Waebrania 12:5-11 “tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na
wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana,
Wala usizimie moyo ukikemewa naye; Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye. Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi
asiyerudiwa na babaye? Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu
ninyi, wala si wana wa halali. Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili
walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali
sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi? Maana ni hakika, hao kwa
siku chache waliturudi kama walivyoona vema
wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake. Kila adhabu
wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye
huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.”
“Kila mmoja anapaswa kuchagua njia mojawapo kati ya mbili,
maumivu ya Nidhamu au maumivu ya Majuto” – John
Rohn
Utangulizi.
Ni muhimu kwa kila mmoja wetu
kufahamu kwamba maisha yetu hayawezi kuwa na wingi wa furaha na amani na hata mafanikio kama tutasahau kuishi kwa
Nidhamu, ni ukweli ulio wazi kwamba Nidhamu ndio njia sahihi ya maisha, Nidhamu
haina mipaka kila mtu anapaswa kuishi kwa nidhamu, Nidhamu haina mwenye pesa,
au asiye na pesa, mwenye utajiri au asiye tajiri, swala la nidhamu
linategemeana na jinsi mtu alivyofunzwa na anavyokubali kujifunza, Nidhamu ni
tabia na haipatikani kwa kurithi, kwa msingi huo kila mmoja anaweza kujifunza
kuishi kwa nidhamu na akafanikiwa katika maisha, wengi wa watu wenye mafanikio
ya kiroho na kimwili, na maswala mengineyo yote ni wale waliofanikiwa kuishi na
kuenenda kwa Nidhamu. Tunahitaji Nidhamu ili kuyafikia maono, tunahitaji
nidhamu ili kutunza utajiri, tunahitaji nidhamu ili kuepuka matatizo,mtu akiwa
na nidhamu ni kama ana stadi ya maisha iliyo ya juu zaidi, watu wanaofanya kazi
kwa bidii na wenye vipawa vikubwa hawawezi kuwa na mafanikio makubwa kama
hawatakuwa na nidhamu, yaani huwezi kuzungumzia huduma, maisha, kazi, kusoma,
mtindo wa maisha, ubora wa shule au taasisi au chuo, au taifa, au michezo, au
jeshi kama katika kila secta watu hawatakuwa wamejifunza kuishi kwa nidhamu.
“We don’t have to be smarter than the rest, we have to be more
Displined than the rest” warren Buffet
“Hatuhitaji kuwa bora kuliko wengine, tunahitaji kuwa na Nidhamu
kuliko wote” Warren Buffet
“Everyone must choose one of two pain, the pain of Displine or the
pain of regret” John Rohn
“Kila mmoja anapaswa kuchagua njia mojawapo kati ya mbili, maumivu ya
Nidhamu au maumivu ya Majuto” – John Rohn
“He who lives without discipline dies without
HONOR”
“Wanaoishi bila Nidhamu huwa wanakufa bila
heshima”
Nidhamu inahitajika katika kila Nyanja, huwezi
kuwa mwalimu Mzuri kama huna nidhamu, huwezi kuwa Dereva mzuri kama huna
nidhamu, huwezi kuwa Mchungaji Mzuri kama huna nidhamu, huwezi kuwa daktari
mzuri kama huna nidhamu, huwezi kuwa mwana siasa mzuri kama huna nidhamu,
huwezi kuwa bondia mzuri kama huna nidhamu, huwezi kuwa mchezaji mpira mzuri
kama huna nidhamu, nidhamu ni maisha kula, kuvaa, na hata kuishi ni nidhamu
nidhamu ndio kila kitu, kuomba ni nidhamu, kufunga ni nidhamu kila kitu
kinahitaji nidhamu
“Kama kuna somo kubwa ambalo ningependa Dunia
nzima ijifunze jibu langu lingekuwa ni rahisi Nidhamu tu” – Rev. Kamote
“If there is a great subject that I would like
the world to learn my answer could be simple Discipline”
Nidhamu ndio somo kuu na la kwanza ambalo
wazazi walitufundisha Nyumbani, na walimu wanalikazia shuleni, na wakristo
wameagizwa kulihubiri, Jamii yoyote ile ambayo unaweza kusema kuwa haijaelimika
basi ni jamii wa watu wasio na nidhamu – Rev. Innocent Kamote
Maana ya neno Nidhamu.
Neno nidhamu maana yake ni mfumo
wa kuwafunza watu, ili wawe watii, au wawe wenye tabia njema na mwenendo Mzuri,
Ni malezi au makuzi yenye kuzingatia,
Maonyo, Sheria, Taratibu,mamlaka, uthabiti, weledi, uthibiti, Heshima,
mwelekeo, wajibu, utii, kiasi na kujiongoza na kushikisha adabu kwa ujumla wake
kuwa na Nidhamu.
Neno nidhamu pia linaweza
kutumika kuelezea mafunzo maalumu yenye kumfanya mtu awe mtii kwa sheria tabia
na mwenendo na kurekebishika pale inapohitajika, ni mafunzo, Mafundisho, Shule,
kocha, elimisha, na hekimisha, na kumfanya mtu awe na uwezo wa kujidhibiti
yaani “self control” au Marudia au
nidhamu kwa kiingereza Displine. Kushikisha
adabu au kunadhimisha na kutoa maonyo au adhabu ili kumrekebisha mtu kwa lengo
la kumfanya awe thabiti. Kwa kiibrania kuna maneno mawili yanayotumika
kumaanisha Nidhamu 1 ni “YASAR” (NIDHAMU
AU KUADHIBIWA) NA “YAKACH” (MAONYO) yametumika maneno hayo katika Mithali 3:11 “Mwanangu
usidharau Kuadhibiwa na Bwana wala usione taabu kurudiwa naye”
Biblia
katika Waebrania 12:5-11 inatuasa
kwamba tumeyasahau yale maonyo ni maonyo gani haya ambayo Biblia inatuasa
kutokuacha kuyasahahu? Ni swala la Nidhamu au Marudia Biblia ya kiingereza
inasema hivi katika fungu hilo la maandiko
“5 And have you completely forgotten this word of encouragement
that addresses you as a father addresses his son? It says,
“My son, do not make light of the Lord’s discipline,
and do not lose heart when he rebukes you,
6 because the Lord disciplines the one he loves,
and he chastens everyone he accepts as his son.”[a]
and do not lose heart when he rebukes you,
6 because the Lord disciplines the one he loves,
and he chastens everyone he accepts as his son.”[a]
7 Endure hardship as discipline; God is treating you as his
children. For what children are not disciplined
by their father? 8 If
you are not disciplined—and everyone undergoes discipline—then you are not legitimate, not true sons and daughters at
all. 9 Moreover,
we have all had human fathers who disciplined us and we respected them for
it. How much more should we submit to the Father of spirits and live! 10 They disciplined us for a little while as they
thought best; but God disciplines us for our
good, in order that we may share in his holiness. 11 No discipline seems pleasant at the time, but
painful. Later on, however, it produces a harvest of righteousness and peace
for those who have been trained by it.
Katika kifungu hiki utaweza kuona neno Marudia yaani Nidhamu
katika Biblia ya Kiswahili SUV
limetajwa mara saba (7) na katika Biblia ya kiingereza limetajwa mara kumi
(10), Kama katika kifungu hiki tungeambiwa tutafute neno kuu yaani “key word” basi ni wazi kuwa neno kuu ni
“Descipline” na “Marudia” isipokuwa mimi ningependa
zaidi kutumia neno Nidhamu, au Maonyo Neno hili ni neno la Muhimu sana
sana na ni neno la kutia moyo ambalo kanisa halipaswi kulisahau kamwe Nidhamu,
Nidhamu Nidhamu.
Umuhimu wa kutokuyasahau yale Maonyo (Nidhamu).
Biblia inahitimisha katika
kifungu hiki kwamba wakati tunafundishwa nidhamu au tunazoezwa nidhamu haionekani
kuwa ni jambo lenye kufurahisha sana lakini ukiisha kuzoezwa nayo inaleta faida
yaani matunda ya haki na amani, Ni kama maandiko yanataka kutuambia kuwa kuna
faida kubwa sana kwa mtu aliyejifunza kukaa katika nidhamu, kuzingatia yale
maonyo, ziko faida nyingi sana za kujitia nidhamu ambazo zinajibu swali kwa
nini nidhamu ni Muhimu Waebrania 12:11
“Kila adhabu
wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye
huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani”
1. Nidhamu itakupa kufikia malengo :-
Kama mtu awaye yote ana ndoto ya
aina yoyote na anakusudia kuifikia ni lazima awe na nidhamu, Ushuhuda wa
kidunia unaonyesha kuwa watu wote waliofanikiwa katika kila Nyanja na hata
kutimiza malengo yao katika maisha na kupata mafanikio makubwa walikuwa ni watu
waliojifunza kukaa katika nidhamu, Nidhamu inatusaidia kufaulu masomo, kumaliza
shule salama, kumaliza jeshi salama, kukaa katika kazi zetu salama, kufanya
kazi zetu vema na kufikia malengo vizuri, Mtu awaye yote mwenye makusudi na
mpango mwema atatulia na kufanya kazi kwa bidii kila siku ili kuyafikia
malengo, ni nidhamu pekee inayoweza kumfikisha mtu kule anakokusudia, kinyume
na nidhamu ni vigumu sana kwa mtu kuyafikia malengo, Biblia inaonyesha kuwa
wana michezo wote huwa na tabia ya kujitia nidhamu ili kwamba waweze kushinda
na kupata taji ya kile wanachokikusudia, mwanamichezo yoyote ambaye hana
nidhamu au mwanjeshi yeyote ambaye hana nidhamu atapoteza malengo, Ubora wa
mwanamichezo yoyote bila kujali kipawa alichonacho kama hana nidhamu, kuna
uwezekano mkubwa sana wa kupoteza malengo au kutokuyafikia malengo
1Wakoritho
9:25-27 “Na
kila ashindanaye katika michezo HUJIZUIA KATIKA YOTE; (Maana yake hujitia
nidhamu). basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi
tupokee taji isiyoharibika. Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye;
napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa; bali nautesa mwili wangu na
kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa
kukataliwa.”
Napenda Biblia ya Kiingereza
inavyosema hapa “Everyone who competes in the games goes into strict training”
unaweza kuona neno “STRICT TRAINING”
Ni wazi kuwa Paulo mtume hapo
anazungumzia uhusiano wa kujitia nidhamu kwa wana michezo ili waweze kuwa
washindi, na kwamba hata wale wanaotaka kwenda mbinguni hawana budi kujitiisha
kujifunza kuishi kwa nidhamu ni nidhamu pekee itakayoweza kutusaidia kutoka na
kufanikiwa. Ni watu wenye kujitia nidhamu tu watakaoweza kufika Mbinguni, ni
wahubiri wanaojitia nidhamu ambao hawataweza kukataliwa baada ya kuwahubiri
wengine.
2. Nidhamu inaleta Heshima:-
Ni muhimu kufahamu kuwa tukiishi
kwa nidhamu watu watatuheshimu, watu wengi sana wanapenda kuheshimika kutoka
kwa wengine lakini njia nyepesi ya mtu kuheshimika ni kuishi kwa nidhamu, watu
wengi au wote duniani humkubali na kumuheshimu mtu mwenye nidhamu, sababu kubwa
ni kwamba ni kazi ngumu kuwa na nidhamu na kwa sababu hiyo ukiwa nayo watu
watakuheshimu, ukifanya kazi kwa nidhamu, ukatimiza kazi zako kwa wakati,
ukawepo unapotakiwa kuwepo kwa wakati, ni lazima utaheshimika, Mwanafunzi
mwenye nidhamu anajiandaa vizuri, anafanya kazi alizozipewa kwa wakati na kwa
sababu hiyo ni rahisi kwake kuyafikia malengo. Kwa ujumla utakuwa kielelezo na
mfano wa kuigwa
1Timotheo 4:12 “Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao
waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.”
Paulo mtume ni kama anamweleza
Timotheo kuwa mtu asikudharau kwa sababu u kijana, lakini ni namna gani watu
watakuheshimu? Ni kama utakuwa mfano yaani kielelezo, kwatika usemi, mwenendo,
upendo imani na usafi, ni kama Paulo anamwambia Timotheo kuwa watu
watakuheshimu bila kujali umri wako hata kama ni mdogo endapo tu utaishi kwa
nidhamu. Binti au mwanamke, kijana au mwanaume anayejitia nidhamu anaheshimika
katika jamii,
3. Nidhamu itakupa Afya njema.
Jinsi na namna ya kutunza afya
zetu pia ni swala linalohitaji nidhamu, namna tunavyokula, tunavyotumia chumvi,
sukari au mafuta mengi sana na namna tunavyotumia dawa bila nidhamu au kwa
nidhamu vina mchango mkubwa sana katika kuamua tuwe na afya ya namna gani,
Lazima na ni muhimu kuoga vizuri, kufanya mazoezi, kutembea na kulala kwa
wakati kwa ujumla mtindo wa maisha wenye kujitia nidhamu utaufanya mwili wetu
na akili zetu kuwa njema na zenye afya nzuri wakati wote, magonjwa sugu
hayatakuwa sehemu ya maisha yetu, kula kwa wakati funga kwa mpangilio mwema
bila kuharibu mwili wetu kwa vile miili hii sio mali yetu wenyewe ni mali ya
Mungu.
1Wakoritho 6:19 “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu
aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;”
4.
Nidhamu inaleta uthabiti na uwezo
wa kujitawala.
Kwa ujumla
nidhamu ina faida kubwa sana katika ujumla wa mtazamo wa maisha, inakuumbia
uthabiti na kujitawala au kujiamini na inakuepusha na hali zote za uvivu, kila
mtu mwenye nidhamu utaweza kuona hawezi kuwa mzembe wala kuzembea au kutegea
kazi, inaleta ufanisi kujitawala na kuwa na kiasi, Mtu mwenye nidhamu anauwezo
mkubwa sana wa kujizuia au kujitawala atakuwa makini katika kujua kile
kinatakiwa kuzungungumzwa na wakati kinapaswa kuzungumzwa, anajua nini cha
kuvaaa na wapi pa kuvaa, anajua namna anavyotakiwa kuenenda na kwa sababu hiyo
hujiepusha sana na matatizo na hivyo kuwa na uhusiano mzuri na watu, Nidhamu na
kujitawala ni mfano wa mji wenye boma kama mtu akikosa kujitawala anakuwa kama
mji usio na boma usio na ukuta ni rahisi kuvamiwa na kubomlewa kwa maangamizi
makubwa Mithali 25:28 “Asiyetawala roho yake Ni mfano wa mji uliobomolewa, usio na
kuta.” Kumbe kujitawala yaani
nidhamu ni ulinzi wa hali ya juu, huwezi kupatwa na majanga na mashambulizi ya
aina mbalimbali kama utajiyiisha katika nidhamu.
5.
Nidhamu inakwenda pamoja na ubora
wa Elimu.
Elimu
haiwezi kuwa bora kama hakuna swala la kukazia nidhamu, Lazima kila mwanafunzi
ajifunze nidhamu, Nidhamu itamsaidia mwanafunzi kujifunza vema na kwa ufasaha
darasani na kukamilisha silabasi nzima vema, Mwanafunzi hawezi kuwa mwanafunzi
mzuri kama haamki kwa wakati, haogi, hanywi chai au kula kwa wakati na
anayetoka toka hovyo bila sababu ya msingi, kwenda kujisaidia au kurejea
nyumbani, ni nidhamu ndiyo itakayokufanya uwe na afya njema utulivu, heshima na
adabu na kukua vema na kukuwezesha kujifunza, Hata kanisani haipendezi kuona
watu wanatokatoka saa ya kujifunza neno la Mungu kisha eti wanaenda kujisaidia,
au kusikiliza simu, iliyowekwa katika mtindo wa kimya eti kwamba una maswala
Muhimu, Mungu anataka sikio lako na moyo wako ili akuonye na kukupeleka katika
njia iliyonyooka Mithali 12: 1” Kila apendaye
mafundisho hupenda maarifa; Bali yeye achukiaye kulaumiwa ni kama mnyama”.
Napenda zaidi Biblia ya kiingereza inavyoweka Msatari huu katika namna njema
zaidi angalia “Whoever loves discipline
loves knowledge, but he who hates reproof is stupid” hii ni kwa mujibu wa
ESV, “Whoever loves discipline
loves knowledge, but whoever hates correction is stupid”NIV,
unaweza kuona so kwa lugha nyepesi inayokubaliana na somo langu ningeweza
kusema Kila apendaye Maonyo, au (Nidhamu) anapenda maarifa (Elimu), lakini kila
achukiaye maonyo ni mpumbavu, Kwa hiyo utaweza kuona kuwa hekima na maaruifa na
elimu vinapatikana sambamba na Nidhamu au maonyo au marudia.
6.
Nidhamu inaleta furaha na amani.
Kuishi kwa
nidhamu kunasaidia kufanya mambo yafanyike vema na kwa wakati, ingawa mambo
mengine yanaweza kujitokeza na kuzuia lakini bado nidhamu inaweza kufanya mambo
kufanyika kwa haraka na ufasaha na hivyo
kusababisha furaha na amani. Aidha biblia inaeleza kuwa kama mtoto amefunzwa
vema atakustarehesha na kuifurahisha nafsi yako, lakini kama ameachiliwa
atakuwa ni aibu kwa mama yake Mithali
29:15, 17 Fimbo
na maonyo hutia hekima; Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye., Mrudi
mwanao naye atakustarehesha; Naam, atakufurahisha nafsi yako”.
Makusudi ya Nidhamu katika mpango
wa Mungu.
Ingawa neno
nidhamu lina maana pana sana katika tafasiri yake kwa vila inahusu mambo mengi
sana hata hivyo ni muhimu tukaangalia pia kwa kina makusudi ya nidhamu hasa
katika mpango nwa Mungu, Maandiko ya Msingi yana mengi ya kutufunza kuhusu
makusudi ya nidhamu katika mpango wa Mungu tunapoyaangalia maandiko ya msingi
utaweza kuona kuna sababu kadhaa kama tano hivi ya makusudi ya Nidhamu katikia
mpango wa Mungu
Waebrania 12:5-11 “tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na
wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana,
Wala usizimie moyo ukikemewa naye; Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye. Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi
asiyerudiwa na babaye? Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu
ninyi, wala si wana wa halali. Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili
walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali
sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi? Maana ni hakika, hao kwa
siku chache waliturudi kama walivyoona vema
wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake. Kila adhabu
wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye
huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.”
a.
Kwa
kusudi la kurekebisha mwenendo usiofaa.
Biblia katika kitabu cha
waebrania imeonya kuwa ni jambo la kutisha sana kuanguka katika mikono ya
Mungu, yaani kuachana na neema na katika sura ya kumi na moja imekazia sana
swala zima la mashujaa wa imani na kututaka tujifunze kupitia wao na kisha sura
ya 12 inatutia moyo namna ya kufanya ili tuweze kufanikiwa kama wao kwa ufupi
mashujaa wote wa imani walikuwa watu wenye nidhamu, na kutokana na kujitia
nidhamu waliweza kufanikiwa na kuzirithi ahadi za Mungu
Kizazi cha ma hausegirl tulicho
nacho leo, watoto wanalelewa boarding tangu wakiwa wachanga kwenye vituo vya
day care, waliokosa malezi sahihi ya baba, wajomba mashangazi na wazazi wenye
nidhamu nikizazi kilichopoteza muelekeo, kama kanisa halitakuwa makini (Sirius) katika swala zima la nidhamu
tutakuwa tumepoteza mwelekeo, ili tuweze kufanikiwa lazima turudi katika mpango
wa Mungu wa kutoa maonyo kwa maneno na matendo YASAR (MARUDIA) YAKASH (MAKEMEO) Waebrania 12:5 “tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na
wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana,
Wala usizimie moyo ukikemewa naye” hapa
maneno yanayotumika Marudia au Makemeo yanakaziwa, haya maonyo yanataka wote
wazazi na watoto kwa ujumla wasisahau wasichukulie kirahisi maonyo na makemeo
ya Bwana yaani kutia nidhamu na kurekebisha tabia mbaya.
b.
Kwa
kusudi la kuonyesha kujali na upendo.
Waebrania 12:6-9 “Maana yeye ambaye
Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye. Ni kwa ajili ya
kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi
asiyerudiwa na babaye? Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote,
ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. Na pamoja na hayo
tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali
sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi?” Moja ya njia
iliyo njema zaidi ya kuonyesha kuwa unamjali mtoto wako na kumpenda ni
kuhakikisha kuwa wanakuwa na nidhamu, namna yoyote ile ya kumfanya mtoto
ajisikie kuwa yuko salama kufanya na kuishi vyovyote atakavyo ni makosa makubwa
sana ambayo yatatuletea huzuni kubwa lakini kama tutakubali kuumia wakati wa
kuwatiisha na kuwafunza nidhamu basi ni wazi kuwa tutapata raha Mithali 29: 15, 17 “Fimbo na maonyo hutia hekima; Bali mwana aliyeachiliwa
humwaibisha mamaye, Mrudi mwanao naye atakustarehesha; Naam, atakufurahisha
nafsi yako.” Hatuwezi kuwa na hekima kuliko maandiko wala hatuwezi
kuwa na ufahamu kuliko Mungu, kama Mungu katika neno lake anataka tuchukue
hatua stahiki dhidi ya watoto wetu ni wazi kuwa lazima kufanya kitu kwaajili ya
watoto wote wa Mungu kwa upendo wenye kuonyesha kuwa tunajali badala ya
kusubiri majuto ndio maana mwanafalsafa - John
Rohn akasema “Kila
mmoja anapaswa kuchagua njia mojawapo kati ya mbili, maumivu ya Nidhamu au
maumivu ya Majuto” Tusipochukua hatua za
kuishi kwa nidhamu maana yake tutajuata baadaye, na ndio maana Mungu katika
mpango wake anatuonyesha upendo kupitia maonyo, Kama hatuna kuonywa ni dhahiri
sisi tumekuwa wana wa haramu na maisha yetu yatajaa taabu na majuto mengi.
c.
Kwa
kusudi la kufundisha utii
Tunapojifunza Nidhamu katika
maisha yetu maana yake tunajifunza utii, tunajiweka katika neema ya Mungu,
tunajifunza kutii kwa upendo, japo wakati wa mafunzo linaweza kuwa jambo lenye
kuuma sana lakini linatupa matunda ya milele, mwanzoni itakuwa ni swala lenye
kuumiza kwa nje lakini likihamia ndani linaleta ustaarabu wa kudumu, Biblia
inasema katika Waebrania 12:11 “Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali
cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye
amani.” Unaweza kuona kuwa kila adhabu, yaani nidhamu wakati wa
kuijifunza haionekani kuwa ni furaha ni kama maumivu lakini ina faida kubwa
baadaye.
d. Nidhamu inatupa kuwa na Hekima
Mungu ndiye
chanzo cha Hekima na ni mkarimu kwa kila mmoja anasema katika Yakobo 1:5 “Lakini
mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa
ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.” Mojawapo ya njia ya kupokea
hekima kutoka kwa Mungu ni pamoja na na kukubali maonyo, na hekima atakayotupa
itatuongoza na kutusaidia kuwa waadilifu, watakatifu na kutuepusha na madhara
ya kiroho Mithali 2:10-12 “Maana hekima itaingia moyoni mwako, Na maarifa yatakupendeza
nafsi yako; Busara itakulinda; Ufahamu utakuhifadhi., Ili kukuokoa na njia ya
uovu, Na watu wanenao yaliyopotoka;”, unaweza kuona hatimaye
tutakuwa ytayari kumpenda Mungu na kumwabudu pasipo hofu, hatimaye kuingia
katika uzima wa milele , Mungu anataka tuwe watakatifu na hivyo hututia nidhamu
Waebrania 12:10 “Maana ni hakika,
hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa
faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake”. Yuda 1;21 “jilindeni katika upendo wa Mungu, huku mkingojea rehema ya
Bwana wetu Yesu Kristo, hata mpate uzima wa milele.”
Rev.
Innocent Kamote
Mkuu wa
wajenzi mwenye Hekima!
0718990796
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni