Jumatano, 2 Machi 2016

Wajibu wa kila mshirika wa kanisa la nyumbani !



Wajibu wa kila mshirika wa kanisa la nyumbani pia ni wajibu wa kila mshirika wa kanisa kuu, leo ni vema tukiwa na wakati wa kujikumbusha majukumu aliyonayo kila mshirika wa kanisa letu la nyumbani kila mtu katika kanisa akiyafahamu majukumu yake na kuyatekeleza tutaishi kama familia moja na tutaona faida nyingi sana za kuwa wakristo tutajifunza somo hili kwa kuzingatia majukumu hayo kama ifuatavo;-

§  Kujengana na kufarijiana sisi kwa sisi
§  Kupendana sisi kwa sisi
§  Kutiana moyo wakati wa Misiba na kuzikana
§  Kujuliana halia na kuombeana wakati wa ugonjwa
§  Kushirikiana na wenzetu wakati wa furaha
§  Kuombeana na kuchukuliana mizigo sisi kwa sisi
§  Kuhakikisha kanisa letu linakuwa

Kujengana na kufarijiana sisi kwa sisi.
1Wathesalonike 5;11 Warumi 1;12 Ni muhimu kufahamu kuwa mara baada ya kuokolewa sisi wote tunafanyika watoto wa Mungu Hivyo Baba yetu ni mmoja  yaani Mungu Yohana 1;12, Mara baada ya kokoka katika ulimwenu wa kiroho na wakati mwingine hujitokeza katika halia ya mwili wengine wasiookoka kutuchukia kwa sababu sisi sio wa ulimwengu huu, kwa hiyo wakati mwingine kila mmoja wetu anaweza kupitia hali ya kuuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali 1Petro 1;6, hali hizi zinapoachiwa bila kufarijiana ni rahisi mtu huyo kukata tamaa na kurudi nyuma au kuacha wokovu, Hapo ndipo unapkja umuhimu wa kutembeleana na kufarijiana, Mpendwa anayepitia katika majaribu ili adumu katika imani  hutiwa moyo anapomuona mwenzake, na unapogundua kuwa mwenzako ana huzuni unaweza kumfariji na kumjenga upya kwa neno la Mungu na kumfanya aendelee na wokovu, utamtia moyo kutokana na mateso kutoka kwa Mume  au wazazi, au ndugu kwa msingi huo maneno ya kujengana kwa watu waliookoka ni ya msingi sana na sio ya kukatishana tamaa Waefeso 4;29 endapo mshirika mwenzetu amepatwa na msiba ni muhimu kuwa mstari wa mbele katika kufariji kumbuka Martha na Mariam walipopatwa na msiba wayahudi wengi walijitokeza kuwafariji Yohana 11;19 Hata Yesu alihusika katika kuwafariji Martha na Mariam na kuuhairisha msiba kwa Muuujiza mkubwa Bwana atupe neema ya kulizingatia hili na kuzidi katika Jina la Yesu.
Kupendana sisi kwa sisi
Yohana 13;34 Ni muhimu kufahamu kuwa kupenda ni amri kwa msingi huo  kila mmoja wetu asitafute kupendwa  kabla yeye mwenyewe hajaonyesha upendo kwa wengine , wajibu wetu ni kupenda na sio kupendwa. Njia kubwa ya kuonyesha namna tunavyopendana ni pamoja na kutembeleana sisi kwa sisi majumbani mwetu na kujuana hali 1Petro 4;8-9, waebrania 10;24 hatupaswi kutumia kisingizio cha shughuli za dunia na kazi kama  kiasi cha kusiondwa kutembeleana, si vema kuwa watu tunaokutana katika kusanyiko kubwa kasha kila mmoja baada ya ibada anajua lake huu sio upendo kivitedno ni muhimu kutembeleana  jambo la msingi ni kutembeleana katika ustahivu kaka kwa kaka na dada kwa dada au wakina kaka kwa dada au akida dada kwa kaka ili kumtunzia Mungu heshima  walimwengu wasifikiri kuwa tunafanya uasherati Matedno 24;16,2wakoritho 8;20-21, Waefeso 5;3.
Kutiana moyo wakati wa Misiba na kuzikana
Kuzikana nin jambo la kibiblia na ni ukristo mwenzetu anapoondoka ni muhimu kujihusisha katika shughuli yake na kumsindikiza kwa heshima kubwa kuzika ni jambo la Baraka Mungu mwenyewe alionyesha mano kwa kumzika mtumishi wake Musa yeye mwenyewe Kumbukumbu 34;5-6, wanafunzi wa Yohana Mbatizaji walishirii kikamilifu katika kumzika Yohana Mathayo 14;10,12, watakatifi katika nyakati za kanisa la kwanza walishiriki katika kumzika  mwenzao Stefano na kumfania maombolezo makuu Matendo 8;2 ni muhimu sana kwa wakristo kuwa na tabia hii kama tutasikia wenzetu wamepatwa na msiba  ni muhimu kwetu kujitoa na kuhakikisha kuwa tunahisika kipekee katika kumsindikiza kwa heshima kubwa maswla ya kuzingatia;-
§  Taarifa ya msiba ikipatikana ipelekwe mapema kwa Mchungaji.
§  Kwaya ya kanisa itahusika katika kuhakikisha kuwa mahali pa msiba panaimbwa nyimbo za aina mbalimbali pasiwe kimya tu. Kama ikibidi ni muhimu hata kukesha wakiimba na kuombea faraja familia husika
§  Wahusika watiwe moyo na kuulizwa utaratibu utakavyokuwa.
§  Wahusika watahakikisha wanashiriki michango na pia kuangalia au kuusika katika uchimbaji wa Kaburi na ubebaji wa jeneza na mazishi kwa ujumla umoja na upendo na heshima itakayoonyeshwa itawafanya watu kuvutiwa na imani yetu Jambo la kushangaza ni kuwa watu wengi waliookoka wakimaliza kuzika tu hutawanyika ni muhimu kurudi nyumbani na kufanya maombi na ibada ya faraja kwa waliofiwa na kukemea roho ya misiba isijitokeze tena 
Ni jambo la kushangaza kwamba watu wengi waliookoka maswala ya msiba huchukuliwa kipuuuzi na kama maswala ya kubaatisha hivi hilo sio jambo zuri hata kidogo, kupitia namna tunavyowazika wenzetu tunaweza kuwafikia wengi sana kwa Yesu kwani watu wengi hupenda kuzikwa kwa Heshima kubwa na hilo pekee laweza kuwa kizuizi cha kuokoka.
Kujuliana halia na kuombeana wakati wa ugonjwa
Ni muhimu kufaamu kuwa tangu zamani za Biblia watu walitembeleana wakati wa uonjwa 2Wafalme 8;29 Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda  alikwenda kumtazama mfalme Yoramu alipokuwa anaumwa, Yehoashi mfalme wa Israel alikwenda kumtazama nabii Elisha alipokuwa ameshikwa na ugonjwa na kumlilia  katika maombi 2Wafalme 13;14 ni muhimu kufanya hivyo na kuzidi katika nayakati hizi za agano jipya hususani sisi tuliookoka, mwenzetu anapoumwa na kuugua hatuna budi kwenda kumtazama kama ni nyumbani kwake au Hospitalini na kuomba pamoja naye na kumfariji kwa kufanya hivyo Kristo atatupa thawabu kubwa na kutuhesabu kuwa tulikwenda kumtazama yeye Mathayo 25;36,40, hiyo ndiyo dini ya kweli iliyo safi isiyo na taka ni kuwajali watu katika dhiki zao Yakobo 1;27 Taarifa za ugonjwa wa mpendwa awaye yote ni muhimu zikajulikana kwa kanisa ili wazee waweze kuomba Yakobo 5;13-15.
Kushirikiana na wenzetu wakati wa furaha.
Ni muhimu kwetu kuwa na ufahamu  wa kushirikiana na wenzetu wakati wa furaha kama mtu akijifungua  hatuna budi kufurahi pamoja naye na kumpelekea zawadi kama walivyofanya mamajusi kwa Yesu Mathayo 2;11, mwenzetu akifanikiwa kujenga shiriki katika ibada ya kuweka wakfu nyumba yake mpya  na kuifungua kwa furaha, mwenzetu anapofanikiwa kuoa au kuolewa katika harusi hatuna budi kumpa zawadi au kufanikisha harusi yake kwa michango yetu ya hali na malipia kufurahi pamoja na ndoa mpya 1Wakoritho 12;26. Ni muhimu kanisa kuwa na roho ya kupenda mafaniko ya wengine na kuyafurahia badala ya kuoneana wivu.
Kuombeana na kuchukuliana mizigo sisi kwa sisi
Yakobo 5;16 Maandiko yanakazia swala zima la kuombeana na kusameheana  ni muhimu katika kanisa kila mmoja kuwa na Orodha ya majina ya washirika wengine na kuwaombea mbele za Mungu kwa kuwataja majina yao, na ni lazima kuwaombea viongozi wa kanisa na mchungaji wetu, wakati huo huo tukichukuliana mizigo Wagalatia 6;2,10 kwa kadiri ya neema tuliyopewa na Mungu kila mmoja wetu anapaswa aitumie neema aliyopewa kuchukua mizigo ya wenziwe 1Petro 4;10, kama una nama ya kumtafutia mtu kazi mpatie kazi, kuwalipia nauli kuja ibadani kutoa mitaji ya kibiashara na ushauri wa nini cha kufanya  kwa kufanya hivyo unajiwekea hazina yao mbinmguni Mathayo 6;19-21.
Kuhakikisha kanisa letu linakuwa
Ni wajibu wa kila mshirika kuwa na mzigo na maono ya kuhakikisha kanisa linakuwa na kuongezeka kamwe usiridhike kuona watu ni wachache wakatai wengi wanamtumkia shetani, hakikisha unawashuhudia wengine na kuwaalika kuja katika ibada kila mmoja aliyeokoka anawajibu wa kumzalia Bwana matunda Yohana 15;2 kanisa linalozaa Yesu hulitunza na maombi yetu mengi yatakuwa yakijibiwa Yohana 15;16 ndiyo maana ni muhimu kuwaalika wengine kuja ibadani na siku ya mwisho tutang’aa kama jua kwa kuongoza wengi katika kutenda mema.

Jinsi ya Kuwa na Ushindi dhidi ya Uchawi !



Uchawi ni moja ya maeneo makubwa ya utendaji wa kazi wa ibilisi katika kuwaonea wanadamu na kushindana kinyume na Mungu, katika somo hili tutajifunza kwa undani asili ya uchawi na jinsi ya kuwa na ushindi dhidi ya uchawi makusudi makuu hasa ikiwa ni kukusaidia mtu aliyeokoka kutokuwa na hofu dhidi ya uchawi endapo utazingatia ufahamu utakaoupata katika somo hili tutazingatia vipengele vifuatavyo;-

·         Asili ya Uchawi
·         Jinsi ya kuwa na Ushindi dhidi ya uchawi.

Asili ya Uchawi.
Uchawi ni kazi ya Shetani na mtu yeyote anayejishughulisha na Uchawi ni mtumishi wa shetani anayekuwa amepewa kibali cha kuwatumia mapepo na majini kwa kusudi la kuwadhuru wanadamu na kuwafanya wanadamu wamuabudu shetani, kwa lugha nyepesi mtu awaye yote anayejishughulisha na uchawi anafanya ushirikiano na shetani kwa hiyo huitwa MSHIRIKINA, Biblia inakataza wakristo kushirikiana na shetani kwa gharama yoyote 1Wakoritho 10; 20-21 Matendo 13; 6-10. Ni muhimu kufahamu kuwa ili mtu awe na Ushindi dhidi ya uchawi anapaswa kwanza kuamini kwamba Uchawi uko ufahamu huu haukufanyi wewe kuwa na mawazo ya kizamani lakini ni ufahamu unaokubaliana na neno la Mungu ambalo lenyewe linatambua kuwa uchawi uko  Kutoka 7; 11 Nahumu 3;4 Matendo 8;9-10, Ezekile 47;8-15, Moja ya mbinu kubwa ya shetani anayoitumia ni kuwapandikizia watu wazo potofu kuwa kusema kuwa uchawu upo ni imani potofu zilizopitwa na wakati ni imani za kishirikina Huu ni uongo wa Ibilisi ili aendelee kutesa watu kupitia njia za kichawi huku wao wakidhani kila kitu ni cha kawaida tu!
Ni muhimu kufahamu kuwa Pepo wabaya wao walikuwa malaika ambao waliasi na wamekwisha kuhukumiwa na hatima yao ni katika ziwa la Moto waliowekewa tayari mileleWaefeso 6;12,Mathayo 25;41 Shetani na majeshi yake yote hayana uwezo wowote mbele za Yesu Kristo aliye Bwana na mwokozi wetu alipokuwa Duniani na hata akiwa huko mbinguni shetani na mapepo yanamuogpa sana Bwana Yesu kwani ana mamlaka ya kuwatesa Marko 5;1-13, tunapokuwa tumemuamini Yesu tunakuwa ndani yeke na kwa sababu yeye ndiye kongozi wetu Uchawi wa kila namna hauna nguvu tena ju yetu Ufunuo 3;20; Hesabu 23;23 Historia ya kibiblia inaonyesha kuwa wachawi wakati wote walipokumbana na nguvu za Mungu  walikiri kuwa Bwana ni mwenye uwezo na kuwa hawawezi kushindana naye Kutoka 7;10-13,8;16-19,9;9-11, Simeon aliyekuwa anaogopewa sana huko Samaria alipokutana na uweza wa Bwana alisalimu amri na kukiri kuwa Uweza wa Bwana ni mkuu Matendo 8;9-13, Elima Yule mchawi naye alisalimu amri wakati Paulo alipoliitia jina la Bwana kumshughulikia Matendo 13;6-12.
Ni muhimu kufahamu kuwa hata katika nyakati hizi tulizonazo watakuweko wachawi huko mitaani na vijijini na mijini na nyumba tunazoiishi watakuwa wakijaribu kupambana nasi ili kututia woga tutahisi miili ikisisimka, kutembelewa na viumbe vya ajabu dalini au usumbufu wa panya wasio wa kawaida n.k kila uonapo dalili hizo usiogope kwani tumepewa amri ya kukanyaga nyoka na nge na NGUVU ZOTE ZA YULE ADUI hakuna kitakachotudhuru! Luka 10; 19
Jinsi ya kuwa na Ushindi dhidi ya wachawi.
Tubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha  ili muovu asiwe na nguvu juu yetu Mithali 28;13 1Yohana 5;18 1Yohana 2;1-3, Kataa kazi zote za kishetani na kuchoma moto aina zozote za maagano na hirizi Matendo ya Mitume 19;17-20, Kaa katika kweli ya Neno la Mungu Yohana 8;31-32, Hesabu 23;23.

Thamani ya Neno la Mungu!



Neno la msingi; Zaburi 119; 72 “Sheria ya kinywa chako ni njema kuliko maelfu ya dhahabu na fedha.” Sheria inayotajwa hapo ni neno la Mungu mwandishi wa Zaburi hii analiona neno la Mungu kuwa ni jema kuliko maelfu ya dhahabu na fedha maana yake ni kuwa katika ujuzi wake na maarifa aligundua kuwa thamani ya neno la Mungu inazidi thamani ya fedha na dhahabu.

 Neno la Mungu lina thamani kuu kuliko dhahabu na fedha

§  Madhara ya kutokujua uthamani wa Neno la Mungu.
§  Uthamani wa Neno la Mungu.

Madhara ya kutokujua Uthamani wa Neno la Mungu.
Kwa kukosa maarifa watu wengi wameshindwa kufahamu uthamani wa neno la Mungu, Mwandishi wa zaburi 119;72 alifahamu thamani ya neno la Mungu kuliko wengi wetu ni kweli kuwa neno la Mungu lina thamanikubwa kuliko maelfu ya dhahabu na fedha, Watakatifu wengi waliotutangulia kwenda mbinguni walikuwa na ushuhuda kama huo kuhusu Neno la Mungu, walijua kuwa neno la Mungu lina tahamani kubwa kuliko vyote vilivyotamanika, iwe ni dhahabu, madini ya marijani au rubi ama fedha, vyote hivi havilingani na thamani ya mafundisho ya neno la Mungu au hekima itokanayo na ufahamu wa neno la Mungu Mithali 8;10-11,3;13-15, ni muhimu kumbuka kuwa mtu aliye tajiri akiitumia fedha kununua vyote anavyovitamani anapokufa huviacha duniani na haendi na chochote Zaburi 49;16-17. Kwa msingi huo ni muhimu kwa kila Mtu kuwa naufahamu wa neno la Mungu ambalo lenyewe ni la milele.

Uthamani wa Neno la Mungu.
Watu wengi ambao hawajui uthamani wa neno la Mungu hawatengi muda wa kuwa na saa chache za kulisikia na kulisoma neno la Mungu badala yake hutenga muda wote katika kujishughulisha na utafutaji wa fedha na kujihusisha na anasa za Dunia, Neno la Mungu likitiliwa maanani lina uwezo wa kutufikisha katika uzima wa milele na milele lakini endapo hauatalijali hata kama tunaweza kufanikiwa sana katika utajiri wa ulimwengu huu tunaweza kujikuta tunaingia katika Hasara na mateso ya milele na milele Mfano wa Lazaro na Tajiri Luka 16;19-24. Ni muhimu basi kila mtu aliyeokolewa akatoa kipaumbele kwa maswala ya kujitajirisha kwa Mungu Luka 12; 16-21. Kujitayarisha kwa Mungu ni kuwa katika hali ya kuwa na Muda wa kujifunza Mapenzi yake na kuyatendea kazi, juhudi ambazo tunaweza kuzielekeza katika kujitafutia mali zinaweza pia kuelekezwa kwa kiwango Fulani katika kujitafutia hekima ya neno la Mungu ambalo nalo tunapaswa kulitafuta  kama fedha au hazina iliyositirika Mithali 2;2-5 kwa msingi huo ni muhimu sana kwetu kuhakikisha kuwa tunawekeza katika kujitafutia kumjua Mungu kupitia neno lake  na hata kutumia mapato yetu katika kujipatia ufahamu wa neno la Mungu Mithali 4;4,7, kukubali kugharimika kufika katika siku za mafundisho hata kama yanapatikana mbali na pale tulipo Mathayo 12;42 Kristo alipendezwa na Malikia wa sheba aliyetoka mbali kwaajili ya kusikiliza hekima ya Sulemani atafurahishwa nasi endapo tutatafuta hekima yake kwa gharama Yoyote, wakati mwingine tunaweza kupata vikwazo kadhaa kwaajili ya kuitafuta kweli, unaweza kupigwa na Mumeo kwa sababu tu ya kuja kuyasikiliza maneno ya Mungu au wazazi wakakupinga katika hatua za mwanzoni upinzani huo ni jambo la kawaida hatimaye  Mungu ataupa hekima na namna ya kushinda, lazima tukumbuke kuhangaika kwaajili ya nafsi zetu kwani hatimaye siku ya mwisho kila mtu atatoa hesabu yake mwenyewe, hatutakuwa na udhuru kuwa nani alikuzuia usiyasikiemaneno ya Mungu ambayo tumejifunza kuwa ni ya thamani kulio fedha Warumi 14;12. Bwana ampe neema kila mmoja wetu kuyapenda, kuyatafuta na kuyatendea kazi maneno yake na kutenga Muda wetu wa kuhudhuria Ibada Bila udhuru wa aina iwayoyote ili tupate kibali kwake. Ukiyajua hayo Heri wewe ukiyatenda Yohana 13;17.

Hapa yupo Aliyemkuu Kuliko Sulemani


Mathayo 12: 38-42 Biblia inasema “38. Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako. 39. Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona.  40. Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi.  41. Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona. 42. Malkia wa kusini atasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu yeye alikuja kutoka pande za mwisho za dunia ili asikie hekima ya Sulemani, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.” 



Kifungu hicho hapo juu cha maandiko ni cha muhimu sana na tunapokifanyia uchambuzi yakinifu itatupa mwanga wa kumfahamu Yesu Kristo kwa kina na upana na urefu zaidi, kifungu hiki ni matokeo ya mjadala uliokuweko kuhusu Yesu Kristo, Baada ya Wayahudi hasa jamii ya  mafarisayo kumnenea Yesu maneno mabaya zaidi, Baada ya kuwa Yesu amemponya mtu aliyekuwa ana pepo, kipofu na ni Bubu, Mathayo 12:22-23, Muujiza huu uliwashangaza watu na kumfanya Yesu aanze kukubalika miongoni mwa jamii kuwa “MWANA WA DAUDI” hii ilikuwa ni wazi kuwa walikubali kuwa Yesu ndiye MASIHI, ni wazi kuwa kwa kazi hii na nyinginezo alizozifanya Yesu zilipelekea watu kumuamini na kuondoa shaka kuwa ndiye mfalme ajaye kwa JIna la Bwana, Hata hivyo kwa sababu ya wivu wa Mafarisayo ambao waliona Yesu anaheshimika zaidi na kuwa gumzo kuliko wao waliamua kwa makusudi kuharibu kibali cha Yesu kwa kusema kuwa anatoa pepo kwa nguvu za mkuu wa Mapepo Belzebuli (Mathayo 12:24)

Yesu Kristo akitambua hilo alitoa hutuba kali sana ya maonyo dhidi ya watu wanaopinga kazi ya Mungu Roho mtakatifu, na zaidi ya yote aliwaonya watu kuhusu kuzungumza maneno yasiyo na maana kwa vile watatoa hesabu kwa kila neno lisilo na maana wanalolitoa katika vinywa vyao, Mathayo 12:33-37.

Baada ya hutuba hii ya Yesu ambayo ilikuwa kali na yenye maonyo baadhi ya Mafarisayo waliogopa sana Lugha “Hapo” inatumika kuonyesha kuwa iliwalazimu sasa waombe ishara ya kumfahamu Yesu vema kuwa yeye ni nani, Tupe ishara itakayotusaidia kukutambua wewe ni nani? Ndipo Yesu aliwajibu kwamba watamtabua kupitia Ishara kuu mbili.

1.       Ishara ya Nabii Yona.
Yesu aliwaeleza kwa uwazi kuwa Ishara ya kumtambua Masihi iko wazi, ishara hii ndiyo iliyowavutia watu wa Ninawi wakatubu na kumgeukia Mungu kupitia mahubiri ya Yona, Mathayo 12:38-41, Kimsingi Yesu alitaka kukazia kuwa kile kilichomtokea Yona kilikuwa ni ishara halisi, na kilikuwa ni kivuli cha kumtambua Masihi, ambaye Yesu alikazia kuwa ni mkuu kuliko Yona, Yesu alikazia kuwa namna njema ya kumtambua yeye nip ala atakapokufa na kufufuka siku ya Tatu, hii ndio kazia kubwa ya ukombozi itakayowavuta wengi katika ufalme wa Mungu.

2.       Ishara ya Malkia wa Sheba.
Yesu aliwapa Mafarisayo Ishara nyingine ya muhimu. Ambapo sasa anaeleza kuhusu Malkia wa kusini yaani Sheba kwamba alitoka mbali sana pande zamwisho wa Nchi kuja kusikiliza Hekima ya Sulemani, Yesu ni kama alikuwa anakazia kuwa njia nyingina ya kumtambua ni kumsikiliza, usikivu ungeliwasaidia kujua kuwa hakuna mwingine anayeweza kunena au kutenda katika kiwango kama cha Yesu, Mathayo 12:42 hata hivyo  mahali hapa ndipo paliponisukuma zaidi kufanya Uchambuzi hususani Yesu alipohitimisha kuwa malikia huyu alisafiri kutoka mbali kusikiliza Hekima ya Sulemani, hata hivyo Yesu alitamka wazi kuwa Yeye ni mkuu kuliko Sulemani.

Suleimani ni mfalme aliyeishi kwa anasa na ufahari wa hali ya juu, mfalme huyo alikuwa na Hekima na ufahamu na maarifa ya hali ya juu sana kuliko wafalme wote ambao wamepata kuweko, Biblia inasema kabla yake hajakuweko na badala yake hatokuweko 1Wafalme 3:9-13, 4;29-34 unaweza kuona!, wengi waliosikia Hekima ya Suleimani katika enzi zake walisafiri kutoka mbali ili kwenda kumsikiliza, Lakini ziara ya kifahari na maarufu sana na iliyoelezewa kwa kina ni safari ya Malkia wa Sheba au Ethiopia ambaye alikwenda kwa mikogo mingi na mikubwa  1Wafalme 10:1, 2Nyakati 9:1-6 Biblia inasema malkia huyu alikwenda akiwa na maswalai magumu sana “She came to Jerusalem to test him with Hard Questions” pamoja na ziara yake ya kifahari na zawadi kibao alizozibeba alipofika Yerusalem kwa Suleimani alijibiwa maswali yake yote  na mambo yake yote hata aliyokuwa ameyaficha sirini, hakuna kilichofichika kwa Suleimani, alitosheleza mahitaji yake yote na hisia zake zote zilijibiwa na kuzidi.

Dunia ya leo ina maswali magumu mengi yasiyo na majibu, pamoja na kuendelea na kukua kwamaarifa na uvumbuzi wa kisayansi na Teknolojia, Watu wanazidi kuharibikiwa dunia imejaa hekina ya uharibifu, wizi,ufisadi,uchochezi,uchoinganishi, majungu na fitina, kuliza wengine, kutoa mimba udanganyifu, na hakuna majibu ya maswala muhimu katika matatizo ya watu, Sulemani alikuwa na ujuzi zaidi ya wa kibailojia, Chemistry, Physics, aliishi kwa anasa kuliko mtu yeyote, mwisho aliona hekina na maarifa bila ya Mungu ni upuuzi au ubatili,alishauri watu kumkubuka Muumba wao siku za ujana wao, Muumba huyu ndiye mkuu kuliko Sulemani, Yesu Kristo anatajwa kama Hekima yetu 1Wakoritho 1:18 kwa kiyunani Epignosis sofia, Full of wisdom Knowledge and Understanding, yesu aliposema Hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani alimaanisha Yeye ndiye aliyemuumba huyo Sulemani, Yeye ndiye mwenye majibu yote hata ya mambo magumu, Yeye ndiye Masihi, ni zaidi ya mfalme Sulemani, watu watatoka kila pande za dunia kumjia yeye, na atawahukumu wote waliomkataa yey.

Hapa yupo aliye mkuu Kuliko Sulemani.