Mbinu za ukuaji wa
kanisa Strategy For church Growth
Neno Mbinu au Strategy linamaanisha ni kampeni za kijeshi
·
Linatokana na neno la kiasili la kiyunani Strategy Strategy ambalo maana yake ni kuongoza Jeshi kwa hivyo
kimsingi linatokana na maswala ya uongozi wa kijeshi lakini linaweza kutumiika
pia katika kampeni za mambo mengine na mikakati ya aina yoyote
·
Yesu alisema Nitalijenga kanisa langu juu ya
mwamba wala malengo ya kuzimu hayataliweza ni tamko la mikakati ya kijeshi
kwani shetani amejaribu kuliharibu kanisa, kulidhoofisha na kulisambaratisha na
kulitoa katika malengo yake makuu na kulifanya lisiendelee lakini wewe kama
kiongozi wa kiroho katika eneo lako unapaswa uwe na mbinu na mikakati ya
kuhakikisha kuwa kazi hii inaendelea na ushindi dhidi ya upinzani wa adui
unapatikana na kazi inaendelea
·
Uiongozi hapa unajumuisha kuwasaidia watu kufuata vema mpango mkakati
na kushinda vikwazo na kufikia malengo yaliyokusudiwa katika staili ya kijeshi
hii ndio mbinu
Neno kukua kwa kanisa lina maanisha kuwa kanisa ni
·
Ni zaidi ya dhehebu au shirika, ni kitu chenye
uhai
·
Ni kama mwili ulio hai wenye uwezo wa kukua na
kujizalisha wenyewe, hii ina maana ya kuwa kila kanisa la mahali pamioja lina
uwezo wa kukua na kujizalisha lenyewe na kupenda makanisa mengine hivyo kama
kanisa lina uhai basi ni muhimu kanisa likaelewa jambo hili la msingi Yesu
mwenyewe alitoa msingi wa ukuaji wa kanisa wenye nguvu Matendo 1;8 hii ina
maana ya kuwa kanisa linaweza kupendwa mahali kokote na katika jamii
yoyote na likaongezeka kutoka katika
jamii hiyo na lika sambaa kuelekea katika jamii nyingine na kuweza kufika hata sehemu nyingine
ulimwenguni au mwisho wa nchi, huu ndio msingi wa kimungu kwa hivyo mtu awaye
yote asiogope kupenda kanisa au kuanzisha kanisa huu ndio ulikuwa mkakati wa Yesu Kristo
kuhusu kanisa lake na ahadi yake ni kuwa
pamoja nasi hata ukamilifu wa Dahari.
Kwanini tunasoma Mbinu za ukuaji wa kanisa?
·
Somo hili litatusaidia jinsi ya kushughulikia na
maswala ya kiroho,tamaduni na nguvu ya jamii husika katika upandaji au ukuaji
wa kanisa na litakufundisha asili na
ukuaji wa kanisa
·
Litasaidia kukuonyesha wewe na jamii ya watu
unaowahudumia umuhimu na ulazima wa
agizo kuu katika Mathayo 28;18-20, hii itakusaidia kuweza kuwa mfuatiliaji wa karibu
wa kujua kuwa kanisa linakua au la kwa kutumia grafu au utafiti wa kawaida wa
Ugunduzi kuhusu ukuaji wa kanisa, litakufundisha namna ya kuanzisha na
kuendeleza kanisa.
·
Somo litakupa mifano mbalimbali ya ukuaji wa
makanisa katika maeneo mbalimbali Duniani na kukuonyesha faida na uzuri au
utamu wa kukua kwa kanisa pia katika eneo lako utajifunza tamaduni na muundo wa
jamii unayoihudumia na kuchagua njia
inayo faa kwa ajili ya kujenga kanisa lenye nguvu litakalojieneza na
kujiendesha na kijitegemea lenyewe indigenous church.
·
Kujifunza jinsi na namna ya kupanga mikakati ya
kushambulia kwa injili miji na pamoja na kufikia kila jamii kwa injili,kupenda
makanisa na kufanya kazi na watu na makundi yao katika namna mbalimbali,
kutumia mbinu za kifundi kugundua ni maeneo gani yanapokea injili kwa
haraka na kuchukua hatua za haraka
kupenda kanisa hapo, pia kupanga mipango au kuweka malengo ya baadaye katika
eneo unalo lighudumia au uatakalolihudumia.
·
Kuwa na uelewa kuwa nguvu ya ukuaji wa kaniwsa
inategemeana na uhusiano wetu na Roho Mtakatifu kwako na kwa watu unaowahudumia
ili kuweza kuubeba agizo lile kuu na
kanuni hizi zinazotolewa zinaweza kufanya kazi katika eneo lolote iwe
mijini,kijijini kwa kanisa kubwa au kanisa lililo dogo
SURA YA KWANZA; FANYA KAZI
SAWA NA KANUNI ZA KIBIBLIA ZA UKUAJI WA KANISA
Mtu awaye tote ambaye anataka
kanisa lake liweze kukua au anataka kupenda kanisa ni muhimu kwanza akafanya
kazi au akakubaliana na kanuni za ukuaji wa kanisa zinazotolewa na Biblia hii
ndio kanuni ya msingi ya upandaji na ukuaji wa kanisa katika sura hii
tinashughulikia msingi huu wa Kibiblia na kitheolojia wa ukuaji wa kanisa
katika msingi huu basi tutajifunza kwa kuzingatia maeneo manne.
·
Lazima ujue kuwa unajenga kanisa lenye msingi wa
Agano jipya
·
Lazima ukubali kuwa mwaminifu katika majukumu ya
Shughuli hii
·
Laizma uweke au utoe kipaumbele kwa kile ambacho
Mungu anakipa kipaumbele
·
Lazima ujue kufanya kazi na Mungu katika Uamsho
LAZIMA UJUE KUWA UNAJENGA KANISA LENYE MSINGI WA AGANO JIPYA
Biblia ni neno la Mungu na ndio msingi mkuu
wa kwanza unaotuongoza katika mbinu yoyote ya ukuaji na upandaji wa kanisa,
Biblia inafunua kuwa ni aina gani ya kanisa Mungu anataka na ni namna gani anataka kanisa likue kwa
msingi huo mbinu yoyote mbadala ya ukuaji au upandaji wa kanisa ni lazima
itokane na misingi inayopatikana katika Biblia, Unapopanda kanisa kinyume na
msingi ule unaowekwa na Biblia tunaouona katika agano jipya Basi ukuaji wa
kanisa hilo utaingia matatani kama tunataka makanisa yetu yakuwe basi lazima
tujenge msingi wa kanisa linalokuwa kwa mujibu wa makanisa ya agano jipya
kumbuka kuwa mjenzi mkuu wa kanisa ni Yesu Kristo na ndiye aliyetualika sisi na
si kujenga pamoja naye( Mathayo 16;18) kwa msingi huo ili kanisa liweze kukua
linatakiwa kuzingatia maswala ya msingi makuu matatu yafuatayo
a. Lazima
ujenge kanisa kwa msingi wa kibiblia
b. Lazima
ujenge kanisa ambalo Yesu Kristo ndiye kiini kikuu
c. Lazima
ujenge kanisa ambalo Roho Mtakatifu anapewa kipaumbele
Lazima ujenge kanisa kwa msingi wa kibiblia
Ni muhimu kabla ya kuangalia
kanisa kwa msingi wa kibiblia tuchukue Muda kujifunza neno kanisa kwanza lina
maana gani
1. Neno
kanisa kwa kiingereza Church limetokana na neno la kiyunani Kuriake yaani mali
ya Bwana
2. Neno
linalotumika katika agano jipya kuhusu kanisa ni neno la kiyunani Ekklesia ekklesia
ambalo maana yake ni kusanyiko
ambalo neno lake la msingi ni Ekkleo yaani “ walioitwa watoke miongoni
mwa”
3. Kwa
msingu huo Yesu alipokuwa anazungumzia habari za kujenga kanisa hakuwa
anamaanisha kuwa atajenga Hekalu zuri juu ya mawe, alikuwa akizungumzia watu
ambao angewaita watoke miongoni mwa udunia na kuwa awakusanye pamoja wawe wake
kwa Makusudi yake ya milele
4. Hata
hivyo Biblia inapotumia neno kanisa hususani agano jipya ambalo hutueleza jinsi
kanisa lilivyoanza na kukua na kuenea tunaweza kusema neno kanisa pia linamaana
kuu nne zifuatazo
·
Ni kanisa la mahali pamoja Warumi 16;5 yaani
kundi la watu waliookoka wanaokusanyika pamoja kila wakati kwa Makusudi ya
kuabudu
·
Ni wakristo Matendo 11;22 wakristo wote
wanaoishi mahali fulani ni kanisa
·
Au wakristo wote walioishi wakati fulani Waefeso
5;32
·
Ni kila mwamini wa kweli katika Kristo
waliopita, walioko na watakaokuja walio duniani au mbinguni kokote ni kanisa
Efeso 1; 22. Waebrania 12;23.
5. Maana
nyingine za kanisa ni pamoja na
·
Jengo mahali mambapo wakristo hukutana kwa ajili
ya ibada
·
Dhehebu, huu ni ushirika wowote wa Kikristo
wenyemafundisho fulani sahii
·
Namana fuilani ya ibada za Kikristo na namna
zinavyoendeshwa
Kwa msingi huo kuhitimisha maana
ya kanisa tunaweza kusema kuwa kanisa ni kundi la watu wanapokutana pamoja
kuabudu, kujifunza, na kuhudumiana na wanaomkubali Yesu kuwa Bwana na mwokozi
wakifuata mafundisho yake na kumtumikia.
Kanisa lenye msingi wa kibiblia
·
Nyakati za kanisa la kwanza walitambua na
kulikubali neno la Mungu kuwa limevuviwa na kuwa kanisa limetokana na Neno la
Mungu
·
Waliamini katika ahadi za kibiblia na mafundisho
ya mitume
·
Walikubali kuongozwa na neno la Mungu na kuwa
ndio mamlaka ya mwisho lenye kuongoza kimaadili na kiimani
·
Walikuwa na imani yenye nguvu iliyojengwa katika
msingi wa neno la Mungu
·
Walikataa kila aina ya fundisho lisilikubaliana
na neno la Mungu au lenye msingi wa mila na tamaduni za kimapokeo
·
Walikubali kuteseka na walipotawanyika walieneza
injili,walikubali kufa kwa ajili ya imani na walihubiri kotekote
·
Mafundisho yao yalikuwa yenye msingi wa kibiblia
Kwa msingi huo
mtu awaye yote akipanda kanisa kulingana na msingi wa neno la Mungu kanisa hilo
litakua na kuendelea mbele na kamwe halite tikiswa
Kanisa lenye
msingi wa kibiblia
Lilizaliwa kutimiza andiko
|
Matendo 2;1-21
|
Imani yeke katika Kristo ilitokana na maandiko
|
Matendo 17;2-4, 18;28
|
Mafundisho yalitokana na maandiko
|
Matendo 17;11-12
|
Washirika walifundishwa neno
|
Warumi 15;4,Matendo 18;11
|
Matumaini na kujitia moyo sawa na maandiko
|
Warumi 15;4
|
Maadili sawa na maandiko
|
1Koritho 10;5-11,1Timotheo 3;15-16
|
Mafundisho ni Neno la Mungu
|
Matendo 6;2-4,18;11
|
Imani na nguvu yao ni neno la Mungu
|
Efeso 6;13-17
|
Kukua kwake kulitegemea Neno la Mungu
|
2Petro 2;2
|
Kutawanyika kwao kulitegemea Neno la Mungu
|
Matendo 6;7,8;4,12;24.13;49
|
Lazima ujenge kanisa ambalo Yesu Kristo ndiye kiini kikuu
Kanisa lolote lile haliwezi kukua
kama Kristo sio kiini kikuu cha kanisa hilo, Lazima tujenge kanisa lenye
uhusiano na Kristo aliye mizabibu wa kweli Yohana 15;1-8 na sisi tu matawi
ndani yake na ya kuwa hatuwezi kufanya neno lolote pasipo yeye hii ndio kanuni
nyakati za kanisa la kwanza walizingatia swala zima la kumpa Kristo kipaumbele.
·
Kanisa lilikuwa kwa sababu lilikuwa na uhusiano
mzuri na Kristo
·
Kristo alihesabiwa kuwa kichwa na kanisa ni
mwili wake walimtii walitumia mamlaka yake na jina lake waliamini kuwa yeye ndiye anayetoa maelekezo
anayelitunza na kulilisha kanisa Wakolosai 1’9-18,24,Waefeso
1;16-23,5;29-30,4;1-16,1Koritho 12;27
·
Kristo alihesabiwa kama Mume na kanisa kama bibi
harusi kwa hivyo Yesu alilipenda kanisa
,akajitoa kwa ajili yake analisafisha na
kulitunza na kanisa kama bibi harusi linajitoa kwa Kristo linampenda na kumtii
linajitunza katika usafi na uzuri
2Koritho 11;2-3,Warumi 7;2-4,Efeso 5;23-30,Ufunuo 19;7-8,21;2.
·
Kristo anahesabiwa kama Mjenzi au jiwe kuu la Pembeni ndiye mjenzi mkuu na mbunifu wa swala zima la
kanisa na kanisa ni Jengo la Mungu kwa msingi huu walifuata mpango wake
walikuwa na umoja kwa ajili yake walijifanya
kuwa nyumba halisi ya Mungu
·
Kwa msingi huo basi kanisa linalohitaji kukua ni
lazima lijenge msingi wake katika kumuweka Kristo kama kiini kikuu cha maswala
yote ya kikanisa.
Lazima ujenge kanisa ambalo Roho Mtakatifu anapewa kipaumbele.
Kabla ya kuondoka kwake kwenda
mbinguni Yesu aliwaambia wanafunzi wake waziwazi kwamba wanapaswa kusubiri
nguvu za Roho mtakatifu kabla ya kuanza kujaribu chochote katika agizo kuu Luka
24;44-49,Matendo 1;1-8 kwa msingi huo Matendo yote ya kanisa tunayo yasoma
katika kitabu cha Matendo ya mitume ni matokeo ya Nguvu hizo au agizo katika
Matendo 1;8 Roho ndiye anayetoa nguvu ya huduma na kusababisha kanisa kuubeba
kazi ya Mungu kwa ufasaha kwa msingi huo kanisa likizingatia hili na washirika
wakiwa ni waliojaa Roho na Viongozi litafanikiwa katika kila walifanyalo na
walitendalo kwa ajili ya ujenzi wa ufalme wa Mungu.
Kwanini Roho Mtakaifu apewe kipaumbele katika Shughuli za upandaji na
ukuaji wa kanisa?
·
Kwa ajili ya kushuhudia na kueneza injili
Matendo 1;8
·
Kwa ajili ya kumtukuza Mungu na kuelezea kazi
zake Matendo 2;1-11
·
Kwa ajili ya kuhubiri na kufundisha Matendo
2;14-47
·
Kwa ajili ya kutumia nafasi kuhudumu na
kushuhudia Matendo 3;1-26
·
Kwa ajili ya ujasiri wakati wa upinzani Matendo
4;5-20
·
Kwa ajili ya kutiwanguvu upya kueneza neno Matendo4;23-31
·
Kwa ajili ya kuelewa na kutambua unafiki Matendo
5;14-16
·
Kwa ajili ya uponyaji na mijadala Matendo
5;28-29
·
Kwa ajili ya furaha wakati wa majaribu Matendo
5;40-42
·
Kwa ajili ya kumhudumia watu kwa haki Matendo
6;1-7
·
Kwa ajili ya uaminifu hata kufa Matendo 7;1-60
·
Kwa ajili ya kuhubiri kila mahali Matendo 8;1-13
·
Kwa ajili ya kupambana na nguvu za upinzani Matendo
8;9-13,Matendo 13;6-11.
·
Kwa ajili ya kusaidia wengine kuipokea Roho
Mtakatifu Matendo 9;14-17
·
Kwa ajili ya kazi maalumu alizotuitia Matendo
9;10-20
·
Kwa ajili ya kuvuka mipaka ya kitamaduni Matendo
10;1-48
·
Kwa ajili ya kuwapelekea injili watu wasio wa
utamaduni wetu Matendo11;1-26
·
Kwa ajili ya kufikia mahitaji ya wale wenye
kuhitaji Matendo11;27-30
·
Kwa ajili ya kutuokoa kimuujiza wakati wa hatari
Matendo12;1-17
·
Kwa ajili ya uongozi wake katika safari za
umisheni Matendo 13;1-52
Lazima uweke msingi sio wa kumpa
kipaumbele Roho Mtakatifu tu bali nafasi ya kuliongoza kanisa
LAZIMA UKUBALI KUWA MWAMINIFU KATIKA MAJUKUMU YA SHUGHULI HII
Ukuaji na upandaji wa kanisa ni
somo gumu kueleweka kivitendo kutokana na mfumo wa kanisa na njia mbalimbali za
ukuaji wake hii maana yake ni kuwa
Shughuli hii inahitaji uaminifu kwa majukumu yoyote ambayo Mungu anakupa hata
kama wakati mwingine mambo yaweza kuwa kinyume na matarajio hata kinyume na
yale tunayokuwa tumemuomba Mungu kuyafanya pamoja nasi
Utata katika ukuaji wa makanisa
1. Yesu
alisema nitalijenga kanisa langu juu ya Mwamba na malengo ya kuzimu
hayataliweza Mathayop 16;18 kwa msingi huo jambo la muhimu ni kutimiza kusudi
lake na kwa kweli kanisa linakua kwa kasi ulimwenguni
·
Kanisa la Presbyterian huko Korea ya kusini
lilikuwa kwa kasi na kuongezeka mara mbili katika miaka ya 1950 hata leo
·
Huko Ethiopia waongofu wapatao 120,000
walibatizwa
·
Watu 80,000 wa nyanda za juu walimfuata Yesu
huko Formosa
Huu ni ushahidi ulio wazi kuwa kanisa linakua lakini
wakati mwingine ni vigumu kujua kuwa kanisa linakua kwa sababu kadhaa zifuatazo
·
Mlipuko wa ukuaji au kuongezeka kwa idadi ya
watu na hivyo kuongezeka kwa idadi ya watu wasiofikiwa
·
Kiburi cha udhehebu na matatizo ya kugawanyika
kwa makanisa
·
Matukio yanayozuia ukuaji wa kasi wa kanisa kama
vita, upinzani wa injili, ukimbizi n.k.
·
Kukosekana kwa taarifa za ukuaji wa makanisa
duniani, kutokutunzwa kwa Kumbukumbu za ukuaji wa kanisa na kushindwa kutoa
kipaumbele kwa maswala ya kuwafikia wale wasiofikiwa na injili
·
Kuwafikia wasiofikiwa na injili leo limekuwa si
swala la muhimu katika makanisa ,Makanisa yanayotuma wamishionari na Fedha za
kusaidia kazi za umisheni wako gizani hawajui yanayoendelea huko, Matukio
yanayozuia ukuaji wa kanisa hayabadilishwi na hubakia hivyo hivyo
Je Kanisa linaweza kukua kwa kasi kwa njia gani?
1. Weka
msingi wa ukuaji wa kanisa mapema wakati watu wanapoanza kuokoka
a.
Ukuaji wa kanisa ni jambo ambalo linatakiwa
kupendwa mapema ndani ya watu wanaookolewa katika kanisa lako njia hii
ilitumiwa na kanisa la Yoido Full Gospel Church (Assemblies of God) huko Seoul,
Korea na kupata mafanikio makubwa sana
Ø
Mwaka 1973 Washirika walifikia 20,000 na kabala
ya mwaka 1979 kanisa lilifikia idadi ya washirika 100,000.
Ø
Mwaka 1994 kanisa lilikuwa na washirika 700,000
watu wazima
2. Zingatia
umuhimu wa kuwa na makanisa ya nyumbani
Ø
Moja ya njia nyingine iliyotumika Korea ni
kutawanya makanisa ya nyumbani Mungu alimuongoza Mchungaji David Yonggicho na
kumpa uwezo wa kukabidhi madaraka au kugawa majukumu kwa washirika kuhudumiana
katika makanisa ya nyumbani
Ø
Washirika walikubali majukumu hayo na kuanza
kufungua makanisa ya nyumbani ya kujifunza Biblia na maombi
Ø
Majirani walianza kukubali wokovu na matokeo
yake idadi ya kanisa iliongezeka na
mwishoni mwa mwaka 1979 kulikuwa na makanisa ya nyumbani yapatayo 7,000
waliokuwa wakikutana kila wiki kwa ajili ya kuabudu pamoja
Ø
Ilipofika Mwaka 1994 kulikuwa na makanisa ya
nyumbani yapatayo 21,800
3. Zingatia
umuhimu wa kuligawa kanisa linapokuwa limeongezeka
Ø
Mpango huu ndio mpango wa ukuaji wa kanisa
unaouma lakini unasaidia sana katika ukuaji wa kanisa au ni mojawapo ya njia ya
ukuaji wa kanisa kwani wakati mwingine inashauriwa kutumika kwa njia hii
maadamu tu Mchungaji asiwe na roho ya ubinafsi
Ø
Njia hii inaweza kuleta uchungu na kuzuia ukuaji
wa kanisa wengi wameiacha imani kutokana
na tabia zisizo za Kikristo na kukosekana kwa upendo kunakotokana na mafarakano
Ø
Wakati mwingine kundi moja linapoondoka lile
linalobaki huona wanazidiwa katika kukabiliana ana majukumu yaliyokuwa mbele
yao mgawanyo huu unaweza kusababisha kutokuweko kwa umoja katika kanisa katika
mwili wa Kristo vyovyote iwavyo Historia ya kanisa inaonyesha ya kuwa Mungu
huitumia njia hii wakati mwingine ili kusababisha ukuaji wa kanisa, Baadhi ya
madhehebu pia yamezaliwa kutokana na kuchangiwa na tabia za kutokupokelewa vema
katika makanisa yao ya awali
Moja ya njia
za ukuaji wa kanisa wakati mwingine ni kugawanyika.
Mambo ya kufanya
njia hii inapotokea
Kanisa
linapogawanyika hata kama ni kwa mafarakano au kwa Ridhaa ya Mchungaji wa
kanisa mama ni muhimu kufahamu kuwa unawajibika kufanya mambo ya msingi
yafuatayo
·
Kumbuka kuwa ni mpango wa Mungu Kanisa kukua
hata kama njia inaweza kuwa sio sahii lakini wakati mwingine Mungu kwake ni
sahii
·
Omba kwamba Bwana awabariki wale walioondoka na
kuwa Mungu awatumie kuwa Baraka na kufanya kazi ya injili na kuieneza katika
eneo lao
·
Waonyeshe upendo wale walioondoka na shirikiana
nao kwa njia yoyote iwezekanayo ambayo haiku kinyume na Biblia
·
Hakikisha kuwa unalifanyioa kazi swala la
kusamehe na kutokuwaona wapendwa katika Bwana kuwa maadui zako na elewa kuwa ni
njia ya lazima katika kuzalisha ukuaji wa kanisa
4. Zingatia
umuhimu wa kanisa mama kuzaa kanisa jipya
Maswala ya kuzaa
makanisa mengine ni lazima yawekewe msingi katika makanisa mama au wachungaji
husika, mara nyingu kunakuwa na visingizio vingi lakini kama tupo kwa ajili ya
Mungu mpango huu ni wa lazima
Ø
Unaweza kupunguza idadi ya washirika wanaotokea
upande fulani au familia zinzotokea upande fulani kisha kisha ukazaa kanisa
jipya
Ø
Au unaweza kuweka mpango wa aina nyingine kutoka
kanisa mama kuzaa kanisa
Ø
Au unaweza kuweka mpango wa kufundisha watenda
kazi au kuandaa watumishi ndani ya kanisa lako kisha ukawatuma katika eneo
jipya na kuzaa makanisa kanisa lililo hai huzaa na kuongezeka lenyewe
5. Kumbuka
kuwa njia kubwa ya mafanikio ni ile ya makanisa ya nyumbani
Ø
Njia hii ndio njia nzuri zaidi kwani watenda
kazi walioandaliwa kumhudumia makanisa ya Nyumbani makanisa hayo yanapokuwa
katika mitaa yao baadaye yanaweza kugawanywa na kuwa makanisa kamili hii imefanikiwa kule Korea
6. Njia
nyingine za upandaji au ukuaji wa makanisa ni pamoja na
Ø
Kushuhudia nyumba kwa nyumba katika maeneo ya
kanisa
Ø
Kulenga kuyafikia maeneo yaliyo mbali na kanisa
, kuwafikia walioko magerezani,kufanya mikutano ya injili, kugawa tracts na
kuwazuia Biblia kwa bei nafuu
Ø
Kuongezeka kwa kuzaliana
Ø
Kuwatumia washirika wanaohamishwa katika maeneo
yasiyofikiwa kuanzisha makanisa
Ø
Kujaribu kuwarejesha wale waliorudi nyuma
Ø
Kuanzisha vyuo vya Biblia kwa wale wanaopenda
kujifunza Biblia kwa mitindo hii kanisa litaweza kukua
Kanisa kukua ni swala la uaminifu kwa Mungu
Uaminifu kwa Mungu katika
kuhakikisha kuwa kanisa lake linakuwa hujumuisha swala zioma la
1. Kuhubiri
injili lakini kuhubiri injili bila kufanya wanafunzi au kufanya ufuatiliaji ni
tabia isiyo ya uaminifu kwa kanisa
2. Kuhubiri
injili kisha kutokufanya ufuatiliaji wa kiuanafunzi kwa waongofu wapya ni
kutimiza au kuwa mwaminifu kwa sehemu tu ya lile agizo kuu
3. Ni
kushindwa kuliko wazi kwa kutafuta waliopotea ambao wameweza kuitikia vema
ujumbe wa injili
4. Ni
kushindwa kuona umuhimu wa nini kifanyike baada ya kushuhudia au Kuhubiriwa kwa
injili na watu kuokolewa hili ndilo tatizo la makanisa mengi leo
Kuna njia Tano muhimu za kuonyesha uaminifu wetu kwa Mungu sambamba na
ukuaji wa makanisa
1. Kutoa
zaka kwa uaminifu kama utii kwa neno la Mungu ili Fedha itumike kwa Makusudi ya
injili
2. Kumtangaza
Kristo kama mwokozi
3. Kuweka
mikakati na kuwafikia waliopotea kwa njia na namna mbalimbali
4. Kuhakikisha
kuwa waongofu hao wapya wanafuatiliwa na kulishwa neno la Mungu
5. Kueneza
kanisa lililojaa Neno na nguvu za Roho Mtakatifu
6. Kutunza
Kumbukumbu ya watu wanaookolewa na idadi yao
Uaminifu kwa Mungu ni swala gumu na wala sio swala rahisi kama tunavyofikiri
Historia inaonyesha kuwa ukuaji
wa kanisa unatofautiana katika kila eneo kutokana na hali zinazochangiwa na
eneo husika au na watu husika na ziko sababu mbalimbali zinazochangia hali kuwa
rahisi au kuwa ngumu sababu hizi zinaweza kuwa ni kanisa lenyewe husika au
jamii au siasa au uchumi au hali ya tamaduni na maswala mengineyo yanaweza
kuchangia katika ukuaji au kutokukua kwa kanisa
na wakati mwingine sababu zinaweza kuwa za kipekee sana kiasi cha kuweza
kusababisha hali iliyotumika mahali fulani isifanye kazi katika mazingira
mengine
Uamsho huko Philippines.
