Sikuwa nafikiria kuwa jambo lile
kuna siku litakuja kuniumbua Hata wewe nikikusimulia utakuja kuniunga mkono
kwamba isingekuwa rahisi kwangu kuhisi hivyo, mimi ni mzaliwa wa mkata, kijiji
kimoja maarufu sana kwa kuuza mbuzi na nyama ya mbuzi, kando ya barabara ya
chalinze hadai Segera kwa wale ambao
wamekwisahawahi kupita barabara hiyo, huenda wanakijua vema kijiji hicho. Mzazi
wangu mmoja yaani baba alishafariki wakati nikiwa na umri wa miaka sita hivyo
nililelewa na mama.
Nilifanikiwa mwaka 1998 kuendelea
na masomo ya kidato cha kwanza, nilifanya mtihani wa mwaka 1997 ambapo
sikufaulu lakini mjomba wangu mmoja alinitafutia shule ya kurudia mkoani Pwani,
nilifaulu mwaka uliofuatia na kwenda pale kibaha, ni ujiko eh! Mtu kusoma shule
aliyosoma Kikwete! Kila aliyesoma kibaha hivi sasa bila kuulizwa atakuwa
anasema mwenyewe.
Mwaka 2002 nikiwa nimemaliza
masomo ya kidato cha nne na kuja Dar kwa dada yangu anayeishi tandika, nilifanikiwa
kupoata rafiki wa kike, huyu binti ni mtoto wa mtu mkubwa na alinipenda siku moja nikiwa nimekwenda
kutazama matokeo yangu ya Baraza la mitihani, nilikuwa nimefaulu kidato cha
tano kwa kweli mimi ninajipenda na jinsi nilivyo mtu akiniona anaweza kuniamini
kabisa kwamba natoka kwenye familia babu kubwa, huyu binti naye aliamini hivyo
pia, sikutaka kujiangusha, kwani tulipozoeana aliniuliza kuhusu familia yangu
nilimwambia mama yangu amekuwa anaishi Namibia kwa miaka mingi anafanya
biashara na baba yangu alikuwa ubalozini
Urusi lakini Alisha kufa.
Naona mtoto kusikia hivyo aliona
amekutana na mtu ambaye wanakaribiana kwa uthamani, Basi mwezi wa sita tangu
kujuana siku moja Yule binti akaniomba nijifanye kuwa nimesahau nitie timu kwao
yaani nimtembelee Nyumbani kwao.
Nilimuuliza kama haita wakera
wazazi wake akasema isingewezekana kuwakera, Basi kijana nikaamua siku hiyo ya
juumapili, nikaenda kwao huyu binti, nikasema mtoto wa mtu mkubwa ujue maeneo
anayoishi sio tandika shauri lako Nilifika kwao kwenye milango ya saa tano
asubuhi, Nilipokelewa kwa shangwe sana. Baba wa mtoto hakuweko lakini mama yake
alikuweko nyumbani, nilitambulishwa kwa
mama na nikaulizwa kinywaji nikajifanya muungwana, nikaomba maji, halafu
tukaanza kupiga stori na Yule binti na mama naye alijiunga na kuniuliza habari,
niligundua kuwa huyu mama alikuwa akipenda watu wa bei ghali kidogo, nami
nikawa nashindilia mauongo na maujiko mengi sana katika kujipandisha wakati wa kula ulipofika
ndipo balaa lilipoanza na kuishia nikiwa nimekaa aliingia jamaa mmoja
mchafumchafu kidogo He kuhiona tu akaniita kwa jina langu na kuanza kuangusha
kilugha yaani lugha ya kizigua halafu kabla sijajiandaa kuepusha gharika
janga lingine lilitokea “mama huyu ndugu yangu kule kijijini tena hata juzi
nilipokwenda kule kijijini nilikutana naye akitokea shambani…………”
Unajua kuwa kuna watu ambao akili
zao zinafanya kazi kwa kusigishana na midomo yaani vitu hivyo havikubaliani .
Aisee nilionana na mama akasema uko shule, alikuwa anatoka kwenye lile shamba
lenu la mihogo kule juu…” Mfumo wangu wa kufikiri ulikuwa kama umepigwa radi
kwa hiyo netiweki zilidumaa na kukata mawasiliano kwa muda.
Wewe vipi kwani mama yeke huyu
yuko kijijini analima au yuko Namibia wewe umechanganyikiwa au unachanganya
watu nini? Yule demu wangu alisema akiwa katahayari, Sasa sister wewe na mimi
ni nani anamjua huyu jamaa vizuri? Mama yake tunaishi mtaa mmoja kule home
tangu tukiwa wadogo ………”
Unategemea kulitokea nini? Kama
hujui kulitokea nini huna haja ya kuamini kuwa zako ziko sawa hata mwanao wa
miaka sita ukimuuliza atakwambia, niliadhirika na kufedheheka yaani ilikuwa
noma la mwaka! siku hizi nikiona kila mkata majani kwenye nyumba ya afisa
namchukia tu bila sababu! Unataka kujua yaliishaje Ni umbea unaokusumbua au
kitu gani ona mijimacho yako kutaka kujua ya watu we yako lini?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni