HITAJI LA KUWA NA MTAFASIRI WA MAANDIKO
Wako watu ambao wanaweza kusema kwa
hisia zao kubwa kuwa hatuhitaji kuitafasiri Biblia kinachohitajika ni kuisoma
na kutenda kile ilichoagiza kwa kawaida huu unaweza kuwa usemi wa kawaida wa
watu wa kawaida tu na watu wa jinsi hii wanaweza kuwachukia wasomi au
wachungaji na waalimu wanaosisitiza umuhimu wa kuitafasiri Biblia wanaweza
kuonekana wako kimwili zaidi na labda wanataka kujitukuza kwa kuifanya Biblia
isionekane kuwa ya kawaida kwa watu wa kawaida kitaalamu tunasema mawazo hayao
ni ya watu punguani wenye nusu ubongo kwani wakati mwingine kile tunachofikirti
kuwa ni sahii tunapokisoma kinaweza kuwa sio sahii na hivyo mtafasiri
anahitajika.
SIFA ZA MSINGI ZA MTAFASIRI WA MAANDIKO;
A. SIFA
ZA KIROHO;
1. Lazima awe amezaliwa mara ya pili
ameokoka– Yohana 3:1-8 kuzaliwa mara ya pili pia kunahusisha Kuzaliwa kwa Neno
au maji mtu ambaye haja zaliwa kwa neno kamwe hawezi kuwa mtafasiri mzuri wa
Maandiko kwa sababu hajaungwa na asili ya Mungu ambayo ni Neno.
2. Awe na kiu na hamu na shauku ya
kulijua neno la Mungu– Mathayo. 5:6, Ps. 119:97 Biblia inaonyesha ya kuwa ukiwa
na kiu ya kitu utazidishiwa lakini ukifikiri ya kuwa unacho hata kile
ulichozani unacho kitachukuliwa mtu anayehitaji kuyatafasiri Maandiko ni lazima
awe na kiu
3. Awe mtu aliyepondeka kwa Neno la Mungu
– Isaya 66:2. Watu walio wanyenyekevu wanaolihofu neno la Mungu mungu
nhuwaangalia hao na hivyo ni rahisi kwa Mungu kujifunua kwao Mungu huwapingwa
wenye kiburi bali huwapa wanyenyekevu neema unyenyekevu ni moja ya njia
inayokusaidia kuipokea mambo ya rohoni kutoka kwa Mungu na kwa wanadamu wwenye
ujuzi
4. Awe mtu anaye mtegemea Roho
Mtakatifu na maongozi yake– 1Kor. 2:10-14, Yohana 16:13-14 Paulo anaelezea
vizuri kuwa mtu ambaye hajazaliwa kwa Roho katika 1Wakoritho 2; 10-14 hawezi
kuyatambua mabo ya Rohoni kwani kwae huyo ni upuuzi,Paulo anatumia neno kali
sana kuhusu kulipokea Neno la Mungu kwa Mtu wa rohoni yaani
- Dechomai - yaani kulipokea kwa shauku kubwa inayotokana na Roho wa Mungu na sio
- Lambano - kulipokea juujuu,au katika haliya kawaida au
- Ginosko - kulipokea kwa akili za kibinadamu Ufahamu wa kawaida wa kisayansi na kisomi au
- Oida - Ufahamu mwepesi wa kiakili
B.
SIFA
ZA KUWA NA AKILI TIMAMU
1.
Je Mtafasiri ana akili timamu au ni –
Mgerasi? (au mtu mwenye kutegemea ndoto na Maono?)
2.
Anapenda kujifunza? Au ana shingo
ngumu?
C.
SIFA
ZA KIELIMU
1. Awe na elimu ya ujumla wa mambo yote
(a) Tamaduni, Mila desturi tabia za
mwanadamu, n.k
(b) Sayansi (c) Sanaa na Ubunifu. ( d) Saikolojia.
2.
Kuwa na maarifa kuhusu maswala ya kihistoria katika.
(a) Falsafa (b) Jiografia
(c). Siasa & (d) Historia.
3.
Kuwa na ujuzi kuhusu lugha zilizotumika kuleta Biblia
(a) Kiebrania (b) Kiyunani
(c) Kiaramu. (d) Kilatini
4.
Kuwa na ujuzi kuhusu Theolojia yaani Elimu kuhusu Mungu.
(a) Misamiati ya kitheolojia
(b) Ufahamu kuhusu Agano la kale na Agano
jipya
5. Mwenye bidii sana katika maswala ya
Kujisomea.
(a)
Biblia yenyewe na Vitabu vinavyosaidia kusaidia kutafasiri Biblia na
Vitabu vingine vya kiroho.
NYENZO MUHIMU ZINAZOSAIDIA KATIKA
KUYATAFASIRI MAANDIKO KWA USAHIHI
A. ROHO
MTAKATIFU;
1. Ni nyenzo ya kwanza na ya Muhimu sana mtu awaye yote
anayetaka kuwa mtafasiri mzuri wa Maandiko ni lazima akubali kujazwa Roho
mtakatifu kumbuka kuwa yeye ndiye aliyevuvia watu kuliandika neno na ni mwalimu
anaweza kutukumbusha na kutufundisha kile ambacho Mungu amekikusudia kwetu
hivyo lazima mtafasiri wa maadniko awe amejazwa Roho ikiwa wale waliokuwa
mashemasi nyakati za kanisa la kwanza walizingatiwa kuwa wenye Roho je si zaidi
sana wanaojitia katia kazi ya kuyatangaza Maandiko ona mfano wa Stefano Matendo
6;8-55 kwanini ni muhimu kuwa na Roho mtakatifu?
2. Ni Mtafasiri mzuri
(a) Ndiye Mwandishi wa Biblia 1Kor. 2:10-16, Yoh 14:26, 16:13
(b) Anajua kile Ambacho Mungu anakijua
B. HAKIKISHA KUWA UNA BIBLIA ZA MATOLEO
TOFAUTI
1.
Biblia ya Kiswahili na za aina mbalimbali za matoleo ya kiswahili cha kisasa
2. English Bible matoleo tofauti
3. Zile zilizoandikwa katika Lugha Tofauti
Tofauti (Greek, Hebrew, Latin, Aramaic, etc)
C. UWE NA UJUZI KUHUSU AINA ZA MATOLEO
YA BIBLIA
Kwa kawaida kuna matoleo makuu ya aina tatu za
kibiblia zile zilizotafasiri neno kwa neno Literal translations, Zile
zilizotafasiri kutokana na maana iliyokusudiwa, Dynamic Equivalent na zile tafasiri
huru za lugha za kisasa Free translation
Literal translations Dynamic Equivalence translations Free translations
KJV, RSV,
Weymoth, NIV JB TEV, MOFFAT,
PHILIPS, LB
NASB NAB NEB
NEB GNB
Neno kwa neno Maana kwa maana Tafasiri huru
D.
D. UWE NA BIBLIA ZENYE MAFUNZO NDANI YAKE ; REFERENCE
OR ANNOTATED
·
Uwe na Biblia zenye mafunzo Studies
Bible Zinatoa maana ya baadhi ya aya:
(i) Mfano mzuri ni Full life study Bible
(NIV)Biblia ya mafunzo ya uzima tele
(ii) Life Application Bible (LB)
(iii) Dake Bible
(iv) Scafield Bible, etc.
E.
COMMENTARIES: (Zenye uchambuzi wa mstari
kwa mstari).
Baadhi ya Commentaries nzuri ni Pamoja na
1. Adam Clarke’s Commentary
2. The New International
Commentary
3. The Evangelical Bible
Commentary
4. Mathew Henry Commentary.
F. CONCORDANCES
ITIFAKI
o
Itifaki yenye maneno yafananayo
o
Itifaki za maana ya meneno mfano Malazi yawe safi -Ndoa
o
Mlinganio wa maneno yanayopatikana
katika sehemu nyingine za Biblia.
o
Mfano Upendo upi? – Agape? Phileo?
Storge? Eros?
o
Mahali lilipo neno Fulani
§
Mfano wa itifaki nzuri ni pamoja na ;-
- Young’s Analytical Concordance
- Strong’s Exhaustive Concordance etc.
- Niv Exhaustive Concodance.
·
Kumbuka nyingine zina Kamusi za kiibrania na Kiyunani Lexicons (=Dictionaries )
F.
VITABU VINAVYOHUSU TAMADUNI ZA KIBIBLIA &
MASWALA YA UCHIMBAJI WA MAMBO YA KALE
·
Hii itakusaidia kuufahamu na kuwa na
ujuzi kuhusu mambo ya kale kama na maneno yaliyotumiwa kama Busu takatifu, Tundu
la sindano na mambo mengineyo.
G.
KAMUSI ZA BIBLIA NA ZA LUGHA ZA KAWAIDA
& ENCYCLOPAEDIAS:
Zinafafanua
maana ya maneno Mbalimbali kwa ajili ya maswala ya kibiblia na maswala ya
kawaida
1. Kamusi za kawaida ni pamoja na zile
za Kiingereza na kiswahili
(a) English Language Dictionary
(b) Swahili Language Dictionary etc. (Kamusi)
2. Kamusi za Biblia ni pamoja na
zilizo maarufu kama zifuatazo nyingi ni za kiingereza
(a) Unger’s Bible Dictionary
(b) Pictorial Bible Dictionary
(c) Westminster Bible Dictionary
(d) Greek Lexicon & Hebrew Lexicon
(b) Pictorial Bible Dictionary
(c) Westminster Bible Dictionary
(d) Greek Lexicon & Hebrew Lexicon
3.
Kamusi za kitheolojia (Theological
Dictionary).
Kwa ajili ya
kujifunza Mambo mbalimbali ya kitheolojia Mfano ni
1. Baker’s Dictionary of Theology
4. Encyclopedias,
Mfano; - International Standard
Bible Encyclopedia
H.
MAFAFANUZI YA KIBIBLIA (BIBLE HANDBOOKS
:)
·
Kwa ajili ya ufafanuzi wa Maswala
mbalimbali, Vifungu, Maandiko, Tamaduni, Matukio ya kihistoria, Ugunduzi wa maswala ya kale (archaeology), na
kadhalika
Mfano
1. Halley’s Bible Hand Book
2. Unger’s Bible Hand Book
I.
MASOMO MBALIMBALI AU JUMBE MBALIMBALI (TOPICAL BIBLE).
·
Vitabu vinavyo weka mpangilio wa
ufafanuzi wa masomo mbalimbali vikiwa na maandiko yoote husika sawa book
arranged according to different topics with all the texts related to each
topic.
Mfano Nave’s topical Bible
J.
ATLASI ZA KIBIBLIA NA MSWALA YA KIHISTORIA (BIBLE ATLASS) & HISTORY
Kwa
ajili ya kutambua sehemu Mbalimbali na umbali kwa kilomita za mraba n.k na
vipimo kama homeri, yadi, mwendo wa sabato,Ridhaa n.k
e.g. 1. Baker’s
Bible Atlas
2. The Oxford Bible Atlas
JINSI YA KUISOMA BIBLIA;
A. SOMA
Biblia
kama kitabu kingine chochote kwa namna gani?
1.
Kwa kutumia akili: Kufikiri na kwa kujiuliza Maswali. Mathayo. 22:37, Daniel
10:12, Warumi 14:5 (tumia akili
Lakini usizitumainie akili zako mwenyewe yaani si kwa kiburi .Mitthali. 3:5)
2.
Kumbuka kuwa Neno Biblia kwa kiingereza ni BIBLE (English) limetokana na neno
BIBLIA (Katika kilatini) ambalo maana yake ni “Kitabu” hivyo Biblia ni kitabu
Lakini ni kitabu cha Mungu na ni maktaba maktaba ya Mungu
B. SOMA Biblia
kama kitabu ambacho si cha kawaida ni ya pekee
Hii ni kwa sababu Biblia ni kitabu cha
Mungu na hiyo sio kitabu cha kawaida kama vinginevyo na kinaeleweka kwa msaada
wa Roho Mtakatifu kwani Yeye ndiye
(a) Mwandishi
(b) Kubali kuongozwa na yeye (1Wakoritho. 2:14)
(c) Anajua mambo yoote ya Mungu.
(d) Ni Mtafasiri Mzuri na ni Nyenzo mahususi,.
(Yohana 16:13,14:26)