Jumamosi, 30 Oktoba 2021

Chuma hunoa chuma!

Mithali 27:17 “Chuma hunoa chuma; Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake


Utangulizi:

Chuma hunoa chuma ni moja ya andiko maarufu na lenye hekima sana katika utumishi tulioitiwa hapa duniani, biblia ya Kiswahili inatumia neno chuma hunoa chuma ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake lakini katika kiingereza andiko hilo linasomeka “As Iron sharpens Iron, so one person sharpens another”, kwa hiyo tungeweza kusema hivi kwa lugha ya Kiswahili changu kama chuma kinavyonoa chuma ndivyo ilivyo kwa kila mtu na jirani yake.

Usemi huu unatusaidia kujitambua kuwa tunategemeana na hakuna mtu anaweza kutoboa peke yake, yaani ili kwamba wewe uweze kuwa mtu mwema zaidi, unaweza kuwa mzuri zaidi kwa kuwafanya wengine kuwa wazuri zaidi.  Au unaweza kuwa mzuri zaidi kwa kujifunza kutoka kwa wengine, sisi peke yetu hatutoshi, lakini tuko hivi tulivyo kwa sababu tulijifunza kutoka kwa wengine, tulikubali kuongozwa, na tulipokea hekima na maonyo kutoka kwa wengine, Biblia inasema enenda pamoja na wenye hekima nawe utakuwa na hiyo hekima! Ona

Mithali 13:20Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.”

Chuma kunoa chuma katika hali ya kawaida maana yake kuna manufaa ya ajabu sana inapotokea vyuma vikasuguana kwa pamoja, inatengeneza makali ambayo yana uwezo mkubwa sana wa kukata kitu kwa urahisi, chuma kinaweza kubaki na makali yake ya kawaida, na kikapoteza ufanisi au kubaki hali ileile kwa utendaji uleule au kuwa butu, lakini kinaponolewa  au kugongwa na chuma kingine kinakuwa tofauti kabisa, kwa msingi huo kwa kadiri chuma hicho kinavyozidi kunolewa au kugongwa au kufuliwa ndio kinavyozidi kuwa na makali zaidi, chuma hunoa chuma humaanisha au inamaanisha ni kumchonga mtu kitabia, mwenendo, maisha, kitaaluma, kihekima, uzoefu na kadhalika, kwa msingi huo kunakuwa na faida pande zote mbili na matokeo yake ni kuwa pande zote mbili huwa kali na hatimaye wote hufanya vizuri katika kazi zao, kama ni kukatua au kukata vitu vipande vipande.  Au kufanikisha wajibu ule uliokusudiwa na mwenye chuma. Mwanadamu hakuumbwa awe peke yake tunasema kwa kiingereza “human being is a social being” kwa hiyo tunahitajiana katika mazingira mbalimbali ili tuweze kufika

Mwanzo 2:18 “BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.”

Wataalamu wa Elimu ya jamii katika ukristo Christian sociology wanakubaliana kuwa andiko hilo licha ya kuwa kwaasili lilimuhusu Adam na Eva, lakini kwa upana linahusu ile hali ya mty kuwa peke yake haikuwa njema katika uumbaji wa Mungu, na kuwa Mungu aliona kuwa mtu anahitaji watu, wenzake wengine, na ndio maana aliwabariki ili waongezeke na kuitawala Dunia so its absolutely that human being is a social being

Na ndio maana nyakati za kanisa la kwanza walionywa kutokuacha kukusanyika ili watu waendelee kuonyana kwa kadiri siku ile ilivyokuwa inakaribia, tunaweza kusali peke yetum, tunaweza kumuabudu Munghu tukiwa wenyewe lakini kwanini tunahitaji kwenda ibadani kwanini tunahitaji kujumuika na wenzetu katika ibada kwa sababu tunahitajiana pia hata kama tumeokolewa

 Waebrania 10:24-25 “tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri; wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.”

Kwa msingi huo basi jni wazi kuwa usemi huu chuma hunoa chuma unamaana pana sana kwetu na kwa jamii nzima na kuna mambo mengi mno ya kujifunza tunayoweza kuyapata kutokana na usemi huu kama ifuatavyo:-

1.       Chuma hunoa chuma ni usemi unaotufundisha kuwa na umoja

 

Tumeona kuwa usemi unasema chuma hunoa chuma ina maana ya pia mtu wa aina Fulani anaweza kumsaidia au kusaidiwa au kusaidiana na mwingine kuwa wa aina Fulani kwa hiyo kanuni hii ya biblia inatufundisha nguvu ya umoja katika kanuni za kiroho umoja una nguvu sana, biblia inaeleza wazi kuwa umoja ni wa thamani sana popote pale unapotaka mafanikio kama ni ya kitaasisi au serikali au taifa lazima kwanza watu wawe na umoja hilo ni la msingi sana.

 

Muhubiri 4:9-10 “Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao. Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!

 

Maandiko yanaonyesha kuwa ni afadhali au ni heri kuwa wawili kwa sababu kuna kuinuliwa kuliko mtu akiwa peke yake, lakini kazi yao pia huwa kubwa kuliko kazi ya mtu mmoja sio hivyo tu, watu wapoomba wakiwa wawili au watatu Mungu hufanya au hujibu maombi yao kwa urahisi zaidi kwa msingi huo umoja au kuwa zaidi ya mmoja kuna uwepesi unaoweza kupatikana kwa kusaidiana na kwa kutegemeana na kwa kuwekana sawa na kuna faida kubwa sana za kimwili, kiroho, kiuchumi, kisaikolojia, kisiasa, na kijamaa na kadhalika

 

Mathayo 18:19-20 “Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.”

 

Maombi ya watu wawili waliopatana yana nguvu kubwa sana na Mungu huyajibu lakini sio hivyo tu Mungu anakuwepo katikati ya watu wanapokusanyika kwa jina lake, maandiko yanasema watu wanapokaa kwa umoja Mungu huachilia upako wake kwa namna ya kushangaza kutoka kwa kluhani mkuu Yesu Kristo

 

Zaburi 133:1-3 “Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja. Ni kama mafuta mazuri kichwani, Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni, Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake. Kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana ndiko Bwana alikoamuru baraka, Naam, uzima hata milele.” 

 

Kwa hiyo katika ulimwengu war oho Mungu anafahamu sana umuhimu wa umoja, kama kuna jambo mojawapo muhimu ambalo Yesu aliliombea kanisa na wanafunzi wake ni kuwa na umoja ona

 

Yohana 17:20-22 “Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.”

 

Hakuna taasisi yoyote ile inayoweza kusimama kama tasisi hiyo haina umoja, shetani anajua kuwa ili aweze kuwaharibia watu atamwaga roho ya mafarakano ili kuwe na makundi nah ii ndio dalili mbaya sana ya kuanguka kwa taasisi au taifa au hata ndoa.ni pale umoja unapokuwa umeondoka. Lazima tuwe na nia moja, tupendane inapotokea kila mtu anaangalia maslahi yake, moyo wa ubinafsi na kujiona bora kuliko wengine hapo ndipo mambo huanza kuharibika

 

Wafilipi 2:1-4 “Basi ikiwako faraja yo yote katika Kristo, yakiwako matulizo yo yote ya mapenzi, ukiwako ushirika wo wote wa Roho, ikiwako huruma yo yote na rehema, ijalizeni furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkinia mamoja.Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine

 

kwa msingi huo kanuni ya chuma kunoa chuma ina maanisha kuwa na umoja kushikamana kwa nyenzo zinazofanana ili kujenga na kufanikisha kazi ya Mungu au ujenzi wa jamii au taifa kwa mshikamano unaokubaliana na kuelekezana, kwa msingi huo kujitenga na jamii au kutiokukubali kuchangamana na wenzako kunaweza kuwa na mchango mbaya sana katika makuzi na ufanisi wa mtu mmoja mmoja.

 

2.       Chuma hunoa chuma ni usemi unaotufundisha pia kutoambatana na watu wenye tabia mbaya.

 

Chuma hunoa chuma ni msemo pia unaotufundisha kuambatana na watu wenye tabia njema

1Wakoritho 15:33  Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.” Ni vema kuuangalia mstari huu kwa kiingereza unasema hivi 1Corinthians 15:33 “Do not be misled, Bad Company corrupts good characterusemi huu umetokana na usemi wa kiyunani unaotafasirika hivi  “DO NOT BE FOOLED, DECEIVED, MISLED, BAD FRIEND, COMPANY WILL RUIN GOOD HABITS, OR CHARACTER, OR MORALS, Imenukuliwa kutoka katika mashairi ya zamani sana ya kigiriki kati ya mwaka 342-291 KK., Yaani kama chuma hunoa chuma basi chuma hicho vilevile kikiwa kiovu kitakufanya uwe muovu zaidi, kwa msingi huo maandiko yanatufundisha kujihadhari na watu waovu, au kuacha kuwa na mahusianio na watu wabaya, huwezi kuwa na tabia njema kama u nashikamana na watu wenye tabia mbaya mafundishio ya yesu Kristo ya na ukatili mikubw zaidi wakati masihi alipokuwa akitahadharisha mambo ya kukosesha

 

Mathayo 18:7-9 “Ole ni wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana budi kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake mtu yule aliletaye jambo la kukosesha! Basi mkono wako au mguu wako ukikukosesha, ukate ukautupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima hali umepungukiwa na mkono au mguu, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na kutupwa katika moto wa milele. Na jicho lako likikukosesha, ling'oe, ukalitupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum ya moto.”

 

Yesu alitumia maneno haya kumaanisha kuvunja uhusiano na mtu anayesababisha wewe ukosee, anazungumzia kuacha kuambatana na watu waovu wanaokuharibia ambao badala ya kukunoa uwe mzuri wanakunoa uwe mbaya, badala ya kukuongoza katika mkema wanakuongoza kufanya uovu, utaharibikiwa lugha ya Paulo mtume inanyoosha pia moja kwa moja katika tahadhari ya swala hili ona

 

2Wakoritho 6:14-18 “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,”

 

maandiko yako wazi na yanatutaka tuwe makini na wale tunaoambatana nao, wana ushawishi wa ina gani je ni chuma cha aina gani usije ukanolewa kuwa muovu zaidi hivyo ni muhimu ukawa makini na kuchagua mtu wa kuambatana naye asiwe mvuta bangi, asiyetumia madawa ya kulevya, walevi, wazinzi, makahaba, majambazi, wezi, waongo, matepeli, watu wa misheni town, wenye tama, wasengenyaji, watukanajim  wasagaji, mashoga, wavuta sigara, waasi maandiko yanatuasa kuachana na makutano wa aina hii hawa tukiambatana nao watatunoa na tutakuwa waovu zaidi, Musa anasema mtu akikushawishi katika uovu muue

 

Kumbukumbu la Torati 13:6-10 “Atakapokushawishi kwa siri ndugu yako, mwana wa mamaako, au mwana wako, au binti yako, au mke wa kifuani mwako, au rafiki yako aliye kama moyo wako, akikuambia, Twende tukaabudu miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako; katika miungu ya mataifa yaliyo kando-kando yenu karibu nawe au mbali nawe, tokea ncha moja ya dunia hata ncha ya pili ya dunia; usimkubalie wala usimsikize; wala jicho lako lisimwonee huruma, wala usimwache, wala usimfiche;mwue kweli; mkono wako na uwe wa kwanza juu yake katika kumwua, na baadaye mikono ya watu wote. Nawe mtupie mawe hata afe; kwa kuwa alitaka kukupotoa na Bwana, Mungu wako aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.”

 

Maandiko yanatuonya kuacha kuandamana na mkutano katika kutenda maovu, kwa sababu hiyo hata kama utaona kuwa kuna kundi au watu wanakusudia kufanya jambo baya ni muhimu wewe ukajihadhari kama lengo la umoja wao ni kwenda kufanya maovu, pima wewe mwenyewe lolote lile iwe ni maandamanio, migomo uasi au lolote ambalo unaona liko kinyume na Mapenzi ya Mungu au neno lake wewe usiambatane nao hata kama wako wengi

 

Kutoka 23:2 “Usiandamane na mkutano kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lo lote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotoa hukumu;”  

 

Neno la Mungu liko makini sana kuhusu kuambukizwa kutenda uovu, na lina msimamo mkalisana kuhusu kujiunga na jamii isiyotaka kutenda mema, kwa msingi huo kama ni chuma hunoa chuma basi kama chuma hicho ni cha uovu waovu hunoa waovu wenzao na hivyo utakua uemambatana na wapumbavu na wala sio wenye hekima na biblia inaonyesha matokeo kuwa utaumia.     

 

3.       Chuma hunoa chuma ni usemi unatufundisha kuwa na tabia ya kutiana moyo.

 

Chuma hunoa chuma maana yake pia kuna watu wanaoweza kututia moyo, tunachohitaji sisi ni kutiwa moyo, kuna watu wakitiwa moyo tu wanafanya vizuri chuma hunoa chuma humaanisha ni kupata mtu anayeweza kujua hali yako na ni nini unachohitaji kukifanya kisha akakutia moyo kufanya vizuri, Mungu mwenyewe amefanya kazi ya kututia moyo kwa neno lake akitutaka tusigope kabisa anajua kuwa wako watu wakitiwa moyo hufanya vizuri. imani yao hupanda na Mungu ametuhakikishia ushindi mkubwa usiokuwa wa kawaida watu wanapotiwa moyo ona mifano ya kutiana moyo katika maandiko:-

 

Isaya 41:6-13 “Wakasaidiana, kila mtu na mwenzake, kila mtu akamwambia ndugu yake; Uwe na moyo mkuu. Seremala akamtia moyo mfua dhahabu, na yeye alainishaye kwa nyundo akamhimiza yule apigaye fuawe, akiisifu kazi ya kuunga, akisema, Ni kazi njema; naye akaikaza kwa misumari isitikisike. Nawe, Israeli, mtumishi wangu; Yakobo, niliyekuchagua; mzao wa Ibrahimu, rafiki yangu;  wewe niliyekushika toka miisho ya dunia, na kukuita toka pembe zake, nikikuambia, Wewe u mtumishi wangu; nimekuchagua wala sikukutupa; usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. Tazama, wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia. Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa kama kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako. Kwa maana mimi, Bwana, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia.”

 

Wakati mwingine sio tu kungoja kutiwa moyo lakini unaweza kujitia moyo mwenyewe kama chuma kwelikweli kwa kuuthibitishia ulimwengu kuwa wewe sio dhaifu na wewe ni hodari jikabidhi kwa Mungu na Bwana Mungu yeye hatajali hata kama uko peke yako atakusaidia yeye ni sehemu yetu ya kujitia moyo hivyo wakati unapokuwa katika halia inayokuhusu wewe pekee hakikisha kuwa unajitia moyo mwenyewe .

 

Yoeli 3:9-10 “Tangazeni haya kati ya mataifa; takaseni vita; waamsheni mashujaa; watu wa vita na wakaribie; na wapande juu. Yafueni majembe yenu yawe panga, na miundu yenu iwe mikuki; aliye dhaifu na aseme, Mimi ni hodari.”

 

Watu wawapo duniani wanahitaji kutiwa moyo, ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa tunawatia moyo wengine, lakini wako watu ambao kazi yao ni kuvunja moyo, lakini usikubali kwa namna yoyote ile kuvunjika moyo Maandiko yanatutaka pia tujitie moyo, ukijitia moyo mwenyewe unakuwa chuma na baadaye utawasaidia watu wanaovunjika moyo!

 

Nehemia alipokuwa anaujenga ukuta wa Yerusalem alikutana na changamoto za wapinzani ambao walikuwa ni wakatishaji tamaa na walikuwa wanatoa maneno ya kejeli kuhusiana na ukuta wa jiji la Yerusalem alilokuwa analijenga Nehemia kama msimamizi, ni ukweli usiopingika kuwa kama Nehemia hangekuwa shupavu yeye angekata tama na hivyo watu wengine neo wangekata tama! Ona

 

 Nehemia 4:1-3 “Lakini ikawa, Sanbalati aliposikia ya kwamba tulikuwa tukiujenga ukuta, akaghadhibika, akaingiwa na uchungu sana, akawadhihaki Wayahudi. Akanena mbele ya nduguze na mbele ya jeshi la Samaria, akisema, Wayahudi hawa wanyonge wanafanyaje? Je! Watajifanyizia boma? Watatoa dhabihu? Au watamaliza katika siku moja? Je! Watayafufua mawe katika chungu hizi za kifusi, nayo yameteketezwa kwa moto? Basi Tobia, Mwamoni, alikuwa karibu naye, akasema, Hata hiki wanachokijenga, angepanda mbweha, angeubomoa ukuta wao wa mawe.”

 

Nehemia alitishiwa na hata kutumiwa manabii wa uongo, lakini hata hivyo hakukata tama na matokeo yake kazi ilisonga mbele kupitia yeye na wale aliokuwa akiwaongoza ona matisho aliyokutana nayo na namna alivyoweza kustahimili:-

 

Nehemia 6:11-13 “Nami nikasema, Je! Mtu kama mimi nikimbie? Naye ni nani, akiwa kama nilivyo mimi, atakayeingia hekaluni ili kuponya maisha yake? Sitaingia. Nikatambua, na tazama, siye Mungu aliyemtuma; lakini amefanya unabii huu kinyume changu; nao Tobia na Sanbalati ndio waliomwajiri. Kwa sababu hii aliajiriwa, ili mimi niogope, nikafanye hivyo na kutenda dhambi, kisha wao wawe nazo habari mbaya, ili wanishutumie.”   

 

Chuma kuona chuma kunamaanisha kusaidiana kuinuana kutiana moyo ambako mwisho wa yote kutakuwa na faida kwa watu wote, sio mtu mmoja kila mmoja anahitaji kutiwa moyo au kujitoa moyo ili hatimaye aweze kuwa Baraka kwa wengine, kwa eneo lake ili mambo yaweze kuwa mema.

 

4.       Chuma hunoa chuma ni usemi unatufundisha kuwa tayari kubadilika:-

 

Chuma kunoa chuma maana yake vilevile ni kukubali kubadilika, vile vyuma vinaposuguana kunatokea mabadiliko chanya, lakini wakati mwingine chuma kunoa chuma humaanisha unaweza kuchoma moto chuma kimojawapo kikaiva katika moto kisha ukatumia nyundo kugonga kile chuma kingine mpaka kikanyooka, chuma kinachogongwa kinabadilika na kuwa katika umbile lililokusudiwa na mhunzi, kwa hiyo unapogongwa badilika usipobadilika utagongwa zaidi au utaondolewa,  Mungu anaweza kutuinulia marafiki wazuri ambao wanaweza kutusaidia kukua na kukomaa wao wanaweza kuwa wakweli kwetu na wanaweza kutuambia ukweli, kutushauri au kutukemea na kutujenga, na kutukosoa, kosoa zao zinaweza kuwa za kutusaidia hivyo kuna umuhimu kwetu kukubali kubadilika  na kufuata mashauri yao ama kufuata ushauri wa neno la Mungu, ni Baraka kuwa na watu wanaotunyoosha japo tunaweza tusijisikie vizuri kwa wakati Fulani, kibinadamu iko wazi kuwa wanadamu wachache sana wanaopenda kuambiwa ukweli, na wanaokubali kukemewa  lakini lazima tukubali kukemewa kuna watu hawakubali maonyo, hawataki kukemewa hawataki kuambiwa ukweli, tabia ya aina hii ni sawa na chuma kukataa kunolewa na anguko linaweza kutokea kwa watu wasiokubali maonyo.

 

Mithali 29:1 “Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, Atavunjika ghafula, wala hapati dawa.”

 

Neno la Mungu linatutahadharia kwamba ni muhimu kukubali maonyo wako watu hawataki kuonywa wakiguswa tu wanavimba wanageuka wanakuwa jeuri wanajibu wanajitetea wanajigamba wanajiona kuwa hawastahili kuguswa maandiko yanasema hao wamekuwa wana haramu kama sisi ni wana wa halali basin i muhimu kwetu tukawa watu tunaokubali maonyo

 

Waebrania 12:5-11 “tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, Wala usizimie moyo ukikemewa naye; Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye. Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali.Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi? Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake. Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani. Maandiko aidha yanawataka viongozi wa kiroho kukaripia na kuonya na kukemea

 

2Timotheo 4:2-4 “lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.”

 

 Watu waliyakubali maonyo baadaye walikuja kuwa viongozi wazuri sana Petro ndiye mwanafunzi nwa Yesu aliyekemewa mara nyingi sana, lakini alikuwa na uelewa mkubwa sana kuwa kwa Yesu kuna maneno ya uzima wa milele,

 

Mathayo 16:21-23 “Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata. Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.”     

 

Petro pamoja na makemeo makali sana hakumwacha Yesu aliendelea kushikamana naye Yohana 6:66-68 “Kwa ajili ya hayo wengi miongoni mwa wanafunzi wake wakarejea nyuma, wasiandamane naye tena. Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, Je! Ninyi nanyi mwataka kuondoka? Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.

 

Petro alikuwa na uelewa kuwa kukemewa kule kungekuja kumleta katika nafasi ya kuwa kiongozi na kufanya vizuri, Nyakati za kanisa la kwanza watu waliokuja kuwa viongzi wazuri ni wale ambao waliwahi kukemewa hadharani mbele ya wote na wakiwa wanajua umuhimu wa maonyo waliyapokea na kubadilika na kuja kuwa viongozi wazuri sana akiwemo Tizo aliyekuja kuwa askofu wa makanisa, Mungu aklimuinua sana na kuja kuwa kiongozi mkubwa sana na Paulo mtume alijivunia baadaye kwa sababu alikubali maonyo

 

 2Wakoritho 8:16-23Lakini ahimidiwe Mungu atiaye bidii ile ile kwa ajili yenu katika moyo wa Tito. Maana aliyapokea kweli yale maonyo; tena, huku akizidi kuwa na bidii, alisafiri kwenda kwenu kwa hiari yake mwenyewe. Na pamoja naye tukamtuma ndugu yule ambaye sifa zake katika Injili zimeenea makanisani mwote. Wala si hivyo tu, bali alichaguliwa na makanisa asafiri pamoja nasi katika jambo la neema hii, tunayoitumikia, ili Bwana atukuzwe, ukadhihirike utayari wetu. Tukijiepusha na neno hili, mtu asije akatulaumu kwa habari ya karama hii tunayoitumikia; tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele za Bwana tu, ila na mbele ya wanadamu.Nasi pamoja nao tumemtuma ndugu yetu tuliyemwona mara nyingi katika mambo mengi kuwa ana bidii, na sasa ana bidii zaidi sana kwa sababu ya tumaini kuu alilo nalo kwenu.  Basi mtu akitaka habari za Tito, yeye ni mshirika wangu, na mtenda kazi pamoja nami kwa ajili yenu; tena akitaka habari za ndugu zetu, wao ni mitume wa makanisa, na utukufu wa Kristo.” Baadaye sifa zake zilienea makanisani kote alikuwa ni mtu mwema mtendakazi pamoja na Paulo mtume  na mtume wa makanisa unapokuwa kanisani, shuleni kazini na kila mahali ili uweze kuwa mzuri na kufiti kwa kazi basin i vema ukakubali kunolewa.

 

5.       Chuma huona chuma ni usemi unaotukumbusha kujifunza kutoka kwa wengine

 

Wakati mwingine Mungu hutumia watu, kujifunza kutoka kwa mtu mwingine hii ni kanuni pia ya chuma kunoa chuma training

 

2Timotheo 2:2 “Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.”

 

Paulo mtume hapa anaonyesha kuwa Timotheo alijifunza vitu kutoka kwake  na anataka Timotheo ayatumie yale aliyiojifunza kutoka kwake awakabidhi watu waamini fu watakaofaa kuwafundisha na wengine, kujifunza kutoka kwa wengine ni njia sahihi ya kujinoa, chuma kinapokinoa chuma kingine husaidia kukifanya chuma kilichonolewa kutumika kama jinsi chuma kile kilivyokusudiwa na aliyekinoa, Maandiko yanaionyesha wazi kuwa wale waliojifunza kutoka kwa Yesu Kristo walitambulika kwa namna walivyokuwa na ujasiri mkubwa sawasawa na ule aliokuwa nao Yesu Kristo,  hii ilisababishwa na yule aliyewanoa namna alivyo ona

 

Matendo 4:13 “Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.”

 

Viongozi wa dini walishangazwa sana na uwezo mkubwa wa Petro na Yohana, ujasiri, uwezo wa kujieleza na kujiamini na miujiza waliyoifanya walitaka kujua kuwa watu hawa ni watu wa namna gani wamesomea wapi, wengi wa viongozi wa dini ya kiyahudi walikuwa walimu waliwafunza watu lakini walishangaa neno watu wasio na Elimu na Maarifa lina maana ya (watu wasiokuwa na ujuzi wa Torati maamuma, hawakupitia darasa lolote la viongozi wa kidini wanaotambulika lakini wasio na maarifa unlearned and ignorant kwa kiyunani (Idiotai)  watu walioibuka tu, wasiojulikana wanatokea wapi) walikuja kubaini kuwa watu hawa ni ni wazi kuwa mafunzo yao waliyapata kwa Yesu, Yesu alipochagua wanafunzi wake hakwenda kwenye madarasa ya watu maalumu alichukua watu wa kawaida tu wasio na Elimu na kuwanoa wakawa vile anavyotaka

 

Mathayo 4:18-22 “Naye alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi. Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata. Akaendelea mbele, akaona ndugu wengine wawili, Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, ambao walikuwamo chomboni pamoja na Zebedayo baba yao, wakizitengeneza nyavu zao; akawaita. Mara wakakiacha chombo na baba yao, wakamfuata.”

 

Hawa walikuwa watu walionolewa na Yesu mwenyewe, walikuwa mashujaa, walikuwa majasiri, walikuwa na uwezo wa kunena, walikuwa na uwezo wa kujenga hoja za kimaandiko na kuthibitisha wazi kuwa Yesu ni Bwana, jambo lililopelekea wajiulize hawa wametokea wapi ni ukweli ulio wazi kuwa wao walikuwa wamejifunza kila kitu kutoka kwa Yesu Kristo,

 

Wakati Paulo mtume yeye alikuwa mtu aliyejifunza kutoka katika shule za viongozi wa kiyahudi waliokuwa maarufu sana wakati huo,

 

Matendo 22:3-5 “Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi; nikawaudhi watu wa Njia hii hata kuwaua, nikawafunga, nikiwatia gerezani, wanaume na wanawake. Kama Kuhani Mkuu naye anishuhudiavyo, na wazee wa baraza wote pia, ambao nalipokea barua kwao kuwapelekea ndugu wale, nikaenda Dameski, ili niwalete wale waliokuwa huko hata Yerusalemu, hali wamefungwa, ili waadhibiwe.”

 

Sasa unaweza kuona kuwa Paulo mtume tofauti na Petro na Yohana yeye alikuwa amepitia shule za kiyahudi na aliweza kujitambulisha hivyo na hawa wazee walikuwa wanamjua na Gamaliel alikuwa ni Rabbi aliyeheshimika sana ona

 

Matendo 5:34-35 “Lakini mtu mmoja, Farisayo, jina lake Gamalieli, mwalimu wa torati, mwenye kuheshimiwa na watu wote, akasimama katika baraza, akaamuru mitume wawekwe nje kitambo kidogo, akawaambia, Enyi waume wa Israeli, jihadharini jinsi mtakavyowatenda watu hawa.”

 

Unaona Gamaliel anatajwa kama Mwalimu wa Torati aliyeheshimika sana alikuwa rabbi wanahistoria wa nyakati za kanisa la kwanza wanaeleza kuwa rabbi huyu alifundisha kati ya mwaka wa 22-55 Baada ya Kristo, na hivyo kuna uwezekano mkubwa alimfundisha Paulo aliyekuwa na umri wa miaka kama 16 hivi, gamaliel alikuwa ni farisayo aliyebobea kutika katika shule ya Rabbi Hillel, wa kizazi kabla kidogo ya Yesu kristo, wakati huo kulikuwa na marabbi maarufu sana Rabi Hillel na rabbi Shammai, hawa walihusika kwa kiwango kikubwa kuwanoa wayahudi wengi katika maswala ya sharia na mitazamo mikubwa miwili yay a Reberal  na conservative, kwa msingi huo kila mmoja alinolewa kwa namna Fulani kutoka kwa mwingine, Muda usingeliweza kutosha kuonyesha kuwaona wengi waliopata mafunzo kutoka vyanzo mbalimbali 

 

Musa alipata Elimu ya kimisri ona Matendo 7:22-25 “Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa hodari wa maneno na matendo. Umri wake ulipopata kama miaka arobaini akaazimu moyoni mwake kwenda kuwatazama ndugu zake Waisraeli.Akamwona mmoja akidhulumiwa, akamtetea, akamlipia kisasi yule aliyekuwa akionewa, akampiga huyo Mmisri. Alidhani kwamba ndugu zake watafahamu ya kuwa Mungu anawapa wokovu kwa mkono wake, lakini hawakufahamu.” Ni Elimu hii aliyoipata na elimu ya dini aliyoipata kule Midian kwa Yethro mkwewe vilimuwezesha kuwa mwanzilishi na kiongozi mkubwa na wa kwanza au baba wa Taifa la Israel na kulijengea ustaarabu mwingi sana, tukubali kumbe basi kujifunza kutoka kwa wengine na hasa wale wakali kweli kweli ili watunoe na tuwafuate Waebrania 13:7 “Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni imani yao.”

 

Kwa hiyo hapa usemi unatukumbusha wazi kwamba ili tuweze kuwa wazuri sana kuna manufaa ya kujifunza kutoka kwa wengine na kuwasaidia wengine kuwa wazuri zaidi, kumbuka hakuna mtu nanaweza kuwa mtu peke yake                 na hivi tulivyo ni matokeo ya kujifunza kutoka kwa wengine!

 

6.       Chuma hunoa chuma ni usemi unaotukumbusha umuhimu wa neno la Mungu

 

Kwa karne nyingi sana imethibitika wazi kuwa neno la Mungu limekuwa na nguvu kubwa sana ya kubadilisha maisha ya mwanadamu kuliko namna nyingine zozote, kama mtu anataka kunolewa vema kunyooshwa na kuwa mwema awe tayari kunyenyekea kwa neno la Mungu Biblia inalisifia neno la Mungu kama upanga ukatao kuwili ona

 

Waebrania 4:12-13 “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.

 

Lenyewe lina uwezo wa kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo, na limekuwa na sifa za kubadilisha maisha ya watu  wa makabila mbalimbali na kuwapa utamaduni wa kibiblia lenyewe kama nyndo vilevile linauwezo wa kuvunja vunja na kulainisha

 

Yeremia 23:28-29 “Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema Bwana. Je! Neno langu si kama moto? Asema Bwana; na kama nyundo ivunjayo mawe vipande vipande?

 

Neno la Mungu lina nguvu ya kuumba Mwanzo 1:1-31 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.  Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji. Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo. Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili. Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo. Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo. Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tatu. Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka; tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi; ikawa hivyo. Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia. Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi na kuutawala mchana na usiku na kutenga nuru na giza; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne. Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu. Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tano. Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo. Mungu akafanya mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu; na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo. Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.”

 

Neno la Mungu lina nguvu ya kuhekimisha 2Timotheo 3:14-17 “Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao; na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.  Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.”

 

Neno la Mungu lina nguvu ya kuleta mabadiliko Isaya 55:10-11 “Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.”             

 

Neno la Mungu lina uwezo wa kutusaidia kuzishinda dhambi Zaburi 119:9-11 “Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako. Kwa moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na maagizo yako.Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.”

 

Mtu awaye yote anayetaka kunolewa katika maisha yake basi na ajifunze kunyenyekea na kukaa katika neno la Mungu, Mungu analiheshimu sana neno lake lakini sio hivyo tu anawaangalia watu waliopondeka watetemekao wasikiapo neno lake Isaya 66:2 “Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema Bwana; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.”

 

Muda usingeliweza kutosha kuona namna na jinsi neno la Mungu linavyofanya kazi katika mazingira mbali mbali lakini lenyewe ni chuma ni nyundo ivunjayo mawe vipande vipande lina uwezo wa kuzalisha nguvu za aina yoyote ile tuitakayo, lina uwezo wa kutunoa na kutufanya upa na kututakasa na kutuweka sawa!

 

Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye hekima



Jumatatu, 18 Oktoba 2021

Msiba katika bonde la kukata maneno!


Yoeli 3:12-14Mataifa na wajihimize, wakapande juu katika bonde la Yehoshafau; maana huko ndiko nitakakoketi niwahukumu mataifa yote yaliyo pande zote. Haya! Utieni mundu, maana mavuno yameiva; njoni, kanyageni; kwa maana shinikizo limejaa, mapipa nayo yanafurika; kwani uovu wao ni mwingi sana. Makutano makubwa, makutano makubwa, wamo katika bonde la kukata maneno! Kwa maana siku ya Bwana i karibu, katika bonde la kukata maneno.”


Utangulizi:

Maandiko matakatifu yanatufundisha kuwa kila mtu na aitii mamlaka iliyokuu, kwa sababu hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu na kuwa ile iliyoko imeamriwa na Mungu au imeruhusiwa na Mungu, na kwa sababu hiyo kuiasi mamlaka ni kumuasi Mungu mwenyewe ona

Warumi 13:1-4 “Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake; kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu.”

Maandiko yanathibitisha wazi kuwa kama mtu atashindana na mwenye mamlaka ni wazi kuwa anashinda ana agizo la Mungu na sio hivyo tu washindanao na Mungu watajipatia hukumu! Kanuni ya Mungu siku zote hasimami na muasi, Mungu husimama na mtu wake au mtumishi wake aliyemuweka, Mungu hajipingi mwenyewe wala hawezi kushindana kinyume na kusudi lake hivyo atasimama na Mtumishi wake, aliyemuweka kwa kusudi lake

1Samuel 2:9-10 “Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; Bali waovu watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda; Washindanao na Bwana watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; Bwana ataihukumu miisho ya dunia; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake.”

Nyakati za agano la kale Mungu katika Hekima yake, alipokuwa amekusudia kuamua lipi ni lipi au watu walipokuwa wanataka kuamua jambo au kutafuta suluhu ya kivita mara nyingi maamuzi yao yalifanyika katika bonde, pande zinazoshindanda zingekaa upande huu wa mlima na upande huu wa mlima na kisha baada ya uamuzi kufanyika pale bondeni ndipo mahali ambapo watu wangeweza kufanya maamuzi yao na hapo palijulikana sana kama Bonde la kukata maneno. Vita ingapiganwa hapo na damu ingemwagika hapo bila kuinajisi nchi, na Mungu angetoa ushindi kwa mtu husika.


Maana ya Bonde la kukata maneno!

Kama nilivyogusia katika utangulizi neno Bonde la kukata maneno, limetumika katika maandiko kumaanisha eneo la kufanya uamuzi, au bonde la kumaliza maneno hususani wakati kuna jambo linahitaji kufanyiwa uamuzi ikiwemo kumaliza vita, au bonde la kumaliza migogoro kati ya watu wa Mungu na adui wa watu wa Mungu, Nyakati za biblia watu walipokuwa na vita kati ya taifa moja na taifa jingine au ufalme mmoja na ufalme mwingine walikuwa na tabia ya kukaa upande mmoja wa mlima na upande wa pili wa mlima na kutupiana maneno ya kujigamba, kila mmoja angeweza kusema kile anachoweza kukisema lakini hatimaye wangeshuka katika Bonde na kumaliza mgogoro au maneno kwa kuonyeshana umwamba  bonde la kukata maneno lilikuwa kama Mahakama ya usuluhishi au kumaliza ubishi wa kila mmoja kwa namna yake mfano

1Samuel 17:1-11 “Wakati huo Wafilisti walikusanya majeshi yao kwa vita, nao wakakusanyika huko Soko, ulio mji wa Yuda, wakatua kati ya Soko na Azeka, katika Efes-damimu. Naye Sauli na watu wa Israeli wakakusanyika, wakatua katika bonde la Ela, nao wakapanga vita juu ya hao Wafilisti. Wafilisti wakasimama juu ya mlima upande huu, na Waisraeli wakasimama juu ya mlima upande huu, napo palikuwa na hilo bonde katikati. Ndipo akatoka shujaa katika kambi ya Wafilisti, aliyeitwa Goliathi, wa Gathi, ambaye urefu wake ulikuwa mikono sita na shibiri moja. Alikuwa na chapeo ya shaba kichwani, tena amevaa darii ya shaba; na uzani wake ile darii ya shaba ulikuwa shekeli elfu tano za shaba. Tena amevaa mabamba ya shaba miguuni mwake, naye alikuwa na mkuki wa shaba kati ya mabega; yake. Na mti wa fumo lake ulikuwa kama mti wa mfumaji; na kichwa cha mkuki wake kilikuwa shekeli mia sita za chuma uzito wake; na mtu aliyemchukulia ngao yake akamtangulia. Naye akasimama, akawapigia kelele majeshi ya Israeli akawaambia, Mbona mmetoka kupanga vita? Je! Mimi si Mfilisti, na ninyi si watumishi wa Sauli? Jichagulieni mtu, akanishukie mimi. Kama akiweza kupigana nami na kuniua, sisi tutakuwa watumwa wenu; nami nikimshinda yeye na kumwua, ninyi mtakuwa watumwa wetu, na kututumikia. Yule Mfilisti akasema, Nayatukana leo majeshi ya Israeli; nipeni mtu tupigane. Basi Sauli na Israeli wote waliposikia maneno hayo ya Mfilisti, wakafadhaika na kuogopa sana.”

Kwa hiyo utaweza kuona kuwa katikati walipokuwa wakitupiana maneno walikaa upande huu wa mlima na upande huu wa mlima na walitupiana maneno, lakini hapa katikati ya bonde ndio mahali sasa paliitwa bonde la kukata maneno, kwamba sema utakavyosema na tukana utakavyotukana tamba utakavyotamba na kunya utakavyo kunya na harisha uatakavyoharisha toa shombo za kila namna lakini tutakutana katika bonde la kukata maneno na hapo ndio Mungu ataonyesha kuwa nani ni mbabe? Nani yuko pamoja naye na ni nani aliyechaguliwa na Mungu, nani anapigana vita vya kishetani na ni nani anapigana vita vya Bwana!, Bonde la kukata maneno kwa msingi huo liliitwa bonde la maamuzi, kibiblia pia liliitwa bonde la Yehoshafau kwa mujibu wa nabii Yoeli, hii ni kwa sababu katika bonde hili Mungu aliwadhalilisha maadui wa Israel mara kadhaa hususani wakati wa Yehoshafati  mara mbili, lakini pia jina Yehoshafati maana yake Yehova ndiye muamuzi wangu,  kinabii mahali hapa ndipo Mungu atakapokuja kuuhukumu Mataifa yote yatakayosimama kinyume na Israel na Mungu atawaangamiza watu wengi sana katika eneo hili  hivyo patakuwa na mauti ya kutisha na kushangaza patakuwa ni mahali pa msiba kwa wale wote wasiomcha Mungu ona

Ezekiel 39:13-16Naam, watu wote wa nchi hiyo watawazika; itakuwa ni sifa kwao katika siku ile nitakapotukuzwa, asema Bwana MUNGU. Nao watawachagua watu wa kufanya kazi ya daima, watakaopita kati ya nchi, ili kuwazika waliosalia juu ya uso wa nchi, ili kuisafisha; miezi saba itakapokwisha kupita watatafuta. Na hao wapitao kati ya nchi watatafuta; na mtu ye yote aonapo mfupa wa mtu, ndipo atakapoweka alama karibu nao, hata wazishi watakapouzika katika bonde la Hamon-Gogu. Tena, Hamona litakuwa jina la mji. Hivyo ndivyo watakavyosafisha nchi.

Ezekiel analiona bonde hilo pia kuwa ni mahali watakapozikwa watu wengi sana walio kinyume na mapenzi ya Mungu, maiti zao zitazikwa mahali hapo na kumbukumbu lao litapotelea mahali hapo, Kijiografia eneo hilo linasemekana liko Israel karibu na bonde la Kidron Mashariki ya Yerusalem, eneo hili kinabii pia ndio litakuja kuwa eneo ambalo Yesu atabagua Kondoo na Mbuzi na kutoa hukumu kwa mataifa yatakayokuwa kinyume na Israel

Mathayo 25:31-46 “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto. Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia. Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia? Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe; nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama. Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie? Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi. Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.” Watu wasiotaka kutawaliwa na Yesu aidha watachinjwa katika eneo hili Luka 19: 27 “Tena, wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa mwachinje mbele yangu.”

Msiba katika Bonde la kukata maneno!

Kama tulivyoona maana ya bonde la kukata maneno kwa kawaida Hapa ndio mwisho wa mabishano yote na mashindano yote, Mungu anapokuja katika bonde la kukata maneno huwa anaonyesha wazi wazi nani ni mshindi na ni nani yuko upande wake na kwa kawaida katika Bonde la kukata maneno huwa ndio mwisho wa maamuzi ya Mungu, kwa kawaida hata kama mahali hapo hapana bonde Mungu huweza kuifunua ardhi na kufanya bonde popote na kupoteza watu waliomuasi,

Hesabu 16:1-34 “Basi Kora, mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, akatwaa watu, pamoja na Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu, na Oni, mwana wa Pelethi, waliokuwa wana wa Reubeni; nao, pamoja na watu kadha wa kadha wa wana wa Israeli, watu mia mbili na hamsini, Wakuu wa mkutano, waliokuwa wateule wa mkutano, watu wenye sifa, wakainuka mbele ya Musa; nao wakakusanyika kinyume cha Musa na Haruni, na kuwaambia, Ninyi inawatosha, kwa kuwa mkutano wote ni mtakatifu, kila mmoja miongoni mwao, Bwana naye yu kati yao; n'nini basi kujitukuza juu ya mkutano wa Bwana? Musa aliposikia maneno haya, akapomoka kifudifudi;  kisha akanena na Kora na mkutano wake wote, akawaambia, Asubuhi Bwana ataonyesha ni kina nani walio wake, kisha ni nani aliye mtakatifu, tena ni nani atakayemkaribisha kwake; maana, yeye atakayemchagua ndiye atakayemsongeza kwake. Fanyeni neno hili; twaeni vyetezo, ninyi Kora na mkutano wake wote; vitieni na moto, mkaweke na uvumba juu yake mbele za Bwana kesho; kisha itakuwa ya kwamba mtu Bwana atakayemchagua, yeye atakuwa mtakatifu; inawatosha ninyi, enyi wana wa Lawi. Musa akamwambia Kora, Sikizeni basi, enyi Wana wa Lawi; Je! Mwaona kuwa ni jambo dogo kwenu, kuwa Mungu wa Israeli amewatenga ninyi na mkutano wa Israeli, ili apate kuwakaribisha kwake; ili mfanye utumishi wa maskani ya Bwana, na kusimama mbele ya mkutano ili kuwatumikia; tena ya kuwa amekuleta uwe karibu, na ndugu zako wote wana wa Lawi pamoja nawe? Nanyi, je! Mwataka na ukuhani pia? Kwa sababu hii wewe na mkutano wako wote mmekusanyika kinyume cha Bwana; na Haruni, je! Yeye ni nani hata mkamnung'unikia? Kisha Musa akatuma kuwaita Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu; nao wakasema, Hatuji sisi; je! Ni jambo dogo, wewe kutuleta kutoka nchi iliyojawa na maziwa na asali, ili kutuua jangwani, lakini pamoja na haya wajikuza mwenyewe uwe mkuu juu yetu kabisa? Kisha, hukutuleta katika nchi iliyojawa na maziwa na asali, wala hukutupa urithi wa mashamba, na mashamba ya mizabibu; je! Unataka kuwatoboa macho watu hawa? Hatuji. Musa akakasirika sana, akamwambia Bwana. Usiikubali sadaka yao; mimi sikutwaa hata punda mmoja kwao, wala sikumwumiza hata mtu mmoja miongoni mwao. Kisha Musa akamwambia Kora, Wewe na mkutano wako wote iweni hapa mbele ya Bwana kesho, wewe, na wao, na Haruni; mkatwae kila mtu chetezo chake, na kutia uvumba juu yake, mkavilete mbele za Bwana, vyetezo mia mbili na hamsini; wewe pia, na Haruni, kila mtu na awe na chetezo chake. Basi wakavitwaa kila mtu chetezo chake, wakatia na moto ndani yake, wakatia na uvumba juu ya moto, na kusimama pale mlangoni pa hema ya kukutania, pamoja na Musa na Haruni. Kisha Kora akakutanisha mkutano wote kinyume chao mlangoni pa hema ya kukutania; na utukufu wa Bwana ukatokea mbele ya mkutano wote. Kisha Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,Jitengeni ninyi mkaondoke kati ya mkutano huu, ili nipate kuwaangamiza mara moja. Nao wakapomoka kifudifudi, wakasema, Ee Mungu, Mungu wa roho za wenye mwili wote, je! Mtu mmoja atafanya dhambi, nawe utaukasirikia mkutano wote? Bwana akasema na Musa, na kumwambia, Nena na mkutano, na kuwaambia, Ondokeni ninyi hapo karibu na maskani ya Kora, na Dathani, na Abiramu. Basi Musa akainuka na kuwaendea Dathani na Abiramu; na wazee wa Israeli wakaandamana naye.  Akasema na mkutano, na kuwaambia, Nawasihi, ondokeni penye hema za hawa watu waovu, wala msiguse kitu chao cho chote, msiangamizwe katika dhambi zao zote. Basi wakaondoka hapo karibu na maskani ya Kora, na Dathani na Abiramu, pande zote; nao kina Dathani na Abiramu wakatoka nje wakasimama mlangoni mwa hema zao, pamoja na wake zao, na wana wao na watoto wao wadogo. Musa akasema, Kwa jambo hili mtajua ya kwamba Bwana amenituma, ili nifanye kazi hizi zote; kwa kuwa mimi sikuzifanya kwa akili zangu mwenyewe. Kama watu hawa wakifa kifo cha sikuzote, kama watu wote wafavyo, au kama wakipatilizwa kwa mapatilizo ya watu wote; hapo basi Bwana hakunituma mimi. Lakini Bwana akiumba kitu kipya, na hiyo nchi ikifunua kinywa chake na kuwameza, pamoja na wote walio nao, nao washukia shimoni wali hai; ndipo mtatambua ya kwamba watu hawa wamemdharau Bwana Basi ilikuwa, hapo alipokwisha kusema maneno haya yote, nchi iliyokuwa chini yao ikapasuka; nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao na wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote. Basi wao, na wote waliokuwa nao, wakashukia shimoni wali hai; nayo nchi ikawafunika wakaangamia kutoka mle mkutanoni. Nao Israeli wote waliokuwa kando-kando yao wakakimbia kwa ajili ya kilio chao; kwa kuwa walisema, Nchi isije kutumeza na sisi.”

Haijalishi kuwa wapinzani wako wana maneno kiasi gani, wana nguvu kiasi gani, wana tisha kiasi gani, lakini mwisho wa siku wataingia katika bonde la kukata maneno na hapa Mungu ataingilia kati na kutenda mambo ya ajabu, atamsambaratisha adui na kumfutilia mbali, heri leo kuwa upande wa Bwana, fungua macho yako uelewe kuwa Mungu yuko upande gani simama kule aliko Mungu na ushindi utakuwa dhahiri, usipokuwa upande wa Bwana na usipotaka Bwana akutawale utachinjwa

Goliati alijitamba kwa siku 40 kila siku akiwatisha watu wa Israel lakini alipotokea mtu aliyepakwa mafuta katika bonde la kukata maneno Daudi mwana wa Yese. Goliathi alizimia na kukatwa kichwa

1Samuel 17:44-51 “Mfilisti akamwambia Daudi, Njoo huku kwangu; nyama yako nitawapa ndege wa angani na wanyama wa mwituni. Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana. Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kuku ondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli. Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu. Ikawa, hapo Mfilisti alipojiinua, akaenda akamkaribia Daudi, ndipo Daudi naye akapiga mbio, akalikimbilia jeshi ili akutane na yule Mfilisti. Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe moja, akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe hilo likamwingilia kipajini, akaanguka chini kifudifudi. Hivyo Daudi akamshinda yule Mfilisti kwa kombeo na jiwe, akampiga Mfilisti, akamwua; walakini Daudi hakuwa na upanga mkononi mwake. Ndipo Daudi akapiga mbio, akasimama juu ya Mfilisti, akautwaa upanga wake, akaufuta alani mwake, akamwua, akamkata kichwa kwa upanga huo. Nao Wafilisti walipoona ya kuwa shujaa wao amekufa, wakakimbia.”   

Kama wako watu wanakushambulia katika maisha yako wanatangaza vita na wewe usiogope uko mwisho wao katika Bonde la kukata maneno Mungu ataingilia kati na bonde lako la vita litageuka kuwa Bonde la Baraka kwako lakini litakuwa bonde la msiba kwa maadui zako

2Nyakati 20:17-27 “Hamtahitaji kupigana vita, jipangeni, simameni, mkauone wokovu wa Bwana ulio pamoja nanyi, enyi Yuda na Yerusalemu; msiogope, wala msifadhaike; kesho tokeni juu yao; kwa kuwa Bwana yu pamoja nanyi. Yehoshafati akainama kichwa, kifulifuli; wakaanguka mbele za Bwana Yuda wote na wakaao Yerusalemu, wakimsujudia Bwana.Na Walawi, wa wana wa Wakohathi na wa wana wa Wakorahi, wakasimama ili wamsifu Bwana, Mungu wa Israeli, kwa sauti kuu sana. Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje katika jangwa la Tekoa; nao walipokuwa wakitoka, Yehoshafati akasimama, akasema, Nisikieni, enyi Yuda nanyi wenyeji wa Yerusalemu; mwaminini Bwana, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa. Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia Bwana, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni Bwana; kwa maana fadhili zake ni za milele. Nao walipoanza kuimba na kusifu, Bwana akaweka waviziao juu ya wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, waliokuja juu ya Yuda; nao wakapigwa. Kwani wana wa Amoni na wa Moabu waliwaondokea wenyeji wa mlima Seiri kuwaulia mbali na kuwaharibu; nao walipokwisha kuwakomesha hao wakaao Seiri, wakajitia kuharibu kila mtu mwenziwe. Hata Yuda walipofika mnara wa kulindia wa jangwani, wakalitazama hilo jeshi; nao, angalia, walikuwa maiti walioanguka nchi, wala hapana aliyeokoka. Nao Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara zao, wakaona kati yao wingi wa mali, na mavazi, na johari za thamani, walivyojivulia, zaidi kuliko wawezavyo kuchukua; wakawa siku tatu katika kuteka nyara, maana zilikuwa nyingi sana. Hata siku ya nne wakakusanyika katika bonde la Baraka; maana ndipo walipombarikia Bwana; kwa hiyo jina lake mahali pale pakaitwa Bonde la Baraka hata leo. Kisha wakarudi, kila mtu wa Yuda na Yerusalemu, na Yehoshafati mbele yao, ili kuurudia Yerusalemu kwa furaha; kwa kuwa Bwana amewafurahisha juu ya adui zao.”

Bonde lilikuwa ni kama ulingo wa mabondia waliotambiana kwa muda mrefu, afile munu asigale munu, acholile kachola, show show na kadhalika, Bonde la kukatya maneno ni ikama kiwanja cha mpira wa soka watu wataingia kati dakika 90 utachezwa na mwamba ataonekana, watu wataingia ulingoni zitapigwa na mwamba ataonekama

Siku ya leo haijalishi una vita na nani, haijalishi nani ametangaza vita na wewe kumbuka liko Bonde la kukata maneno, liko bonde ambalo kwalo Mungu atamaliza migogoro yote atamaliza kesi zote atafanya maamuzi na mwisho wa siku wale ambao Bwana amewachagua atawaleta kwake naye ataligeuza Bonde lako kuwa sio la vita tena bali la ushindi na bonde la Baraka  na bonde la kuteka mateka na bonde la kukusanya nyara na wapinzani wako na maadui zako itakuwa ni msiba katika bonde la kukata maneno!, Ukiwa na Yesu hutaogopa kama mfalme Yehoshafati, watu walio na Mungu hawapigani tu vita vya maneno, kama Goliathi sisi tunalitaja jina la Bwana Mungu wetu yeye ndio tegemeo letu na tumaini letu hakuna mtu aliyemtumainia akatahayari, hatutatahayarika kamwe, Mungu atamaliza ngebe za adui zako, Penina alikuwa na maneno sana kuliko Hanna kwa sababu hana alionekana kuwa tasa na hazai, lakini siku moja mwenye nguvu akaingilia kati na hana akasema maneno ya ushindi, ona

1Samuel 2:2-9 “Hakuna aliye mtakatifu kama Bwana; Kwa maana hakuna ye yote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu. Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa maarifa, Na matendo hupimwa na yeye kwa mizani.Pinde zao mashujaa zimevunjika, Na hao waliojikwaa wamefungiwa nguvu. Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula, Na hao waliokuwa na njaa wamepata raha. Naam, huyo aliyekua tasa amezaa watoto saba, Na yeye aliye na wana wengi amedhoofika. Bwana huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu. Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu. Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina Bwana, Naye ameuweka ulimwengu juu yake. Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; Bali waovu watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda;”
 

Bwana ampe neema kila mmoja wetu na maisha ya ushindi kwa kila anayemtegemea Bwana na asiyezitegemea akili zake mwenyewe na tukutane katika bonde la kukata maneno!

Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!


Jumapili, 3 Oktoba 2021

Jilindeni na chachu ya Mafarisayo


Luka 12:1 “Wakati huo, makutano walipokutanika elfu elfu, hata wakakanyagana, alianza kuwaambia wanafunzi wake kwanza, Jilindeni na chachu ya Mafarisayo, ambayo ni unafiki.”


Utangulizi:

Mojawapo ya lengo kuu la kibiblia watu wanapojifunza neno la Mungu kupitia watumishi wa Mungu, ni kuhakikisha kuwa watu wote wanakua kiroho na kiadilifu kwa kumjua Yesu na kukua hata kufikia kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo

Waefeso 4:11-13 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo

Kristo Yesu Bwana wetu katika mafundisho yake alikuwa na lengo la kumtaka kila Mwanafunzi wa Yesu afikie ngazi ya ukamilifu na kuwa kama baba yetu wa Mbinguni alivyo Mathayo 5:48 “Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.” Haya ndio makusudi makuu ya mafundisho yetu kwamba mioyo yetu ifanywe imara ili iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu ona 1Wathesalonike 3:12-13 “Bwana na awaongeze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu; apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.”

Kwa msingi huo basi, ili mioyo yetu iweze kuimarishwa, na sisi sote tuweze kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo, na mioyo yetu iweze kufanywa imara, ili tuwe watakatifu na watu wasio na lawama sio kwa wengine tu hata katika mioyo yetu mbele za Mungu, somo hili tunalojifunza leo ni moja ya masomo ya msingi sana katika kuwapata wanafunzi wa kweli wa Yesu Kristo. Kwa msingi huo basi tutajifunza somo hii jilindeni na chahu ya mafarisayo kwa kuzingatia vipengele sita vifuatavyo:-

  • Jilindeni na chachu ya Mafarisayo:-
  • Maana ya chachu ya mafarisayo:-
  • Chachu ya Mafarisayo ni tabia ya shetani:-
  • Chachu ya Mafarisayo ni jaribu la wanadamu wote:-
  • Madhra ya  Chachu ya Mafarisayo:-
  • Jinsi ya kujilinda na Chachu ya Mafarisayo:-

 

Jilindeni na Chachu ya Mafarisayo:-

Moja ya masomo ya muhimu sana ya Bwana Yesu kwa wanafunzi wake ilikuwa ni kujilinda na chachu, Neno hili Bwana Yesu alilirudia mara kwa mara katika injili kuonyesha jinsi alivyokuwa makini na swala hili ona Mathayo 16:6 “Yesu akawaambia, Angalieni, jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.” Neno chachu kwa kifupi katika maandiko limetumika kuelezea Dhambi Wagalatia 5:7-9 “Mlikuwa mkipiga mbio vizuri; ni nani aliyewazuia msiitii kweli? Kushawishi huku hakukutoka kwake yeye anayewaita ninyi. Chachu kidogo huchachua donge zima.” Kwa hivyo kimsingi Yesu alikuwa anawaonya wanafunzi wake wajihadhari na dhambi ya mafarisayo au masadukayo ambayo ilikuwa ni unafiki,  Yesu alikuwa ameiona dhambi hii kuwa ni dhambi ya kuichukulia tahadhari, kwa sababu kwa kujua au kwa kutokujua Mafarisayo wengi na watu wengi wa dini walikumbwa na aina hii ya dhambi, Ni kwaajili ya haya maandiko yanawataka watu waliomwamini Yesu wawe tofauti. Wakiwa wamejaa, upendo, utokao katika moyo safi na imani isiyo na unafiki. 1Timotheo1:5 “Walakini mwisho wa agizo hilo ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki.” Sio hivyo tu utaweza kuona hata mitume waliwakumbusha wanafunzi wa nyakati za kanisa la kwanza kuwa mbali na uovu wa kila namna lakini pia na unafiki 1Petro 2:1 “Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote.”

Maana ya chachu ya mafarisayo:-

 

Sasa chachu ya mafarisayo inayotajwa hapa ni hii ni dhambi yao ya unafiki, Unafiki hasa ni nini? Neno linalotumika katika Biblia kuelezea unafiki ni “hypocrisy” – kwa kiyunani ni “Ypokrisia” – tafasiri yake kwa kiingereza ni The practice of claiming to have higher standard or more noble beliefs that the really case, unreality, pretending, kwa Kiswahili ni Hali ya kujionyesha au kujifanya kuwa uko kwenye kiwango cha juu sana au uko vizuri sana kiroho wakati hali halisi haiku hivyo, ni tabia ya kuigiza, ni hali ya kujidanganya mwenyewe, Dhambi hii inaweza kujifunua katika namna mbalimbali mfano Mtu anaweza akakusifia sana lakini moyoni akiwa na kusudi lingine

 

Marko 12:13-17 “Wakatuma kwake baadhi ya Mafarisayo na Maherodi, ili wamnase kwa maneno. Hata walipofika walimwambia, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, wala hujali cheo cha mtu; kwa maana hutazami sura za watu; lakini katika kweli waifundisha njia ya Mungu. Je! Ni halali kumpa Kaisari kodi au siyo? Tumpe, tusimpe? Naye, akijua unafiki wao, akawaambia, Mbona mmenijaribu? Nileteeni dinari niione. Wakaileta. Akawaambia, Ni ya nani sanamu hii na anwani hii? Wakamwambia, Ni ya Kaisari. Yesu akajibu, akawaambia, Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na yaliyo ya Mungu mpeni Mungu. Wakamstaajabia sana.”

 

Mafarisayo walituma watu kwa Yesu, kwa kusudi la kumjaribu lakini tunawaona wakiwa wanajifanya kumsifia kumbe wakiwa na kusudi la kumleta pabaya, wako watu wa aina kama hizo wakati mwingine ukiona anakusifia tu ujue atakukopa, kwa hiyo unaweza kusifiwa kwa uwongo ili mtu aweze kutimiza maslahi yake

 

Mtu mnafiki pia hufanya jambo kwa kusudi la kuonekana na watu, ili asifiwe, au ili aonekane Mathayo 6:1-6 “Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.”     

 

Watu wanafiki, hufanya mambo kwa kusudi la kujionyesha tu, au kwa kusudi la kuonekana tu, au ili wasifiwe na watu  wanaweza hata kufanya jambo la kidini kama kusali au kufunga lakini sio kwa dhamiri ya kiungu, Mathayo 6:16-18 “Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.”

 

Watu wanafiki huwa na utakatifu wanje tu, lakini ndani ni waovu kupindukia, utakatifu wao ni wa nje tu wao hufanya mambo kwa kusudi la kutaka kutazamwa na watu, au ili waonekane kuwa ni wema na wazuri na watu wakubwa sana  na hujiweka mbele sana katika kila kitu,

 

Mathayo 23:5-8 “Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao; hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi, na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi

 

Yesu alikemea vikali dhambi ya unafiki kwa sababu, ni udanganyifu wa njia ya nje lakini wanafiki wengi kwa ndani ni watu waliojaa uozo wa kila namna Mathayo 23:23-33 “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia. Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang'anyi na kutokuwa na kiasi. Ewe Farisayo kipofu, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa safi. Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote. Vivyo hivyo ninyi nanyi, kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki, bali ndani mmejaa unafiki na maasi. Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnayajenga makaburi ya manabii, na kuyapamba maziara ya wenye haki,na kusema, Kama sisi tungalikuwako zamani za baba zetu, hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii. Hivi mwajishuhudia wenyewe, ya kwamba ninyi ni wana wao waliowaua manabii. Kijazeni basi kipimo cha baba zenu. Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum? Yesu hakuwahi kuwa na huruma na wanafiki, wala hakuwa na lugha nyepesi ya kichungaji kwa wanafiki Yesu alikemea vikali na kuwaeleza watu waziwazi za uso, aliwapa makavu laivu, walitambua na kuthamini mchango wa Mtu baada ya kufa, lakini alipokuwa hai walihusika kuwaua, hii ndio tabia ya unafiki.

 

Wanafiki huona makosa ya wengine, nay a kwao wenyewe hawayaoni, Luka 6:41-42 “Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? Au, utawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu yangu, niache nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako, nawe huiangalii boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi kilichomo katika jicho la ndugu yako.”

 

Watu wanafiki huwadharau watu wengine wakijifikiri kuwa wana ubora zaidi kuliko wengine laki mbele za Mungu wamekataliwa Luka 18:9-14 “Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote. Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru. Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang'anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote. Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi. Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.”

 

Yesu hata siku moja hakufanya jambo jema na kutaka kuonekana na watu, Marko 1:40-44 “Akaja kwake mtu mwenye ukoma, akamsihi na kumpigia magoti, na kumwambia, Ukitaka, waweza kunitakasa. Naye akamhurumia, akanyosha mkono wake, akamgusa, akamwambia, Nataka, takasika. Na mara ukoma wake ukamtoka, akatakasika. Akamkataza kwa nguvu, akamwondoa mara, akamwambia, Angalia, usimwambie mtu neno lolote, ila enenda zako ukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe alivyoamuru Musa kwa kutakasika kwako, iwe ushuhuda kwao.” Ni watu tu wasiotosha, au wasio jitosheleza kisaikolojia ambao wanataka wakifanya jambo wajulikane, waonekane, na watu, ijulikana wema ambao wameufanya, tabia ya aina hiyo ndio huitwa Tabia ya kinafiki.

 

Mtu mnafiki anaweza kuonyesha kuwa anakupenda usoni kumbe moyoni anatamani ufe, uharibikiwe, ushindwe, uchanganyikiwe na kadhalika, Kaini alimwambia ndugu yake twende uwandani kana kwamba wanakwenda bichi kupunga upepo kumbe moyoni amekusudia kumdhuru Mwanzo 4:8-10 “Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye,akamwua. BWANA akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.”

 

Mtu mmnafiki anaweza kuonekana kuwa anakuhug anakukumbatia anakukubali kumbe amekuuza Luka 22:48 “Yesu akamwambia, Yuda, wamsaliti Mwana wa Adamu kwa kumbusu?”mtu mnafiki anaweza kakakubusu kumbe ameshakuuza, wakati wote wanatafuta hila na namna ya kufanya, kuharibu.      

 

Chachu ya Mafarisayo ni tabia ya shetani:-

 

Chachu ya Mafarisayo au dhambi ya mafarisayo ambayo ni Unafiki ni tabia ya shetani yeye ndiye mnafiki wa kwanza, Alionekana yuko bise akimsifu Mungu lakini moyoni alikuwa anatamani kuwa kama Mungu Isaya 14:12-15Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu. Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo.”  Shetani alionekana Mbinguni akijishughulisha na kazi za Mungu, lakini kumbe moyoni alikuwa mnafiki, na hata leo watumishi wake wote hutembea katika tabia yake ya kinafiki 2Wakoritho 11:13-15 “Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.”   

Chachu ya Mafarisayo ni jaribu la wanadamu wote:-

 

Chachu ya mafarisayo Ambayo ni unafiki ni jaribu la wanadamu wote bila kujali kuwa mtu yuko ngazi gani ya kiroho anaweza kuchukuliwa na dhambi hii, awe ni mtume nabii na kadhalika dhambi hii inantafuta mtu awaye yote Petro wakati fulani aliwahi kujaribiwa na dhambi hii na mtume Paulo akamkemea mbele ya wote Wagalatia 2:11-14 1Lakini Kefa alipokuja Antiokia, nalishindana naye uso kwa uso, kwa sababu alistahili hukumu. Kwa maana kabla hawajaja watu kadha wa kadha waliotoka kwa Yakobo, alikuwa akila pamoja na watu wa Mataifa; lakini walipokuja wao, akarudi nyuma akajitenga, huku akiwaogopa waliotahiriwa. Na hao Wayahudi wengine wakajigeuza pamoja naye, hata na Barnaba pia akachukuliwa na unafiki wao. Walakini, nilipoona ya kuwa njia yao haiendi sawasawa na ile kweli ya Injili, nalimwambia Kefa mbele ya wote, Ikiwa wewe uliye Myahudi wafuata desturi za Mataifa, wala si za Wayahudi, kwa nini unawashurutisha Mataifa kufuata desturi za Wayahudi?         

 

Madhara ya Chachu ya Mafarisayo:-

 

Chachu ya mafarisayio yaani ndhambi hii ya unafiki, Yesu aliikemea vikali sana na kuwaonya wanafunzi wake kwanza kuwa wajilinde na dhambi hii ka sababu Yesu alifahamu kuwa ndio dhambi itakayowapeleka wengi motoni Yesu alionyesha kuwa moja ya makundi ya watu watakaopata adhabu ni pamoja na wanafiki  Mathayo 24:48-51 “Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia; akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.”

 

Ukiacha kuwa wanafiki watahukumiwa na kupewa adhabu kali lakini vilevile wanafiki ndio wanaofanya imani ya bwana wetu Yesu Kristo itukanwe kwa sababu wanawafungia watu, wasiuone ufalme wa Mungu huku na wao wenyewe hawaingii ona Mathayo 23:13, “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie.,15 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnazunguka katika bahari na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehanum mara mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe.”

 

Unafiki utaleta aibu kubwa sana siku ya hukumu heri kila mmoja atubu sasa Muhubiri 12:14 “Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.”

Jinsi ya kujilinda na chahu ya mafarisayo:-

Kila mmoja atubie dhambi hii na kuhakikisha kuwa anakuwa mkweli ndani nan je maandiko ynasema Afichaye dhambi zake hatafanikiwa, Bali aziungamaye na kuziacha atapata rehema Mithali 28:13 “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.”

Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye hekima!