1.Timotheo
4:12 “Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe
kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na
usafi.”
Yakobo
alikuwa makini wakati wa Kuweka Mikono Mkono wa kuume ni Yule unayekusudia
kumfanya kuwa kicha na Mkono wa Kushoto ni Yule unayekusudia awe mdogo Je
wachungaji nwa leo wanaweka vipi Mikono? Wakati wa kubariki Ndoa ua viongozi wa
kanisa, usiweke mikono hovyo hovyo kuna kanuni Yusufu na Yakobo walizijuaMwanzo 48:1-22
Utangulizi:
Maisha ya Yusufu ni moja ya Maisha ya mfano, na ya kuigwakatika Biblia,
Tunaona Biblia ikizungumza kwa upana kuhusu uumbaji kwatika Mwanzo 1-2,
wakati Mwanzo 3 pekee ikizungumzia Anguko la Mwanadamu, Mwanzo 4-5
habari ya kaini na Habili pamoja na kuongezeka kwa maasi, Mwanzo 6-9 Ni
habari za Gharika na Nuhu mtu wa Mungu, Mwanzo 10-11 ni habari za Mnara
wa Babeli na kutawanyika kwa mataifa, Mwanzo 12-24 ni Habari za Ibrahimu
baba wa Imani, Mwanzo 25-36
Kidogo Isaka, Esau lakini zaidi sana Yakobo, Mwanzo37:1-50:26 Ni habari
za Yusufu, Kwa hiyo utaweza kuona Kuwa Neno la Mungu linamzungumzia Yusufu kwa
upana na urafu zaidi, huku Biblia ikiwa haijawahi kuonyesha uzaifu wowote
aliokuwa nao Yusufu, Kuna kitu cha ziada cha kujifunza katika maisha yake.
Yusufu anapewa Madaraka makubwa sana Katika Biblia, Miongoni mwa mababa
wa Isarel Yusufu ni Mmojawao “The Patriarchs” hii ilikuwa nafasi ambayo
labda Ruben angepewa Lakini kutokana na uaminifu wa Yusufu baba yake alimpa
mbaraka huu kwa hiyo wakitajwa Mababa wa taifa la Israel basi Yusufu Ni
mmojawao
a.
Abraham baba wa imani
b.
Isaka Mwana wa Ahadi
c.
Yakobo (Israel) Baba wa taifa la kiyahudi baba wa
Kabila 12 za Israel
d.
Yusufu Mwokozi wa Israel na Misri Baba wa Kabila mbili
za Israel Manaseh na Efraimu
Pamoja na umuhimu wao wote
utaweza kuona habariza Yusufu zinaandikwa kwa kina zaidi kuliko wengine na
hakuna dhambi yoyote inaonyeshwa kuhusu Maisha ya Yusufu, Maisha yake yenye
uadilifu wa hali ya juu, Usafi wa Moyo, na maisha, kutokulipiza Kisasi, kuelewa
vema makusudi na mipango ya Mungu, kuna mfanya kuwa mtu wa kuigwa miongoni mwa
watu wa agano la kale na kufananishwa na Yesu Kristo kwa kile alichokifanya kwa
ulimwengu.
Tutajifunza somo hili Muhimu kuhusu Maisha ya yusufu kwa Kuzingatia
vipengele vine vifuatavyo:-
1.
Maisha ya Yusufu Katika nchi ya kanaani
2.
Maisha ya Yusufu Katika Nchi ya Ugeni kama Mtumwa
3.
Maisha ya Yusufu Katika Nchi ya Ugeni kama Mtawala.
Maisha ya
Yusufu Katika Inchi ya Kanaani.
A.
Alichukiwa na Kaka zake
a.
Alifanya kazi za baba yake
kwa bidii na uaminifu Mwanzo 37:2
b.
Alitoa ripoti ya kazi
zilizofanyanyika kwa baba yake Mwanzo 37:2
“Hivi ndivyo vizazi vya Yakobo. Yusufu, aliyekuwa mwenye
miaka kumi na saba, alikuwa akichunga kondoo pamoja na ndugu zake; naye alikuwa
kijana pamoja na wana wa Bilha, na wana wa Zilpa, wake wa baba yake. Yusufu
akamletea baba yao habari zao mbaya”.
c. Yakobo alikuwa na wana kumi na mbili na binti mmoja, Dina (Mwanzo 29:31;30:24;
35:16-18). Wanawe walikuwa:-
·
Wana wa Lea: Reubeni, Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari na Zabuloni
·
Wana wa mjakazi wa Lea (Zilpa): Gadi na Asheri
·
Wana wa Mjakazi wa Raheli (Bilha): Dani na Naftali
·
Wana wa Raheli: Yusufu na Benyamini
d.
Kutokana na uaminifu wake pia
mzaliwa wa kwanza wa Raheli mke aliyependwa sana na Yakobo, Baba yake alimpenda
sana na kumtengenezea vazi maalumu Mwanzo 37:3-4, Maisha ya Yusufu sio
yalimpendeza babaye tu Bali hata Mungu na hivyo Mungu alisema naye kuhusu
Maisha yake ya baadaye Mwanzo 37:5-11, Mungu alisema naye kwa Njia ya
Ndoto kuhusu kusujudiwa na ndugu zake, yaani kuwa mfalme dhidi yao lakini wao
walimchukia upeo.
e.
Yusufu aliuza Misri baada ya
kunusurika jaribio la kuuawa Mwanzo 37:12-36
f.
Ruben alitaka kumuokoa lakini
Mpango wake ulishindikana Mwanzo 37:21-22
g. Yuda alitaka kumuokoa nduguye
na kifo kwa kutoa wazo auzwe utumwani Mwanzo 37:26-27 na mpango wake
ulifanikiwa
Yusufu
alimtii baba yake na hakutaka kuwapendeza ndugu zake kwa kufunika maovu yao,
Pamoja na Yusufu kufanyiwa mabaya na ndugu zake aliendelea kuwa mwaminifu hata
mbali na mzazi wake huko Utumwani Misri.
Maisha ya
Yusufu Katika Nchi ya Ugeni kama Mtumwa
A.
Mungu alikuwa pamoja naye
a. Alinunuliwa kama mtumwa katika nyumba ya Potifa, Mungu alimpa kibali
Mwanzo 39:1-6, aliweza kuwa mwenye kuleta faida na Baraka na kuaminiwa
b. Yusufu alikuwa Mzuri sana “Handsome” kwa sababu hiyo alivutia watu
akiwemo mke wa Potifa Mwanzo39:b-20
c. Mara kwa mara au mara kadhaa mke wa Potifa alimjaribu Yusufu ili alale
naye
d. Lakini Yusufu alikataa kwa sababu alimuheshimu Potifa lakini alimuheshimu
Mungu pia Mwanzo 39:8-9
Je wewe kama kijana wa leo unaliweza hili? Leo hii
ulimwengu umebadilika wanawake wenye uwezo wa kifedha kama ilivyo kwa potifa
wanafuata vijana wadogo wanawashawishi na kutembea nao wanaviita “VIBENTEN” zamani
Serengeti Boys, sio rahisi kwa vijana kushinda katika hili, maswala ya mapenzi
ni yenye kvutia sana hususani kama mwanamke ndiye anayekutongoza, inawezekana
pia haikuwa rahisi kwa Yusufu na ndio maana alikimbia na kuacha vazi lake huko
Biblia inasema “Ikimbieni Zinaa” 1Wakoritho 6:18 “Ikimbieni
zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye
zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.”
1. Kutokana na singizio hilo Yusufu aliwekwa Gerezani
2. Hasira za Potifa ziliwaka juu ya Yusufu.
B.
Maisha ya Yusufu Gerezani.
a.
Mungu aliendelea kuwa Pamoja
na Yusufu Mwanzo 39:21-23
b.
Alipata kibali mbele ya mkuu
wa Gereza na kuamini wa sana
c.
Alifanikiwa katika kila
alilolifanya
d.
Alijihusisha na maisha ya
ndani kabisa ya wafungwa wenzake aliwaonea huruma na alijua kusoma nyuso zao
ili kujua kuwa wana huzuni, wana furaha na amani au la?, Mungu alimpa karama ya
neno la Maarifa na aliitumia kuweza Kufasiri Ndoto
Wakati wote Alimpa Mungu utukufu na hakuchukua
utukufu wa Mungu, Tumeumbwa ili tumtukuze Mungu, Mungu na awe kipaumbele chetu
cha kwanza katika maisha yetu Mwanzo 40:1-41:36
e.
Yusufu alitafasiri Ndoto za
Muokaji na Mnyweshaji gerezani na ndoto zilikuwa za kweli na zilitimia
f.
Mungu ndiye mwenye kutafasiri
Ndoto alisema Yusufu Mwanzo 40:8
g.
Alitafasiri Ndoto ya
mnyweshaji na kumuomnba amkumbuke Mwanzo 40:20-23
Wanadamu wana uwwezo mkubwa sana wa kuwasahau
wenzao, tenda mema bila kutarajia kitu ni Mungu pekee ambaye hataweza kukusahau
Isaya 49:15 “Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake
anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau,
lakini mimi sitakusahau wewe.” Ni Mungu pekee anayeweza kutufadhili na
kutulipia kwa wema wetu wote tunaoufanya yeye fadhili zake zinadumu milele,
Mungu hawezi muacha mtu mwenye haki Zaburi 37:25 “Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini
sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula.”
C.
Mungu anamkumbuka Yusufu.
a.
Mungu alimpa Ndoto Farao
Mwanzo 41:1-7
b.
Wenye hekima, waganga, na
wachawi wote wanashindwa kuitafasiri
Mwanzo 41:8
c. Mungu anaweka mazingira ya lazima kwa mnyweshaji kumkumbuka Yusufu
Mwanzo 41:9-13,.Wanadamu wasipokuwa waaminifu kwetu Mungu ni Mwaminifu
d.
Yusufu aliitwa kutafasiri
Ndoto, alimpa Mungu utukufu Mwanzo 41: 16, 25, 32 Wakati wote Yusufu
alitambua kuwa Mungu ndiye mwenye kutenda kila jambo
e.
Yusufu alibadilishwa mavazi
yake, huwezi kumkaribia mfalme ukiwa katika hali ya mfungwa Mwanzo 41:14.
f.
Licha ya Kufasiri Ndoto
alikuwa na majibu ya tatizo kwa farao Mwanzo 41:33-36
g.
Maisha yalikuwa magumu na
yenye uchungu, alikataliwa na nduguze, aliuzwa kama mtumwa, alihukumiwa kifungo
kwa uonevu, alisahaulika hata na wale aliowatendea wema, kuna haja gani tena ya
kuendelea kuwa mwaminifu katika mazingira kama haya? Lakini Yusufu aliendelea
kutenda haki, alijua kuwa Mungu hawezi kumsahau, Wagalatia 6:9 “Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa
wakati wake, tusipozimia roho.” Mungu alimpa kibali Farao na hatimaye farao
hakuona mtu mwingine sahihi wa kusaidia jamii yake isipokuwa Yusufu. Ndugu
usipozimia roho utavuna mema yote unayowatendea watu.
Maisha ya
Yusufu Katika Nchi ya Ugeni kama Mtawala.
Mungu si
Athumani akiwa na miaka 30 Yusufu
anakuwa mtawala wa Misri chini ya farao anainuliwa sana Mwanzo 41:38-46
a.
Alitawazwa kuwa kuwa mkuu katika nchi yote ya Misri Mwanzo 41:38-40
b. Aliwekwa juu ya
Ncho yote, akavishwa Pete ya Mamlaka Mwanzo
41:41-45
c. Aliozwa mke
Mzuri sana aliyeitwa Asenath
d. Watu wote
walimpigia Magoti, akiwemo Potifa, Mnyeshwaji, Askari wa Magereza na raia wote
e. Aliongoza kwa
Hekima kubwa sana, alianza kufanya wajibu wake hakulipiza kisasi kwa Mtu
f.
Mungu alimbariki kwa watoto wawili wa Kiume Mwanzo 41:50-52
g.
Yusufu anafanyika Mwokozi sio wa Misri tu na ulimwengu mzima
Mwanzo 41:55-57, Kuwa Baraka kwa wengine
kunaanzia katika maisha ya uaminifu tangu nyumbani, shuleni, kazini, na hata
ugenini Mungu alimbariki kweli kweli.
Kutimia kwa Ndoto ya Yusufu.
Baada ya miaka
ipatayo 13 sasa Yusufu alkiwa na miaka 30 anakuwa ameinuliwa sana na Mungu na
kuwa mtawala mwenye heshima ya kifalme Misri Mwanzo 41:38-46, Hekima aliyopewa na Mungu inaonekana katika Utendaji
wa uongozi wake
a.
Alijua nini cha kufanya wakati wa Miaka ya mavuno Mwanzo 41:47-49
b.
Alijua nini cha kufanya wakati wa Miaka ya njaa Mwanzo 41:53-57, 47:13-26
c.
Aliunganisha maisha yake na Mambo aliyotendewa na Mungu Mwanzo 41:50-52
·
Manase Mungu amenisahaulisha taabu za nyumba ya Baba yangu
·
Efraimu Mungu amenineemesha Katika Nchi ya Ugeni
d.
Ndugu zake wanakuja Misri kwaajili ya kununua Chakula
·
Mwanzo 42:1-13 Yusufu
aliwagundua Ndugu zake walipokuja na Kumuinamia na aliikumbuka Ndoto yake yaani
ile ahadi ya Mungu aliyoahidiwa kwa Ndoto
·
Yusufu alitaka kuwakumbusha Ndugu zake Tatizo lao na kujua
kama wamebadilika Mwanzo 42:14-24
·
Reben alikuwa Tayari kupoteza watoto wake wawili ili waende
na Benjamin ambaye Yusufu alimdai waende naye wakati Simeon aliwekwa kizuizini, Mwanzo 42:36-38
·
Yuda naye anaonyesha kuwajibika kwa Maisha ya Ndugu zake Mwanzo 43:1-14
·
Mungu anataka tuwe mbali kabisa na maisha ya ubinafsi,
ukomavu wa kweli unakuja pale tunapoonyesha kujali wengine na hata kuwa tayari
kuyapoteza maisha yetu kwaajili ya wengine
·
Yuda anaonekana kuwa Tayari kuwajibika pia kwaajili ya
Benjamin na kwaajili ya baba yake Mwanzo
44:18-34
·
Yusufu alishindwa kujizuia Mwanzo 45:1-4
·
Alihesabu kuwa kila kilichotokea ilikuwa ni mpango wa Mungu Mwanzo 45:5-15
·
Anawaahidi kuwatunza
katika Nchi ya Gosheni Mwanzo 46:16-20,28-34;47:1-12
·
Yusufu alionyesha Moyo wa Msamaha Mwanzo 45:4-8, 50:15-21
Mungu huweza kutumia njia Mbaya kuleta
jambo zuri Mwanzo 50:20
Mungu ni mwaminifu katika kutunza ahadi
zake Mwanzo 50:24-25
Hitimisho:
Katika maisha
ya Yusufu kuna mambo ya msingi ya Kujifunza
a.
Alimwamini Mungu na Kumtegemea
b.
Alijitoa kumtumikia Mungu na Mwanadamu kwa Heshima naUaminifu
c.
Hakukubali kumezwa na Chuki,Usaliti,Kusahaulika alionyesha
upendo na hakulipiza kisasi
d.
Alikuwa tayari kuwasamehe wengine
e.
Alikuwa na akili na uwezo wa kujua Mapenzi ya Mungu katika
kila alichokuwa anakipitia
f.
Alikuwa mwaminifu tangu ujana wake, na hata alipokuwa mbali
na Nyumbani
g.
Alitambua kuwa Israel waterejea katika inchi ya ahadi na
kuomba mifupa yake izikwe Israel
h.
Kupitia yeye tunaweza kujifunza namna ya kuwa Kielelezo
katika.
usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.
Limeandaliwa na Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima.