2Timotheo 2:15-18 “Jitahidi kujionyesha
kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia
kwa halali neno la kweli. Jiepushe na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya
dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu, na neno lao litaenea kama
donda-ndugu. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto, walioikosa ile kweli,
wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata kuipindua imani ya watu kadha
wa kadha.”
Utangulizi:
Ni muhimu kufahamu kuwa tunaishi
katika nyakati za mwisho sana, katika nyakati hizi, kumekuwepo na madhehebu
mengi sana na kila dhehebu lina misimamo yake na mafundisho yake, hata hivyo
kila Mkristo ana wajibu wa kuhakikisha kuwa yeye mwenyewe anakuwa na ujuzi wa
kutosha kuhusu Neno la Mungu na namna linavyotumiwa ili aweze kupambanua nani
analitumia neno la Mungu kwa halali na nani analitia maji, yaani kulighoshi,
kughoshi ni Kiswahili cha zamani chenye maana ya kuongeza maji, mfano unapokuwa
na maziwa halisi, sasa ili yawe mengi unaongeza na maji yaani kuchakachua, kwa
hiyo katika nyakati zetu hizi vilevile tunao watu wanaolichakachua neno la
Mungu hivyo kila mmoja anapaswa kuwa na akili ya kujua nani anachakachua neno na
ni nani analitendea haki, huu ni wajibu wa kila Mkristo na kila mwanafunzi wa
Yesu!
2Wakorintho 2:17 “Kwa maana sisi si kama
walio wengi, walighoshio neno la Mungu; bali kama kwa weupe wa moyo, kama
kutoka kwa Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo.”
Tatizo liliopo ni kuwa kila mtu duniani
anaweza kuwa na tafasiri yake kuhusu neno la Mungu na akafikiri kuwa yuko
sahihi, kwa sababu kila mtu anasema anaifuata Biblia anaiamini Biblia lakini
wakati huo huo tunashuhudia kuwepo kwa tafasiri na misimamo tofauti tofauti
kuhusu neno la Mungu, sasa basi, ikiwepo miongozo muhimu itatusaidia katika
kulitumia neno la Mungu kwa halali na kuepuka changamoto nyingi zinazoweza
kujitokeza, Mungu ni Mungu wa Utaratibu na sio Mungu wa Machafuko! Kwa hiyo ni wajibu wa Kila Mkristo
kuyachunguza maandiko ili kujithibitishia kama kilichohubiriwa ni cha kweli
bila kujali anayehubiri ni mtu wa namna gani au ana heshima kiasi gani hivyo
ndivyo walivyokuwa watu waungwana katika kanisa la Baroya alipohubiri Paulo
Mtume ona
Matendo 17:10-11 “Mara hao ndugu
wakawapeleka Paulo na Sila usiku hata Beroya. Nao walipofika huko wakaingia
katika sinagogi la Wayahudi. Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa
Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza
maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.”
Watu wa Beroya walikuwa
waungwana, kwa mujibu wa Luka kwanini kwa sababu bila kujali nani anahubiri
walifanya kazi ya kuyachunguza maandiko kila siku ili wajithibitishie kuwa
yanayohubiriwa ni kweli? Mungu hapendezwi na makundi makubwa ya watu ambao
wanabaki kuwa maamuma kila siku, wajinga wasio na mafunzo, wasiothibitishwa,
wasio na ujuzi kwa kiingereza wanaitwa
LAY waliolala au LAY PERSON a person who is not trained, not qualified or
not having an experience in a particular subject or activity unaona kwa wakatoliki wanaitwa WALEI, Mungu
hajatuita ili tuendelee kutengeneza kundi kubwa la watu wajinga Agizo kuu
linatutaka kuwafanya watu wote kuwa wanafunzi, wawe wenye kufaa Qualified wajue neno, wachambue neno, watafasiri neno
wahoji maswali, wajibu maswali watengeneze mijadala yenye faida wawe wakomavu !
Waelimike
2Timotheo 4:1-4 “Nakuagiza mbele za Mungu,
na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa
kwake na kwa ufalme wake; lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati
usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. Maana
utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia
zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya
utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za
uongo”
Waefeso 4:11-14 “Naye alitoa wengine kuwa
mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa
wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya
huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia
umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata
kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe tena watoto
wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa
hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.”
Kwa msingi huo leo tutachukua
muda kutafakari na kujifunza kwa makini somo hili la thamani Kutumia kwa halali
neno la kweli kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo:-
·
Maana ya
kutumia neno la Kweli kwa halali
·
Jinsi ya
kutumia neno la kweli kwa halali
·
Kanuni za
kutumia neno la kweli kwa halali
Maana ya kutumia neno la kweli kwa halali.
2Timotheo 2:15 “Jitahidi kujionyesha kuwa
umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa
halali neno la kweli.”
Paulo mtume alikuwa anamuagiza
Timotheo aliyekuwa Askofu wa Makanisa ya Efeso kuhakikisha kuwa analitumie neno
la Mungu yaani neno la Kweli kwa halali, Neno la kweli linalotajwa hapo ni Neno
la Mungu yaani Biblia, kwa hiyo Mwalimu wa neno la Mungu anaagizwa hapo
kuhakikisha kuwa analitumia kwa halali, nini maana ya kutumia neno la kweli kwa
halali?
Ili tuweze kuelewa Mstari huu
vizuri na kuweza kuweka msingi wa somo letu vizuri kwanza nitauweka mstari huu
katika kiingereza
“Study to shew thyself approved unto God, a
workman that needeth not to be ashamed, rightly dividing the word of truth”
Kwa hiyo katika Biblia ya
kingereza KJV ambayo ndiyo iliyotumika kuleta Biblia ya Kiswahili kwetu Mstari
huo unasomeka namna hiyo, sasa nikianza na neno kutumia kwa halali neno la
kweli, RIGHT DIVIDING tafasiri ya kiyunani
ya neno hilo ni “ORTHOTOMOUNTA” ambalo ni neno la Kiyunani linaloundwa na
misamiati miwili yaani “ORTHOS” na “TOMO” Orthos maana yake ni Perfectly
right au Staright na neno Tomo ni CUT
kwa hiyo neno ORTHOTOMOUNTA maana
yake mega sawa sawa, au kata sawasawa, au kata kwa ukamilifu, maana yake hasa inatokana na asili ya kiroho
ya neno kugawa mkate, au kuumega mkate
Matendo 2:46-47 “Na siku zote kwa moyo
mmoja walidumu ndani ya hekalu, WAKIMEGA MKATE nyumba kwa nyumba, na kushiriki
chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe, wakimsifu Mungu, na kuwapendeza
watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.”
Neno la Mungu ndio Mkate wetu
wenyewe kwa hiyo wakati wa kuuvunja mkate mvunjaji anatakiwa aukate sawasawa,
kama vile watu wanavyokata keki na kutoa vipande vyenye uwiano ili kile
kitakachomfikia mtu kiwe sawasawa bila upendeleo, kwa hiyo Lugha hii ndiyo
inayotumiwa katika kuelezea namna tunavyopaswa kulitumia neno la Mungu kwa
halali na sio kama kila mtu atakavyo au kila kanisa litakavyo au kila dhehebu
litakavyo bali kama Mungu atakavyo ona
2Patro 1:19-20 “Nasi tuna lile neno la
unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, Kama taa ing'aayo mahali penye
giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka
mioyoni mwenu. Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko
upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.”
Unaona? Kwa msingi huo sio sawa
kwa mujibu wa maandiko kwamba kila mmoja ajitafasirie maandiko kama apendavyo
hapana, haiko hivyo, huwezi tu kwenda kwenye maandiko na ukachukua tu chpchote
unachoweza kuchukua na kuunga mkono mawao yako au njia yako, Mungu katika
hekima yake ameweka namna ya kuyatafasiri maandiko na ndio maana kuna umuhimu
wa kujifunza neno la Mungu kama tunavyoweza kuona katika kipengele kifuatacho,
hilo sasa linatuleta katika kutafakari kipengele cha pili
Jinsi ya kutumia neno la kweli kwa halali
Mungu ni Mungu wa utaratibu na
wala sio Mungu wa machafuko!, Mungu ndiye mwanzilishi wa Muda, aliuumba
ulimwengu kwa siku sita, na kila siku ilikuwa ni masaa 24, Mungu aliumba
ulimwengu na akaweka anga, leo hii kutokana na maendeleo makubwa ya kisayansi,
tumegundua kuwa ziko sayari kadhaa ambazo hulizunguka jua, nazo zimewekewa
utaratibu na ndio maana hazigongani! 1Wakorintho
14:40 “Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na
kwa utaratibu.”
Taratibu zote zilizoko Duniani
zimewekwa na Mungu, na wakati mwingine Mungu pia huweka watu wazazilishe au
wasimamie utaratibu, ili mambo yote yatendeke kwa utaratibu, fikiria kwa mfano
waliochinga baba bara kwa nchi zilizotawaliwa na uingereza magari barabarani
hupita upande wa kushoto kwa njia ya kule linakoelekea gari, na zile zinazorudi
hupita kushoto kwao ambako huwa ni kulia kwa anayekwenda, utaratibu wa namna
hii pamoja na sharia zake barabarani ndio unaopelekea kuwepo kwa usalama na
kupungua kwa matukio ya ajali, jaribu
kuwaza kama kusingelikuwa na utaratibu? Fikiria Hospitalini kwenye matibabu, Kama
madaktari wangekuwa wanaandikia watu dawa hovyo hovyo, bila kuzingatia miaka,
uzito, aina ya ugonjwa na dozi, je usalama wa wagonjwa ungekuwaje? Mashuleni Kama kusingelikuwa na maswala ya
hatua, wala silabasi wala walimu wa somo husika wala utaratibu wa vipindi
kungekuwaje? Kungekuwa na machafuko na ukiangalia kwa makini utaweza kuona
ilimutaratibu uweze kwenda vizuri watu wote hata madereva huwa wanaambiwa
wasome, wasomee fani zao ili waweze kuufuata utaratibu uliokusudiwa katika
Nyanja zao unaona? Sasa ili neno la
Mungu liweze kutumiwa kwa halali Paulo anamwambie Timotheo
2Timotheo 2:15 “Jitahidi kujionyesha kuwa
umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa
halali neno la kweli.”
Naomba tena niweke mstari huu
katika kiingereza cha Biblia ya KJV King James Version mstari huo unasomeka
hivi?
“Study to shew thyself approved unto God, a
workman that needeth not to be ashamed, rightly dividing the word of truth”
Paulo mtume anapomwagiza Timotheo
kutumia neno la Mungu kwa halali anaanza nan neno la Msingi kwenye Kiswahili JITAHIDI neno hilo KJV imetumia neno STUDY katika kiyunani ni SPOUDAZO ambalo
maana yake ni BE DILIGENCE yaani makinika, au chukua tahadhari zote
au jielimishe study kwa hiyo Mtafasiri
wa maandiko au Mwalimu wa neno la Mungu anapaswa kutia bidi, kuwa makini,
kusomea, kutafuta kwa bidi kutafasiri neno la Mungu kwa halali ili ampendeze
Mungu, kama hatutakuwa makini na kila mtu akatafasiri maandiko anavyojisikia na
atakavyo uelewa kuhusu Mungu na maagizo yake utakuwa haufanani duniani na neno
hilo hilo litakuwa halijatumiwa kwa halali jambo litakalotuletea hukumu kubwa
zaidi
Yakobo 3:1-2 “Ndugu zangu, msiwe waalimu
wengi, mkijua ya kuwa mtapata hukumu kubwa zaidi. Maana twajikwaa sisi sote pia
katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu,
awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.”
Msiwe waalimu wengi kwa kiyunani DIDASKALOS yaani Doctors, Master teacher, neno hilo limetumika kumtaja Yesu mara 40 kama Mwalimu Master na limejitokeza katika biblia mara 58 katima mistari tofauti
57 yote ikionyesha mtu aliyebobea katika kufundisha, Mtaalamu wa kutafasiri
maandiko au Mwalimu wa neno anatakiwa awe mtu aliyebobea na ili mtu awe mbobevu
anapaswa kuwa na bidi katika kujifunza na kujisomea, kwa hiyo kimsingi maandiko
yanatutaka tuwe wabobezi yaani tusomee, na ndio maana katika vyoa vya Biblia
liko somo maalumu kwaajili ya kusomea jinsi na namna nzuri ya kutafasiri neno
la Mungu somo hilo linaitwa
HERMENEUTICS, somo hilo haliwezi kufundishwa katika somo moja kama hivi,
lakini hapa nakupa tu tahadhari ya kawaida ili ujue kuwa sio kila mtu anaweza
kuwa Mwalimu wa neno la Mungu na kazi hii ni taaluma kama zilivyo taaluma
nyingine, Upako jni wa Muhimu, lakini na upako unaweza kumilikiwa na mtu
yeyote, karama ni za Muhimu nazo zinaweza kumilikiwa na mtu yeyote tu, hata
hivyo, kutafasiri maandiko kunahitaji maarifa na ndio maana kuna walimu,
kumbuka Naye alitoa wengine kuwa Mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na WALIMU kwa hiyo ni kazi ya wabobezi
kutuingiza katika huo utaalamu wa kutafasiri maandiko HERMENEUTICS sio mtu anaamka tu na ndoto zake na anakuwa muhubiri,
kama jinsi ambavyo Dakrati haamki tu na kuwa daktari ili ashughulikie miili ya
watu hali kadhalika hainuki tu Mtu na kusema ni muhubiri na mtafasiri wa neno
la Mungu kama kujifunza na kukaa chini ya walimu utakupuuzia tutakuwa na
wazushi wengi sana katika karne hii, waalimu wote wazuri akiwepo Yesu mwenyewe
walikaa chini nya walimu kwanza kabla ya kuwanza kuwa walimu wa neno la Mungu,
wako watu ambao hujidhani kuwa ni wa kiroho sana na wanapuuzia sana swala la
kusoma wakifikiri kuwa ni kupoteza Muda wako wanaodhani kuwa kwa kuwa wamejaa
Roho Mtakatifu basi hawahitaji kujifunza hapana Roho wa Mungu huwa anaongoza
watu wakajifunze kwanza kabla ya kuwatumia
-
Musa alipata Elimu ya kawaida kule Misri kwa
umri wake wote miaka 40, na kisha alijifunza maswala ya kiroho kwa Kuhani wa
Midian Yethro kwa miaka 40 jambo hili lilipelekea Musa kuwa Mwalimu mzuri sana
na kiongozi aliyeandaliwa kuweka misingi ya kiroho, kisiasa, kisheria na
maongozi na taratibu zote duniani
Matendo 7:22 “Musa akafundishwa hekima yote ya
Wamisri, akawa hodari wa maneno na matendo.”
-
Yesu
Kristo Bwana wetu alikaa chini ya waalimu kabla ya kuwa Mwalimu ona Luka 2:
46-47 “Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni,
ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. Nao wote
waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake.” Unaona na
zaidi ya yote alijifunza kwa Mungu Roho Mtakatifu nay eye alikaa na wanafunzi
wake miaka mitatu na nusu ndipo akawaamuru wakahubiri injili
-
Paulo
Mtume alikaa chini ya Mwalimu maarufu aitwaye Gamaliel Matendo 22:3 “Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa
Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa
sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihadi kwa Mungu kama ninyi
nyote mlivyo leo hivi;” Paulo mtume licha ya kukaa chini ya
Mwalimumaarufu Gamaliel na kujifunza maswala ya torati pia alikaa chini ya Roho
Mtakatifu miaka 14 akijifunza injili aliyotukabidhi, ambayo alifundishwa na
Yesu mwenyewe ona
Wagalatia 1:11-20 “Kwa
maana, ndugu zangu, injili hiyo niliyowahubiri, nawajulisha ya kuwa siyo ya
namna ya kibinadamu. Kwa kuwa sikuipokea kwa mwanadamu wala sikufundishwa na
mwanadamu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo. Maana mmesikia habari za mwenendo
wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba naliliudhi kanisa la Mungu kupita
kiasi, nikaliharibu. Nami naliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi
walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika
mapokeo ya baba zangu. Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu,
akaniita kwa neema yake, alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili
niwahubiri Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na
damu; wala sikupanda kwenda Yerusalemu kwa hao waliokuwa mitume kabla yangu;
bali nalikwenda zangu Arabuni, kisha nikarudi tena Dameski. Kisha, baada ya
miaka mitatu, nalipanda kwenda Yerusalemu ili nionane na Kefa, nikakaa kwake
siku kumi na tano. Lakini sikumwona mtume mwingine, ila Yakobo, ndugu yake
Bwana. Na hayo ninayowaandikia, angalieni, mbele za Mungu, sisemi uongo.”
Aidha licha ya
kuwa alifundishwa na Yesu mwenyewe mtume huyu ambaye alikuwa mwana sharia pia
alikuwa na bidi ya kujisomea na alisisitiza kuwa wahubiri wajisomee ona 2Timothy 4:13 “Lile
joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa, ujapo ulilete, na vile vitabu, hasa vile
vya ngozi.”
Kwa hiyo Paulo
anapomtaka Timotheo awe na bidii katika kujisomea alimaanisha kuwa huwezi
kumtenga Muhubiri na tabia ya kujisomea, kutafakari na kuandaa neno la Mungu
sawa na kanuni alizozikusudia Mungu, kila Muhubiri ni Mwalimu na hivyo kila
Muhubiri anapaswa kusoma na kujisomea, kwenda shule na kuendelea kuwa na tabia
ya kujisomea siku zote za maisha Yetu, kufundisha na kuwaelezea watu neno la
Mungu hakupaswi kuwa kwa kukurupuka tu, Kanisani hakuna wajinga kuna watu
wengine ni wasomi, wengine ni viongozi wengine wana akili wengine wana ujuzi,
kwa hiyo sio mahali ambako utaokota biblia na kuondoa vumbi na kwenda kusema tu
ili mradi unajua kusagia watu hapana kuna kanuni zake kuna hatua zake kuna
utaratibu wake
Isaya 28:9-13 “Atamfundisha
nani maarifa? Atamfahamisha nani habari hii? Je! Ni wale walioachishwa maziwa,
walioondolewa matitini? Kwa maana ni amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni
juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo. La, bali kwa
midomo ya watu wageni, na kwa lugha nyingine atasema na watu hawa; ambao
aliwaambia, Hii ndiyo raha yenu, mpeni raha yeye aliyechoka; huku ndiko
kuburudika; lakini hawakutaka kusikia. Kwa sababu hiyo neno la Bwana kwao
litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni
juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo; ili waende na kuanguka nyuma, na
kuvunjwa, na kunaswa, na kuchukuliwa.”
Kwa hiyo watu
wanaohudumia roho za watu hawapaswi kuwa watu wa kuokota okota tu hapana
wanapaswa kuwa watu wenye akili timamu, sio waliochoka, wala vichaa bali watu
wenye akili na wanaojua kujifunza walio hodari katika maandiko ili waweze
kuijenga jamii kwa hiyo tusifikiri kuwa Mungu anafurahia neno lake lipotoshwe
tu hata wewe unaweza kuwa mkali pale watu wanapokunukuu vibaya,Kama tunamuheshimu Mungu hatuna
budi basi kuyaheshimu na mambo yake badala ya kuibuka tu kama uyoga na
ukachezea roho za watu, tukifanya hivyo kutakuwa na uwiano sawia wa ujuzi wa neno la Mungu kwani ndio maana
Yesu aliagiza kuwafanya watu wote kuwa wanafunzi. Hilo sasa linatuleta katika
mkutafakari kipengele cha tatu na cha mwisho
Kanuni za kutumia neno la kweli kwa halali
Kutafasiri neno la Mungu ni
taaluma, ni sayansi, ni elimu na iko miiko ya jinsi na namna ya kulitafasiri
neno la Mungu, kanuni hizo zikizzingatiwa kutakuwa na upungufu mkubwa wa
tafasiri za neno la Mungu na watu hawatatafasiri maandiko kama wapendavyo tu bali
sawa na kanuni zilizoainishwa na kupendekezwa kitaalamu, Sayansi hii ya
kutafasriri neno la Mungu inaitwa Hermeneutics hermeneutics ni nini kwa
kiingereza
1. Hermeneutics
is a branch of Science that deals with the interpretation of scriputres
especially the Bible
2. Hermeneutics
ni tawi la Maarifa linalohusika na utaalamu (kanuni) wa kutafasiri maandiko
hususani Biblia
Sina mpango wa kufundisha somo
hilo hapa, kwani haya ni maubiri tu, lakini nataka kutoa maswala ya kuzingatia
wakati mtu anataka kufundisha neno la Mungu au kuhubiri, hii ni kwaajili ya
watu wa kawaida watu wote, sio kwaajili ya wahubiri na wachungaji waliokwenda
au waliopo vyuoni japo nimezingatia sana kuwafaa watu wote kama Neno la Mungu
lilivyo:-
Ni muhimu kufahamu kuwa kwa nini
Biblia inahitaji tafasiri? Au kutumiwa kwa halali, tunaweza kusema kuwa je
Mungu si amewakusudia watu wote wafikiwe na neno lake jibu ni ndio lakini watu
hao wana Historia tofauti, tamaduni tofauti, lugha tofauti, na muda au nyakati
tofauti kwa hiyo kuna vitu vya kuzingatia wakati mtu anataka kutafasiri neno la
Mungu, ndio maana umeweza kuona kwa mfano Paulo anamwambia Timotheo JITAHIDI katika Kiswahili lakini katika
kiingereza STUDY bila kucheza na
lugha iliyokusudiwa unaweza kujikuta hupati maana iliyokusudiwa! Kwa hiyo
Lugha, Tamaduni, Historia, na muda unaweza kuwa kwazo kwa Muhubiri na mtafasiri
wa maandiko na ndio maana tunahitaji miongozo! Miongozo hiyo inatusaidia
1- Kulijua
wazo kamili la Mungu alilolikusudia katika neno lake
2- Kuzuia
tafasiri zisizo za kweli ya neno la Mungu
3- Kuzuia
kupotoshwa kwa lengo la injili
4- Kuzuia
hukumu ya Mungu
5- Kuleta
uwiano wa ufahamu na mwenendo na tabia kwa wanafunzi wa Yesu duniani
6- Maandiko yanahitaji Mtafasiri au
mfafanuzi juhudi ya kusoma pekee haitoshi mpaka mtu akufafanulie ona Matendo 8:30-31 Biblia inasema hivi “Ndipo Filipo akakimbilia na kumsikia yule mtu anasoma
kitabu cha nabii Isaya. Filipo akamwuliza, Je, yanakuelea hayo usemayo? Yule
towashi akasema, Nitawezaje kuelewa mtu asiponifafanulia? Hivyo akamkaribisha
Filipo ili apande na kuketi pamoja naye”.
Kwa hiyo kumbe kanuni zitasaidia
kwa kiwango kikubwa kupunguza au kuondoa kabisa changamoto na kutokuruhusu
uzushi kulivamia kanisa la Mungu na kuondoa utata wa kiufahamu, kwa sababu
Mungu anataka tuwe na nia moja
1. Mtafasiri
wa maandiko wakati wote anapaswa kuwa na NIA
NJEMA Hakikisha kuwa una moyo safi, unakwenda katika maandiko kwa kusudi la
kutafuta jambo jema la kuijenga jamii Matendo
24:16 “Nami ninajizoeza katika neno hili niwe na
dhamiri isiyo na hatia mbele za Mungu na mbele ya watu siku zote.” Unaweza
kuwa msomi na unaweza usiwe msomi, lakini Mungu huchunguza nia ya moyo,
huiangalia dhamira, unapodhamiria kuifundisha kweli unajiweka salama mbele za
Mungu na unapodhamiria kupotosha kama balaam Mungu anaiona nia yako, kwa hiyo
ili mtu awe na nia njema na dhamiri safi ni lazima awe na hofu ya Mungu nah ii
ikiwepo utalichukulia neno la Mungu kwa tahadhari kubwa.
2. Neno
la Mungu limevuviwa kwa sababu hiyo kila mtu mwenye nia njema na dhamiri safi
anapotaka kulitumia kwa kusudi la kuwasaidia watu wa Mungu, kuwaonya,
kuwakemea, na kuwakamilisha anaweza bado kuwa kwenye upande sahihi ona 2Timotheo 3:16-17 “Kila
andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa
yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe
kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.”
3. Kumbuka
kwamba maandiko yana tabia ya kujitafasiri yenyewe kwa msingi huo uko umuhimu
wa kuzingatia andiko lingine na lingine linalolingana au kuunga mkono wazo la
kile unachotaka kukisimamia, maana yake huwezi kuwa na fundisho linalotokana na
Mstari mmoja kwa hiyo kila neno lithibitike kwa kina cha ushahidi wa maandiko
mengine zaidi 2Wakorintho 13:1 “Hii ndiyo mara ya tatu ya mimi kuja kwenu. Kwa vinywa vya
mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa.” Kwa hiyo
mtafasiri wa maandiko anapaswa kuzingatia uwiano wa fundisho lake na maandiko
mengine au na biblia nzima uwiano huo wa kimaandiko unaitwa “cross
references” yaani nukuu ya andiko moja ama linguine linalofanana na lile
unalotaka kuelezea fundisho lako
4. Wakati
mwingine ni salama Kurahisisha maandiko kwa kuyachukua kama yalivyo badala ya
kufikiri kuwa kila andiko ni fumbo, watu wengi wanaodhani kuwa maandiko ni
mafumbo wanaweza kushawishika kutafasiri kila kitu hata vile ambavyo havihitaji
tafasiri, na matokeo yake wanapotosha, Hata hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari
kwani pia sio kila andiko unaweza kulichukua kama lilivyo kwa mfano
2Wafalme 6:25 “Biblia
ya Kiswahili inasema hivi Njaa ikawa kuu huko Samaria; na tazama, wakauhusuru,
hata kichwa cha punda kikapata kuuzwa kwa vipande themanini vya fedha, na
kibaba cha mavi ya njiwa kwa vipande vitano vya fedha.”
Unapoona neno
Kibaba cha mavi ya njiwa na ukachukua neno hilo kama lilivyo ni rahisi kufikiri
kuwa Samaria kulikuwa na njaa mpaka mavi ya njiwa yaliuzwa! Jambo hilo sio
sahihi na hapo ndipo unapoweza kuona umuhimu wa sayansi ya kutafasiri maandiko,
andiko hilo hilo ukilisoma katika biblia ya kiingereza linasomeka hivi
2Kings 6:25 “There
was agreat famine in the city; the siege lasted so long that a donkey’s head
sold for eighty shekels of silver and quarter of a cab of seed pods for five
shekels”
Unapoanza tu
kuangalia andiko hilo kitaalamu kwa kuanza kuangalia Lugha iliyotumika katika
matoleo tofauti tofauti ya buiblia utagundua kuwa neno KIBABA CHA MAVI YA NJIWA, kwa kiingereza CUB OF SEED maana yake ni
KIBAKULI CHA MBEGU kwa hiyo kwa maamuma kuchukua njia rahisi au kurahisisha
tu kunaweza kuwa salama na kunaweza kuwa hatari ndio maana maandiko yanahitaji
wataalamu.
5. Andiko
au mstari unaotaka kuubiri au kuutumia lazima uzingatie wazo zima MUKTADHA wa kile kilichokuwa
kinazungumziwa hapo karibu na wazo zima la kibiblia, huwezi kuchukua nyuzi moja
na kuiita nguo, nguo ni mkusanyiko wa nyuzi nyingi. Hakuna andiko lolote katika Biblia ambalo likitafasiriwa vizuri
kwa kuzingatia Mazingira yake MUKTADHA
litaleta utata wa kimaandiko. Na kama utata utatokea basi mtafasiri atapaswa
kuelezea utata huo, bila kutafuta kupuuzia ukweli unaofunuliwa na andiko hilo
6.
Panua ufahamu wako kuhusu Lugha na matumizi ya lugha katika Biblia
kuna lugha za mafumbo Kuna aina mbalimbali za Lugha za
mafumbo zinzotumika katika Biblia inasemekana ziko lugha za mafumbo
zilizotumika katika Biblia zaidi ya 200 pamoja na mifano yake ipatayo 800 lugha
hizo za mafumbo ni kama vile:-
·
Misamiati – (Vocabulary)
·
Mifano na fumbo la maneno (Parable
and allegories)
·
Ulinganisho unaotumia maneno kama,
na na ulinganishi usiotumia neno kama na (Similes and Metaphors)
·
Maneno ya kuongoza chumvi (Hyperboles)
·
Maneno ya kuhuisha au kukipa kitu
au mnyama uhai au ubinadamu ( Personification)
·
Kumliganisha Mungu na mwanadamu (Antropomorphism)
·
Jina moja kwa niaba ya linguine (Metonymy)
·
Sehemu moja kwa jambo lote au
Sehemu nzima kwa sehemu (synecdoche)
·
Kuzungumza kinyume cha uhalisia ( Irony)
·
Lugha za mficho inayotumika badala ya neno chafu Figurative
language au (Euphemism )
·
Mithali (Proverbs)
7. Uwe
na ufahamu wa kutosha kuhusu uhusiano ulioko kati ya agano la kale na agano
jipya na ni matumizi yapi ya kiagano yanatumika mpaka sasa na yasiyotumika
mpaka sasa na yaliyosalia vile vile
8. Uwe
na ufahamu wa kihistoria wa andiko na maana iliyokusudiwa na mwandishi na namna
inavyoweza kutumika katika nyakati za leo
9. Uwe
na ufahamu wa jinsi na namna ya kutafasiri mifano ya kibiblia
10. Uwe
na ufahamu wa jinsi na namna ya kutafasiri unabii, kujua yaliyokwisha kutimizwa
na ambayo badio hayajatimizwa
Hitimisho.
Hiyo ni miongozo tu ambayo
inamsaidia mtu anayetaka kutafasiri maandiko kuweza kuizingatia ili aweze
kulileta neno la Mungu kwa usahihi, Mtafasiri wa maandiko pia anapaswa kuwa na
Nyenzo mbalimbali zinazoweza kusaidia katika kazi hii ya kutafasiri maandiko
Nyenzo hizo ni pamoja na
NYENZO MUHIMU ZINAZOSAIDIA KATIKA KUYATAFASIRI
MAANDIKO KWA USAHIHI
ROHO MTAKATIFU:
Ni nyenzo ya kwanza na ya Muhimu sana mtu awaye
yote anayetaka kuwa mtafasiri mzuri wa Maandiko ni lazima akubali kujazwa Roho
Mtakatifu kumbuka kuwa yeye ndiye aliyevuvia watu kuliandika neno na ni mwalimu
anaweza kutukumbusha na kutufundisha kile ambacho Mungu amekikusudia kwetu
hivyo lazima mtafasiri wa maandiko awe amejazwa Roho ikiwa wale waliokuwa
mashemasi nyakati za kanisa la kwanza walizingatiwa kuwa wenye Roho je si zaidi
sana wanaojitia katia kazi ya kuyatangaza Maandiko ona mfano wa Stefano Matendo
6;8-55 kwanini ni muhimu kuwa na Roho mtakatifu?
·
Ni
Mtafasiri mzuri
·
Ndiye
Mwandishi wa Biblia
·
Anajua
kile Ambacho Mungu anakijua
HAKIKISHA KUWA UNA BIBLIA ZA MATOLEO TOFAUTI
·
Biblia
ya Kiswahili na za aina mbalimbali za matoleo ya kiswahili cha kisasa
·
English
Bible matoleo tofauti
·
Zile
zilizoandikwa katika Lugha Tofauti Tofauti (Greek, Hebrew, Latin, Aramaic, na
kadhalika)
UWE NA UJUZI KUHUSU AINA ZA MATOLEO YA BIBLIA
Kwa kawaida kuna matoleo makuu ya aina tatu za
kibiblia zile zilizotafasiri neno kwa neno Literal translations, Zile
zilizotafasiri kutokana na maana iliyokusudiwa, Dynamic Equivalent na zile
tafasiri huru za lugha za kisasa Free translation mfano
Literal translations. Dynamic Equivalence translations. Free translations
Neno kwa neno Maana kwa maana Tafasiri huru
UWE NA BIBLIA ZENYE MAFUNZO NDANI YAKE; STUDY
BIBLES, REFERENCE OR ANNOTATED
Uwe na Biblia zenye mafunzo Studies Bible
Zinatoa maana ya baadhi ya aya:
1.
Mfano
mzuri ni Full life study Bible (NIV) Biblia ya mafunzo ya uzima tele
2.
Life
Application Bible (LB)
3.
Dake
Bible
4.
Scafield
Bible, na kadhalika
Uwe na
uchambuzi wa kibiblia wa watu wa aina mbalimbali COMMENTARIES: (Zenye
uchambuzi wa mstari kwa mstari au kifungu kwa kifungu na kadhalika ).
Baadhi ya Commentaries nzuri kwa mfano ni Pamoja
na
1. Adam Clarke’s Commentary
2. The New International Commentary
3. The Evangelical Bible Commentary
4. Mathew Henry Commentary.
Uwe na kitabu chenye ulinganifu wa kila neno
katika biblia kuanzia a mpaka z CONCORDANCES
ITIFAKI
- Itifaki yenye maneno yafananayo
- Itifaki za maana ya meneno
mfano Malazi yawe safi -Ndoa
- Mlinganio wa maneno
yanayopatikana katika sehemu nyingine za Biblia.
- Mfano Upendo upi? – Agape?
Phileo? Storge? Eros?
- Mahali lilipo neno Fulani
Mfano wa itifaki nzuri ni pamoja na ;-
o
Young’s
Analytical Concordance
o
Strong’s
Exhaustive Concordance etc.
o
Niv
Exhaustive Concodance.
o
Kumbuka
nyingine zina Kamusi za kiibrania na
Kiyunani Lexicons (=Dictionaries )
Uwe na VITABU VINAVYOHUSU TAMADUNI ZA KIBIBLIA
& MASWALA YA UCHIMBAJI WA MAMBO YA
KALE
Hii itakusaidia kuufahamu na kuwa na ujuzi
kuhusu mambo ya kale kama na maneno yaliyotumiwa kama Busu takatifu, Tundu la
sindano na mambo mengineyo.
KAMUSI ZA BIBLIA NA ZA LUGHA ZA KAWAIDA &
ENCYCLOPAEDIAS:
Zinafafanua maana ya maneno Mbalimbali kwa
ajili ya maswala ya kibiblia na maswala ya kawaida
1. Kamusi
za kawaida ni pamoja na zile za Kiingereza na kiswahili
·
English
Language Dictionary
·
Swahili
Language Dictionary etc. (Kamusi)
2. Kamusi
za Biblia ni pamoja na zilizo maarufu kama zifuatazo nyingi ni za kiingereza
·
Unger’s
Bible Dictionary
·
Pictorial
Bible Dictionary
·
Westminster
Bible Dictionary
·
Greek
Lexicon & Hebrew Lexicon
·
Kamusi
za kitheolojia (Theological Dictionary).
·
Kwa
ajili ya kujifunza Mambo mbalimbali ya kitheolojia Mfano ni
·
Baker’s Dictionary of Theology
4. Encyclopedias,
Mfano;
- International Standard Bible Encyclopedia
Uwe na MAFAFANUZI YA KIBIBLIA (BIBLE HANDBOOKS
:)
Kwa ajili ya ufafanuzi wa Maswala mbalimbali,
Vifungu, Maandiko, Tamaduni, Matukio ya kihistoria, Ugunduzi wa maswala ya kale (archaeology), na
kadhalika
Mfano
·
Halley’s
Bible Hand Book
·
Unger’s
Bible Hand Book
Uwe na MASOMO MBALIMBALI AU JUMBE MBALIMBALI
(TOPICAL BIBLE).
Vitabu vinavyo weka mpangilio wa ufafanuzi wa
masomo mbalimbali vikiwa na maandiko yoote husika sawa book arranged according
to different topics with all the texts related to each topic.
Mfano Nave’s topical Bible
Uwe na ATLASI ZA KIBIBLIA NA MSWALA YA KIHISTORIA
(BIBLE ATLASS) & HISTORY
Kwa ajili ya kutambua sehemu Mbalimbali na
umbali kwa kilomita za mraba n.k na vipimo kama homeri, yadi, mwendo wa sabato,
Ridhaa n.k
·
Baker’s
Bible Atlas
·
The
Oxford Bible Atlas
Uwe na tabia ya kusoma Biblia, kusikiliza
mahubiri ya wahubiri wengine, kuwa na akili ya kusoma vitabu mbalimbali na
kupoanua maarifa kila wakati na kila siku, penda kujifunza na kufundisha na
hakikisha kila wakati unakua na jambo jipya la kushirikiana na wengine
Na Rev. Innocent Samuel Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye
Hekima
0718990796.