Alhamisi, 23 Aprili 2020

Yesu Kristo na Mitandao ya kijamii!


Luka 13:1-5Na wakati uo huo walikuwapo watu waliompasha habari ya Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao.  Akawajibu akawaambia, Je! Mwadhani ya kwamba Wagalilaya hao walikuwa wenye dhambi kuliko Wagalilaya wote, hata wakapatwa na mambo hayo? Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo. Au wale kumi na wanane, walioangukiwa na mnara huko Siloamu, ukawaua, mwadhani ya kwamba wao walikuwa wakosaji kuliko watu wote waliokaa Yerusalemu? Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.”




Utangulizi:


Ni muhimu kufahamu kuwa taarifa (Habari) ni moja ya nyenzo yenye kubwa sana yenye kubeba maana zinazoweza kujenga au kubomoa jamii, taarifa zina nguvu, zina nguvu zote mbili za kujenga au kubomoa, Mungu ndiye mwanzilishi wa taarifa, Alipomuumba mwanadamu alimpa taarifa ya namna na jinsi ya kuutawala ulimwengu alimweleza kama mtu huru namna anavyoweza kuutumia ulimwengu na alimuelekeza namna nzuri ya kuutumia ulimwengu lakini pia alimuonya kuwa kama atautumia ulimwengu vibaya angeweza kuleta madhara makubwa kwa maisha yake na jamii yake yaani kifo. Taarifa inaweza kuwa ndogo lakini kama ikitumika vibaya inaweza kuleta madhara makubwa sana kwa jamii kama njiti ya kiberiti inavyoweza kuchoma msitu mzima!


Ni muhimu kufahamu kuwa nyakati za Biblia pia kulikuwa na namna ambavyo watu waliweza kupokea na kutoa taarifa kama unavyoweza kuona katika kifungu hiki Luka 13:1-5Na wakati uo huo walikuwapo watu waliompasha habari ya Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao.  Akawajibu akawaambia, Je! Mwadhani ya kwamba Wagalilaya hao walikuwa wenye dhambi kuliko Wagalilaya wote, hata wakapatwa na mambo hayo? Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo. Au wale kumi na wanane, walioangukiwa na mnara huko Siloamu, ukawaua, mwadhani ya kwamba wao walikuwa wakosaji kuliko watu wote waliokaa Yerusalemu? Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.” 


Yesu alikuwa amepokea taarifa au habari kuhusu Wagalilaya waliouawa vibaya na Pilato, na baada ya kupokea taarifa hizi tunaona namna Yesu alivyozitumia taarifa hizo sasa kuwafundisha watu wake somo kuhusu toba na pia akiunganisha na taarifa nyingine ya watu kumi walioangukiwa na mnara huko siloamu, Kutoa na kupokea taarifa ni haki ya kila jamii, Yesu aliitumia taarifa hii kwa sababu huenda aliamini au kulikuwa na namna ya uthibitisho kuwa chanzo cha taarifa alichokipokea kilikuwa ni chanzo cha kuaminika na kwa sababu hiyo taarifa alizozipokea zilikuwa na ukweli, na hivyo alizitumia kufundisha kama mfano kwa jamii iliyomzunguka, Unapochunguza kwa kina mafundisho ya Yesu Kristo utaweza kuona alikuwa na mifano mingi sana na alikuwa na stori nyingi sana na khadithi nyingi sana na nyingi alizitumia katika kuielimisha jamii na kuijenga kama jinsi Mungu anavyotaka.


Kutokana na kupanuka kwa technolojia leo hii kumekuweko na vyanzo vingi sana vya kupokea na kutoa habari, lakini ni jambo la kusikitisha sana kuwa jamii ya leo haizingatii uadilifu katika swala zima la kupokea na kutoa habari, Mfano mzuri ni tukio la hivi karibuni ambapo watangazaji/ waandishi wa habari wa TBC walifariki, lakini wakati huo huo kulikuwa na taarifa za kufariki kwa Mtangazaji wa shirika hilo wa habari za biashatra aliyeitwa “Gloria Maiko” aidha kabla ya kuenea kwa taarifa hii kuhusu kufa kwake iliebnea taarifa kuwa Gloria anaumwa sana tena ana ugonjwa wa Corona, Mimi napenda habari, mimi ni mwana habari, mimi nimesoma Introduction to jounalism, napenda kupata taarifa kwa sababu huwa pia natoa taarifa yaani nazitumia kuijenga jamii, sio hivyo tu unaposoma chuo cha Biblia kwaajili ya kazi ya uchungaji hausomei Biblia pekee unaandaliwa pia kuwa mwana habari kwa sababu kanisa linaweza kuwa na gazeti, Kanisa linaweza kuandika vitabu, kanisa linaweza kuwa na televisheni, kanisa linaweza kuwa na radio, kanisa linaweza kuwa na ukurasa wa faceboo, instagram, blog na nyenzo nyingine za utoaji wa taarifa kwa hiyo lazima watu wa Mungu wawe na angalau ufahamu mdogo tu kuhusu upokeaji na utoaji wa habari, wakati huu nilisoma chanzo kingine kuhusu Gloria kinasema hivi ngoja nikinukuu

 “TBC1 tuliwaonya kukusanyika siku ya msiba wa Marini Hassan hamkusikia! Haya leo Joseph Kambangwa mfanyakazi wenu kafa kwa corona na maziko ni kesho saa 4 huko huko Mloganzila! **Gloria Maiko (anatangazaga habari za biashara) yuko hoi ana dalili zote za corona! RIP Kambangwa 

mwisho wa kunukuu, angalia huyu ni mtu mwenye akili timamu, ni mtu ambaye jamii inamtegemea, jamii inaamini labda katika hiki alichokisema lakini je habari hii ilikuwa na malengo gani kwa jamii, ilikusudia nini kwa Gloria? Na kwa familia yake, je ilikuwa inajenga au inabomoa? Kwa sababu baada ya kuenea kwa Taarifa hii Gloria Maiko alijitokeza kwenye mitandao ya kijamii akithibitisha kuwa yeye yuko hai na wala haumwi! Lakini mwandishi anajisikiaje? Baada ya Gloria mwenyewe kutokea je wale walioeneza katika mitandao ya kijamii na kutoa salamu za astarehe kwa amani wanajisikiaje katika mioyo yao baada ya mtu mliyemzushia kifo kujitokeza na kuonyesha yuko hai, nimetoa tu mfano huu lakini Jambo hili limewahi kuwatokea wengi, hapa nchini hata Mheshimiwa Augustin Lyatonga Mrema alizushiwa mara kadhaa mpaka alipojitokeza na kuionya jamii kuwa yeye ni mzima na kuwa kuanzia sasa atawafungulia mashtaka watu wanaoanzisha uzushi huu, Huko ulaya mambo ya aina hii yako sana lakini kwa mujibu wa tamaduni zao, Lakini sisi ni Watanzania na wana Afrika Mashariki je mambo haya ni sawasawa? Je wale waliosomea uandishi wa habari jambo hili ni sawa katika utoaji wa taarifa na upokeaji, Je wale wanaozushia wenzao hujitokeza kuomba radhi? Je wanachukuliwa hatua gani je ni aina gani ya jamii tunaijenga ya watu wanaosema ukweli au jamii ya waongo? Mungu ametupa hekima na akili na maendeleo makubwa ya nyenzo za utoaji wa taarifa lakini ni muhimu zikatumika kwaajili ya utukufu wa Mungu, kwa wakristo tunaambiwa katika maandiko kwamba lolote tulifanyalo kwa neno au kwa tendo tulifanye kwa utukufu wa Mungu ona 

Wakolosai 3:17 “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.” 

Swali kubwa ambalo kila mwana jamii anapaswa kujiuliza na kuhoji ni kuwa kama Yesu angekuwepo Duniani leo ni habari gani angeikubali na habari gani angeikataa na je angetumiaje mitandai ya kijamii, na sisi vilevile tujiulize je tunapopata habari ambazo hazina uhakika haziko sahihi, hazina utu, zina mitazamo hasi, zinaupendeleo, na kama ni za uongo wanaozitoa hawawajibishwi, habari hazina kiasi, na ziko kinyume na uadilifu je tungejisikiaje? Nafikiri wote tuna namna ambavyo tunatarajia jinsi habari au taarifa inavyopaswa kuwa! Mkurugenzi wa Maadili ya uandishi wa habari aitwaye Aidan White anasema ziko kanuni 400 ambazo wanahabari wanapaswa kuzizingatia lakini ziko kanuni 5 Muhimu zaidi ambazo kila mwandishi na mtoa habari anapaswa kuzifuata bila kushindwa.


1.       Ukweli na Uhakika (Accuracy) – “the quality or state of being correct or precise” Maana yake kila mtoa habari na mpokea habari na mtawanya habari au taarifa anapaswa kuhakikisha kuwa taarifa anayoitoa ina UKWELI na pia IMEHAKIKISHWA.  Lakini pia kuzinagatia kuwa habari inaweza kuwa ya ukweli na imehakikishwa lakini swali je ni wakati muafaka kuitoa? Kwa sababu inaweza kuwa kweli na ya uhakika lakini wakati ukawa hauruhusu kuisema au mazingira yakawa hayaruhusu kusema !, tunapohubiri injili watu wa Mungu huwa hatuleti maneno ya kushawishi, wale yenye ufundi wa kibinadamu tunapopeleka habari njema tunapeleka habari ambazo ni za kweli na zinathibitishwa na Roho Mtakatifu, ile Nguvu ya ukweli pekee inauwezo wa kuwaweka watu huru na kuiponya jamii. Waandishi wa habari ni kama manabii wanapaswa kutia habari za ukweli na uhakika ona  Kumbukumbu la Torati 18:22 “Atakaponena nabii kwa jina la Bwana, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena Bwana; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogopeBiblia liagiza kuwa kama nabii atatia taarifa na akadai taarifa hiyo imetoka kwa Mungu na kumbe sivyo yaani haikutimia yaani haina ukweli asiogopwe maana yake achukuliwe hatua, kwa hiyo kama watu wanaotoa habari na habari zao zikawa sio za uhakika torati inashauri wachukuliwe hatua katika agano la kale waliuawa, katika agano jipya  wanapaswa kuchukuliwa hatua, Yesu angelikuwepo leo hangeweza kukubalia habari ambayo haijathibitishwa haina ukweli na haijahakikishwa!


2.       Huru – Independence – yaani taarifa inapaswa kuwa ya haki isiyopendelea upande wowote, Kila mtoa habari na mpokea habari anapaswa kuwa na mtizamo wa haki, hapaswi kuwa mwenye kupendelea upande fulani, mfano kama ni kwa habari ya vyama vya siasa ni vema mtoa habari na mpokea habari wakawa hawana mtazamo wa kisiasa au mtazamo wa siasa zinazofungamana na upande fulani, taarifa itolewe kwa uwazi na kwa haki na ihaririwe kwa uwazi na kwa haki, Maandiko yanatufundisha wale wanaomuamini Yesu kuwa imani yetu katika Kristo isiwe kwaajili ya kupendelea watu Yakobo 2:1 “Ndugu zangu, imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe nayo kwa kupendelea watu unaona Yesu angelikuwepo leo hangeweza kupokea au kutoa habari inayomkandamiza mtu fulani haki ingesimama


3.       Usiyo na Masalahi nayo – Impartiality kwa kiingereza neno hili maana yake “Impartiality is a principle of justice holding that decisions should be based on objective criteria, rather than on the basis of bias, prejudice, or preferring the benefit to one person over another for improper reasons“ yaani kanuni ya haki inayotaka maamuzi yafanyike kwa mujibu wa vigezo na sio kwa sababu mtu una masalahi fulani, au ukungu fulani unaotaka mtu mmoja anufaike dhidi ya mwingine kwa sababu zisizo sahihi, unapopokea au kutoa habari kwa makusudi maovu au kwa uependeleo kwa Mungu hufai kuwa mtu wa haki, Yesu angekuwepo leo kwa habari ya kupokea na kutoa habari angehukumu kwa haki  Isaya 11:1-5Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda. Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana; na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake; bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.Na haki itakuwa mshipi wa viuno vyake, na uaminifu mshipi wa kujifungia” Mtoa habari au mpokea habari anapaswa kuwa mwaminifu na kuwa mtu wa haki, wakati mwingine kwa sababu ya mitazamo fulani na hata kwaajili ya kupokea rushwa tumepokea au kutoa habari kwa maslahi ya upande fulani kwa sababu tunaletu jambo, Mungu hapendezwi na utaratibu huo na ndio maana hatua kali sana zinapaswa kuchukuliwa endapo itabainika mwandishi kuwa ana dalili za kupokea rushwa.


4.       Taarifa yenye kujali utu – Humanity Ni muhimu kufahamu kuwa biblia inasema usiue kuua kuko kwa namna nyingi sana unaweza kuua kwa kutumia maneno, unamuua mtu kisiasa, umamuharibia mtu au unamchafua mtu huku ni kuua mpokea habari au mtoa habari anapaswa kuhakikisha kuwa anajali utu, ni dhambi kuandika, kupokea au kutoa habari yenye kudhuru, yenye kuharibu ubinadamu wa mtu, au yenye kumvunjia mtu heshima hatupaswi kutoa habari wala kusambaza habari au habari picha yenye kuharibu maisha ya wengine au kudhalilisha, watu wasiojua kutumia mitandao ya kijamii wanapiga picha hata za watu waliopata ajali mbaya na kuzisambaza katika mitandao ya kijamii, katika nchi nyingi zilizoendelea hata mwili wa Marehemu anapoagwa haupigwi picha, Picha ya marehemu inayoruhusiwa kuonekana ni ile ambayo wanafamilia wataiweka juu ya jeneza kwaajili ya kumbukumbu yake, nchi nyingi zawatu wasiostaraabika utaona mtu aliyepasuka kichwa kwa ajali, waliovunjika miguu, mtu mwenye ulemavu wa jabu na picha za kutisha sana zinarushwa kwenye mitandao ya kijamii, je umewahi kujiuliza kwanini mtu akipata ajali watu hutoa nguo zao na kuufunika mwili wa marehemu?  Ni kwaajili ya kujali utu, Mungu hawezi kukubali na kufurahia utu wa mtu udhalilishwe, kwa msingi huo kila mtoa habari na mpokea habari namsambazaji anapaswa mno sana kuzingatia utu, Yesu alikubali kifo cha aibu pale msalabani ili kutunza heshima ya mwanadamu, natarajia kuona jamii iliyostaarabika ambayo haitarusha picha ya marehemu yoyote akiwa na pamba puani, wala hata jeneza ikiwezekana na kama umefiwa weka picha ya aliyefariki ikiwa katika hali ya ubora na usiiwekee “X” muonyehse mtu enzi za ubora wake, sikitika kwa kumpoteza mtu huyo lakini usimdhalilishe nduguyo, aidha usisambaze wala usizikubali picha za watu walio katika hali mbaya za ajali, mwanadamu ameumbwa kwa sura na utukufu wa Mungu na lazima utu wa kila mtu uheshimiwe, hali kadhalika picha za ngono na zenye kuonyesha uchi ni mwiko kwa watu waadilifu, Mtu wa haki huwa hadhalilishi mtu mwingine. Mathayo 1:18-19Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.Mtu wa haki huwa hafanyi mambo kwa kusudi la kumuaibisha mtu mwingine hata kama mtu huyo ni kweli amefanya jambo hilo Yesu angekuwepo leo hangekubali kupokea au kutoa taarifa zinazodhalilisha utu wa mwanadamu ambao ni uumbaji wake.


5.       Kuwajibika – accountability - In ethics and governance, accountability is answerability, Maana yake kila mtoa habari na mpokea habari na msambaza habari wanapaswa kujua na kukubali kuwa wanawajibika kwa habari wanazotoa au kusambaza, kwa msingi huo kama utatoa habari na ikasababisha madhara au hata isiposababisha madhara ufahamu kuwa unatakiwa kuwa na utayari wa kuijibia kuitolea maelezo na kuwa tayari kuomba radhi ikiwa umekosea,  au kukubali kukosoelewa na kupokea maoni ya jamii kuhusiana na ulichokitoa au kukisema na ikiwezekana kuwa tayari kushitakiwa mahakamani na hata kufungwa na au hata kuuawa na wale watakaochukizwa na habari ulizozitoa, kila habari unayoitoa ni muhimu kufahamu kuwa itakugharimu Yesu alisema kila neno lisilo na maana atakalolinena mwanadamu atatoa hesabu yake Mathayo 12:36-37Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu. Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwaYesu atakapokuja atawahukumu wazishi wote hapa aliwaonya watu waliokuwa wakitoa habari zisizo sahihi kuhusu utendaji wa Yesu Kristo, Yesu anatoa pepo kwa Roho wa Mungu wapotoshaji wakesema anatumia nguvu za mkuu wa pepo Baalzebub, lazima ieleweke wazi kuwa watioa habari watawajibika sio mbele za wanadamu tu na mbele za Mungu!


Hitimisho!

Biola shaka kuna kitu umejifunza hapo sisi kama wakristo ndio chumvi ya ulimwengu napenda kila mmoja wetu aelimike na kukubalia kujifunza kuwa katika wakati huu wa utandawazi wakati ambapo kila mwanadamu anauwezo wa kutoa taarifa, kupokea taarifa na kusambaza taarifa ni Muhuhimu kwetu tukaacha kujisahau na kukumbuka kuwa ziko kanuni za neno la Mungu ambazo zinatuongoza jinsi na namna ya kuitumia mitandao hii ya kijamii, ninapohitimisha nataka kukukumbusha mambo kadhaa ya msingi yafuatayo:-

a.       Tumia mitandao ya kijamii kuhudumu kwa neno la Mungu na kusambaza habri njema
b.      Kumbuka kujitenga kwa muda na mitandao ya kijamii na kwenda kuomba
c.       Kumbuka kuwakumbusha watu kutubu na kuishi maisha yanayompendeza Mungu
d.      Kumbuka kutia moyo mambo yaliyo mema kwa ku like na kuweka maoni yako na kukosoa vikali maovu na kuonyesha wazi jambo au kitu usichopendezwa nacho tumia neno la Mungu
e.      Tumia mitandao ya kijamii kudumisha uhusiano na kutafuta amani na watu wote na sio kuharibu
f.        Tumia mitandao ya kijamii kuonyesha semina, mikutano ya neno la Mungu na maswala muhimu ya kijamii onya karipia fundisha na jihadhari na matapeli
g.       Zingatia kanuni husika tulizojifunza na muombe Mungu ziwe kanuni muhimu katika maisha yako, asomaye na afahamu, ukiyajua hayo heri wewe ukiyatenda


Na. Mchungaji Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye hekima
0718990796

Jumanne, 21 Aprili 2020

Unapozungukwa na kamba za mauti!


Zaburi 116:1-6Haleluya. Nampenda Bwana kwa kuwa anaisikiliza Sauti yangu na dua zangu. Kwa maana amenitegea sikio lake, Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote. Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na huzuni; Nikaliitia jina la Bwana. Ee Bwana, nakuomba sana, Uniokoe nafsi yangu. Bwana ni mwenye neema na haki, Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema. Bwana huwalinda wasio na hila; Nalidhilika, akaniokoa.”



Utangulizi:


Ni moja ya zaburi ya kipekee sana, Mwandishi haonyeshi kama iliwahusu watu wote lakini ilimuhusu yeye binafsi na hali iliyomzunguka na anaonyesha njinsi anavyompenda Bwana kwa kuwa anamsikia zaburi hii imegawanyika katika maeneo makuu matatu, anamsifu Bwana na kuonyesha ji kwanini anamsifu na anampenda, lakini pia anaelezea mambo magumu yaliyomkuta na jinsi bwana alibyomuokoa na anaelezea namna anatavyo mshukuru, kwa hiyo ni zaburi ya shukurani binafsi kutokana na kuokolewa na mitego au kama au hali zinazolazimisha afe!


Zaburi hii haijulikani mwandishi ni nani na tukui husika ni lipi lakini inaonekana mwandishi alikuwa akimshukuru Mungu kwa kumuokoa na mauti au hali za kifo zilizokuwa zikimuandama, uchunguzi wa kimaandiko unaonyesha kuwa huenda zaburi hii ni ya Nabii Yona ingawa hatuna ushahidi wa kutosha kama Yona alitunza Zaburi, vyovyote vile iwanvyo inaonekana Yiona akliisema zaburi hii alipookuwa akimuomba Mungu kwenye tumbo la Nyangumi, na kinabii inamuhusu Masihi ambaye alipokufa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu tuona 


Yona 2:1-10Ndipo Yona akamwomba Bwana, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki, Akasema, Nalimlilia Bwana kwa sababu ya shida yangu, Naye akaniitikia; Katika tumbo la kuzimu naliomba, Nawe ukasikia sauti yangu. Maana ulinitupa vilindini, Ndani ya moyo wa bahari; Gharika ya maji ikanizunguka pande zote; Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu.  Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako; Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu.Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu; Vilindi vilinizunguka; Mwani ulikizinga kichwa changu;  Nalishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi na mapingo yake yalinifunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka shimoni, Ee Bwana, Mungu wangu, Roho yangu ilipozimia ndani yangu, Nalimkumbuka Bwana; Maombi yangu yakakuwasilia, Katika hekalu lako takatifu. Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongo Hujitenga na rehema zao wenyewe; Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa Bwana.Bwana akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani.” 


Unaona ni Zaburi ambayo tukio lake linafanana kabisa na tukio la Yona Lakini mambo ambayo tunaweza kujifunza kutoka katika zaburi hii ya shukurani ni maswala makubwa matatu



1.       Mwimbaji anaonyesha sababu za kumshukuru Mungu
2.       Mwimbaji anaonyesha nini cha kufanya tunapozungukwa na kamba za Mauti
3.       Mwimbaji anaonyesha mwitikio wa Mungu wetu tunapoliitia jina lake



Sababu za Kumshukuru Mungu.


Ziko sababu nyingi sana za sisi wanadamu kumshukuru Mungu, na kumpenda hata tunapokuwa katika wakati mgumu, sisi kama wenye dhambi Mungu anapotuonyesha kuwa hatustahili na kuwa wakati wowote anaweza kutuangamiza kwa hasira yake kwa kuwa hakuna hata mmoja anayefaa tunaweza kujikuta tunataabika sana na tunajawa na hofu kubwa na huzuni, Hakuna mwanadamu hata mmoja anayestahili kuwa hai wakati Mungu anapoikasirikia Dunia, hakuna anayeweza kudhani ya kuwa yeye anafaa, hakuna kuhani wala nabii, sheihk wala padre askofu wala mpagani, hakuna hata mmoja tunayeweza kusema hastahili kutubu Ni kwa rehema zake tu ndio maana hatuangamii, hakuna asiyejaribiwa au kujaribika hata mmoja ujumbe wa toba unamuhusu kila mmoja kwa sababu neno la Mungu linasema wote wamepotoka wameoza wote pia hakuna mtenda mema kla hata mmoja kwa tendo moja tu la kuwa na uhai na kugundua kuwa yuko Mungu huilo pekee linalazimisha tumpende Mungu na kama tukimuita na akatuitikia hilo nalo linapaswa kuongeza upendo wetu kwake, Yona alipogundua tu kuwa Yuko hai na alipokuwa akimuitia Mungu kama nabii na kujua kuwa Mungu anamuitikia akikumbuka jinsi alivyokataa kutii kwa makusudi akikumbuka jinsi mauti ilivyokuwa ikimuandama hata kura za kifo zilimuangukia yeye akikubalia kwa hiyari yake afe ili wengine wawe salama kwenye melikebu, alimezwa na samaki, alilia katika tumbo la Nyangumi na kuweka nadhiri na Mungu akamisikia tukio hili pekee lilimfanya awe na wingi wa shukurani!


Yona 1:6-17 “Basi nahodha akamwendea, akamwambia, Una nini, Ewe ulalaye usingizi? Amka, ukamwombe Mungu wako; labda Mungu huyo atatukumbuka, tusipotee. Wakasemezana kila mtu na mwenzake, Haya, na mpige kura, mpate kujua mabaya haya yametupata kwa sababu ya nani. Basi wakapiga kura, nayo kura ikamwangukia Yona. Ndipo wakamwambia, Tafadhali utuambie, wewe ambaye mabaya haya yametupata kwa sababu yako; kazi yako ni kazi gani? Nawe umetoka wapi? Nchi yako ni nchi ipi? Nawe u mtu wa kabila gani? Akawaambia, Mimi ni Mwebrania; nami namcha Bwana, Mungu wa mbingu, aliyeziumba bahari na nchi kavu. Ndipo watu wale wakaogopa mno, wakamwambia, Ni jambo gani hili ulilolitenda! Kwa maana watu wale walijua ya kuwa amekimbia, ajiepushe na uso wa Bwana, kwa sababu alikuwa amewajulisha. Basi wakamwambia, Tukutende nini, ili bahari itulie? Kwa maana bahari ilikuwa inazidi kuchafuka. Naye akawaambia, Nikamateni, mnitupe baharini; basi bahari itatulia; kwa maana najua ya kuwa ni kwa ajili yangu tufani hii imewapata. Lakini wale watu wakavuta makasia kwa nguvu, ili wapate kurudi pwani, wasiweze; kwa maana bahari ilizidi kuwachafukia sana. Basi wakamlilia Bwana, wakasema, Twakuomba, Ee Bwana, twakuomba, tusiangamie kwa ajili ya uhai wa mtu huyu, wala usitupatilize kwa ajili ya damu isiyo na hatia; kwa maana wewe, Bwana, umefanya kama ulivyopenda. Basi wakamkamata Yona, wakamtupa baharini, nayo bahari ikaacha kuchafuka. Ndipo wale watu wakamwogopa Bwana mno, wakamtolea Bwana sadaka, na kuweka nadhiri. Bwana akaweka tayari samaki mkubwa ili ammeze Yona, naye Yona akawa ndani ya tumbo la samaki yule muda wa siku tatu, mchana na usiku


Unaona ni kupitia hali hii bahari ilichafuka na kura zilionyesha kuwa yuko mtu ameacha kumtii Mungu na ni kwaajili yake mabaya yanatokea hivyo ingawa alikuwa amelala hana wasiwasi Yona alikuwa anakambiliwa na mauti, kamba za mauti zilikuwa zimemzunguka na kwa kuliitia jina la bwana akaokolewa na hali ile ni kwa sababu hii anaona ziko sababu za kumshukuru Mungu, Yuko Munghu anayeisikiliza sauti yetu hata kama tumemkosea hili ni jambo la kushukuru kwamba tukiliitia jina lake atatusikia na atatujibu, wakati huu sasa dunia inapitia katika majanga ya aina mbali mbali mazito na tishio kubwa sana la kiuchumi hakuna mtu anayeweza kujigamba kwamba yuko salama wote tumeasi, wote tumekosea kuna mahali hatuko sahihi, hatuwezi kuwasingizia watu fulani tu wala hatuwezi kusema kuwa sisi ni bora kuliko wengine Mungu yu atuita katika toba, sio toba ya Kenya pekee, wala sio toba ya Tanzania pekee wala New York Pekee wala Brazil, Ni toba ya ulimwengu mzima nchi chache zimeweza kugundua siri ya kuliitia jina la bwana walifanya vema nchi chache na viongozi wachache sehemu fulani fulani za dunia wameweza kufunnga na kuomba kwaajikli ya janga hili la Corona ambalo ni janga la dunia sasa ni wakati wa umoja wa mataifa kutambua kuwa yuko Mungu wa kweli, sio kenya pekee wala tanzania pekee wala Brazil pekee wao wameshafanya sehemu yao kila mtu anapaswa kufanya toba kwa sehemu yake Lakini wito kwa viongozi wa umoja wa mataifa na mashirika makubwa ya kimataifa ulimwenguni wanapaswa kutambua kuwa Yuko Mungu aliyehai, ambaye tukimuita kwa pamoja bila jujali itikadi zetu atatuitikia katikamelikebu wale watu waliomba na Yona waliomba bila kujali itikadi zao na melikebu ikatulia Yona naye aliomba kwa namna yake na Mungu akamsikia Yona hapa anawakilisha Israel na watu katima melikebu wanawakilisha ulimwengu na Nahodha wa melikebu anawakilisha umoja wa mataifa kupata suluhu hapa ni kuliitia jina la Mungu aliye hai kwa dunia nzima, tukifanya hivi dunia itatulia na wote tutampenda Mungu, Lazima sasa dunia ionyeshe upendo kwa Mungu kwa sababu yeye alitupenda kwanza 

1Yohana 4;19 “Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza.” Mwandishi anampenda Mungu aamtukuza kwa kuwa ni Mungu anayesikia maombi na kuyajibu.


Tunapozungukwa na Kamba za mauti   

 
Kifo ni moja ya adui yetu mkubwa duniani chenyewe huanza kututafuta dakika moja kuanzia unapozaliwa kitakuandama tu kuhakikisha kuwa kinakuondoa duniani, hivyo hatupaswi kujisahahu hata kidogo, tunazungukwa na kamba za mauti zinatuvuta tufe Mungu ametufundisha mambo ya ajabu kupitia gonjwa hili la corona linatunyoosha linatishia kifo cha kiuchumi, linatishia matajiri linatishia masikini Mungu ameruhusu, ni kamba za mauti zinatuzunguka kila mahali bila kujali wewe ni nani, narudia tena bila kujali wewe ni nani? Kama mtoto wa malikia wa uingereza anaugua Corona, kama waziri Mkuu wa uingereza anaingia ICU kwaajili ya Corona, ni Fundisho kuwa wewe na mimi kama si Bwana hatuwezi kupenya, bila neema ya Mungu hatuwezi kutoboa ni kamba za mauti zinazunguka kila mahali, je ni nabii gani sasa anaitisha maombezi dhidi ya korona mbona imebadili mifumo yatu ya maisha mpaka mifumo ya kuabudu, Je ni shetani? Je ni Pepo? Vyovyote iwanvyo yesu ndiye mwenye funguo za mauti na kuzimu bila ruhusa yake corona haiwezi kuitikisa dunia ukiona hili Mungu maeruhusu, ili tuwe wanyenyekevu, ili tukumbuke kumuheshimu, ili tukumbuke kuwa yeye yupo ili tukumbuke kuwa dunia sio ya taifa fulani, Hatari za kifo zilimzunguka mwandishi wa zaburi hii na sio hatari tu mwenyewe anaziita kamba za mauti, shida za kuzimu na taabu na huzuni vilimuandama hii ndio hakli ya dunia kwa sasa, Dunia inazungukwa na kamba za mauti kila mahali watu wamejaa hofu ya kifo, idadi ya wagonjwa inaongezeka na idadi ya vifo inaongezeka, hakuna usalama watu hawaaminiani wala hawajiamini hata wao wenyewe, wale wanaougua ndio zaidi na hata wale waliopona wanaweza kukusimulia maumivu makali waliyokutana nayo, ndoto nza kaburi walizoziona je unapopokea taarifa kuwa una Corona unakuwa katika hali gani, familia ambazo ndugu zao au jamaa zao wamebainika kuwa wana Corona na hata wataalamu wa Afya wanaowauguza wagonjwa hao wako katika hali gani? Unaposafiri nani anakuamini, mbuga za wanyama zina hali gani, sekta za usafiri zina hali gani, secta ya utalii ina hali gani, wafanyakazi wa serikali na secta binafsi zina hali gani wakati huu? Hata makanisa na mkisikiti na vionghozi wa dini tuna hali gani? Kamba za mauti zinaizunguka dunia, Mwandishi anasema


  Zaburi 116:3-4Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na huzuni; Nikaliitia jina la Bwana nakuomba sana, Uniokoe nafsi yangu  


Hii ni halia inayomzunguka mtu aliye hai lakini anayezingirwa na halia ya mauti anakiona kifo kikiwa kinamuwania kwa kila namna hatuwezi nkukikwepa kiko hewani tu, hata kiliowakuta walitoka wakijiamini kama wewe na mimi, Mwandishi anasema alipoona anazungukwa ma kamba za mauti na shida za kuzimu zilimpata na aliona taabu na huzuni yeye aliliitia jina la Bwana, dunia inaangalia suluhu kwamba itapatikana wapi pamoja na tahadhari zote tunazozichukua suluhu ni kuliitia jina la Bwana 

WARUMI 10:13 “KWA KUWA KILA ATAKAYELIITIA JINA LA BWANA ATAOKOKA

 hakuna nafasi kwa mwanadamu kujiokoa yeye mwenyewe Mungu alimleta mwokozi kwaajili ya ulimwengu wakati huu ni lazima tumuite Yesu kwaajili ya usalama wetu tumeweza kufanya kitaifa lakini kanisa linaweza kuendelea, Biblia inatuagiza kuomba bila kukoma, kwa nini tumuombe yeye Mungu mwandishi anasema Mungu ni mwenye rehema ona 

Zaburi 116:5-6 “Bwana ni mwenye neema na haki, Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema. Bwana huwalinda wasio na hila; Nalidhilika akaniokoa”, 

unaona Mungu ataziokoa nafsi zetu, Mungu ataiokoa nafsi yako kwa sababu ni wa neema na haki, kwa sababu ni mwenye trehema kwa sababu huwalinda wasio na hila na tunapodhikika hutusikia ni maombi tu ndio njia pakee ya kututoa katika janga hili Yesu Kristo mwenyewe alitufundisha kivitendo umuhimu wa kumuomba Mungu 

Luka 6;12  Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu.” 

Mungu atashughulika na kila aina ya kamba za mauti zinazokuzunguka. Ukiacha corona ziko kamba nyingine za mauti zinazokuzunguka zote kumbuka kuzisogeza mbele za Munhu wetu naye atakusaidia hatoakuacha


Mwitikio wa Mungu wetu tunapoliitia jina lake


Mwandishi alipokuwa katika hali hizo ngumu zlizomzunguka katika maisha yake na taabu zilizomzunguka katika maisha yake na magumu yaliyokuwa yakimzunguka katika maisha yake Mungu aklimuitikia kwa msingi huo aliweza kugundua kuwa kwekli Mungu ni mwema mno Mungu ni mwingi wa rehema , mwenye huruma na neema naye huwahurumia watu wake wanaoteseka na huwaokoa ndivyo neon lake lisemavyo angalia 

Zaburi 86:5 “Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe, Na mwingi wa fadhili, Kwa watu wote wakuitao.” 

Hatustahili kuishi, tulistahili kufa kwa sababu wote ni wenye dhambi hakuna aliye mwema lakini trehema za mungu na neema yake zinamfanya atuitikie na zinamfanya atuokoe na mauti na kutuweka huru kutoka katika kamaba za Mauti, jambo pekee litakalotuletea neema ya mungu ni kumlilia yeye na kumwambia Eeebwana utuhurumie, eee mwana wa Daudi utuhurumie Roho Mtakatifu utuhurumie, roho zetu na za familia zetu na za watu wa taifa letu na taifa lako Israel na jamii ya dunia na irehemiwe mbele zako na Mungu atasikia dua zetu, tuache ushabiki, wakati huu, tusijitukuze sana wakati huu na kujifikiri kuwa sisi ni bora sana wakati huu hapa ni toba tu bila kujali wewe ni nani na kuziitia rehema za Mungu


Mungu atafanya nini?  Zaburi 116: 6 “Bwana huwalinda wasio na hila; Nalidhilika, akaniokoa Mungu alimuokoa na Mungu alimlinda mtumishi wake mwandishi wa zaburi hii kwa sababu wakati huu aliacha hila aliacha nia mbaya aliacha kiburi na alijinyenyekeza, Neno hilo Nalidhilika maana yake nilijishusha nilijinyenyekesha sikujifanya mtu maalumu, nilijishusha nilishuka chini, nilijinyenyekeza kwenye nafasi ya mtu anayehitaji msaada, wakati huu tuache kiburi cha kidhehebu, tuache kiburi cha kidini, tuache kujifanya sisi ndio manabii na mitume na wachungaji wakubwa na kadhalika tujinyenyekeshe na Mungu wetu ataturehemu, wakati mambo yanapokuwa mabaya acha kujitokeza na kujifanya kuwa wewe ndio msemaji wa Mungu, pekee duniani, Ndio maana wako waliosema corona itafutika na corona ikaendelea huu sio wakati wa kujifanya wewe ni mtu maalumu ni wakati wa kujidhili na wakati wa magoti, ni wakati wa kutulia na kumuacha Mungu atusaidie Mungu asipokuwa msaada wakati huu nafsi zetu zitanyamazishwa ona 

Zaburi 94:17 “Kama Bwana asingalikuwa msaada wangu, Nafsi yangu kwa upesi ingalikaa penye kimya. Wale wenye hekima ya dunia hii na wenye kiburi wanaweza kudhani kuwa Mungu sio msaada wao wakati huu, Lakini huu sio wakati wa kujitukuza na kutafuta kiki, lazima sasa tumuachie Mungu apangue, asafishe afanye yaliyo mapenzi yake na kwa unyenyekevu Mkubwa Mungu atatuponya tu, kwa sababu tuko mbali na hila na kiburi na tumeamua kujinyenyekeza, kumbuka kuwa  Bwana huwapinga wenye kiburi bali huwapa wanyenyekevu neema, sote tuko katika umbo la Nyangumi na tunapaswa kuomba rehema za Mungu naye atatusaidia katika njia anayoijua yeye, sio wakati wa kunyooshea kidole mtu Fulani dhilika yaani nyenyekea, usijifany mwenye hekima wakati huu zaidi ya toba hekima kubwa wakati huu ni toba wala tusidhani imetosha nni toba wala tusiombee kingine chochote ni toba na rehema tu na Mungu atatuitikia alimuitikia yona kwenye tumbo la Nyangumi atatuitikia na sisi katika nchi ya walio hai haleluya!

  1Wakoritho 1:27” bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;asomaye na afahamu.


Na Mchungaji. Innocent Kamote


Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Jumatatu, 20 Aprili 2020

Moyo wangu Unapozimia!


Zaburi 61:1-8Ee Mungu, ukisikie kilio changu, Uyasikilize maombi yangu. Toka mwisho wa nchi nitakulilia nikizimia moyo, Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda. Kwa maana ulikuwa kimbilio langu, Ngome yenye nguvu adui asinipate. Nitakaa katika hema yako milele, Nitaikimbilia sitara ya mbawa zako Maana Wewe, Mungu, umezisikia nadhiri zangu. Umewapa urithi wao waliogopao jina lako. Utaziongeza siku za mfalme, Miaka yake itakuwa kama vizazi vingi. Atakaa mbele za Mungu milele, Ziagize fadhili na kweli zimhifadhi. Ndivyo nitakavyoliimbia jina lako daima, Ili niondoe nadhiri zangu kila siku.



Utangulizi:


Zaburi ya 61 Ni mojawapo ya zaburi iliyoandikwa na Mfalme Daudi wakati alipokuwa amekimbia ikulu na akiwa katika hali ya kutokuwa salama, wakati huu inaonekana Daudi anaaanza kwa kulia  na huku akiwa amezimia moyo yaani amevunjika moyo au amekata tamaa mno, na anaamua kuliitia jina la Mungu wake katika Maombi, kwa nini anamuitia Mungu kwa sababu wakati huu anaona wazi kabisa kuwa njia pekee ambayo kwayo anaweza kuwa salama na kutiwa moyo ni kwa mwamba wa wokovu wake ambaye ni Mungu na ya kuwa yeye pekee naweza kumuinua na kumuweka juu ya mwamba asioweza kuupanda naye atakuwa salama dhidi ya adui zake

Unapoifanyia uchunguzi wa kina zaburi hii unaweza kuona wazi kuwa iliandikwa wakati Daudi akiwa mfalme ona msatri wa  Zaburi 61:6 Utaziongeza siku za mfalme, Miaka yake itakuwa kama vizazi vingi.” Unaona wakati huu inaonekana wazi kuwa Daudi alikuwa amelazimika kukimbia ikulu, lakini pia kwenda mbali na hema ya kukutania ambayo ilikuwa ni ishara inayoonekana ya Mungu asiyeonekana kwa hiyo ni wazi hiki kilikuwa ni kipindi Daudi alipinduliwa kwa Muda na mwanae mpendwa Absalom wakati alipomuasi baba yake, unaweza kuigundua siri hii wazi kama mwanafunzi wa neno lake.

Kila mmoja wetu anaweza kuwa na wakati ambapo anapitia Mambo magumu, vita au mateso na mapambano ambayo wakati mwingine yanaweza kumuumiza moyo kwa kiwango cha kuzimia Moyo, ni muhimu kukumbuka kuwa wewe sio wakwanza sio wewe peke yako unayepitia hali kama hizo sote tunapitishwa, sote tunavunjika moyo sote kuna wakati tunazimia Moyo hata kama kwa nje watu wanatuona kama wafalme, lakini sisi tunaopitia katika dhiki na mapito na mateso hayo kwa kweli wakati mwingine tunalemewa sana kiasi cha kukosa matumaini na kulia au kuvunjika moyo, hali hii ndiyo iliyompata mfalme Daudi wakati huu ona

2Samuel 15:14,30  Basi Daudi akawaambia watumishi wake wote waliokuwa pamoja naye Yerusalemu, Ondokeni, tukakimbie kwa kuwa tusipokimbia hapana mtu miongoni mwetu atakayeokoka mikononi mwa Absalomu; haya! Fanyeni haraka, tuondoke, asitupate Kwa upesi, Na kutuletea maovu, na kuupiga mji huu kwa makali ya upanga.,
Daudi akapanda akishika njia ya kuupandia mlima wa Mizeituni, akilia alipokuwa akipanda; naye alikuwa amejifunika kichwa chake, akaenda hana viatu; na watu wote waliokuwa pamoja naye wakajifunika vichwa vyao, kila mmoja wao, wakapanda juu, wakilia walipopanda.“ 

Daudi anaonyesha kuwa kuna wakati mashujaa wanakata tamaa na hata yeye alikuwa na wakati mgumu mno wakati huu lakini pamoja na magumu hayo yote alijitia moyo kwa namna ambayo itatutia moyo sisi nasi


1.       Alimlilia Mungu, aliomba na alimsihi Mungu asikie Dua zake, inawezekana alichanganya na toba katika maombi yake alimsihi Mungu, alimwambia Mungu kuwa hata kama angepelekwa uhamishoni utumwani ambao wana wa Israel zamani waliita mwisho wanchi yaani mahali ambapo huwezi kujikomboa wala kujitoa ni eneo la mashaka bado aliamini Mungu kuwa anaweza kumtoa huko nako yeye alikuwa amejaa shuhuda kuwa tangu zamani Mungu amekuwa kimbilio lake na wokovu wake anajua na kuamini kuwa Mungu atamtoa katika hakli anayoipitia na atampandisha juu mahali pa juu kwenye mwamba asioweza kuupanda ni Mungu pekee anayeweza kuzihuisha nafsi zetu tunapokuwa tumekata tamaa na kwa sababu hiyo ni muhimu kwetu tukamlilia yeye kwa dua na maombi Zaburi 23:3Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.”

2.       Alimsihi Mungu amuweke mbali na jaribu anasema hivi Zaburi 61:2bUniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda.” Hapa kuna mambo ya msingi mawili Mwamba asioweza kuupanda inaweza kumaanisha kwanza Mungu ampe kulishinda jambo gumu ambalo yeye kwa akili zake na ujuzi wake na utaalamu wake ilikuwa ngumu sana kupambana nalo, wakati mwingine tunakutana na mambo magumu sana duniani ambayo wataalamu, watumishi wa Mungu, makuhani manabii,madaktari na wanasiasa, na watawala wanasaikolojia na wanafalsafa huwa wanakosa majibu, kumbuka Daud alikuwa jemadari wa vita, mtaalamu na mtu hodari lakini hapa majemadari wengine walikuwa upande wa mwanae Absalom na yeye hawezi kupigana kumuua mwanae na huwezi kupigana vita ngumu ya namna hii, unawezaje kumuua mwanao mrithi wako kisha ukajiita shujaa? Unawezaje kumuua mtu ambaye wengine wanampenda na kumuheshimu na kumuona kiongozi? Kama hutaonekana una wivu? Ulikuwa ni mwamba usioweza kupandika ilikuwa ni lazima akate tamaa na kuzimia moyo, ziko vita vyingine unapambana mpaka unazimia moyo, unashindwa kujua utapenya namna gani na ni Mungu pakee anayebaki kujua hatima yako, usiogope endelea kuliitia jina la Bwana Mungu wako, Yeye alimsihi Mungu amuweke mbali na jaribu! Ambalo yeye aliliona kuwa hawezi kulikabili, kila tunapokabniliana na jambo tusiloweza kulikabili duniani basi ni vema tumkabidhi Bwana Mungu wetu!

3.       Alimtambua Mungu kama Ngome yenye nguvu
Zaburi 61:3-5Kwa maana ulikuwa kimbilio langu, Ngome yenye nguvu adui asinipate. Nitakaa katika hema yako milele, Nitaikimbilia sitara ya mbawa zako Maana Wewe, Mungu umezisikia nadhiri zangu. Umewapa urithi wao waliogopao jina lakoTunapomuendea Mungu kwa magumu yoyote tunayokabiliana nayo ni lazima tukubali na kutambua yuko Mungu ambaye ni mkuu mno kuliko jaribu tunalolipitia, Japo Daudi alitambua ukubwa na ugumu wa yale aliyoyapitia lakini alitambua Kuwa Mungu ni ngome yake yenye nguvu na tena amekuwa kimbilio lake na ni ngome yake na hivyo adui hatampata, hii sio tu itatokea katika jaribu hili lakini imekuwa kama shuhuda ya historia ya maisha yake, wakati mwingine ni muhimu kukumbuka kuwa Mungu alitufanyia nini alituvusha katika magumu ya namna gani na tukubali na kutambua kuwa atatuvusha katika hili pia linalotukabili.
Wakati huu dunia inapokbaliana na adui Corona (COVID 19) kila mtu anayeliogopa jina la Mungu atapata urithi, Mungu atakutunza haijalishi corona inatishia kwa kiwango gani vyovyote iwavyo tuihesabu kuwa ni adui kwa maisha yetu, lakini haiba nguvu kama alivyo Mungu wetu yeye aliyetuhifadhi maisha yetu katika namna nyingi na kwa njia nyingi atatupitisha pia katika janga hili na kutuweka mahali salama, usiogope wala usizimie moyo!

4.       Aliagiza fadhili za Mungu zimhifadhi!
Zaburi 61:6-8 “Utaziongeza siku za mfalme, Miaka yake itakuwa kama vizazi vingi.  Atakaa mbele za Mungu milele, Ziagize fadhili na kweli zimhifadhi. Ndivyo nitakavyoliimbia jina lako daima, Ili niondoe nadhiri zangu kila sikuDaud alijiombea aongezewe siku nyingi, alijiombea kukaa katika uwepo wa Mungu milele lakini alimsihi Mungu aagize Fadhili zake zimhifadhi, kuwepo kwetu duniani hakutokani na nguvu zetu, kuwa kwetu kwenye cheo chochote hakutokani na nguvu zetu, Ni fadhili za Mungu tu, Mungu alimuongezea Daudi siku za ufalme kweli alikuwa amekimbia ikulu, kweli mwanaye mwenyewe alikusudia kumuua, lakini dua hii ilisikiwa aliziomba fadhili za Mungu zimhifadhi, Ni lazima tumtegemee Mungutu lazima tuzitegemee fadhili zake, fedha na nguvu na madaraka na ukuu si kitu bila fadhili za Mungu, kule Italy watu walitupa fedha zao, walikuwa wamebaini kuwa fedha haiwezi kukusaidia kitu, cheo hakiwezi kukusaidia kitu, Mungu ndiye kila kitu katika maisha yetu, bila fadhili za Mungu huwezi kujikinga na kifo wala huwezi kujikinga na tauni ya corona, kwa hiyo wakati kila kitu kinasambaratika duniani uko mkono mwingine mkono wenye nguvu unaoweza kutushika wakati wa mambio mabaya, utakaotuongoza na kutuweka juu mahali salama ambako hatuwezi kukumwa na dhuruba ya aina yoyote, ambapo tutasimama na kujisikia kuwa tuko salama huko si kwinhineko ni kwenye fadhili za Mungu ni kwenye uwepo wake tu, huko ndiko kwenye ngome imara ni kwa bwana wetu Yesu Kristo yeye pekee ndiye mwenye sifa ya kuokoa hakuna Mungu mwingine anayeweza kuokoa na kuponya ni Yesu tu yeye ndiye mwenye nguvu na ni yeye pekee anayeweza kutuweka juu ya mawimbi hata mioyo yetu inapozimia, kwake yeye ndiko Tumanini letu liliko hata kutokee nini. Usizimie moyo Yesu ni mkuu kuliko dhuruba tunazozipitia.

Katika nyimbo  za Dini za Kanisa la Anglican kuna wmbo mzuri unaotutia moyo wakati Mioyo yetu ilipozimia na ukiuimba utahuisha moyo wako na kukupa ngvu mpya ni wimbo namba 413 tune 246 unaitwa Ee Mungu Baba, kuna ubeti unaosema Uzimiapo Moyo wangu baba Unipe Roho yako awe name, Roho Mtakatifu ni faraja kubwa sana tunapozimia Mioyo naye atatuhuhisha tena !


Ee Mungu Baba, Haba Duniani
Imeparuza sana njia yangu,
Unipe Moyo wa kusema hivi
Mapenzi yako yatimizwe

Nikiwa nina taabu na huzuni
Nikae kimya nisinung’unike
Niseme tu alivyosema Yesu
Mapenzi yako yatimizwe

Ninapofarakana na rafiki
Niwapendao niko paka yangu
Ni amri yako name ningejibu
Mapenzi yako yatimizwe
Ujaponiamuru nikiache
kinachonipendeza sicho change
nakupa tu kilicho mali yako
Mapenzi yako yatimizwe

Uzimiapo Moyo wangu baba
Unipe Roho yako awe nami
Mengine yote ninakuachia
Mapenzi yako yatimizwe

Nataka nia yako iwe yangu
Utoe kila kitu ndani yangu
Kinachonizuia nisiseme
Mapenzi yako yatimizwe
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
0718990796

Jumamosi, 18 Aprili 2020

Wenye haki ni wajasiri kama simba !

Mithali 28:1 "Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu; Bali wenye haki ni wajasiri kama simba."

Ufunuo 5:1-5Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba. Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, N'nani astahiliye kukifungua kitabu, na kuzivunja muhuri zake? Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, SIMBA ALIYE WA KABILA YA YUDA, SHINA LA DAUDI, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba.”





Utangulizi:


Je ni Jambo gani hukujia kwanza kwenye akili zako mara unapomuona simba? Au unaposikia habari zake, Je nguvu zake, au kutisha kwake?, au ushujaa wake, au uzuri wake, uwezo wake, na muonekano wake, vyovyote vile itakavyokujua ni lazima tukubaliane kuwa simba ni mnyama maalumu sana, na umaalumu wqake utakufanya ukubali kuwa ni mfalme wa nyika, Japo wanapenda sana kukaa katika nyasi, Simba kama mnyama ana tabia ambazo kila mtu shujaa anapaswa kuwa nazo hapa duniani, leo tutachukua muda kujifunza tabia kadhaa za simba na kisha tutaziangalia namna tunavyoweza kuzitumia katika maisha yetu.
1.       Simba ana mtazamo tofauti na wanyama wengine.





Moja ya sifa inayomfanya simba kuwa mwindaji mzuri sana ni uwezo wake wa kuona, yaani mtazamo wake Jicho au macho ya samba katika mwanga wa kawaida yana uwezo wa kuona mara sita zaidi ya macho ya mwanadamu, na ndio maana samba wanauwezo mkubwa wa kuwinda usiku, uwezo wake wa kuona unampa uhakika wa kupata mawindo wakati wowote anapotaka mawindo, ana uwezo wa kukimbia kilomita 80 kwa saa na uwezo wa kuruka juu futi thelathini na sita wakati akikimbia, uwezo wake wa kutazama mambo unamfanya awe bora zaidi kuliko wanyama wengine japokuwa yeye
a.       Yeye sio mrefu kuliko wanyama wote (twiga ni mrefu kuliko yeye)
b.      Yeye sio mkubwa kuliko wengine (Tembo na faru na kiboko ni wakubwa kuliko yeye)
c.       Yeye sii mzito kuliko wengine ( Kiboko ni mzito zaidi na tembo pia)
d.      Yeye sio mzuri kuliko wengine (punda Milia ni mnyama mzuri zaidi)
e.      Yeye hatishi sana kuliko wengine ( Nyati anatisha mno kuliko yeye)
f.        Lakini simba ni mfalme na mtawala wa nyika
Simba anatufundisha kuwa uwezo wa mtu kuongoza hautokani na ukubwa alionao, uzito alionao, akili aliyo nayo, elimu aliyonayo, vitishio alivyonavyo, uzuri alionao utisho ulionao, Lakini namna unavyofikiri au namna unavyoona mambo, uwezo wa kiongozi uko katika mtazamo, tembo ni mkubwa sana lakini ndani hujiona kuwa yeye ni chakula cha simba, Simba huwaona wote hao kuwa ni chakula kwake, Hatuwaongozi watu kwa kuwatisha au kuwaogopesha bali watu wakituona tu watatuheshimu kwa muonekano wetu na mtazamo wetu, Simba hueshimika mara moja watu wanapomuona na kukubali kuwa yeye ndiye, kweli mfalme wa nyika

Isaya 11:1-4
Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda.  Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana; na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana; WALA HATAHUKUMU KWA KUYAFUATA AYAONAYO KWA MACHO YAKE, WALA HATAONYA KWA KUYAFUATA AYASIKIAYO KWA MASIKIO YAKE; bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.”
2.       Simba ana Sauti yenye kusikiika kuliko wengine.






Kuna wanyama wakubwa sana kumzidi Simba nyikani, wana nguvu kumzidi Simba na warefu kumzidi Simba lakini moja ya jambo linalomfanya Simba kuwa tofauti na wao ni sauti, Simba wana sauti kubwa na inayosikika inaemekana kuwa Simba anapounguruma uwezo wa sauti husikika kama miles 5 yaani sawa na kilomita 8, Sauti yake ni kama onyo kwa kila kiumbe kwamba Mfalme wa pori ameunguruma, unaweza kuwa na mawazo mazuri lakini kama hujui kujieleza huwezi kueleweka , unaweza kuwa na nguo za kiaskari lakini kama huna mamlaka huwezi kutiisha wala kutawala, unaweza kuwa na sifa zote njema lakini bila uadilifu huwezi kuogopwa, ukikosa uadilifu huwezi kuheshimiwa, unaweza kuwa na mawazo mazuri lakini usipofungua kinywa kuyasema hakuna atakayejua ni namna gani una hekima, Kuna wanyama wakubwa mno kuliko, Simba kuna wenye nguvu kuliko yeye, kuna wepesi kuliko yeye na wawindaji wazuri kuliko yeye lakini nini ninamfanya samba aogopwe ni sauti yake ni mamlaka yake ni haki yake, wengi wetu hatujawahi kumjua plato lakini tuna maneno yake na hekima yake kwa sababu alisema, tunawajua watu wengi sana ambao hatujawahi kuwaona kutiokana na kile walichiokisema, watu hodari ni wanenaji hodari  Yesu likuwa na uwezo katika kunena na kutenda

Luka 24:19
Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote;

Matendo 7:22
Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa hodari wa maneno na matendo.

Matendo 18:24 -26
Basi Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzalia wa Iskanderia, mtu wa elimu, akafika Efeso; naye alikuwa hodari katika maandiko. Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohana tu. Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Prisila na Akila walipomsikia wakamchukua kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi.
Muungurumo wa simba porini uwezo wake na nguvu ya sauti yake hudhihirisha na kuwajulisha kuwa simba yupo, na hata kama yuko mbali unaweza kufikiri yuko karibu na utisho wake hufika kila mahali, ni muhimu kufahamu kuwa sio kila tunachokisema tu ndio kinaweza kutufanya kuwa viongozi wazuri bali pia  yale tunayoyatenda, viongozi wote wazuri katika biblia walikuwa hodari katika kunena na kutenda, kwa maneno yetu na matendo yetu sifa zetu huenea kila mahali, Simba anakuwa na ujasiri sio tu kwa sauti yake bali pia na kutenda kwake sauti yake inatisha na matendo yake pia sauti yake inaonyesha ujasiri na matendo yake pia , Sauti yake simba humtangulia kila anakokwenda, hivyo ni muhimu maneno yetu na matendo yetu yakawa sambamba, tumia uwezo wako wote kuhakikisha kuwa unatimiza kusudi la Mungu.

3.       Simba huishi kijamaa.






Simba ni mnyama anayeishi kwa ajili ya jamii pamoja na ujasiri na uwezo wake mkubwa alionao wao huishi kijamii kwa kiingereza huitwa “PRIDES” ambayo maana yake - the achievements of those with whom one is closely associated, yaani mafanikio ya mmoja ni mafanikio yao wote kwa lugha nzuri tungeweza kusema kuwa Simba anaishi kijamaa, inasemekana kuwa simba hata kama utamuona peke yake wao huishi kwa makundi na kundi la simba katika familia yaio huwa ni kuanzia simba 15-40 kundi hili laweza kujumuisha masimba dume wakubwa na majike mengi na vitoto vya simba vingi, kadiri kundi linavyokuwa kubwa na  ndio nguvu yao inavyokuwa kubwa zaidi. Majike wengi pia hutegemea madume kwaajili ya ulinzi wa watoto wao. Usipende kubeba mzigo peke yako ulinzi na usalama wako hata kama wewe ni shujaa kiasi gani unategemea watu wote wakubwa kwa wadogo, wana wake kwa wanaume unapokumbana na changamoto mbalimbali ni muhimu kukumbuka kuwa hauko peke yako uko unawatu wanaokuzunguka Familia, tuna marafiki, watenda kazi wenzetu katika bwana, team work tunahitajiana,

Daniel 2:1-17
Hata katika mwaka wa pili wa kumiliki kwake Nebukadreza, Nebukadreza aliota ndoto; na roho yake ikafadhaika, usingizi wake ukamwacha. Ndipo mfalme akatoa amri kuwaita waganga, na wachawi, na wasihiri, na Wakaldayo, wapate kumweleza mfalme ndoto zake. Basi wakaingia, wakasimama mbele ya mfalme. Mfalme akawaambia, Nimeota ndoto, na roho yangu imefadhaika hata niijue tafsiri yake. Ndipo hao Wakaldayo wakamwambia mfalme, kwa lugha ya Kiaramu, Ee Mfalme, uishi milele; tuambie sisi watumishi wako ile ndoto, nasi tutakuonyesha tafsiri yake. Mfalme akajibu, akawaambia Wakaldayo, Neno lenyewe limeniondoka; msiponijulisha ile ndoto na tafsiri yake, mtakatwa vipande vipande, na nyumba zenu zitafanywa jaa. Bali kama mkinionyesha ile ndoto na tafsiri yake, nitawapa zawadi na thawabu na heshima nyingi; basi nionyesheni ile ndoto na tafsiri yake. Wakajibu mara ya pili, wakasema, Mfalme na atuambie sisi watumishi wake ile ndoto, nasi tutamwonyesha tafsiri yake. Mfalme akajibu, akasema, Najua hakika ya kuwa mnataka kupata nafasi, kwa sababu mmeona ya kuwa lile neno lenyewe limeniondoka. Lakini msiponijulisha ile ndoto, iko amri moja tu iwapasayo; maana mmepatana kusema maneno ya uongo, na maneno maovu, mbele yangu, hata zamani zitakapobadilika; basi niambieni ile ndoto, nami nitajua ya kuwa mwaweza kunionyesha tafsiri yake. Wakaldayo wakajibu mbele ya mfalme, wakasema, Hapana mtu duniani awezaye kulionyesha neno hili la mfalme; kwa maana hapana mfalme, wala bwana, wala liwali, aliyetaka neno kama hili kwa mganga, wala kwa mchawi, wala kwa Mkaldayo. Ni neno la ajabu, hili analolitaka mfalme, wala hapana mwingine awezaye kumwonyesha mfalme neno hilo, ila miungu, wasio na kikao pamoja na wenye mwili. Basi kwa hiyo mfalme akaghadhibika sana, akaona hasira nyingi, akatoa amri kuwaangamiza wenye hekima wote wa Babeli. Basi ile amri ikatangazwa, na hao wenye hekima walikuwa karibu na kuuawa; watu wakamtafuta Danieli na wenzake ili wauawe. Ndipo Danieli kwa busara na hadhari akamjibu Arioko, akida wa walinzi wa mfalme, aliyekuwa ametoka ili kuwaua wenye hekima wa Babeli; alijibu, akamwambia Arioko, akida wa walinzi wa mfalme, Mbona amri hii ya mfalme ina ukali namna hii? Ndipo Arioko akamwarifu Danieli habari ile. Basi Danieli akaingia, akamwomba mfalme ampe muda, kisha yeye atamwonyesha mfalme tafsiri ile. Ndipo Danieli akaenda nyumbani kwake, akawapasha habari kina Hanania, na Mishaeli, na Azaria wenzake; ili waombe rehema kwa Mungu wa mbinguni kwa habari ya siri hiyo, ili kwamba Danieli na wenzake wasiangamizwe pamoja na wenye hekima wa Babeli. Ndipo Danieli alipofunuliwa siri hiyo katika njozi ya usiku. Basi Danieli akamhimidi Mungu wa mbinguni.”

Daniel, Shadrack, Meshak na Aberdhego walikuwa mashujaa lakini walishirikiana pamoja katika kumuomba Mungu kwaajili ya changamoto walizokuwa wakikutana nazo wawapo, kazini na katika utumishi wao kwa jamii waliishi katika kundi ambalo kwa pamoja walijihisi salama wakiwa na imani moja.

Nyakati za kanisa la Kwanza tunafahamu kuwa mitume walikuwa na ushujaa mwingi ujasiri na kujiamini lakini hata hivyo wakati walipokutana na changamoto hawakuwa wakizibeba peke yao bali waliwashirikisha na kanisa na kumuomba Mungu pamoja na wote wakatiwa nguvu na Roho Mtakatifu ona Matendo ya

Mitume 4:18-31 “
Wakawaita, wakawaamuru wasiseme kabisa wala kufundisha kwa jina la Yesu. Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia. Nao walipokwisha kuwatisha tena wakawafungua, wasione njia ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu; kwa kuwa watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa hayo yaliyotendeka; maana umri wake yule mtu aliyefanyiwa ishara hii ya kuponya ulipita miaka arobaini. Hata walipofunguliwa, wakaenda kwa watu wao, wakawapasha habari ya mambo yote waliyoambiwa na wakuu wa makuhani na wazee. Nao waliposikia, wakampazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, Mola, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo; nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha babaetu Daudi, mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na makabila wametafakari ubatili? Wafalme wa dunia wamejipanga, Na wakuu wamefanya shauri pamoja Juu ya Bwana na juu ya Kristo wake. Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta, ili wafanye yote ambayo mkono wako na mashauri yako yamekusudia tangu zamani yatokee. Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu. Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.”


Kila mtu ata awe shujaa kiasi gani anahitaji wengine katika mafanikio yake na katika kutimiza malengo ya kiuongozi na kiutawala huwezi kufanikiwa ukiwa mwenyewe hata kama una nguvu na sauti kiasi gani.

4.       Simba wana muda mrefu wa Kupumzika.



Simba wana tabia ya kupumzika kwa muda mrefu sana inasemekana simba hutumia msaa karibu 20 wakiwa wamepumzika  kisayansi simba hawana mate mengi sana hivyo hupumika vya kutosha ili waweze kuwa na nguvu mpya zaidi, kuna tofauti kubwa sana kati ya mfalme na mtumwa, Mfalme anapaswa kuwa na muda wa kupumzika, lakini mtumwa anapaswa kufanya kazi kwa kiwango kikubwa sana mpaka kuwa mtumwa wa kazi, Mungu hubariki kazi za mikono yetu, na neno lake limesisitiza kuwa asiyefanya kazi na asile hivyo kufanya kazi ni mpango wa Mungu, lakini liko jaribu kwa wanadamu la kutaka kufanya kazi kupita kiasi hiii ni dhambi, Mungu ametufundisha katika neno lake kuwa na muda wa mapumziko na kutokuogopa maisha wala kuwaza itakuwaje kesho,

Mwanzo 2:1-3
Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.

kila siku tunaamka tukiwa na malengo au nkusudi fulani la kulitimiza na hatutaki kuacha nkitu kwaajili ya hayo tunajaribiwa kutokupumzika na tunajikuta tumekuwa watumwa wa kazi, Mungu anataka tufanye kazi lakini Mungu hatai tuwe watumwa wa kazi, tunajitoa kirahisi sana kwa watu na kazi, tukijichosha na kujiumiza sana na hivyo tunayafanyua maisha yetu kuwa ya kitumwa kabisa duniani na wala hatufurahii matunda ya kazi zetu, Simba hawako hivyotunapaswa kujifunza kutoka kwao, wana wanajua kuwa wanapaswa kula kila siku, lakini wanajua pia umuhimu wa mapumziko, simba halali na njaaa, ana uhakika wa kula, lakini wanapumzika kwa muda wa kutosha, kama mtu anataka kuyafurahia maisha ni lazima ajifunze kuwa hatupaswi kuacha hofu nza maisha zikatutawala kwa hiyo ni muhimu kuwa na muda wa kuyafurahia maisha na kujipumzisha relax

Mathayo 6:25-34
Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja? Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo. Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba? Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.
Simba wanapumzika wakijuankuwa wana uhakika watapata wanachikitaka na maisha yataendelea hawalali na njaa na hawaogopi njaa, wanajua watatumia muda mfupi na watapata wakitakacho.

5.       Simba hawana choyo




Simba hawana tabia ya choyo kwa kawaida samba wakiwa katika familia Jike ndiye anayefanya kazi ya kutafuta chakula na dume hubaki na familia na kulinda watoto, samba wanatabia ya kuwinda chakula cha kutosha kwaajili ya familia nzima na wanakula na kushiba na kusaza kasha samba huwaachia chakula fisi na tai mla mizoga aitwaye vulture ili nao waponee kwenye mawindo yake, hivyo simba huwinda kwaajili yake na wengine, Uwezo wa kuhsirikisha wengine Baraka za Mungu ni moja ya alama ya kiongozi na mtu aliyekomaa kiroho, Yesu alitufundisha kwamba ni muhimu kujilinda na choyo, uhai wa mtu hauko katika wingi wa vitu alivyonavyo ona

Luka 12:15-21
Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo. Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana; akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu. Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu. Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi. Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?  Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.”

Mungu anapokuwa amekufanikisha kwa Baraka zozote zile Baraka hizo sio kwaajili yetu wenyewe bali ni kwaajili yatu na wengine Simba huwa hasemi kwamba hii ni nguvu yangu mimi, nimetafuta mwenyewe, kwaajili ya nafsi yangu tu, hapana Simba hutafuta vya kutosha kwaajili ya jamii yaka na kwaajili ya wale wasio wa jamii yake samba wakishiba wanabakiza chakula cha kutosha nkisha fisi na ndege wa mwituni hujipatiamo humo, watu walio bora na viongozi walio bora hawana kitu chao wenyewe hufanya mambo kwa manufaa ya jamii na kwa manufaa ya watu wote, ni muhimu nkukumbuka kuwa wajibu wetu sio kutoa amritu na kuwatisha wengine au kuwafanya wengine wafanye kazi tu, tunao wajibu wa kuwatia moyo wengine na kuwaachia na wengine Baraka , Simba wakishiba baada ya kuwinda mawindo huwaachia wengine mabaki, ili nao wale waishi kwa nguvu za Simba, watu wenye choyo huzoa kila kitu hawaachi akiba hata kwa wanyonge hawajali yatima wala wajane wanakula kila kitu huo sio mpango wa Mungu

Kumbukumbu la Torati 24:18-22 “
bali kumbuka ya kuwa ulikuwa mtumwa katika Misri, Bwana, Mungu wako, akakukomboa huko; kwa hiyo nakuamuru kutenda neno hili. Uvunapo mavuno yako katika shamba lako, ukasahau mganda shambani, usirudi kuuchukua; na uwe wa mgeni, au yatima, au mjane; ili Bwana, Mungu wako, akubariki katika kazi yote ya mikono yako. Utakapochuma matunda ya mizeituni yako, usirudi kuchuma mara ya pili; yaliyobaki apewe mgeni, na yatima, na mjane. Uchumapo zabibu katika shamba lako la mizabibu, usichume mara ya pili; zilizobaki apewe mgeni, na yatima, na mjane. Nawe kumbuka ya kuwa ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri; kwa hiyo nakuamuru kutenda neno hili.Mungu anataka watu wake wajifunze ukarimu wawe watoaji kuna Baraka nyingi sana katika kutoa imeandikwa kuwa ni heri kutoa kuliko kupokea samba ni watoaji

Matendo 20:34-35 “Ninyi wenyewe mnajua ya kuwa mikono yangu hii imetumika kwa mahitaji yangu na ya wale waliokuwa pamoja nami. Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.


Kama unataka kuheshimiwa na watu hakikisha kuwa unatoa, hakuna kiwango cha maisha ambayo unapaswa kutokutoa kama hujayafikia waingereza wana usemi unaosema kumpa mbwa mfupa sio ukarimu ukarimu ni kushiriki mfupa na mbwa wakati wote mkiwa na njaa” Simba anapokula fisi huja kushiriki kula mwindo yake na hata hivyo akishiba huwaachia, ni mfalme gani anayekula vyote asiwaachie wale walio wanyonge wapate chochote.6.       Simba hugawana majukumu.

Simba wana mgawanyo wa majukumu hawafanyi kila kitu wenyewe, Mwandishi mmoja alisema hivi anaamini kuwa iko sababu kubwa sana kwa nini tumepewa mikono miwili na miguu miwili, na iko sababu ya kwa nini mwanadamu ana nguvu za kibinadamu na sio nguvu za farasi, hii maana yaka ni nini hatuwezi kufanya kila kitu wenyewe kwa sababu huwezi kuwa mahali kote kwa wakati mmoja hata kama utakuwa unatumia mafuta, hakuna muda wa kutosha kwa siku kwa mtu mmoja kufanya kila kitu, kwa msingi huo ni lazima tuwape majukumu watu wengine pia kuna usemi unaosema “ kama unataka kila kitu kifanyike kwa ukamilifu, basi fanya mwenyewe”  kwa bahatimbaya ukitaka kufanyia kazi  msemo huu utakufa haraka, ndio maana samba hugawana majukumu, wakati jike likienda kutafuta mawindo na kuleta chakula dume hubaki na familia na kuwalinda watoto, ni lazima tujifunze kuwa kumpa mtu mamlaka haimaanishi kuwa mtu huyo atakudharau, au atakuwa na mamlaka kuliko wewe, lakini badala yake ni utambuzi ya kuwa unatambua uweza na ufundi wa wenmgine katika kukamilisha mambo, na kuwa wao pia ni muhimu, kwa hiyo kiongozi mzuri haogopi kuwaamini wengine, Simba anapoacha jike likawinde yeye hubaki na majukumu mengine ya kuilinda familia kwa hiyo samba sio mvivu, lakini anatambua umuhimu wa kila mmoja katika familia na jamii na umuhimu wa majukumu ya kila mmoja  wagogo wanausemi kuwa ukikimbiza panya wawili kwa wakati mmoja mmoja atakuponyoka kwa hiyo ni muhimu kumuamini kila mmoja sawa na kipawa na karama aliyo nayo.

1Wakoriho 12:3-4
Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule.  Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.


Warumi 12:6-8 “Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.


Waefeso 4:11-13 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;”   
          
7.       Simba hulinda jamii yao na hatari






Kama tulivyoona kuwa simba jike mara kadhaa ndiye anayehusika na kuwinda kwa asilimia 85-90% wakati asilimia chache zinazosalia za uwindaji ndizo hufanywa na Simba Dume, katika mgawano wao wa kazi na majukumu wakati simba jike anawinda simba dume hufanya kazi ya kulinda jamii yake, Simba hulinda kundi lake lote lakini pia hulinda mipaka ya kundi lake kwa kiwango cha mile 100, yaani sawa na kilomita za mraba 160, katika eneo hilo lote chochote kitakachoaribia, kitaweza kufyekelewa mbali, Simba hatakubali adui akaribie jamii yake atapambana kuhakikisha jamii yake iko salama na wanaishi kwa amani, ni mpiganaji wa amani, wanautulivu hekima na busara na hutumia akili sana katika uwindaji wake lakini ni wapambanaji kwaajili ya jamii huyatoa maisha yao kwaajili ya wengine hawakubali kuona uonevu, hulinda simba wadogo na kundi zima


Yuda - Mwanzo 44:1-34,Akamwamuru yule msimamizi wa nyumba yake akisema, Jaza magunia ya watu hawa chakula kwa kadiri wawezavyo kuchukua, utie na fedha ya kila mtu kinywani mwa gunia lake. Na kikombe changu, kikombe kile cha fedha, ukitie kinywani mwa gunia la yule mdogo pamoja na fedha ya nafaka yake. Akafanya kama vile alivyomwambia Yusufu. Asubuhi kulipopambazuka, hao watu wakapewa ruhusa, wao na punda zao. Na walipotoka mjini, wala hawajaendelea sana, Yusufu akamwambia yule msimamizi wa nyumba yake, Ondoka, uwafuate watu hawa, nawe utakapowapata, waambie, Kwa nini mmelipa mabaya kwa mema? Je! Kikombe hiki, sicho anyweacho bwana wangu? Naye hufanya uaguzi kwa hicho. Mmefanya vibaya kwa kufanya hivi. Akawafuata, akawapata, na kuwaambia maneno hayo. Wakamwambia, Kwa nini bwana wangu anasema maneno kama haya? Hasha! Watumwa wako wasifanye hivi; tazama, hizo fedha mlizoziona kinywani mwa magunia yetu, tumekuletea tena kutoka nchi ya Kanaani. Tuwezeje sisi kuiba nyumbani mwa bwana wako fedha au dhahabu?  Atakayeonekana kuwa nacho miongoni mwa watumwa wako, na afe, na sisi nasi tutakuwa watumwa wa bwana wangu. Akasema, Basi na iwe hivyo kama mlivyosema, Mtu atakayeonekana kuwa nacho atakuwa mtumwa wangu, na ninyi mtakuwa hamna hatia. Wakafanya haraka, wakashusha kila mtu gunia lake, na kufungua kila mtu gunia lake.Naye akatafuta, akaanza kwa mkubwa na kuisha kwa mdogo. Kikombe kikaonekana katika gunia la Benyamini. Wakararua nguo zao, wakaweka kila mtu mzigo wake juu ya punda wake, wakarudi mjini. Akaja Yuda na ndugu zake nyumbani kwa Yusufu, naye mwenyewe alikuwamo, nao wakamwangukia kifudifudi. Yusufu akawaambia, Ni tendo gani hili mlilolitenda? Hamkujua ya kwamba mtu kama mimi naweza kufanya uaguzi? Yuda akasema, Tumwambie nini bwana wangu? Tusemeje! Tujivutieje haki? Mungu ameona uovu wa watumwa wako. Tazama, sisi ni watumwa wa bwana wangu, sisi na yeye ambaye kikombe kilionekana mkononi mwake. Akasema, Hasha! Nisifanye hivi; mtu ambaye kikombe kilionekana mkononi mwake, ndiye atakayekuwa mtumwa wangu. Nanyi enendeni zenu kwa amani kwa baba yenu. Ndipo Yuda akamkaribia, akasema, Tafadhali, bwana wangu, mtumwa wako na aseme neno moja masikioni mwa bwana wangu, wala hasira yako isimwakie mtumwa wako, maana wewe u kama Farao. Wewe, bwana wangu, ulituuliza watumwa wako, ukisema, Je! Mnaye baba, au ndugu? Tukakuambia wewe, bwana wangu, Tunaye baba, naye ni mzee, na mwana wa uzee wake ni mdogo, na nduguye amekufa; amebaki yeye peke yake wa katika tumbo la mamaye, na baba yake anampenda.Ukatuambia watumwa wako, Mleteni kwangu, ili macho yangu yamwangalie. Tukakuambia, bwana wangu, Kijana hawezi kumwacha babaye, maana akimwacha babaye, babaye atakufa.Ukatuambia watumwa wako, Asiposhuka ndugu yenu mdogo pamoja nanyi, hamtaniona uso wangu tena Ikawa tulipokwenda kwa mtumwa wako, baba yangu, tukamwarifu maneno yako, bwana wangu. Kisha baba yetu akanena, Rudini huko, mkatununulie chakula kidogo. Tukasema, Hatuwezi kwenda; ndugu yetu mdogo akiwapo pamoja nasi, tutashuka, maana hatutaweza kuuona uso wa mtu huyo, ndugu yetu mdogo asipokuwa pamoja nasi. Mtumwa wako, baba yangu, akatuambia, Mnajua ya kuwa mke wangu alinizalia wana wawili; mmoja alitoka kwangu, nikasema, Bila shaka ameraruliwa, wala sikumwona tangu hapo. Na mkiniondolea huyu naye, na madhara yakimpata, mtashusha mvi zangu na msiba kaburini. Basi, nikienda kwa mtumwa wako, baba yangu, na huyu kijana hayupo pamoja nasi, iwapo roho yake imeshikamana na roho ya kijana; itakuwa atakapoona ya kwamba huyu kijana hayuko, atakufa; na watumwa wako watashusha mvi za mtumwa wako, baba yetu, kwa huzuni kaburini Kwa maana mtumwa wako alijifanya mdhamini wa huyu kijana kwa baba yangu, nikisema, Nisipomrudisha kwako, nitakuwa na hatia kwa baba yangu sikuzote. Basi, sasa nakusihi, uniache mimi mtumwa wako nikae badala ya huyu kijana kuwa mtumwa wa bwana wangu; na huyu kijana umwache aende pamoja na nduguze. Kwa maana nitawezaje kumwendea baba yangu, na huyu kijana hayuko pamoja nami? Nisije nikayaona mabaya yatakayompata baba yangu.”

       
 Kutokana na kujitoa kwake na upendo wake mkuu aliokuwa nao Yuda Yakobo alipombariki alimtaja kuwa kama mwana Simba

Mwanzo 49:8-10 “Yuda, ndugu zako watakusifu, Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakuinamia.Yuda ni mwana-simba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakayemwamsha? Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.


Hiki ndio alichokifanya Bwana Yesu kwaajili yetu pamoja na waamuzi hawakukubali uonevu dhidi ya watu wao walipambana kuhakikisha nusalama wa watu wao hivyo ndivyo samba walivyo
Isaya 53:1-5Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani? Maana alikua mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani. Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.” Huu ni upendo mkubwa sana Yesu alikufa kwaajili yetu, Hatuna budi kuhakikisha kuwa tunasimama upande wake siku zote za maisha yetu, tusihesabu damu yake ya thamani kuwa kitu cha hovyo tudumu katika wokovu na kuwa wavumilivu kwaajili ya Mungu wetu.”
Ujumbe na Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
0718990796