Jumanne, 7 Juni 2016

Kuzaliwa kwa Masihi na Mioyo ya watu


Leo ni sikukuu ya CHRISTIMAS  Wakristo wote Nchini tunajiunga na wakristo wengine Duniani katika kuadhimisha siku kuu hii ya Kuzaliwa kwa Mwokozi, Zaidi ya miaka 2000 iliyopita huko Bethelehemu, Katika siku hii muhimu namna hii ni muhimu sana kwetu pia kujifunza na kutafakari kwa pamoja kuhusu kuzaliwa kwa Yesu Kristo, Ingawa kiini kikuu ni kuzaliwa kwa Yesu Kristo eneo kubwa tunatafakari mioyo mioyo ya watu kadhaa wakati wa kuzaliwa kwa Masihi, tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele viwili vifuatavyo:

 Wise man means a man versed in magic, witchcraft, or astrology
(Mamajusi maana yake ni mtu anayejishughulisha na Uganga, Uchawi na Unajimu)

·         Maana ya CHRISTIMAS
·         Kuzaliwa kwa Masihi na mioyo ya watu

Maana ya CHRISTIMAS

Neno CHRISTMAS ni muungnaniko wa Maneno mawili ya KILATINI CHRIST na MASS ambapo maana zake ni kama ifuatavyo
Christ maana yake KRISTO au MASIHI
Mass Maana yake ni Jumuiya au mjumuiko au Ibada misa au Kuadhimisha
Kwa hiyo neno Christ na Mass yanapounganishwa tunapata neno CHRISTMAS ambalo maana yake ni Kumuadhimisha Kristo, au kumuabudu Kristo au jumuiya ya Kristo, maana muhimu zaidi ni KUMUABUDU KRISTO.

Kuzaliwa kwa mashi na mioyo ya watu.

Ni muhimu kufahamu kuwa leo tunapoadhimisha kuzaliwa kwa Masihi Biblia inatufunulia kuwa wakati Yesu anazaliwa huko Bathelehemu. Mioyo ya watu iligawanyika katika makundi kadhaa ambayo huenda hata leo makundi hayo yakawepo na huenda hata Yesu Kristo atakaporudi tena mara ya pili atayakuta

1.       Mioyo ya walimwengu 

Yohana 1:10-11 Biblia inasema hivi “Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua. Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.” Biblia inapozungumzia ulimwengu inazungumzia mfumo wa kawaida wa uharibifu wa Dunia kiyunani Cosmos ni njamii inayojiendesha bila kujali uwepo wa Mungu, Neno lake wala utawala wake, Ulimwengu siku zote ni mpinzani mkubwa sana wa Historia ya wokovu, kuifuata dunia hii au mfumo wa ulimwengu huu ni kujifanya adui wa Mungu Yakobo 4:4 Biblia inasema hivi “Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.” Biblia inamuagiza kila mtu anayemfuata Yesu Kristo kutokuifuatisha namna ya dunia hii Warumi 12:2Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.” Awaye yote ambaye anaifuatisha namna ya dunia hii yaani mfumo wa ulimwengu huu au kawaida ya ulimwengu huu au kufanya urafiki na dunia au kuipenda ni wazi kuwa mtu huyo yuko nje na kusudi na mpango wa Mungu wa kuokoa, Yesu ni mwokozi na alikuja Duniani ili awaokoe wanadamu lakini awaye yote ambaye hamuanimi ama amesikia habari za Yesu lakini bado anaupenda ulimwengu huu, huyo amemkataa Yesu, 1Yohana 2:15 Msiipende dunia wala mambo yaliyomo katika dunia Mtu akiipenda Dunia , kumpenda Baba hakumo ndani yake” Unaona! Kumbe watu wanaofuata kawaida za ulimwengu huu ni raia wa ulimwengu huu wale wanaomfuata Yesu sio raia wa ulimwengu huu kufuata kawaida ya ulimwengu huu ni dhambi Yesu alipozaliwa alikuta mioyo ya watu ikiwa iko katika kawaida zao za kila siku za kijamii na kisiasa na hakukuwa na mtu aliyeonyesha kujali kama Yesu amezaliwa Luka 2:1-7 Biblia inasema “Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu. Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa hapo Kirenio alipokuwa liwali wa Shamu. Watu wote wakaenda kuandikwa, kila mtu mjini kwao. Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi;  ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba.  Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia,  akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng'ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.”  Wakati Yesu anazaliwa watu wa ulimwengu walikuwa katika sense na agizo la kifalme ili kuandikishwa hakuna mtu aliyekuwa na wazo la kufikiri kuhusu kuzaliwa kwa masihi. Watu wengi leo wamekuwa busy na shughuli zao za kila siku za biashara, kazi kilimo na shughuli nyingine za utafutaji jambo ambalo si baya lakini hawatoi nafasi ya mioyo yao kufatakari mambo ya Mungu au hata kuhudhuria Ibada jambo kama hili lilipelekea Yesu kuzaliwa katika hori ya kulishia Ng’ombe kwani alikosa nafasi kwa walimwengu.

2.       Mioyo ya wanasiasa.

Kundi hili la pili ni kundi la wanasiasa kundi hili nalo wakati Yesu alipokuwa anazaliwa lilishindwa kumpokea, kundi hili katika biblia linawakilishwa na mfalme Herode Mathayo 2:1-7, 12-16 1. “Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, 2. Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia. 3. Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye. 4. Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi? 5. Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii, 6. Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli. 7. Kisha Herode akawaita wale mamajusi faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu ilipoonekana ile nyota.”

“12. Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine. 13. Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize. 14. Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake Misri;

unamuona Herode? Huyu alikuwa ni mtu wa namna gani

  • Alikuwa mtu wa Idumeya na Hakuwa Myhahudi Idumeya ni eneo la Edom watu wa Esau
  • Alikuwa Mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa, warumi walimfanya awe kiongozi kibaraka wa Kaisari na mfalme wa jimbo la Galilaya na  Uyahudi au Yuda
  • Alioa mtoto wa kuhami mkuu
  •  Na ili aweze kukubalika na wayahudi alijenga Hekalu, Hili ndilo Hekalu ambalo yesu alilitumia alipokuwa duniani

Pamoja na hayo yote kama tulivyosoma maadniko na sifa za Herode mwanasiasa huyu hakufurahi aliposikia Yesu amezaliwa, aidha alikusudia kumuua Yesu ingawa ilionekana kama anampenda Mungu wa wayahudi kwa kuwajengea hekalu, lakini moyo wake haukumfurahia Mungu hii ndio tabia ya wanasiasa wanaweza kujenga nyumba za ibada kwa kusudi tu la kuiteka mioyo ya watu kisiasa lakini mioyo yao haiku tayari kumkaribia Mungu wanaweza kuonekana kama wema wanaposalimia salama za kidini lakini wanachokitaka sio Mungu sio Yesu bali wanataka mioyo ya kuwapigia kura kutokana na hali hii neema ya Mungu ilikuwa mbali nah erode na akafa bila kumshuhudia Masihi, aidha alikuwa tayari kumiza na kuua watoto wengi sana kwaajili ya kulinda cheo chake na faida yake ni mara ngapi tumeshuhudia, utu ukitoweka karibu na uchaguzi watu wenye ualbino wakiuawa kama hapa Tanzania kwa kusudi la watu wajinga na washirikiana kujipatia kibali cha kisiasa Bwana aliangalie hili na kulikemea!

3.       Mioyo ya Viongozi wa Kidini

Mathayo 2:1-6 Biblia inasema “1.Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, 2. Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia. 3. Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye. 4. Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi? 5. Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii, 6. Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli.”

Biblia inaeleza kuwa Herode aliposikia habari ya kuzaliwa kwa Masihi kutoka kwa Mamajusi alikusanya Makuhani pamoja na waandishi akatafuta habari kwao Kristo azaliwa wapi, Makuhani ni viongozi wa dini na waandishi walikuwa ni walimu wa torati hawa walikuwa ni watu wenye ujuzi sana kuhusu neno la Mungu na unabii lilikuwa ni kundi la watumishi wa Mungu Mungu anirehemu hapa maana na mimi pia ni kiongozi wa kidini kundi hili linanihusu na maonyo yake pia yananihusu, Kundi hili walipouliszwa swali kuwa Masihi azaliwa wapi ilikuwa rahisi kwao kujibu kutokana na ujuzi wao katika maandiko walitafuta na walimjulisha mfalme kuwa Masihi anazaliwa bethelehemu kama anenavyo nabii bila shaka walinukuu unabii katika Mika 5:2Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.” Unaona watu hawa wa Mungu yaani watumishi walikuwa na ujuzi mkubwa sana kuhusu maandiko, walijua kuwa masihi ni kiongozi mkubwa ambaye matokeo yake yaani asili yake ni tangu milele walitambua kuwa kiongozi huyu mkubwa sana na wa kuheshimika sana Duniani anazaliwa Bethelehemu lakini jambo la kusikitisha viongozi hao wa dini pia mioyo yao ilikuwa mbali na Mungu, hakuna hata mmoja aliyeonyesha shauku ya kutaka kumuona Masihi ambaye walikuwa na taarifa zake kuwa ameshazaliwa na walijua wapi anazaliwa

Ni dhahiri kuwa kuwa na ujuzi wa maandiko hakuwezi kutupa nafasi ya kuwa na uhusiano wa kweli na Yesu Kristo, aidha kuwaelekeza wengine neno hakumaanishi kuwa ndio nafasi ya sisi kukubaliwa na Mungu, kama kwa matendo yetu tutamuabudu Mungu na kumuadhimisha lakini mioyo yetu iko mbali naye tutakataliwa katika ufalme wa Mungu Mathayo 15:7-9Enyi wanafiki ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu akisema watu hawa huniheshimu kwa midomo Ila mioyo yao iko mbali nami, Nao waniabudu Bure wakifundisha mafundisho yakiyo maagizo ya wanadamu Paulo mtume alikuwa muhubiri wa ngazi yajuu sana lakini alijionya Ole wangu mimi nisije nikawahubiri wengine kisha mimi nikawa mtu wa kukataliwa  1Wakoritho 9: 26-2726. Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa;27. bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.” Kumbe uko uwezekano wa wahubiri wengi kukataliwa katika ufalme wa Mungu kutokana na mkao wa mioyo yetu, leo hii wako watumishi wa Mungu wana kesi ziko mahakamani wameshitakiana wakidaiana mali na hawataki kusameheana, yako matumizi mabaya ya sadaka, uzinifu, Mafarakano, choyo uadui ugomvi kusemana vibaya na maswala kedekede ni muhimu kujikumbusha kuwa kuwa na Elimu kubwa za kidini, kutumiwa na Mungu kwa karama mbalimbali kutoa Pepo na na kufanya unabii kamwe sio tiketi ya kutufanya tuingie katika ufalme wa Mungu ni jambo la kustaabisha kuwa viongozi wa dini ndio waliokuwa mstari wa mbele katika kumpinga Yesu Kristo na hata kutafuta namna ya kumuua Mungu unikumbuke na kunisamehe na kamwe usinipite na kuniacha

4.       Mioyo ywa watu Masikini na waliokata tamaa
Ni jambo la Kushangaza kuwa Mungu anawaangalia sana wanyonge masikini na waliokata tamaa wakati dunia haijali na mfumo wa dunia hauwajali watu masikini Mungu aliwapa neema watu duni, walikuwa hawana ujuzi wa maandiko wala hawako karibu na ikulu, na huenda walikuwa wamejikatia tamaa Mungu aliwatuma malaika zake kutoa habari maalumu kwa kundi hili kuwa masihi amezaliwa

Luka 2:8-20 Biblia inasema hivi “8. Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku. 9. Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang'aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu. 10. Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; 11. maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana. 12. Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng'ombe. 13. Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema, 14. Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia. 15. Ikawa, malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya, na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika, alilotujulisha Bwana. 16. Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini. 17. Walipomwona wakatoa habari waliyoambiwa juu ya huyo mtoto. 18. Wote waliosikia wakastaajabu kwa hayo waliyoambiwa na wachungaji. 19.Lakini Mariamu akayaweka maneno hayo yote, akiyafikiri moyoni mwake. 20. Wale wachungaji wakarudi, huku wanamtukuza Mungu na kumsifu kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona, kama walivyoambiwa”. Ni jambo la kushangaza kabisa kuwa malaika aliwaambia wachungaji hao kuwa Leo hii katika mji wa Daudi amezaliwa kwaajili yenu Mwokozi ndiye Kristo Bwana natamani kabisa Mungu angenifanya maalumu kama wachungaji hawa ni watu wanyenyekevu wenye mioyo iliyopondeka hawakuwa na ujuzi wa neno hawakuwa wanasiasa lakini Mungu hakuwanyima vyote aliwapa habari njema na hili likawa kundi la kwanza kwenda Bethelehemu na kujionea kundi hili likatoa habari ya kuzaliwa kwake Yesu kristo na kushangaza watu, hii ndio ilikuwa iwe kazi ya makuhani lakini mioyo yao iliwanyima kumjua masihi mioyo iliyopondeka aidha hawa waliishuhudia kundi la malaika wakiimba kwa furaha na kumtukuza Mungu kuhusu kuzaliwa kwa masihi mwe Mungu ni Mungu wa waliotupwa wanyonge na waliohesabika kuwa si kitu, Mungu huwapinga wajikwezao bali huwapa neema wanyenyekevu.

5.       Mioyo ya watu wenye subira.

Kundi hili linawakilishwa na Simeon na Anna Binti Fanuel Simeon alikuwa mtu Mcha Mungu na nabii alikuwa mwenye haki na alikuwa akisubiri kwa shauku kuzaliwa kwa masihi alikuwa ni mzee mmno lakini Roho Mtakatifu alikuwa amemwambia kuwa hatakufa mpaka amemwona masihi, huyu alikuwa mtu mvumilivu umri wake ulikuwa umekwenda lakini bado alikuwa akiutazamia ukombozi, alipomuona masihi Roho Mtakatifu alimuonyesha wazi habari za Mtoto huyo kule hekaluni na sasa alifurahi na kutoa unabii kuhusu Mateso ya Yesu lakini sasa alikuwa tayari kufa kwa amani kwa vile Mungu alikuwa amemtimizia ahadi, Anna binti Fanuel mjane alikaa ujane miaka 84 aliishi na mume miaka 7 tu alidumu katika maombi mwanamke huyu pia alikuwa nabii yeye naye aliwaeleza wazi wote waliokuwa wakisubiria habari zake na kuwathibitishia kuwa huyu ni masihi
Luka 2 25-38 “ 25. Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. 26. Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. 27. Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria, 28. yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema, 29. Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema; 30. Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako, 31. Uliouweka tayari machoni pa watu wote; 32. Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli. 33. Na babaye na mamaye walikuwa wakiyastaajabia hayo yaliyonenwa juu yake. 34. Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa. 35. Nawe mwenyewe, upanga utaingia moyoni mwako, ili yafunuliwe mawazo ya mioyo mingi. 36. Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake. 37. Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba. 38. Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake.  Ni muhimu kwa kila mmoja wetu kuwa mtu mwenye subira na mwenye uvumilivu huku tukimtazamia masihi bila shaka hatuataibika atakapofunuliwa Bwana wakati wa kuja kwake mara ya pili, watu wa rohoni kama ilivyo kwa Simeon na Anna wataelewa wazi Kristo atakapokuja na halitakuwa fumbo kwao hawa walikuwana mioyo yenye kusubiri

6.       Mioyo ya watu wasiotegemewa.

Kundi hili linawakilishwa na jamii ya Mamajusi hili nimeliita kundi la watu wasiotegemewa kwa vile hawakuwa wanamjua Mungu kabisa, hawakuwa na ujuzi wa neno la Mungu, walitokea nchi ya mbali sana na ndio watu wa kwanza kugundua kuwa Kuna Mfalme mkubwa sana wa Wayahudi amezaliwa na kwa vile wafalme huzaliwa ikulu walisafiri kutoka Ukaldayo au mashariki ya mbali yaani Iraq kwa kuchunguza nyota mpaka wakagundua kuwa masihi amezaliwa,\

Ni muhimu kufahamu kuwa watu hawa walijulikana kama watu wenye Hekima na walikuwa ni watu wenye ujuzi na maswala ya nyota yaani wanajimu walihusika na maswala ya uchawi pia Daniel 2: 2 huko ukaldayo kulipotokea jambo gumu sana wao zamani walikuwa ni watu waliotegemewa kutoa majibu Daniel 2: 2 inasema hiviNdipo mfalme akatoa amri kuwaita waganga, na wachawi, na wasihiri, na Wakaldayo, wapate kumweleza mfalme ndoto zake. Basi wakaingia, wakasimama mbele ya mfalme.” Wakristo wengi na wataalamu wa maandiko hufikiri nkuwa Mamajusi walikuwa watu wazuri na watakatifu Hapana lilikuwa ni kundi la Waganga, wachawi na wasihiri yaani wapiga lamri hawa sasa walikuwa wanajimu kama ilivyokuwa kwa Marehemu Yahaya Husein kwa hapa Afrika mashariki ndio maana hili ni kundi la watu wasiotegemewa Mungu aliruhusu katika ufahamu wao na unajimu wao kuona Nyota iliyomuhusu Masihi na kwa moyo waliokuwa nao walijua kuwa wanapaswa kumsujudia na kumuabudu na cha kushangaza zaidi ni kuwa Mungu alisema nao na kuwaonya wasiende kwa Herode maana anataka kumuua mtoto nao wakarudi kwao kwa njia nyingine 

Mathayo 2:10-12 10. Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno. 11. Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane. 12. Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.”

Ni wazi kuwa kundi hili linawakilisha watu watakaoingia katika Ufalme wa Mungu bila sisi kuwatarajia, Mungu haukumu wala hatazami kama wanadamu watazamavyo, sikun ya hukumu na katika ufalme wa Mungu tunaweza kabisa kushangaa wale tunaowadhani ndio wakawa sio na wale tunawadhani sio wakawa ndiyo, Mioyo iliyopondeka Mungu huiangalia sana , unyonge na kutokujihesabia haki ni wazi kuwa kama  mioyo yetu itafanana na makundi makuu matatu ya awali tunaweza tukajikuta tumekataliwa katika ufalme wa Mungu, ni jukumu letu kuangalia na kujiangalia na kujipima namna tunavyoeneda ni mioyo ya makundi matatuya mwisho ndio ambao waliweza kupata nafasi ya kumuadudu Yesu yani kusheherekea CHRISTMAS jihoji je wewe utaweza kuisherekea siku hii na unaisheherekea katika mkao upi wa Moyo?

Ujumbe. Na Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Rev. Innocent Kamote.

Jumapili, 5 Juni 2016

Ujumbe: Makusudi ya Bwana Hayawezi Kuzuilika!



Ayubu 42:1Ndipo Ayubu akamjibu BWANA na Kusema Najua ya kuwa waweza Kufanya Mambo yote  Na ya makusudi yakohayawezi kuzuilika.”

 Ayubu alielewa Kuwa makusudi ya Mungu hayawezi kuzuilika
 
Watu wengi sana Duniani wanaishi Maisha ya huzuni na kukata tamaa kwa sababu ya kutokuwa na ujuzi wa kutosha kuhusu Mungu na makusudi ya Mungu katika maisha yao, Na huuzunika zaidi wanapopitia katika Magumu, masumbufu na Mateso ya aina mbalimbali wakati mwingine ikiwa ni magonjwa, kuchukiwa na hata kutendewa mambo mabaya au kupatwa na Mabaya, Ni muhimu kufahamu kuwa Mungu katika mambo yoote (Mema au mabaya) anaweza kuyatumia katika kutimiza Mpango wake mwema katika maisha Yetu. 

Warumi 8:28Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema yaani wale walioitwa kwa kusudi lake

Andiko la msingi linatoka katika kitabu cha Ayubu ni kitabu cha kifalsafa kinachojadili dhana kuhusu Mateso kwa wanadamu na Mtazamo wa Mungu, wote tunajua kuwa Ayubu alipatwa na Mateso na mitihani migumu ya kupita kawaida, Muda Hautoshi kuangalia ni hasara gani na mateso gani aliyapitia, lakini wote tunajua kuwa Ayubu hakutenda dhambi, na hata kama angetenda Mungu ni wa rehema na hawezi kutulipa mabaya kwa sababu ya ubaya wetu, Rafiki za Ayubu walimlaumu Ayubu na kumtetea Mungu walionyesha wazi kuwa haiwezekani Mateso hayo yampate Ayubu kama Ayubu hakuwa na Makosa, aidha Ayubu alijitetea sana kuwa hakuna makosa aliyoyafanya, Ayubu ingawa hakufanya dhambi lakini alimlaumu Mungu katika kiwango cha kufikia kuonyesha Kiburi na kuonyesha kuwa Mungu hayuko sawa, ni kama alikuwa akimhoji Mungu kwa nini niyapitia haya
Kutokana na majibu ya Mungu kwa Ayubu hatimaye Ayubu alitambua

1.      Mungu huruhusu mambo yote yatupate kwa makusudi yake mema
2.      Kila jambo ambalo Mungu uliruhusu litokee katika maisha yetu katika hekima yake Mungu huruhusu kwa makusudi
3.      Hata mateso ya Mwanadamu na mapito magumu yana maana katika kusudi la Mungu

Kwa sababu hiyo basi ni muhimu kwetu kuamini kuwa Mungu anaweza kufanya mambo yote, Kuamini kuwa kama tunatembea katika Makusudi ya Mungu basi hakuna cha kutuzuia, wala mtu wa kuzuia kusudi la Mungu kwetu katika maisha yetu.

Ni muhimu kwetu tu kutambua makusudi ya Mungu katika maisha yetu, na kutambua kuwa hakuna jambo linalotokea kwa Bahati mbaya “Socrates alisema maisha yasiyotafakariwa Hayafai kuyaishi” mimi nasema “Kuishi maisha yasiyo na kusudi nikupoteza mwelekeo” Mungu ametuumba kwa Makusudi na ni lazima makusudi hayo yatimizwe.

Mungu akikusudia Jambo katika maisha yako hakuna anyeweza Kulibatilisha

Mungu huyabatilisha Mashauri ya watu waovu Dhidi yako

Yusufu alipewa Ndoto yale yalikuwa ni Makusudi ya Bwana katika maisha yake hata hivyo alipitia changamoto za aina mbali mbali, tunapopitia hayo ni muhimu kutambua kuwa Kusudi la Mungu haliwezi kubatilika.

Daudi alipakwa mafuta kwa kusudi la Kuwasaidia Israel kama Mfalme, Sauli alitaka kumuua mara kadhaa alimtupia mkuki ili kuharibu kusudi na mpango wa Mungu lakini hatimaye Daudi alimiliki na kutawala

Musa alikuwa auawe katika mpango mbaya wa mfalme wa Misri aliyeamuru watoto wa kiume wauawe, Mungu katika hekima yake alimfanya Musa huyohuyo alelewe ikulu na kuwa salama zaidi
Kiko mifano mingi inayothibitisha kuwa Makusudi ya Mungu hayawezi kuzuilika, Adui zetu wanapotufikiria mabaya Mungu hutufikiria mema au kutumia ubaya wao kutuletea mambo mema.

Zaburi 33:10-11“Bwana huyabatilisha Mashauri ya mataifa, Huyatungua makusudi ya watu, Shauri la Bwana lasimama milele. Makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi”

Mithali 21:30 - 31 “Hapana Hekima wala ufahamu, wala shauri juu ya Bwana, farasi huwekwa tayari kwa siku ya vita Lakini bwana ndiye aletaye wokovu” 

Isaya 8:10 “ Fanyeni Shauri pamoja nalo litabatilika, Semeni neno, Lakini halitasimama kwa maana Mungu yu pamoja nasi”

Mungu akikusudia hakuna anayeweza kubatilisha
 
Isaya 14:27 “Maana Bwana wa majeshi amekusudia, naye ni nani atakayelibatili? Na Mkono wake uliionyooshwa ni nani atakayegeuza nyuma?

Hata wanadamu wafanye hila bado kusudi la Mungu ndio litakalo simama
 
Mithali 19:21 “Mna hila nyingi moyoni mwa mtu, Lakini Shauri la Bwana ndilo Litakalosimama”

Paulo Mtume alikuwa amekusudia kuuona na Rumi pia
Warumi 1:15 “Kwa hiyo kwa Upande wangu mimi ni tayari kuihubiri injili hata na kwenu ninyi mnaokaa Rumi” 

Lakini Wayahudi walikusudia kwa kila namna kuharibu mpango na makusudi ya Paulo, walitaka kumuua kabla hajafika Rumi Angalia
 
Matendo 23:12-15 “Kulipopambauka,Wayahudi wakafanya mapatano, wakajifunga kwa kiapo kwamba hawatakula wala hawatakunywa hata wamwue Paulo.  Na hao walioapiana hivyo walipata zaidi ya watu arobaini. Nao wakaenda kwa wakuu wa makuhani na wazee, wakasema, Tumejifunga kwa kiapo tusionje kitu hata tumwue Paulo. Basi sasa ninyi pamoja na wazee wa baraza mwambieni jemadari amlete chini kwenu, kana kwamba mnataka kujua habari zake vizuri zaidi; na sisi tu tayari kumwua kabla hajakaribia.  
        
Angalia je hila zao zilifanikiwa?
Matendo 23: 11 “.Usiku ule Bwana akasimama karibu naye, akasema, Uwe na moyo mkuu; kwa sababu, kama ulivyonishuhudia habari zangu Yerusalemu, imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo Rumi nako.”

Ni muhimu kufahamu kuwa kama unatembea katika kusudi la Mungu basi hakuna anayeweza kuzuia kusudi hilo na kamwe hupaswi kukata tamaa unapoona mambo magumu, vikwazo na hila za ibilisi na mipango ya kukukatisha tamaa hila na matendo mabaya ya watu dhidi ya ndoto zako hakuna muda wa kumlaumu mtu au kutafuta mchawi ni nani, jambo moja unalopaswa kulitambua ni kuwa “Makusidi ya Mungu hayawezi kuzuilika” Mungu amekupa nguvu na mamlaka ya kubatilisha hata Mashauri ya Adui zako hata kama mashauri hayo yanaonekana kana kwamba yanatoka kwa Mungu angalia.

 2Samuel 16:23, Na shauri lake Ahithofeli alilokuwa akilitoa siku zile lilikuwa kama mtu aulizapo kwa neno la Mungu, Ndivyo yalivyokuwa mashauri yake Ahithofeli kwa Daudi na Kwa Absalom”

Daudi alitambua kuwa Ahithofeli alikuwa mtu mashuhuri kwa Ushauri na ushauri wake ilikuwa kama kuuliza kwa Mungu na Ahithofeli  alipokuwa ameasi kwa Daudi Dua za daudi kwa Mungu ilikuwa ni kuilaani karama ya ushauri ya Ahithofeli na kuibatilisha 

2Samuel 15:31 “Mtu mmoja akamwambia Daudi ya Kwamba Ahithofeli yu katika hao walioambatana na Absalom, Daudi akasema Ee Bwana nakusihi Uligeuze Shauri la Ahithofeli liwe Batili”

Ni muhimu kwa kila mmoja wetu kumsihi Mungu ili mashauri mabaya yanayotolewa dhidi yatu yaweze kuwa Batili, mawazo mabaya yanayotolewa dhidi yetu yabatilike maneno mabaya yanayotolewa dhidi yako yabatilike Bwana na abatilishe manuizo yote ya wachawi na laana zote na kila mpango ambao sio makusudi ya Bwana dhidi ya maisha yetu katika Jina la Yesu Amen.

Ujumbe na Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote.

Ijumaa, 27 Mei 2016

Mwaka wa Bwana Uliokubaliwa!


Luka 4:18-22
18. Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, 19. Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. 20. Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. 21. Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu. 22. Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake, wakasema, Huyu siye mwana wa Yusufu?

Moja ya maswala ya msingi namambo muhimu tunayopaswa kuyafahamu ni pamoja na kufahamu maneno haya ya neema kubwa yaliyopata kutamkwa na Bwana wetu Yesu Kristo, ni Maneno ambayo hata wale waliyoyasikia waliyastaajabia maneno hayo ni “KUTANGAZA MWAKA WA BWANA ULIOKUBALIWA”

Ni muhimu kwetu kufahamu ni nini maana ya Mwaka wa Bwana uliokubaliwa? Katika kiingereza maneno hayo husomeka hivi  To proclaim the Year of Lords Favour” Neno Favour katika Biblia ya Kiyunani yaani Greek linasomeka “Dektos”  ambalo maana yake ni Kukubalika au “Neema” 

Kwa kawaida Mungu aliwaamuru wana wa Israel kuadhimisha sikukuu iliyoitwa Mwaka wa Bwana wa Neema kila Baada ya miaka 49 mwaka wa 50 Uliitwa mwaka wa Neema au mwaka wa Bwana uliokubaliwa mwaka huu ulikuwa maalumu na ulikuwa na mafundisho makuu manne yafuatayo
1.      Ulikuwa ni mwaka wa kupuliza tarumbeta yaani mwaka wa kuukaribia mlima au uwepo wa Mungu 



Kutoka 19:10-13 Biblia inasema hivi;-

10. BWANA akamwambia Musa, Enenda kwa watu hawa, ukawatakase leo na kesho, wakazifue nguo zao, 11. wawe tayari kwa siku ya tatu; maana siku ya tatu BWANA atashuka katika mlima wa Sinai machoni pa watu hawa wote. 12. Nawe utawawekea mipaka watu hawa pande zote, ukisema, Jihadharini, msipande mlima huu, wala msiuguse, hata mapambizo yake; kila mtu atakayeugusa mlima huu, bila shaka atauawa. 13. Mkono wa mtu awaye yote usimguse mtu huyo, ila hakika yake atapigwa kwa mawe, au kupigwa kwa mkuki; kwamba ni mnyama au kwamba ni mwanadamu, hataishi. Hapo panda itakapotoa sauti kwa kufuliza ndipo watakapoukaribia mlima.

Ilikuwa ni vigumu na ni hukumu ya kifo kuukaribia uwepo wa Mungu, lakini ilipopigwa tarumbeta au panda ndipo watu waliporuhusiwa kuukaribia uwepo wa Bwana, hivyo mwaka wa Bwana unazungumzia kukaribishwa uweponi mwake

2.       Ulikuwa ni mwaka wa KISABATO yaani mwaka wa MAPUMZIKO Walawi 25:8-17 Biblia inasema hivi: - 

8. Nawe utajihesabia Sabato saba za miaka, maana, miaka saba mara saba; zitakuwa ni siku za Sabato saba za miaka kwenu, maana miaka arobaini na kenda. 9. Ndipo utakapoipeleka pande zote hiyo baragumu yenye sauti kuu, siku ya kumi ya mwezi wa saba; katika siku hiyo ya upatanisho mtaipeleka baragumu katika nchi yenu yote. 10. Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kupiga mbiu ya kuachwa mahuru katika nchi yote kwa watu wote wanayokaa; itakuwa ni yubile kwenu, nanyi kila mtu atairudia milki yake mwenyewe, nanyi mtarejea kila mtu kwa jamaa yake.11. Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni yubile kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu za mizabibu isiyopelewa. 12. Kwa kuwa ni yubile; utakuwa mwaka mtakatifu kwenu; mtakula maongeo yake yatokayo shambani. 13. Mwaka huo wa yubile mtairudia kila mtu milki yake. 14. Tena kama ukimwuzia jirani yako cho chote, au kununua cho chote mkononi mwa jirani yako, msidanganyane wenyewe kwa wenyewe; 15. kwa hesabu ya miaka iliyo baada ya yubile, ndivyo utakavyonunua kwa jirani yako, na kama hesabu ya miaka ya mavuno ndivyo atakavyokuuzia wewe. 16. Kama hesabu ya miaka ilivyo ni nyingi ndivyo utakavyoongeza bei yake, na kama hesabu ya miaka ilivyo ni chache ndivyo utakavyopunguza bei yake; kwani yeye akuuzia mavuno kama hesabu yake ilivyo. 17. Wala msidanganyane; lakini utamcha Mungu wako; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

Mungu alikuwa anataka watu wake wastarehe wapumzike wafurahi Jubilei, kwa hiyo ulikuwa ni wakati wa Kustarehe na kuburudika na kupumzika na kurudishiwa milki ya nkila ulichopoteza

3.       Ulikuwa ni Mwaka wa Kuachia Ardhi (25-38)

25. Kwamba nduguyo amekuwa maskini, na kuuza sehemu ya milki yake, ndipo jamaa yake aliye karibu naye atakuja, naye ataikomboa ile aliyoiuza nduguye. 26. Na kama mtu hana atakayeikomboa, naye mwenyewe amepata mali na kujiona kuwa anayo ya kutosha kuikomboa; 27. ndipo na aihesabu hiyo miaka ya kuuzwa kwake, na kilichozidi kumrudishia huyo mtu aliyeinunua; naye atairejea milki yake. 28. Lakini asipoweza kujipatia mwenyewe, ndipo hiyo iliyouzwa itakaa mkononi mwake huyo aliyeinunua, hata mwaka wa yubile; na katika yubile itatoka, naye atairejea milki yake. 29. Tena kwamba mtu anauza nyumba ya kukaa, iliyo ndani ya mji wenye kuta, ndipo ana ruhusa kuikomboa katika mwaka mmoja mzima baada ya kuiuza; atakuwa na amri ya kuikomboa muda wa mwaka mzima. 30. Na kama haikukombolewa katika muda wa mwaka mzima, ndipo hiyo nyumba iliyo ndani ya mji wenye kuta itathibitishwa milele kuwa ya huyo aliyeinunua, katika vizazi vyake; nayo haitatoka katika yubile. 31.Lakini nyumba za vijiji, ambavyo havikuzingirwa na kuta, zitahesabiwa pamoja na mashamba ya nchi; nazo zina ruhusa ya kukombolewa, nazo zitatoka katika yubile. 32. Pamoja na hayo, miji ya Walawi, nyumba za miji ya milki yao, Walawi wana ruhusa ya kuzikomboa majira yo yote. 33. Tena kama mtu mmoja wa hao Walawi akikomboa, ndipo nyumba iliyouzwa, na mji wa milki yake, itatoka katika yubile; maana, hizo nyumba za miji ya Walawi ni milki yao kati ya wana wa Israeli. 34. Lakini konde la malisho ya miji yao lisiuzwe kwa kuwa ni milki yao ya daima. 35. Na ikiwa ndugu yako amekuwa maskini, na mkono wake umelegea kwako, ndipo utamsaidia, atakaa nawe kama mgeni, na msafiri. 36. Usitake riba kwake wala faida, bali mche Mungu wako, ili ndugu yako akae nawe. 37. Usimpe fedha yako upate riba, wala usimpe vyakula vyako kwa kujitakia faida. 38. Mimi ndimi BWANA, Mungu wako, niliyewatoa katika nchi ya Misri ili niwape nchi ya Kanaani, nipate kuwa Mungu wenu.”

4.       Ulikuwa ni Mwaka wa kuwaachia watumwa uhuru na kila mtu kurejea nyumbani kwao (39-55)

39. Tena kwamba nduguyo amekuwa maskini pamoja nawe, akajiuza kwako; usimtumikishe mfano wa mtumwa; 40. kwako wewe atakuwa mfano wa mtumishi aliyeajiriwa, au mfano wa msafiri; naye atatumika kwako hata mwaka wa yubile;   41. ndipo atakapotoka kwako aende zake, yeye na wanawe pamoja naye, naye atairejea jamaa yake mwenyewe, tena atairejea milki ya baba zake. 42. Kwa kuwa hao ni watumishi wangu, niliowaleta watoke nchi ya Misri; wasiuzwe mfano wa watumwa. 43. Usitawale juu yake kwa nguvu; ila umche Mungu wako. 44. Tena katika habari za watumwa wako na wajakazi wako, utakaokuwa nao; mataifa walio kando-kando yenu, katika hao mtanunua watumwa na wajakazi. 45. Tena katika wana wa wageni wakaao kati yenu mtajinunulia, na katika jamaa zao walio pamoja nanyi, waliowazaa katika nchi yenu; wao watakuwa milki yenu. 46. Nanyi mtawafanya kuwa urithi kwa watoto wenu baada yenu, wawe milki yao; siku zote mtatwaa watumwa wenu katika hao; lakini msitawale kwa nguvu juu ya ndugu zenu, hao wana wa Israeli, wenyewe kwa wenyewe. 47. Tena kama mgeni au mtu akaaye nawe akitajirika, na nduguyo amekuwa maskini karibu naye, akajiuza kwa huyo mgeni, au kwa huyo akaaye kwako, au kwa ukoo wa jamaa ya huyo mgeni; 48. baada ya kuuzwa aweza kukombolewa; mtu mmoja miongoni mwa ndugu zake ana ruhusa kumkomboa;   49. au mjomba wake, au mwana wa mjomba wake, ana ruhusa ya kumkomboa, au mtu awaye yote aliye karibu naye wa jamaa yake, ana ruhusa ya kumkomboa; au kwamba yeye mwenyewe amepata mali, ana ruhusa ya kujikomboa mwenyewe.    50. Naye atafanya hesabu na huyo aliyemnunua, tangu mwaka huo aliojiuza hata mwaka wa yubile; na ile bei ya kuuzwa kwake itakuwa kama hesabu ya hiyo miaka ilivyo; atakuwa pamoja naye kama majira ya mtumishi aliyeajiriwa yalivyo. 51. Kwamba ikali imesalia miaka mingi, kama hesabu yake ilivyo ndivyo atakavyolipa bei ya ukombozi wake, katika hiyo fedha ambayo alinunuliwa kwayo. 52. Tena kwamba imesalia miaka michache tu hata mwaka wa yubile, ndipo atafanya hesabu naye, kama hesabu ya miaka yake ilivyo, ndivyo atakavyolipa tena bei ya ukombozi wake. 53. Kama mtumishi aliyeajiriwa mwaka hata mwaka, ndivyo atakavyokuwa pamoja naye; asitawale juu yake kwa nguvu mbele ya macho yako. 54. Tena kwamba hakukombolewa kwa njia hizi mojawapo, ndipo atatoka katika mwaka wa yubile, yeye, na watoto wake pamoja naye. 55. Kwa kuwa wana wa Israeli ni watumishi; ni watumishi wangu niliowaleta watoke katika nchi ya Misri; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

Kimsingi katika agano jipya pia Yesu alipoutangaza alitangaza wakati wa neema ambapo kila alichokisema Yesu, kilikuwa ni lazima kifanyike , watu wengi katika Israel walijua kuwa mwaka huo kinabii ulikuwa unahusu ujio wa Masihi na kuwa mwenye uwezo na mamlaka ya kuutangaza mwaka huo wa Neema alikuwa ni Masihi peke yake ulikuwa ni mwaka uliokuwa ukisubiriwa ilistaajabisha sana Yesu laliposoma andiko na kutoa hutuba ya maneno sita tu “LEO MAANDIKO HAYA YAMETIMIA MASIKIONI MWENU”

Ni wazi kuwa Masihi Yesu alikuwa ametangaza maneno ya neema kubwa sana  kwamba kuanzia wakati ule hata sasa tunaishi ndani ya kipindi cha neema na ni mwaka wa Bwana ni mwaka ya Jubilei Kristo alitangza wazi kuwa ni mwaka wa 

Ø  Kukomesha kila aina ya uonevu
Ø  Kuweka huru waliosetwa na kukandamizwa na shetani
Ø  Kutangaza kuwa kila mtu anaweza kuukaribia uwepo wa Mungu bila kuuawa
Ø  Amekuja kupumzisha watu wenye mizigo na wenye kuelemewa na matatizo mbalimbali
Ø  Amekuja kuweka huru wafungwa wote wa vifungo mbalimbali

Shetani anafahamu wazi kuwa Tarumbeta imekwisha kupulizwa na kuwa anapaswa kumuachia huru kila mmoja name nakutangazia msomaji wangu Bwana akuweke huru na kukutoa katika vifungo mbalimbali na kila aina ya uonevu wa Ibilisi

Huu ni mwaka wa Bwana uliokubalika, kila kifungu na kikuachie, Roho amanitia mafuta nikutangazie uhuru uwe Huru sasa katika Jina la Yesu Kristo, Ufunguliwe, kutoka katika vifungo vya nguvu za giza, uonevu wa Ibilisi, Biashara zisitawi, upandishwe cheo, waliokufunga wadhoofike na kukuachia huru, kila kifungo nakiharibu na kukivinja katika jina la yesu Kristo aliye hai Achiaaaaaaaaa haraka  Achia wasomaji wangu huna mamlaka ya kuwatesa nina waweka huru kwa kupakwa mafuta navunja nira zote Katika Jina la yesu Kristo, Pepo majini  na mashetani huna nafasi ya kumtesa msomaji wangu mwachie sasa hivi katika jina la Yesu Uko huru sema amen kwa imani 

Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote.