Ruthu 1 : 19-22
Biblia inasema hivi:-
“19. Hivyo hao wakaendelea wote
wawili hata walipofika Bethlehemu. Na ikawa walipofika Bethlehemu, mji wote
ulitaharuki kwa habari zao. Nao wanawake wakasema, Je! Huyu ni Naomi? 20.
Akawaambia, Msiniite Naomi niiteni Mara,kwa sababu Mwenyezi Mungu amenitenda
mambo machungu sana.21. Mimi nalitoka hali nimejaa, naye Bwana amenirudisha
sina kitu, kwani kuniita Naomi, ikiwa Bwana ameshuhudia juu yangu, na Mwenyezi Mungu
amenitesa?
Nyakati za Biblia hususani nyakati za
agano la kale watu wengi sana walipopatwa na mabaya walifikiri kuwa mabaya hayo
yanatoka kwa Mungu, ni muhimu kufahamu kuwa mambo mabaya na machungu sana
hutoka kwa Yule Muovu, lakini hata hivyo wakati mwingine ni kwa ruhusa ya
Mungu, Mungu huweza kuruhusu mabaya yatupate kwaajli ya utukufu wake, na katika
nyakati nyingine Mungu katika hekima yake huweza kuyatumia mambo mabaya ili
kutuletea mambo mema!
Katika Mistari ile tuliyoisoma
Ruthu 1:19-22 tumesoma habari za mwanamke aliyeitwa Naomi (mwenye kupendeza
ndio maana ya Jina lake) akirudi Bethelehem na mkwewe wakiwa katika hali ngumu
sana na wimbi la umasikini na kufilisika huku kila mmoja akiwa hajui maisha
yake yatakuwaje mbeleni (No feature), Matumaini yake yote aliyokuwanayo
yalitoweka, alikuwa na uchungu uliokuwa umemzunguka na ni uchungu wa mauti tu
na hakukuwana tumaini la uhai, jumla ya mawazo yake ni kuwa Mwenyezi Mungu
amemtenda mambo machungu sana
Ruthu 1-13 aliona ni kama mkono
wa Bwana umeondoka juu yake ni kama vile Mungu hashughuliki naye tena
Alikuwa na Mume aliyeitwa Elimeleki Maana yake Mungu ndiye Mfalme au
Mtawala
Alikuwa na mtoto wa kiume mkubwa aliyeitwa Maloni maana yake Magonjwa
Na wa kiume mdogo aliyeitwa Kilioni maana yake Kufilisika
Historia ya Familia hii inaonekana kama waliokuwa wakijaribu kuokoa
maisha yao kwa vile walikimbia njaa katika nchi ya Israel huko Bethelehem na
kuelekea nchi ya Moabu Jordani ya leo kwaajili ya chakula lakini familia hii ilikutana na wakati mgumu kwani
ni wazi kuwa wakati Maloni anazaliwa ilikumbwa na magonjwa mazito na labda ndio
maana walimpa mtoto wao jina hilo na
huenda walipokuwa huko moabu walifilisika kabisa na ndio maana walimuita mtoto
wa pili kilioni yaani kufilisika na kama haitoshi ingawa kilioni na maloni
walioa mara Baba yao alifariki, kisha Maloni na kisha kilioni bila kuacha
watoto, na Naomi alijikuta maebaki na wakwe vijana Orpa na Ruthu, katika hali
ya mashaka makubwa Naomi aliwasihi wakweze kurejea makwao katika hali ya ukwasi
mkubwa Orpa alikubali huyu alikuwa mke wa Maloni na Ruthu alikazia kubakia na
mkwewe huyu alikuwa mke wa kilioni
Hali ya Naomi ilikuwa ni ya kusikitisha nay a majonzi mno hakutamani
tena kuitwa Naomi bali mara yaani machungu, mkwewe alifuatana naye katika hali
hiyo ya umauti na kukosekana kwa matumaini, kazi kubwa aliyofanya ni kuokota
ngano na masazo yaliyosazwa na waliovuna Ngono huko Bethelehemu
Mkwe wa naombi Ruthu aliyekuwa mwaminifu na kuendelea kumtunza mkwewe
hatakatika hali ya umasikini na shida alipata mchumba na kuolewa sawa na
desturi zao na Mchumba huyu aliitwa Boazi na baada ya kumuoa Ruthu walipata
mtoto wa kiume na Kumuita Obedi yaani Kurejezewa Uhai! Huyu Obedi alimzaa Yese
na Yese alimzaa Mfalme Daudi
Msomaji wangu mpendwa Mungu huweza kuruhusu mambo machungu yatupate,
na wakati mwingine tukafikiri kuwa umefika mwisho wetu, hatuwezi kuinuka tena
hata maadui zetu na wale wasiotutakia mema wanaweza kufikiri kuwa mwisho wetu
umefika, lakini ninazo habari njema kwako leo kuwa Mungu amerejeza Uhai,
haijalishi ni magumu kiasi gani unapitia Mungu yuko Nyuma ya mambo ili
kusababisha mambo mema yatokee Na ndio
maana njia zake hazichunguziki wala mawazo yake si kama ya wanadamu njia zake ziko juu sana na hekima
yake kwa wanadamu ni ujinda Lakini upumbavu wa Mungu una hekima kuliko Hekima
ya wanadamu Hatupaswi kumlaumu Mungu kwa lolote tunalolipitia au linalotutokea,
Mshukuru Mungu kwa Kila Jambo
Na Rev. Innocent Kamote Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni