Jumapili, 27 Septemba 2020

Bwana ni Mtu wa Vita!

Kutoka 15:2-3 BWANA ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza. BWANA ni mtu wa vita, BWANA ndilo jina lake.


 

Bwana ni Mtu wa Vita.

Ni muhimu kufahamu kuwa moja ya ufunuo mkubwa zaidi wa Mungu kwa wana wa Israel ukiacha kujitambulisha kama NIKO AMBAYE NIKO Mungu vilevile alijifunua kama Bwana wa vita au Mtu wa vita! Katika Biblia ya Kiebrania mara zote jina Yahweh, na jina Elohim wakati wote huambatana na neno tzevaotao Sabaothambayo maana yake ni Majeshi kwa hiyo jina la Mungu katika israel husomeka YHWH Elohe Tzevaot kwa kiingereza Jehova Lord of Host kwa kiswahili Bwana Mungu wa majeshiNeno hili Bwana wa Majeshi limejitokeza mara 300 katika biblia, Ufunuo huu kuhusu Mungu ulikuwa dhahiri hasa pale wana wa Israel  walipokuwa wamekwama katika eneo ambalo kushoto kulikuwa na mwamba mkubwa sana na kulia kulikuwa na mwamba mkubwa sana na mbele yao ilikuweko bahari ya shamu, wakati huu wakiwa katika kona hii, Farao aliwaamuru majeshi yake kuwafuatia wana wa israel na kuwaangamiza kabisa majeshi yake yalitii na kuwafuatia wana wa Israel ambao wakati huu walikuwa hawajajifunza vita na hawana wa kuwapigania

Kutoka 14:9-10
Wamisri wakafuata nyuma yao, farasi zote na magari yote ya Farao, na askari zake wenye kupanda farasi, na jeshi lake, nao wakawapata hali wamepanga pale karibu na bahari, karibu na Pi-hahirothi, kukabili Baal-sefoni. Hata Farao alipokaribia, wana wa Israeli wakainua macho yao, na tazama, Wamisri wanakuja nyuma yao; wakaogopa sana; wana wa Israeli wakamlilia BWANA.

  
Kwa Mujibu wa mwana historia wa kiyahudi wa nyakati ya karne ya kwanza Flavious Josephus anasema kwamba Majeshi yaliyokuwa yakiwafuatia Israel yalikuwa ni majeshi katili ya makomandoo hodari waliokuwa na Magari ya farasi 600, wapiganaji wa juu ya farasi 50,000 na askari wa miguu 200,000. kwa hiyo unaweza kupata picha kwa taifa hili changa ilikuwa ni haki yao kupiga kelele na kuhitaji msaada wa Mungu, Musa kama Nabii wa Bwana alisema kwa niaba ya Mungu kuwa Israel hawapaswi kuogopa badala yake wanatakiwa kusimama na kuuona wokovu wa Bwana!  Na kuwa hawa wamisri wanaowaona leo hawatawaona tena milele! Bwana atawapigania nao watanyamaza kimya 

Kutoka 14:13-14
Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.

Ni ukweli usiopingika kwamba Jeshi hili kali lingewamaliza Vibaya Israel bila huruma, lakini hata hivyo Bwana aliwapigania kwa jinsi ya ajabu mno, Kumbuka ya kuwa unaposikia Bwana anampigania mtu ni muhimu kufahamu kuwa huwa hapigani yeye, Yeye hutumia malaika wake

Mathayo 26:52-56
Ndipo Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga. Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika? Yatatimizwaje basi maandiko, ya kwamba hivyo ndivyo vilivyopasa kujiri?  wanauwezo mkubwa sana na wanapiga vibaya mno, Jambo kubwa ambalo Mungu alilifanya kwanza ni kumtuma malaika aliyesimama kuwatenga Israel na Majeshi ya wamisri

Malaika wa Bwana ndio hufabya kazi ya kupigania watu wa Mungu, Mungu hawezi kupigana na yoyote wala hawezi kupigana na kiumbe chake Yeye ni mwenye nguvu sana uwezo wake ni mzito mno ukimuona tu unakufa mwenyewe hata kabla ya lolote kwa hivyo yeye hutumia malaika ni malaika wa Bwana aliyekwenda kusimama katikati ya wana wa Israel na wamisri ona
 

Kutoka 14:19
Kisha malaika wa Mungu, aliyetangulia mbele ya jeshi la Israeli, akaondoka akaenda nyuma yao; na ile nguzo ya wingu ikaondoka hapo mbele yao, ikasimama nyuma yao;

Hapa Malaika wa Bwana alikuwa anatenganisha kwanza kwa ulinzi wake kwa kawaida Mungu anapotulinda hutumia malaika lakini pia hutumia ukuta wa moto ona
 

Zekaria 2:5
Kwa maana mimi, asema Bwana, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo utukufu ndani yake.”  

kuna hatua kadhaa hapa ambazo Mungu alizifanya na hatimaye Bwana akawapigania Israel ona
 Kutoka 14:19-28 Kisha malaika wa Mungu, aliyetangulia mbele ya jeshi la Israeli, akaondoka akaenda nyuma yao; na ile nguzo ya wingu ikaondoka hapo mbele yao, ikasimama nyuma yao; ikafika kati ya jeshi la Misri na jeshi la Israeli; napo palikuwa na lile wingu na lile giza, lakini lilitoa nuru wakati wa usiku; na hawa hawakuwakaribia hawa usiku kucha. Musa; akanyosha mkono wake juu ya bahari; BWANA akaifanya bahari irudi nyuma kwa upepo wa nguvu utokao mashariki, usiku kucha, akaifanya bahari kuwa nchi kavu, maji yakagawanyika. Wana wa Israeli wakaenda ndani kati ya bahari katika nchi kavu; nayo maji yalikuwa ukuta kwao mkono wa kuume, na mkono wa kushoto.  Na wale Wamisri wakawafuatia, wakaingia ndani kati ya bahari, farasi zote za Farao, na magari yake, na wapanda farasi wake. Ikawa katika zamu ya alfajiri, BWANA akalichungulia jeshi la Wamisri katika ile nguzo ya moto na ya wingu, akalifadhaisha jeshi la Wamisri. Akayaondoa magurudumu ya magari yao, hata yakaenda kwa uzito; na Wamisri wakasema, Na tukimbie mbele ya Israeli; kwa kuwa BWANA anawapigania, kinyume cha Wamisri. BWANA akamwambia Musa, Nyosha mkono wako juu ya bahari, ili maji yarudi tena juu ya Wamisri, juu ya magari yao, na juu ya farasi zao. Musa akaunyosha mkono wake juu ya bahari, na kulipopambazuka, bahari ikarudi kwa nguvu zake; Wamisri wakakimbia mbele yake; na BWANA akawakukutia mbali hao Wamisri kati ya bahari. Yale maji yakarudi yakafunikiza magari na wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahari nyuma yao; hakusalia hata mtu mmoja.

ni baada ya israel kushuhudia tukio hili kubwa la kushangaza na utaratibu ambao Mungu aliutumia kuwapigania israel, Waliimba nyimbo za furaha na sasa walianza kumtambua Mungu kama Mtu wa vita , watu wengi wanamjua Mungu kama Mwingi wa rehema na fadhila, wanamjua kama Mungu wa upendo lakini hawajui pia kuwa Bwana ni Mtu wa vita  A man of war” “warriorsasa basi kwanini linatumika jina Mtu kwa kawaida Mungu sio mtu lakini kwanini hapa linatumika neno Mtu? Biblia ya kiebrania inatumia neno Iyshlinasomeka ishi ambalo maana yake ni Mwanaume, kwa hiyo kiebrania Mwanaume wa Vitalakini vilevile mwanaume ni mtu na neno Mtu linapotumika kwa Mungu linamaanisha Yesu Kristo ambaye yeye ni jemadari wa vita ni amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Mbinguni, Yesu ana nguvu dhidi ya taifa lolote linalompinga yeye, anauwezo dhidi ya yeyote anayesimama kinyume na kusudi lake anauweza na nguvu za kupigana kinyume na yeyote anayeshindana kinyume na agano lake, hakuna mtu, wala mfalme wala rais, wala taifa, wala mamlaka wala wakuu wa giza wala majeshi ya pepo wabaya yanayoweza kupambana naye yeye ni Mtu wa vita israel waliona hili alipowapigania

Farao alifanya ujinga kuamuru majeshi yake kusonga mbele alipaswa kuwaonya mapema warejee nyumbani lakini kwaajili ya kiburi na ubishi aliendelea kupambana na kuwafuatia israel Mungu alimuonyesha uwezo wake wa ajabu wa kupambana Mungu alimtia fadhaa, mungu alichomoa magurudumu yao Mungu alirejesha maji ya bahari mungu aliwafutilia mbali

Jinsi Bwana anavyopigana vita

Ni muhimu kufahamu kuwa Mungu hapigani au hapiganii mtu au watu hovyo hovyo tu, kama watu wengi wanavyofikiri Mungu hupigania watu wake katika medani ya uadilifu na haki kwa njia ya  juu sana  Kumbukumbu 32:4 Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili.kwa msingi huo ili Mungu akupiganie kwanza ni lazima uzingatie maswala kadhaa yafuatayo;-

1. Lazima ujue Bwana yuko upande wa nani!

Maandiko yanasema Bwan akiwa upande wetu Ni nani aliyejuu yetu? Warumi 8:31 Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?kwa hiyo swali kubwa unapohitaji msaada wa Bwana kwanza ni lazima ujue uko upande gani na Bwana yuko na nani Joshua 5:13-15 Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akavua macho yake na kuangalia, na tazama, mtu mume akasimama kumkabili mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu? Akasema, La, lakini nimekuja sasa, nili amiri wa jeshi la Bwana. Yoshua akapomoka kiusouso hata nchi, naye akasujudu, akamwuliza, Bwana wangu aniambia nini mimi mtumishi wake? Huyo amiri wa jeshi la Bwana akamwambia Yoshua, Vua viatu vyako miguuni mwako; kwa kuwa mahali hapo usimamapo ni patakatifu. Yoshua akafanya vivyo.”  Hapa Yoshua anatokewa na yule mtu mume yule mtu wa vita amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Bwana na Yoshua anauliza swali la Muhimu sana uko upande gani, kwanini swali hili ni la Muhimu kwa sababu watu wote ni mali ya Mungu Mungu ni Mungu wa wote wenye mwili, kwa hiyo unaweza kudhani yuko na wewe kumbe hayuko nawe, ni hatari kupigana upande ambao Bwana yuko kisha wewe ukawa kinyume naye kwa hiyo ili uweze kushinda ni lazima uwe upande wake na Bwana awe pamoja nawe hii ni kanuni muhimu sana Kumbukumbu 1:42-45 Bwana akaniambia, Uwaambie, Msiende, wala msipigane; kwani mimi si kati yenu; msije mkapigwa mbele ya adui zenu. Basi niliwaambia, msinisikize, bali mliasi amri ya Bwana, mkajikinai, na kukwea mlimani. Na Waamori waliokuwa wakikaa katika mlima huo, waliwatokea juu yenu, wakawafukuza, kama wafukuzwao na nyuki,

wakawapomoshea Seiri mpaka Horma. Mkarudi mkalia mbele za Bwana; Bwana asiisikize sauti yenu, wala hakuelekeza masikio yake kwenu.

 unaweza kuona unapomtaka Bwana akupiganie kanuni ya kwanza Lazima Bwana awe upande wako na ndio maana watu wengi waliokuwa hodari wa vita kama Daudi mara kadhaa kabla ya kupigana vita ya aina yoyote waliuliza kwa Bwana kutaka kujua kuwa yuko na nani ona 2Samuel 2:1 Ikawa baada ya hayo, Daudi akauliza kwa Bwana, akasema, Je! Niupandie mji wo wote wa Yuda? Bwana akamwambia, Haya! Panda. Daudi akasema, Niupandie mji upi? Akasema, Hebroni.

 na 2Samuel 5:19 Basi Daudi akauliza kwa Bwana, akisema, Je! Nipande juu ya Wafilisti? Utawatia mkononi mwangu? Naye Bwana akamwambia Daudi, Panda; kwa kuwa hakika nitawatia Wafilisti mikononi mwako.

unaweza kuona kwa msingi huo kila mtu ambaye anataka Mungu ampiganie ni lazimaahakikishe kuwa Mungu yuko upande wake na ili Mungu awe upande wako ni lazima uishi maisha matakatifu, na yanayompendeza yeye nhuku ndiko kupigana katika mapenzi yake vinginevyo kichapo kitakuhusu.

2. Mungu hupigania mtu mwenye kusudi lake

Wako watu ambao wanabeba kusudi la Mungu, na umuhimu wao unakuwa ni mkubwasana katika macho ya Mungu kutokana na lile kusudi wanalolibeba, kama utapigana na mtu mwenye kusudi la Mungu, haraka sana Mungu atakuondoa wewe na atamuacha mtu mwenye kusudi lake aendelee kuwepo Matendo 5: 38-39 Basi sasa nawaambia, Jiepusheni na watu hawa, waacheni; kwa kuwa shauri hili au kazi hii ikiwa imetoka kwa binadamu, itavunjwa, lakini ikiwa imetoka kwa Mungu hamwezi kuivunja; msije mkaonekana kuwa mnapigana na Mungu.unaona Mungu hupigania mtu au watu ambao ana kusudi nao na kama utapambana na mtu mwenye kusudi la Mungu Mungu haoni vibaya kukushughulikia vikali yeye makusudi yake hayawezi kuzuilika hata kidogo ona Ayubu 42:2 Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika.kwa msingi huo kama mtu anapigana na Kanisa au israel au mtu mwenye kusudi la Mungu ni wazi kuwa unaweza kujikuta unapamba ana Mungu na ukasambaratika vibaya watu kama Ibrahimu, Isaka, Yakobo, Daudi na kadhalika ambao walikuwa wanabeba kusudi la Mungu ndani mwao, Mungu huingilia kati na kuwatetea sio kwa sababu wao ni wema sana bali kwa sababu wanakusudi lake ndani yao.

3. Mungu hupigania watu wanyonge wasioweza kujitetea

Mtu awaye yote ambaye ni masikini, mjane au yatima Zaburi 140:12 Najua ya kuwa Bwana atamfanyia mnyonge hukumu, Na wahitaji haki yao.Wanyonge masikini na wajane na yatima hutetewa na Mungu kwa msingi huo neno la Mungu linaahidi kuwa awaye yote atakayewadhulumu atapata hasara kubwa sana Mithali 22:16 Yeye awaoneaye maskini ili kuongeza mapato, Naye ampaye tajiri, hupata hasara. Mungu anachukizwa sana na dhuluma na uonevu hususani dhidi ya masikini unapoingia katika vita na watu wa namna hii ambao hawana uwezo wa kujitetea kutokana na unyonge wao basi ujue unapambana na Bwana ! Mithali 22:22-23 Usimnyang'anye maskini, kwa kuwa ni maskini; Wala usimdhulumu mtu mnyonge langoni; Kwa sababu Bwana atawatetea; Naye atawateka uhai wao waliowateka.Mungu hawezi kuvumilia uonevu wa mtu mnyonge hata kama Mtu huyo yuko mikononi mwa mtu wa Mungu, Kuna wakati Sara alimtesa hajiri sana mpaka hajiri akakimbia jangwani, Sara alikuwa tajiri na hajiri alikuwa mtumwa wake kwa msingi huo sara alifikiri ya kuwa ana hati miliki ya Mungu, Kumbe Mungu huweza kujali na kutetea yoyote amtakaye ona Mwanzo 16:1-10 Basi Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana, naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri. Sarai akamwambia Abramu, Basi sasa, BWANA amenifunga tumbo nisizae, umwingilie mjakazi wangu labda nitapata uzao kwa yeye. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai. Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri Mmisri mjakazi wake, baada ya kukaa Abramu katika nchi ya Kanaani miaka kumi, akampa Abramu mumewe, awe mkewe. Basi akamwingilia Hajiri, naye akapata mimba. Naye alipoona ya kwamba amepata mimba, bibi yake alikuwa duni machoni pake. Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. BWANA na ahukumu kati ya mimi na wewe. Naye Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake. Malaika wa BWANA akamwona kwenye chemchemi ya maji katika jangwa, chemchemi iliyoko katika njia ya kuendea Shuri. Akamwambia, Hajiri, wewe mjakazi wa Sarai, unatoka wapi, nawe unakwenda wapi? Akanena, Nakimbia mimi kutoka mbele ya bibi yangu Sarai. Malaika wa BWANA akamwambia, Rudi kwa bibi yako, ukanyenyekee chini ya mikono yake. Malaika wa BWANA akamwambia, Hakika nitauzidisha uzao wako, wala hautahesabika kwa jinsi utakavyokuwa mwingi.

4. Mungu hupigania watu wanyenyekevu /wapole.

Ogopa sana Mtu anayejishusha au mtu mpole ambaye yeye anamuachia Mungu tu kila kitu ili Mungu aingilie kati na kumtetea, Katika neno lake Mungu ameahidi kumwangalia mtu mnyonge ona Isaya 66:2 Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema Bwana; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.Mungu hana muda na mtu mwenye kiburi, unapokuwa na kiburi haraka sana unanyimwa neema na kupingana na Mungu ona Yakobo 4:6 Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu. mtu mnyenyekevu au mpole sana unapoingilia kati na kumsumbua Mungu ndiye atakayejibu kwa niaba yake ona Hesabu 12:1-10 Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi. Wakasema, Je! Ni kweli Bwana amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? Bwana akasikia maneno yao. Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi. Bwana akanena ghafula na Musa, na Haruni na Miriamu, na kuwaambia, Tokeni nje ninyi watatu, mwende hemani mwa kukutania. Basi hao watatu wakatoka nje. Bwana akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili. Kisha akawaambia, Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, Bwana, nitajifunua kwake katika maono, Nitasema naye katika ndoto. Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa? Hasira za Bwana zikawaka juu yao; naye akaenda zake. Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma.

5. Mungu hupigana kwaajili ya Jina lake takatifu

Kuna mambo Mungu anaweza kuyafanya katika maisha yetu kwa sababu tu tunabebajina lake Zaburi 23:1-3 Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.”  Kama ikitokea kuwa Mungu anaona jina lake linachafuliwa, Yeye amejikuza sana Duniani na jina lake amelitukuza mno Walawi 22:32 Wala msilinajisi jina langu takatifu; lakini nitatakaswa mimi katika wana wa Israeli; mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi,Inapotokea mtu anafanya mambo ya ajabu ajabu kisha anajivunia upuuzi wake kuliko jina la Mungu aliyehai Mungu husimama na mtu amabaye anajua kupitia yeye jina lake litatukuzwa ona 1Samuel 17:45 Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.

6. Mungu hupigana kwaajili ya masihi wake.

Watu waliotengwa kwa kusudi la kumtumikia Mungu huwa wanapakwa mafuta kwa kazi hiyo na maandiko huwa yanasema mtu akimtumikia Mungungu atamuheshimu ona Yohana 12:26 Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.wote wanaomtumikia Yesu, baba huwaheshimu sana Mungu hataacha heshima ya watumishi wake ivunjwe kwani kuvunjwa heshima ya watumishi wake ni kuvunjiwa hehsima yeye  ona Zaburi 105:14-15 Hakumwacha mtu awaonee, Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao. Akisema, Msiwaguse masihi wangu, Wala msiwadhuru nabii zangu.unapopambana na mtu wa Mungu na hasa aliyepakwa mafuta mwisho wa siku wewe ndiye utakayepondwa na kupigwa radi kisha Mungu ataitukuza pembe ya masihi wake 1Samuel 2:10 Washindanao na Bwana watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; Bwana ataihukumu miisho ya dunia; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake.

Muhimu.
Mungu anaupendo mwingi na mkubwa sana na wala hapigani pasipo sababu, awaye yote akipigana na Mungu atakufa haraka sana, Na ndio maana Mungu sio mwepesi wa hasira wala hahesabu maovu yaya anatoa mwaliko kwa kila mtu kumjia kwa dhati na kumtegemea na kumtumainia kwa moyo wa dhati na yeye atakuwa pamoja nasi wakati wote tutakapomuomba Mungu atatusikia kama tutakuwa pamoja naye na kuishi kwa mujibu wa kanuni zake, Yeye ni Mtu wa vita lakini hapendi vita lakini uko wakati Mungu hupigana au hupigania watu wake kwa sababu kadhaa wa kadhaa zaidi ya zile zilizotajwa hapo juu hivyo kaa katika kusudi la Mungu uweze kutetewa na Mungu!

Na Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Rev. Innocent Samuel Kamote

0718990796.

Alhamisi, 13 Agosti 2020

Imba wewe uliye tasa!

Isaya 54:1-4Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na utungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye aliyeolewa, asema Bwana. Panua mahali pa hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako; usiwakataze; ongeza urefu wa kamba zako; vikaze vigingi vya hema yako. Kwa maana utaenea upande wa kuume na upande wa kushoto; na wazao wako watawamiliki mataifa; wataifanya miji iliyokuwa ukiwa kukaliwa na watu. Usiogope; maana hutatahayarika; wala usifadhaike; maana hutaaibishwa; kwa kuwa utaisahau aibu ya ujana wako, pia mashutumu ya ujane wako hutayakumbuka tena”.


Utangulizi.

Katika changamoto mbaya sana duniani, tunazoweza kuorodhesha na zinazotesa sana watu utasa inaweza kuwa mojawapo, Utasa ni moja ya tatizo baya sana katika historia ya mwanadamu, utasa ni hali ya mwanamke au mwanaume kushiriki tendo la ndoa bila kinga yoyote kwa zaidi ya miezi kumi na mbili bila kupata matokeo!, Tatizo la utasa ni tatizo gumu sana na linaweza kusababishwa na kutokuwa sawa kwa homoni za mwanamke au mwanaume kunakopolekea kuleta shida katika mfumo wa uzazi. Tatizo kubwa linalozaliwa ni uwezo mdogo wa kubeba ujauzito na kunaweza kusiwepo ugonjwa mwingine. Kwa kuwa utasa sio ugonjwa lakini ni tatizo na lina uwezo wa kuathiri eneo kubwa sana la maisha ya mwanadamu, linasababisha kuweko kwa Mauvimbe ya ajabu kuzalishwa tumboni, fadhaa kubwa kwa mtu anayehitaji matokeo, matatizo ya kisaikolojia, wasiwasi, kupoteza matumaini, msongo wa mawazo, hatia, na kujihisi kama mtu usiyefaa kitu na hata kujisikia kufa, licha ya matatizo ya ndani anayoyapitia mtu aliye tasa pia kuna shutuma kutoka nje wanazopitia watu wasio na uwezo wa kuzaa

Wataalamu wa maswala ya uzazi wanaeleza kuwa katika utafiti walioufanya kwa wagonjwa 200 wanandoa wanaohudhuria clinic kwaajili ya kutaia uzao asilimia 50% ya wanawake na asilimia 15% ya wanaume walibainika kuwa na matatizo ya kiakili yaani kisaikolojia, aidha walipitia aina fulaninya mateso na manyanyaso na hayo yaliwapotezea furaha na kusababisha utasa, aidha katika utafiti mwingine wanawake 488 waliokuwa na tatizo la utasa walipoulizwa maswali walibainika kuwa na tatizo la msongo wa mawazo linalopelekea wao kuwa tasa.

Kwa ufupi utasa ni tatizo baya sana  ambalo wakati mwingine matabibu hawana uwezo nalo, na wakati mwingine ni Mpaka Mungu mwenyewe aingilie kati, Katika jamii ya Israel Mtu alipokuwa tasa alinyanyaswa sana na alijiona duni na mtu asiyefaa katika Israel utasa lilikuwa ni kama jambo la aibu kubwa na fedhea na watu waliokuwa tasa walinyanyapaliwa hata na wanawake wenzao kwa hiyo maumivu ya wanawake tasa katika jamii yalikuwa makubwa na yenye uchungu mno

a.       Sara alinyanyaswa na kijakazi wake ambaye alishika mimba ilihali bibi yake akiwa hana kitu mara baada ya hajiri kupokea ujauzito alimdharau sana Sara na kumdhihaki huku akijiona yeye kuwa ni bora zaidi ona Mwanzo 16:1-5Basi Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana, naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri. Sarai akamwambia Abramu, Basi sasa, BWANA amenifunga tumbo nisizae, umwingilie mjakazi wangu labda nitapata uzao kwa yeye. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai. Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri Mmisri mjakazi wake, baada ya kukaa Abramu katika nchi ya Kanaani miaka kumi, akampa Abramu mumewe, awe mkewe. Basi akamwingilia Hajiri, naye akapata mimba. Naye alipoona ya kwamba amepata mimba, bibi yake alikuwa duni machoni pake. Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. BWANA na ahukumu kati ya mimi na wewe.”

b.      Rebbeca alikuwa ni mwanamke mwingine anayetajwa katika Biblia kuwa alikuwa tasa mwanamke huyu kutokana na manyanyaso katika jamii alimsumbua mumewe akimwambia nipe watoto, alilewa Isaka akiwa na miaka 40 na alipata mtoto akiwa na mika 60 ona Mwanzo 25:20-26Isaka akawa mwenye miaka arobaini alipomtwaa Rebeka binti Bethueli, Mshami, wa Padan-aramu, ndugu wa Labani, Mshami, kuwa mke wake. Isaka akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye BWANA akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba.Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza BWANA. BWANA akamwambia, Mataifa mawili yamo tumboni mwako, Na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako. Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili, Na mkubwa atamtumikia mdogo. Siku zake za kuzaa zilipotimia, tazama! Mapacha walikuwamo tumboni mwake. Wa kwanza akatoka, naye alikuwa mwekundu mwili wote kama vazi la nywele. Wakamwita jina lake Esau. Baadaye ndugu yake akatoka, na mkono wake unamshika Esau kisigino. Akaitwa jina lake Yakobo. Isaka alikuwa mwenye miaka sitini mkewe alipowazaa.”

c.       Hanna aliteseka na hali ya utasa inaonekana mumewe pamoja na upendo mkubwa sana alishauriwa aoe mke mwingine na kama haitoshi mwanamke huyo alizaam, Hana hakuwa na mtoto hivyo alichokozwa na kutendewa vibaya na mke mwenza hali hii ilisababisha maumivu makubwa sana        kiasi cha kumfanya mwanamke huyu kushinda hekaluni akilia na kumuomba Mungu ona 1Samuel 1:1-10Palikuwa na mtu mmoja wa Rama, Msufi, wa nchi ya milima milima ya Efraimu, jina lake akiitwa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu, mwana wa Sufu, Mwefraimu naye alikuwa na wake wawili; jina lake mmoja akiitwa Hana, na jina lake wa pili aliitwa Penina; naye huyo Penina alikuwa na watoto, lakini Hana hakuwa na watoto. Na mtu huyo alikuwa akikwea kutoka mjini kwake mwaka kwa mwaka, ili kuabudu, na kumtolea Bwana wa majeshi dhabihu katika Shilo. Na wale wana wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, makuhani wa Bwana, walikuwako huko. Hata siku ile ilipofika Elkana alipotoa dhabihu, kumpa mkewe Penina sehemu, akawapa na watoto wake wote, waume kwa wake, sehemu zao; lakini Hana humpa sehemu mara mbili; maana alimpenda Hana, ingawa Bwana alikuwa amemfunga tumbo. Ila mwenzake humchokoza sana, hata kumsikitisha, kwa sababu Bwana alikuwa amemfunga tumbo. Tena mumewe akafanya hivyo mwaka kwa mwaka, hapo yule mwanamke alipokwea kwenda nyumbani kwa Bwana, ndivyo yule alivyomchokoza; basi, kwa hiyo, yeye akalia, asile chakula. Elkana mumewe akamwambia, Hana, unalilia nini? Kwani huli chakula? Kwa nini moyo wako una huzuni? Je! Mimi si bora kwako kuliko watoto kumi? Ndipo Hana akainuka, walipokwisha kula na kunywa huko Shilo. Naye Eli, kuhani, alikuwa akiketi kitini pake penye mwimo wa hekalu la Bwana.Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba Bwana akalia sana.”

Unaona wanawake hao na wengine wengi wanatajwa katika maandiko kuwa walipitia changamoto ngumu sana ya utasa, utasa ni tatizo bay asana kila mwanadamu na mwanamke mwenye akili timamu anatamani kuzaa, tena anatamani kuzaa kwa kiwango cha kutosha uzao ni Baraka kubwa nay a kwanza ya mwanadamu Mwanzo 1:28 “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.” ili mwanadamu aendelee kuwepo juu ya uso wan chi anapaswa kuwa na uzao, uzao ndio unaoendeleza ukoo, mali na shughuli zote ntunazozifanya zitakosa warithi kama hatuna uzao, Mungu akikupa uzao amekupa urithi juu ya nchi  amekupa silaha tena hasa watotowanaozaliwa ujanani Zaburi 127:3-4” Tazama, wana ndio urithi wa Bwana, Uzao wa tumbo ni thawabu. Kama mishale mkononi mwa shujaa, Ndivyo walivyo wana wa ujanani.” Kukosa watoto ilihesabika kama adhabu kubwa sana duniani ilikuwa kama laana, utasa ni kitu kibaya sana aidha pia kuharibika kwa mimba ni tukio bay asana Mungu aliwaahidi watu wake kama watamtumikia ataondoa kabisa utasa kabisa na kuwa hatakuwako aliye tasa wala mwenye kuharibu mimba ona Kutoka 23:25-26 “Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako.   Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza.

Katika mstari wa msingi Mungu analiona taifa la Israel na mataifa mengine na kumtumia Isaya nabii kuwaletea habari njema Israel walikwenda utumwani, katika hali ngumu sana wakidharauliwa na watu kama ilivyo kwa mwanamke aliye tasa, Na mataifa mengine wakiwa kama mwanamke asiyeolewa kila mmoja kwa jinsi yake anapitia hali Fulani katika maisha ambayo haizai, inaweza kuwa taifa, inaweza kuwa mtu, unapokuwa na hali ya umasikini, kile unachotaka kukitimiza au kukifanya hakifanikiwi, uko katika hali ya kushindwa kuzalisha au mipango isiyofanikiwa ni kama unataka mpenyo na hupati mpenyo unaokusudiwa hiyo ni hali ya utasa, huna furaha huna amani ni hali ya utasa, huna unalilifanya likafanikiwa ni hali ya utasa Nabii Isaya anawataka wote wanaopitia hali kama hiyo waimbe kwa maana Mungu anaahidi kuuondoa utasa, utasa ni tatizo ambalo linaweza kukabiliwa na Mungu pekee, yeye ndiye anayeweza khbadili hali ya mambo katika maisha yako, huduma yako, ukoo wako kijiji chako, taifa lako, familia yako, kushindwa kuzalisha kumekuletea fadhaa kubwa Isaya anasimama leo kutoa habari njema anasema imba wewe uliye tasa kwa maana watoto wako ni wengi mno watoto wako wanakuja , hakuna sababu ya kufadhaika yeye aliyebadili maisha ya Sara, akabadili maisha ya Rebbeka, akabadili maisha ya Hanna akabadili masiha ya Manoa akabadili maisha ya Elizabeth ana uwezo wa kubadili maisha yako leo na kuyafuta machozi yako na kukufanya uwe productive uwe mwenye faida mahali ambako umeonekana huna faida yoyote Mungu anajua fadhaa zako anajua uchungu wako anajua unayoyapitia na yuko tayari kutoa msaada unaolinga na na mahitaji yako! Kwa kawaida mambo yanapokuwa magumu mwanadamu hulia na hawezi kuimba lakini Isaya anatangaza mtu aimbe mtu achangamke kwa kuwa bwana anaahidi kubadilisha mambo katika maisha yako! Ni maombi yangu kuwa unapomaliza kusoma ujumbe huuu Mungu abadilishe mtazamo wako na kukupa uzao, uwe ni uzao wa tumbo lako, huduma yako, kanisa lako, biashara yako, kazini kwako shambani kwako na amani yako Mungu na akufanie muujiza akupobnye na kuondoa fedhea katika kila eneo la maisha yako akupe nguvu kwa upya ili uwe na uzalishaji katika maisha yako amen!

Na Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima

Jumanne, 4 Agosti 2020

Haki yenu isipozidi hiyo haki ya Waandishi na Mafarisayo



Mathayo 5:20 “*Maana nawaambia haki yenu isipozidi Hiyo haki ya waandishi na mafarisayo hamtaingia kamwe katika ufalme wa Mbinguni*



Utangulizi:

Waandishi na Mafarisayo ni akina nani ?

Ni muhimu kufahamu kuwa  nyakati za ulimwengu wa agano jipya yaani wakati wa Yesu Kristo katika Dini ya kiyahudi kulikuwa na Makundi (Madhehebu) mbalimbali ya watu mbalimbali wenye misimamo kadhaa ya kidini lakini makundi makubwa yaliyojulikana zaidi walikuwa Mafarisayo na Masadukayo, lakini kulikuwa na kundi lingine maarufu lililojulikana kama waandishi au wanasheria, na mengineyo yenye misimamo ya kisiasa na kidini lakini hapa nitawazungumzia Waandishi na mafarisayo tu kwa sababu ndio ambao wametajwa katika mstari wa Msingi kwamba “Haki yetu (Wakristo au wanafunzi wa Yesu) isipozidi hiyo haki ya Waandishi na mafarisayo Hatutaingia kamwe katika ufalme wa Mungu” kwanza tuwajue hao ni kina nani:-

Waandishi

Waandishi ni kundi la jamii katika dini ya kiyahudi waliokuwepo wakati wa Agano jipya ambao walikuwa ni walimu na watafasiri wa Sheria ya Musa Yesu alilitaja kundi hili kwa sababu walikuwa wasomi na watu waliobobea katika ujuzi wa torati, kazi yao kubwa pia ilikuwa kunakili sheria kutoka katika magombo ya chuo yanayochakaa au ya zamani na kuyanakili katika magombo mapya aidha watu hawa pia walijikita katika kusoma na kuielewa sheria ili kuwafundisha au kuwafafanulia watu.

                      Walijulikana pia kama wanasheria
                      Ni kundi la uamsho wa kimaandiko lililoanza wakati wa Ezra mwandishi baada ya watu kurejea kutoka uhamishoni Babeli
                      Waliitwa “SOFERIM” Kwa Kiebrania, maana yake watu wanaojua maandiko lakini pia waliitwa wenye hekima.

Ezara 7:10 “Kwa maana huyo Ezra alikuwa ameuelekeza moyo wake kuitafuta sheria ya Bwana, na kuitenda, na kufundisha maagizo na hukumu katika Israeli”.

Mafarisayo.

Kundi lingine la kidini katika dini ya kiyahudi waliokuwepo pia wakati wa agano jipya na wakati wa Yesu walijulikana kama Mafarisayo hawa walikuwa watu walijitahidi sana kuishi kwa haki na kuitii sheria ya Mungu kivitendo na kwa kujiamini na kujivunia Yesu alilitaja kundi hili kwa sababu lilikuwa na bidii katika utii wa torati lakini sio kwa moyo mweupe na hata wale waliokuwa na moyo mweupe waliishika sheria katika misingi ya kujipatia haki nje ya neema ya Mungu  Matendo 26:4-5Kwa maana Wayahudi wote wanajua maisha yangu tangu ujana, yaliyokuwa tangu mwanzo katika taifa langu huko Yerusalemu, wakinijua sana tangu mwanzo, kama wakipenda kushuhudia, ya kwamba nalikuwa Farisayo kwa kuifuata madhehebu ya dini yetu iliyo sahihi kabisa
               
                      Pamoja na Torati ya Musa pia waliamini maandiko mengine ya manabii na masimulizi ya kale ya kiyahudi kuwa ni neno kamili la Mungu
                      Walikazia sana maswala ya uadilifu kuliko Theolojia
                      Waliamini kuwa kuna maisha baada ya kufa, na pia wafu watafufuliwa
                      Wakliamini uwepo wa malaika, maono, na kuwepo kwa pepo wabaya

Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na mafarisayo!

Moja ya maandiko ambayo hutumiwa vibaya na wahubiri wengi wa injili ni na walimu wa Biblia  ni pamoja na andiko hili  *Mathayo 5;20* Maana nawaambia haki yenu isipozidi Hiyo haki ya waandishi na mafarisayo hamtaingia kamwe katika ufalme wa Mbinguni*” kimsingi kutokana na maandiko haya wakristo waliookoka na hata wale wasiookoka wametengenezewa makongwa mengi  na mazito sana  siku zote watafasiri wa neon la Mungu au maandiko wakikosea hata kidogo tu katika kuitafasiri maandiko wanaweza kusababisha tatizo kubwa sana sawa na Daktari kuzidisha dozi au kutoa dozi iliyo chini ya kiwango na ndivyo ilivyotokea kwa miaka mingi katika tafasiri ya mstari huu hebu sasa tuuangalie tena mstari huu kwa kina kwa kawaida mstari huo unasomeka hivi “*Maana nawaambia haki yenu isipozidi Hiyo haki ya waandishi na mafarisayo hamtaingia kamwe katika ufalme wa Mbinguni*” ndugu msomaji wakristo wengi  narudia tena wamefanywa kuwa watumwa na kubeba mizigo isiyowahusu kupitia andiko hili jinsi andiko hili lilivyo na kile kinachotafasiriwa au kukaziwa na wahubiri  na badhi ya walimu wa maandiko ni tofauti sana na hata na jinsi Kristo alivyokusudia  andiko hili kutumika.

Kwa ujumla kile ambacho wahubiri  na waalimu wengi wa neon la Mungu wengi wanakimaanisha katika maandiko haya ni kama maandiko haya yanasomeka hivi “*Maana nawaambia Matendo yenu yasipozidi Hayo Matendo ya waandishi na mafarisayo hamtaingia kamwe katika ufalme wa Mbinguni*” nimewahi kuwasikia wahubiri wakikazia wakristo kuwa na matendo yanayowazidi mafarisayo na waandishi yaani waalimu wa sheria tunapounganisha na swala zima la wokovu mafundisho ya aina hiyo sio injili sahihi tuliyoipokea toka kwa Bwana,

Wakati Fulani kwa sababu ya mafundisho ya aina hiyo nilikuwa nimejipangia kuwa ni lazima niamke kuomba Alfajiri kama vile waislam wafanyavyo na kwakuwa niliamini kuwa wao hawana Mungu wa kweli na aliye hai  kama niliye naye, Na kutokana na msisitizo wa mahubiri ya wachungaji wengi nilijifunza kuwa ninalazimika kuamka kabla ya Waislamu  hawajaamka na kumuomba Mungu ili matendo yangu yazidi hayo matendo ya mafarisayao na kwakuwa maisha yangu ya mwanzo kabla ya kumjua Mungu nilikuwa nikilala na kuamka kwa saa nilizotaka uamkaji wa Alfajiri lilikuwa jambo jipya katika maisha yangu na halikuwa jambo jepesi kusema ukweli. niliambiwa kuwa huko Korea ya kusini wakristo huamka alifajiri na kumuomba Mungu na wamepata mafaniko makubwa sana lakini sisi Afrika Mashariki wamishionari wetu  waliokuja mapema na kuleta Ukristo hawakuwa wametufunza kuamka alfajiri kwa  Msingi huo mwanzoni nilichapa usingizi lakini nilipomjua Mungu na kujifunza kuhusu kuamka alifajiri niligundua kuwa ninapaswa kuwawahi waislamu na siku kama ikitokea nimechelewa kuamka na wakanitangulia nilijihisi vibaya na kuonakama  kuwa siku hiyo ni chungu na sio siku nzuri  na labda imeharibika na nilihisi au niliiishi kwa maumivu ambayo sikuwa nayo kabla ya kuokoka kwa nini nilijifunza kuwa matendo yangu lazima yazidi yale ya Mafarisayo.

Kumbe nilikuja kugundua siri kutoka kwa Roho wa Mungu kuwa Mungu hakumaanisha kile nilichokifanya kimsingi Yesu alikuwa akizungumzia “*HAKI*” na sio “*MATENDO*” nililazimika kujifunza kuhusu haki kama mstari halisi unavyosema na niligundua kuwa kwanza hakuna mwanadamu mwenye haki hata mmoja *Warumi 3:10-12, Biblia inasema hivi “Kama ilivoandikwa ya kwamba hakuna mwenye haki hata mmoja hakuna afahamuye, Hakuna amtafutaye Mungu Wote wamepotoka wameoza wote pia hakuna mtenda mema la! Hata mmoja”* nilijiuliza kama hakuna mwenye haki hata mmoja inakuwaje Yesu aseme haki yetu isipozidi haki ya mafarisayo hatutauona ufalme wa Mbinguni?

Nikagundua kuwa kumbe Mafarisayo hawakuwa na haki hawakuwa na haki ya kweli haki waliyokuwa nayo ilikuwa haki ya nje tu, Yesu aliwataja waandishi kwa sababu walikuwa wasomi waliobobea katika maandiko na aliwataja mafarisayo kwa kuwa walikuwa na juhudi ya kutafuta haki kwa nguvu zao, Makundi haya yalikuwa na haki ya nje ya kidini tu na haikuwa haki yenye faida yoyote kwa ufalme wa Mungu haki yao iliwekwa katika misingi ya matendo ya nje yasiyotoka moyoni na yenye kubeba utukufu wa kibinadamu tu na zaidi sana waliwadharau watu wengine wakifikiri kuwa watu hao ni wenye dhambi na wasiofaa au ambao hawawezi kukubaliwa na Mungu kwa sababu ya kujifikiri kuwa waio ni bora zaidi  ona kwa mfano Luka 18:10-14  Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote. Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru. Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang'anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote. Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi. Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.” Unaweza kuona kwa hiyo kwa mtazamo wa nje na wa kibinadamu waandishi na Mafarisayo waliokuwa wenye haki iliyochanganyika na kiburi, wakijidhani kuwa wao ni watakatifu na wenye kibali kwa Mungu kuliko wengine walikuwa hawana ujuzi kuwa Mungu ndiye mwenye kutuhesabia haki na kuwa ni Mungu ndiye anayeujua moyo wa Binadamu.      

 “*Mathayo 23;25-28* “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia. Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang'anyi na kutokuwa na kiasi. Ewe Farisayo kipofu, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa safi. Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote.Vivyo hivyo ninyi nanyi, kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki, bali ndani mmejaa unafiki na maasi”.

Yesu anawaonya mafarisayo “*Ole wenu waandishi na Mafarisao wanafiki …..*” kumbe mafarisayo walikuwa wanafiki hawakuwa na haki ya kweli, Haki yao ilikuwa haki ya nje walifanya mambo ili waonekane na watu *Mathayo 23;5a* “*Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu*;” kumbe mafarisayo haki yao ilikuwa ni haki ya nje haki ya kujionyesha tu walionekana na watu kuwa ni wenye haki lakini kwa kweli hawakuwa na haki ya kweli na ndio maana na sio hivyo tu walikuwa na dhambi ya dharau au walikuwa na kiburi wakijifikiri kuwa waoa ni watakatifu au wana kibali kwa Mungu kuliko watu wengine waliowadhani kwa akili zao na mawazo yao kuwa ni wenye dhambi ona maneno haya Luka 18:9 “Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote.   Ni kwaajili ya haya utaweza kuona kuwa Yesu alisisitiza kuwa ni lazima iwepo haki mbadala, haki ambayo ni tofauti na haki na ile ya  waandishi na mafarisayo  ambayo kimsingi ni haki ya nje.  Sasa ili mtu aweze kuingia katika ufalme wa mbinguni hawezi kuingia kwa haki kama ile ya waandihi na mafarisayo ambayo ilikuwa ya nje ni kweli walionekana wanashika sheria walionekana wanaomba, walisifu na kufunga walisoma neno la Mungu  na hata kuhudhuria ibada  hata hivyo walifanya hayo ili waonekane na watu wasifiwe waonekane kuwa wao ni wa kiroho na washika dini wakubwa huu haukuwa mtazamo sahii, haki mbadala ni haki ambayo haitokani na matendo ya sheria  ni haki kutoka moyoni ni haki itokanayo na imani  ni neema ya kukubali kazi aliyoifanya Yesu Kristo kwaajili yetu Msalabani ni haki itokanayo na Kristo *Warumi 3;21-26*Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa na torati na manabii; ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti;  kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake,ili aonyeshe haki yake ,kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa MUNGU dhambi zote zilzotangulia kufanywa.apate kuonyesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabu haki yeye amwaminiye Yesu.*

Angalia pia Waefeso 2;1-9 *Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine. Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu; ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu. Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu

hii ndio haki mbadala aliyoizungumzia Bwana Yesu kwa hiyo Kristo hajatuita katika mashindano ya kuwazidi wale tunaowaita mafarisayo kwa matendo kama ukifanya hivyo wakikushinda unakuwa chini ya kongwa ambalo hata kabla ya kuokoka hukuwa nalo, Mtu anapomuamini Yesu mara moja Yesu anafanyika kuwa haki yetu ipatikanayo kwa neema na  wala sio kwa matendo  neema ya Kristo ndani yetu inatugeuza na kutufanya kuwa wema yenyewe na hivyo kutupelekea katika Tito 2:11-12 “Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na HAKI, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;  Kwa hiyo Yesu hakumaanisha kuwa matendo mema ni mabaya la hasha matendo mema yanakubalika kwake ykihusisha imani na rehema kutoka kwake Yesu yeye ndiye anakuwa haki yetu ambayo ni zawadi kutoka kwake ni neema kutoka kwake  Biblia inasema hivi

1Wakoritho 1:30 -31 “Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na HAKI, na utakatifu, na ukombozi; kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana.

2Wakoritho 5:21 “Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa HAKI ya Mungu katika Yeye.”

Kumbe unaweza kuona haki halisi haitokani na nafsi zetu haki halisi ni ile tunayopewa kwa imani kwa kumuamini Yesu na kukubali kazi yake aliyoifanya pale msalabani, ni aina hii ya haki ndiyo ambayo Yesu alikuwa anaizungumzia na manabii walitabiri kwa kumuamini Mungu yeye sasa anafanyika kuwa haki yetu

Yeremia 23:5-6 “Tazama siku zinakuja, asema Bwana, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atamiliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi. Katika siku zake Yuda ataokolewa, Na Israeli atakaa salama, Na jina lake atakaloitwa Ni hili, Bwana ni haki yetu.”   

Kujaribu kwa njia za kibinadamu kuishi maisha ya kujitafutia haki bila imani kwa Yesu Kristo kutatufabya tuishi katika Kongwa kubwa sana la matendo yatakayotufanya tuuone wokovu kuwa ni kitu kigumu sana na kumbe wokovu ni mwepesi na raha nafsini mwetu

Ukiyajua hayo heri wewe ukiyatenda

Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima!

Jumatatu, 27 Julai 2020

“Na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala”


Mwanzo 3:16Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.



Utangulizi:


September 4-15 Mwaka 1995 Kulifanyika mkutano mkubwa wa nne wa dunia wa wanawake huko Beijing nchini China.  Mkutano huo ulipewa jina la kiingereza “Action for Equality: development and peace”, yaani kwa tafasiri ya Kiswahili changu naweza kusema “Haki sawa kwa maendeleo na amani” Kongamano hili la wanawake lilipewa jina hilo na umoja wa mataifa, Katika mkutano huu mkubwa, serikali za dunia zilikusanyika zikiwakilishwa na wanawake maarufu kutoka sehemu mbalimbali duniani zikiwa na wito wa kuitaka dunia kufikia malengo ya usawa yaliyokubaliwa na jukwaa hilo la wanawake lililofanyika Beijing likijulikana kama “The Beijing Platform for Action”, Kutoka Tanzania mwakilishi mmojawapo maarufu alikuwa mama Gertrude Mongella (Kushoto pichani hapo juu) ambaye wakati huo pia alikuwa ni spika wa bunge la Africa kwa upande wa wanawake, pamoja na maswala mengine  swala kubwa lilosisitizwa ni usawa katika uwakilishi lakini kubwa zaidi ni haki za wanawake duniani. Mkutano huo wa Beijing ulihitimishwa kwa kutoa tamko la Beijing yaani “Beijing Declaration.” Na lilikuwa ni tamko lenye maazimio yapatayo 38 na mengi yakiwa na mkazo kuhusu haki za wanawake.


Je unapata picha gani unaposoma habari za mikutano mikubwa kama hii na maazimio makubwa ya wanawake? Hasa yanayodai haki na haki hii ni usawa baina yao na wanaume, ni ukweli ulio wazi na usiopingika kuwa katika jamii mwanamke amebaki nyuma kwa kiwango kikubwa na sehemu kubwa sana uwezo wao haufanani na ule wa wanaume, tangu katika malezi na hata ukuaji kumekuwa na kipaumbele zaidi kwa watoto wa kiume penginepo kuliko watoto wa kike, maumbile na maswala mengine ya kijamii mila na tamaduni zimemuacha mwanamke nyuma kwa kiwango kikubwa na kwa sababu hiyo kuna uwezekano mkubwa kuwa labda umoja wa mataifa umeliona hilo na hivyo ukaandaa makongamano kadhaa yenye maazimio ya kumuinua mwanamke,  hatuna shaka kabisa kuwa uko ukweli ulio wazi kuwa mwanamke akiendelea jamii inaeweza kuendelea na kupiga hatua kwa kiwango kikubwa, Mwanafalsafa mmoja maarufu wa Afrika nchini Ghana James Aggrey alisema ulimuelimisha mwanamke umeielimisha jamii, kwa hiyo wanawake wakiendelezwa na kupewa fursa sina shaka kabisa watakuwa msaada mkubwa kwa jamii duniani.


Hata hivyo ni muhimu kufahamu na kujiuliza kuwa kwa nini wanawake wamejikuta katika changamoto hizi na swala kubwa zaidi kwanini wanapigania haki na usawa linapokuja swala la ulinganifu na wanaume? Fahamu ya kuwa wanawake wanajaribu au wanataka kujikomboa, wanataka kujikomboa kutoka katika kile ambacho maandiko yametamka kuwahusu, Liko tatizo ambalo wala sio la mfumo dume, wala sio la mila na desturi wala sio la kitamaduni ni tatizo la kiroho ni tatizo ambalo msingi wake na chanzo chake kilisababishwa na wanawake wenyewe, na hii ni kwa mujibu wa maandiko matakatifu, wakati mwingine wanawake wanapokuwa katika harakati zao huwa wanatamka kirahisi tu kuwa hata tamaduni mila na kidini ziliwakandamiza! Lakini leo nataka itambulike wazi kiini cha tatizo ili kwamba mwanamke aweze kuwa na ukombozi sahihi anapaswa kujua haki zake za msingi kama zilivyotamkwa na Maandiko matakatifu au na Mungu mwenyewe ili ajue mipaka yake ya haki na ukombozi anaoupigania wakielewa hayo watakuwa na amani ya kweli na watapata uhuru wa kweli.


Chanzo cha tatizo.


Neno la Mungu linaonyesha wazi kabisa kuwa mwanamke na mwanaume waliumbwa wote wakiwa na haki sawa, wote wakiwa wakamilifu na wote wakiwa wamepokea tamko la Baraka za Mungu katika kuutawala ulimwengu ona Mwanzo 1:26-31 “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu; na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo. Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.” 


Unaona maandiko yako wazi kabisa kuwa Mungu amewapa wanadamu namaanisha wanawake na wanaume kwa pamoja thamani kubwa sana wote walitamkiwa baraka ya kuongezeka na kuijaza nchi na kuitiisha na kuitawala wote walipewa mtaji sawa utawala sawa na uhuru sawa kwa msingi huo mwanamke na mwanaume walikuwa ni watawala wenza wenye usawa unaofanana, lakini wote pia walikuwa na jukumu la kumuabudu Mungu na kumtii kwa usawa na kwa pamoja, Hata hivyo Mwanamke alipaswa sio kumsikiliza Mungu tu, lakini alipaswa kumsikiliza na Mumewe sawasawa na kumsikiliza Mungu, agizo la kutokula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya kimsingi lilitolewa kwa Adamu pekee na huenda labda mwanamke alisikia agizo hilo baadaye kutoka kwa mwanaume angalia 


Mwanzo 2:15-17 “BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza. BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika”. 


Unaposoma maandiko haya ya uchanganuzi wa uumbaji utaweza kuona kuwa agizo hili lilitolewa kwa Adamu na kisha baadaye Eva aliumbwa kwa hiyo ni wazi katazo la ule mti wa ujuzi wa mema na mabaya Eva alilisikia kutoka kwa mumewe, lakini haki ya utawala iliwahusu wote, hii maana yake kwa kuwa mwanaume aliumbwa kwanza kisha mwanamke baadaye na kwa kuwa mwanaume alipaswa kumfundisha mwanamke amri  na maagizo ya Mungu, ni wazi na haki utakubaliana nami kuwa Mwanaume, alikuwa na majukumu yenye ngazi ya juu zaidi ya mwanamke kutokana na kuwa aliumbwa kwanza, Lakini vilevile alikuwa mwalimu na amri ile alipewa yeye hivyo alikuwa ni msimamizi wa kazi ya uumbaji na maelekezo aliyopewa na Muumba. Ni wazi basi kuwa swala la Kufundisha na kutawala lilikuwa jukumu kuu la Mwanaume na swala la kusikiliza lilikuwa la mwanamke yaani Mungu angetoa maelekezo kwa Adamu na Adamu angeleta ufafanuzi na maelekzo kwa mwanamke naye pamoja na jamii wangetekeleza kile Mungu alichokusudia kwa hivyo kwa itifaki, Mungu ni kichwa cha kila mwanaume na mwanaume ni kichwa cha mwanamke hapo ndipo itifaki ya uumbaji na upokelewaji wa maagizo ya Mungu ungepaswa kwenda kwa namna hiyo ona 

1Wakoritho 11:3 “Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.Unaweza kuona kwa msingi huo ili Baraka za Mungu ziweze kutiririka lazima itifaki ya kiungu izingatiwe, hili lisipoeleweka vema na wala kuzingatiwa mambo mabaya sana yatatokea na uwepo wa Mungu utaondoka, Mungu ni Mungu wa utaratibu wala sio Mungu wa machafuko!


Sasa basi jambo mojawapo kubwa na la kusikitisha ni kuwa mwanamke alikuwa ni kiumbe mwenye udadisi mkubwa na akili za kuhoji na kutafiti kile kilichosemwa na Mungu na mumewe Adamu na kutokana na udadisi wake mwanamke akawa mwanadamu au kiumbe wa kwanza kuharibu utaratibu huo uliokusudiwa na Mungu ona sasa Mwanzo 3:1-6 “Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.” Hiki ndio chanzo cha tatizo, Mwanamke amekuwa mwanadamu wa kwanza kusababisha dhambi na mauti kuingia ulimwenguni, ndio kiumbe wa kwanza kuharibu utaratibu, ndie kumbe wa kwanza kutokutaka kumsikiliza Mungu wala mumewe na alichagua kumsikiliza ibilisi na kusababisha kuharibika kwa utaratibu na mpango kamili wa Mungu katika maisha ya wanadamu, Paulo mtume akimuasa Timotheo katika waraka wake anamtaka Timotheo kukumbuka habari hizi na kuwaonya wanawake wawe katika utulivu, akimkumbusha kile kilichotokea bustanini na namna ya kuhakikisha kuwa utaratibu unafuatwa kanisani ona 1Timotheo 2:12-14Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu. Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.”


Ni muhimu kufahamu kuwa katika kifungu hiki Paulo mtume hakumaanisha kuwa wanawake hawawezi kusimama na kufundisha katika kanisa, Nyakati za kanisa la kwanza wanawake walifanya kazi ya kuhubiri injili na kufundisha neno la Mungu na mfano mzuri ni Prisilla na mumewe Akila wanaotajwa katika Matendo ya Mitume 18:24-26 “Basi Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzalia wa Iskanderia, mtu wa elimu, akafika Efeso; naye alikuwa hodari katika maandiko. Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohana tu. Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Prisila na Akila walipomsikia wakamchukua kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi.”  Lakini vilevile tunasoma habari za Fibi aliyekuwa na huduma katika kanisa huko Kenrea ona  katika Warumi 16:1 “Namkabidhi kwenu Fibi, ndugu yetu, aliye mhudumu wa kanisa lililoko Kenkrea;” Huenda muhudumu huyu alikuwa mwanamke na alifundisha katika kanisa lakini kimsingi lugha inayotumika katika 1Timotheo 2:12-14  kwamba simpi mwanamke nafasi ya kufundisha sio inayotokana na neno la Kiyunani “DIDASKEIN” (Didasko) Ambalo maana yake ni kufundisha yaani kutoa maarifa  na ujuzi na kuupeleka kwa wengine, Neno linalotumika pale simpi mwanamke nafasi ya kufundisha ni neno la Kiyunani “AUTHENTEIN” (Authenteo) ambalo kwa kiingereza lingeweza kusomeka kama “exercise authority” au “Dominate” yaani to have control over a place or person yaani wanawake wasishikishe adabu wanaume au wasitiishe wanaume, wasiwaamuru kama wenye mamlaka hii ndio lugha halisi ya kibiblia hapa wasiwatawale wasiwe na amri juu yao.


Hivyo basi tunapata picha kuwa ni Eva aliyekuwa wakwanza kutamani na kujaribu kula matunda ya mti ule wa ujuzi wa mema na mabaya ambao Mungu alikuwa amekataza, na ni yeye aliyeweza kutumia ushawishi wake na mamlaka yake kuamuru na kumkosesha na Mumewe Adamu naye akala ni sawa na kusema wazi kuwa dhambi iliingia ulimwenguni kupitia amri ya mwanamke na matokeo yake na athari zake zikawa nyingi ikiwemo kuvurugika kwa mpango kamili wa Mungu kwa mwanaume na mwanamke kama watawala wenza. Kwa hiyo dhambi ya mwanamke ilikuwa ni kujiamulia, kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya na kumuamuru mumewe naye ale. Na hivyo kuingiza mauti ulimwenguni. 


Na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala


Mungu ni Mtakatifu na ni lazima aihukumu dhambi, imefanyika kwa kusudi au kwa bahati mbaya lazima ataishughulikia tu, Mungu aliwahukumu wote na kuwaadhibu wote kutokana na kosa walilolifanya lakini kila mmoja kwa namna yake, Adamu alimlaumu Eva kwa kosa lake, na Eva alimlaumu nyoka kwa kosa lake na wote akiwemo nyoka waliadhibiwa na Mungu kutokana na makosa yao, sisi nasi kila mmoja ataadhibiwa mbele za Mungu kutokana na makosa yake, bila kujali ni mazingira gani yamepelekea tukafanya dhambi lakini ni lazima tukae na kukumbuka kuwa mshahara wa dhambi ni mauti na kila dhambi ni lazima iadhibiwe na kuhukumiwa na Mungu mwenyewe mwenye haki!


1.       Kwa Nyoka.


Kwa kuwa Nyoka ndiye aliyetumiwa na Ibilisi moja kwa moja Mungu alimlaani, ni jambo gumu sana Mungu kutoa laana kwa kiumbe chake chochote, Lakini shetani alikuwa ana ujuzi kuwa wao ni malaika na malaika kama viumbe vya kiroho hawafi, na hivyo alistahili laana, kwani kupitia ushawishi wake amesababisha mwanadamu kuwa na mauti katika mwili wake hivyo shetani kama mwanzilishi wa dhambi alilaaniwa, Aidha nyoka ambaye alikuwa kiumbe wa kawaida aliyetumiwa na Shetani kuzungmza na mwanamke yeye alilaaniwa kutembea kwa tumbo na kula mavumbi lakini pia kuwa adui wa mwanadamu, Nyoka alitumiwa na shetani kuwashawishi wazazi wetu wa kwanza kufanya dhambi, kwa kusudi na kwa nia ovu kabisa na hivyo alilaaniwa bila mjadala na kupokea adhabu yake, adhabu ya nje ilimuhusu nyoka halisi na adhabu ya ndani kiroho ilimuhusu shetani na majeshi yake. Ona

Mwanzo 3:14BWANA Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako; nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.


2.        Kwa Mwanamke.


Eva alikuwa ni kiumbe wa pili kutamkiwa adhabu japo wanadamu hawakulaaniwa, Eva alipokea kifurushi cha adhabu chenye mafungu matatu, Ikiwa ni pamoja na kuzaa kwa uchungu, Tamaa yake kuwa kwa mumewe, na mumewe kumtawala, huu haukuwa mpango wa Mungu katika mahusiano, lakini ni mpango uliotokana na kuharibika kwa mwanadamu kutokana na kuingia kwa dhambi ulimwenguni, wanawake wote waliowahi kuzaa wanaujua au wameuonja uchungu huo, na uchungu huu unaendelea katika uhalisia wa maisha ya wanadamu wote


Mwanzo 3:16. “Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.


Hata hivyo swala la tamaa yako itakuwa kwa mumeo naye atakutawala ndio mahali panapochanganya watu kwa miaka mingi na wasiweze kuelewa maana ya msemo huu, ili kuweza kuelewa jambo hili hatuna budi kuliangalia kwa jicho linguine Biblia ya kiingereza ya The New Living Translation ndio imetafasiri kwa namna iliyonyooka zaidi kwani inasomeka hivi “you will desire to control your husband, but he will rule over you” yaani kwa Kiswahili chake tungeweza kusema namna hii “Utatamani kumtawala mwanaume lakini yeye atakutawala wewe” unaweza kuona kumbuka kuwa Mungu alikuwa anatamka adhabu kutokana na anguko la mwanadamu kwa kila mmoja kulingana na kukosea kwake, kwa hiyo mwanamke hapa kutokana na kuwa wa kwanza kwa hiyo kwa neno hili dhambi inaathiri uhusiano wa mwanamke na mwanaume katika ndoa na laana moja wapo au adhabu mojawapo ya kudumu ambayo haiondoki hata kwa wokovu, ni hii wanawake watatafuata wawe wanajua au hawajui watatafuta kuwatawala wanaume na sio kuwatawala tu hata kuwaondoa au kuwaua, au kuwaondoa kabisa wasiwepo hata kama wanaume watawapenda vipi wake zao, wao badala ya kufurahia upendo na muungano huu ambao Mungu aliukusudia, Mungu hapa anatangaza mgogoro utakaokuwepo kati ya mwanaume na mwanamke kutokana na madhara ya dhambi, lakini pia anahitimisha kwa kuonyesha matokeo ya mgogoro huo, hiki ndio wanawake watakuwa wanakitafuta siku zote za maisha yao hata kama watakuwa wameokoka jaribu kubwa la wanawake litakuwa hilo na matokeo ya mgogoro huu ni wao ndio watakaotawalika, Lugha inayotumika hapo na mumeo atakutawala katika lugha ya kiibrania linatumika neno “Mashal” linasomeka “Maw-shal Maana yake ni KUTAWALIWA, kwa msingi huo sasa katika utaratibu mpya wa haki na utawala Mwanamke anapaswa kujinyenyekeza chini ya utawala wa mumewe ili aweze kuwa sawa na aweze kuwa na furaha na amani japo jambo hili halitawafurahishwa kwa vile ni adhabu kutoka kwa Mungu unaona! Waefeso 5:22-25 “Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo. Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;Kwa msingi huo ni muhimu kufahamu kuwa swala la wanawake kujitiisha chini ya mwanaume ni adhabu na hivyo haliwezi kuleta furaha kwao, wao ndio wa kwanza kuleta dhambi na mauti na kutumia uwezo wao wa kushawishi na mwanaume akatii, adhabu yake ilikuwa awe mtii kwa mumewe japo hawatakuwa na furaha kwa sababu watajiona kama wamekuwa duni lakini vilevile heshima yao inapatikana kwa kuolewa na kupendwa, siri kubwa ya mafanikio ya mwanamke na ili aweze kuishi kwa furaha ni kujinyenyekeza kwa Bwana zao yaani waume zao, mwanamke hata awe na fedha kiasi gani, hata awe na mafanikio kwa kiwango gani au awe na cheo kikubwa kiasi gani jambo pekee linaloweza kumjengea heshima ni kuwa na mume na kujinyenyekeza kwa mumewe, endapo mwanamke atakataa jambo hili heshima yake na furaha yake haiwezi kuwa kamili. Kama wanawake hawatagundua siri hii watajikuta wanafanya mikutano mikubwa mingi na kupitisha maazimio mengi sana lakini wanapaswa kukumbuka kuwa mwanaume kuwa juu  na kuwa na mamlaka dhidi yao ni mgogoro uliotangazwa na Mungu katika bustani ya Adeni na dawa yake ni kuukubali mgogoro huo na kukubali kutawalika kinyume cha hapo watakuwa wanamuasi Mungu.


3.       Kwa Wanaume.


Mwanzo 3:17-18 “Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.”


Kiumbe wa mwisho kutamkiwa adhabu alikuwa Mwanadamu na kwa Mara ya kwanza Biblia inamtaja kwa jina lake Adam yeye anahukumiwa kutokana na kosa la kumsikiliza mwanamke na kukubali ushawishi wake Ushauri wa Mungu ni bora zaidi kuliko wa mwanamke Mithali 15:22-26 “Pasipo mashauri makusudi hubatilika; Bali kwa wingi wa washauri huthibithika. Mtu hulifurahia jibu la kinywa chake; Na neno linenwalo wakati wa kufaa ni jema kama nini! Kwa mtu mwenye akili njia ya uhai huenda juu; Ili atoke katika kuzimu chini. Bwana ataing'oa nyumba ya mwenye kiburi; Bali atauthibitisha mpaka wa mjane. Mashauri mabaya ni chukizo kwa Bwana; Bali maneno yapendezayo ni safi Kuzungumza ukweli kuwa ni huyu mwanamke uliyenipa alinishawishi nikala hakukuwa na msaada kwa Adamu alikuwa amesikiliza ujinga na hivyo alikuwa amefanya machukizo kwa Mungu, hukumu yake itakuwa katika kujipatia riziki zake za kila siku, yaani kazi za mikono yake zitampa shida Adamu, wakati mwanamke familia itamtesa mwanaume atapatatabu kazini, atakula mkate kwa shida kazi ambazo zingempa raha nafsini mwake zitampa taabusiku zote za maisha yake, adhabu ya Eva inahusisha taabu za kifamilia na kuwa mtumwa wa mwanaume lakini adhabu ya Adamu inahusisha kuwa mtumwa wa mazingira na kuishi kwa shida au kwa jasho yaani lazima afanye kazi


Hitimisho.


Adhabu zilizotajwa hapo juu haziondoki kwa wokovu wala kwa maombezi, njia ya kweli ya kufanikiwa ni kufanya kazi kwa bidii, kila mwanaume anapaswa kujituma na kufanya kazi kwa bidii ili aweze kuwa mwenye furaha lazima ajaribu kwa kila njia kuyatawala mazingira, ambayo ingekuwa rahisi kuyatawala kwa neema ya Mungu kabla ya anguko lakini sasa atayatawala kwa jasho, wanawake nao hawawezi kuwa na uwezo wa kufikia kilele cha mafanikio bila kuwa wanyenyekevu, Ndoa na kuheshimu mumeo hata kama una kitu gani ndiko kutakakomfanya mwanamke awe na furaha ya kweli huu ndio mpango wa Mungu uliokamili, hivyo wanawake wanapotafuta haki zao na usawa miongoni mwa jamii wasome kwa bidii, wasaidie katika kufanya kazi na wafanikiwe katika kila Nyanja lakini wakumbuke Mungu amemuweka mwanaume juu yao, wanawake wanapookolewa hawana tofauti na wanaume wote wana haki sawa. Wanawake wote hawajaamuliwa kuwanyenyekea wanaume, lakini ilivyo ni kuwa kila mwanamke aliyeolewa anapaswa kumtii mumewe na sio kila mwanaume, kwa hiyo ili furaha yako itimie mtii mumeo swala hili linatakiwa lifanyike kwa hiyari ili liweze kuleta Baraka kwa nini kwa wanawake kuwatii waume zao kunafananishwa na kumtii Kristo hivyo mwanamke anaweza kuyatenda mapenzi ya Mungu akiwa chini ya mumewe, na kwa nini hili lifanyike kwa sababu Mungu amemuweka mwanaume katika nafasi ya utawala, kwa hiyo yanapokuwepo makongamano ya haki sawa wanawaka wanapaswa kupigania haki zao ili wainuke na kutatua changamoto zao lakini katika muktadha wa kukumbuka kuheshimu utaratibu ambao Mungu ameuweka ili amani ya kweli iwatawale na waweze kupendwa na waume zao.

Na. Rev. Innocent Kamote. 

Mkuu wa wajenzi mwenye hekima