Mstari wa Msingi: Zaburi
91:10
“Mabaya hayatakupata wewe, wala
tauni haitakaribia hema yako!”
Utangulizi:
Zaburi hii ni mojawapo kati ya Zaburi zilizotungwa na
kuandikwa na Daudi, Inaonekana wazi kabisa zaburi hii ikizungumzia pigo la
ugonjwa wa Tauni, ambayo Mungu aliipiga Israel kuokana na kosa la Daudi
kuwahesabia wanajeshi wake na kusahau kuwa ushindi unatoka kwa Mungu, katika
wakati huu Mungu aliruhusu malaika wake na kuua watu wapatao 70 elfu kwa muda
mfupi sana kutoka Dani mpaka Beersheba na sasa malaika wa Bwana alikuwa
anaelekea kuuharibu Yerusalem unaweza
kuona vema habari hii katika 2Samuel 24:
10-17
“10. Ndipo
moyo wake Daudi ukamchoma baada ya kuwahesabu hao watu. Naye Daudi akamwambia
Bwana, Nimekosa sana kwa haya niliyoyafanya; lakini sasa, Ee Bwana, nakusihi
uuondolee mbali uovu wa mtumishi wako; kwani nimefanya upumbavu kabisa. 11. Na
Daudi alipoondoka asubuhi, neno la Bwana likamjia nabii Gadi, mwonaji wake
Daudi, kusema, 12. Nenda, ukanene na Daudi, Bwana asema hivi, Nakuwekea mambo
matatu; katika haya uchague moja, nikutendee hilo. 13. Basi Gadi akamwendea
Daudi, akamweleza, akamwambia, Basi, miaka saba ya njaa ikujie katika nchi
yako? Au miezi mitatu ukimbie mbele ya adui zako, huku wakikufuatia? Au siku
tatu iwe tauni katika nchi yako? Fanya shauri sasa, ufikiri, ni jawabu gani
nimrudishie yeye aliyenituma. 14. Naye Daudi akamwambia Gadi, Nimeingia katika
mashaka sana; basi sasa na tuanguke katika mkono wa Bwana; kwa kuwa rehema zake
ni nyingi; wala nisianguke katika mkono wa wanadamu. 15. Basi Bwana akawaletea
Israeli tauni tangu asubuhi hata wakati ulioamriwa; nao wakafa watu toka Dani
mpaka Beer-sheba sabini elfu. 16. Lakini huyo malaika aliponyosha mkono wake
kuelekea Yerusalemu ili auharibu, Bwana akaghairi katika mabaya, akamwambia
huyo malaika mwenye kuwaharibu watu, Yatosha, sasa ulegeze mkono wako. Naye
yule malaika wa Bwana alikuwako karibu na kiwanja cha kupuria cha Arauna,
Myebusi.17. Daudi, alipomwoma malaika aliyewapiga watu, akanena na Bwana,
akasema, Tazama, ni mimi niliyekosa, ni mimi niliyepotoka; lakini kondoo hawa,
wamefanya nini? Mkono wako na uwe juu yangu, na juu ya nyumba ya baba yangu.”
Baada ya tukio hili la kutisha la watu kupigwa kwa tauni,
ambalo linaonekana kumuuma moyo sana Daudi, aliamua kumuomba Mungu na ingawa haiku
wazi alikuwa anaombea nini lakini bila shaka alijiombea yeye na wakazi wa mji
wa Yerusalem na hasa alikuwa anaomba kwa mji wa Yerusalem na maombi yake
yalikuwa na uhakika kuwa Mungu hawezi kuipiga Yerusalem, kutokana na uzoefu
wake Daudi anaonyesha mambo ya msingi makuu mawili
1.
Kuutafuta uwepo wa Mungu siku zote za
masiha yetu Mstari wa
1-9 Katika Mistari hii Daudi alikuwa
anaonyesha umuhimu wa kuwa na uhusiano usioonekana na Mungu “AKETIYE MAHALI PA SIRI PAKE ALIYE JUU
ATAKAA KATIKA UVULI WA MWENYEZI” Daudi anasisitiza kuwwa na uhusiano
usioonekana kati yetu na Mungu, Ukristo wetu sio tu ule unaoonekana, tunapoomba
maombi ya kanisani kwa pamoja ni vema lakini uhusiano wetu na Mungu ni zaidi ya
maombi ya kanisani, uko uhusiano wa siri kukaa katika uwepo wake Mathayo
6:2.-4, 7-8.16-18. Daudi anaonyesha
kuwa mtu atakayedumisha uhusiano wa siri na Mungu na kukaa naye katika namna
ambayo wengine wanaweza wasijue, Na kumtegemea Mungu, Mungu atakufanyia haya Zaburi 91:3-9
·
Atakuokoa
na mtego wa Mwindaji
·
Mungu
atakufunika kwa mbawa zake na utapata
nkimbilio
·
Hutakuwa
na hofu ya aina yoyote
·
Mapigo
kama tauni na magonjwa ya kutisha na
vita hutaviogopa
·
Hata
watu elfu na kumi elfu walianguka mapigo kwao hayatakukaribia wewe
·
Macho
yako yataona mwisho wa wabaya
2. Mabaya hayatakupata wewe.
Ni muhimu kufahamu kuwa Mabaya
yanayozungumzwa hapa kama Pestilence
(Magonjwa yasio na tiba), au plague (Mapigo
ya hukumu) kama biblia nyingi za kiingereza zilivyoandikwa, Biblia ya
kiebrania inatumia neno “NEGA” ambalo maana yake ni KURUDIWA, au KUADHIBIWA
au KUPUNGUKIWA NA NEEMA YA MUNGU, neno hili lina maana kuwa Mungu hatazuia
majaribu yasitupate lakini, lakini Mungu hatatuadhibu, au anapotuadhibu hataacha tuangamiie katika mkono wake,
atatutisha lakini hataacha tauni disaster zikaribie Hema yako, yaani amakazi
yako hayatapigwa Daudi alikuwa anajua kuwa Mungu anaweza kupiga miji Mingine
lakini ni vigumu kuruhusu Yerusalem kupigwa , haitakaribiwa ni makazi yake
matakatifu, ukifanya masikani na Mungu, Mungu akifanya makazi kwako hakuna
mabaya yatakayokupata, Mungu atatuma malaika zake wakulinde, Yeye ana Rehema
nyingi hata anapotuadhi,
Mungu hatatuadhibu
Mungu hahatuondolea neema
Hatatupungukia
Hatoondoa rehema zake
Ikiwa tutaimarisha uhusiano wetu wa
siri na yeye
Ikiwa tutautafuta uwepo wake,
atatuhifadhi, hata wengine wakianguka ka maelfu yao sisi tutabaki salama
Ikiwa Mungu aliwaokoa watu wengi sana katia Biblia wasipatwe na mabaya kuna ushahidi wa
kutosha kimaandiko kwamba Mungu hatakuacha upatwe na Mabaya
Rev. Innocent
Kamote
Mkuu wa
Wajenzi mwenye hekima!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni