Jumanne, 26 Januari 2016

Abraham Lincoln ni nani? (who is Abraham Lincoln)


Mwezi juni 6-20 mwaka huu nilipata neema ya kutembelea Marekani, ambalo ni moja ya Mataifa makubwa na Yenye Kuheshimika sana Duniani, katika siku chache nilizokuweko huko katika program iliyoitwa Vision Trip makusudi yetu makubwa ilikuwa ni kujifunza Maswala Mbalimbali na kasha kuja na kuyatumia yale yatakayoweza kutuletea maendeleo makubwakatika taifa letu, Mimi na wanafunzi wangu tuliotembelea huko tulikuwa tunataka kujua chanzo cha Maendeleo ya wenzetu na kisha tutumie ujuzi huo kuendeleza Taifa Letu kama viongozi wa sasa na wa baadaye
 
Moja ya maswala Muhimu yaliyosababisha taifa hili kuendelea ni pamoja na kupata neema ya kuwa na Viongozi Bora! Msingi mkubwa wa Taifa hili uliwekwa na rais wa Kwanza Mzee George Washington mzee huyu alikuwa anamcha Mungu na Hivyo Mungu aliwekwa mbele katika taifa hili na ndio msingi wa maendeleo makubwa kwenye taifa hili, hata hivyo leo nataka kumzungumzia  moja ya viongozi muhimu sana ambaye anawekwa katika orodha ya Maraisi wakubwa sana wa Marekani wanaoheshimika the Greatest Presidents of United States Huyu si mwingine bali ni Abraham Lincoln

Abraham Lincoln
Nilianza kuhisi umuhimu wa Rais huyu wa Marekani hata kabla sijaingia Marekani kwenyewe kwani tulipokuwa tumeomba Visa na kufanikiwa kuipata nilitamani kuona Visa ya kimarekani ikoje kwa vile upatikanaji wake nimtihani nilipochungilia visa hiyo haraka sana niliona Jengo muhimu sana lenye kuashiria makao makuu ya serikali ya Marekani US Capitol na picha ya Rais huyo wa zamani wa Marekani, licha ya kuwamo katika mamlaka hayo ya utoaji visa pia Lincon anaonekana katika baadhi ya fedha za Kimarekani Dollar 
Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima Rev Innocent Kamote akiwa Marekani, Jijini Washington nyuma ni sanamu ya Abraham Lincoln moja ya maraisi wanaoheshimika sana Nchini humo

Na tulipofika Marekani pale Washington moja ya maeneo tuliyotembezwa ilikuwa ni pamoja na Hekalu kubwa lijulikanalo kama Abraham Lincoln Memorial  nikataka kujua undani wa Rais huyu na kwa nini anatukuzwa sana na kusifiwa? Licha ya kutembelea Makumbusho yake pia nilifika eneo alikouawa na Kupigwa risasi nilikuta watu wengi wanatembelea hapo who is Abraham Lincoln Huyu jamaa ni nani

Abraham Lincoln Ni rais wa 16 wa Marekani, alilitumikia taifa hilo mwezi March 1861 mpaka alipouawa April 1865, rais huyu aliongoza Marekani katika wakati mgumu kwani kulikuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilimwaga damu za wengi, Majimbo saba ya kusini walitangaza kujitenga mara moja mara baada ya kuapishwa kwa Lincoln wakijua kuwa angekomesha shughuli za watumwa, pamoja na kuwa aliongoza katika kipindi kifupi sana Rais huyu alifanikiwa kulijenga Taifa hili Kimaadili, hivyo wamarekani walikuwa na kiwango cha juu sana cha maadili wakati wake, aliimarisha umoja wa Majimbo yote ya marekani, aliimarisha Katiba na kumaliza kabisa migogoro ya kisiasa iliyokuweko kwa kufanya hivyo alifanikiwa sana katika kujenga umoja wa kitaifa wa Taifa la Marekani unayoiona Leo.
Moja ya Maswala yaliyompa heshima mkubwa huyo pia ni pamoja na kukomesha Biashara ya Utumwa na ubaguzi Amerika alisema “hatuwezi kuwa na uhuru wa kweli katika taifa ambalo wengine ni Mabwana na wengine ni watumwa” Hatuwezi kuwana taifa ambalo wengine wanafurahia uhuru huku wengine wakiwa ni watumwa!”
Licha ya kupngwa na baadhi ya watu waliokuwa wakiwatumia watumwa kwa faida zao, Lincoln ni chanzo kikuu cha kuimarika kwa Uchumi wa wamarekani walio nao leo ndani ya kipindi kifupi alichoonngoza, aliimarisha sekta ya Viwanda, aliimarisha Mabenki, alijenga Mifereji ya kupita chini kwa chini, alijenga reli na kuimarisha ukusanyaji wa kodi, Lincoln alikataa pia kupigana vita au kusaini vita kati ya Marekani na Mexico mnamo mwaka 1846.
Abraham Lincoln
Alizaliwa mwala 1809 na kuuawa mwaka 1865, alitokea katika Familia  masikini nay a kawaida sana Babu yake Samuel Lincoln alihamia kutoka Uingereza, Baba yake aliitwa Thomas Lincolin Abraham Lincoln hakuweza kupata hata elimu ya awali katika familia yake na hivyo alijiendeleza mwenyewe kwa kufanya kazi na kujisomesha, alisoma kwa kutumia taa ya mafuta ya taa, al;ijiendeleza na kufanikiwa kuwa mwanasheria na baadaye kujiunga na siasa nyumba aliyoishi na familia yao mwanzoni ilikuwa ya mbao na yenye chumba kimoja tu, alipojiunga na siasa Lincoln alikuwa na Ushawishi mkubwa sana kiasi ambacho ukimsikiliza akizungumza unakubali kuwa yaya ni kiongozi, alikuwa na uwezo wa kujenga hojana mwenye uwezo mkubwa sana wa Ushawishi, Familia yao ilihamia huko Illinois Jimbo analotokea rais wa Sasa wa Marekani Barak Obama, alipofanikiwa kuwa rais aliondoka Illinois kuelekea Washington akitumia Treni jambo ambalo limewahi kuigizwa na Kiongozi wa sasa wa Marekani.
 