Nchini Ufilipino Philippines
kumewahi Kuweko na Uamsho mkubwa sana kwa sababu ya Mafundisho kushuhudia na
makanisa mengi yalipandwa na kustawi lakini ni hali gani zilichangia Filipino
Kuweko na Uamsho huu
a. Wakati
wa vita vya pili vya dunia wafilipino wengi waliamua kuishi milimani mbali sana
b. Mchungaji
mmoja aliyeitwa Dia na mkewe waliamua kukataa kushirikiana na maadui na kwenda
kuhubiri huko ndani milimani na Mungu aliwaongoza kuifikia miji mitatu midogo,
huko walipata washirika ingawa Mchungaji wao alikuwa dikteta Kanisa
lilikuwa licha ya Historia hiyo ya
kukatisha tamaa,kuzunguka nakutawaliwa na maadui mazingira ambayo sehemu
nyingine huweza kufanya kanisa lisikue , kuzungukwa kwa hatari kwa Mchungaji
Dia na nchi ya milima kulimfanya kupuuzia kuyafikia makundi ambayo Mungu
alitaka aweze kuyafikia na kuleta Uamsho
c. Mambo
yaliyochangia kukua kwa kanisa huko Ufilipino ni pamoja na mialiko,uwezo wa
kuwafuata watu ndani sana ,Mafundisho na mahubiri mazuri Uamsho wa wakristo,
ushuhudiaji wa nyumba kwa nyumba ,ufuatiliaji na kustawisha makanisa
yaliyozaliwa hali hii ilipelekea kuwako kwa Uamsho mkubwa nchini Filipino
Maeneo mapya ya kinjili
India
·
Mpaka mnamo nusuya Karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20 Tatizo kuu nchini India
lilikuwa ni ubaguzi wa wenyewe ka wenyewe ujulikanao kama Caste system mpaka
nyakati za hivi karibuni bado jamii ya kihindu wanafuata ubaguzi huu wa kijamii
kwa sheria iitwayo Manu jamii ya kihindui imegawanyika katika makundi manne y
jamii
·
1 Brahmins hii ni jamii ya makuhani na wasomi
·
2 Kshatriya
hii ni jamii ya mashujaa wanajeshi
·
3 vaishyas hii ni jamii ya wasanii,wafanya
biashara na wakulima
·
4 Sudras hii ni jamii ya vibarua na walala hoi
jamii ya watu wenye hali ngumu na waliolaaniwa
Brahimas Kshatriyak Vaisyas Sudras Outcastes
Jamii ya madaraja ya ubaguzi ya kihindu kama
yanavyoonekana katika michoro Picha na maelezo kwa hisani ya Library ya Mwalimu
wa somo Mchungaji Innocent Mkombozi Kamote
·
Katika
madaraja hayo manne ya watu huko India kuna madaraja ambayo yanaingilika na kuna madaraja ambayo
hayaingiliki kwa maswala ya kuwapelekea injili au hata mawasiliano ya kawaida
·
Mahatma
Gandhi wakati fulani aliwahi kufunga siku 21 na kuhatarisha maisha yake ili
kuwapandisha watu hao daraja na alifanya
kila jitihada kuwainua na walijulikana
kama Harijan ambalo ni jina maalumu kuwa watu wa Mungu hili ni jina walilopewa
na Mahatma Gandhi
·
Jamii
hii ya watu wa daraja la chini ni rahisi kuipokea injili huko india
ukilinganisha na madaraja mengine
Zambia
·
Zambia
injili iliingizwa kwa kupandikiza shule wamishionari wengi waliopanda makanisa
kusini mwa jangwa la sahara walitumia shule na hivyo ilisaidia watoto wa
wapagani waliokuja kusoma kuingiziwa injili na kuikubali
·
Kwa
msingi huo njia ya kuingiza injili katika eneo fulani inategemea kuwa mazingira
hayo yakoje na Mungu anakupa namna gani ya kupenda kanisa au kupeleka injili
kulingana na eneo husika
Iceland
·
Injili
ilipandwa kupitia kuongoka kwa fanilia nzima nzima mpaka mwaka wa 1000 baada ya
Kristo kisiwa chote kilikuwa kimeukubali ukristo
Amerika ya kusini Latin
America
·
Injili
iliwafikia kupitia Vyombo vya habari Redio ,Television na magazeti yalitumika
kuwafikishia ujumbe wa injili vilitumika
aidha kwa ajili ya kutangazia semina za kuandaa Viongozi, kampeni za
maombi,watenda kazi na mikutano mikubwa ya injili iliyokuwa na nguvu za Roho na
uponyaji vilizifanya nchi za Brazil na America ya kusini na kati kufikiwa kwa
injili
·
Waliompokea
Kristo walifanyiwa ufuatiliaji, walipewa Biblia na madarasa ya waongofu wapya
yalianzishwa ,makanisa ya nyumbani na shule za Biblia kwa njia ya Posta
Kwa msingi huo ni muhimu kufahamu kuwa ukuaji wakanisa
unatofautiana kati ya udongo na udongo au kati ya sehemu na sehemu na nivigumu
wakati mwingine kutumia kanuni iliyotumika sehemu fulani ikafanya kazi sehemu
nyingine na kama tulivyoona maeneo mengine Fedha inahitajika sana katika
kuwafikishia injili
LAIZMA UWEKE AU UTOE KIPAUMBELE KWA KILE AMBACHO MUNGU ANAKIPA
KIPAUMBELE
Jambo kubwa la msingi kabla ya
kuangalia kanuni zozote za ukuaji wa kanisa ni kukubali kutoa kipaumbele kwa
kile ambacho Mungu anakipa kipaumbele yaani kusudi lake la kuwafikia watu wote
duniani ni la Muhimu sana ukiisha kuwa na moto amabao Mungu anao ndipo sasa
yeye atakupa njia na msaada wa kukujulisha wapi uweke nguvu kubwa, wapi utoe
Muda wa kutosha ,wapi utapata Fedha kwa ajili ya kutimiza huduma
aliyokuitia ni kitu gani ambacho Mungu
anakipa kipaumbele?
·
Ni mpango mzima wa Mungu kwa wanadamu
·
Kila kinachofanywa sawa na maagizo ya Yesu ni
mpango wa Mungu na Mungu amekipa kipaumbele
mfano ,Kutoa chakula kwa wenye njaa, kuonyesha upendo na kuipeleka
injili kwa kila jamii au kushughulikia na yatima na wajane n.k.
·
Kubwa zaidi ni kuipeleka injili na kutimiza
agizo kuu kusudi kuu la Mungu ni kutafuta waliopotea ni kuwarudishia watu
uhusiano wake na Mungu Yohana 20;21,2Koritho 5;18
·
Kanisa ndilo lenye wajibu huu na kila mwamini
anao wajibu huu pamoja na kutimiza Mathayo 5;16
Kusudi la Mungu ni kutafuta kile kilichopotea
1. Luka
15 ina mafundisho yanayohusu Jinsi Mungu anavyotoa kipaumbele katika kutafuta
kile kilichopotea kuna mifano kadhaa inayotolewa katika sura hii kama vile
·
Mchungaji kutafuta mwana kondoo aliyepotea
·
Mwanamke kutafuta shilingi iliyopotea
·
Baba kutafuta mwana mpotevu
·
Mifano yote hiyo inaishia na kuonyesha furaha na
ushindi wa kukipata kile klilichokuwa kimepotea
·
Mungu ni lazima atafute kile kilicho chake
kilichopotea ni haki yake kwa sababu ni uumbaji wake kwa msingi huo kusudi la Mungu ni kuokoa na
kuhakikisha wale waliopotea wanarudi kwake na sio kupotelea huko
·
Kutafuta ni muhimu na kwa sababu hiyo kusudi kuu la Mungu au
kile amabacho Mungu anakipa kipaumbele ni kuhakikisha kuwa waliopotea wanakuja nyumbani
·
Kusudi la Mungu na huruma zake limefunuliwa
katika Luka 15 aidha tunaona katika sehemu nyingine pia za Biblia zikiunga
mkono kusudi hili la Mungu kwa mfano
Maombi ya Bwana Yesu kwa wanafunzi wake Mathayo
9;37-38
Agizo la Bwana Yesu kwa wanafunzi wake Mathayo
28;19-20
Mifano hiyo ya Bwana yesu kuhusu vilivyopotea
Lika 15
Kusudi Yesu alilolitoa kwa ajili ya kuja kwake
Luka 19;10
Msukumo wa Mungu kumtoa mwana wake wa pekee
Yohana 3;16
Kazi ya mitume katika kutimiza agizo kuu Matendo
2;37-38
Ujumbe kwetu kama mabalozi wa Kristo 2Koritho
5;18-20
·
Kwa msingi huu basi Mungu anataka kila kanisa la
mahali pamoja kuweka kipaumbele katika
maswala ambayo yeye ameyapa kipaumbele na tukafanya hivyo makanisa yatakua
2.
Fuata
maelekezo ya Mungu katika huduma
a.
Biblia inatoa maelekezo ya namna ya kutimiliza
huduma tulizo nazo katika kuwafikia wasio fikiwa kwa msingi huo kila muumini katika kanisa ni
lazima atumie nafasi uwezo na kipato alicho nacho katika kuhakikisha kuwa
wanavitumia vile Mungu alivyowapa katika kazi yake.
Kila mshirika atiwe moyo kutumia kile alichopewa
na Mungu kwa faida ya ufalme wa Mungu
Kumbuka ule mfano wa talanta Mathayo 25;14-30
unatupa ujumbe gani
Unato aonyo kwa wale wasiotumia kile walicho
nacho hata kama ni kidogo
Kanisa litakuwa na kuongezeka kama kila mshirika
atatumia kwa makini au kufuata kwa makini maelekezo ya Mungu na kutumia njia na uwezo aliopewa na Mungu
kwa namna yoyote ile kuwafikia wengine
Kwa msingi huo kila mmoja anahitaji maelekezo
Binafsi ya Mungu ili kushiriki au ashiriki namna gani katika kulitimiza Jukumu
lililoko mbele yetu
b.
Wajibu wetu Kibiblia sasa ni lazima kuweka
kipaumbele katika mambo yale ambayo Mungu anayapa kipaumbele tukikumbuka kuwa
watu Bilioni tatu hivi duniani hawajafikiwa wala kuisoma Biblia hata ile ya agano
jipya Jukumu hili si la watu fulani ni Jukumu la kila mtu kwa hiyo watu wafanya nini sasa ili kutimiza
majukumu yao?
Kila mtu anawajibu wa Kushuhudia watu nyumba kwa
nyumba au mtu kwa mtu
Kuwezesha
vipindi katika vyombo vya habari
Kufanya mikutano ya mitaani
Kutembela wagonjwa mahospitalini na magereza
Huduma kwa wanafunzi mashuleni na vyoni
Na kuwafikia wasiofikiwa kwa kubuni mbinu ambazo
zitaleta matunda
Kuonyesha upendo kivitendo
Kufanya kazi hii na Roho Mtakatifu
LAZIMA UJUE KUFANYA KAZI NA MUNGU KATIKA UAMSHO
Uamsho ni nini?
Hakuna malezo ya kutosheleza
katika msemo mmoja juu ya Uamsho lakini kuna semi nyingi zinazoweza kutumika
kuelezea Uamsho
1. Ni
nguvu kubwa ya kiinjilisti iliyoamka inayowaleta watu katika mguso wa Roho wa
Mungu
2. Ni
kazi ya Roho Mtakatifu ya kupandikiza maisha mapya na nguvu za Ukristo na
kanisa
3. Ni
Kuamka kwa hali ya kujirudia ndani ya waamini ili kuwafikia wasio fikiwa au
wenye dhambi
4. Ni
Ufufuo au hali ya kurudisha uhai tena , ni kuamsha hali za kulipuka kwa
utendaji mkuu wa kimungu katika kanisa
Mambo sita yanayo saidia kuleta Uamsho
1. Kusudia
kuwa na uhitaji wa Uamsho
Lazima kama
unahitaji Uamsho katika kanisa lako basi kiwe ni kitu kilichomaanishwa kabisa
hii ni kwa sababu kuna wakati mwingine hutokea washirika wengine hawahitaji
Uamsho kwa sababu kadhaa zifuatazo
Wako washirika wanaogopa Uamsho
Wanahofia kuwa kutatokea mitikisiko mikubwa na maswala mengine yatafumuka
Wanahofia kutokea kwa migawanyiko kwani baadhi
watakuwa wanakiu ya kumtafuta Mungu kwa undani sana na wengine hawata mtafuta
Mungu
Hivyo ni lazima kama unataka Uamsho ukusudie
kweli kweli na washirika pia
2. Kubaliana
na Hali za Kipentekoste
Kumbuka kuwa ile hali ya wakati wa pentekoste
itashuka katika kanisa
Mabadiliko ya waamini binsfi na kundi lazima
yatokee
3. Kubaliana
na Mfumuko wa maombi
Watu wataungana kwa pamoja katika kuomba sawa na
matedno 4;24-31
Ujasiri wa kushuhudia na kuhubiri matedno
28;30-31
Kuokoka kwa wenye dhambi Matedno 9;3-5
Huduma za uponyaji na miujiza Matedno 19;11-12
Mapepo kufumuka na kutolewa matedno 19;11-12
Kusamehe maadui na kuwaombea maadui Matendo
57;54-60
Kutokea kwa mateso na majaribu makali na watu
kukubali hata kufa Matendo 20;9-12
Matukio ya kupita kawaida wakati wa ibada na wakati wa kuabudu
4. Soma
kwa undani kitabu cha Matendo ya mitume
Wengi wa watu waliofanikiwa kulpata Uamsho
wanashuhudia kuwa walipata nguvu hiyo kutokana na usomaji wa kitabu cha matendo
ya mitume na kutamani kuyaona waliyoyasoma
Uamsho mara nyingi huwajia watu wanaouhitaji na
kuuomba kwa bidii na hivyo lazima kuukaribisha na kusoma kitabu cha Matendo ya
mitume ni maandalizi ya Uamsho na namna ya kuukaribisha Uamsho kwa kawaida unaturejesha katika kile
kilichofanyika katika nyakati za kanisa la kwanza na hivyo tunahitaji kujua
nini kilitokea ili kujiandaa
5. Omba
kwa ajili ya Uamsho
Hakuna mahali ambapo Uamsho ulitokea Bila maombi
ya bidii kila mahali katika historia za Uamsho watu walianza kuomba sana kwa
bidii wakati mwingine kwa kuendelea kwa majuma na miezi bila kukoma
Huko Korea mwaka 1907 waamini walianza kuomba
kila saa 11 alfajiri na jambo hilo
lilichangia katika kukua kwa kanisa
Amerika Mwka 1858 watu walihudhuria maombi kwa
viwango vikubwa sana mpaka ikashidnikana
namna ya kupatamahali pa kuwaweka muungano
wa madhehebu katika maombi ulichangia sana katika kukua kwa kanisa
Huko Scotland 1859 walianzisha maombi ya jioni
kila siku jioni kwa muda wa mwaka mzima
na Uamsho mkubwa ulitokea
Swala la kuomba na Uamsho linaonekana kwa wale
120 walioamua kusubiri kwa maombi kusubiri nguvu waliyoahidiwa na Kristo
Uamsho uliotuletea makanisa ya Kipentekoste ya
karne hii ya 20 ulianza na maombi kulikuwa na vikundi vya waombaji kutoka
makanisa mbalimbali kama Lutheren, Methodist, Presbyterian, catholics na
washirika wa makanisa mengine
Ni muhimu kuimba ,kuhubiri na kufundisha kuhusu
Uamsho pangeni Muda manaokubaliana kikanisa kwa ajili ya maombi ya Uamsho
Mahubiri kuhusu Uamsho yatawahamasisha kuwa na
hamu na shauku kwa ajili ya Mungu na kupandisha imani na kutaka Uamsho huo
Miwsho fanyia kazi yale yote unayoayaombea kwani
Imani bila Matendo imekufa Yakobo 2;20.
Ombea watu ujazo wa Roho Mtakatifu,hubiri,panda
makanisa,ombeni,anza kiri Uamsho.
Vikwazo Vikuu vya Uamsho katika makanisa
Mambo yanayosaidia kukua kwa
kanisa
Vikwazo vinavyozuia kukua kwa kanisa
Mazingira
Mazingira
1. Watu wanaopokea injili kirahisi 1. Watu wasiopokea injili
kwa urahisi
2. Mazingira ya watu wakaribishaji 2. Mazingira ya watu wasio
wakaribishaji
3. Watu wanaoingilika 3.
Watu wasioingilika wagumu kuwafikia
Watu wa ndani ya kanisa
Watu wa ndani ya kanisa
4. Watu waliobadilishwa hasa na
Kristo 4. Watu ambao
hawajajitoa kwa Kristo vuguvugu
5. Furaha na amani ya Mchungaji na 5. Watu wasio na amani
,mafarakano na migongano
Watu wake
6. Wakristo washuhudiaji 6. Kazi
ya injili imeachiwa Mchungaji tu
7. Mchungaji na washirika waliojaa
Roho 7.
Washirika na Mchungaji wasio na Roho
8. Mvuto wenye nguvu wa maisha 8.
Maisha yasiyo na ushuhuda
9. Maono ,imani na maombi. 9. Hakuna maono maombi wala imani.
10. Imani katika Neno la Mungu 10. Hawana imani katika
Neno la Mungu.
Program za ndani za
kanisa
Program za ndani za kanisa
11. Ibada zenye mpangilio na mvuto
mzuri 11. Ibada zisizo na mpangilio
unaoeleweka
12. Roho wa Mungu kupewa nafasi 12. Ibada zisizo na mwelekeo
13. Kanisa linye lengo la kufikia
wengine 13. Kanisa lenye
kujiangalia lenyewe pale pale lilipo
14. Mafunzo kwa washirika wote 14. Mafunzo kwa baadhi
ya washirika tu
15. Kanisa linalojali mshirika
mmojammoja 15.Kanisa ambalo Mshirika
anapotelea humo hajaliwi
16. Wote wanashiriki huduma
kikamilifu 16. Huduma inaachiwa
wale wanaolipwa tu
17. Watenda kazi wazuri wanafungua
kazi 17. Watenda kazi wazuri
wanapewa uongozi
Njia zinazotumiwa na
kanisa husika Njia
zinazotumiwa na kanisa husika
18. Kuhubiri na kuifundisha Biblia 18. Mafundisho na
mahubiri duni
19. Watoto wa washirika wanaokoka 19. Watoto wa washirika
wanasahaulika
20. Wanayafikia maeneo yasiyofikiwa 20. Wanahubiri ndani ya kanisa
tu
21. Mikutano ya injili mara kwa mara 21. Ibada za kawaida tu zinaendelea
22. Kutembelea na kushuhudia 22. Hakuna
kutembelea wala kushuhudia
23. Kutumia vyombo vya habari. 23. Hakuna matumizi ya
vyombo vya habari
24. Mafunzo ya Biblia kwa njia ya Posta 24. Hakuna mafunzo kwa njia ya
Posta
25. Maombezi ya miujiza na uponyaji 25. Hakuna maombezi ya uponyaji
na miujiza
26. Watu wanajitoa hasa 100% 26. Hakuna kujitoa
kwa dhati ni unafiki tu
27. Mipango ya kuongezeka 27. Hakuna
mipango madhubuti ya kuongezeka
SURA
YA PILI; UPANDAJI WA MAKANISA NI MOJA YA NJIA YA KUKUA KWA KANISA.
Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa ukuaji wa kanisa umegawanyika
katika makundi makuu matatu yaani
Kiroho, Kiidadi na kijiografia kukua kiroho ni hali ya kutoka katika uchanga
kuelekea katika hali ya kukomaa, kiidadi ni kuongezeka kwa idadi ya watu
wanaookolewa katika kanisa la mahali Pamoja, na kijiografia ni kutwawanyika
kutoka mahali pamoja na kupeleka injili na amakanisa katika maeneo mengine
KUKUA KIROHO
Kukua Kiroho ndio msingi wa kukua kwa namna nyinginezo zinazobakia,
njia ya ukuaji wa kiroho ambayo Bwana Yesu
ametuachia ni pamoja na Roho Mtakatifu na watumishi wenye wito maalumu ambao
wanaoitwa na Bwana kwa kusudi la kulikamilisha kanisa Matendo 1;8,Efeso 4;1-16
kwa msingi huo Kujumuika na wengine pia ni njia ya kukua Kiroho.
KUKUA KIIDADI
Kukua kiidadi ni moja ya njia ya kuonyesha uhai wa kanisa hata
hivyo yako mambo yawezayo kuchangia ukuaji wa kanisa hasa unapoangalia hali
halisi ya ukuaji wakati wa Kanisa la kwanza Kanisa lilikuwa kwa namna ya kupita
kawaida lakini moja au baadhi ya mambo yaliyochangia ukuaji ni pamoja na
Miujiza na Ushirika Biblia inatoa mwanga unaochangia katika ukuaji wa kanisa
kuwa ni pamoja na Kuhubiriwa kwa injili, kumruhusu Bwana afanye kazi pamoja nao
na kuthibitishwa kwa neno kupitia Ishara na miujiza Marko 16;20, “Kisha wanafunzi Wake wakatoka, wakahubiri
kila mahali, naye Bwana akatenda kazi pamoja nao na kulithibitisha neno Lake
kwa ishara zilizofuatana nalo.” Mambo mengine yaliyochangia katika ukuaji wa kanisa yako wazi katika
kitabu cha matendo ya mitume kiidadi.
Matendo
|
Tukio au matukio
|
Matokeo
|
2:1-41
|
Pentecoste,
Kujazwa Roho, Kunena kwa lugha, Mahubiri.
|
a
|
2:42-47
|
Mafundisho,
Ushirika, maombi, Miujiza, Umoja, Kuabudu, Kuwapendeza watu wote
|
b
|
4:4
|
Kuponywa
kwa mtu aliyepooza na mahubiri
|
c
|
5:12-16
|
miujiza, *
kumbuka inawavuta wengi wasioamini na ni chambo chambo
|
d
|
5:42-6:1-7
|
Mafundisho
na kushuhudia Hekaluni na nyumba kwa nyumba.
|
e
|
9:31
|
Wakati wa
amani,Kuishi kwa ajili ya Kristo na kutiwa moyo kwa Roho Mtakatifu
|
f
|
14:1
|
Kuhubiri
kwa ujasiri katika masinagogi
|
g
|
16:4-5
|
Kukataa mafundisho ya sheria,kutembelea
makanisa na kutoa msaada Kiroho
|
h
|
17:10-12
|
Kuhubiri
huko Beroya na kuyachunguza maandiko
|
i
|
19:8-20
|
Kuhubiri
na kufundisha na miujiza ya kila siku
|
j
|
Kwa hiyo utaweza kuona kuwa kanisa la kwanza lilianza na
idadi ya watu 120 na likakua na kuongezeka toka siku ya Pentekoste kwa kufikia
3000 na baadaye 5000 na baadaye watu waliendelea kuongezeka kiasi ambacho
Mwandishi wa kitabu cha matendo yaani Luka
anaeleza kuwa idadi ya watu wanaume kwa wanawake wakaongezeka kwa Bwana
Matendo 5;14 inasema “Lakini
walioamini wengi wakaongezeka kwa Bwana, idadi kubwa ya wanaume na wanawake” Kwa msingi huo kuongezeka kiidadi
ni mpango wa Mungu na tunapaswa kuuwaza na kuufanyia kazi aidha ni muhimu
kuweka Rekodi ya idadi ya watu kanisa la kwanza walijuaje kuwa kanisa
linaongezeka hii iko wazi kuwa walikuwa wakiwahesabu kila wakati chukua idadi
ya washirika wanaohudhuria.
KUKUA KIJIOGRAFIA
Huku ni kukua kutoka eneo moja kuelekea eneo lingine Ni
muhimu kufahamu kuwa kanisa la kwanza pia walikuwa kijiografia ingawa
kutawanyika kwao mwanzoni ilikuwa kwa ajili ya mateso lakini waamini
waliotawanyika walikuwa kama mbegu zilizokufa na kuzaa matunda, aidha agizo kuu
pia liko kijiografia Matendo 28; 18-28 Marko 16; 15 Matendo 1; 8 Kwa hiyo Yesu
alikuwa na mpango wa kijiografia wa kuifikisha injili ulimwenguni kuanzia
Yesrusalem, Uyahudi, samaria, na hata mwisho wa nchi
Umuhimu wa kukua
kijiografia
Kukua kijiografia ndio kiini cha
somo hili kwa ufupi ndio kupenda makanisa, kupenda makanisa ni njia nzuri ya Kufanya
uinjilisti iliyo bora zaidi kuliko zote Mchungaji ukiona kanisa lililo komaa
lina kusumbua unaweza kulikabidhi kwa wachungaji wengine na ukaamua kupanda
kanisa jipya utajisikia Raha ya ajabu sana na utafurahia aina hii ya uinjilisti
kuna usemi usemao “NI RAHISI KUWA NA
MTOTO KULIKO KUFUFUA MFU” hapa simaanishi kuwa kanisa lililo kwisha
anzishwa ni mfu hapana lakini hapa nazungumzia kushughulikia na kanisa lililo
na udumavu wa kiroho ni kazi ngumu kuliko kuanzisha kanisa
Kwa nini ni muhimu kupanda makanisa
1. Kupanda
kanisa ni mpango wa Mungu wa Kibiblia na ni mpango wa Mungu sawa na Matendo 1;8
2. Kupanda
kanisa ni njia ya kuzalisha Viongozi wapya wa kanisa
3. Kupanda
makanisa ni njia ya kuleta Uamsho kwa makanisa ya zamani mara nyingi tunajua
kuwa makanisa yaliyotanguia huwa na tabia ya kujisahau na hivyo linapoanzishwa
kanisa jipya tayari hofu huwapata wale waliotangulia na hivyo Mungu hufurahia
sana huko mbinguni kwani ni changamoto kwa kazi na ufalme wa Mungu unajengeka
4. Kupanda
kanisa ni kuzuri kwani kunakusaidia kulifikia eneo jipya ambalo halijafikiwa na
injili Paulo mtume alisema hamu yake na shauku ni kuipeleka injili kule ambako
Kristo hajasikika Warumi 15;20
5. Kupanda
makanisa kunaimarisha Dhehebu lako si kwamba kupanda kanisa kwa kweli kwa
undani kunaimarisha mwili wa Kristo tu lakini dhehebu lako unalofanya kazi
pamoja nalo linaimarika kwa kueneza injili na kufikia maeneo yasiyo fikiwa.
Maadui wakuu wa upandaji wa makanisa
a.
Wakristo
wa mwilini
Tunapozungumzia
wakristo wa mwilini tunazungumzia jamii ya watu ambao aidha walimwamini Yesu na
kuipokea babdiliko la kiroho na kuwa na uwezo wa kushinda dhambi lakini baadaye
wakapoa na wakabaki na jina tu kuwa ni wakristo lakini wamekufa Ufunuo 3;1“Haya ndiyo maneno Yake Yeye aliye na zile
Roho saba za Mungu na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, kwamba una sifa ya
kuwa hai, lakini umekufa.” Pai ni jamii ya wakristo wanaoishi maisha
vuguvugu Ufunuo 4;14-16 “Haya ndiyo
maneno Yake Yeye aliye Amen, shahidi mwaminifu na wa kweli, mtawala wa uumbaji
wote wa Mungu. 15. Nayajua
matendo yako, ya kwamba wewe si baridi wala si moto. Afadhali ungelikuwa baridi
au moto. 16. Hivyo kwa kuwa u
uvuguvugu, kwamba wewe si baridi wala si moto, nitakutapika utoke kinywani
Mwangu.” Hawa ni wakristo wa majina tu na sio wakristo halisi pia wanaweza
kuwa wakristo waliozaliwa katika dini za Kikristo na hivyo wanaishi maisha ya
kawaida sana hawa wanakuwa kizuizi katika kupenda makanisa kwa vipi?
Hawawezi kuubeba injili na kuwapelekea wale
ambao bado hawajafikiwa na injili Warumi
10;14-15
Kanisa linakuwa na Jeshi dhaifu wakati Ufalme wa
Mungu unatekwa na wenye nguvu yaani watu wenye wivu wa kimapinduzi kwa ajili ya
Mungu Mathayo 11;12
Kanisa linakuwa na watu wasioweza kuzaa matunda
kwani wako nje ya mizabibu Yohana 15;5
Kanisa linaweza kuwa na watumishi wasio na wito
au kuwapa uongozi watu wasio wakristo, ndoa zisizoeleweka, na kuweza kupata
makanisa mbali sana na watu kukosa
sehemu za kuabudu
b.
Chanzo
cha wakristo wa mwilini Kuweko
·
Kukosekana kwa maombi
·
Kuanza kuchukuliana na dunia
·
Ubinafsi katika kutoa
·
Kuhubiri dini zaidi kuliko injili
·
Kushindwa kuwafikia wanafunzi kuanzia shule za
msingi mpaka vyuo vya Biblia
·
Kukosa Viongozi wazuri wa kiroho
c.
Uongozi Mbaya
Ni muhimu kufahamu kuwa aina za
Viongozi tunaowaandaa inaweza kuleta mafanikio makubwa au kutofanikiwa kwa kiasi
kikubwa katika ukuaji wa kanisa na upandaji wa makanisa,Yesu alichukua Muda wa
kutosha kuandaa Viongozi, mwanzoni hakulenga tu kujikusanyia maelfu ya watu
lakini alikaa na wachache ili kuwapandikizia kusudi la Baba yake na kisha kupitia wao kanisa lilikuwa na
kuongezeka Viongozi hufananishwa na Nguzo Wagalatia 2;6-9, utafiti unaonyesha
kuwa moja ya matatizo makubwa ya kutokukua kwa makanisa mengi ni Viongozi
d.
Kukosa majibu ya matatizo ya watu na
mahitaji yao
Kanisa linalokua ni lile ambalo
matatizo ya watu hupata ufumbuzi,kama kanisa haliwezi kukutana na mahitaji ya
watu basi halitimizi wito wake kwa ukamilifu chunguza duniani ukaone Popote
duniani mahali kanisa limekua ni pale ambapo watu hupokea majibu ya mahitaji
yao hii ndio huchangia wakati mwingine kuwa hata imani potofu zenye majibu ya
matatizo ya watu watu hujikusanya huko ni muhimu kuwa na kanisa ambalo Mwenye
dhambi anapokea Msamaha, wenye kiu wanakunywa, wenye njaa ya roho wanajazwa, wenye
magonjwa wanapona, walioteswa na ibilisi wanafunguliwa asiye na matumaini
anapokea matumaini watu wanatiwa moyo na wanautazamia uzima wa milele.
e.
Kukosekana kwa maombi endelevu
Maombi endelevu yanapokuweko katika
kanisa ni lazima kanisa litakua na kufunikwa na furaha ya kimungu watu
wanapokusanyika kwa ajili ya Mungu na kuomba Mungu huwa katikati yao na Mungu
humwaga Roho ya furaha kwa kujibu maombi na kushughulikia na mahitaji ya watu
na watu wanapotoka na furaha watu
huvutiwa kuwako mahali penye furaha, shetani hakimbii watu wanapohubiri au
wanaposhiriki meza ya bwana yeye hukimbia watu wanapoomba maombi yana nguvu
kubwa ya kulifanya kanisa kusimamia na kukua na kuongezeka
f.
Kushindwa kuwaachilia watu wa kawaida kwenda
kuanzisha kazi mpya
Kama watumishi Viongozi wa makanisa
wanataka makanisa yao yakuwe ni lazima wakubali kuwaachia watu wa kawaida
kutoka na kuanzisha kazi mpya lakini ni muhimu pia kanisa likiwaandaa kwa kazi
hizo kama kanisa halina muundo unaoruhusu watu kumtumikia Mungu basi hata kama
kubna watu wenye kiu ya kufanya hivyo hawawezi kufanya hivyo wachungaji wanao
wajibu wa kuwafundisha na kuwatia moyo watu wa kawaida na kuwatuma katika
huduma hata kama wakati mwingine watu hao ni muhimu katika kanisa mama
unapoacha ubinafsi na kujaribu kulifanyia kazi hili kanisa litakua kwanini
kanisa lisikue kwa mtu wa aina hii.
g.
Kukosekana kwa maono
Makanisa mengi yasiyokuwa ni yale
yenye Viongozi wabinafsi na wasio na maono ya kiulimwengu wao hujitazama
wenyewe tu jambo hili linaweza kupelekea watu kujichokea kanisa lazima liwe na
maono ya kupeleka injili kila mahali kusikofikiwa, lazima liwaombee watu hao na
kuwawezesha kanisa linapofanya haya haliwezi kuzeeka bali linakuwa kijana,zuri
na lenye nguvu kinyume cha hapo linakomaa na mazoea huchukua nafasi na kunakua
hakuna jipya
h.
Kukosa kiongozi mwenye uwezo mkubwa wa
kimaongozi
Mchungaji anatakiwa kuwa mtu mwenye
maono makubwa imani na uwezo mkubwa wa kuongoza akiwa amejaa maombi, asiyekata
tamaa, mwenye uwezo wa kuipokea maono toka kwa Mungu na kuongoza watu, Kama
katika kanisa lako hakuna mtu anaweza kufanya lolote mpaka kwa ruhusa ya
Mchungaji fahamu kabisa kanisa hilo haliwezi kukua lakini lazima Kuweko na
umoja yanapokuja maono kama ni kwa Mchungaji Viongozi wakiyaunga mkono kwa
kauli moja kunakuwa na nguvu kubwa na
kazi itafanikiwa, Kama uongozi wa Mchungaji ni dhaifu kanisa lote linakuwa
dhaifu Mchungaji akiwa na uwezo mkubwa wa kuubeba maono basi washirika
watayapokea kwa nguvu na kumuunga mkono na kumtia moyo,makanisa mengi hayakui
kwa sababu tu hayana Viongozi wenye uwezo wa kubeba Jukumu kubwa la kimaongozi
SURA YA TATU: SIFA ZA MTU MWENYE KUANZISHA KANISA
Kanisa linaweza
kuanzishwa na mtu Yeyote
Kanisa linaweza kuanzishwa
na mtu wa aina yoyote anaweza kuwa Mmisheni, Mwinjilisti, Mchungaji, mtume au
nabii au mtu yeyote wa kawaida ambaye katika mpango wa Mungu amepata nafasi ya
kufanya hivyo lengo likiwa ni kumpanda Kristo katika jamii ya watu wasiomfahamu
na kuanzisha ushirika wa mahali pamoja kwa msingi huo kupenda kanisa hakuhitaji
mtu fulani maalumu sana au mwenye sifa ambazo ni za hali ya juu sana Nyakati za
kanisa la kwanza makanisa mengine mengi yalianzishwa na watu wa kawaida tu Matendo
8;4 “Lakini wale waliotawanyika wakaenda
huko na huko wakilihubiri neno” kwa
msingi huo hatupaswi kuogopa kuanzisha makanisa unahitaji imani tu je unafikiri mtu anayepaswa kuanzisha kanisa
anatakiwa kuwa wa namna gani?
·
Hakuna
sifa maalumu za mtu anayepaswa kuanzisha kanisa Mungu hutimia watu wa kawaida
tu
·
Mtu
anaye anzisha kanisa anapaswa tu kuwa mtu anayekubalika na watu wale anaotaka
kuwafikia katika jamii na Elimu yao
·
Awe
ni mtu mwenye haiba ya kuingiliana na watu wapya na kuwavutia kwa muda mfupi tu
na kuweza kuzungumza na watu wa kila aina na kila ngazi,Mtu anayejificha, na
kujitenga na watu na kutokusikia raha kuhusu watu hasa wageni hawezi kufanikiwa
katika kuifanya kazi hii
·
Awe ni mtu anayejali sana watu na kuwajibika kwa
ndani sana kuhusu matatizo yao ya
binafsi
·
Lazima
awe mtu wa Mungu yaani aliyeokolewa ingawa si lazima awe na ujuzi sana
·
Lazima
awe anasukumwa na upendo wa ndani sana wa kimungu kwa ajili ya watu
wanaopotea sawa na Mchungaji anayetafuta
kondoo aliyepotea Luka 15;3-7
·
Awe
mtu wa maombi Wakolosai 1;9-11,2;1-3,Efeso 3;14-19 1thesalonike 1;2-3 Mathayo
9;39 Yesu alisema Ombeni ili Bwana wa mavuno atume watenda kazi katika shamba
lake
·
Anatakiwa
kuwa mtu wa maono na mbunifu huku akiwa na mvumilivu na mtu asiyeweza kukata
tamaa akiwa mtu wa imani kwamba anachokifanya ni mpango wa Mungu na kuwa Mungu
amemtuma kuifanya kazi hii.
Jinsi ya kuanzisha
kanisa
Ni muhimu kufahamu kuwa hakuna njia maalumu ya kuanzisha kanisa
uongozi wote wa namna ya kuanzisha kanisa unaachwa kwa Roho Mtakatifu, njia
iliyotumika eneo fulani inaweza isifanya kazi katika eneo lingine kwa msingi
huo tunaweza kujifunza tu kutoka katika uzoefu wa namna watu wengine
walivyotumiwa na Mungu katika kuanza makanisa na mafanikio waliyoyapata
kutokana na njia walizozitumia wakawapata watu waliookolewa na makanisa yakakua,
tunajua kuwa kuna shuhuda nyingi sana kuwa kuanzisha kanisa ni kazi ngumu
lakini kumbuka kuwa Roho wa Mungu ndiye anayefanya kazi na mtu anaye anzisha
kanisa njia hizi hutumika katika kuanzishwa kwa makanisa.
·
Kuanzishwa
kanisa kupitia Mikutano ya injili na baadaye kuwa na mpango wa namna ya
kuwatunza wale waliookolewa na kuwalisha Neno, Kumbuka kuwa kuhubiri pakee
hakutoshi ni lazima kuhubiri injili kuambatane na Kuweko kwa mipango ya malezi
ya watu wanaookolewa
·
Kuanzishwa
kupitia ushuhudiaji wa mtu kwa mtu hii
ni njia yenye matokeo makubwa sana kuliko hata mkutano wa injili katika maeneo
mengine na imeleta matokeo mazuri na mahusiano mazuri yanayoweza kufungua njia
ya kufanya ufuatiliaji kwa waongofu wapya
·
Kanisa
mama kugawa watu na kuanzisha tawi lingine kwa amani hii nayo ni njia inayoweza
kutumika katika kuanzisha kanisa jipya na kuyafikia maeneo yasiyofikiwa
inawezekana tu kwa wachungaji wasiojali maslahi yao Binafsi.
·
Kuna
njia nyingine yoyote inayoweza kufaa katika uanzishaji wa kanisa basi inaweza
kutumiwa katika kuanzisha kanisa
Mambo ya kuzingatia
wakati wa kupanda kanisa
1.
Hakikisha unafanya uchunguzi wa eneo
unalotaka kuanzisha kanisa (Survey).
Kufanya survey ni jambo la msingi
sana na la kibiblia kabisa wote tunakumbuka kuwa wakati Mungu alipokuwa anataka
kuwarithisha wana wa israel nchi ya kanaani alimwamuru Musa kuwatuma watu 12
wapelelezi ili kuipeleleza nchi maana yake ni kufanya uchunguzi kuwa nchi ile
ni ya namna gani Hesabu 13; 1-21. “BWANA akamwambia Musa, “Watume baadhi ya watu wakaipeleleze nchi
ya Kanaani,ambayo ninawapa Waisraeli. Kutoka katika kila kabila la baba zao
tuma mmoja wa viongozi wao.’’ Hivyo kwa agizo la BWANA Musa akawatuma kutoka
Jangwa la Parani. Wote walikuwa viongozi wa Waisraeli. Haya ndiyo majinayao:
Kutoka kabila la Reubeni, Shamua mwana wa Zakuri, kutoka kabila la
Simeoni, Shafati mwana wa Hori, kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune,
kutoka kabila la Isakari, Igali mwana wa Yosefu, kutoka kabila la Efraimu,
Hoshea mwana wa Nuni, kutoka kabila la Benyamini, Palti mwana wa Rafu, kutoka
kabila la Zabuloni, Gadieli mwana wa Sodi, kutoka kabila la Manase (kabila la
Yosefu), Gadi mwana wa Susi, kutoka kabila la Dani, Amieli mwana wa Gemali,
kutoka kabila la Asheri, Sethuri mwana wa Mikaeli, kutoka kabila la Naftali,
Nabi mwana wa Wofsi, kutoka kabila la Gadi, Geueli mwana wa Maki. Haya ndiyo
majina ya watu ambao Musa aliwatuma kuipeleleza nchi. Mose akampa Hoshea mwana
wa Nuni jina la Yoshua.” Musa alipowatuma wakaipeleleze Kanaani, alisema,
‘‘Pandeni kupitia Negebu, mwende mpaka nchi ya vilima. Mwuone nchi ni ya namna
gani na kama watu waishio humo wana nguvu au dhaifu, iwapo ni wachache au
wengi. Kwamba wanaishi katika nchi ya namna gani? Je, ni nzuri au mbaya?
Wanaishi katika miji ya namna gani? Je, haina kuta au ngome? Ardhi ikoje? Ina
rutuba au la? Je, kuna miti ndani yake au la? Jitahidini kadri mwezavyo kuleta
baadhi ya matunda ya nchi.’’ (Ulikuwa msimu wa kuiva zabibu za kwanza.) Hivyo
wakapanda na kuipeleleza nchi kutoka Jangwa la Sini hadi Rehobu, kuelekea Lebo
Hamathi”.
·
Peleleza
mfumo wa jamii yao jinsi ulivyo
·
Chunguza
vikwazo vya kiroho vilivyoko katika eneo husika
·
Chunguza
sheria zao na mila na tamaduni zao
·
Mahusiano ya
kifamilia katika jamii
·
Dini na
mdhehebu yaliyoko hapo
·
Viwango vyao
vya maadili aina ya watu, uchumi wao Lugha zao,tamaduni zao
Maswala ya kuyachunguza katika jamii unayokwenda kupanda kanisa
2. Hakikisha unaanza na eneo ambalo linapokea injili kwa urahisi
(Receptive Areas)
Jambo la msingi katika kupenda makanisa baada ya kuwa umefanya
Survey chunguza ni wapi mavuno yako tayari kisha anzia huko ndege kubwa
huanguka na kuvunjika kunapokuwa na wing uzito au ukungu unaomfanya Pilot
asione vizuri na wakati mwingine ndege inaweza kupata ugumu wa kutua na kugonga
milima kwa sababu ya kutokuona
vizuri hii ni kwa sababu ya kushindwa
kuona vizuri, hali kama hii huweza kutokea wakati wa kupenda kanisa Mungu anapokutuima katika eneo fulani atakuongoza kule ambako kuna upenyo wa watu
kuipokea injili wakati mwingine atakuongoza kwa Roho wake na wakati mwingine atakuongoza kupitia
kutazama vema Matendo 10;1-23 Yohana 4;30-35 kwa msingi huo ni muhimu kugundua
maeneo ambayo injili inapokelwa kwa uarahisi na kuyafikia kwanza ili utaligundua kwa upokeaji wao wa injili na
mwitiko mkubwa wanaoonyesha kwa ujumbe wa injili
3. Hakikisha kuwa unayafikia makundi yote
Mpango wa Mungu ni kuwafikia watu wote kwani kwa Mungu watu wote ni sawa ,Yeye
hushughulika na watu wote na mahitaji yao na matatizo yao kwa viwango vyovyote
walivyo navyo awe masikini au tajiri,msomi au mjinga kwea msingi huo Mungu hana upenmdeleo kwa
hiyo zingatia kuyafikia makundi yote kosa moja lifanywalo na watumishi wengi
sana ni kulenga kundi fulani na kuacha kundi jingine huu sio mpango wa Mungu
fikia Masikini, wafanya biashara, matajiri, wanasiasa,Viongozi, vibarua ,wasio
na kazi usipendelee kundi fulani kwa ajili ya mafungu Ubaguzi ni dhambi Yakobo
2;1-9
4. Panda kanisa linalojitegemea (the Indigenous churches)
Moja ya matatizo yanayoyapata makanisa mengi na kuathiri ukuaji wa
makanisa hayo ni kutegemea msaada hii ni sumu mbaya sana mchungaji au mpandaji
wa kanisa lazima ahakikishe kuwa kwa kadiri inavyowezekana anapanda kanisa
linalojitegemea na kujiendesha na kujiongoza
na kujieneza na kujitafasiria Maandiko
sawa na mazingira yake kanisa la namna hii lipande kila mahali ambako injili
hupokelewa kirahisi, sio dhambi kutegemezwa kwa sababu ni mpango wa Mungu pia
lakini msingi mzuri ni kutokutegemea watu bali kumtegemea Mungu jambo la namna
hii litakusaidia katika kuhakikisha unakuwa na kanisa lenye ufahamu wa kutosha
na linaloweza kuwa na faida kubwa katika ufalme wa Mungu kwa kazi za baadaye
Ufunguo wa kanisa linalotaka kukua lazima uwe Kanisa linalojitegemea
Self suppoting church, kanisa linalojiongoza Self governing, Kanisa
linalojieneza self propagating linalojaa roho na kujitafasiria Maandiko
kulingana na mazingira yake.
5. Hakikisha kuwa unaweka msingi mzito wa
muhimu kwa kanisa jipya
Mtu anayeanzisha kanisa anapaswa kuahakikisha kuwa anajenga msingi
imara kwa kanisa analolianzisha msingi
huo ni mafundisho mazuri na sahii kwa, Mwanzilishi wa kanisa ni kama mjenzi na
kwa msingi huo anapashwa kujenga msingi imara katika kanisa analolianzisha kwa
faida ya umaliziaji wa baadaye na ili
kanisa liweze kuwa na msingi wa kukua lazima lifundishwe majukumu ya kila
mkristo na Baraka za kutimiza majukumu hayo na waelekeze kazi na wajibu wa
kanisa kwa Mungu kwa kanisa lenyewe na kwa jamii inayolizunguka kanisa yaani
kuabudu, ushirika na kuwafgikia wasiofikiwa.
6. Hakikisha kuwa unapanda kanisa lenye
nidhamu
Kanisa linalopandwa lazima liwe kanisa linaloweka msingi wa nidhamu
mbele na pia kutowaaacha wale walioanguka katika neema ya Mungu bila
kuwarejesha katika ushirika na utumishi Mungu anachukizwa na wachungaji
wasiojali kondoo Soma ezekieli 34, Wagalatia 6;1-2 mithali 24;16Mika 7;8
1Thesalonike 5;14 Isaya 35;3 na Waebrania 12;13 Lengo likiwa kurekebisha, kurudisha
kutunza ushuhuda na kuwaonya wengine Mungu atakupa Hekima ya kushughulikia na
matatizo hayo kwa njia mbalimbali.