Ijumaa, 8 Desemba 2017

Huyu ndiye Rais Halali wa Kenya!




Uhuru Muigai Kenyatta.

Uhuru Kenyata alizaliwa tarehe 26 October 1961 ni moja ya wanasiasa mahiri na raisi  wa awamu ya nne wa jamhuri ya Kenya.

Mheshimiwa Kenyatta amewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Gatundu ya kusini kati ya mwaka 2002 mpaka 2013, Kenyatta ni mtu aliyejaa upendo, imani, na mwenye kuheshimu utu, ni mpole na mnyenyekevu, ni mpenda maendeleo na ni mtu anayeipenda Afrika kwa dhati na mwenye moyo wa Kumcha Mungu.

Kabla ya kuwa raisi wa awamu ya nne wa Kenya ndugu Kenyata amewahi kuwa mwanachama wa Kenya African National Union, chama ambacho kilihusika kudai Uhuru wa Kenya chini ya baba yake Mzee Jomo Kenyatta. Kwa sasa Kenyatta ameingia madarakani kwa tiketi ya chama cha “Jubilee” jina ambalo kwa asili ni la kibiblia lenye kuzungumzia mwaka wa Bwana wa kuwaweka huru watu wake sawa na Luka 4:18-19. “Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.”  Neno mwaka wa Bwana uliokubaliwa kibiblia ndio ulijulikana kama Jubilee.

Uhuru Kenyatta ni moja ya watoto wa kiume wa aliyekuwa rais wa Kwanza wa jamhuri ya Kenya na mama yake Mama Ngina Kenyatta ambaye kwa bahati nzuri bado yu hai, Mheshimiwa Uhuru alishinda Uchaguzi  kwa mara ya pili August 2017 katika uchaguzi mkuu na kupata ushindi kwa asililia 54% kupitia kura za wakenya wote waliokuwa wamejiandikisha, Hata hivyo ushindi huu uliokuwa umetangazwa na mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi wa nchi hiyo “Independent Electoral and Boundaries Commission” Ndugu Wafula Chebukati. Ushindi huu ulipingwa kisheria na mahakama kuu nchini humo baada ya kuzingatia madai ya muungano wa vyama pinzani unaojulikana kwa ufupi kama NASA uonaoongozwa na “Raila Odinga” kwa kuzingatia madai kadhaa tarehe 1 September 2017 Mahakama kuu ilibatilisha matokeo hayo na kuamuru kuwa uchanguzi urudiwe tena tarehe 26 October 2017 yaani ndani ya siku 60 tangu kutanguliwa kwake, hata nhivyo katika namna ya kushangaza uchaguzi huu wa marudio ulipingwa na kukosolewa vibaya  na wapinzani na watu wa maswala ya haki za binadamu, Huku mpinzani mku Raila Amolo Odinga akisusia uchaguzi huo.

Maswala kadhaa ya ya uvunjifu wa amani yalijitokeza kwaajili ya kupinga matokeo ya uchaguzi huo uliorudiwa kwa mara ya pili, huku wafuasi wa raila wakiandamana katika mitaa kama Kawangware,  Nairobi na maeneo mengine wakipinga vikali na kuchoma moto maduka na kuchoma matairi, watu kadhaa walijeruhiwa na wengine kufariki dunia, waandamanaji walikuwa wakimtaka Raila kuchukua hatua, kabla ya kura kurudiwa tena,  Huku yeye mwenyewe akiwachochea wafanye fujo na kupinga uchaguzi huo kwa madai kuwa hakukuwa na uwanja huru na wa haki wa ufanyikaji wa uchaguzi huo, Na baadaya bwana Odinga alijitoa katika kinyanganyiro hicho cha uchaguzi wa mara ya pili, kutokana na tukio hilo Muheshimiwa Kenyatta alipata nafasi ya kushinda uchaguzi wa Marudio kwa njia iliyo laini zaidi na hivyo kumpa nafasi ya kuiongoza Kenya kwa miaka mitano ijayo.

Katika uchaguzi huo wa Marudia muheshimiwa Uhuru Kenyatta alipata ushindi mkubwa wa kishindo kwa asilimia 98% ya kura zote zilizopigwa, Wakati akiapishwa Rais Kenyata aliahidi kuwa daraja la maendeleo lenye kuwaunganisha wakenya kuwa kitu kimoja na kusonga mbele huku akiweka moyo wake wote, katika Hutuba yake iliyojawa na utukufu wa Mungu Mheshimiwa Kenyata alisoma andiko na Nabii Isaya  akihusisha tukio la kuapishwa kwake tarehe 28/11/2017 kuwa bila Mungu haikuwa rahisi namnukuu 
Today is yet another historic day for our great motherland.  First and foremost, our gratitude is to our Almighty God. The Prophet Isaiah proclaimed: When you pass through the waters, I shall be with you. When you pass through the rivers, they shall not overwhelm you. When you walk through fire, the flames will not consume you, Our God is faithful.  He heard our voices when we cried out to Him.  He listened, and answered our prayers.  He has brought us thus far, and He will take us even further.This is the testimony of our country today; and for this we thank Him
Tafasiri isiyo rasmi Leo ni siku nyingine ya kihistoria katika ardhi mama yetu, Kwanza ningependa kumshukuru Mwenyezi Mungu, Nabii Isaya alisema, “Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.” Mungu wetu ni mwaminifu, amesikia sauti zetu tulipomlilia na kuhitaji msaada wake. Amesikia na kuyajibu maombi yetu, ametufikisha hapa leo na atatuvusha zaidi ya hapa na huu ni suhahidi ulio wazi leo na kwaajili ya hili tunamshukuru mwisho wa kumnukuu
Maandiko yaliyotumiwa na Mheshimiwa Kenyatta ni Isaya 43:2, Ni wazi kuwa Kenyatta hakunukuu maandiko haya hivihivi tu Kenyata pamoja na willium Rutto ambaye siku ile Kenyata alimuita Pastor ni wazi kuwa walimtegemea Mungu, ni wazi kuwa walimtanguliza Mungu mbele, ni wazi kuwa walikuwa na timu kubwa ya watu walioomba pamoja nao na kwaajili yao mapema waimbaji kadhaa walisikika katika uwanja ule wakiimba kuwa sio uchawi ni Maombi, hii ilikuwa ni ushahidi wazi kuwa kuna watu walikuwa wakiomba kwaajili ya wakenya.
Kwanini naandika makala haya, ? wanafunzi wangu wote waliosoma Living Stone Boys’ Seminary ni mashahidi kuwa kwa neema aliyonipa Mungu niliweza kuwatabiria maraisi kadhaa na wakawa katika nafasi nilizowatabiria, akiwepo Rais John Pombe Magufuli, Rais Trump na Kenyatta, Niliwaambia wazi wanafunzi wangukwa vile tulikuwa tunaomba pamoja mara kadhaa nilitaka wayajue mapenzi ya Mungu niliwaambia kuhusu ujio wa maraisi hao madarakani na ikawa kama nilivyowaambia, niliwaambia kuwa mimi sio Muhubiri mkubwa sana kwa maana ya umarufu, wala sijiiti nabii lakini nilimsikia nabii mmoja mkubwa mwenye kituo kikubwa cha tv huko Dar es Salaam akisema wazi kuwa anamuona Raila Ikulu, mimi hapohapo nmilimwambia mke wangu hapana mimi namuona Kenyetta Ikulu, na jiono nilipokwenda kuomba niliwaambia wanafunzi waziwazi kuwa yuko nabii mwenye kituo cha TV huko Dar es Salaam amesema kuwa amemuona Raila akiwa ikulu mimi naomba nieleze wazi kwamba tuiombee Kenya kwani nimeona Moto katikati ya mji, na moshi mkubwa karibu na jengo moja refu sana nchini humo, na tukiomba vema moto huo unaweza kuzimishwa lakini mimi simuoni Raila Ikulu namuona Kenyatta.
Leo ninapoandika naandika mambo haya yakiwa yametimia lakini kwa nini nataka kuandika hili leo nataka kukiri Mbele za Mungu kuwa Kenyatta yuko Kihalali madarakani, si kwa sababu ya uchaguzi kurudiwa, si kwa sababu, ameapishwa lakini kwa sababu Mungu amemchagua na kukusudia awepo na nataka kuitumia nafasi hii kutoa maonyo kwa raila Odinga, kuwa ajihadharina jaribio la kutaka kujiapisha kuwa Rais kwani tukio hili licha ya kuwa na madhara kwa wafuasi wake kadhaa lina madhara makubwa sana kwake mwenyewe, huu ndio utakuwa mwisho wa Raila, kisiasa, kiimani na kwa heshima aliyonayo, litakuwa tukio la aibu kubwa sana kwake na lenye kufedhehesha, kwani licha ya kuwa kinyume cha sheria liko kinyume na Mungu, Mungu hakukuchagua Raila, wala hatakuchagua tena kuwa Rais wa Kenya wakati wowote na nataka kuweka wazi wazi wazi kuwa Rais ajaye wa Kenya mara baada ya Kenyata atakuwa Mcha Mungu zaidi mara mbili ya Kenyatta atalitaja jina la Mungu maradufu zaidi na atatokea Jubelee tena na  Raila hataonekana tena. Katika Historia ya mageuzi nchini Kenya.
Wito kwa wakenya wote tusikubali kamwe kumwaga Damu, tusikubali kushawishiwa na wapinga maendeleo na wapinzani na maadui wa Kenya walioko ndani na nje, Kenyatta anaweza asiwe mkali kama Magufuli, watu hawafanani, lakini moyo wake una mapenzi mema kwa wakenya na Afrika kwa ujumla, Mimi ni Mtanzania sina asili yoyote ya Kenya, lakini nabii hana mipaka kwa vile Mungu ni wa watu wote, lakini Kenya ikiendelea ni Afrika imeendelea, uchumi wa Kenya ukikua ni uchumi wa Afrika umekua,
Naitakia Kenya wakati wa utulivu na wakati wa kufanya kazi na kuachana na aina yoyote ya ushawishi ulio na nia ovu wa kutokuitambua serikali halali iliyoko Madarakani, niwaonye wakenya wote kutokujitokeza tarehe 12 kwaajili ya kuapisha mtu asiyehusika na  wamuache mwenyewe aidha serikali ya Kenya iliyoko madarakani ichukue hatua stahiki na kali za kisheria kwa jaribio hilo la kipumbavu litakalojaribiwa kufanya na uongozi wa Nasa.
Mungu Ibariki Kenya
Mungu Ibariki Afrika
Rev. Innocent Kamote Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima.

Kwa taya la Punda!


Waamuzi 15:16Samsoni akasema, Kwa taya ya punda chungu juu ya chungu, Kwa taya ya punda nimepiga watu elfu.”


Then Samson said, "With a donkey's jawbone I have made donkeys of them. With a donkey's jawbone I have killed a thousand men

Ni Muhimu kufahamu kuwa ushindi wetu katika mazingira ya aina yoyote ile na katika vita vya kiroho unatoka kwa Mungu, Mungu alikwisha kutuahidi mapema sana katika torati kuwa atatupa ushindi, bila kujali ni aina gani ya silaha inayotumiwa na adui, yeye anatia moyo kuwa tusiogope wala mioyo yenu isizimie, Mungu asiyeonekana kwa macho ya kibinadamu yuko nyuma ya watu wake kuwapa nguvu isiyoweza kuonekana na kusababisha ushindi. 

Kumbukumbu  20:1-4Utokapo kwenda vitani kupigana na adui zako, na kuona farasi, na magari, na watu wengi kuliko wewe, usiwaogope; kwa kuwa Bwana Mungu wako, yu pamoja nawe, aliyekukweza kutoka nchi ya Misri. Na iwe, msongeapo mapiganoni, kuhani na akaribie na kusema na watu, awaambie, Sikizeni, enyi Israeli, hivi leo mwasongea mapiganoni juu ya adui zenu mioyo yenu na isizime; msiche, wala msiteteme, wala msiingiwe na hofu kwa ajili ya wao; kwa maana Bwana, Mungu wenu, ndiye awaandamaye kwenda kuwapigania juu ya adui zenu, ili kuwaokoa ninyi.”

Mungu aliahidi kuwa atatupa Ushindi, na kuwa ndani yetu ameweka uwezo wa kupiga watu elfu uwezo huu unatoka kwake na sio wa mtu binafsi au kwa akili ya mtu binafsi Kumbukumbu 32:30Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi, Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama Bwana asingaliwatoa?”

Ni wazi tu kuwa Samson alielewa ahadi za Mungu na aliamua kutunga shairi na kutengeneza Fumbo kubwa sana la siri ya nguvu zake kwamba ameweza kupiga watu elfu KWA TAYA LA PUNDA, lakini ukweli ulio wazi ni kuwa Samsoni alijiliwa na ROHO WA MUNGU na ndiye aliyempa ushindi huu na nguvu ya kupiga watu 1000

Tunajifunza wazi kuwa siri ya ushindi wetu inatokana na NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU ambaye hapa Samson anamtaja kama taya la Punda, sio kweli kwamba Samson aliwaangamiza maadui kwa Taya la punda bali nyuma ya taya la punda ilikuweko nguvu isiyoonekana iliyomuwezesha Samson kupata ushindi

Waamuzi 15:14-20. Alipofika Lehi, Wafilisti wakapiga kelele walipokutana naye; ndipo roho ya Bwana ikamjia kwa nguvu, na zile kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitani iliyoteketezwa kwa moto, na vile vifungo vyake vikaanguka mikononi mwake. Naye akaona mfupa mbichi wa taya ya punda, akautwaa, akapiga watu elfu kwa mfupa huo;  Samsoni akasema, Kwa taya ya punda chungu juu ya chungu, Kwa taya ya punda nimepiga watu elfu. Ikawa, alipokuwa amekwisha kunena akautupa ule mfupa wa taya mkononi mwake; na mahali pale pakaitwa Ramath-lehi.Kisha akaona kiu sana, akamwita Bwana akasema, Wewe umetupa wokovu huu kwa mkono wa mtumishi wako; na sasa nitakufa kwa kiu, na kuanguka katika mikono ya watu wasiotahiriwa. Lakini Mungu akapasua mahali penye shimo palipo katika Lehi, pakatoka maji; naye alipokwisha kunywa, roho yake ikamrudia, akaburudika; kwa hiyo jina la mahali pale likaitwa Enhakore, napo pa katika Lehi hata hivi leo.Naye akawa mwamuzi wa Israeli: katika siku za Wafilisti muda wa miaka ishirini.”

Ushindi wa Samsoni haukuwa katika mikono yake wala katika taya la punda bali ulitokana na nguvu za Roho wa Mungu yaani Roho Mtakatifu,

Samson aliweza kusababisha uharibifu mkubwa miongoni mwa maadui za Mungu Wafilisti, kwa kutumia Taya la Punda huu ulikuwa ni muujiza mkubwa wenye maana ya kuwa Mungu hutumia mambo manyonge na mapumbavu na yaliyodharaulika  ya dunia kudhihirisha Nguvu zake, kwa sababu hiyo ushindi huu ni dhahiri kuwa haukutokana na aina ya silaha, wala mikono ya Samson Lakini alikuwa ni Roho Mtakatifu aliyetumia Mkono pamoja na taya la punda kuleta ushindi, tunayaweza yote katika yeye atutiaye Nguvu Wafilipi 4:13Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” Mungu anapokusudia kutupa ushindi dhidi ya adui zetu ni lazima kuitunza ile nguvu ya asili inayotupa ushindi nguvu hii ni Roho Mtakatifu.

Aidha ni muhimu kukumbuka kuwa  Pale “Ramoth lehi” Kulikuwa na hekalu la miungu ya kifilisti ambamo ndani yake kulikuwa na alama ya taya la punda alama hii ilikuwa inawakilisha nguvu za siri za miungu ya wafilisti ambao waliamini kuwa Mungu huyu aliwapa ushindi dhidi nya adui zao, ni wazi kabisa na inawezekana kabisa kuwa watu wale 1000 waliopigwa na Samsoni huenda walikuwa ni makuhani wa miungu hiyo pale “Ramoth lehi” Jina “Ramoth lehi” ni muungano wa Maneno mawili ya Kiebrania na wafilisti Ramoth kwa Wafilisti ilimaanisha DRAGON au Joka na LEHI maana yake Palipotupwa mfupa wa Punda Taya la punda,  Nguvu ya joka iliyokuwa linaabudiwa na wafilisti katika eneo hili tendo la Samsoni kuwapiga kwa kutumia taya la punda ilikuwa ni ishara ya wao kupigwa na nguvu ya siri, na kwa sababu hawakuwa wametambua nguvu ya Samsoni bila shaka wakati hu ndipo walipoanza uchunguzi wa kutaka kujua siri ya Nguvu ya Samsoni ni nini?



Pichani Samsoni akiwa amepiga watu wengi 1000 pale Ramoth lehi, 

Samson alikuwa ametumiwa na Roho Mtakatifu kwani nguvu za Mungu zilikuja juu yake kwa nguvu lakini maadui hawakutambua, ndugu msomaji wangu ni muhimu ukafahamu kuwa iko nguvu ya siri itakayosambaratisha kila anayekupinga na kukusaidia wakati nwa mahitaji yako nguvu hii ni Roho Mtakatifu, Bwana atawasambaratisha wote wanaoshindana nawe kupitia nguvu za Roho Mtakatifu, nguvu hii ya Mungu isiyoonekana kwa macho iliweza kuwapa ujasiri watakatifu wote waliotutangulia na ndio itakayohusika na inayohusika kuwashughulikia adui zako hata Leo, Kule Marekani watu fulani hutumia alama ya vidole viwili, kwa kulaza vidole viwili vya katikati na kusimamisha viwili, wakimaanisha nguvu ya siri nguvu hii inayowapa ushindi inaweza kuwa ya Joka (Satanic Sign) au kwa Wakristo wanaomjua Mungu inaweza kuwakilisha Heshima kwa Roho Mtakatifu aliyewapa ushindi dhidi ya adui zao (Honor Sign)  kwa hiyo taya la punda kwa wafilisti ilikuwa nguvu ya siri ya Joka na kwa wayahudi taya la Punda ilitumika kama alama ya Nguvu za siri za Roho wa Bwana.

Na. Rev. Innocent Kamote.

Mkuu wa wajenzi wa mwenye Hekima

Jumatatu, 27 Novemba 2017

Kuwa wajinga Katika mambo mabaya !



Mstari wa Msingi: Warumi 16:19Maana utii wenu umewafikilia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya.”

Ni lazima watoto walelelwe katika njia iwapasayo kabla mioyo yao haijawa zege iliyokauka na Rev. Innocent Kamote Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Utangulizi.

Ni muhimu kufahamu kuwa tunaishi katika nyakati za mwisho zaidi na katika nyakati hizi nza mwisho Shetani amekusudia kuharibu kanisa na kuiharibu jamii kupitia mmomonyoko wa maadili, na ili aweze kufanikiwa kuharibu jamii anaweza kupata mafanikio makubwa kama atakusudia kuwaharibu watoto ambao ndio kanisa na taifa la kizazi kijacho.

Kwa muda mrefu katika jamii ya wasomi wa Kikristo kumekuwako na mijadala mikubwa miwili, mmoja ni msimamo mkali unaolenga kuwa watoto ni lazima wafundishwe njia za Mungu mapema kabisa katika maisha yao ili neno la Mungu likae ndani yao kwa iwngi kabla ya kuwa watu wazima, lakini wazazi wengine na baadhi ya wanatheolojia wa kikristo wanapinga kwa madai kuwa watoto hawawezi kuzaliwa na Ukristo wetu hivyo ni muhimu wakaachwa na kujifunza mema na mabaya na kuijua Dunia kisha wakutane na Mungu wao binafsi ndipo watakuwa na imani ya kweli, hata hivyo wazo hili la pili ingawa linaweza kuonekana kama lenye hekima ni wazo baya zaidi kupata kutokea duniani kwani liko kinyume na maandiko.

Biblia imeagiza kuwa ni lazima watoto waelekezwe na kukua katika njia ya Mungu,  

Kumbukumbu la torati 6:1-9Na hii ndiyo sheria, na amri, na hukumu, alizoziamuru Bwana, Mungu wenu, mfundishwe, mpate kuzitenda katika nchi ile mnayoivukia kuimiliki; upate kumcha Bwana, Mungu wako, kushika amri zake zote, na sheria zake, ninazokuamuru, wewe na mwanao, na mwana wa mwanao, siku zote za maisha yako; tena siku zako ziongezwe. Sikiza basi, Ee Israeli, ukaangalie kuzitenda; upate kufanikiwa, mpate kuongezeka sana, kama Bwana, Mungu wa baba zako, alivyokuahidi, katika nchi ijaayo maziwa na asali. Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako;  nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.  Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako. Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.” 

Biblia inaonyesha kuwa watoto wakifundishwa vema njia ya Mungu hawataiacha hata watakapokuwa watu wazima  

Mithali 22:6Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.” 

Kutokuwalea watoto katika njia iliyonyooka na kosa kubwa sana katika mapenzi ya Mungu Nyakati za Biblia hususani wakati wa waamuzi kulitokea kizazi ambacho hakimjua Mungu wala njia zake na hivyo waliishi kwa kutenda kila aina ya uovu  

Waamuzi 2:10-11Tena watu wote wa kizazi hicho nao walikusanywa waende kwa baba zao; kikainuka kizazi kingine nyuma yao, ambacho hakikumjua Bwana, wala hawakuijua hiyo kazi ambayo alikuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli. Wana wa Israeli walifanya yaliyokuwa ni maovu mbele za macho ya Bwana, nao wakawatumikia Mabaali.” 

Kwa sababu hiyo ni jukumu la Wachungaji walimu na wazazi kuhakikisha kuwa watoto wanaikulia njia ya Mungu, na hawajifunzi uovu kutoka kwetu, na kuhakikisha kuwa tunawasaidia kwa namna yoyote ile kukua kiakili, kimwili, kitaaluma na kiroho, huiku wakiwa wenye nidhamu thabiti, Yesu alitangaza hukumu kubwa sana kwa watu watakaowakwaza watoto na kuwafanya wakengeuke alisema yafaa wafungiwe jiwe kubwa la kusagia na kutoswa katika kilindi cha bahari  

Mathayo 18:6bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari.

Mungu alimchagua Ibrahimu na kumfanya kuwa Baraka kubwa sana Duniani lakini sababu kuu ya kumchagua Ibrahimu Mungu anaieleza katika  

Mwanzo 18:17-19BWANA akanena, Je! Nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo, akiwa Ibrahimu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa? Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake waishike njia ya BWANA, wafanye haki na hukumu, ili kwamba BWANA naye akamtimizie Ibrahimu ahadi zake.  
             
Kumbe ni kwa kusudi hili katika andiko la Msingi Paulo mtume anatoa wito kwa kanisa la rumi kuwa na hekima Yaani ujuzi wa kutosha katika mambo mema na kuwa wajinga katika mambo mabaya neno kuwa wajinga katika biblia ya kiyunani linasomeka kama “AKERAIOS” Ambalo maana yake kuwa incorruptible au kuwa Innocent,  kwa Kiswahili ni kuwa safi kabisa, wasiochanganywa, kutokuujua kabisa uovu wala mwenendo wa Dunia, Biblia inatumia neno hilo pia katika

 1Wakoritho 14:20Ndugu zangu, msiwe watoto katika akili zenu; lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mkawe watu wazima.”

Unaweza kuona kwa msingi huo basi Msingi wa kibiblia haufudnishi kuwaachia huru watoto, Bibloia inataka watoto wabanwe katika sheria, waelekezwe nini cha kufanya na nini sio cha kufanya , haiwezekani watoto waachiwe kufanya lolote wanalojisikia kilifanya, tusiwaruhusu kukaa katika njia ya shetani eti ili nao wakutane na neema ya Mungu binafsi, ni lazima sisi tutumike kama chombo cha kuwanyoosha wakae katika njia iliyonyooka, kujua maovu kuna mateso mengi sana ni waarabu na wayahudi tu Duniani ndio wanaojua kuwalea watoto wao na kuwafanya wafuate imani zao kwa uthabiti na kuwarithisha kama Ibrahimu, sehemu nyingi duniani na wakristo wameshindwa kabisa kufanya wajibu huu

Hatupaswi kuwaacha watoto wakajikulia tu kana kwamba kuna bahati nasibu ya kukua kwao, lazima tuhusike katika kuwajenga na kuwalea watu wengi sana wanatumia mamilioni ya fedha duniani kusomesha wachungaji, walimu madaktari na wataalamu mbalimbali na hata makanisani lakini hakuna watu wanaofanya utafiti wa kutosha kuhusu watoto zaidi tu tunasoma kina “Maria Montessori” mwana falsafa wa zamani tu wakizungumza kuhusu watoto na namna yao ya kujifunza, Zamani kulikuwa na kozi katika chuo cha biblia Inaitwa “Children Ministry” mimi niliisoma katika ngazi ya Diploma zamani sijui kama mkozi hii siku hizi ipo lakini kanisa limepuuza kabisa huduma ya watoto na ukiwauliza Wachungaji wengi watakuambia kuwa tatizo watoto hawana mafungu ya kumi, 

Ni lazima tufanye kila jitihada ya kuwalinda watoto wetu katika udanganyifu wa dhambi na maasi ili kuwalinda watoto wetu na uovu duniani Roho mtakatifu anataka wawe wajinga katika mambo ya uovu

Tukiwaachia watoto wetu waijue dunia watabikiriwa kama Dinah binti Lea wa Yakobo Mwanzo 34:1-2, 7 Wana wa Yakobo waliposikia walikasirika sana na walisikitika waliona kuwa dada yao amefanyiwa mambo ya kipumbavu kwa nini hii ni kwa sababu Yakobo alikaa na watu wabaya karibu nao ni lazima tuwalinde watoto wetu, Naamini ya kuwa hukuchagua mahali hapa kwa bahati mbaya, wazazi waliochagua mahali hapa wanajua kuwa watoto wao wako katika mikono salama na hatutaruhusu mambo ya kipumbavu yatokee Katika jina la Yesu amen

“Songs “Bless the Lord” Rebbeca Malope”
Rev. Innocent Kamote.

Mkuu wa Wajenzi mwenye hekima

Jumanne, 31 Oktoba 2017

Aonavyo mtu nafsini mwake Ndivyo alivyo!


 Mithali 23:7 aMaana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.”

Utangulizi:

Ni muhimu kufahamu, kwamba Biblia inaonyesha ya kuwa maisha yetu yanaweza kutabiriwa na kila tunachokifikiri au kukiwaza, yale tunayoruhusu yaingie katika mioyo yetu ndiyo yenye nafasi kubwa sana katika kuamua hatima na muelekeo wa maisha yetu, kwa msingi huo kile tunachokisema na kukitenda ni matokeo ya pili ya kile tunachokiwaza, hatuwezi kujificha kuwa sisi ni watu wa namna gani, kwani kusema kwetu na kutenda kwetu kutafunua hatimaye kuwa sisi tukoje, ndio maana ni vigumu sana kumsoma mtu anayenyamaza. Mtu halisi ni vile tunavyofikiri, Biblia inaonyesha udhahiri wa watoto wa Mungu na watoto wa ibilisi kutokana na utendaji waoa au usemaji wao.  1Yohana 3:10Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.

Mkuu wa wajenzi Rev. Innocent Kamote wa pili Kutoka kushoto akiwa na waalimu wa Living Stone, Mwalimu Oscar, Kushoto, Nicolous Luchenja watatu kushoto na Jimmy Molel wanne kutoka kushoto wakiwa katika mazoezi ya Taekondoo. Aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo!

Mithali 23:7a “ Maana aonavyo mtu ndivyo alivyo”

Proverbs 23:7a “For as he thinketh in his heart, so he is”

Kwa msingi huo vile tunavyofikiri ndivyo, uhalisia wa utu wetu

I.                    Wewe ni matokeo ya kile unachokifikiri na kwa sababu hiyo ni muhimu kufikiri pia kuhusu nini unakiwaza na kama kina kibali mbele za Mungu Zaburi 19:13-14 Biblia inasema “Umzuie mtumishi wako asitende mambo ya kiburi, Yasinitawale mimi. Ndipo nitakapokuwa kamili, Nami nitakuwa safi, sina kosa lililo kubwa. Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na mwokozi wangu”. Kwanini mwandishi wa Zaburi anataka mawazo ya moyo wake yapate kibali mbele za Mungu? Maana yake ni kama anamuomba Mungu amsaidie kuwaza sawasawa, hii ni Muhimu sana vile tunavyowaza ndivyo tunavyoweza kusema na kutenda, kama tutawaza sawasawa tutakuwa tumejizuia, kutenda, kutawaliwa, kusema na kijiepusha na makosa makubwa na uovu.

Yale tunayoyafikiri yana vyanzo, Mtu ili aweze kuwa kama alivyo ni lazima kuweko maswala kadhaa ynayochangia katika kumjenga moja ikiwa ni wakati wa kuzaliwa kwetu, lakinimengine ni vile tunavyopokea kutoka ulimwenguni kutokana na mazingira na milango yetu mitano ya fahamu kwa msingihuo ni muhimu kwetu kujilinda na vyanzo vinavyoingiza taarifa katika nafsi zetu na akili zetu mfano :-

a.       Yale tunayoyasoma?- Tunayoyasoma yanaingia katika akili zetu na kwa hivyo yana mchango mkubwa sana katika kuyajenga maisha yetu na ndio maana biblia inasema tujae nenola Mungu mioyoni mwetu Wakolosai 3:16-17 “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.” 2Timotheo 3:14-17 “14. Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao; na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu. Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.” Maandiko matakatifu yanaweza kutuhekimisha na kutuongoza katika haki, kwa msingi huo yale tunayoyasoma yanaweza kuathiri maisha yetu na hivyo ni muhimu kwa mtu mwema kuhakikisha anaingiza mambo yaliyo mema katika moyo waake “Ubongo”
b.      Yale tunayoyaangalia Ayubu 31:1 “Nilifanya agano na macho yangu; Basi nawezaje kumwangalia msichana?Ayubu aliweka agano na macho yake kuwa hataangalia mwanamke kwa tamaa yaani kumwangalia kwa nia mbaya, kumbe kuangalia kunaweza kuathiri mitazamo yetu na mfumo wa maisha yetu ni muhimu kwetu pia kujilinda katika yale tunayoyaangalia.
i.                     Kuyaangalia kupitia Internet,jihanadhari angalia vitu vyema
ii.                   Kuyaangalia kupitia Movies, TV, na kadhalika watoto wetu wengi siku hizi wanangalia sana ngumi na uharibifu wa kwenye sinema na hivyo vijana wengi sana wa leo wamekuwa ni waharibifu wakubwa wa vitu na vifaa majumbani na mashuleni
c.       Yale tunayoyatafakari Wafilipi 4:8.” Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.” Kuna maswala ya kutafakari ambayo biblia inayapendekeza hapa kwenye kutafakari ndipo panapoweza kutusaidia kujenga misimamo yetu iliyo thabiti, ni muhimu kwa kila mmoja kujipima kuwa anatafakari nini.
d.      Yale tunayoyasikia, ukisikia taarifa zisizo sahihi hutakuwa sahihi na ukisikia taarifa sahihi unakuwa sahihi. Hakikisha kuwa unasikiliza mambo ya msingi, Biblia ya Kiswahili inasema Mazungumzo mabaya huaribu tabia njema, kwa maana ya kuwa tunapozungumza pia tunasikia, Biblia ya kiingereza inasema “Bad Company corrupt Good Character”  sawa na kusema marafiki wabaya huaribu tabia njema kwa msingi huo ni muhimu kwetu kuangalia wale wanaotuzunguka kwa vile wanahusika kwa kiwango kikubwa katika kuyajenga maisha yetu
II.                  Mioyo yetu ndio chemichemi ya tabia zetu.
a.       Mti hutambulikana kwa matunda yake Luka 6:43-45Kwa maana hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala mti mbaya uzaao matunda mazuri; kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu. Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake”. Unaona kile Yesu anakizungumza hapa ni kama anasema aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo! Kumbe kusema kwetu na kutenda kwetu ni matokeo ya asili yetu ya moyoni, tunza saba moyo wako! Kuna athari kubwa sana katika kuwaza kwetu au katika yale tunayoyajaza mioyoni mwetu kwani hatima yeke ni kuyazalia matunda. Kipengele kifuatacho kinasaidia kutujulisha namna tutakavyokua endapo tutaielekeza mioyo yetu katika maswala mhaya:-    
III.                Maisha yako yanafafanuliwa na moyo wako na fikira zako:-
1.       Kama unajifikiri mwenyewe sana utakuwa mbinafsi sana 2Timotheo 3:1-2 “Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,”    
2.       Kama utafikiri sana kuhusu wengine utakuwa mkarimu, na mwenye kujali Warumi12:10-13. “Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu; kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana; kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu; kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi.”, Waefeso 4:32
3.       Kama unafikiri sana kuhusu fedha utakuwa mtu mwenye tamaa 1Timotheo 6:9-10 “. Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu. Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.”               
4.       Kama utakuwa mwenye kushukuru sana utakuwa mtu mwenye kuridhika 1Timotheo 6:6-8 “6. Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa.  Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu; ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo.”
5.       Kama utafikiri sana kuhusu ngono utakuwa  mwenye tamaa au kahaba Mathayo 5: 27-28 “Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.”
6.       Kama tutafikiri sana kuhusu uadilifu tutakuwa wenye moyo safi  1Wakoritho 6:18, Mathayo 5:8 “Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.”
7.       Kama utafikiri sana kuhusu kutenda hila utakuwa muongo mkubwa Wakolosai 3:9-10 “Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake; mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba.”
8.       Kama utakuwa mwenye kufikiri kuhusu ukweli utakuwa mtu muaminifu Waefeso 4:25 “Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake.”
9.       Kama utakuwa mwenye kutaka sifa kutoka kwa watu utakuwa mnafiki Mathayo 6:5,23:12  Mathayo 6:5 “Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.”
10.   Kama utakuwa mwenye kufikiri sana kuhusu kumuinua Mungu, utakuwa mtumishi wake mkubwa sana 1Petro 2:1-3. “Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote. Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;  ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili.
  
Hitimisho.

Wewe ni mtu wa namna gani, na je Mungu anaona nini kwako? Matendo 1:24, Waebrania 4:13
Ni lazima uamue kuwa mtu wa aina gani kwa kuhakikisha kuwa unawaza vema wakati wote
Kila unachokitafakari na jinis unavyojiona ndani ndivyo unavyoamua maisha yako yawe Mungu alichukizwa na wana wa Israel ambao walijiona nafsi zao kama panzi walipojilinganisha na wakanaani na kusahau ukuu wa Mungu na hivyo Mungu alichukizwa nao Mafanikio yetu na maisha yetu ya kiroho na kimwili yanategemeana sana na namna tunavyojiona ndani na namna tunavyojiona ndani inategemeana sana na yake  tunayoyaingiza katika mioyo yetu, ukijiona duni wewe ni duni, ukijiona shujaa wewe ni shujaa, ukijiona huwezi wewe hutaweza, ukijiona mbaya wewe ni mbaya, ukijiona mwema wewe utakuwa mwema,ukijichukia hakuna mtu atakayekupenda, ukijipenda utapendwa, ukiwa na amani, utazalisha amani ukiwa na uchungu utazalisha uchungu, Aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo

Na Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!

Rev. Innocent Kamote.