Jumatano, 2 Machi 2016

Wajibu wa kila mshirika wa kanisa la nyumbani !



Wajibu wa kila mshirika wa kanisa la nyumbani pia ni wajibu wa kila mshirika wa kanisa kuu, leo ni vema tukiwa na wakati wa kujikumbusha majukumu aliyonayo kila mshirika wa kanisa letu la nyumbani kila mtu katika kanisa akiyafahamu majukumu yake na kuyatekeleza tutaishi kama familia moja na tutaona faida nyingi sana za kuwa wakristo tutajifunza somo hili kwa kuzingatia majukumu hayo kama ifuatavo;-

§  Kujengana na kufarijiana sisi kwa sisi
§  Kupendana sisi kwa sisi
§  Kutiana moyo wakati wa Misiba na kuzikana
§  Kujuliana halia na kuombeana wakati wa ugonjwa
§  Kushirikiana na wenzetu wakati wa furaha
§  Kuombeana na kuchukuliana mizigo sisi kwa sisi
§  Kuhakikisha kanisa letu linakuwa

Kujengana na kufarijiana sisi kwa sisi.
1Wathesalonike 5;11 Warumi 1;12 Ni muhimu kufahamu kuwa mara baada ya kuokolewa sisi wote tunafanyika watoto wa Mungu Hivyo Baba yetu ni mmoja  yaani Mungu Yohana 1;12, Mara baada ya kokoka katika ulimwenu wa kiroho na wakati mwingine hujitokeza katika halia ya mwili wengine wasiookoka kutuchukia kwa sababu sisi sio wa ulimwengu huu, kwa hiyo wakati mwingine kila mmoja wetu anaweza kupitia hali ya kuuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali 1Petro 1;6, hali hizi zinapoachiwa bila kufarijiana ni rahisi mtu huyo kukata tamaa na kurudi nyuma au kuacha wokovu, Hapo ndipo unapkja umuhimu wa kutembeleana na kufarijiana, Mpendwa anayepitia katika majaribu ili adumu katika imani  hutiwa moyo anapomuona mwenzake, na unapogundua kuwa mwenzako ana huzuni unaweza kumfariji na kumjenga upya kwa neno la Mungu na kumfanya aendelee na wokovu, utamtia moyo kutokana na mateso kutoka kwa Mume  au wazazi, au ndugu kwa msingi huo maneno ya kujengana kwa watu waliookoka ni ya msingi sana na sio ya kukatishana tamaa Waefeso 4;29 endapo mshirika mwenzetu amepatwa na msiba ni muhimu kuwa mstari wa mbele katika kufariji kumbuka Martha na Mariam walipopatwa na msiba wayahudi wengi walijitokeza kuwafariji Yohana 11;19 Hata Yesu alihusika katika kuwafariji Martha na Mariam na kuuhairisha msiba kwa Muuujiza mkubwa Bwana atupe neema ya kulizingatia hili na kuzidi katika Jina la Yesu.
Kupendana sisi kwa sisi
Yohana 13;34 Ni muhimu kufahamu kuwa kupenda ni amri kwa msingi huo  kila mmoja wetu asitafute kupendwa  kabla yeye mwenyewe hajaonyesha upendo kwa wengine , wajibu wetu ni kupenda na sio kupendwa. Njia kubwa ya kuonyesha namna tunavyopendana ni pamoja na kutembeleana sisi kwa sisi majumbani mwetu na kujuana hali 1Petro 4;8-9, waebrania 10;24 hatupaswi kutumia kisingizio cha shughuli za dunia na kazi kama  kiasi cha kusiondwa kutembeleana, si vema kuwa watu tunaokutana katika kusanyiko kubwa kasha kila mmoja baada ya ibada anajua lake huu sio upendo kivitedno ni muhimu kutembeleana  jambo la msingi ni kutembeleana katika ustahivu kaka kwa kaka na dada kwa dada au wakina kaka kwa dada au akida dada kwa kaka ili kumtunzia Mungu heshima  walimwengu wasifikiri kuwa tunafanya uasherati Matedno 24;16,2wakoritho 8;20-21, Waefeso 5;3.
Kutiana moyo wakati wa Misiba na kuzikana
Kuzikana nin jambo la kibiblia na ni ukristo mwenzetu anapoondoka ni muhimu kujihusisha katika shughuli yake na kumsindikiza kwa heshima kubwa kuzika ni jambo la Baraka Mungu mwenyewe alionyesha mano kwa kumzika mtumishi wake Musa yeye mwenyewe Kumbukumbu 34;5-6, wanafunzi wa Yohana Mbatizaji walishirii kikamilifu katika kumzika Yohana Mathayo 14;10,12, watakatifi katika nyakati za kanisa la kwanza walishiriki katika kumzika  mwenzao Stefano na kumfania maombolezo makuu Matendo 8;2 ni muhimu sana kwa wakristo kuwa na tabia hii kama tutasikia wenzetu wamepatwa na msiba  ni muhimu kwetu kujitoa na kuhakikisha kuwa tunahisika kipekee katika kumsindikiza kwa heshima kubwa maswla ya kuzingatia;-
§  Taarifa ya msiba ikipatikana ipelekwe mapema kwa Mchungaji.
§  Kwaya ya kanisa itahusika katika kuhakikisha kuwa mahali pa msiba panaimbwa nyimbo za aina mbalimbali pasiwe kimya tu. Kama ikibidi ni muhimu hata kukesha wakiimba na kuombea faraja familia husika
§  Wahusika watiwe moyo na kuulizwa utaratibu utakavyokuwa.
§  Wahusika watahakikisha wanashiriki michango na pia kuangalia au kuusika katika uchimbaji wa Kaburi na ubebaji wa jeneza na mazishi kwa ujumla umoja na upendo na heshima itakayoonyeshwa itawafanya watu kuvutiwa na imani yetu Jambo la kushangaza ni kuwa watu wengi waliookoka wakimaliza kuzika tu hutawanyika ni muhimu kurudi nyumbani na kufanya maombi na ibada ya faraja kwa waliofiwa na kukemea roho ya misiba isijitokeze tena 
Ni jambo la kushangaza kwamba watu wengi waliookoka maswala ya msiba huchukuliwa kipuuuzi na kama maswala ya kubaatisha hivi hilo sio jambo zuri hata kidogo, kupitia namna tunavyowazika wenzetu tunaweza kuwafikia wengi sana kwa Yesu kwani watu wengi hupenda kuzikwa kwa Heshima kubwa na hilo pekee laweza kuwa kizuizi cha kuokoka.
Kujuliana halia na kuombeana wakati wa ugonjwa
Ni muhimu kufaamu kuwa tangu zamani za Biblia watu walitembeleana wakati wa uonjwa 2Wafalme 8;29 Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda  alikwenda kumtazama mfalme Yoramu alipokuwa anaumwa, Yehoashi mfalme wa Israel alikwenda kumtazama nabii Elisha alipokuwa ameshikwa na ugonjwa na kumlilia  katika maombi 2Wafalme 13;14 ni muhimu kufanya hivyo na kuzidi katika nayakati hizi za agano jipya hususani sisi tuliookoka, mwenzetu anapoumwa na kuugua hatuna budi kwenda kumtazama kama ni nyumbani kwake au Hospitalini na kuomba pamoja naye na kumfariji kwa kufanya hivyo Kristo atatupa thawabu kubwa na kutuhesabu kuwa tulikwenda kumtazama yeye Mathayo 25;36,40, hiyo ndiyo dini ya kweli iliyo safi isiyo na taka ni kuwajali watu katika dhiki zao Yakobo 1;27 Taarifa za ugonjwa wa mpendwa awaye yote ni muhimu zikajulikana kwa kanisa ili wazee waweze kuomba Yakobo 5;13-15.
Kushirikiana na wenzetu wakati wa furaha.
Ni muhimu kwetu kuwa na ufahamu  wa kushirikiana na wenzetu wakati wa furaha kama mtu akijifungua  hatuna budi kufurahi pamoja naye na kumpelekea zawadi kama walivyofanya mamajusi kwa Yesu Mathayo 2;11, mwenzetu akifanikiwa kujenga shiriki katika ibada ya kuweka wakfu nyumba yake mpya  na kuifungua kwa furaha, mwenzetu anapofanikiwa kuoa au kuolewa katika harusi hatuna budi kumpa zawadi au kufanikisha harusi yake kwa michango yetu ya hali na malipia kufurahi pamoja na ndoa mpya 1Wakoritho 12;26. Ni muhimu kanisa kuwa na roho ya kupenda mafaniko ya wengine na kuyafurahia badala ya kuoneana wivu.
Kuombeana na kuchukuliana mizigo sisi kwa sisi
Yakobo 5;16 Maandiko yanakazia swala zima la kuombeana na kusameheana  ni muhimu katika kanisa kila mmoja kuwa na Orodha ya majina ya washirika wengine na kuwaombea mbele za Mungu kwa kuwataja majina yao, na ni lazima kuwaombea viongozi wa kanisa na mchungaji wetu, wakati huo huo tukichukuliana mizigo Wagalatia 6;2,10 kwa kadiri ya neema tuliyopewa na Mungu kila mmoja wetu anapaswa aitumie neema aliyopewa kuchukua mizigo ya wenziwe 1Petro 4;10, kama una nama ya kumtafutia mtu kazi mpatie kazi, kuwalipia nauli kuja ibadani kutoa mitaji ya kibiashara na ushauri wa nini cha kufanya  kwa kufanya hivyo unajiwekea hazina yao mbinmguni Mathayo 6;19-21.
Kuhakikisha kanisa letu linakuwa
Ni wajibu wa kila mshirika kuwa na mzigo na maono ya kuhakikisha kanisa linakuwa na kuongezeka kamwe usiridhike kuona watu ni wachache wakatai wengi wanamtumkia shetani, hakikisha unawashuhudia wengine na kuwaalika kuja katika ibada kila mmoja aliyeokoka anawajibu wa kumzalia Bwana matunda Yohana 15;2 kanisa linalozaa Yesu hulitunza na maombi yetu mengi yatakuwa yakijibiwa Yohana 15;16 ndiyo maana ni muhimu kuwaalika wengine kuja ibadani na siku ya mwisho tutang’aa kama jua kwa kuongoza wengi katika kutenda mema.

Maoni 2 :

Bila jina alisema ...

Somo zuri sana

Njinyembamba alisema ...

somo safi sana,limenibariki.