Ni
muhimu kufahamu kuwa ni ujinga kusema kuwa kanisa halijawahi kukutana na
changamoto zinazolilazimisha kujaribu
kutunza kweli ya neno la Mungu katika viwango vyake vinavyohitajika, Kwakweli
changamoto hizo zimeongezeka sana leo kuliko wakati mwingine wowote, Hata
pamoja na ukuaji wa kasi kwa makanisa yanayohubiri injili bado kanisa
linakutana na changamoto zinazolipelekea hitaji la kuwepo namna ya kutunza
viwango vya kweli vya usafi wa neno na utakatifu unaotokana na mafundisho
sahihi ya kibiblia, hili sio jambo jipya kwani tangu wakati wa Kristo
kulikuweko na changamoto za falsafa mbalimbali ambazo zilitafuta kuharibu
mafundisho ya kanisa, Leo kuna changamoto zaidi kwa sababu kuna televisheni, magazeti,
Radio, na vyombo vingine vingi vinavyotumika kueneza mafundisho Lakini mengine
ni ya uongo na yako chini ya kiwango cha viwango vilivyokusudiwa na neno la
Mungu tutafanyaje? Kanisa linapaswa kuishindania imani somo hili la
hermeneutics linasaidia katika kukabiliana na tatizo husika kama linavyoletwa
kwako na Mchungaji Innocent Kamote Fuatana naye katika somo hili lenye ufunuo
wenye Baraka kwako na kwa yeyote utakaye mfundisha somo hili Mungu na
akubariki.
HERMENEUTICS.
ni nini?
Hermeneutics ni sayansi inayohusu namna na kanuni za
kuitafasiri Biblia
-
Ni sayansi inayohusu jinsi ya kutafuta
maana iliyokusudiwa na Mwandishi maana ya neno au kifungu cha maneno ili uweze
kulifafanua neno kwa wengine
-
Ni somo linalohusu kanuni za kutafasiri
Maandiko
Hermeneutics ni neno lenye asili ya
kiyunani Hermeneuo lenye maana ya kutafasiri hivyo ni sayansi inayohusu kanuni
za kutafasiri Maandiko. Neno kutafasiri limejitokeza katika agano la kale na
agano jipya kama Pathar kiebrania au Pithron yakiwa na maana ya kutafasiri
Kutumia neno la Mungu kwa halali ni
agizo la kibiblia 2Timotheo 2;15 “Jitahidi
kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu mtenda kazi asiye na sababu ya
kutahayari,ukitumia kwa halali neno la
kweli”
Mambo muhimu makuu mawili huzingatiwa
katika kuifanya kazi ya kutafasiri Maandiko
i.
KUGUNDUA maana ya andiko katika maana iliyokusudiwa na
Mwandishi kwa watu wake wakati ule tendo hilo kitaalamu huitwa “EXEGESIS”
ambalo maana yake kutafuta maana halisi ya andikokwa wakati wa Mwandishi na
kisha kuitumia kulingana na wakati wetu tulionao. Kutafuta mawazo yako kisha
kuyasingizia Maandiko yamesema tendo hilo huitwa “EISOGESIS”.
EISOGESIS
EXEGESIS
Eisogesis hutokea pale mtafasiri
anapoacha au kudharau kutumia kanuni za
kutafasiri Maandiko na kusababisha isiendane na maana iliyokusudiwa na
mwandishi ni sawa na kujitafutia maana kisha ukayasingizia Maandiko, Exigesis
hutokea pale Mtafasiri anapozingatia kanuni za kutafasiri Maandiko na hivyo
kusababisha kupata maana ambayo Mwandishi alikuwa ameikusudia katika kuhubiri
jumbe za aina mbalimbali kama Textual. Expository na Topical ujumbe wa somo,
Ingawaje Topical ni hatari kama moyo wa muhubiri huyo utakuwa umeharibika kwani
ni rahisi kufanya Eisogesis kupitia jumbe hizi kwa hivyo wale wanaohubiri jumbe
za Kuchanganua Maandiko Expository huwa salama zaidi ukilinganisha na wale
wanaohubiri topical sermon yaani ujumbe wa somo.
ii).
Kuamua namna ya KUTUMIA Maandiko katika wakati wetu baada ya kuwa umepata maana
iliyokuwa imekusudiwa au kufanya application kwa msingi huo mpaka mtafasiri awe
anauwezo wa kulitumia au kuyatumia Maandiko kwa halali atakuwa amekumbana na
vikwazo anavyopaswa kuvibabadua vikwazo hivyo ni tamaduni, lugha zilizotumika,
muda na historia hivi vyote vinaweza kuwa vipingamizi vinavyoweza kusababisha
mtu kutumia neno la Mungu kwa halali hivyo ni Jukumu la mtafasiri kuchunguza
vipingamizi hivyo ili kupata maana iliyokusudiwa na aweze kutumia neno la Mungu
kwa halali angalia mfano huu;-
MTAFASIRI
MWANDISHI:
(PAULO) KUFANYA
TAFASIRI WASIKILIZAJI
Tamaduni
lugha muda
historia
ENZI HIZO DARAJA LA VIPINGAMIZI LEO
HII
Jukumu
la mtafasiri
Kutatua lugha, tamaduni, historia na muda.
UMUHIMU
WA KULITUMIA NENO LA MUNGU KWA HALALI
Kuzuia
tafasiri zisizo halali katika kanisa
Kulitafasiri Neno la Mungu katika njia
sahii kunahitajika sana hususani katika Nyakati tulizo nazo, Kanisa lisipokuwa
na kanuni maalumu za kulitafasiri neno kila mtu atalitafasiri kama apendavyo na
hivyo hatutakuwa na kweli kamili zinazoweza kutetewa kiimani, kumbuaka kuwa
Biblia ni kitabu maarufu sana cha karibu
Nyakati zote huku kinabeba ujumbe wa Muhimu wa wokovu ni kweli ya kimungu inayotufafanulia
Mungu ni nani?, anafanya nini kinatuambia pia asili ya vitu vyote, na
kinatabiri mambo yajayo, kinabadilisha maisha ya watu na kinafariji kina
ushawishi zaidi ya tamaduni yoyote na kimeandikiwa Vitabu vingi kuliko
maandishi yoyote ambayo yamepata kuwako duniani. Hivyo ni kitabu muhimu sana.
Lakini pamoja na umuhimu huo Biblia
imetefasiriwa kizembeau vibaya na jamii kubwa ya wahubiri na waalimu kuliko
Vitabu vya kawaida vya hadithi. Kwa msingi huu basi kwa kuwa ni kitabu cha
kimungu na cha muhimu si vema kutumia kanuni za kawaida za mawasiliano katika
kukitafasiri au kukiacha kitafasiriwe kama mtu Fulani anavyofikiri au
anavyotaka Biblia ni lazima itafasiriwe katika maongozi ya kimungu
yanayokubalika, Na kutokulizingatia hilo tutapata maana mbovu sana zitakazo
sababisha madhara.
Mfano;-andiko katika Zaburi 137;9
linasema “Heri yeye atakayewakamata wadogo wako Na kuwaseta wao juu ya Mwamba”.
Ukilichukua andiko hili kama lilivyo utauwa watu! Inasemakana kuwa baadhi ya
Wanazi wa kijerumani waliwauwa sana wayahudi wakitumia Maandiko katika Mathayo
27;25 kwa kuwa walisema Damu yake mtu huyo na iwe juu yetu sisi na watoto wetu.
Katika makanisa pia kunatafasiri nyingi mbovu za kimaandiko ambazo zinapaswa
kuwekwa vizuri wako watu wanaamini hata leo kuwa wanaposhiriki meza ya Bwana
wanakula mwili wa Yesu na kunywa damu yake kwa kutumia 1 Wakoritho 15;29 au
watu wanaojaribu kushika nyoka kwa kufikiri kuwa watalindwa kwa kuwa ni ahadi
katika Biblia Marko 16;18, Biblia pia imetumika kuhalalisha zinaa kwa watu kutafasiri
vibaya maswala ya malimbuko au Mwanafunzi na amshirikishe mkufunzi katika mema
yoote Wagalatia 6;6 ikimaanishwa hata
ngono! Au msinyimane 1 Wakoritho 7; 5a na mifano mingine mingi sana kama hivi
ndivyo basi kusipokuwepo na kanuni na
Muongozo wa kuitafasiri Biblia tafasiri za Biblia zitaakisi mioyo ya wanadamu na
sio kile ambacho Mungu anakitaka kwetu hivyo basi iko haja ya kuwako na
Muongozo unaotusaidia ni namna gani tutafasiri Maandiko na kuwa swala hili ni
nyeti kuliko tunavyosisitiza.
Kuzuia
kutokufikia lengo kuu la kuhubiri kwetu
Historia
inaonyesha ya kuwa katika namna ya kushangaza ambayo inakubalika hata kwa watu
wasioiamini Biblia ni kuwa watu wa Ninawi ambao walikuwa wakatili sana na
wapenda vita walitulia kwa kipindi cha kizazi kimoja bila ya kuwashambulia
majirani zao yaani kulikuwa na
mabadiliko makubwa ya kijamii ambayo
yalitokana na ujumbe wa Yona alipotangaza ujumbe aliokuwa amepewa na Mungu,
Leo hii pia ulimwengu unaweza kubadilika na jamii ikawa na maadili mazuri iwapo
tutahubiri kile ambacho Mungu amekikusudia kwa watu, Kama injili ya kweli
iatahubiriwa matokeo ya kuibadilisha jamii yanawezekana Lakini kama kutakuweko
na Tofauti za tafasiri za kiini cha ujumbe ambao Mungu ameukusudia basi ni
dhahiri kuwa hatuwezi kufikia lengo katika kuhubiri kwetu.Lengo kubwa la
kuhubiri kwetu na kufundisha ni ili watu waishi kama Mungu anavyotaka lakini
watu wataishije kama Mungu anavyotaka iwapo neno lake litatafasiriwa kama kila
mtu apendavyo? Ni wazi kuwa hatuwezi kufikia lengo
Kuzuia kutofikia lengo la kufundisha Neno la Mungu.
Kama
kila mtu atajihubiria ujumbe vyovyote atakavyo ni wazi kuwa na kufundisha pia
kutakuwa katika hali kama hiyohiyo na kumbuka kuwa ni rahisi sana kuwaleta watu
kwa Yesu Lakini ni vigumu sana kuwafanya watu kuwa wanafunzi Yona alifanya kazi
nzuri ya kuwahubiri watu wa Ninawi Lakini hukufanya vizuri kwa kuwanyima
mafundisho watu wa Ninawi Mungu anapotuma uamsho mkubwa na kuokoa wengi
analitegemea kanisa kuwafundisha wanaookolewa hata hivyo si mafundisho yoyote
tu bali ni mafundisho yaliyo ya weli iliyotafasiriwa katika viwango sahii
Shetani ni lazima ataendelea kujaribu kuharibu kanisa Kupitia silaha yake kuu ambayo ni uongo
Kupitia mafundisho ya uongo Paulo alifanikiwa sana kuihubiri injili katika
Efeso na watu wakaacha kuabudu sanamu Matendo 19;26, Lakini pia alionya sana
kuwa mbwa mwitu wakali watainuka wasilihurumie kundi hii ni kwa kufundisha
yasiyopasa au yasiyo sahii Matendo 20;27-30.
Kusaidia kujua kwa nini Mungu ametupa Biblia.
Watu wengi sana wakristo wanaamini kuwa Biblia ni neno la Mungu, Lakini
ni muhimu kujiuliza maswali kuwa je Mungu angejenga msingi huu wa Neno katika
hali ya Machafuko? Lazima uko msingi wa muhimu sana na msingi huu ni wa zege la
ufunuo wa kimungu usiyoweza kutikiswa, Lakini hata hivyo ni wakristo wachache
sana ambao wanavutiwa na kutafasiriwa
kwa usahihi kwa neno la Mungu Ni wakristo wachache tena wenye Ufahamu wanaweza
kuona jambo hili kuwa ni hatari kutokuweko na mwongozo sahihi au na watu makini
ambao wanapaswa kusimamia misingi na kanuni za kuyatafasiri Maandiko katika njia
iliyo sahihi Hivi ingekuaje kama tu tungekuwa tunamtumikia Mungu bila hata ya
kuwepo Neno lililoandikwa? Watu wangekuwa na maoni Tofauti kuhusu Mungu na
wangekuwa na njia Tofauti kuhusu wokovu namna ya kuhubiri au hata kuabudu kwa
msingi huo Mungu alitoa neno Lakini hali kadhalika kusipokuwepo na Muongozo
katika kutafasiri pia kutakuwa na tatizo linalofanana na kutokuweko kwa Neno la
Mungu
Kuzuia hukumu ya Mungu kwa kutumia vibaya Maandiko au
kuhubiri kitu kingine.
Biblia inatutahadharisha kuwa Mungu huliheshimu sana neno lake na hivyo
mtu awaye yote mwenye madai kuwa ametumwa na Mungu kufanya kazi ya kufundisha
au kuhubiri Maandiko basi ni muhimu kusema kile ambacho Mungu amekusudia
kisemwe Yeremia 23;1-4,15-30, aidha
Paulo mtume naye aliwatahadharisha watu watakakohubiri injili ya aina nyingine
kuwa walaaniwe Wagalatia 1;8-9, si hivyo tu Yakobo mtume aliyeheshimika na
ndugu wa Bwana alitahadharisha kuwa tusiwe waalimu wengi kwani kuna hukumu
iliyo kubwa zaidi Yakobo 3;1.kwa msingi huo kuna hukumu ya Mungu pia kwa watu
ambao wataongeza au kupunguza katika kile Mungu alicho maanisha Ufunuo 22;18-19
kwa hivyo basi kuna umuhimu wa kuhakikisha kuwa kweli inahubiriwa au neno
linahubiriwa kwa kuzingatia misingi yake ili kweli ipatikane kwa kanisa na
kuzuia hukumu ya Mungu kwa kuhubiri yale yasiyotupasa hivyo ni muhimu
ikafahamika kuwa kuna hukumu ya Mungu kwa kutumia neno lake isivyo halali.
JE KUNA UMUHIMU WA KUWA NA KANUNI ZA
KUTAFASIRI MAANDIKO?.
Kama tulivyoona katika vifungu vilivyotutangulia chukulia kuwa
umezungumza jambo na kisha mtu akalipokea vibaya na kwenda kuwaelezea wengine
katika namna isiyofaa ni nini kinaweza kutokea? Bila shaka mahusiano ya
kirafiki yanaweza kuharibika na hivyo itakupasa kuelezea kwa usahihi mara ya
pili kwamba ulikuwa umemaanisha nini? Hiki ndicho humpata Mungu, tunapotafasiri
Neno lake katika njia isiyo sahihi, angalia jinsi watu wasiofaa walivyofanya
Nyakati za Kanisa la kwanza hata ikampasa Petro kusisitiza jambo kuhusu nyaraka
za Paulo Mtume “ “Nanyi hesabuni uvumilivu wa Bwana kuwa ni
wokovu, kama vile ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima ile
aliyopewa na Mungu. Huandika vivyo hivyo katika nyaraka zake zote akizungumzia
ndani yake mambo haya. Katika nyaraka zake kuna mambo mengine ambayo ni vigumu
kuyaelewa, ambayo watu wajinga na wasio thabiti huyapotosha kwa maangamizi yao
wenyewe, kama wapotoshavyo pia Maandiko mengine”. 2Petro 3; 15-16 kwa
msingi huo kunahitajika Tafasiri sahihi na kanuni sahihi za kuyatafasiri
Maandiko. Ziko sababu maalumu zinazoonyesha kwanini ni muhimu kuwa na tafasiri
za Maandiko ikiwemo Tamaduni za wakati ule ni Tofauti na zetu, Lugha
zilizotumika ni Tofauti, Muda wa watu
hao walipoishi ni Tofauti historia ya wakati ule ni Tofauti hivyo mtafasiri wa
Biblia ili apate maana halisi anapaswa kuruka vikwazo hivyo vyote ili kulileta
neno kwetu leo .
Kwa msingi huo utaweza kuona kuwa iko
haja ya kujua tamaduni za wakati wa Muandishi, lugha, Historia na nyakati au Muda
utahitaji kujua kwa mfano mafarisayo ni akina nani masadukayo, Neno Abba, tamaduni
Tofauti na nyakati mfano kitabu cha kutoka kiliandikwa miaka zaidi 3500
iliyopiata Nyakati na lugha na tamaduni kamwe haviwezi kulingana hivyo utaweza
kuona kuwa kutafasiri Maandiko kunakuwa kazi ya kitaalamu zaidi na ya uangalifu
zaidi kulijko tunavyofikiri
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni