Wagalatia 6:9 “Tena tusichoke
katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.”
Msichoke katika kutenda mema, Mstari huu katika biblia ya kiingereza
unasomeka “And let us not grow weary while doing good, for in
due season we shall reap if we do not lose heart”
Neno
“weary” linalotumika hapo halizungumzii kuchoka kwa mwili ambako kunaweza kukarabatiwa kwa kula, kunywa maji mengi, kuoga maji ya baridi na kupumzika vya kutosha ambako kitaalamu kunaweza kuwa tiba ya kuchoka kwa mwili, Neno hili Weary maana yake spiritless, Exhausted, lose heart, despair hii inazungumzia kuchoka kwa nafsi huku ndio kuchoka kubaya zaidi kunakoweza kuleta madhara makubwa
“weary” linalotumika hapo halizungumzii kuchoka kwa mwili ambako kunaweza kukarabatiwa kwa kula, kunywa maji mengi, kuoga maji ya baridi na kupumzika vya kutosha ambako kitaalamu kunaweza kuwa tiba ya kuchoka kwa mwili, Neno hili Weary maana yake spiritless, Exhausted, lose heart, despair hii inazungumzia kuchoka kwa nafsi huku ndio kuchoka kubaya zaidi kunakoweza kuleta madhara makubwa
Kuchoka huku ni hali ya kukata
tamaa, ni hali ya kutokuendelea au hali ya kuvunjika moyo, Hali hii inatokana
na kukosekana kwa muamko wa Moyo na sio kuchoka kwa mwili, Hali ya kukosa
muamko inaweza kupelekea mtu kuchoka katika nafsi mwili na roho. Hivi karibuni
watu tumeshuhudia huko Africa ya kusini watu waliochoka nafsi waliweza
kuwavamia waafrika wenzao na kuharibu vitu na kuiba na kuchoma moto matendo
ambayo yameleta aibu duniani lakini sababu kubwa inatokana watu kukata tamaa,
watu wanapokata tamaa huweza kucha kutenda mema na wakatenda mabaya!
Maandiko yanatuonya kutokukata tamaa
kutokuchoka, kuchoka kunaweza kuletwa na Maswala mbalimbali makubwa katika
maisha yetu, Nyakati za Kanisa la kwanza wakati mwingine Makanisa yalikata
tamaa kutokana na kukamatwa kwa viongozi na kuwekwa ndani mara kwa mara Waefeso 3:13 “Basi
naomba msikate tamaa kwa sababu ya dhiki zangu kwa ajili yenu, zilizo utukufu
kwenu.” Watu wanapokosa mwamko ni rahisi sana kukata tamaa,
wanafunzi wanapokosa mwamko ni rahisi kuchoka katika kusoma, walimu wanapokata
tamaa ni rahisi sana kuendelea kuwafundisha wanafunzi kwa weledi, Baba
anapochoka anapochoshwa na tabia za
watoto au mkewe nyumbani anaweza kukata
tamaa, kila tunalilofanya linahitaji motosha ili tusiweze kuchoka.
Msichoke Katika kutenda Mema.
Msichoke katika kutenda mema,
hili ni swala ambalo neno la Mungu linatutia moyo, kwamba tuendelee kutenda
mema kwa imani, kwa upendo, na nguvu tuliyonayo katika jina la Yesu, hii ni
kanuni ambayo ina mavuno ndani yake , lakini sio hivyo tu ni jambo lenye
kumpendeza Mungu; Hatupaswi kuchoka hata kidogo Mungu azitie moyo roho zetu na
nia zetu, Hata tunapokutana na vikwazo vya namna mbalimbali, Mara nyingi ni
vigumu kupata muelekeo na kuchoka kwa nafsi, Mabadiliko mbalimbali ya kiuchumi,
Madeni, kupoteza maswala kadhaa katika ulimwengu, kukosekana kwa shukurani au
kupongezwa au hata kutiwa Moyo ulimwengu unapokuwa sio ulimwengu wenye kutia
moyo ni rahisi sana watu kukata tamaa na kuacha kufanya kile wanachojisikia
kukifanya na hapo Biblia inatusukuma kutokuacha au kuchoka katika kutenda mema 2Wathesalonike 3:13 “Lakini ninyi, ndugu, msikate tamaa katika kutenda mema.”
Kunapotokea Maswala
magumu ya kukatisha tamaa na kukosekana kwa motisha miongoni mwa wakristo ni
rahisi sana kwa jamii ya kanisa kuacha kuendelea kutumika katika kiwango kile
tulichokuwa nacho, ni rahisi kutoa udhuru, ni rahisi kupoteza mwelekeo na ni
rahisi kuacha hii inatokana na kukata tamaa Tunahitaji neema ya Mungu na
kutokukata tamaa kabisa Yakobo 5:7-8 “Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama,
mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata
yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho. Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo
yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia”
Neno la Mungu
linatutia moyo kuwa Kutenda mema kunalipa na kuwa tutavuna kwa wakati, aidha
wakati huu wa sasa ama wakati ujao liko tumaini kubwa mbele yetu na kamwe
hatupaswi kuzimia moyo uvumilivu wetu unapaswa kuwa sawa na ule wa mkulima
Mungu atatulipa tu kwani kila tulifanyalo lililo jema ni mbegu kwa MUngu na kwa
wakati wake tutavuna kama hatutazimia moyo
Mfano:
Katika mji mmoja kulikuwa na vijana
wawili waliokuwa Ndugu, Ndugu mkubwa alimuonea sana na kumtendea vibaya ndugu
yake mdogo na wala hakuwahi kumuonyesha upendo, na wakati mwingine alikula
chakula chake, na pia alichukua nguo zote nzuri za ndugu yake mdogo na kuzivaa
yeye, Nduguye aliendelea kuvumilia na kumuonyesha upendo hatahivyo, Siku moja
Ndugu yule mkubwa alikwenda msituni kwa kusudi la kutafuta kuni na kuziuza,
alipokuwa msituni akikata kuni, kutoka mti mmoja mpaka mti mwingine, alikutana
na mti mmoja wa ajabu, na mti huu ulimwambia tafadhali sana usikate matawi
kutoka kwangu na kama utafanya hivyo nitakupa peasi la dhahabu, Kijana yule
mkubwa alikubali, Lakini hata hivyo mti ule wa ajabu ulimpa matunda machahe ya
dhahabu,kwa uroho na uchungu na tamaa, aliamua kutisha ule mti kuwa
ataukata!kama mti huu hautatoa peasi nyingi zaidi, Mti huu wa ajabu kwa namna
iaisyoweza kuelezeka ulitoa miiba mingi sana na ikamchoma yule jama amwili
mzima na akawa anagaa gaa kwaajili ya kujinasua kutoka katika kujitoa miiba ile
Ndugu yake mdogo alipoona kuwa jua
linakuchwa alipata hofu na aliamua kumtafuta kaka yake, na alikwenda mpaka
msituni na kumkuta akiwa katika hali ngumu sana na aliamua kumsaidia kwa upendo,
na kumuondoa miiba yote mwilini alipomaliza kaka yake alitambua wazi kuwa mdogo
wake alikuwa na upendo wa kweli, aliomba radhi,kwa jinsi alivyokuwa akimfanyia
ubaya ndugu yake na alimuahidi kumtendea mema tangu siku ile , Mti ule wa ajabu
uliona yote yaliyotendeka na ukaridhika na badilikola kaka mkubwa ukawapa wote
mapeas ya dhahabu waliyohitaji, wote maisha yao yalibadilika na wakaishi maisha
ya upendo
tunajifunza nini kutoka kwa ndugu yule
mdogo angechoka kutenda mema aisngevuna kwa wakati muafaka nay eye na kak ayake wasingeweza kuwa na
maisha ya furaha na mafanikio
Rev.
Innocent Kamote.
Mkuu
wa Wajenzi mwenye Hekima!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni