Kutoka 8:20-22 “BWANA akamwambia Musa, Inuka asubuhi na mapema usimame mbele ya Farao; angalia! Atoka aende majini; kamwambie, BWANA asema, Wape watu wangu ruhusa waende zao, ili wanitumikie mimi. Au kwamba huwapi ruhusa watu wangu, tazama, nitaleta wingi wa mainzi juu yako wewe, na juu ya watumishi wako, na juu ya watu wako, nao wataingia ndani ya nyumba zako; na nyumba za Wamisri zitajawa na wingi wa mainzi, na nchi nayo ambayo wa juu yake. Nami siku hiyo nitatenga nchi ya Gosheni, watu wangu wanayokaa, ili hao mainzi wasiwe huko; ili kwamba upate kujua wewe ya kuwa mimi ndimi BWANA kati ya dunia.”
Utangulizi:
Watu wengi sana huwa wanachukizwa sana na wakati mwingine wanapata hasira wanaposumbuliwa na Inzi katika nyumba zao, hii ni kwa sababu inzi katiika jamii nyingi wanahusishwa na uchafu, na wakati mwingine pia kusambaza magonjwa hivyo kimsingi inzi hawapendwi na ni machukizo kwa watu wengi sana duniani, wakati mwingine nzi wanaweza hata kutoa milio Fulani ya kuudhi au kujazana mahali, Jambo ambalo linakera na linaleta maudhi na wakati mwingine kuruka ruka katiika miili ya watu! Hata hivyo katika lugha ya kinabii inzi wanapotokea katika nyumba yako wana habari Fulani njema au mbaya ya kukupasha, katika ulimwengu wa kiroho, na hivyo ni muhimu kuwa na usikivu wa rohoni mainzi yanapotawala katika nyumba yako! Tutajifunza somo hili Inzi wanaposumbua nyumba yako kwa kuzingatia maeneo manne yafuatayo:-
i.
Inzi katika mtazamo wa
kibiblia
ii.
Inzi wakiwa ni ishara njema
iii.
Inzi wakiwa ni ishara mbaya
iv.
Mambo ya msingi yakupasayo
kufanya
Inzi katika Mtazamo wa
kibiblia
Hatunabudi kufahamu kuwa nzi ukiacha kwamba ni
wadudu wa kawaida lakini pia wanatazamwa tofauti katika mtazamo wa kibiblia
kwanza wanawakilisha malaika waovu au pepo wachafu, na dhana hii iko katika
maandiko agano la kale na jipya ambapo hata mkuu wao aliitwa Beelzebubu ona
mfano katika
Luka 11:14-15 “Naye alikuwa akitoa pepo bubu; ikawa pepo
alipotoka, yule bubu akanena, makutano wakastaajabu. Wengine wao wakasema, Atoa
pepo kwa Beelzebuli, mkuu wa pepo.”
Katika kifungu hicho cha maandiko Wayahudi
walimshutumu Yesu wakidhani ya kuwa anatumia nguvu za mkuu wa pepo Beelzebuli kutoa Pepo, kumbe yeye
alitoa pepo kwa uweza wa Roho Mtakatifu na alifafanua kuwa shetani hawezi
kumtoa shetani, sio kusudi langu kufafanua jambo hilo kwa undani kwani
ninachikitaka hapa ni kufafanua tu huyu
BEELZEBULI ni nani ? Kimsingi jina
hili Wayahudi walitoka nalo huko ukaldayo na hapa limeandikwa kwa lugha ya
Kiyunani, kiyunani ni BEELZEBOUL ambalo
tafasiri yake ni mkuu wa Pepo wachafu, au mfalme wa pepo wachafu jina ambalo
kimsingi linamuhusu shetani, aidha
katika maandiko pia huko katika nchi ya wafilisti katika mji ulioitwa Ekron
kulikuwa na mungu baali ambaye alikuwa anahusishwa na swala la kufukuza Inzi
huyu aliitwa Baal-Zebub mungu wa
Ekron ona katika
2Wafalme 1:2-4 “Na Ahazia akaanguka katika dirisha la chumba chake
orofani, katika Samaria, akaugua; akatuma wajumbe, akawaambia, Enendeni
mkaulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, kwamba nitapona ugonjwa huu. Lakini
malaika wa Bwana akamwambia Eliya Mtishbi, Ondoka, uende ukaonane na wale
wajumbe wa mfalme wa Samaria, ukawaambie, Je! Ni kwa sababu hapana Mungu katika
Israeli, hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni? Basi sasa,
Bwana asema hivi, Hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika
utakufa. Eliya akaondoka.”
Mungu huyu wa wafilisti aliitwa BAAL ZEBUBU jina ambalo kwa kiingereza humaanisha “BAAL OF FLIES” yaani mungu wa mainzi, mungu huyu alisadikiwa kuwa na uwezo wa kufukuza mainzi, Hakuna
uhakika sana kama kuna muununganiko wa kimaana kwa majina hayo na lile la agano
jipya lakini huyu pia alikuwa ni shetani kwa hiyo bado tunaweza kuona Mapepo na
mashatani yakihusishwa na mainzi, kwa sababu ya uchafu. Au jina lile pepo
wachafu.
Huko Misri nako wakati wa hukumu ya Mungu dhidi ya
Farao ili awaachie wana wa Israel Mungu aliipiga Misri kwa hukumu ya pigo la mainzi
Kutoka 8:20-22 “BWANA akamwambia Musa, Inuka asubuhi na mapema
usimame mbele ya Farao; angalia! Atoka aende majini; kamwambie, BWANA asema,
Wape watu wangu ruhusa waende zao, ili wanitumikie mimi. Au kwamba huwapi
ruhusa watu wangu, tazama, nitaleta wingi wa mainzi juu yako wewe, na juu ya
watumishi wako, na juu ya watu wako, nao wataingia ndani ya nyumba zako; na
nyumba za Wamisri zitajawa na wingi wa mainzi, na nchi nayo ambayo wa juu yake.
Nami siku hiyo nitatenga nchi ya Gosheni, watu wangu wanayokaa, ili hao mainzi
wasiwe huko; ili kwamba upate kujua wewe ya kuwa mimi ndimi BWANA kati ya dunia.”
Kimsingi pigo
hili pia ilikuwa sio hukumu kwa Farao na wamisri tu bali pia kwa miungu ya wamisri,
mungu aliyekuwa anahukumiwa hapa kwa wamisri ambao walikuwa na miungu wengi
mmoja wapo ni mungu aliyekuwa anajihusisha
na kufukuza inzi, kwa uweza wa Mungu alikuwa akionyesha kuwa kama Mungu
akiwatumia inzi kama sehemu ya hukumu miungu hiyo haiwezi kuzuia kusudi kuu
likiwa lile lile Farao aweze kujua ya kuwa Yehova ndiye Mungu pekee duniani.
Kwa hiyo
tunaweza kukubaliana wazi na wazo la kibiblia kuwa inzi wanawakilisha pepo
wabaya na mkuu wao ni shetani, katika lugha ya kinabii, hata hivyo ni muhimu
kufahamu kuwa kinabii inzi wa kawaida wanapoanza kuiandama nyumba yako huwa
kunakuwa na maana za msingi za kiroho zinazowakilishwa maana hiyo inaweza kuwa
ya hatari na mbaya au maonyo ya kutokupuuzia maeneo Fulani muhimu katika maisha
yetu. Inzi kinabii pia wanawakilisha chuki, uovu, au lawama kwa sababu wanaruka
ruka hovyo na kubughudhi watu, wanawakilisha pia tabia mbaya, kukosa kiasi na
hisia mbaya, lakini pia wanawakilisha mambo mazuri kama tunavyoweza kujifunza
katika vipengele vifuatavyo:-
Inzi wakiwa ni ishara njema
Inzi wakiwa na ishara njema huwa wanabeba maana
zifuatazo:-
1.
Inzi wanashiria kuwa kuna
mambo unapaswa kuyafanyia maamuzi magumu - Inzi
wanapokufuata futa katika nyumba yako wanakupa ujumbe kuwa kuna maamuzi magumu
unapaswa kuyafanya ili kuleta mabadiliko makubwa katika maisha yako, yako mambo
aidha unapaswa kuachana nayo, au kuna jambo unapaswa kuliachia kabisa katika
maisha yako, kama iko tabia mbaya ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa
kuharibu maisha yako tabia hiyo iachwe mara moja, kama yuko mtu anakusababishia
kufanya mambo mabaya mtu huyo uachane naye haraka, au mara moja, kuna ujumbe
wanaokupa nzi kuwa kitu hicho kibaya kiondoke katika maisha yako, hivyo
utapaswa kujitafakari na kuangalia ndani yako na mazingira yako na kile
utagundua kuwa ni sababu ya wewe kutokuendelea au kuharibikiwa basi utapata
jibu kuwa unatakiwa kukifukuzilia mbali kama vile tunavyotafuta kuachana na nzi,
tahadhari hapa usichukue maamuzi bila kufikiri kwa kina na ukijisikilizia kwa
ndani ndipo utagundua ni kitu gani watu au mtu gani mbaya anakusababishia mkwamo
katika maisha kisha utatafuta njia mbadala za kuachana na jambo hilo kwa amani!
2.
Inzi wanakupa taarifa ya
jambo jipya kutokea katika maisha yako – Ishara ya nzi sio tu wakati wote ni mbaya kama
watu wanavyodhani lakini wanapokuandama inamaanisha kuwa kuwa kuna kitu
kinaenda kuisha au kufikia mwisho katika maisha yako na jambo jipya kabisa linaenda kutokea katika
maisha yako, ni ishara ya kuisha kwa jambo Fulani katika maisha yako na kuanza
kwa jambo jipya kabisa, hivyo kuwaona inzi wazi wazi kabisa au kwenye
ndoto ni ujumbe ambao unakueleza
kuangalia jambo jipya kabisa katika maisha yako, a kulipokea vizuri kwani
mabadiliko hayo yanaweza kuleta nafasi
usiyoitarajia.
3.
Inzi wanakupa taarifa ya
kwamba kuna jambo linalokuondolea umakini - aidha unalijua au hulijui kama ni mtu aidha
unamjua au humjui anakunyima usingizi, anakusumbua au ndio sababu ya
kuharibikiwa kwako na kukuletea migandamizo katika moyo , unapoona inzi fikiria
kwa kina kama kuna mtu katika maisha yako uwe unamjua au humjui anasababisha
mabaya katika maisha yako iwe unajua au hujui, mtu huyo lazima umfanyie mkakati
wa kumuacha au kuharibu nguvu anayoitumia kuharibu maisha yako mtu huyo aondoke
au uache mawasiliano naye katika maisha yako kabisa. Kumbuka isiwe kwa ugomvi
Mungu ametuita katiia mani.
4.
Inzi wana ujumbe kuwa kuna
watu au mtu unampuuzia – kama
unavyoona inzi wanapotusumbua huwa tunawapuuza, na kuwafukuza kwa dharau japo
nzi hao hawataenda mbali na wataendelea kutusumbua hii ni ishara kuwa kuna watu
wanakuhitaji lakini unawapuuzia hujawapa kipaumbele, ni mtu au watu wanaokupenda
sana lakini umewapuuzia, au ni marafiki wa maana sana lakini umewapuuzia,
inawezekana hata wakituma ujumbe unawapuuzia hujibu, anza kujihoji kwa makini, na kwa uangalifu
mkubwa kama umepuuzia na kuharibu urafiki na watu muhimu katika maisha yako au
umeshindwakugundua umuhimu wa watu hao tunza na kurudisha urafiki haraka imarisha
mahusiano na wote walio muhimu kwenye maisha yako
5.
Inzi wanakupa taarifa wazi
kuwa unakabiliwa na hofu – Hofu hii ni hofu ya kupoteza mtu wa karibu sana
umpendaye au kupoteza kazi, labda mambo hayaendi vizuri kazini na una mashaka
ya kupoteza kazi hivyo kuna hofu inaanza kujengeka ndani yako, inzi
wanakutaarifu kuhusu hofu yako ili uweze kujihami mapema kwa kufikiri kuondoka
kazini au kutafuta kazi nyingine ambayo itaendana na hisia zako na kuachana na
ile inayokupa mikandamizo ya moyo.
6.
Inzi wanawakilisha uwezo
wako wa kukabiliana na mazingira – Inzi wanakupa ujumbe kwamba wewe sio wa kupuuzwa
kuna nguvu kubwa ndani yako ya kukabiliana na mazingira nzi wanauwezo wa kuishi
kokote na katika mazingira yoyote yawe mazuri au mabaya, wanauwezo wa kujipatia
chakula hata katika mazingira yanayofikiriwa kuwa hayafai, wana wanakupa ujumbe kuwa hata wakikutupa
kama taka taka wewe ni hazina kwa wengine, inzi wanakupa ujumbe wa kufanikiwa,
kuwa na vingi sana kuwa tajiri, kuwa na uwezo mkubwa wa kuhamasisha watu kuwa
na uwezo wa kuishi katika mazingira hata ya kukataliwa, uwezo mkubwa wa
kuvumilia magumu, huku ukiendelea na maisha na kujitafutia chakula , inzi
wanakukumbusha kuwa wewe ni mtu mgumu sana
na unaweza kukabiliana na mazingira yoyote yanayobadilika, yawe mazuri
au mabaya.
7.
Inzi wanakukumbusha kuwa
una hasira - na kwamba unatakiwa kumudu hasira yako,
katika maisha, inzi hatuwezi kuwadhibiti sisi wenyewe kwa msingi huo, hata hasira lazima tujifunze
namna ya kuidhibiti ili isituletee madhara
Inzi wakiwa ni ishara mbaya
Inzi pia wana ujumbe mbaya
na wa kuvunja moyo
1. Inzi wanaujumbe wa kukutaarifu kuwa kuna jambo
baya. – kuna jambo
baya lisilopendeza, la kuudhi au lenye kuingilia mipango yako na kukuharibia
kama vilevile tunavyoona inzi wakiwa wasumbufu, wenye maudhi na kutua tua
katika mazingira tusiyoyapenda ndivyo wanavyoashiria kuwa kuna tukio
litaingilia kati katika maisha yako kulete usumbufu, kukuharibia kukukatisha
kukuudhi na kadhalika au jambo la kukuondolea amani, na au kukupa fadhaa, kiroho
unajua nini unachopaswa kukifanya kuifuta hali hiyo.
2. Inzi ni taarifa ya kifo – Kwa kawaida inzi pia
wanapenda kitu kilichokufa au kilichooza au chenye harufu mbaya au shombo, nzi
wanapoonekana katika ndoto au halisi wakiwa nyumbani kwako huashirikia kifo cha
mtu aliye karibu sana na wewe ambaye hungependa afe hata hivyo Inzi pia wana ishara ya ufufuo,
kwa kuwa huzaliwa kama yai kisha buu kisha inzi hutokea kwa hiyo kuna ishara ya
maisha mapya.
3. Uwepo wa Inzi pia huashiria kuvunjika kwa
mahusiano, - kwa hiyo watu
wanapaswa kuzungumzia mahusiano yao ili ikiwezekana wayajenge kama wanaweza
kuimarisha uhusiano wao na kila mmoja ajali hisia za mwenzake, kama watu
hawataimarisha mahusiano yao ni dalili inayoonywa na nzi kuwa uhusiano
unakwenda kuvunjika, inzi wanakupa ishara mbaya ya matukio mabaya ya kiroho,
hivyo tunapowaona tunaweza kurekebisha hali ya mambo isiwe mbaya vinginevyo
kitu kibaya kinakwenda kutokea na watu watafukuzana kama unavyofukuza inzi.
4. Inzi wanashirikia haribiko – inaweza kuwa haribiko
ambalo limekwishatokea au linalokwenda kutokea, labda ulikuwa ukifanya kazi na
kuwafurahisha wanaokuzunguka na kukuajiri na umesahahu jambo muhimu sana
unalotakiwa kulifanya sasa unapaswa kuangalia kile unachotakiwa kukifanyia kazi
na kile kinachohusina na maisha yako, panga mipango yako mwenyewe na kaa katika
hiyo ili uweze kufikia malengo, vunja malengo makubwa na angalia madogo ambayo
unayamudu inaweza kuwa jambo sahihi kwako, kama unagundua kuwa umetoka katika
mpango anza kujipanga sasa panga mpango
utakaokufaa ni rahisi kuwa kutokujisikia vizuri lakini itakusaidia kufanya
mambo ya muhimu.
5. Huwezi kufanya lolote – Inzi wanakupa ujumbe kuwa
mambo yanayokutokea au yatakayokutokea yako nje ya uwezo wako huwezi kuyadhibiti
kinachokutokea kiko nje ya uwezo wako kama unavyoona inzi hujawaleta wewe
unawaona tu na wanakuletea usumbufu ndivyo ilivyo katika maswala yanayokutokea
au yatakayokutokea kwa imani kumbuka tu
kuwa Mungu anatawala.
Mambo ya msingi yakupasayo
kufanya
Hakuna sababu ya kuogopa unapoona inzi katika
nyumba yako, hawako hapo kwa makusudi ya kukutisha lakini wako hapo kukupa ujumbe
kuhusu mambo yajayo, hivyo jipange jipe moyo kaa tayari kukabiliana na lolote
litakalokusibu, weka moyo wako kwenye mipango yako, wasiliana na watu muhimu
sana katika maisha yako, fanya kazi kwa bidii weka mahusiano yako vizuri,
usiogope jambo baya wala taarifa mbaya jiandae kukabiliana na lolote gumu
litakalokukabili, Muombe sana Mungu kwa kuahirisha mambo mabaya na kumshihi
Mungu alete mambo mema siku zote za maisha yako, hakikisha kuwa unakuwa safi
kwani kama jinsi ambavyo inzi wanavutiwa na uchafu, lisiwepo ovu katika maisha
yako litakalokuchafua.
KUMBUKA. Mafundisho haya ya katika
shule za kinabii na kama imani yako inakinzana usitilie maanani wala
usifundishe kanisani kwako!
Rev. Innocent Samuel Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye
Hekima!