Nikiwa mahali alipopigwa risasi na nyumba aliyofia Abraham Lincoln angalia kibao  juu ya kichwa changu hapo juu


sasa waweza kukiona kwa ukaribu House where Lincolin Died yaani Nyumba ambayo Lincolin alifia


Aliingia madarakani akiwa haeshimiki sana lakini amepokea Heshima kubwa na nyingi sana baada ya kuuawa kwake, Pamoja na Lincolin kuwa mwanademocrasia mkubwa katika unenaji alikuwa na Madaraka makubwa kuliko raisi yeyote wa marekani aliyepatakuweko kiasi ambacho kimaamuzi ni kama alikuwa Dikteta. Nanaheshimika sana kwa kiwango ambacho jamii kubwa hutembelea Makumbusho yake wakiwemo wayahudi, waasia na watu wa mataifa Mengineyo


Lincolin aliuawa kwa kupigwa risasi na wanaosadikiwa kuwa wapinzani wake hususani wa sera ya kukataa kumiliki watumwa wa majimbo ya kusini, aliyemuua alijulikana kwa jina la John Wilkes Booth tarehe 14 April 1865 siku ya Ijumaa kuu wakati alipokuwa ametembelea Ford Theatre Washington Booth alikuwa amechukizwa alipomsikia Lincoln akizungumza na alikuwa amakusudia kumteka lakini aliposhindwa aliamua kumuua, wakati wa Pasaka hata hivyo lincolin alifariki asubuhi yake Tarehe 15 April 1865 saa moja na dakika 20. Siku ya kuuawa kwake mapema alikuwa na Mawaziri wake na aliwaeleza ndoto yake aliyoiota usiku na wakaitafasiri kuwa ni ya ushindi dhidi ya Sherman na kuwa vita hiyo imefikia mwisho, siku hiyo Rais Lincoln alionekana mwenye furaha kuliko kawaida hata waliomuona walisema haijawahi kuonekana akiwa na Furaha kiwango hicho Lincoln alizikwa nyumbani kwake Springfield kwa Hesmika kubwa za kijeshi, Katika Maraisi wa Marekani hakuna Rais amabaye amaewahi kuandikwa nn maandishi mengi sana Kama ilivyo kwa Abraham Lincolin 

Mambo ya kujifunza:
1.      Kiongozi bora haitaji miaka mingi sana ili aweze kufanya mambo mazuri Lincoln aliweza kufanya mambo mengi mazuri huku akiwa na kipindi kidogo cha uongozi
2.      Kuweko kwa matatizo hakuzuii shughuli za maendeleo Lincolin aliweza kuleta maendeleo licha ya kuweko na vikwazo na kuwa na wakati mgumu ni vema viongozi wa afrika tukakubali kuwa Mbaazi zikikosa Mvua husingizia jua, kwa Lincoln changamoto alizokuwa nazo hazikuzuia yeye kusababsha maendeleo
3.      Nguzo ya maadili ni nguzo muhimu sana kwaajili ya kujenga ufanisi wa kazi
4.      Taifa lisilokusanya kodi au kutoa mianya ya misamaha ya kodi na ubadhirifu kuendelea kwake ni menemene tekeli na peresi
5.      Viongozi wasiojali matumizi mabaya ya mali za umma matumizi mabaya ya Magari ya serikali watajifunza kwa Lincoln aliyeamua kwenda ikulu akitumia treni
6.      Mwisho nimejifunza kuwa kama Tukiwatumikia watu kwa moyo wetu wote bila kujali ni vikwazo gani tunakutananavyo nkatika maisha yetu ama upinzani toka kwa maadui heshima itatufuata siku zote za maisha yetu hata tujapokufa tutakuwa tungali tunaishi Lincoln anakumbukwa na kuhesimiwa na watu Milele

Hakuna maoni: