametoweka Mwanzo 37:31-33
3.       Baadaye alipata heshima nyingine kutoka kwa Potifa Mwanzo 37:1-5
4.       Heshima hiyo iliharibiwa kwa Mke wa Potifa na akakimbia na kuacha vazi Mwanzo 39:11-15
5.       Mungu aliirudisha Heshima ya Yusuphu na akavikwa mavazi tena Mwanzo 41:41-43
Mavazi pia yanazungumzia Heshima ya Kifalme katika Ufalme wa Mungu 1Samuel 15:27-29 Vazi linaporaruliwa maana yake ufalme umeondolewa!
Vazi linawakilisha Heshima, mamlaka, Ufalme na ndio maana wanafunzi wanapohitimu huvaa mavazi maalumu ya kuonyesha kuwa wanastahili heshima hiyo Vazi lina ashiria Upako 1Wafalme 19:19-21, 2Wafalme 2:11-15
Yesu alippokari bia kupaa mbinguni aliahidi kuwa atatuachia Roho wake mtakatifu maana yeke
Anatuachia Heshima ambayo wanadamu waliipoteza
Anatupa mamlaka  ambayo Adamu aliipoteza
Mtu anapompokea Roho Mtakatifu anapokea Heshima, mamlaka, utawala, ufalme, upako, uwezo na   nguvu na aibu yake inaondolewa, Ndio maana Yesu akawaambie msitoke Humu mjini mpaka mmevikwa uwezo utokao juu Yaani Roho Mtakatifu, anafaida nyingi katika masisha ya Ukristo analeta Heshima na kufunika aibu!

Maoni 2 :

Unknown alisema ...

Ubarikiwe mtumishi kwa somo zuri,

Bila jina alisema ...

Amina