Jumanne, 14 Aprili 2020

Mfano wa tai ayashukiaye Mawindo!



Andiko: Ayubu 9: 25 -26 Biblia inasema “ Basi siku zangu zina mbio kuliko Tarishi; Zakimbia wala hazioni mema, Zimepita kama merikebu ziendazo mbio; Mfano wa tai ayashukiayemawindo.”



Utangulizi:


Leo tutachukua muda kutafakari kwa kina somo kuhusu Mfano wa tai ayashukiaye Mawindo, Ni muhimu kuwa na ufahamu kuwa Mungu aliviumba viumbe vingi duniani kwa makusudi mbali mbali lakini mojawapo ya kusudi kuu ni kutufunza mambo mbalimbali ya msingi, Tai ni moja ya Ndege au kiumbe ambaye biblia imezungumza sifa zake kwa kina na mapana na marefu na tunaweza kujifunza mambo kadhaa ya muhimu kutoka kwa kiumbe hiki.
Kuna usemi wa wahenga kuwa ndege wa aina moja huruka pamoja, Usemi huu kwa Tai ni tofauti tai wanaruka pekeyao na wanafurahia kuruka juu sana, sifa zake zinawekwa katika Biblia kwa vile ni ndege mwenye sifa za kipakee ni ndege asiyeshindwa na ukubwa wa mawindo yake.
Kwa nini Biblia inampa Tai sifa za hali ya juu sana ni muhimu kwetu kujifunza sifa zake na kuzilinganisha na maisha yetu.


  Tai ni wenye uwezo mkubwa wa kuona mbali.

1.    



Ayubu 39:27-29 Biblia inasema hivi “ Je! Tai hupaa juu kwa amri yako, Na kufanya kioto chake mahali pa juu?  Hukaa jabalini, ndiko kwenye malazi yake, Juu ya genge la jabali, na ngomeni. Toka huko yeye huchungulia mawindo; Macho yake huyaangalia toka mbali.”
Tai kama utamfanyia uchunguzi na kumchungulia kwa mbali ni ndege makini sana Biblia inamsifia kuwa “macho yake huyaangalia mawindo toka mbali” ndi ndege hodari katika kuwinda macho yake amebarikiwa uwezo wa kuona mbali sana na anaona kwa uwazi kabisa inasemekana anauwezo wa kumuona mwenzake akiwa Maili 50 kwa uwazi kabisa! Jambo hili linatufundisha nini? Naamini unaweza kupata picha Fulani



ž  Tai huona kwa uwazi kabisa Maili “50”
ž  I Maili =1.6 km
ž  Maili 50 = 80 km


Mamia ya watu hodari wamewahi kuishi duniani na kupita wakiwemo watu maarufu sana duniani na viongozi wakubwa



Ili dunia iweze kuwa na Mafanikio makubwa sana inahitaji watu na viongozi wenye uwezo wa kuona mbali sana, Abraham Lincoln rais wa 16 wa Marekani aliongoza katika wakati mgumu sana wenye matatizo mengi na inchi ikiwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, lakini ndiye aliyefanikiwa kuweka misingi ya umoja na kukomesha utumwa na kuifanya Marekani iwe kama ilivyo leo,



Ili dunia iweze kuwa na mafanikio ni lazima iwe na watu wenye uwezo wa kuona mbali, wanaoangalia faida za mbeleni za kwao na za kizazi kinachokuja badala yao

Ili uweze kuwa na mafanikio:-


·         Ni lazima uwe na uwezo wa kuona mbali Mithali 29:18Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.”
·         Watu wasio na maono ya mbali wanaweza kutugawa kupitia dini na ukabila
·         Watu wasioona mbali hawajali kutunza Mazingira
·         Watu wasioona mbali hawaogopi kuharibu mahusiano
·         Watu wasioona mbali hawaogopi kuua wanyama kama tembo kwa faida yao
·         Watu wasioona mbali hawaogopi kufanya Ufisadi kwa kuifilisi nchi
·         Watu wasioona mbali hawafikiri kujisomea kwa bidii
·         Watu wasioona mbali hawafikiri kujiwekea akiba

Mithali 6:6-8 “Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima. Kwa maana yeye hana akida, Wala msimamizi, wala mkuu, Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.”
·         Watu wasioona mbali hawafikiri kuhusu maisha yao baada ya kufa duniani  Waebrania 11:9-10 Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.


Luka 12:16-21,
Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana; akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu. Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu. Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi. Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.”

Yakobo 4:13-15Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida; walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka. Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi.”


·         Kuna majuto kama hatutaweka mipango yenye kumuhusisha  Mungu.
Awaye yote aliye kama tai atakuwa na ujuzi wa kuona mbali na kuzingatia faida za siku zijazo kuliko kuangalia leo. Unayaona mwindo yako kwa mbali. Ni lazima tuwe na maono makubwa yaliyopimwa kwa kina na yatakayoleta faida kubwa na matokeo makubwa katika jamii.

Tai ni ndege wasioogopa Mawindo. wala maadui



2.     



Tai ni ndege asiyeogopa hata kidogo, wakati wote anapambana kuhakikisha anashinda, atapambana kuhakikisha anapata mawindo yake au anatawala,unapoangalia sinema za maisha ya tai utaweza kuona  hawaogopi mawindo haijalishi mawindo yao ni makubwa kiasi gani hata kama ni mbuzi ambaye anaonekana kuwa mkubwa kuliko uwezo wake tai ni lazima atabeba, wana ujuzi mkubwa wa kuwinda na ni mahodari, tai haogopi


Ni muhimu kufahamu kuwa kama unataka kufanikiwa katika maisha haya usiogope kufanya jambo gumu, usiogope kukabiliana na watu wakubwa au waliokuzidi umri, hakikisha kuwa unakipigania kile unachokipenda,


·         Usiogope kupigania unachokipenda Waamuzi  14:1-7 ”Samsoni akatelemkia Timna, akaona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti. Kisha akapanda, akawaambia baba yake na mama yake, akasema, Nimemwona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti; basi mnipatie, nimwoe. Ndipo baba yake na mama yake wakamwambia, Je! Hapana mwanamke hata mmoja katika ndugu zako, au katika jamaa zangu zote, hata uende kumwoa mwanamke kwa hawa Wafilisti wasiotahiriwa? Samsoni akamwambia baba yake; Mnipatie huyo, kwa maana ananipendeza sana. Lakini baba yake na mama yake hawakujua ya kuwa jambo hili ni la Bwana; maana alitaka kisa juu ya Wafilisti. Basi wakati ule Wafilisti walikuwa wakiwatawala Israeli. Ndipo Samsoni na baba yake na mama yake wakatelemkia Timna, wakafika mashamba ya mizabibu huko Timna; na tazama, mwana-simba akamngurumia. Roho ya Bwana ikamjilia kwa nguvu, naye akampasua kana kwamba anampasua mwana-mbuzi, wala hakuwa na kitu cho chote mkononi mwake; lakini hakuwaambia baba yake na mama yake aliyoyafanya.Basi akatelemka na kuzungumza na huyo mwanamke; naye akampendeza Samsoni sana.


·         Usiogope kusimama katika kweli hata kama itakuletea madhara
·         Usiogope ukubwa wa tatizo unalopambana nalo pigania mpaka kieleweke Kataa hofu Hesabu 13:25-33 "Wakarejea baada ya kuipeleleza nchi, mwisho wa siku arobaini. Wakaenda wakafika kwa Musa, na kwa Haruni, na kwa mkutano wote wa wana wa Israeli, katika jangwa la Parani, huko Kadeshi; wakawaletea habari, wao na mkutano wote, wakawaonyesha matunda ya nchi.  Wakamwambia wakasema, Tulifika nchi ile uliyotutuma, na hakika yake, ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali, na haya ndiyo matunda yake. Lakini watu wanaokaa katika nchi ile ni hodari, na miji yao ina maboma, nayo ni makubwa sana; na pamoja na hayo tuliwaona wana wa Anaki huko.  Amaleki anakaa katika nchi ya Negebu; na Mhiti, na Myebusi, na Mwamori wanakaa katika milima, na Mkanaani anakaa karibu na bahari; na kando ya ukingo wa Yordani. Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa, akasema, Na tupande mara, tukaitamalaki; maana twaweza kushinda bila shaka. Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi.Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno. Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.



·         Usiogope ugumu wa masomo unayosoma
·         Usiogope au kuonea aibu aina ya kazi unayoifanya
·         Lengo lako kuu ni kuhakikisha unafanikiwa
·         Usiogope mateso utakayoyapata kwaajili ya imani au kile unachokipigania
·         Usiogope kuanzisha huduma au kufungua kanisa, usiogope kuwa mmisionary, usiogope kugombea urais kama Mungu anataka ufanye jambo kwa faida yake lifanye
·         Uisogope kufanya lolote ili kufanikisha malengo yako, Tai hawaogopi mawindo yao hata kama anachokiwinda ni kikubwa kuliko umbile lake.

3.     Tai ni Hodari hawaogopi Dhuruba.



Ukitaka kujua uhodari wa Tai utaweza kuuona wakati wa dhoruba, wakati huu ndege wengine wote hukimbia na kujificha kwa kuogopa dhoruba , kwa tai mambo ni tofauti anafunua mbawa zake na kuzitanua na kupaa kwenda juu zaidi, taia wanatabia ya kutumia dhoruba kwa faida, wakati ndege wa kawaida wakiogopa, ni muhimu kufahamu kuwa watu wanaolinganishwa na tai hawakimbii changamoto zozote bali huzitumia changamoto kusimama na kuongeza viwango, Mungu anataka watu wasiokimbia changamoto bali wenye uwezo wa kukabiliana nazo huku wakisimama katika kusudi au kuelekea juu zaidi
Mtu yeyote anayeogopa Changamoto hawezi kufanikiwa
·         Wakati wa Dhuruba tai Hakimbii kama wengine
·         Tai hupanua mbawa zake na dhuruba humpeleka juu sana
·         Tai huitumia dhoruba kwa faida
·         Usikimbie changamoto wala usiziogope
·         Tumia changamoto kuongeza viwango au kujiongeza  Matendo 14:21-22, "Hata walipokwisha kuihubiri Injili katika mji ule, na kupata wanafunzi wengi, wakarejea mpaka Listra na Ikonio na Antiokia,wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi.


   1Petro 4:12 "Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho."




4.     Tai wanaruka juu sana.




ž  Ndege huyu ndiye anayejulikana kama mfalme wa anga inasemekana tai wanauwezo wa kuruka juu kiasi cha fiti 10,000, katika kiwango hicho hutaweza kumuona ndege mwingine na ukimuona ni lazima atakuwa tai, Tai haruki wala kutafutiza chakula pamoja na njiwa, alisema Dr, Myles Munroe Marehemu, alisema wakati njiwa wakiwa ardhini wanachakuachakua siku nzima na kulalamika,Tai hawanung’uniki, hawapigi kelele, wanapaa juu sana wakisubiri mawindo wakisubiri nafasi waweze kuitumia, watu wakuu duniani ni wale wanaotatua matatizo na sio wanaolalamika, wanatumia nafasi na changamoto yoyote kama tai dhoruba inapotokea. Ni watu wanaojitunza na kutokuchangamana na wengine Wakolosai 3:1-2 “Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.


5.     Tai hawali kibudu


Ni muhimu kufahamu kuwa sifa nyingine ya tai ni pamoja na kutokula kibudu tai hawali wasichokiua wenyewe, siku zote wanakula nyama ya mawindo yao wenyewe, wanakula nyama safi na mpya hivi ndivyo watu wakuu katika dunia wanavyopaswa kuwa,
Watu wakubwa duniani hukaa na watu wenye mawazo mpana na wenye kufikiri na wenye uwezo wa kuamua, watu hodari wasiokata tamaa, hawa ndio watu wanaoweza kuleta mabadiliko makubwa Duniani, watu wenye uwezo wa kuleta badiliko unapowasikiliza au kukaa nao karibu, watu wenye ushawishi
Kamwe usipoteze muda na watu wanaopoteza muda
Kamwe usipoteze muda na watu wenye kusengenya
Kamwe usipoteze muda na watu wasio na imani
Kamwe usipoteze muda na watu wenye kuzungumzia wengine 

Walawi 6:9-13 “Haya, mwagize Haruni na wanawe, uwaambie, Amri ya sadaka ya kuteketezwa ni hii; hiyo sadaka ya kuteketezwa itakuwa pale motoni juu ya madhabahu usiku wote hata asubuhi; na huo moto wa madhabahu utawaka juu yake usizimike. Naye kuhani atavaa nguo yake ya kitani, na suruali zake za kitani atazivaa mwilini mwake; naye atayazoa majivu ambayo huo moto umeiteketezea sadaka juu ya madhabahu, kisha atayaweka kando ya madhabahu. Kisha atayavua mavazi yake, na kuvaa mavazi mengine, kisha atayachukua yale majivu kwenda nayo nje ya marago hata mahali safi. Na huo moto ulio madhabahuni atautunza uwake daima juu yake, usizimike; naye kuhani atateketeza kuni katika moto huo kila siku asubuhi; naye ataipanga sadaka ya kuteketezwa juu yake, naye atayateketeza mafuta ya sadaka za amani juu yake. Moto utatunzwa uwake juu ya madhabahu daima; usizimike.”


Kamwe usipoteze muda na watu wenye kupiga majungu na fitina
Kamwe usipoteze muda na watu ambao kuanguka kwa wengine ndio furaha yao
Kamwe usipoteze muda na watu wenye kuhukumu
Kamwe usipoteze muda na watu wenye mitazamo hasi wenye kujihusisha na rushwa na uovu hivyo ni vibudu, tafuta vya kwako mwenyewe mawindo yako mwenyewe.


Tai anayekula Mizoga!


Ni muhimu kufahamu kuwa tai tunayemzungumzia hapa  mwenye sifa tulizozitaja anaitwa Eagle huyu hali mizoga na taia anayetajwa katika Mathayo 24:28 huyu ndiye taia anayekula mizoga huyu anaitwa VULTURE
§  Mathayo 24:28Kwa kuwa popote ulipo mzoga ndipo watakapokusanyika tai
§  “Whenever there is carcass, there the VULTURE will gather” NIV.
§  For wheresoever' the carcase  is there will eagles be gathered together KJV
Tai anayekula Mizoga haitwi “Eagle” anaitwa  Vulture
Huyu ni aina nyingine ya tai ambaye hupatikana mashariki ya kati nyikanani na katika mbuga za wanyama Afrika tai huyu ndiye anayekula mizoga kiingereza sahii anaitwa VULTURE huyu ndiye ambaye Yesu anazungumza katika injili ya Mathayo

Tai wanauwezo wa kujitia nguvu mpya

6.    



Zaburi 103:4-5 “ Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,  Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema, Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai;”


Isaya 40:31 “Bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.”


Moja ya tabia ya tai ya kushangaza sana ni uwezo wake wa kujitia nguvu kwa upya ukiacha kuwa wanauwezo wa kuona mbali lakini wana maisha marefu inasemekana Tai anapofikisha miaka 30 anakuwa anachakaa na manyoya yake yanakuwa yamezeeka hivyo kuathiri uwezo wake wa kiutendaji, inapofikia hivyo tai hakati tamaa ya kuishi badala yake hutafuta kilele kikubwa cha mlima na kutulia kwa miezi mitano anagonga mdomo wake katika mawe ya miamba na kungoa ngozi ya juu, hujinyonyoa manyoa nyake yote wakati huu ajajigomoa na kuanza kuwa na manyoya mapya mdomo mpya na magamba mapya jambo hili humfanya tai awe na uwezo wa kurejeza uhai wake kwa miaka mingine 30-40, Ndo maana biblia inasema ujana wako utarejezwa kama tai


 Watu wenye akili ni watu wanaoweza kujitafakari na kuangalia yote waliyoyafanya katika maisha yao liwe jema au baya linapokuwa baya unaachana nalo  wanatafuta nini lililo jema na lipi wanaweza kuliendeleza na jipya gani wanaweza kuenda nalo, na kujifunza jambo jipya la kufanya siku hadi siku. 1Samuel 30:1-8 “Ikawa, Daudi na watu wake walipokuwa wamefika Siklagi siku ya tatu, hao Waamaleki walikuwa wameshambulia Negebu, na Siklagi, nao wameupiga Siklagi, na kuuchoma moto; nao wamewachukua mateka wanawake waliokuwamo wakubwa kwa wadogo; hawakuwaua wo wote, ila wakawachukua, wakaenda zao. Basi Daudi na watu wake walipoufikilia mji, tazama, ulikuwa umechomwa moto; na wake zao, na watoto wao, waume kwa wake, wamechukuliwa mateka. Ndipo Daudi na watu waliokuwa pamoja naye wakainua sauti zao na kulia, hata walipokuwa hawana nguvu za kulia tena. Na hao wake wawili wa Daudi walikuwa wamechukuliwa mateka, Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili, aliyekuwa mkewe Nabali, wa Karmeli. Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana nafsi za hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi alijitia nguvu katika Bwana, Mungu wake. Kisha Daudi akamwambia Abiathari, kuhani, mwana wa Ahimeleki, Tafadhali niletee hapa hiyo naivera. Naye Abiathari akamletea Daudi naivera huko. Daudi akauliza kwa Bwana, akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote.”
Kamwe usikubali kudumaaa
Usikubali kubaki vilevile siku zote



7.     Tai wanatoa mafunzo kwa vifaranga vyao

Kumbukumbu la torati 32:10-11 “Alimkuta katika nchi ya ukame, Na katika jangwa tupu litishalo; Alimzunguka, akamtunza; Akamhifadhi kama mboni ya jicho; Mfano wa tai ataharikishaye kioto chake; Na kupapatika juu ya makinda yake, Alikunjua mbawa zake, akawatwaa, Akawachukua juu ya mbawa zake;”



Amini usiamini tai wanaotoa mafunzo kwa vijana wao, tai wanafikiriwa kuwa ni ndege katili sana wakati wa kutoa mafunzo na kama hujui makusudi yao unaweza kukubaliana kuwa ni ndege wakatili, jambo moja la kushangaza kuhusu tai ni uwezo wake wa kutoa mafunzo kwa vifaranga vyake, utafiti unaonyesha kuwa hakuna aina ya ndege mwenye mvuto na mpole kama tai kwa watoto wake kushinda tai


Mama wa tai anapogundua kuwa wakati umefika kwa vifaranga vyake kujifunza kuruka, anawabeba vifaranga wake mgongoni na kupanua mbawa zake anaruka juu sana kisha anajiondoa kutoka kifaranga chake na kukiachia kiangukekinapoanguka kinajifunza kuruka akiona kinaogopa na kinataka kuanguka anakidaka na kukirejeza katika kiota chake, atafanya hivyo mpaka kimejifunza kuruka.


Watu wakubwa sana duniani sio mabosi, wakati wote wanawafanya wengine kukua katika jamii na wanawapa changamoto lakini wanawasaidia kukua na kujiamini na kuendelea kuwapa maelekezo wengine mpaka wameweza kufanya vilevile kama wao wafanyavyo.

Kumbukumbu 8:1-6 “Amri hii ninayokuamuru leo mtaishika kuitenda, mpate kuishi na kuongezeka, na kuingia katika nchi ile ambayo Bwana aliwaapia baba zenu; nanyi mtaimiliki. Nawe utaikumbuka njia ile yote Bwana, Mungu wako aliyokuongoza miaka hii arobaini katika jangwa, ili akutweze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo. Akakutweza, akakuacha uone njaa, akakulisha kwa mana, usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha Bwana. Mavazi yako hayakuchakaa, wala mguu wako haukuvimba, miaka hiyo arobaini. Nawe fikiri moyoni mwako, ya kuwa kama vile baba amrudivyo mwanawe, ndivyo Bwana, Mungu wako, akurudivyo. Nawe uzishike amri za Bwana, Mungu wako, upate kwenda katika njia zake, na kumcha.”

8.     Tai hutoa mafunzo kwa wengine


Amini usiamini tai wanaotoa mafunzo kwa vijana wao, tai wanafikiriwa kuwa ni ndege katili sana wakati wa kutoa mafunzo na kama hujui makusudi yao unaweza kukubaliana kuwa ni ndege wakatili, jambo moja la kushangaza kuhusu tai ni uwezo wake wa kutoa mafunzo kwa vifaranga vyake, utafiti unaonyesha kuwa hakuna aina ya ndege mwenye mvuto na mpole kama tai kwa watoto wake kushinda tai

Mama wa tai anapogundua kuwa wakati umefika kwa vifaranga vyake kujifunza kuruka, anawabeba vifaranga wake mgongoni na kupanua mbawa zake anaruka juu sana kisha anajiondoa kutoka kifaranga chake na kukiachia kiangukekinapoanguka kinajifunza kuruka akiona kinaogopa na kinataka kuanguka anakidaka na kukirejeza katika kiota chake, atafanya hivyo mpaka kimejifunza kuruka. “2Timotheo 2:2” Ebra 5: 11-14, Math 5:3-4; Ayub 5:11; Zab 91:14).

9.      Tai huyatoa maisha yake kwa ajili ya wengine Eagle do sacrifice



·         Tai anapotaka kuangua vifaranga vyake
·         Hujenga kiota cheke juu sana kwenye miti mirefu mno
·         Kiota cha tai huwa na vipande vya miti migumu
·         Kwaajili ya kuwahurumia vifaranga vyake Tai hujinyofoa manyoya yake mwili mzima ili vifaranga vyake visipate maumivu wakati huu tai huwa hali vizuri hufunga na kuatamia ili vifarabga vyake visiumie
·         Ukomavu wa juu kabisa wa kiroho ni mtu kujitoa kwaajili ya wengine
·         Ukomavu wetu wa juu sana Kiroho utajulikana pale tunapokuwa tayari kuyatoa maisha yetu kwaajili ya wengine

·         Yuda - Mwanzo 44:1-34,"Akamwamuru yule msimamizi wa nyumba yake akisema, Jaza magunia ya watu hawa chakula kwa kadiri wawezavyo kuchukua, utie na fedha ya kila mtu kinywani mwa gunia lake. Na kikombe changu, kikombe kile cha fedha, ukitie kinywani mwa gunia la yule mdogo pamoja na fedha ya nafaka yake. Akafanya kama vile alivyomwambia Yusufu.Asubuhi kulipopambazuka, hao watu wakapewa ruhusa, wao na punda zao. Na walipotoka mjini, wala hawajaendelea sana, Yusufu akamwambia yule msimamizi wa nyumba yake, Ondoka, uwafuate watu hawa, nawe utakapowapata, waambie, Kwa nini mmelipa mabaya kwa mema? Je! Kikombe hiki, sicho anyweacho bwana wangu? Naye hufanya uaguzi kwa hicho. Mmefanya vibaya kwa kufanya hivi. Akawafuata, akawapata, na kuwaambia maneno hayo. Wakamwambia, Kwa nini bwana wangu anasema maneno kama haya? Hasha! Watumwa wako wasifanye hivi; tazama, hizo fedha mlizoziona kinywani mwa magunia yetu, tumekuletea tena kutoka nchi ya Kanaani. Tuwezeje sisi kuiba nyumbani mwa bwana wako fedha au dhahabu? Atakayeonekana kuwa nacho miongoni mwa watumwa wako, na afe, na sisi nasi tutakuwa watumwa wa bwana wangu. Akasema, Basi na iwe hivyo kama mlivyosema, Mtu atakayeonekana kuwa nacho atakuwa mtumwa wangu, na ninyi mtakuwa hamna hatia. Wakafanya haraka, wakashusha kila mtu gunia lake, na kufungua kila mtu gunia lake. Naye akatafuta, akaanza kwa mkubwa na kuisha kwa mdogo. Kikombe kikaonekana katika gunia la Benyamini. Wakararua nguo zao, wakaweka kila mtu mzigo wake juu ya punda wake, wakarudi mjini. Akaja Yuda na ndugu zake nyumbani kwa Yusufu, naye mwenyewe alikuwamo, nao wakamwangukia kifudifudi. Yusufu akawaambia, Ni tendo gani hili mlilolitenda? Hamkujua ya kwamba mtu kama mimi naweza kufanya uaguzi? Yuda akasema, Tumwambie nini bwana wangu? Tusemeje! Tujivutieje haki? Mungu ameona uovu wa watumwa wako. Tazama, sisi ni watumwa wa bwana wangu, sisi na yeye ambaye kikombe kilionekana mkononi mwake. Akasema, Hasha! Nisifanye hivi; mtu ambaye kikombe kilionekana mkononi mwake, ndiye atakayekuwa mtumwa wangu. Nanyi enendeni zenu kwa amani kwa baba yenu.  Ndipo Yuda akamkaribia, akasema, Tafadhali, bwana wangu, mtumwa wako na aseme neno moja masikioni mwa bwana wangu, wala hasira yako isimwakie mtumwa wako, maana wewe u kama Farao.  Wewe, bwana wangu, ulituuliza watumwa wako, ukisema, Je! Mnaye baba, au ndugu? Tukakuambia wewe, bwana wangu, Tunaye baba, naye ni mzee, na mwana wa uzee wake ni mdogo, na nduguye amekufa; amebaki yeye peke yake wa katika tumbo la mamaye, na baba yake anampenda.  Ukatuambia watumwa wako, Mleteni kwangu, ili macho yangu yamwangalie. Tukakuambia, bwana wangu, Kijana hawezi kumwacha babaye, maana akimwacha babaye, babaye atakufa. Ukatuambia watumwa wako, Asiposhuka ndugu yenu mdogo pamoja nanyi, hamtaniona uso wangu tena Ikawa tulipokwenda kwa mtumwa wako, baba yangu, tukamwarifu maneno yako, bwana wangu. Kisha baba yetu akanena, Rudini huko, mkatununulie chakula kidogo. Tukasema, Hatuwezi kwenda; ndugu yetu mdogo akiwapo pamoja nasi, tutashuka, maana hatutaweza kuuona uso wa mtu huyo, ndugu yetu mdogo asipokuwa pamoja nasi. Mtumwa wako, baba yangu, akatuambia, Mnajua ya kuwa mke wangu alinizalia wana wawili;mmoja alitoka kwangu, nikasema, Bila shaka ameraruliwa, wala sikumwona tangu hapo.  Na mkiniondolea huyu naye, na madhara yakimpata, mtashusha mvi zangu na msiba kaburini. Basi, nikienda kwa mtumwa wako, baba yangu, na huyu kijana hayupo pamoja nasi, iwapo roho yake imeshikamana na roho ya kijana;  itakuwa atakapoona ya kwamba huyu kijana hayuko, atakufa; na watumwa wako watashusha mvi za mtumwa wako, baba yetu, kwa huzuni kaburini.Kwa maana mtumwa wako alijifanya mdhamini wa huyu kijana kwa baba yangu, nikisema, Nisipomrudisha kwako, nitakuwa na hatia kwa baba yangu sikuzote. Basi, sasa nakusihi, uniache mimi mtumwa wako nikae badala ya huyu kijana kuwa mtumwa wa bwana wangu; na huyu kijana umwache aende pamoja na nduguze. Kwa maana nitawezaje kumwendea baba yangu, na huyu kijana hayuko pamoja nami? Nisije nikayaona mabaya yatakayompata baba yangu.




·         Daudi - 2Samuel 18:31-33 "Na tazama, yule Mkushi akafika; Mkushi akasema, Nina habari kwa bwana wangu mfalme; kwa maana Bwana amekulipizia kisasi leo juu ya hao wote walioinuka kupigana nawe. Naye mfalme akamwambia yule Mkushi, Yule kijana, Absalomu, je! Yu salama? Yule Mkushi akajibu, Adui za bwana wangu mfalme, na wote wainukao ili kukudhuru, na wawe kama alivyo yule kijana.  Naye mfalme akataabika sana, akapanda juu, akaingia kile chumba kilichokuwa juu ya lango, akalia; na katika kwenda kwake alisema hivi, Mwanangu Absalomu! Ee mwanangu! Mwanangu Absalomu! Laiti ningalikufa badala yako, Absalomu, mwanangu, mwanangu! "



·         Yohana 18: 7-8 ". Basi akawauliza tena, Mnamtafuta nani? Wakasema, Yesu Mnazareti. Yesu akajibu, Nimekwisha kuwaambieni ya kwamba ni mimi; basi ikiwa mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao."




·         1Yohana 4:10 “Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu” Kuja kwa Yesu Kristo Duniani ni matokeo ya upendo mkuu wa Mungu kwa mwanadamu, ni matokeo ya juu kabisa ya upendo usioweza kupimika


·         Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”


·          Yohana 15:13:- “Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake”.


Ni Muhimu kufahamu kuwa upendo unaotajwa hapa sio upendo wa kawaida ni upendo wa kimungu ni upendo wenye huruma za kiungu sio upendo wa kibinadamu kwa kawaida katika lugha ya kiyunani neno upendo lime gawanyika katika tafasiri kuu nne za upendo ambazo ni Phileo, Storge, Eros, na Agape au agapan:- aina hizi za upendo tunaweza kuzichambua kama ifuatavyo:- • PHILEO aina hii ya upedno kwa kiingereza tunaiita “Companionable love”yaani ni upendo wa Kirafiki, Ni upendo unaojengeka kutokana na kushirikiana kuzungumza kukubaliana kupeana zawadi,kuendana na kadhalika huu ni upendo wa kirafiki • STORGE aina hii ya upendo kwa kiingereza tunaiita “Natural affection love” yaani ni upendo unaotokana na kuweko kwa undugu wa damu, unampenda mtu kwa sababu ni baba, mama, mwana, mjomba shangazi, dada, kaka na kadhalika katika mahusiano ya kindugu na damu • EROS aina hii ya upendo kwa kiingereza tunaiita “Erotic love” yaani ni upendo unaotokana na mvuto wa kimapenzi, ni upendo unaohusu jinsia tofauti na yako, unampenda mtu kwa sababu ya muonekano wake , umbile lake na uzuri wake hii husababishwa na mvuto wa kimapenzi, body morphology is concern Muonekana wa mwili au mvuto unahusika na upendo huu ni wa kihisia. • AGAPE aina hii ya Upendo kwa kiingereza tunaiita “unconditional love” Yaani ni upendo wenye kupitiliza mipaka ya kibinadamu, ni upendo ambao asili yake ni Mungu ni upendo unaomtakia mema kila mmoja awe adui au ndugu upendo huunapita mipaka ya kawaida ya kibinadamu, hauangalii hali ya hewa, unampenda Mungu au mtu bila kutarajia kitu kutoka kwake, bila kujali mtu huyo ni mwema au mbaya, bila kujali ni wakati mzuri au mbaya, bila kujali ni wakati wa matatizo au raha upendo huu unabaki vilevile na haubadilishwi na matukio, Mungu anapoamuru kupendana au kumpenda Yeye katika maandiko anamaanisha upendo huu wa Agape. Upendo huu pia hujulikana kama Sacrificial love , upendo wenye kujitoa sadaka kwaajili ya wengine, ni upendo unaojali kuwahudumia wengine zaidi ya sisi wenyewe, Huu ndio upendo ulioamriwa katika 1Wakoritho 13 upendo wa kiungu.

1. Daktari mmoja wa Uingereza aitwaye Will Pooley alikuwa ni moja ya madaktari waliokuwa mstari wa mbele Nchini “Sierra Leone” huko walikuwa na wenzake wengi wakipambana na wagonjwa wa EBOLA na virusi vyake katika harakati hizo Madaktari wengi sana na Manesi wengi sana wakiwemo wa Afrika Magharibi waliambukizwa virusi vya ebola wakati walipokuwa wakiwauguza wagonjwa na wengi wao walikufa Ugonjwa utokanao na kirusi cha Ebola ni ugonjwa hatari wenye uwezo wa kusababisha kifo kwa asilimia 90. Shirika la afya duniani, WHO katikatovuti yake inasema kwa mara ya kwanza ulibainika mwaka 1976 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Sudan. Chanzo cha kirusi hiki hadi sasa hakijulikani lakini popo aina ya (Pteropodidae) wanaonekana kuwa wabebaji wa kirusi hicho, kwa mujibu wa ushahidi uliopo sasa. Maambukizi hupatikana kwa kila aina ya majimaji yanayotoka katika mwili wa binadamu ni ugonjwa hatari na unaoua kwa haraka na hauna tiba Will Pooley alipoupata ugonjwa huu alirejeshwa katika ndege maalumu na kuanza kutibiwa chini ya uangalizi maalumu huko uingereza Jambo la kushangaza ni kuwa baada ya kupona kwa bahati tu Will Pooley alitangaza nia yake ya kurudi tena Sierra Leone kusaidiana na wenzake kupambana na ugonjwa huo. Mtu huyu aliwashangaza wengi sana na kuwaogopedha wengi sana akiwa amepona kwa asilimia 100%alisema atarudi Africa kusaidia zaidi maana alizaliwa kwaajili ya hayo, jambo hili lilimfanya aandikwe kama shujaa na mwanadamu mwenye uwezo wa kujitoa kwa kiwango cha juu.

2. Maximilian Kolbe alikuwa ni Padre aliyetokea Poland aliuawa kama mfungwa tarehe 14 August 14,1941, Jeshi la wa NAZI waligundua kuwa baadhi ya wafungwa wamejaribu kutoroka na hivyo waliamua kuwaua wafungwa kadhaa, walijaribu kuwaua kwa njia mbalimbali, na hivyo walichagua wafungwa 10 ili wauawe na kifo chao kiliamuriwa kuwa kifo cha njaa, wafungwa waliamuriwa kujitoa mmoja mmoja yeye mwenyewe na mfungwa wa kwanza kuchaguliwa alijulikana kama Franciszek Gajowinczek mfungwa huyu alipochaguliwa alilia kwa huzuni kubwa akimtaja mkewe, watoto wake na familia yake na kusikitika kuwa hatowaona tena kutokana na swala hili Maximillian alisimama na kusogea mbele na kuomba afe yeye kwa niaba ya Franciszek ombi lake lilikubaliwa, wafungwa waliwekwa kizuizini kwa muda wa siku kadhaa bila kula wengine walikunywa mikojo yao ili waweze kuishi, Maximillian alikaa kwa wiki mbili bila kufa huku wengine wote wakiwa wamekufa, walimchoma sindano ya kufa hakufa na hivyo waliamua kukata kichwa Pope John Paul II alimtangaza kuwa Mtakatifu kutokana na moyo wake

3. Mifano hii inatusaidia kujua kile ambacho Bwana wetu Yesu amekifanya Pale alipojibu kuwa kwaajili ya haya Nalizaliwa alikuwa akimkumbusha Pilato kuwa yeye amekuja kuwafia wanadamu, amekuja kuwaonyesha upendo wa Mungu jinsi ulivyo

Isaya 53:1-5
Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani? Maana alikua mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani. Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.” Huu ni upendo mkubwa sana Yesu alikufa kwaajili yetu, Hatuna budi kuhakikisha kuwa tunasimama upande wake siku zote za maisha yetu, tusihesabu damu yake ya thamani kuwa kitu cha hovyo tudumu katika wokovu na kuwa wavumilivu kwaajili ya Mungu wetu.”

Mukhtasari:

·         Tai ni wenye uwezo mkubwa wa kuona mbali.
·         Tai ni ndege wasioogopa Mawindo.
·         Tai ni Hodari hawaogopi Dhuruba.
·         Tai wanaruka juu sana.
·         Tai hawali kibudu
·         Tai wanauwezo wa kujitia nguvu mpya
·         Tai wanatoa mafunzo kwa vifaranga vyao
·         Tai hutoa mafunzo kwa wengine
·         Tai huyatoa maisha yake kwa ajili ya wengine


Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima
0718990796

Jumatatu, 30 Machi 2020

Nguvu ya Machozi!

Waebrania 5:7Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;


 
Utangulizi:

Tunajifunza kutoka katika maandiko kuwa kwa kila jambo kuna majira yake Muhubiri 3:1-4Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa yaliyopandwa;  Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga; Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;kwa msingi huo kila mwanadamu ana wakati wa kulia na kuna wakati wa kufurahi na kadhalika hata hivyo kwa kuwa nazungumzia kuhusu kulia kila mwanadamu ana wakati wake wa kulia na  wakati wa kucheka, yako mambo ambayo katika maisha ama watu wanaotuzungunga  na ama aina ya mapito tunayoyapitiatyanaweza kukufikisha katika point ambayo kwa vyovyote vile tunaweza kulia.
Dunia huwa inasema kuwa wanaume hawalii, Lakini maandiko yanatuambia watu wakubwa sana wa Mungu walilia, watu ambao ni majasiri na wenye nguvu na mashujaa pia wakati fulani walilia, Hata Yesu Kristo ambaye ni Mungu alipokuwa katika mwili duniani alilia, Wakati fulani katika ulimwengu huu itatupasa kulia na kuliitia jina la Mungu kwaajili ya maswahibu mbalimbali na Mungu yule tumuabuduye atatupa amani, atatufariji na kutokeza msaada kwa nini kwa sababu maandiko yanaonyesha kuwa iko nguvu kubwa sana katika machozi.

Mungu anawajali sana wanadamu.

Ni muhimu sana kufahamu kuwa Mungu anawajali sana wanadamu ni jambo la kushangaza kuwa mwandishi  wa kitabu cha waebrabia alihoji kuwa mwanadamu ni nani hata umkumbuke Waebrania 2:6Mwanadamu ni nini hata umkumbuke, Ama mwana wa binadamu, hata umwangalie? “ Mungu anatamini sana wanadamu kiasi ambacho tukiomba anatusikia na ni Mungu mwenye kujishughulisha sana na mambo yetu 1Petro 5:6-7Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.”Unaweza kuona tunamuabudu Mungu ambaye anajishugulisha sana na wanadamu anatujali mno, maandiko yanasema anajishughulisha sana na mambo yetu, sisi hatupaswi kunung’unika tunapaswa kumuomba na kumkabidhi njia zetu zote, hivyo ndivyo maandiko yanavyotufunza angalia katika Zaburi 37:5Umkabidhi Bwana njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya.” Unaona kwa msingi huo tunaweza kumkabidhi Mungu mahitaji yetu yote, naye atashughulika nayo, kwa sababu hiyo maandiko yanatutia moyo kwamba hatupaswi kufadhaika Wafilipi 4:6-7Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.Mungu huwa ndio kimbilio letu na ni asili ya nguvu zetu na yuko tayari kutusaidia wakati wa mahitaji hususani Mateso kama tukimuomba Zaburi 46:1 “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.” Hata tunapopitia mateso na mapito ya aina mbalimbali Mungu bado ni ngao yetu Zaburi 9:9Bwana atakuwa ngome kwake aliyeonewa, Naam, ngome kwa nyakati za shida.” Wakati wote tupitiapo shida na kuonewa Mungu anakuwa ngoime yetu ba anatoa msaada unaotatikana au unaohitajika, kwa msingi huo maandiko yanataka tusiogope kwa sababu Mungu atatusaidia Isaya 41:10usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.Kwa hivyo tupitapo katika majaribu hatupaswi kuona kuwa cha ajabu na kama ikiwezekana tunapaswa kufurahia Yakobo 1:2-4Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.”Hata hivyo pamoja na maandiko kututia Moyo kuhusu maombi na namna Mungu anavyojali maisha yetu na namna anavyojihusisha nayo mamandiko yanatuonyesha kuwa liko jambo lingine kubwa na la ziada ambalo likiambatanishwa na maombi Mambo makubwa sana hutokea jambo hilo Mungu analithamini sana na hili sio lingine ni Maombi yanapoambaanishwa na Machozi, Mungu anayathamini sana machozi, machozi yana faida kubwa sana kisayansi na kiroho, leo tutachukua Muda kuangalia nguvu ya machozi na kujibu swali kwa nini Mungu anayathamini sana Machozi!

Mungu anathamini sana Machozi!


Utafiti usio rasmi wa kisayansi umebaini kwamba kulia machozi kunampa mwanadamu nafasi ya juu zaidi ya kujitibu kutoka katika mgandamizo mkubwa wa mawazo yaani stresses, Hii ni kwa sababu wakati mtu analia anatoa chemikali iitwayo Oxytocin na Endorphins, Chemikali hizi zinapotoka zinaleta unafuu kwa mwanadamu na kumfanya ajisikie vizuri kimwili na kihisia na kuondoa maumivu ya moyo na kwa sababu hiyo inakubalika kuwa kisayanzi kulia kunaondoa uchungu na kuleta unafuu wa roho.

Wanadamu hulia machozi kutokana na hisia za hali ya juu tofauti tofauti katika nafsi zao, Machozi yanabeba hisia za juu kabisa za homoni kuliko aina nyingine yoyote ya chemikali za homoni, kutoa machozi kuna faida kubwa sana kiafya. Na Endapo mtu atapatwa na jambo lenye kuumiza sana hisia zake na kujizuia kutokulia atakuwa amejeruhika kwa kiwango kikubwa nafsini mwake.

Katika namna isiyoweza kuelezeka ulimwengu wa kiroho nao unathamini sana machozi, Mungu anayaangalia sana machozi, kiasi ambacho hawezi kuyadharau kwa namna yoyote, Machozi huwa yana nguvu kubwa sana katika ulimwengu wa Kiroho, wakati wowote watu walipolia na kuugua Mungu hakuweza kuvumilia alishuka na kuleta wokovu au msaada Zaburi 107:4-6Walitanga-tanga jangwani katika njia ya nyika; Hawakuona mji wa kukaa. Waliona njaa, waliona na kiu, Nafsi yao ilikuwa ikizimia ndani yao. Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao.” Zaburi 107:19 “Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao.” Zaburi 34:17Walilia, naye Bwana akasikia, Akawaponya na taabu zao zote.” Mungu anazingatia sana Machozi ya mwanadamu, mtu anapolia maana yake amefikia kiwango cha juu zaidi cha kukata tamaa katika maisha yake, hana mlango mwingine wa msaada zaidi ya Mungu, hana namna ya kujieleza tena, hakuna mtu anaweza kumuelewa hakuna mtu anaweza kumtetea, amebanwa hakuna njia nyingine isipokuwa Mungu mwenyewe aingilie kati na ndio maana wakati wote wanadamu wanapoteseka wakilia Mungu hawezi kuyapuuzia machozi yao, Machozi yana uwezo mkubwa sana wa kumvuta Mungu karibu, yana nguvu ya kumfanya Mungu kuingilia kati na kubadili mambo

Nguvu ya Machozi:


-          Machozi yana uwezo wa kumuokoa mtu na Mauti.

Biblia inaonyesha kuwa Mungu alimfufua Yesu siku ya tatu, kwa sababu aliomba, Mara kadhaa pia tunaona kuwa wako watu waliahirishiwa mauti yaani kifo kwa sababu walilia sana Waebrania 5:7Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;” Unaona Yesu Mwana wa Mungu aliomba, alifanya dua na aliiambatanisha na machozi na alisikilizwa na kufufuliwa siku ya tatu Mungu hakumuacha Kaburini aone uharibifu, kumbe maombi yana nguvu ya kuhairisha mauti, Katila injili ya Luka 7 tunaelezwa habari ya mjane mmoja katika mji wa Naini mjana huyu alikuwa na mtoto mmoja tu na mtoto huyo alikufa watu wengi sana walijitokeza kumfariji mjane yule na walikuwa tayari kushiriki mazishi ya kijana huyo wa pekee wa mwanamke mjane na bila shaka mjane yule inaonekana alilia sana, Maombi yake na kulia kwake kulimgusa sana Bwana Yesu na  kutokana na machozi yale Yesu alihairisha msiba ule ona Katika Luka 7:11-15 Baadaye kidogo alikwenda mpaka mji mmoja uitwao Naini, na wanafunzi wake walifuatana naye pamoja na mkutano mkubwa. Na alipolikaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, ni mwana pekee wa mamaye ambaye ni mjane, na watu wa mjini wengi walikuwa pamoja naye.  Bwana alipomwona alimwonea huruma, akamwambia, Usilie. Akakaribia, akaligusa jeneza; wale waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Inuka. Yule maiti akainuka, akaketi, akaanza kusema. Akampa mama yake.” Unawezaje kujua kuwa mwanamke yule mjane alikuwa analia ni neno moja tu la Yesu, Alimuonea huruma akamwambia “USILIE” ni kwa nini huruma za Mungu zilikuja juu ya mwanamke huyu mjane ni kwasababu yule alikuwa kijana wake wa pekee kwa hiyo msiba wake mama huyu mjane ulikuwa mkubwa sana moyoni mwake na hapa Yesu aliiahirisha mauti, tunapolia machozi Mungu huweza kutuokoa na mauti, ona vilevile yakwamba Mungu alimuongeza Hezekia miaka 15 ya maisha yake japo ni yeye aliye mtum anabii isaya akamtangazie kufa  Isaya 38:1-5Siku hizo Hezekia aliugua, akawa katika hatari ya kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, Bwana asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona. Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana, akasema, Ee Bwana, kumbuka haya, nakusihi, kwamba nimekwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana. Ikawa, neno la Bwana likamjia Isaya, kusema, Enenda ukamwambie Hezekia, Bwana, Mungu wa Daudi, baba yako, asema hivi, Mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama, nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano.” Katika namna ya kushangaza sana wote tunafahamu namna na jinsi Nabii Isaya alivyokua mkali na sirias na hapa Mungu alimtuma amwambie Hezekia ajiandae kufa Hezekia hakuwa na jinsi isipokuwa kumgeukia Mungu na tunaambiwa kua Hezekia AKALIA SANA SANA na vilevile tunaambiwa kuwa Mungu alimjibu kuwa amesikia maombi yake lakini AMEYAONA MACHOZI YAKE, hapa tena tunaona nguvu kubwa iliyomo katika machozi ikimkinga mtu na kifo, Kaka yangu na dada yangu, maombi yako yakiambatana na hisia kali na machozi kwa dhati kutoka moyoni Mungu huyaona na kuyafanyia kazi, usipende kulia tu bila kuambatanisha maombi yako na Machozi.

Aidha maandiko yanaonyesha kuwa Mauti ya rafiki wa Yesu aliyeitwa Lazaro iliahirishwa kwa sababu ya mtiririko wa machozi ya watu kadhaa yakiwemo ya Yesu Kristo mwenyewe ona Yohana 11:32-35,43-44 “Basi Mariamu alipofika pale alipokuwapo Yesu, na kumwona, alianguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. Basi Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana naye wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake, akasema, Mmemweka wapi? Wakamwambia, Bwana, njoo utazame. Yesu akalia machozi”. 43-44 “Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.


Eneo lingine ambalo tunaona Mungu akihairisha kifo kwa sababu ya machozzi ni pamoja na eneo ambalo Yona alimezwa na Nyangumi kwa ujumla hali hiii ni ngumu sana kuelezea namna ilivyokuwa sidhani kama mtu katika tumbo la nyangumi anaweza kuwa hai ukweli ni kuwa Mungu alimpa neema Yona katika Tumbo la Nyangumi angalau kusema maneno kadhaa ambayo yalimfanya Mungu amkumbuke na samaki akaona kuwa sio sahihi kumeza Yona na akamtapika Yona 2:1-6, 10Ndipo Yona akamwomba Bwana, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki, Akasema, Nalimlilia Bwana kwa sababu ya shida yangu, Naye akaniitikia; Katika tumbo la kuzimu naliomba, Nawe ukasikia sauti yangu. Maana ulinitupa vilindini, Ndani ya moyo wa bahari; Gharika ya maji ikanizunguka pande zote; Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu. Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako; Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu. Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu; Vilindi vilinizunguka; Mwani ulikizinga kichwa changu; Nalishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi na mapingo yake yalinifunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka shimoni, Ee Bwana, Mungu wangu,” 10 “Bwana akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani.”

               
-           Machozi yana nguvu ya kumfanya Mungu kushuka.


Biblia inaonyesha kuwa mara kadhaa vilevile watu walipopata shida za aina mbalimbali na mateso na wakalia, licha ya kuwa Mungu alisikia na licha ya kuwa Mungu yuko mahali kote Mungu vilevile hushuka na kujishughulisha na maisha ya watu wanaolia na kuugua kwa kusudi la kuleta msaada Kutoka 3:7-9BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa.” Unaweza kuona pia Katika Matendo 7:34Yakini nimeona mateso ya watu wangu waliomo Misri, nimesikia kuugua kwao, nami nimeshuka niwatoe. Basi sasa, nitakutuma mpaka Misri.” Mtu anapolia kwa kuugua Mungu huguswa kwa namna ya ajabu sana na hushuka kwaajili ya kutoa msaada husika Bwana na ampe neema kila mmoja wetu, kumlilia Mungu kila tunapokumbwa na maswaibu ya namna mbalimbali ili uwepo wake ushuke kuja kutusaidia.


-          Machozi humfanya Yesu ajifunue kwetu


Mara baada ya kufa kwa Yesu na kuzikwa siku ya tatu alfajiri na Mapema Wanawake wanaompenda Yesu walijihimu Kaburini bila shaka kwa kusudi la kuuhudumia mwili wa Bwana Yesu ili kuuhudumia usiharibika, katika namna ya kushangaza sana hawakuweza kuuona mwili huo na kwa vile Kaburi lilikuwa wazi na jiwe nlimeondolewa Mariam Magdalene alikata tamaa akijua kuwa mwili huo wa Bwana Yesu umeondolewa na kwa sababu alimpenda sana Yesu alilia kwa uchungu mkubwa sana  kwa sababu ya Machozi Yesu alijifunua kwake Yohana 20:11-15Lakini Mariamu alikuwa akisimama karibu na kaburi, nje yake, analia. Basi akilia hivi, aliinama na kuchungulia ndani ya kaburi. Akaona malaika wawili, wenye mavazi meupe, wameketi, mmoja kichwani na mmoja miguuni, hapo ulipolazwa mwili wake Yesu. Nao wakamwambia, Mama, unalilia nini? Akawaambia, Kwa sababu wamemwondoa Bwana wangu, wala mimi sijui walikomweka.  Naye akiisha kusema hayo, akageuka nyuma, akamwona Yesu amesimama, asijue ya kuwa ni Yesu. Yesu akamwambia, Mama, unalilia nini? Unamtafuta nani? Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa. Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, Raboni! (Yaani, Mwalimu wangu).  Unaona Malaika wa Mungu unapolia wanaguswa mno na Yesu alipoona Mariam analia alijifunua kwake, kumbe endapo tunataka Yesu ajifunue kwetu hatuna budu kuambatanisha Maombi yetu pamoja na kulia sana na Machozi na Bwana atatutokea katika maisha yetu!


-          Machozi hufanya Mungu akuone



Biblia inatuonyesha kuwa moja ya watu waliopitaia mateso ni Pamoja na Hajiri na Ishamel tangu akiwa tumboni, Lakini mara kadhaa Mungu alionyesha kujali kwa sababu ya machozi yao, Hajiri alipoteswa na Sarai alikimbia jangwani akiwa amekata tamaa, ukweli ulio wazi ni kuwa alikuwa analia, Mwanadamu anapolia au kutoa machizi maana yake amefikia kilele cha juu kabisa cha hisia zenye kuumiza na kuhitaji msaada, Mungu alimtokea Hajiri na kumthibitishia kuwa amesikia kilio cha Mateso yake ona

Mwanzo 16:6-13 “Naye Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake. Malaika wa BWANA akamwona kwenye chemchemi ya maji katika jangwa, chemchemi iliyoko katika njia ya kuendea Shuri. Akamwambia, Hajiri, wewe mjakazi wa Sarai, unatoka wapi, nawe unakwenda wapi? Akanena, Nakimbia mimi kutoka mbele ya bibi yangu Sarai.Malaika wa BWANA akamwambia, Rudi kwa bibi yako, ukanyenyekee chini ya mikono yake. Malaika wa BWANA akamwambia, Hakika nitauzidisha uzao wako, wala hautahesabika kwa jinsi utakavyokuwa mwingi. Malaika wa BWANA akamwambia, Tazama! Wewe una mimba, utazaa mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Ishmaeli, maana BWANA amesikia kilio cha mateso yako. Naye atakuwa kama punda-mwitu kati ya watu, mkono wake utakuwa juu ya watu wote na mkono wa watu wote utakuwa juu yake, naye atakaa mbele yao ndugu zake wote.  Akaliita jina la BWANA aliyesema naye, Wewe U Mungu uonaye, kwani alisema, Hata hapa nimemwona yeye anionaye?


Aidha Hajiri yuleyule akiwa sasa na kijana wake Ishmael walipofukuzwa na kuishia Jangwani maji yaliwaishia na Mama alijikuta anakata tamaa sana alimtupa mtoto chini ya kijimti, ili ikiwezekana asishuhudie mtoto huyo anavyokufa bila shaka Hajiri alipaza sauti alilia lakini vilevile Ishamel alilia sana jambo hili lilipelekea Mungu kusikia na kufanya muujiza wa kupatikana kwa maji. Unaweza kuona katika maandiko yafuatayo

Mwanzo 21:12-20 “Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa. Naye mwana wa mjakazi nitamfanya kuwa taifa, maana huyu naye ni uzao wako. Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba. Yale maji yakaisha katika kiriba, akamlaza kijana chini ya kijiti kimoja. Akaenda akakaa akimkabili, mbali naye kadiri ya mtupo wa mshale; maana alisema, Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, akapaza sauti yake, akalia. Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko. Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa. Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana. Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde.”


Hii maana yake ni nini? Neno la Mungu limejawa na shuhuda nyingi sana zinazoashiria kuwa Mungu atakutokea na kufanya muujiza, Mungu anaposikia mama analia, Mungu anachungulia anaposikia mtoto analia, Mungu husikia kilio cha mtu aliyekosa matumaini, maombi ya kulia humfanya Mungu kuona na kusikiliza haraka!


-          Machozi humfanya Mungu akukumbuke!



Ni muhimu kufahamu kuwa kibiblia neno kukumbuka maana yake ni “KUTOA KIPAUMBELE” first priority Neno hili kukumbuka kwa kiebrania maana yake ni “Zakar” to bring someone to mind and then act upon that person's behalf." Maana yake kuweka akilini na kushughulika naye kwa haraka kabla hajakata tamaa Neno hili limetumika katika Mwanzo 8:1Na Mungu akamkumbuka Nuhu, na kila kilicho hai, na wanyama wote waliokuwamo pamoja naye katika safina; Mungu akavumisha upepo juu ya nchi, maji yakapungua; “ na Mwanzo 30:22Mungu akamkumbuka Raheli; Mungu akamsikia, akamfungua tumbo.”  Sasa kwa kawaida kutokana na Maumbile ya wanadamu ni vigumu wanadamu kutoa kipaumbele kwa wanadamu wengine  ni vigumu wanadamu kukumbuka wenzao ona Mwanzo 40:14 “Ila unikumbuke mimi, utakapopata mema, ukanifanyie fadhili, nakuomba, ukanitaje kwa Farao, na kunitoa katika nyumba hii.”          Yusufu alijiombea neno hili kwa rafiki yake aliyemtafasiria ndoto kwa kumuomba amkumbuke hata hivyo baada yamafanikio rafiki yake Yusufu alimsahau Mwanzo 40:23 “Lakini huyo mkuu wa wanyweshaji hakumkumbuka Yusufu, alimsahausasa basi Mungu katika mpango wake hawezi kusahu yeye anasema mama anaweza kumsahau mtoto anayenyonya lakini Mungu hatakusahau wewe Isaya 49:15-16Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe. Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima. “ Kumbe Mungu hawezi kukusahau wajibu wetu sisi ni kumuomba tu atukumbuke aweke kipaumbele akuangalie Zaburi 106:4Ee Bwana, unikumbuke mimi, Kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako. Unijilie kwa wokovu wako”,                             

Moja ya jambo ambalo linaumiza sana katika jamii, ni Pamoja na kukosekana kwa uzao, hali hii katika biblia inatajwa kama sababu kubwa ya uchungu mkubwa kwa watu wengi hususani wanawake, katika jamii ya Israel utasa ulifikiriwa kama laana, ulifikiriwa kama hali ya kutokuwa na faida au kuzalisha, Hali hii ilimuumiza sana mwanamke aliyeitwa Hana ambaye alikuwa akisanifiwa na kuchokozwanamwanamke mwenzake mke mwenza kwa  sababu yeye alikuwa anazaa na Hana akuwa na mtoto, hali hii ilimuumiza sana Hana kiasi ambacho aliamua kuambatanisha maombi yake na machozi Biblia inaonyesha kuwa kutokana na maombi yake yaliyoambatana na machozi Munguhatimaye alimkumbuka na kumpa Mtoto aliyeitwa Samuel ambaye alikuja kuwa Nabii mkubwa, mwamuzi, kuhani na kiongozi mkubwa wa Taifa la Israel, maombi ya kulia machozi humfanya Mungu atukumbuke ona;-

1Samuel 1:5-10 “lakini Hana humpa sehemu mara mbili; maana alimpenda Hana, ingawa Bwana alikuwa amemfunga tumbo. Ila mwenzake humchokoza sana, hata kumsikitisha, kwa sababu Bwana alikuwa amemfunga tumbo. Tena mumewe akafanya hivyo mwaka kwa mwaka, hapo yule mwanamke alipokwea kwenda nyumbani kwa Bwana, ndivyo yule alivyomchokoza; basi, kwa hiyo, yeye akalia, asile chakula. Elkana mumewe akamwambia, Hana, unalilia nini? Kwani huli chakula? Kwa nini moyo wako una huzuni? Je! Mimi si bora kwako kuliko watoto kumi? Ndipo Hana akainuka, walipokwisha kula na kunywa huko Shilo. Naye Eli, kuhani, alikuwa akiketi kitini pake penye mwimo wa hekalu la Bwana. Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba Bwana akalia sana.”


1Samuel 1:19 “Wakaondoka asubuhi na mapema, wakasali mbele za Bwana, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye Bwana akamkumbuka.”


Unaona ndugu yangu Mungu hukumbuka machozi, huyahifadhi hayataachwa bure, machozi ni kama Damu machozi ni sadaka ya thamani sana yako mambo mengi sana duniani yanayoweza kutufanya tulie, wakati mwingine kwa sababu ya mawimbi ya maisha au kwa sababu ya matatizo na majanga sugu, yanayoyakumba maisha yetu, ndoa zisizo na amani, watoto wasiotii, kudhulumiwa, misiba isiyotarajiwa, na wakati mwingine tunaweza kulia hata pasipokujua sababu hii yote hutokana na uchungu wa maisha lakini kumbuka Mungu atayafuatilia machoziyako atayakumbuka

-          Machozi humfanya Mungu akuokoe na majanga.


Nabii Yona alikataa wito wa Mungu na kuamua kukimbilia Tarshish, kwa mujibu wa wanajiopgrafia Ninawi mji alikotumwa Yona ulikuwa ni katika nchi ya Syria au Iraq lakini mjia aliokuwa akikimbilia uko katika nchi ya Spain leo na unaambiwa kuwa alilipa Nauli, kutokana na kuukimbia uso wa Mungu safari ile ilikuwa na dhuruba nyingi mno na hivyo kiasi ambacho mabaharia walipata Hasara kubwa sana na kutupa shehena za mizigo ili kujaribu kujiokoa lakini dhuruba haikutulia waliamua kupiga kura ili kujua sababu na mtu aliyesababisha majanga yale na kura ilimuangukia Yona, kwa kweli hakukuwa na jinsi kwani ililazimu atupwe kilindini mwa bahari na mara akamezwa na Nyangumi, hii ilikuwa ni kama kifo kwa Yona ni kama alitumbukia kuzimu Yona alilia ndani ya tumbo la Nyangumi na Bwana akasema na Nyangumi yule na akamtapika Yona angalia.

Yona 2:1-10 “Ndipo Yona akamwomba Bwana, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki, Akasema, Nalimlilia Bwana kwa sababu ya shida yangu, Naye akaniitikia; Katika tumbo la kuzimu naliomba, Nawe ukasikia sauti yangu. Maana ulinitupa vilindini, Ndani ya moyo wa bahari; Gharika ya maji ikanizunguka pande zote; Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu. Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako; Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu. Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu; Vilindi vilinizunguka; Mwani ulikizinga kichwa changu; Nalishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi na mapingo yake yalinifunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka shimoni, Ee Bwana, Mungu wangu, Roho yangu ilipozimia ndani yangu, Nalimkumbuka Bwana; Maombi yangu yakakuwasilia, Katika hekalu lako takatifu. Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongo Hujitenga na rehema zao wenyewe; Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa Bwana. Bwana akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani.”



-          Machozi yanaleta wokovu  na Neema na huruma za Mungu


Kitabu cha waamuzi ni moja ya mfano wa watu walioteseka sana wakati wa mpito wa uongozi kutoka yoshua mpaka mfalme wa Kwanza Israel walikuwa na viongozi walioteuliwa na Mungu kuwaamua viongozi hao waliitwa kuwaokoa pale walipomlilia na kumuomba kutokana na mateso waliyokuwa wakiyapitia, Mungu alileta neema wokovu na msaada kutokana na israel kumlilia Mungu, ni wazi kuwa tunapopitia aina mbalimbali za majaribu na mapito kisha tu7kamkumbuka Mungu na kumlilia mara moja Bwana ataonyesha uwezo wake kwetu na kutuhurumia na kutupa msaada kama alivyofanya nyakati za waamuzi

Waamuzi 3:14-15 “Wana wa Israeli walimtumikia Egloni mfalme wa Moabu muda wa miaka kumi na minane.Lakini wana wa Israeli walipomlilia Bwana, Bwana akawainulia mwokozi, Ehudi, mwana wa Gera, Mbenyamini, mtu aliyekuwa mwenye shoto; nao wana wa Israeli walimpelekea Egloni mfalme wa Moabu tunu mkononi mwa huyo Ehudi.

     
Waamuzi6:6-14 ”Israeli walitwezwa sana kwa sababu ya Wamidiani; nao wana wa Israeli wakamlilia Bwana. Kisha ikawa, hapo wana wa Israeli walipomlilia Bwana kwa sababu ya Midiani, Bwana akamtuma nabii aende kwa hao wana wa Israeli; naye akawaambia, Bwana, yeye Mungu wa Israeli, asema hivi, Mimi niliwaleta ninyi mkwee kutoka Misri, nikawatoa katika nyumba ya utumwa; nami niliwaokoa na mikono ya Wamisri, na mikono ya wote waliokuwa wakiwaonea, nami niliwafukuza watoke mbele zenu, nami niliwapa ninyi nchi yao; kisha niliwaambia, Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu; msiiche miungu ya Waamori, ambayo mwaketi katika nchi yao; lakini hamkuitii sauti yangu. Malaika wa Bwana akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani. Malaika wa Bwana akamtokea, akamwambia, Bwana yu pamoja nawe, Ee shujaa. Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa Bwana yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyotuhadithia baba zetu, wakisema, Je! Siye Bwana, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani.Bwana akamtazama, akasema, Enenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli na mkono wa Midiani. Je! Si mimi ninayekutuma?“


Mashujaa wa machozi.


Machozi yanaashiria upendo mkubwa na uchungu alionao mtu wakati mwingine kutokana na mateso au aina ya mapito waliyopitia, jamii kubwa sana ya watu wa zamani walikuwa na tabia ya kusalimiana na kupeana taarifa kwa zamu na kisha kila walipopeana taarifa kuhusu mtu fulani aidha aliumwa au alikufa au wamefarakana muda mrefu walikatika maongezi nhayo na kulia Jambo hili lilionyesha nupendo na kujali kuliko kukubwa sana , upweke na mateso waliyonayo wanadamu unaweza kuwafanya wao kulia sana Katika biblia wako watu wengi sana walilia na kisha Mungu baadaye aliyabadilisha maisha yao

Shujaa wa kwanza wa machozi alikuwa Yusufu


Ona katiika maandiko mkadhaa akitajwa kama mtu aliyelia mara kwa mara kulia kwake kuliashiria kujali na upendo aliokuwanao kwa ndugu zake na jamaa zake na baba yake na wana wa baba yake, kwanza maisha yake ya kupotea Huko Misri yalisababisha baba yake kumlilia siku zakeo zote akikataa kufarijiwa kwa sababu alikuwa ni mwana wake aliyempenda angalia Mwanzo 37:34-35Yakobo akararua mavazi yake, akajivika gunia viunoni, na kumlilia mwanawe siku nyingi. Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba yake akamlilia.” Uaona kutokana na upendo Yakobo aliokuwa nao kwa Yusufu Biblia inaonyesha ya kuwa babaye alimlilia siku nyingi kwa nini kwa sababu alikuwa ni mwana mwenye utii mwenye kupendeza mwenye heshima na adamu na mwaminifu kwa babaye na aliyekuwa na maono makubwa kwaajili ya familia yake, Maisha yake yaliyokuwa yamejaa upedno yalisababisha na yeye kuwa mtu wa machozi mara kwa mara hasa kwaajili ya ndugu zake Mwanzo 42:24 “Akajitenga nao akalia. Kisha akawarudia, na kusema nao, akamtwaa Simeoni miongoni mwao, akamfunga mbele ya macho yao.” Mwanzo 43:30 “Yusufu akafanya haraka, kwa sababu moyo wake ulimwonea shauku nduguye, akatafuta pa kulia, akaingia chumbani mwake, akalia humo. Akanawa uso, akatoka, akajizuia, akasema, Leteni chakula.” Mwanzo 45:2 “Hapo Yusufu hakuweza kujizuia mbele yao wote waliosimama karibu naye. Akapiga kelele, na kusema, Mwondoeni kila mtu mbele yangu. Wala hakusimama mtu pamoja naye, Yusufu alipojitambulisha kwa nduguze. Akapaza sauti yake akalia, nao Wamisri wakasikia. Watu wa nyumba ya Farao nao wakasikia.” Mwanzo 45:14-15 “Akaanguka shingoni mwa ndugu yake Benyamini, akalia; Benyamini naye akalia shingoni mwake. Akawabusu ndugu zake wote, akalia nao, baada ya hayo, nduguze wakazungumza naye”     Mwanzo 46:29-30Yusufu akatandika gari lake, akapanda kwenda kumlaki Israeli, babaye, huko Gosheni; akajionyesha kwake, akamwangukia shingoni, akalia shingoni mwake kitambo kizima. Israeli akamwambia Yusufu, Na nife sasa, kwa kuwa nimekuona uso wako, ya kuwa ungali hai.” Mwanzo 50:1-6 “Yusufu akamwangukia babaye usoni, akamlilila, akambusu.  Yusufu akawaagiza watumishi wake waganga, kwamba wampake baba yake dawa asioze. Waganga wakampaka dawa Israeli.  Siku zake arobaini zikaisha, maana hivyo hutimizwa siku za kupaka dawa. Wamisri wakamlilia siku sabini. Siku za kumlilia zilipopita, Yusufu alisema na watu wa nyumba ya Farao, akinena, Kama nimeona neema machoni penu, tafadhalini mkaseme masikioni mwa Farao, mkinena, Baba yangu aliniapisha, akisema, Mimi ni katika kufa, unizike katika kaburi langu nililojichimbia katika nchi ya Kanaani. Basi tafadhali uniruhusu niende sasa nikamzike babangu, nami nitarudi. Farao akasema, Uende, ukamzike baba yako, kama alivyokuapishaMwanzo 50:17 “Mwambieni Yusufu hivi, Naomba uwaachilie ndugu zako kosa lao na dhambi yao, maana walikutenda mabaya; sasa twakuomba utuachilie kosa la watumwa wa Mungu wa baba yako. Yusufu akalia waliposema naye.” Maisha ya Yusufu yalijaa machozi alikuwa mtu wa machozi pamoja na mafanikio makubwa na heshima kubwa aliyokuwa nayo machozi yaliambatana na maisha yake lakini wakati wote maisha ya machozi ya Yusufu yalikuwa na muunganiko kuhusu Ndugu zake upendo wake kwa Israel .

Shujaa mwingine wa kulia ni Daudi.


Daudi ndiye shujaa wa juu bzaidi nkatika swala la kulia machozi yeye alimujuanmUngu vema sana kwa sababu hiyo mara nyingi katika dua na maombi yake alilia sana na machozi utaweza kugundua njambo hili unapopata nafasi ya kuzipitia zaburi mbalimbali Mwenyewe anasema Zaburi 6:6-9 “ Nimechoka kwa kuugua kwangu; Kila usiku nakieleza kitanda changu; Nalilowesha godoro langu kwa machozi yangu. Jicho langu limeharibika kwa masumbufu, Na kuchakaa kwa sababu yao wanaoniudhi. Ondokeni kwangu, ninyi nyote mtendao uovu; Kwa kuwa Bwana ameisikia sauti ya kilio changu. Bwana ameisikia dua yangu; Bwana atayatakabali maombi yangu.” Unaweza kuona pia katika Zaburi 69:3 “. Nimechoka kwa kulia kwangu, Koo yangu imekauka. Macho yangu yamedhoofu Kwa kumngoja Mungu wangu.” Ni kupitia machozi Daudi alimlilia Mungu na kumuimbia zaburi kadhaa wa kadhaa, ushaujaa wa Daudi na uanajeshi wake haukumfanya asiwe mwenye kuklia mbele za Mungu wake maombia yake na dua zake zilijawa na machozi ni machozi pekee yanayoweza kutuinua juu, kwani machozi ni Ishara ya kushuka kwetu chini nana kuinyesha namna na jinsi tunavyomuhitaji Mungu, Na Mungu kamwe hatakuja ayadaharu machozi yetu, Hisia zetu ni sehemu kamili ya hali zetu za kiroho pia na zinaweza kutumika katika maombi na kuabudu, ni shara ya kuwa tunaweza kuzama ndani nzaidi na kujielezea na kujipambanua kwa Mungu wetu, Mungu huyaiona machozi yetu na anasukumwa kufanya jambo, na siku moja atayafuta machozi yetu yote kwa hiyo hatupaswi kuona aibu kulia lakini tuyatoe machozi yetu kwa imani na Mungu atayageuza machozi yetu kuwa kichezo.

1Samuel 20:41 Basi mara alipokuwa amekwisha ondoka yule mtoto, mara Daudi akatoka mahali pale karibu na kile kichuguu, akaanguka kifudifudi, akajiinama mara tatu; nao wakabusiana, wakaliliana, hata Daudi akazidi.” Daudi alikuwa na upendio wa ajabu sana yeye a rafiki yake Yionatahan walipokuwa wakiagana walilia lakini Daudi alilia zaidi

1Samuel 24:12-16 “Bwana atuamue, mimi na wewe, na Bwana anilipizie kisasi changu kwako; lakini mkono wangu hautakuwa juu yako.Kama vile walivyosema watu wa kale katika mithali yao, Katika waovu hutoka uovu; ila mkono wangu hautakuwa juu yako. Na mfalme wa Israeli ametoka ili kumfuatia nani? Unamwinda nani? Ni kuwinda mbwa mfu, au kiroboto. Basi Bwana atuamue, akatuhukumu mimi na wewe, akaone, akanitetee neno langu, akaniokoe na mkono wako. Ikawa, Daudi alipokwisha kumwambia Sauli maneno hayo Sauli alisema, Hii ndiyo sauti yako, Daudi, mwanangu? Naye Sauli akapaza sauti yake, akalia.” Daudi alikuwa na uwezo wa kujieleza na kusimamia haki katika kiwango ambacho kingeweza kumfanya mtu alie machozi Sauli alilia kwa sababu Daudi alikuwa amemueleza ukweli kile ambacho angewza kumfanyia lakini alikuwa amemuachia Mungu aingilie kati uadui wao.

1Samuel 30:1-8Ikawa, Daudi na watu wake walipokuwa wamefika Siklagi siku ya tatu, hao Waamaleki walikuwa wameshambulia Negebu, na Siklagi, nao wameupiga Siklagi, na kuuchoma moto; nao wamewachukua mateka wanawake waliokuwamo wakubwa kwa wadogo; hawakuwaua wo wote, ila wakawachukua, wakaenda zao. Basi Daudi na watu wake walipoufikilia mji, tazama, ulikuwa umechomwa moto; na wake zao, na watoto wao, waume kwa wake, wamechukuliwa mateka. Ndipo Daudi na watu waliokuwa pamoja naye wakainua sauti zao na kulia, hata walipokuwa hawana nguvu za kulia tena. Na hao wake wawili wa Daudi walikuwa wamechukuliwa mateka, Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili, aliyekuwa mkewe Nabali, wa Karmeli. Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana nafsi za hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi alijitia nguvu katika Bwana, Mungu wake. Kisha Daudi akamwambia Abiathari, kuhani, mwana wa Ahimeleki, Tafadhali niletee hapa hiyo naivera. Naye Abiathari akamletea Daudi naivera huko. Daudi akauliza kwa Bwana, akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote.”  Daudi alipopatwa na fadhaa alilia lakini npia alimuomba Mungu na kupata suluhu ya mahitaji yake alijua umuhimu wa Machozi kama atayaunganisjha na maombi alijitia nguvu na Mungu alimsikia na kujibu maombi yake

Daudi alilia sana siku alipokufa Sauli na Yonathan  na kufunga kwaajili ya kuomboleza

2Samuel 1:11-12 “Ndipo Daudi akashika nguo zake akazirarua na kadhalika watu wote waliokuwa pamoja naye; wakaomboleza, wakalia, wakafunga hata jioni, kwa ajili ya Sauli, na kwa ajili ya Yonathani mwanawe, na kwa ajili ya watu wa Bwana na kwa ajili ya nyumba ya Israeli; kwa sababu wameanguka kwa upanga.”
   
           
Daudi alilia machozi siku alipokufa Abneri 2Samuel 3:31-33Kisha Daudi alimwambia Yoabu, na watu wote waliokuwa pamoja naye, Rarueni nguo zenu, mkajivike nguo za magunia, mkamlilie Abneri. Naye mfalme Daudi akaifuata jeneza. Wakamzika Abneri katika Hebroni; naye mfalme akapaza sauti yake, akalia kaburini kwa Abneri, nao watu wote wakalia. Ndipo mfalme akamwomboleza Abneri, akasema, Ilimpasaje Abneri kufa afavyo mpumbavu?

Daudi alilia machozi alipokuwa akipambana kivita na mwanae Absalom na Mungu alisikia dua yake  2Samuel 15:30Daudi akapanda akishika njia ya kuupandia mlima wa Mizeituni, akilia alipokuwa akipanda; naye alikuwa amejifunika kichwa chake, akaenda hana viatu; na watu wote waliokuwa pamoja naye wakajifunika vichwa vyao, kila mmoja wao, wakapanda juu, wakilia walipopanda”.   

  
Daudi alilia vilevile aliposikia ya kuwa mwanae amefariki

2Samuel 18: 33Naye mfalme akataabika sana, akapanda juu, akaingia kile chumba kilichokuwa juu ya lango, akalia; na katika kwenda kwake alisema hivi, Mwanangu Absalomu! Ee mwanangu! Mwanangu Absalomu! Laiti ningalikufa badala yako, Absalomu, mwanangu, mwanangu!

Lia kwa Mujibu wa Kanuni za Mungu


Kama ukikiuka kanuni za kimungu kisha ukalia tu kuna aina za kilio Mungu hatasikiliza mfano Esau aliuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kisha baadaye akaanza kuulilia Mungu hakumsikiliza, Kwa sababu Mungu alikuwa ni shahidi wa Mwanzo 27:34-35Esau aliposikia maneno ya babaye, akalia kilio kikubwa cha uchungu sana, akamwambia babaye, Nibariki na mimi, mimi nami, Ee babangu. Akasema, Nduguyo amekuja kwa hila, akauchukua mbaraka wako”. Esau alikuwa maeuza urithi wake wa mzazliwa wake wa kwanza na alimuapia Yakobo kwa Mungu hivyo Mungu alikuwa ni shahidi wa kile alichokifanya hivyo kilio cha Esau kilikuwa kiko na kinyume na maswala ya haki kwa kile alichokifanya, aidha kama tutadumu sana katika dhambi na kuwa na tabia ya kurudia rudia makosa yale yale unaweza ukafika wakati Waamuzi 10:10-16 ”Ndipo wana wa Israeli wakamlilia Bwana, wakisema, Sisi tumekufanyia dhambi, kwa sababu tumemwacha Mungu wetu, na kuyatumikia Mabaali. Naye Bwana akawaambia wana wa Israeli, Je! Sikuwaokoa ninyi na hao Wamisri, na Waamori, na wana wa Amoni, na Wafilisti? Hao Wasidoni nao, na Waamaleki, na Wamaoni, waliwaonea, nanyi mlinililia, nami niliwaokoa na mikono yao. Lakini mmeniacha mimi, na kuitumikia miungu mingine; basi kwa ajili ya hayo mimi sitawaokoa tena. Haya, endeni mkaililie hiyo miungu mliyoichagua; na hiyo iwaokoe wakati wa kusumbuka kwenu.  Wana wa Israeli wakamwambia Bwana Tumefanya dhambi; utufanyie yote uyaonayo kuwa ni mema; lakini tuokoe, twakusihi, siku hii ya leo, haya tu. Nao wakaiondoa hiyo miungu ya kigeni iliyokuwa kati yao, nao wakamtumikia Bwana; na roho yake ilihuzunika kwa sababu ya msiba wa Israeli.” Kama tunataka kumuona Mungu katika maisha yetu kupitia machozi yetu ambayo Mungu huyaheshimu sana ni lazima tuhakikishe kuwa tunalia katika kanuni za Mungu yaani tutubu na kuyaacha makosa yetu na kukaa katika kanuni zake kisha yanapoibuka maswala magumu na kuliitia jina la Mungu, Mungu ataonekana katika maisha yetu na kututokea na ile nguvu ya machozi tutaiona waziwazi.


Siri iliyofichikakatika machozi.

Mungu hatakuja kuyadgarau machozi yetu tunapougua Zaburi 51:17Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.”
 Mwisho wa Machozi:
Ufunuo 21:4-5Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.”
Na Rev, Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima