Uchawi ni moja ya maeneo makubwa
ya utendaji wa kazi wa ibilisi katika kuwaonea wanadamu na kushindana kinyume
na Mungu, katika somo hili tutajifunza kwa undani asili ya uchawi na jinsi ya
kuwa na ushindi dhidi ya uchawi makusudi makuu hasa ikiwa ni kukusaidia mtu
aliyeokoka kutokuwa na hofu dhidi ya uchawi endapo utazingatia ufahamu utakaoupata
katika somo hili tutazingatia vipengele vifuatavyo;-
·
Asili ya Uchawi
·
Jinsi ya kuwa na Ushindi dhidi ya uchawi.
Asili ya Uchawi.
Uchawi ni kazi
ya Shetani na mtu yeyote anayejishughulisha na Uchawi ni mtumishi wa shetani
anayekuwa amepewa kibali cha kuwatumia mapepo na majini kwa kusudi la kuwadhuru
wanadamu na kuwafanya wanadamu wamuabudu shetani, kwa lugha nyepesi mtu awaye
yote anayejishughulisha na uchawi anafanya ushirikiano na shetani kwa hiyo
huitwa MSHIRIKINA, Biblia inakataza wakristo kushirikiana na shetani kwa
gharama yoyote 1Wakoritho 10; 20-21 Matendo 13; 6-10. Ni muhimu kufahamu kuwa
ili mtu awe na Ushindi dhidi ya uchawi anapaswa kwanza kuamini kwamba Uchawi
uko ufahamu huu haukufanyi wewe kuwa na mawazo ya kizamani lakini ni ufahamu
unaokubaliana na neno la Mungu ambalo lenyewe linatambua kuwa uchawi uko Kutoka 7; 11 Nahumu 3;4 Matendo 8;9-10,
Ezekile 47;8-15, Moja ya mbinu kubwa ya shetani anayoitumia ni kuwapandikizia
watu wazo potofu kuwa kusema kuwa uchawu upo ni imani potofu zilizopitwa na
wakati ni imani za kishirikina Huu ni uongo wa Ibilisi ili aendelee kutesa watu
kupitia njia za kichawi huku wao wakidhani kila kitu ni cha kawaida tu!
Ni muhimu kufahamu
kuwa Pepo wabaya wao walikuwa malaika ambao waliasi na wamekwisha kuhukumiwa na
hatima yao ni katika ziwa la Moto waliowekewa tayari mileleWaefeso 6;12,Mathayo
25;41 Shetani na majeshi yake yote hayana uwezo wowote mbele za Yesu Kristo
aliye Bwana na mwokozi wetu alipokuwa Duniani na hata akiwa huko mbinguni shetani
na mapepo yanamuogpa sana Bwana Yesu kwani ana mamlaka ya kuwatesa Marko
5;1-13, tunapokuwa tumemuamini Yesu tunakuwa ndani yeke na kwa sababu yeye
ndiye kongozi wetu Uchawi wa kila namna hauna nguvu tena ju yetu Ufunuo 3;20; Hesabu
23;23 Historia ya kibiblia inaonyesha kuwa wachawi wakati wote walipokumbana na
nguvu za Mungu walikiri kuwa Bwana ni
mwenye uwezo na kuwa hawawezi kushindana naye Kutoka 7;10-13,8;16-19,9;9-11,
Simeon aliyekuwa anaogopewa sana huko Samaria alipokutana na uweza wa Bwana
alisalimu amri na kukiri kuwa Uweza wa Bwana ni mkuu Matendo 8;9-13, Elima Yule
mchawi naye alisalimu amri wakati Paulo alipoliitia jina la Bwana
kumshughulikia Matendo 13;6-12.
Ni muhimu
kufahamu kuwa hata katika nyakati hizi tulizonazo watakuweko wachawi huko
mitaani na vijijini na mijini na nyumba tunazoiishi watakuwa wakijaribu
kupambana nasi ili kututia woga tutahisi miili ikisisimka, kutembelewa na viumbe
vya ajabu dalini au usumbufu wa panya wasio wa kawaida n.k kila uonapo dalili
hizo usiogope kwani tumepewa amri ya kukanyaga nyoka na nge na NGUVU ZOTE ZA YULE ADUI hakuna
kitakachotudhuru! Luka 10; 19
Jinsi ya kuwa na Ushindi dhidi ya wachawi.
Tubu dhambi
zako zote kwa kumaanisha kuziacha ili
muovu asiwe na nguvu juu yetu Mithali 28;13 1Yohana 5;18 1Yohana 2;1-3, Kataa
kazi zote za kishetani na kuchoma moto aina zozote za maagano na hirizi Matendo
ya Mitume 19;17-20, Kaa katika kweli ya Neno la Mungu Yohana 8;31-32, Hesabu
23;23.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni