Alhamisi, 23 Juni 2016

Watu wa Kizazi Hiki!



Mstari wa Msingi: Luka 7: 29 – 35.
 
Biblia inasema :-  29. Na watu wote na watoza ushuru waliposikia hayo, waliikiri haki ya Mungu, kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohana. 30. Lakini, Mafarisayo na wana-sheria walilipinga shauri la Mungu juu yao, kwa kuwa hawakubatizwa naye. 31. Bwana akasema, Niwafananishe na nini watu wa kizazi hiki? Nao wamefanana na nini? 32. Wamefanana na watoto walioketi sokoni na kuitana, wakisema, Tuliwapigia filimbi wala hamkucheza; tuliomboleza, wala hamkulia. 33. Kwa kuwa Yohana Mbatizaji alikuja, hali mkate wala hanywi divai, nanyi mwasema, Ana pepo. 34. Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa; nanyi mwasema, Tazama, mlafi huyu, na mnywaji wa divai, rafiki wao watoza ushuru na wenye dhambi. 35. Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa watoto wake wote”.
 
Katika kifungu hiki cha maandiko kuna maswala ya msingi sana ya kujifunza, kuhusiana na watu wa kizazi cha leo ambao hawatofautiani sana na Kizazi cha wakati wa Yesu na Yohana Mbatizaji walipokuwa Duniani.

Kifungu kinaonyesha kuwa:-

·         Watu wote walilisikia neno la Mungu yaani Shauri la Mungu na kusudi lake, waliosikia shauri la Mungu walikuwa watu wabaya, wenye dhambi,  watoza ushuru nk, lakini pia Mafarisayo na waandishi (waandishi wanaitwa Lawyers au an Expertise of the law of Moses) yaani wataalamu wa Sheria na Torati ya Musa wote walisikia ujumbe wa Mungu kupitia Yohana na baadaye Yesu

·         Wote walisikia Unabii na walifahamu sana habari za Zakaria aliyemzaa Yohana na Yohana mwenyewe walitambua kuwa walikuwa watu wa namna gani

·         Lakini jambo la kushangaza ni kuwa  Mafarisayo na waandishi walikataa ujumbe wa Yohana mbatizaji na zaidi ya yote walikataa pia ujumbe wa Yesu Kristo, hawakukubali kutii Ushauri wa Mungu, Hata pamoja na Mungu kutumia njia mbalimbali na mitindo mbalimbali ili waelewe kusudi lake

·         Kilikuwa ni kizazi ambacho huwezi kukifurahisha kwa namna yoyote, ukiwajia kwa shangwe na filimbi HAWACHEZI, sawa Ukiwajia kwa Maombolezo HAWALII, Yesu alikuwa anaonyesha ni Jinsi gani anawathamini sana na wanadamu na anataka kwa namna yoyote ile wamgeukie yeye na kufuata njia zake Lakini Yesu anaonyesha wazi kuwa ni vigumu sana Kumpendeza Mwanadamu kwa sababu Mungu mwenyewe walimkataa hata pamoja na kuwajia kwa njia mbalimbali.

Katika Nchi Yetu pia tunaweza kushuhudia maswala yanayofanana na hayo, Rais aliyepita alikuwa mpole, na alikuwa anasafiri sana kwenda nje, na hakuweza kuwashughulikia wabadhirifu, watu walipiga kelele sana , akaja rais ambaye ni mkali na ameanza kuwashughulikia mafisadi waziwazi, wakasema he is self appointed Judge, Hasafiri wakasema rais gani hasafiri, wekea wanafunzi Pilau kila siku na nyama kila siku watasema tumechoshwana nyaka kila siku, weka Pelege watasema zina minyoo, wapige maharage watasema kila siku maharage, weka Kade watasema makande tu, ondoa watasema tumeyamisi makande, Ni kawaida ya wanadamu kutokucheza mziki wowote ule iwe “Ragge”r au “Blues”

Maandiko yanatushauri kuwa tusikatae mashauri ya Mungu ziko sababu za msingi kwanini tuukubali Ushauri wa Mungu.

1.       Mwanadamu hawezi kujiongoza Mwenyewe Yeremia 10:23
2.       Mwanadamu akijiongoza mwenyewe mwisho wake ni mauti Mithali 14:12
3.       Nje ya Mungu Hakuna njia Nyingine Yohana 6:68
4.       Watu wakimkataa Mungu Mungu huwacha wafuate njia zao zilizopotoka na hatimaye ataleta hukumu  Warumi 1:28.

 Watu wa Kizazi Hiki
5.       Mwisho ni hekima ya Mungu tu ndiyo itakayoshinda na shauri la Mungu litadumu na kujulikana kuwa la haki. Luka 7:35

Mwisho ni muhimu kufuata Mashauri ya Mungu na kusimama nayo kabla hatujachelewa
Rais wa Marekani John F Kennedy alisem:-

~“The time to repair the roof is when the sun is shining.”~

Tafasiri yangu isiyo rasmi
 
~“Muda wa kukarabati paa ni wakati jua linawaka”~
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote

Hakuna maoni: