Maswahibu haya yalimkuta rafiki
yangu mmoja kwa bahati mbaya kwa sasa jamaa ni marehemu na alifariki mwaka juzi
ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu alipopatwa na fedheha ile, siandiki kisa hiki ili
kwamba labda nataka kumuadhiri, hapana naandika kisa hiki kwa sababu
tulijifunza jambo moja kubwa sana baada ya kufedheheka kule,
Mmea Jamii ya Bangi ni mmea wenye utata Duniani
Ilikuwa ni mwaka 2001, nilikuwa
wakati huo ndio kwanza nimeanza kibarua kwenye kampuni moja ya kuuza mafuta na
nilikuwa na rafiki yangu ambaye alikuwa anafanya kazi katika kituo cha kuuza
mafuta pia, lakini huyu rafiki yangu alikuwa ameanza kazi zamani kidogo ni
miaka mine kabla yangu. Mwaka 2000 jamaa yangu alifikiria swala la kuoa na
kuamua kutafuta mchumba, huyu mchumba alikuwa ni wa kutoka katika familia ya
dini sana, wazazi wake walikuwa ni waislamu wale wanaoitwa waswalihina, ingawa
nilikuwa najua kuwa rafiki yangu huyu alikuwa hana kitu, uchumba uliiva
ilipofika januari 2001,Tulifanya mipango na taratibu ili ndoa ifungwe kabla ya
mei lakini lilitokea tatizo kubwa februari. Yule jamaa alituhumiwa kwa upotevu
wa fedha pale kazini kwake na hivyo alisimamishwa kazi, mtafaruku huu ulifanya
kasi ya kuoa ipungue ingwa ndugu wa
jamaa yangu walishinikiza mambo
yaendelee kama yalivyokuwa yamekusudiwa, Jamaa yangu alijaribu kupinga mawazo yao na kusema hawezi kuoa wakati hana
kazi lakini ndugu zake walimzidi nguvu na alilazimika kukubaliana nao kwa hiyo
ilipangwa ndoa ifanyike kabla ya Augosti tuliendelea na maandalizi ingawa jamaa
yangu hakuwa na furaha kufuatia kufukuzwa kazi.
Ilifika tarehe ya mahari ukweni
na hivyo ilibidi wana ndugu maalumu wafanye kazi hiyo, miongoni mwa wanandugu
wanne waliotumwa kupeleka mahari baada ya barua yetu kukubaliwa mimi nilikuwa mmoja
wao, tulituma ujumbe kwanza kuwa tutafika saa sita mchana siku ya jumamosi pale
kariakoo kwa wakwe watarajiwa, ni kweli tuliondoka saa 5;30 pale kwetu
Kinondoni na kufika hapo kariakoo saa
5;45 hivi tuliegesha gari tulilokodi na kuanza kuelekea pale kwa wakwe. Lakini
ghafla walitokea vijana kama sita hivi
ambao walikuwa wanaonyesha kila dalili ya kwamba walikuwa wamevuta bangi na kubwia unga,
walituzuia na wenyeji wetu walikuwa wameshatoka kuja kutulaki “Leo
utatwambia kama sisi ni Waisrael au Wayahudi mmoja wa wale vijana sita alisema akiwa
anamwangalia Yule jamaa yangu halafu ghafla walikuwa wamemzunguka na kutuacha
sisi tukiwa tumeduwaa, tunaomba mkwanja wetu au tufanya kisichotarajiwa sasa
hivi, mwingine ambaye ndiye aliyeonekana kuwa kiongozi wao alisema
akionyesha ala ya kisu ambayo ilikuwa ikining’inia kiunoni Yule jamaa yangu alibaki mdomo wazi kwa muda Alipopata nguvu ya kusema alisema sasa, mbona
tunataka kuadhiriana jamaa zangu? Kabla hawajajibu kaka wa jamaa yangu
aliiingilia kati na kuuliza jamani hebu tumswalie mtumee ni jambo gani
linaendelea hapo? Mmoja kati ya wale vijana walevi alisema labda tumesha mswalia sana huyu jamaa yako ndiyo bado anataka
kujifanya yeye Mpalestina sana…’
Ilibidi wenyeji wetu nao
kuingilia Baba mkwe aliwasogelea wale vijana na kumshika mmoja Ati vijana wangu
kuna tatizo gani? tunaweza kuyamaliza haya mambo kiungwana bila mikwaruzano
hebu tuliweke wazi….’ Kabla haja maliza mwingine kwenye kundi la vijana wale alisema hapo sasa umekuja penyewe, Huyu bwana
anayejifanya leo kakwendea kipemba kwa
tarabushi tuna…’ Kabla hajamalizia Yule jamaa yangu aliingilia kati Sikiliza
Bajalo tutayamaliza ngojeni kwanza
nimalize mambo yangu hapa halafu tutajadili baadaye na nitafiksi kila kitu, kijana mwingine
aliingilia kati na kusema kila siku
utafiksi utafiksi jana umetwambia kuwa umeacha
mzigo kwa demu wako, tukaenda patupu, tukaenda kwa Yule manzi wako wa
huku kawe naye miyeyusho tu mshikaji
wangu sasa leo lazima kieleweke mkubwa wetu…’
Yule aliyeonekana kuwa mkubwa wa
kikosi alimgeukia baba mkwe wetu mtarajiwa na kumwambia Sikiliza mkuu huyu
jamaa tunamuuzia kitu yaani unajua huwa tunamuuzia bangi, mzee mwenzetu, hakutulipa
ndo hivyo hadi kwanza ……..halafu zamani hakuwa hivi alikuwa freshi tu..”
Kwakweli hata mimi nilishituka
kwa sababu sikuwa najua kwamba jamaa anavuta bangi ingawa nilikuwa na wasiwasi
na jambo hilo mkwe mtarajiwa aling’aka na kuuliza bila kutarajia ni kweli haya
mwanangu? Wale walevi wenzie walipaza sauti kwa pamoja mzee hiyo haina noma
hapakaziwi mtu hapa mmoja aliendela kung’aka tunataka michome yetu Laki taslimu
halafu wote tulishangaa kusikia deni la bangi la lakimoja Yule baba mkwe
mtarajiwa alirudia swali lake kama vile
hakuwa akisikia kitu kingine chochote
pale jamaa yangu aliinama na kusema ndio mzee.
Mzee Yule yaani baba mkwe mtarajiwa alisema astaghafirulah!
Tulitulia kwa muda. Najua unataka niendelee kukusimulia kwa akili yako unadhani
tuliruhusiwa kutoa mahari sawa kwa sababu unadhani wote wana njaa ya mahari na sio nidhamu si ndio eee muangalie vile!.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni