Andiko la Msingi: Zaburi 16:8
“Nimemweka Bwana mbele yangu
daima, Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa.”
Utangulizi:
Zaburi hii ni zaburi iliyotungwa
na kuimbwa na Daudi, Ni zaburi ya kimasihi hasa kutokana na unabii unaomuhusu
Yesu Kristo moja kwa moja, hata hivyo kupitia zaburi hii bado kuna mambo ya
muhimu ya kujifunza kutokana na maisha ya Daudi, na uwezo wake aliokuwa nao
katika kumtegemea Mungu na faida zake Daudi anatufunulia siri mojawapo kubwa ya
ushindi na mafanikio yake katika kudumisha uhusiano na Mungu, katika mstari huu
wa nane kuna maswala ya msingi matatu ya kujifunza
·
Kumuweka
Bwana mbele Daima
·
Kwa kuwa
yuko kuumeni kwangu
·
Sitaondoshwa!
Kumuweka Mungu mbele Daima.
Moja ya siri kubwa ya ushindi katika
maisha ya Daudi ilikuwa ni pamoja na kumuweka Mungu mbele, Katika biblia ya
kiingereza neno kumuweka Mungu mbele linasomeka hivi “I have set the Lord always before me”
Neno “SET” la kiingereza linalotumika hapo liko sawa na neno la kiebrabia
“SAWA” kwa msingi huo tafasiri
rahisi ya mstari wa aya hiyo katika kiingereza inaweza kusemeka hivi “I have equally set” ambalo katika
Kiswahili tunaweza kutumia neno Nimekwenda sambamba na Mungu, au nimetembea
sawasawa na Mungu, au kwenda pamoja na Mungu, au kuendenda kwa jinsi ya Mungu
lugha hii ya kibiblia ndiyo ambayo imetumika katika Mwanzo 5:22,24 ikionyesha jinsi “Henoko akaenda pamoja na Mungu” kwa hiyo duniani kuna aina tatu za
mwenendo, kwa jinsi ya Mungu, kwa jinsi ya kishetani na kwa jinsi ya kibinadamu.
1Wakoritho 3:3 “Kwa maana hata sasa
ninyi ni watu wa tabia ya mwilini, maana ikiwa kwenu kuna husuda, na fitina Je
si watu wa tabia ya mwilini; tena mnaendenda kwa jinsi ya kibinadamu”
Daudi alidhamiria
katika maisha yeke kuenenda kwa jinsi ya Mungu siku zake zote. Hakutaka
kuendenda kwa jinsi nya mwili wala ya kishetani aliamua maisha yake yote
kumuweka Mungu mbele hii ilikuwa siri ya maisha ya ushindi kwa daudi siku zote
za maisha yake.
Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu.
Mkono wa kuume yaani mkono wa
kulia kama unavyojulikana sana kwa lugha ya Kiswahili ni kuwekwa mahali pa
Heshima kubwa sana, ni sawa na kutawala pamoja, au kukaa katika meza ya
kifalme, kuamua pamoja naye, kula pamoja naye kushauriana na kufanya maamuzi ya
pamoja, hivyo mtu alipomuweka mtu mkono wake wa kuume maana yake kumuweka
mahali pa heshima kubwa
2Samuel 9:1-9, “1. Kisha Daudi akasema, Je! Amesalia mtu mmoja katika nyumba
ya Sauli, nipate kumtendea mema kwa ajili ya Yonathani? 2. Palikuwa na mtumishi
mmoja wa nyumba ya Sauli, jina lake Siba, basi wakamwita aende kwa Daudi; na
mfalme akamwuliza, Wewe ndiwe Siba? Naye akasema Mimi, mtumwa wako ndiye. 3.
Mfalme akasema, Je! Hakuna hata sasa mtu ye yote wa nyumba ya Sauli, nipate
kumtendea mema ya Mungu? Siba akamwambia mfalme, Yonathani anaye mwana hata
sasa, aliye na kilema cha mguu. 4. Mfalme akamwambia, Yuko wapi? Siba
akamwambia mfalme, Tazama, yumo katika nyumba ya Makiri, mwana wa Amieli,
katika Lo-debari. 5. Basi mfalme Daudi akatuma watu, akamwondoa katika nyumba
ya Makiri, mwana wa Amieli, katika Lo-debari. 6. Basi Mefiboshethi, mwana wa
Yonathani, mwana wa Sauli akaenda kwa Daudi, akaanguka kifudifudi, akasujudu.
Daudi akasema, Mefiboshethi! Naye akaitika, Mimi hapa, mtumwa wako! 7. Daudi
akamwambia, Usiogope, maana bila shaka nitakutendea mema; kwa ajili ya
Yonathani, baba yako, nami nitakurudishia mashamba yote ya Sauli, baba yako;
nawe utakula chakula mezani pangu daima. 8. Akasujudu, akasema, Mimi mtumwa
wako ni nini, hata ukamwangalia mbwa mfu kama mimi? 9. Ndipo mfalme akamwita Siba,
mtumwa wa Sauli, akamwambia, Mali yote yaliyokuwa ya Sauli na ya nyumba yake
nimempa mwana wa bwana wako. 10. Nawe utamlimia nchi hiyo, wewe, na wanao, na
watumwa wako; nawe utamletea mwana wa bwana wako matunda yake, apate chakula
ale; lakini Mefiboshethi, mwana wa bwana wako, atakula chakula mezani pangu
sikuzote. Basi huyo Siba alikuwa na wana kumi na watano na watumwa ishirini.
11. Ndipo Siba akamwambia mfalme, Mimi, mtumwa wako, nitatenda hayo yote kama
bwana wangu, mfalme, alivyoniamuru. Na kwa habari za Mefiboshethi, mfalme
alisema, Atakula mezani pangu, kama mmojawapo wa wana wa mfalme. 12. Huyo
Mefiboshethi alikuwa na mwana mdogo, jina lake akiitwa Mika. Na watu wote
waliokaa nyumbani mwa Siba walikuwa watumwa wa Mefiboshethi. 13. Basi Mefiboshethi
akakaa Yerusalemu; maana alikuwa akila chakula sikuzote mezani pa mfalme; naye
alikuwa na kilema cha miguu yote miwili.
Watu wa nyakati za agano jipya
walifahamu vizuri umuhimu wa swala hili, swala la kumuweka mtu mkono wa kuume
lilimaanisha kumuheshimu mtu huyo kwa kiwango kikubwa na cha hali ya juu,
katika serikali kumuweka mtu mkono wa kuume ni sawa na kumfanya kuwa makamu wa
rais, wana wa Zebedayo kupitia mama yao
waliwahi kumuomba Yesu wapewe nafasi hii lilikuwa ni ombi la ajabu sana ambalo
gharama yake ilikuwa ni kupitia mateso na aibu ileile aliyoipitia Yesu Kristo
Mathayo 20:20-23
Biblia inasema:- 20. Ndipo mama yao wana wa Zebedayo akamwendea pamoja na wanawe,
akamsujudia, na kumwomba neno. 21. Akamwambia, Wataka nini? Akamwambia, Agiza
kwamba hawa wanangu wawili waketi mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono
wako wa kushoto, katika ufalme wako. 22. Yesu akajibu akasema, Hamjui
mnaloliomba. Je! Mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi? Wakamwambia,
Twaweza. 23. Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu; lakini kuketi mkono
wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, sina amri kuwapa, bali watapewa
waliowekewa tayari na Baba yangu.”
Aidha kumuweka mtu mkno wa
kuume maana yake ni kumfanya kuwa msaada wako, na ngao yako au mlinzi wako au
mtetezi wako.
Daudi kutokana na kumtegemea
kwake mungu na kutembea naye alikuwa na uhakika kuwa Mungu yuko mkono wake wa
kuume ndiye anayemshauri, ndiye anayemlinda na ndiye anayemtegemea na kwa
sababu hiyo alikuwa na uhakika kuwa hatoondoshwa.
Sitaondoshwa!
Kutokuondoshwa kunakotajwa mahali
hapo, maana yake ni kuwa salama, kutokusumbuliwa na maadui, kutokuogopa,
kutokutikiswa, kulindwa dhidi ya maadui, kuokuingia matatani, kutokuwamo
taabuni Zaburi 10:6, kudumu milele Zaburi 15:5, kutokutetemeshwa Zaburi 46:5, Hutotikisika
Kwa ufupi Daudi anatufundish.
1. Kumuweka
Mungu mbele siku zote za maisha yetu
2. Kumfanya
kuwa ngao yetu
3. Kumfanya
kuwa kinga yetu
4. Kumfanya
kuwa tegemeo letu
5. Kumfanya
kuwa mwangalizi wetu
6. Kumueshimu
na kutembea naye
Na tukiyafanya hayo
1. Tutakuwa
na furaha
2. Hatutatikisika
milele
3. Mungu
atakuwa tegemeo letu na ngao yetu
Taifa lolote, chama chochote, mtu
yeyote na taasisi yoyote kama tumedhamiria kumuweka Mungu mbele katika maisha
yetu mafanikio ni lazima, furaha ya Bwana ndio nguvu zetu, amani ya Mungu ndio
nguvu yetu kubwa sana, kama ukimuweka Mungu, katika mitihani, katika maisha ya
kila siku, katika kazi zetu, katika ndoa zetu, katika dua zetu na ibada na
maombi yetu kila kitu mfanye Mungu kuwa mkono wako wa kuume na utakuwa msindi
na zaidi ya kushinda.
Hivi karibuni katika uchaguzi wa Marekani watu wengi sana walishangazwa na matokeo ya uchaguzi huo uliompa Ushindi mkubwa Muheshimiwa Donal Trump wa Republican na ambaye ni kama alikuwa hakubaliki wala kuongoza katika kura za Maoni, na kuking'oa chama cha Democtratic lakini siri kubwa ya Ushindi wa Trump bila kujali madhaifu yake alimuweka Mungu mbele, wakati Democratic walifanya maovu yafuatayo
1. Waliondoa Amri kumi na alama ya Biblia iliyowekwa na George Washington kutoka ikulu ya Marekani
2. walifungisha ndoa za jinsia moja kwa wafanyakazi wa ikulu ya Marekani
Makamu wa Rais wa Marekani wa Chama cha Democratic Joe Biden akifungisha ndoa ya Mashoga ambao ni wafanyakazi wa ikulu ya Marekani jijini Washington DC
3. Uhusiano na Israel wakati wa utawala wa Obama na Chama chake cha Democratic ulipoa na ulikuwa wa kinafiki
Sriri ya ushindi wa Donal Trump wa Republican
1. Alumuweka Mungu mbele na kuchukizwa na uovu unaofanyika Washington DC ikulu
2. Ana uhusiano mzuri na Israel na ameahidi kuhamisha ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv Jaffa kwenda Mji mkuu wa milele wa kiyahudi Yerusalem
3 baada ya kuteuliwa alifanyiwa maombi na watumishi wa Mungu kuonyesha kumtanguliza Mungu katika kila jambo
Katika mifano hii iliyohai utakuwa umejifunza kwamba kumuweka Mungu mbele na kumuheshimu kutakufanya usiondoshwe milele
Rev. Innocent Kamote
“Mkuu wa Wajenzi mwenye hekima”