Jumanne, 1 Mei 2018

Neno la Mungu na utawala wa Kidemokrasia!



Ni muhimu kufahamu kuwa nyakati hizi tulizonazo ni nyakati za mwisho, Yeye ajaye anakuja wala hatakawia. Waebrania 10:37 “Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia.Katika nyakati hizi ambazo maandiko yanaziita za hatari; ni muhimu kuwa na ufahamu wa rohoni na kuwa na macho ya rohoni ili kwamba tuweze kujua majira na nyakati na kujiandaa vema na kurudi kwa Bwana Yesu, na ili kwamba pia tusiwe miongoni mwa hao wanaopotea.


Katika nyakati za kizazi cha leo tumekuwa tukisikia sana neno “Demokrasia” au utawala wa kidemokrasia na tumeona jinsi ambavyo kupitia utawala huu wa kidemokrasia kumekuwepo na mwamko mkubwa sana wa watu kutaka kuwa na uhuru, uhuru wa kuzungumza, uhuru wa kutoa au kupokea habari, uhuru wa kuchagua lolote mtu atakalo, uhuru wa kuamua, kumuoa au kuolewa na yeyote umtakaye uhuru wa kuabudu,Usawa wa kijinsia, vurugu na ugaidi pamoja na Haki za watoto, Hakiza Binadamu na aina nyingine za usawa na maswala yanayofanana na hayo, Yote yakiwa yamekuja na kifurushi hiki kiitwacho demokrasia kwa nini neno demokrasia linapata nguvu sana katika nyakati zetu, na linaonekana kuwa na washabiki wengi sana duniani? Leo tutachukua Muda kulitafakari neno hilo chini ya somo hili Muhimu Neno la Mungu na utawala wa kidemokrasia, na tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele muhimu vifuatavyo:-

·         Maana ya neno Demokrasia
·         Mifumo ya utawala wa dunia na serikali za wanadamu duniani
·         Neno la Mungu na utawala wa kidemokrasia
·         Hatari ya uhuru uliokithiri chini ya mfumo wa Kidemokrasia

Maana ya neno Demokrasia.

Neno Demokrasi limetokana na neno la kiyunani “DemosKratein” ambalo ni muunganiko wa maneno mawili ya kiyunani Demos – ambalo maana yake ni watu na Kratein- ambalo maana yake kutawala au utawala, Kwa msingi huo neno Demokrasia maana yke ni Utawala unaotokana na nguvu ya watu au nguvu ya umma, Demokrasia ni mfumo wa siasa za dunia ambao unatoa mamlaka makubwa kwa watu kuamua, nani awaongoze, waongozwe vipi, wawajibike vipi, na kadhalika, Katika tawala za kidemokrasia viongozi nyeti kabisa huchaguliwa na watu, hivyo watu ndio wenye nguvu kuu ya maamuzi katika mifumo ya tawala za kidemokrasia, sio hivyo tu watu ndio wenye maamuzi ya kumkataa kiongozi na hata kumuwajibisha,  Mfumo huu wa utawala umepata nguvu kubwa sana katika nyakati hizi za mwisho wa dunia kuliko nyakati za tawala nyingine za kihistoria ambazo zimewahi kuitawala dunia, Katika maswala ya kiimani mfumo huu ni hatari zaidi kwa maisha ya kiroho na kanisa kuliko tunavyofikiri ingawa unaonekana kuwa unakubalika zaidi katika maisha ya wanadamu na unaungwa mkono zaidi duniani, na wakati mwingine tunaweza kusema kuwa una nguvu na umeangusha aina nyingine za tawala kwa vile zinaonekana kuwa za kizamani. Kabla hatujaona kwa undani hatari zake ni vema tukaangalia namna maandiko yalivyoweka wazi aina za tawala za serikali za wanadamu zilizotawala Dunia, kabla haujaa utawala wa Ufalme wa Mungu.


Mifumo ya utawala wa dunia na serikali za wanadamu duniani
 
Ni muhimu kufahamu kuwa mfumo wa utawala wa kidemokrasia na tawala nyingine duniani, sio kitu kigeni kwa wataalamu wa maandiko, Mungu ndiye ayatetawala Daniel 4:17 “Hukumu hii imekuja kwa agizo la walinzi, na amri hii kwa neno la watakatifu; kusudi walio hai wapate kujua ya kuwa Aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge.” Kwa kuwa Mungu ndiye anayetawala ulimwengu na ndiye anayeruhusu nani atawale na aina za utawala, Mungu anajua yote na hivyo aliwafunulia watumishi wake Tangu nyakati za Nebukadneza na Daniel ili kutujulisha majira na nyakati tangu wakati huo hata ufalme wa Mungu utakapotawala duniani, Unabii kuhusu mifumo ya serikali za dunia uko katika maono na ndoto aliyoota Nebukadreza na ikatafasiriwa na nabii Daniel kwa ajili ya vizazi vyote ili tuweze kuwa na akili ya kile kinachoendelea katika nyakati zetu, Unabii huu ulionyeshwa kwa njia ya Sanamu ya ajabu ambayo tutaiangalia na kupata uchanganuzi wake kama ifuatavyo:-



Daniel 2:1- 49. “Hata katika mwaka wa pili wa kumiliki kwake Nebukadreza, Nebukadreza aliota ndoto; na roho yake ikafadhaika, usingizi wake ukamwacha. Ndipo mfalme akatoa amri kuwaita waganga, na wachawi, na wasihiri, na Wakaldayo, wapate kumweleza mfalme ndoto zake. Basi wakaingia, wakasimama mbele ya mfalme.Mfalme akawaambia, Nimeota ndoto, na roho yangu imefadhaika hata niijue tafsiri yake. Ndipo hao Wakaldayo wakamwambia mfalme, kwa lugha ya Kiaramu, Ee Mfalme, uishi milele; tuambie sisi watumishi wako ile ndoto, nasi tutakuonyesha tafsiri yake. Mfalme akajibu, akawaambia Wakaldayo, Neno lenyewe limeniondoka; msiponijulisha ile ndoto na tafsiri yake, mtakatwa vipande vipande, na nyumba zenu zitafanywa jaa. Bali kama mkinionyesha ile ndoto na tafsiri yake, nitawapa zawadi na thawabu na heshima nyingi; basi nionyesheni ile ndoto na tafsiri yake. Wakajibu mara ya pili, wakasema, Mfalme na atuambie sisi watumishi wake ile ndoto, nasi tutamwonyesha tafsiri yake. Mfalme akajibu, akasema, Najua hakika ya kuwa mnataka kupata nafasi, kwa sababu mmeona ya kuwa lile neno lenyewe limeniondoka. Lakini msiponijulisha ile ndoto, iko amri moja tu iwapasayo; maana mmepatana kusema maneno ya uongo, na maneno maovu, mbele yangu, hata zamani zitakapobadilika; basi niambieni ile ndoto, nami nitajua ya kuwa mwaweza kunionyesha tafsiri yake. Wakaldayo wakajibu mbele ya mfalme, wakasema, Hapana mtu duniani awezaye kulionyesha neno hili la mfalme; kwa maana hapana mfalme, wala bwana, wala liwali, aliyetaka neno kama hili kwa mganga, wala kwa mchawi, wala kwa Mkaldayo. Ni neno la ajabu, hili analolitaka mfalme, wala hapana mwingine awezaye kumwonyesha mfalme neno hilo, ila miungu, wasio na kikao pamoja na wenye mwili. Basi kwa hiyo mfalme akaghadhibika sana, akaona hasira nyingi, akatoa amri kuwaangamiza wenye hekima wote wa Babeli. Basi ile amri ikatangazwa, na hao wenye hekima walikuwa karibu na kuuawa; watu wakamtafuta Danieli na wenzake ili wauawe. Ndipo Danieli kwa busara na hadhari akamjibu Arioko, akida wa walinzi wa mfalme, aliyekuwa ametoka ili kuwaua wenye hekima wa Babeli; alijibu, akamwambia Arioko, akida wa walinzi wa mfalme, Mbona amri hii ya mfalme ina ukali namna hii? Ndipo Arioko akamwarifu Danieli habari ile. Basi Danieli akaingia, akamwomba mfalme ampe muda, kisha yeye atamwonyesha mfalme tafsiri ile. Ndipo Danieli akaenda nyumbani kwake, akawapasha habari kina Hanania, na Mishaeli, na Azaria wenzake;  ili waombe rehema kwa Mungu wa mbinguni kwa habari ya siri hiyo, ili kwamba Danieli na wenzake wasiangamizwe pamoja na wenye hekima wa Babeli. Ndipo Danieli alipofunuliwa siri hiyo katika njozi ya usiku. Basi Danieli akamhimidi Mungu wa mbinguni. Danieli akajibu, akasema, Na lihimidiwe jina la Mungu milele na milele; kwa kuwa hekima na uweza ni wake. Yeye hubadili majira na nyakati; huuzulu wafalme na kuwamilikisha wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa; yeye hufunua mambo ya fumbo na ya siri; huyajua yaliyo gizani, na nuru hukaa kwake. Nakushukuru, nakuhimidi, Ee Mungu wa baba zangu, uliyenipa hekima na uwezo, ukanijulisha hayo tuliyotaka kwako; maana umetujulisha neno lile la mfalme. Basi Danieli akaenda kwa Arioko, aliyewekwa na mfalme kuwaangamiza wenye hekima wa Babeli; alikwenda akamwambia hivi, Usiwaangamize wenye hekima wa Babeli; niingize mimi mbele ya mfalme, nami nitamwonyesha mfalme ile tafsiri. Ndipo Arioko akamwingiza Danieli mbele ya mfalme kwa haraka, akamwambia hivi, Nimemwona mtu wa hao wana wa Yuda waliohamishwa, atakayemjulisha mfalme ile tafsiri. Mfalme akajibu, akamwambia Danieli, aliyekuwa akiitwa Belteshaza, Je! Waweza kunijulisha ile ndoto niliyoiona, na tafsiri yake. Danieli akajibu mbele ya mfalme, akasema, Ile siri aliyoiuliza mfalme, wenye hekima hawawezi kumfunulia mfalme; wala wachawi, wala waganga, wala wanajimu; lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri, naye amemjulisha mfalme Nebukadreza mambo yatakayokuwa siku za mwisho. Ndoto yako, na njozi za kichwa chako ulizoziona kitandani pako, ni hizi; Wewe, Ee mfalme, mawazo yako yaliingia moyoni mwako kitandani pako ya mambo yatakayokuwa halafu; na yeye afunuaye siri amekujulisha mambo yatakayokuwa. Lakini mimi, sikufunuliwa siri hii kwa sababu ya hekima iwayo yote niliyo nayo zaidi ya watu wengine walio hai, bali kusudi mfalme afunuliwe ile tafsiri, nawe upate kujua mawazo ya moyo wako. Wewe, Ee Mfalme, uliona, na tazama, sanamu kubwa sana. Sanamu hii, iliyokuwa kubwa sana, na mwangaza wake mwingi sana, ilisimama mbele yako; na umbo lake lilikuwa lenye kutisha. Na sanamu hii kichwa chake kilikuwa ni cha dhahabu safi; kifua chake na mikono yake ni ya fedha; tumbo lake na viuno vyake ni vya shaba; miguu yake ni ya chuma; na nyayo za miguu yake nusu ya chuma na nusu ya udongo.  Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande. Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu, vilivunjwa vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa hari; upepo ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote. Hii ndiyo ile ndoto, nasi tutaihubiri tafsiri yake mbele ya mfalme. Wewe, Ee mfalme, u mfalme wa wafalme, na Mungu wa mbinguni amekupa ufalme, na uwezo, na nguvu, na utukufu; na kila mahali wakaapo wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani amewatia mkononi mwako, naye amekumilikisha juu ya hao wote; wewe u kichwa kile cha dhahabu.  Na baada ya zamani zako utainuka ufalme mwingine mdogo kuliko wewe; na ufalme mwingine wa tatu wa shaba, utakaoitawala dunia yote. Na ufalme wa nne utakuwa na nguvu mfano wa chuma; kwa maana chuma huvunja vitu vyote na kuvishinda; na kama chuma kisetavyo vitu hivi vyote, ndivyo utakavyovunja-vunja na kuseta. Na kama vile ulivyoziona hizo nyayo za miguu na vidole vyake, kuwa nusu udongo wa mfinyanzi, na nusu chuma, ufalme ule utakuwa ufalme uliogawanyika; lakini ndani yake zitakuwako nguvu za chuma, kama vile ulivyoona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope. Na kama vidole vya zile nyayo vilikuwa nusu chuma na nusu udongo, kadhalika ufalme ule utakuwa nusu yake una nguvu, na nusu yake umevunjika. Na kama vile ulivyokiona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope, watajichanganya nafsi zao kwa mbegu za wanadamu; lakini hawatashikamana, kama vile chuma kisivyoshikamana na udongo. Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele. Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono, na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile shaba na ule udongo, na ile fedha, na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti. Ndipo Nebukadreza, mfalme, akaanguka kifudifudi, akamsujudia Danieli, akatoa amri wamtolee Danieli sadaka na uvumba. Mfalme akajibu, akamwambia Danieli, Hakika Mungu wenu ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa wafalme, awezaye kufumbua siri, kwa kuwa wewe uliweza kuifumbua siri hii. Basi mfalme akamtukuza Danieli, akampa zawadi kubwa nyingi sana, akamfanya kuwa mkubwa juu ya uliwali wote wa Babeli, na kuwa liwali mkuu juu ya wote wenye hekima wa Babeli. Tena, Danieli akamwomba mfalme, naye akawaweka Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wawe juu ya mambo yote ya uliwali wa Babeli; lakini huyo Danieli alikuwa akiketi katika lango la mfalme.”

Ukiangalia kwa undani kuhusu tafasiri ya Daniel kutokana na ndoto aliyoiiota Nebukadreza ambayo ilikuwa ikionyesha dalili za kuja kwa ufalme wa Mungu tangu wakati wa utawala wa nebukadreza unabii huu unatuonyesha mifumo ya serikali za dunia kabla haijaja ile serikali ua utawala wa Masihi, Mungu ametaka kutujua sisi kuhusu wakati ujao, kwa kuchambua sasa tawala hizi ndoto hii ilikuwa na ujumbe ufuatao



1.       Kichwa cha Dhahabu – kiliwakilisha utawala wa Babeli uliokuwa chini ya Nebukadneza
Nebuchadnezzar alitawala kati ya mwaka wa 605-562 hivi kabla ya Kristo alikuwa ni mtawala mkubwa sana wa ufalme katika ufalme wa kabila za Wakaldayo, aliyeshinda falme kuu za Asia na asia ya kusini mashariki na utawala wa Dunia ya wakati huo, alijulikana kwa uhodari mkubwa wa ujenzi kwani alijenga miji mikubwa sana ukiwemo mji wa Babeli ambao ulikuwa wa kifahari sana, alikuwa ni mtawala mwenye nguvu aliyeruhusiwa na Mungu kuharibu Yerusalem na kuchukua mateka Wayahudi na hata kuwapeleka utumwani na kuwafanya watumwa wake, Utawala wake ulikuwa unawakilisha mfumo wa kidikteta kuitawala dunia ya wakati huo, Yaani wafalme au mfalme alikuwa na nguvu kuliko kitu chochote, mtu yoyote na sheria yoyote alichokiamuru yeye ndio kilikuwa jambo la mwisho na hakuna wa kumpinga Dunia ya wakati wake iliongozwa na Mfumo wa utawala wa Kidikteta

Utawala wa kidikteta ni mfumo wa utawala ambao mtawala anatumia nguvu ya dola kutawala, mamlaka nguvu na utawala anakuwa navyo yeye na huwezi kumpinga, Mtawala anajifikiri kuwa ana mamlaka yote juu ya kila kitu hata maisha ya watu, kumpinga kwako kungeweza kuhatarisha maisha, watu walipaswa kumuogopa na kumtii mtawala katika mazingira yoyote yale, utawala huu uliwakilisha aina za serikali za zamani za kifalme na watemi, utawala wakeulidumu kwa miaka kama 70 hivi na baadaye mifumo ya serikali za aina hii ilikuwepo duniani na kuondoka kidogokidogo.

2.       Kifua cha Fedha –  kiliwakilisha utawala wa uamedi na uajemi utawala wa sheria

Baada ya anguko la utawala wa kidikteta uliowakilisha na Nebukadneza mfumo wa utawala na serikali uliofuata uliigawanya babeli vipande viwili na kukaweko utawala wa waamedi na waajemi ambazo ni sawa na Iran na Iraq ya leo, utawala huu ulidumu kwa miaka 206 (536KK-330 KK) Utawala huu unawakilisha na madini ya Fedha maana yake hakukuwa bora sana ukilinganishwa na Madini ya dhahabu, utawala huu ulikuwa wa kisheria na hakuna aliyekuwa juu ya sheria utawala huu, Sheria iliheshimika zaidi na hata wafalme walitakiwa kuzitii, sheria iliheshimika sana ikiwekwa imewekwa na kila mtu alipaswa kuitii ni mara chache sana mfalme aliweza kutangua lakini hata hivyo wakati huu Hakuna mtu aliyekuwa juu ya sheria, hii inawakilisha mfumo wa serikali zilizofuata duniani baada ya ule wa kidikteta.

3.       Tumbo la Shaba – linawakilisha utawala ugiriki au uyunani chini ya Aleksandria

Utawala wa kiyunani au kigiriki unawakilishwa na madini ya shaba na ni sehemu ya tumbo, ulikuwa ni utawala wa kijeshi chini ya mfalme Alexander mkuu, utawala hu wa kiyunani ulidumu kwa miaka 300 (330KK-30KK), kinabii tawala za kijeshi zilifanana kiasi na tawala za kidikteta, shaba inafanana na dhahabu kwa kiwango fulani lakini si bora wala ya thamani kama Dhahabu na fredha huu ni mfumo wa nyakati za serikali za kijeshi zilizotawala sehemu mbalimbali duniani, Nguvu yako yamkijeshi ndiyo ingekuwezesha kuitawala Dunia.

4.       Miguu ya Chuma –Inawakilisha utawala wa warumi chini ya mataifa ya ulaya. Utawala wa kikoloni.

Aina hii ya utawala ilianzia huko ulaya ambapo wao hawakuwa wanachukua watu na kuwapeleka utumwani lakini badala yake waliwatawala watu hukohuko katika inchi zao. Kulikuwa na mabadiliko mengi sana nyakati za utawala huu, Utawala wa kikoloni ni utawala ambapo taifa kubwa na lenye nguvu Super power Nations, linaondoka na kwenda kuwatawala wengine kiuchumi, kijamii, kisiasa na hata kitamaduni. 

Utawala wa chuma unawakilisha utawala wa Kirumi ambao ulikuwa na unaowakilishwa na miguu ya chuma katika sanamu kabla haujagawanyika miguu miwili inawakilisha kugawanyika katika maeneo makuu mawili, mguu mmoja unawakilisha ubepari Magharibi chini ya ushawishi wa papa na kanisa lake  na mguu mwingine unawakilisha Ujamaa mashariki, chini ya utawala au ushawishi wa kiyunani  Kanisa la Othodox, Ukoloni ilikuwa ni sehemu ya utawala wa mataifa yote yanayowakilishwa na mguu wa kulia na wa kushoto, yaani magharibi na mashariki mpaka wakati wa mataifa yote kuwa huru na kujitegemea,

Kuchanua kwa mtini na miti mingine kunawakilishwa kinabii na swala zima la kupata uhuru kwa mataifa yaliyokuwa chini ya ukoloni Kama alivyoeleza Yesu katika unabii wake Luka 21:29-33Akawaambia mfano; Utazameni mtini na miti mingine yote. Wakati iishapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu.Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu. Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatimie..
Tawala kubwa ni tawala ambazo zilipanua utawala wake mpaka katika mataifa mengine, tawala hizi kubwa zilidumu kwa karne nyingi na zilikuwa na hatua za maendeleo zilizowafuatiwa nazo, Ukoloni  na ubepari uliletwa na tawala hizi kubwa, Twala kuu zilidumu mpaka mwaka wa 30 KK – 1453 BK, Mtawala mkuu wa kwanza aliku kaisari Augusto. Yesu Kristo alizaliwa wakati wa mtawala huyu, watawala wengi waliofanikiwa walitawala wakati wa utawala wa rumi na waliwatesa sana wakristo, Mshauri wa Mtawala aliyeitwa Pliny na barua yake aliyoiandika kumshawishi Mtawala Trajan katika mwaka 112 jinsi ya kuwashughulikia wakristo ilikuwa na mchango mkubwa sana katika swala hili, ilipofika mwaka 117 wakati utawala wa Rumi ukiwa bado uko chini ya Trajan Ukristo ulikuwa na kuwa dini kubwa sana ulimwenguni yenye ushawishi mkubwa katika uatwala wa Rumi, Mtawala wa rumi alianzisha ibada za miungu ya Rumi na sanamu zake

Utawala huu uliweka sheria zenye lengo la kukandamiza na kutiisha, ili kuendeleza ulimwengu na jamii za ulimwengu na pia walianzisha maswala ya kuhamisha watu na maswala ya kutokuwatendea watu haki kama sehemu ya swala hilo, Baadaye swala hili linasemekana ndilo lililochochea kuweko kwa ukoloni na utumwa, Wanadamu waliaza kufanywa watumwa na kuwa kama bidhaa, wanadamu wengine wakiwanunua na wengine wakiwamiliki bila wao kuwa na uchaguzi wa nini cha kufanya na kuwatumikia mabwana zao, Mswada wa kukomesha  biashara ya utumwa ulipitishwa mwaka 1807 na Bunge la Waingereza, Lakini huko Zanzibar  Afrika Mashariki ambako ilikuwa bandari na soko kuu la utumwa na  chini ya utawala wa Waarabu wa Oman biashara iliendelea mpaka karne ya 19, na hii inafunua jinsi ambavyo wanadamu ni waovu na wabaya pasipo na Mungu. 

Ubepari ambao ulitawala magharibi unaweza kuelezewa kuwa ni mfumo wa kisiasa wenye misingi ya haki za binadamu za mtu au shirika kuwa na uwezo wa kimiliki mali.

Ukomonisti ambao ulitawala Mashariki ni wazo kutoka ugiriki ya kale, lililoelezewa na Plato kama wazo lenye daraja za ushirikiano na umiliki wa pamoja wa mali, hiki ndicho kilichikuja kuzaa ukomonisti, na usoshalisti, lengo likiwa ni kuwa na serikali ambazo watu wake wanashirikiana mali na ikawa kinyume na ubepari, Katika nyakati hizi baada ya kuchanua kwa Mtini yaani Israel na mataifa mengine yaani kupata uhuru athari za tawala hizi zilisalia katika mataifa mbalimbali hata leo na umeishababisha dunia kutokuwa na mshikamano hata sasa
5.       Chuma na Udongo.Inawakilisha mfumo wa serikali za Kidemokrasia ukoloni mambo leo na sharia Mchanganyiko wa mambo.

Inawakilisha tawala za kidemokrasia zinazoendelea lakini dhaifu, kwa mujibu wa unabii hii ni aina ya mwisho wa tawala za kibinadamu duniani na ni wa muda mfupi, utakuwa na uhuru mkubwa wa kupita kawaida kwa dhambi na uovu ambao utaenea dunaini, Uislamu udongo ukiwa na mgogoro mkubwa na mifumo ya serikali hizo kwa kuwa watafanya kazi ya kutafuta kuwa na mfumo waserikali zinazotaka kuwa na nguvu dhidi ya Kanisa. Uislamu umekuwa ukiendeleza chuki za wazi dhidi ya wayahudi na kanisa  na kuandaa njia ya ujio wa Mpinga Kristo, Chuma kinawakilisha tawala ambazo zina ushawishi wa Kikristo na udongo unawakilisha tawala zenye ushawishi wa kiislamu chini ya utawala wa Sharia, mtu anaweza asikubaliane na tafasiri hii lakini angalia kile kinachoendelea sasa duniani katika jamii yatu ya sasa utaelewa. Kuwa unabii  wa maandiko unatimizwa. Tawala za Chuma na Udongo haziwezi kushikamana na udongo ni dhaifu, inawakilisha tawala za Demokrasia na Sharia, kutokana na mkazo wa kukua kwa demokrasia na uhuru wa watu kuwa na sauti duniani na uhuru wa kuabudu, kutatokea kutokuelewana kukubwa sana katika jamii na mchanganyiko usioshikamana , huu utakuwa ni wakati wa kilele cha uovu wa aina binadamu na serikali chafu sana kutokana na kivuli cha Demokrasia kama tukakavyojadili kwa undani zaidi.

6.       Jiwe lisilochongwa kwa mikono ya kibinadamu linawakilisha Ufalme wa Mungu chini ya Yesu Kristo 

THEOCRACIA  huu ni utawala wa Mungu, Utawala ambao  Yesu Kristo baada ya kurudi kwake mara ya pili Duniani ataitawala dunia nzima, utakuwa utawala wa amani juu ya mataifa kwa miaka 1000, Hili jiwe ni Yesu Kristo atakapokuja mara ya pili duniani, ambaye atakomesha vita vya harmagedon,  na migogoro yote mikubwa duniani na  kufikisha mwisho aina zote za serikali za kibinadamu ambazo zinamalizikia na tawala za kidemokrasia, Atasitawisha amani na ufalme wake kwa kuyashinda mataifa yatakayokusanyika kwaajili ya vita vya Harmagedoni, Wayahudi na waisrael wote wakati huu watamkubali Yesu Kristo yeye waliyemchoma kuwa Ndiye Masihi Mfalme wa wafalme. Utakuwa ni ufalme wa utulivu na amani SHALOM au Irene itatawala Duniani. Huu ndio ufalme ambao Israel wanautazamaia makao makuu ya utawala huu yatakuwa Israel na mji mkuu utakuwa Yerusalem.

Neno la Mungu na utawala wa Kidemokrasi.

Historia inaonyesha kuwa kila aina ya utawala na mifumo ya kiserikali ilikuwa na faida zake na hasara zake, Mungu aliwaacha wanadamu wajitawale, baada ya kuwa wanadamu waliukataa utawala wake na kutaka kuwa huru kufanya kila wanaliloiona kuwa jema machoni pao, Mara kadhaa Mungu aliadhubu na kukemea wanadamu lakini walikuwa ni wenye shingo Ngumu Mwanzo 6:3 “BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.

Mungu aliona kuwa wanadamu wamekuwa na desturi ya kukataa ufalme wake na utawala wake na kwa sababu hiyo amewacha wafuate kila wanachikitaka, katika nyakati hizi za tawala za Kidemokrasia maovu yataongezeka mno kwa sababu madai makuu ya wanadamu yatakuwa kwenye uhuru wa kujifanyia kila wanaloliona jema machoni pao, wanadamu watakuwa wamechoka kuingiliwa  na kila mtu ataona anahitaji kuliamulia anachoweza kujiamulia na kwa sababu ya kukataa kuwa na Mungu, Mungu atawaacha wanadamu wafuate njia zao za uharibifu na kujiletea hukumu  

Warumi 1:18-25Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu. Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia.Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru; kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika; wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo. Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina

Huu ndio wakati ambapo watu watalikataa neno la Mungu na kufuata na kujitafutia waalimu kutokana na kuwawatafiti watafuata khadhithi na kulikataa neno la Mungu, katika nyakati hizi ndio watu wa Mungu tunatiwa moyo kwa maandiko kukemea kukaripia kuonya na kufundisha kwa bidii 

2Timotheo 4:1-5 “Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake; lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo. Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako.”

 Mfumo wa utawala wa Kidemokrasia umeharibu sana jamii, muhubiri wa Kimarekani mwenye asili ya Afrika “Creflo Dollar” aliwahi kuitwa polisi kutoa maelezo ya kumchapa kibao binti yake, kumekuwapo na sheria za kijinga kiasi ambacho huwezi kumuonya mtu, kumpiga mtoto ni kosa kubwa, wanawake wnahisi kuwa walikandamizwa kwa miaka mingi na sasa wanataka kuwa na sauti na maamuzi yao, kuwatii waume zao sawa na maandiko limeonekana kuwa swala la utumwa,  kudaiwa kwa haki na usawa wa kijinsia, ndoa za jinsia moja  ambazo zinatiwa moyo na mataifa yote ya kidemokrasia ambayo yanafikiri kuwa yameendelea sana, uhuru wa kuabudu uliokithiri kiasi ambacho watu wanaweza kufanya lolote kwa jina la Mungu, vikundi vya kigaidi vya watu wenye kuua wenzao kwa misingi ya chuki na visingizio vya dini zenye siasa kali, machafuko ya kila aina uhuru wa kutoa au kupokea habari, uhalifu wa kimtandao, wizi, udanganyifu na utapeli ufisadi na kadhalika ni matukio ambayo yametawala katika nyakati hizi za utawala wa chuma na udongo kabla haujaja utawala wenye nguvu wa Yesu Kristo, hizi ni dalili za ujio wa mpinga Kristo na kunyakuliwa kwa kanisa ambako wengi wataacha kutokana na kuvutiwa na uovu na anasa na tamaa za dunia hii
Yesu anaonya kwamba katika wakati huu watu wajihadhari 

Luka 21:34-36. “Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo; kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima. Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.” 

Yesu ataikuta dunia iko katika hali mbaya sana kutokana na kuwepo kwa serikali ovu na legevu, ni lazima kanisa liwe macho na kutokukubali kuifuatisha namna ya ulimwengu huu 
  
Hatari ya uhuru uliokithiri chini ya mfumo wa kidemokrasia.

Uhuru wa kupita kawaida sio mpango wa Mungu kabisa tangu pale alipomuumba mwanadamu, Mungu alipomuumba mwanadamu aliweka mipaka ili kutokuruhusu uhuru uliokithiri, uhuru ambao ungemuongoza mwanadamu katika kumtenda Mungu dhambi, uhuru  bila mipaka sio mpango wa Mungu, kizazi tulicho nacho kwa bahati mbaya kinataka uhuru huo chini ya kifurushi cha maendeleo na demokrasi.

Kwa Adamu na Hawa Mungu hakuwapa uhuru bila mipaka Mwanzo 2:16-17 inasema “BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.” 

Kwa wana wa Israel Mungu hakuruhusu wawe na uhuru wa kujifanyia kila wanachokitaka kwani wangefanya dhambi aliwapa amri kumi na sheria nyingine ndogondogo ili waweze kuzizingatia, Kutoka 20-40, amri hizi zilipelekea wana wa Israel waweze kudumisha uhusiano wao na MUngu na watu wengine wanaowazunguka  

Kutoka 20:1-17Mungu akanena maneno haya yote akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu. Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure. Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa. Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako. Usiue.  Usizini. Usiibe. Usimshuhudie jirani yako uongo. Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.”

Kwa kanisa zaidi ya kuangalia amri kumi  Yesu Kristo katika hutuba yake ya mlimani aliweza kutoa muongozo wa kiroho ili kila mmoja aweze kuzingatia na ili aweze kuwasehemu ya  ufalme wa Mungu, katika injili ya Mathayo 5-7, Yesu alitoa na kuorodhesha sifa za kiroho ambazo mtu anapaswa kuwa nazo ili aweze kuwa na uhusiano na Mungu na kuurithi uzima wa milele. Aidha sheria maarufu ya Yesu Kristo iitwayo sheria ya dhahabu ni smingi muhimu katika kuishi kwa utaratibu Mathayo 7:12Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.”

Jambo la muhimu ninalotaka kulizungumzia hapa ni kwamba mfumo wa serikali za kidemokrasia unaoonekana kuwa ni mzuri zaidi na kupendwa ndio mfumo mbaya  na muovu na unaoharibu hali ya kiroho na kudhoofisha  uadilifu wa watu na Kanisa na ndio mfumo wenye kuvumilia dhambi kwa kiwango kikubwa na cha uhuru uliopitiliza, msisitizo wa kisheria unaendelea kuwa dhaifu kila siku, watu wanataka uhuru zaidi na wako tayari hata kuasi, viongozi wakubwa wa mataifa ya dunia wamekuwa wakichukuliana na kila kinachoonekana kuwa ni sawa na kwa ujumla wamelemazwa na mfumo huu. Mfumo huu wa kisiasa una nguvu ya shetani na wanadamu na hivyo kila kiongozi duniani atakayeonekana ana viashiria vya kidikteta anapigwa anadhoofishwa na Demokrasia inatawala kisha uovu mkuu unafuata hii ni sihara kuwa muda wa ile sanamu ya Nebukadreza umekamilika na sasa tunasubiri utawala wa Jiwe lisilochongwa kwa mikono Utawala wa Yesu Kristo duniani.

Asomaye na afahamu

Na mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima

Rev. Innocent Kamote.

Jumapili, 15 Aprili 2018

Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha!

Yohana 2:19  Yesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha." 

John 2:19. “Destroy this temple . and I will raise it again in three days”

 
 Utangulizi.

Ni muhimu kufahamu kuwa moja ya matamko ya Yesu Kristo yaliyowahi kulete utata, mojawapo ni tamko hili “Livunjeni Hekalu hili nami katika siku tatu nitalisimamisha”, Tamko hili liliweza kutumiwa na maadui wa Yesu Kristo kama moja ya ushahidi mkubwa wa kumshitaki Yesu wakati wa kuhukumiwa kwake Marko 14:58Sisi tulimsikia akisema, Mimi nitalivunja hekalu hili lililofanyika kwa mikono, na katika siku tatu nitajenga jingine lisilofanyika kwa mikono.” Na Mathayo 26:59-61Basi wakuu wa makuhani na baraza yote wakatafuta ushuhuda wa uongo juu ya Yesu, wapate kumwua; wasiuone wangawa walitokea mashahidi wa uongo wengi. Hata baadaye wawili wakatokea, wakasema, Huyu alisema, Naweza kulivunja hekalu la Mungu, na kulijenga kwa siku tatu.” Unaweza kuona jinsi ambavyo matamshi haya yalivyoweza kutafasiriwa kwa utata na wale waliotafuta kumhukumu Yesu Kristo, usemi huu unaweza kubaki kuwa tata hata kwa jamii yetu leo kama hatutaweza kumsikiliza Mwalimu mkuu Roho Mtakatifu ili kwamba atusaidie kuyaelewa maandiko haya na kupata maana muhimu zilizokusudiwa, Ni kwa makusudi hayo basi leo tunachukua muda kujifunza kuhusu usemi huu wa Yesu “LIVUNJENI HEKALU HILI, NAMI KATIKA SIKU TATU NITALISIMAMISHA” usemi huu wenye nguvu Baba na autumie kumjenga kila mmoja wetu katika jina la Yesu Kristo amen. Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele  viwili vifuatavyo:-

·         Maana ya Hekalu.
·         Livunjeni Hekalu hili nami katika siku tatu nitalisimamisha!

Maana ya Hekalu.

Ni muhimu kufahamu kuwa Jina Hekalu limetokana na jina la kiingereza cha zamani “HEKAHAL” ambalo maana yake ni “main building” au “Hall”, ambalo pia lilitafasiriwea kama neno “Temple” kwa kiingereza cha zamani, Katika lugha ya kiebrania neno Hekalu linatumika kama “BEIT YHWH” yaani nyumba ya Mungu au “BEIT HA ELOHIM” yaani nyumba ya Mungu, na neno nyumba yangu ni “BEIT” au BEITEKHA

Kwa kawaida  kwa mara ya kwanza neno hekalu lilitumika kumaanisha nyumba ya Mungu ambayo ilikuwa ni hema ya kukutania iliyokuwako Shilo  1Samuel 1:9Ndipo Hana akainuka, walipokwisha kula na kunywa huko Shilo. Naye Eli, kuhani, alikuwa akiketi kitini pake penye mwimo wa HEKALU la Bwana.”

Katika agano Jipya neno hekalu limekuwa na maana pana  zaidi na zenye tafasiri kadhaa kadhaa:-

1.       Hekalu linamaanisha mwili wa Yesu Kristo Yohana 2:19, 2:21
2.       Hekalu pia humaanisha mtu aliyemwamini Yesu Kristo 1Wakoritho 3:16-17
3.       Hekalu pia humaanisha Kanisa yaani watu waliomwamini Yesu Kristo Waefeso 2:21
4.       Lakini mbinguni pia kunaitwa hekalu Ufunuo 7:5
5.       Lakini yako pia majengo ya miungu mingine ambayo pia huitwa hekalu hapa duniani mfano ni lile hekalu na mungu mke Diana au Artremi Matendo 19:27.

Ni muhimu kufahamu hata hivyo kibiblia na kwa mujibu wa Imani ya kiyahudi na Kikristo kwa ujumla neno hekalu lilitumika zaidi kumaanisha nyumba ya Mungu iliyokuwako katika mlima Sayuni kwaajili ya kumuabudu Mungu, hili lilitwa Hekalu 1Falme 6:17, Nyumba ya Mungu 2Wafalme 11:10, Hekalu takatifu Zaburi 79:1, Nyumba ya Bwana 2Nyakati 23:5, 12, Nyumba ya Mungu wa Yakobo Isaya 2:3 Nyumba ya utukufu  Isaya 60:7, Nyumba ya sala Isaya 56:7, Mathayo 21:13 Nyumba ya sadaka 2Nyakati 7:12 Patakatifu 2Nyakati 36:17 Mlima wa nyumba ya Mungu Isaya 2:2 Patakatifu nyumba ya uzuri Isaya 64:11 Mlima mtakatifu Isaya 27:13 Mahali kwa Bwana 1Nyakati 29:1 Hema la ushuhuda 2Nyakati 24:6 Sayuni Zaburi 74:2, 84:7 na Yesu aliita Nyumba ya baba yangu Yohana 2:16.

Livunjeni Hekalu hili nami katika siku tatu nitalisimamisha!

Yohana 2:19-21.Yesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha. Basi Wayahudi wakasema, Hekalu hili lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu? Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake.”

Kimsingi wakati Yesu alipokuwa akiyatamka maneno haya Wayahudi walifikiri kuwa Yesu alikuwa akizungumza juu ya Hekalu ambalo lilikuwa limekarabatiwa na Herode mnamo karne ya 19 Kabla ya Yesu, Hekalu hilo la kifahari ambalo wayahudi walikuwa wanajivunia lilikuwa limechukua muda wa miaka 46 hivi,  Yesu hakujisumbua kutoa ufafanuzi wa maana ya meneo haya, Wanafunzi wake tu ndio walioelewa kuwa Yesu alikuwa akizungumza juu ya mwili wake na juu ya uhai wake kwamba yeye ana uwezo wa kuutoa uhai wake na kuutwaa tena Yohana 10:17-18Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena. Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu. Wayahudi walikuwa hawako tayari kumpokea Yesu na walikuwa tayari wamekwisha kupanga mpango wa kumwangamiza Yesu, Kwa hiyo Yesu alikuwa akizungumza habari ya mpango wao na kifo chake, hivyo usemi huu waoa hawakuuelewa lakini wanafunzi waliuelewa baadaye kuwa Yesu alikuwa anazungumza habari ya kusulubiwa kwake kufa na kufufuka, kwa hiyo Yesu alipofufuka siku ya tatu wanafunzi walishangaa neno la Mungu na unabii wa Yesu Kristo mwenyewe , hivyo walitambua kuwa kufa kwa Yesu Kristo halikuwa tukio la bahati mbaya bali ulikuwa ni mpango wa Mungu kwaajili ya uzima wa milele.

Usemi huu ulikuwa usemi wenye kuonyesha nguvu kubwa na uweza wa Yesu Kristo, kwamba yeye ni mweny nguvu na anazo funguo za mauti na za kuzimu yaani ana mamlaka yote hata leo Yesu bado analiangalia kanisa lake na hekalu lake ambao ni sisi wanadamu, kutokana na kazi za shetani katika maisha ya mwanadamu na kazi zake ulimwenguni pamoja na anguko la Mwanadamu,  kumekuweko na hali za kutokumcha Mungu, kuipenda dunia tamaa na kila aina ya dhambi  na vimekuwa ni matokeo makubwa ya kumomonyoka kwa uadilifu wa mwanadamu katika maisha yake  na kumekuwa ni mwanzo wa kaburi, Mwanadamu kwa asili ndani yake ameumbwa na Mungu kuwa Hekalu, Mioyo yetu iliumbwa na Mungu kwa kusudi la kuifanya kuwa nyumba ya ibada ya kwa Roho Mtakatifu, mioyo yetu imekusudiwa kuwa nyumba ya Mungu aliye hai, lakini kutokana na ubinafsi, dhambi na tamaa za dunia watu   na ibilisi wameharibu maisha yao matakatifu na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, wameharibu nyumba ya Mungu kwa nyundo na mawe na mashoka wameweka chukizo la uharibifu mahali patakatifu, wamelinajisi hekalu, wameharibu dhamira zao na hazina hisia ya hofu ya Mungu kabisa, kila wanachokiwaza wanadamu, walichojaza mioyoni mwao, katika maamuzi yao na mapenzi yao uwepo wa Mungu umepewa nafasi ndogo sana au umenyimwa kabisa kuweko katika nafasi ya Moyo wa Binadamu

Ulimwengu umekuwa wa tofauti sana wanadamu wameharibika badala ya kuchagua mema wamechagua mabaya, maovu yanaonekana kuwa ni sifa na wema unaonekana kuwa ni ujinga Yesu alilijua hilo mapema inasikitisha kuwa watu walimchagua Baraba aliyekuwa muhaini na kumsulubisha Yesu aliyekuwa akiponya Magonjwa yao na kutoa muda wake akiwafundisha njia za Mungu kwa usahihi zaidi, Yesu alijua kuwa ni kwa kupitia kulinda heshima zao na tamaa zao na ubinafsi wao viongozi wa dini wana makusudi ya kumuua na hivyo kuleta uharibifu wa Mwili wake kama Hekalu la Roho Mtakatifu na shetani ameaharibu mioyo ya wanadamu ili kuleta uharibifu ndani yao ziko roho za uharibifu zimetumwa kukuharibia kila walichikifanya wanadamu katika dhamiri zao na mioyo yao ni uharibifu wa hekalu la Mungu.

Yesu akijua uweza na mamlaka alio nao alizungumza juu yamauti yake lakini pia anazungumza juu ya mauti yako na kwa ujasiri najua kuwa anao uwezo wa kurejesha tena, kile ambacho shetani ameharibu katika maisha yako yeye ana uwezo wa kukarabati ndani na Muda mfupi kama utampa maisha, yeye atafukuza wafanya biashara miungu na mapepo yanayoharibu maisha yako na atayahuisha tena kwa nguvu alizonazo, siku tatu inamaanisha kwa kazi yake aliyoifanya , kwa kusulubiwa na kufa na kufufuka inamaanisha ukweli kuwa alikufa kwa dhambi zetu na amefufukwa kwaajili ya haki Yesu ni wazi kuwa kwa kazi aliyoifanya msalabani inauwezo wa kumjenga na kumrejesha upya mwanadamu wa aina yoyotena kabila lolote na aliyeharibika kwa kiwangochopchote na mtu huyo akawa makazi ya roho mtakatifu wa Mungu, haijalishi sasa una miaka mingapi, haijalishi tatizo lako lina miaka mingapi Mungu anataka uamini kazi iliyofanyika msalabani kwamba ina nguvu za kipekee za kufanya kitu kipya katika maisha yako, Ndio maana Yesu Hakushughulika kuhesabu miaka ya hekalu kujengwa Yeye amesema livunje na ndani ya siku tatu atalisimamisha, Hekalu lililokuwa limejengwa kwa miaka 46 hata hivyo lilikuwa bado halijakamilika, Lakini kazi aliyoifanya yesu ni kamilifu kama ulimkubali yeye atalijenga hekalu tena atakamilisha mapungufu yako na atalijenga Hekalu lako bila nyundo kusikika 
 
1Wafalme 6:7 “Na nyumba ilipokuwa ikijengwa, ikajengwa kwa mawe yaliokwisha kuchongwa chimboni; wala nyundo, wala shoka, wala chombo cha chuma cho chote, sauti yake haikusikiwa ilipokuwa ikijengwa nyumba.”

Ni Yesu Kristo pekee ndiye mwenye uwezo wa kulijenga Hekalu lake bila kelele, wakati mwingine tumepiga nyundo, tumetumia shoka na vyombo vya chuma katika kuwajenga wanadamu Lakini Yesu anaweza kumjenga awaye yote bila Kelele, Leo atakujenga wewe pia bila kelele za wanadamu.

Na mkuu wa wajenzi mwenye Hekima 

Rev. Innocent Kamote.

Jumamosi, 31 Machi 2018

Je Mtu akifa atakuwa hai tena?


Ayubu 14:13-14Laiti ungenificha kuzimuni, Ukanilinda kwa siri, hata ghadhabu zako zitakapopita, Na kuniandikia muda ulioamriwa, na kunikumbuka! Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena? Mimi ningengoja siku zote za vita vyangu, Hata kufunguliwa kwangu kunifikilie.”

 Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele
 
Leo hii wakristo wote nchini wanaungana na wakristo wengine duniani kote pamoja na wayahudi kuadhimisha sikukuu ya Pasaka, kukumbuka tukio la kusulubiwa, kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo kulikotokea miaka zaidi ya 2000 iliyopita, huku Wayahudi wakiadhimisha miaka zaidi ya 3000 Tangu walipoadhimisha Pasaka ya kwanza katika siku ya 15 ya mwezi wa Nisan kwa mujibu wa Kalenda ya kiyahudi  Hapo walipookolewa kutoka Misri.

Miaka mingi sana kabla ya kufufuka kwa Yesu, mtumishi wa Mungu Ayubu aliwahi kuuliza swali la msingi sana katika maisha ya mwanadamu, swali hili ni moja ya miongoni mwa maswali ya kifalsafa, swali hili liliulizwa kutokana na hoja zilizotolewa na watu wenye hekima mbali mbali waliokuja kumtia moyo ayubu na kujiuliza swali kwanini wanadamu wanateseka, swali kuhusu mateso hata leo limekuwa ni swali kubwa sana lenye mjadala mkubwa sana katika imani mbalimbali

·         Wahindu wanaamini mateso yanatokana na KARMA yaani kuishi kwa kutenda Mema wanaamini kama ukiishi vibaya utazaliwa kitu kibaya na utapata shida, na hivyo katika mzunguko wa maisha Mungu atakupa mabaya na utachelewa kufika NIRVANA yaani mbinguni kukaa na Mungu

·         Wabudha wanaamini kuwa mateso yanatokana na tamaa, yaani kama mwanadamu ataishi mbali na tamaa atakuwa ameingia NIRVANA hata kama bado yuko Duniani, hivyo wao hujifunza kuridhika na kujikana na kuitesa miili yao 

·         Waislam wanaamini kuwa mateso ni matokeo ya Kudra za mwenyezi Mungu, yaani ni mapenzi ya Mungu kwa kadiri ya majaliwa yake 

·         Wayahudi waliamini kuwa mtu anaweza kupata mateso kama matokeo ya dhambi zake au za wazazi wake kutokana na Mungu alivyoahidi kushuhulika na kizazi hata ta tatu na nne cha wampendao au wanaomchukiza

·         Wakristo swala kuhusu Mateso ni swala pana sana na linaweza kuwa na ufafanuzi mpana sana wa kwanini wanadamu wanateseka, hata hivyo Kiongozi mkuu wa wokovu wetu yaani Yesu alikamilishwa kwa njia ya mateso

Katika kitabu cha Ayubu ni wazi kuwa Ayubu pamoja na rafiki zake walikuwa wakijadili kuhusu Mateso na sio mateso ya kawaida bali mateso ya mtu aliyeishi kwa haki, Ayubu ambaye inasemekana kuwa aliihi maisha ya hali alikuwa anateseka sana na hakuwa amepata tiba, licha ya mali yake kuwa imetekekea, licha ya kuwa amepoteza watoto wake wote, pia alikuwa na majipu mabaya yaliyokuwa yakifumba na kufumbuka mwili mzima kutoka kichwani hata unyayoni, Ayubu na wenzake walikuwa wamejadili na kutafuta suluhu bila kupata ufumbuzi na hivyo Aybu alikuwa anatazamia kufa aliamini kuwa sasa hakuna tumaini lingine lililosalia zaidi ya kifo  tu, ndipo Ayubu akauliza katika hali yakukata tamaa

Kwamba mbona miti ikikatwa shina lake huchipuka? Na maji ya bahari hupwa na kujaa ni kama inaonekana kuwa viumbe hivyo vina matumaini lakini sivyo ilivyo kwa mwanadamu, inaonekama kama mtu akifa ni mwisho wa kila kitu na hakuna matumaini ya kurejea tena, Ayubu anamwambia Mungu kwa kuwa siku za mwanadamu za kuishi ni chache na zimejaa taabu, ni afadhali angewaacha tu bila kupata mateso maana hawatakuwako tena, Hata hivyo Ayubu alikuwa na imani kuwa iko namna atamuona Mungu tu hata kama mwili wake utaharibiwa alikuwa na imani kuwa macho yake yatamuona tu   

Ayubu 19: 25-27Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi.  Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu; Nami nitamwona mimi nafsi yangu, Na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine. Mtima wangu unazimia ndani yangu.”   

Swali lililoulizwa na Ayubu Mungu aliwahi kumuuliza mtumishi wake Ezekiel katika namna nyingine,  

Ezekiel 37:1-3 “.Mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu, naye akanichukua nje katika roho ya Bwana, akaniweka chini, katikati ya bonde; nalo limejaa mifupa; akanipitisha karibu nayo pande zote; na tazama, palikuwa na mifupa mingi katika ule uwanda! Nayo, tazama, ilikuwa mikavu sana.  Akaniambia, Mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza kuishi? Nami nikajibu, Ee Bwana MUNGU, wajua wewe”. 

Wakati huu taifa la Yuda lilikuwa limechukuliwa utumwani Babel na kila kitu iimeaharibiwa na kufa hakukuwa na matumaini ya uhai tena ndio maana swali hili lilikuwa Gumu kwa Ezekiel yeye alijibu tu kuwa Bwana unajua wewe! Mtu awaye yote anapopitia katika mateso na huzuni na kukata tamaa huwa anafikiri kuhusu kurejeshwa tena katika hali aliyokuwa nayo mwanzoni your Golden Age!

Mtume Yohana ndiye mtume aliyeteseka sana kuliko mitume wote, inasemekana aliwahi kuviringishwa katika yasi na kuwashwa moto lakini alitoka akiwa safi, aliwahi kuchemshwa katika pipala mafuta ya lami lakini alitoka akiwa hai, alishuhudia wenzake na wakrito wengine wakifa na kuawa kwa kuliwa na simba kuchomwa moto na kadhalika yeye kutokana na kushindikana kufa waliamua kumpeleka katika kisiwa cha Patmo ili akateseke huko maisha yalikuwa ni yenye kuhuzunisha na kukatisha tamaa, Yesu alimuona Yohana akiwa amekata tamaa na alimpa ujumbe mkubwa wa kutia moyo  

Yohana 1:17-18 “Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.”

Swali la muhimu la kujiuliza ni kwanini Yesu alijitambulisha kuwa yu hai yaani amefufuka? Ni muhimu kufahamu kuwa ujumbe muhimu kwa mtu ANAYETESEKA, ALIYEKATA TAMAA, na ALIYE KATIKA HALI YA KUFA ni UJUMBE WA UFUFUO Yesu alifahamu kuwa huu ndio ujumbe pekee unaoweza kumpa mtu tumaini Jipya!

Habari njema kwa ndoa iliyokufa sio kuolewa tena ni kurejea tena kwa furaha iliyotoweka na upendo uliotoweka katika ndoa yake.

Tunapoisheherekea pasaka na kukumbuka kufufuka kwa Bwana wetu Yesu ni ujumbe wa matumaini  kwamba Bwana Yesu alikufa na akafufuka na kuwa mauti haimuwezi na kuwa ni yeye ndiye mwenye funguo za mauti na kuzimu, ki msingi Yesu anajibu la swali la Ayubu kuwa mtu akifa atakuwa hai tena Yesu anajibu swali hili kuwa ndio mtu akifa anaweza kuwa hai tena na anatutangazia wazi kuwa yeye anazofunguo za mauti na kuzimu na hivyo anauwezo wa kufufua matumaini yaliyotoweka kwako, anauwezo wa kufufua huduma yako, anauwezo wa kurejesha watoto wako, ana uwezo wa kurejesha kila kilicho haribiwa na kuuawa na ibilisi, ana uwezo wa kurejesha na kufufua taifa linalomtumaini yeye, Pasaka hii mimi sihitaji habari nyingine yoyote nahitaji kusikia habari za matumaini ya kuwa Yesu Kristo yuko hai na ndiye mwenye Mamlaka ya kifo  na uzima na ana uwezo wa kufufua ndoto zetu, maisha yetu,  matumaini yetu, uzima wetu, mimi sihitaji waraka wa maaskaofu nahitaji kumuona mteteaji wangu akisimama kiunitetea dhidi ya kila aina ya unyonge na utumwa Pasaka ina uhusiano na ukombozi nahitaji kumuoja Yesu akinikomboa mimi na familia yangu na watu wangu na taifa langu hii ndio habari njema ya ujasiri kuwa mauti haina nguvu katika maisha yetu, imepoteza mamlaka ni yesu pekee mwenye mamlaka hiyo yeye atafufuka pamoja na mashaka yangu yeye atahuisha nafsi yangu!

Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima