Jumapili, 14 Februari 2016

Umuhimu wa Kutumia Neno la Mungu kwa Halali 2


HITAJI LA KUWA NA MTAFASIRI WA MAANDIKO
 
Wako watu ambao wanaweza kusema kwa hisia zao kubwa kuwa hatuhitaji kuitafasiri Biblia kinachohitajika ni kuisoma na kutenda kile ilichoagiza kwa kawaida huu unaweza kuwa usemi wa kawaida wa watu wa kawaida tu na watu wa jinsi hii wanaweza kuwachukia wasomi au wachungaji na waalimu wanaosisitiza umuhimu wa kuitafasiri Biblia wanaweza kuonekana wako kimwili zaidi na labda wanataka kujitukuza kwa kuifanya Biblia isionekane kuwa ya kawaida kwa watu wa kawaida kitaalamu tunasema mawazo hayao ni ya watu punguani wenye nusu ubongo kwani wakati mwingine kile tunachofikirti kuwa ni sahii tunapokisoma kinaweza kuwa sio sahii na hivyo mtafasiri anahitajika.

 Matendo 8:26-40 Towashi wa Kushi alihitaji kutafasiriwa Maandiko ili alielewe neno vema

SIFA ZA MSINGI ZA MTAFASIRI WA MAANDIKO;


A.            SIFA ZA KIROHO;
1.             Lazima awe amezaliwa mara ya pili ameokoka– Yohana 3:1-8 kuzaliwa mara ya pili pia kunahusisha Kuzaliwa kwa Neno au maji mtu ambaye haja zaliwa kwa neno kamwe hawezi kuwa mtafasiri mzuri wa Maandiko kwa sababu hajaungwa na asili ya Mungu ambayo ni Neno.

2.             Awe na kiu na hamu na shauku ya kulijua neno la Mungu– Mathayo. 5:6, Ps. 119:97 Biblia inaonyesha ya kuwa ukiwa na kiu ya kitu utazidishiwa lakini ukifikiri ya kuwa unacho hata kile ulichozani unacho kitachukuliwa mtu anayehitaji kuyatafasiri Maandiko ni lazima awe na kiu 

3.           Awe mtu aliyepondeka kwa Neno la Mungu – Isaya 66:2. Watu walio wanyenyekevu wanaolihofu neno la Mungu mungu nhuwaangalia hao na hivyo ni rahisi kwa Mungu kujifunua kwao Mungu huwapingwa wenye kiburi bali huwapa wanyenyekevu neema unyenyekevu ni moja ya njia inayokusaidia kuipokea mambo ya rohoni kutoka kwa Mungu na kwa wanadamu wwenye ujuzi 

4.          Awe mtu anaye mtegemea Roho Mtakatifu na maongozi yake– 1Kor. 2:10-14, Yohana 16:13-14 Paulo anaelezea vizuri kuwa mtu ambaye hajazaliwa kwa Roho katika 1Wakoritho 2; 10-14 hawezi kuyatambua mabo ya Rohoni kwani kwae huyo ni upuuzi,Paulo anatumia neno kali sana kuhusu kulipokea Neno la Mungu kwa Mtu wa rohoni yaani


  • Dechomai - yaani kulipokea kwa shauku kubwa inayotokana na Roho wa Mungu na sio
  • Lambano - kulipokea juujuu,au katika haliya kawaida au
  • Ginosko - kulipokea kwa akili za kibinadamu Ufahamu wa kawaida wa kisayansi na kisomi au
  • Oida - Ufahamu mwepesi wa kiakili


B.                  SIFA ZA KUWA NA AKILI TIMAMU

1.                   Je Mtafasiri ana akili timamu au ni – Mgerasi? (au mtu mwenye kutegemea ndoto na Maono?)
2.                   Anapenda kujifunza? Au ana shingo ngumu?

C.                  SIFA ZA KIELIMU
1.  Awe na elimu ya ujumla wa mambo yote
(a)           Tamaduni, Mila desturi tabia za mwanadamu, n.k
(b)           Sayansi    (c)        Sanaa na Ubunifu.    ( d) Saikolojia.
2. Kuwa na maarifa kuhusu maswala ya kihistoria katika.
(a)           Falsafa                  (b)           Jiografia
(c).          Siasa &                  (d)           Historia.
3. Kuwa na ujuzi kuhusu lugha zilizotumika kuleta Biblia
(a)           Kiebrania              (b)           Kiyunani
(c)           Kiaramu.                (d)           Kilatini
4. Kuwa na ujuzi kuhusu Theolojia yaani Elimu kuhusu Mungu.
(a)           Misamiati ya kitheolojia
(b)           Ufahamu kuhusu Agano la kale na Agano jipya
5. Mwenye bidii sana katika maswala ya Kujisomea.
 (a)       Biblia yenyewe na Vitabu vinavyosaidia kusaidia kutafasiri Biblia na Vitabu vingine vya kiroho.


NYENZO MUHIMU ZINAZOSAIDIA KATIKA KUYATAFASIRI MAANDIKO KWA USAHIHI

A.            ROHO MTAKATIFU;

          1. Ni nyenzo ya kwanza na ya Muhimu sana mtu awaye yote anayetaka kuwa mtafasiri mzuri wa Maandiko ni lazima akubali kujazwa Roho mtakatifu kumbuka kuwa yeye ndiye aliyevuvia watu kuliandika neno na ni mwalimu anaweza kutukumbusha na kutufundisha kile ambacho Mungu amekikusudia kwetu hivyo lazima mtafasiri wa maadniko awe amejazwa Roho ikiwa wale waliokuwa mashemasi nyakati za kanisa la kwanza walizingatiwa kuwa wenye Roho je si zaidi sana wanaojitia katia kazi ya kuyatangaza Maandiko ona mfano wa Stefano Matendo 6;8-55 kwanini ni muhimu kuwa na Roho mtakatifu?
            2. Ni Mtafasiri mzuri

                         (a)           Ndiye Mwandishi wa Biblia  1Kor. 2:10-16, Yoh 14:26, 16:13

                        (b)           Anajua kile Ambacho Mungu anakijua


B.          HAKIKISHA KUWA UNA BIBLIA ZA MATOLEO TOFAUTI
1. Biblia ya Kiswahili na za aina mbalimbali za matoleo ya kiswahili cha kisasa 
                2. English Bible matoleo tofauti        
3.  Zile zilizoandikwa katika Lugha Tofauti Tofauti (Greek, Hebrew, Latin, Aramaic, etc)
C.          UWE NA UJUZI KUHUSU AINA ZA MATOLEO YA BIBLIA
 Kwa kawaida kuna matoleo makuu ya aina tatu za kibiblia zile zilizotafasiri neno kwa neno Literal translations, Zile zilizotafasiri kutokana na maana iliyokusudiwa, Dynamic Equivalent na zile tafasiri huru za lugha za kisasa Free translation

         Literal translations          Dynamic Equivalence translations      Free translations

        KJV, RSV,   Weymoth,            NIV         JB           TEV,       MOFFAT, PHILIPS, LB

         NASB                                                                                            NAB        NEB
                                                                                                                  NEB  GNB

           Neno kwa neno              Maana kwa maana                                  Tafasiri huru
       

D.                   D. UWE NA BIBLIA ZENYE MAFUNZO NDANI YAKE ; REFERENCE OR ANNOTATED
·         Uwe na Biblia zenye mafunzo Studies Bible Zinatoa maana ya baadhi ya aya:
(i)    Mfano mzuri ni Full life study Bible (NIV)Biblia ya mafunzo ya uzima tele
(ii)   Life Application Bible (LB)
(iii) Dake Bible
(iv)  Scafield Bible, etc. 

E.                   COMMENTARIES: (Zenye uchambuzi wa mstari kwa mstari).
Baadhi ya Commentaries nzuri ni Pamoja na
               1.              Adam Clarke’s Commentary
                  2.           The New International Commentary
                  3.           The Evangelical Bible Commentary
               4.         Mathew Henry Commentary.
F.           CONCORDANCES   ITIFAKI
o   Itifaki yenye maneno yafananayo
o   Itifaki za maana ya meneno mfano  Malazi yawe safi -Ndoa
o   Mlinganio wa maneno yanayopatikana katika sehemu nyingine za Biblia.
o   Mfano Upendo upi? – Agape? Phileo? Storge? Eros?
o   Mahali lilipo neno Fulani
§  Mfano wa itifaki nzuri ni pamoja na ;-

  1. Young’s Analytical Concordance
  2. Strong’s Exhaustive Concordance etc.
  3. Niv Exhaustive Concodance.

·         Kumbuka nyingine zina Kamusi za  kiibrania na Kiyunani  Lexicons (=Dictionaries )
F.                    VITABU VINAVYOHUSU TAMADUNI ZA KIBIBLIA & MASWALA YA UCHIMBAJI WA   MAMBO YA KALE
·         Hii itakusaidia kuufahamu na kuwa na ujuzi kuhusu mambo ya kale kama na maneno yaliyotumiwa kama Busu takatifu, Tundu la sindano na mambo mengineyo.

G.                  KAMUSI ZA BIBLIA NA ZA LUGHA ZA KAWAIDA & ENCYCLOPAEDIAS:
Zinafafanua maana ya maneno Mbalimbali kwa ajili ya maswala ya kibiblia na maswala ya kawaida
1.             Kamusi za kawaida ni pamoja na zile za Kiingereza na kiswahili
                (a)           English Language Dictionary
                (b)           Swahili Language Dictionary etc. (Kamusi)

2.             Kamusi za Biblia ni pamoja na zilizo maarufu kama zifuatazo nyingi ni za kiingereza

                (a)           Unger’s Bible Dictionary                                   

                (b)           Pictorial Bible Dictionary                                   
   
               (c)          Westminster Bible Dictionary                                   

                (d)           Greek Lexicon & Hebrew Lexicon                      

3.              Kamusi za kitheolojia (Theological Dictionary).
 Kwa ajili ya kujifunza Mambo mbalimbali ya kitheolojia Mfano ni 


1.              Baker’s Dictionary of Theology
4.             Encyclopedias,
                Mfano; - International Standard Bible Encyclopedia

H.                  MAFAFANUZI YA KIBIBLIA (BIBLE HANDBOOKS :) 

·         Kwa ajili ya ufafanuzi wa Maswala mbalimbali, Vifungu, Maandiko, Tamaduni, Matukio ya kihistoria,  Ugunduzi wa maswala ya kale (archaeology), na kadhalika
Mfano
                1.             Halley’s Bible Hand Book
             2.           Unger’s Bible Hand Book

I.             MASOMO MBALIMBALI AU JUMBE MBALIMBALI (TOPICAL BIBLE).
·         Vitabu vinavyo weka mpangilio wa ufafanuzi wa masomo mbalimbali vikiwa na maandiko yoote husika sawa book arranged according to different topics with all the texts related to each topic.
Mfano Nave’s topical Bible
J.             ATLASI ZA KIBIBLIA NA MSWALA YA KIHISTORIA  (BIBLE ATLASS) & HISTORY
Kwa ajili ya kutambua sehemu Mbalimbali na umbali kwa kilomita za mraba n.k na vipimo kama homeri, yadi, mwendo wa sabato,Ridhaa n.k
e.g.         1.             Baker’s Bible Atlas
                2.             The Oxford Bible Atlas
JINSI YA KUISOMA BIBLIA;

A.       SOMA   Biblia kama kitabu kingine chochote kwa namna gani?
1. Kwa kutumia akili: Kufikiri na kwa kujiuliza Maswali. Mathayo. 22:37, Daniel 10:12, Warumi 14:5 (tumia akili Lakini usizitumainie akili zako mwenyewe yaani si kwa kiburi .Mitthali. 3:5)
2. Kumbuka kuwa Neno Biblia kwa kiingereza ni BIBLE (English) limetokana na neno BIBLIA (Katika kilatini) ambalo maana yake ni “Kitabu” hivyo Biblia ni kitabu Lakini ni kitabu cha Mungu na ni maktaba maktaba ya Mungu
B.    SOMA  Biblia kama kitabu ambacho si cha kawaida ni ya pekee
Hii ni kwa sababu Biblia ni kitabu cha Mungu na hiyo sio kitabu cha kawaida kama vinginevyo na kinaeleweka kwa msaada wa Roho Mtakatifu kwani Yeye ndiye
(a)   Mwandishi
(b)   Kubali kuongozwa na yeye (1Wakoritho. 2:14)
(c)   Anajua mambo yoote ya Mungu.
(d)   Ni Mtafasiri Mzuri na ni Nyenzo mahususi,. (Yohana  16:13,14:26)
 

Hakuna maoni: