Mstari wa Msingi: Kutoka
22:18 “Usimwache mwanamke mchawi kuishi.”
Utangulizi:
Ni muhimu kufahamu kuwa moja ya
amri kuu katika maandiko inasema “Mpende Bwana Mungu wako kwa
moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili yako yote”
Luka 10:27, Amri hii inaonyesha wazi
kuwa Mungu anataka aabudiwe yeye peke yake na kwamba kuabudu miungu mingine ni
moja ya machukizo makubwa sana kwa Mungu; Kutoka
20:3-6 “Usiwe
na miungu mingine ila mimi. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu
cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini
chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu
wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi
cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.”
Swala la watu
kutafuta miungu mingine nje ya Mungu mwenyezi ni swala la siku nyingi na la
zamani sana na shetani amefanikiwa sana kuwafanya watu waabudu miungu mingine
kupitia waganga na wachawi badala ya Mungu, shetani anatumia Waganga, wachawi,
wanajimu na kadhalika ili kuwafanya watu wasimuabudu Mungu na badala yake
wamuabudu yeye au washirikiane na mashetani. Maandiko yanakataza kwa mkazo
mkubwa mno swala la kushirikiana na Mashetani yaani ushirikina na uganga na
uchawi. 1 Wakoritho 10:20-21 “Sivyo, lakini vitu
vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi
kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha
mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya
mashetani.” Paulo mtume
alikataza kabisa kwa herufi kuwa Kanisa kuwa na ushirika na Mashetani,
Unaposikia mtu anaitwa mshirikina maana yake ni mtu mwenye ushirika na
mashetani aidha kupitia wachawi au waganga wa kienyeji, swala hili ni katazo la
kibiblia katika agano la kale Mungu aliwakataza kabisa wana wa Israel
kujihusisha na maswala haya kabisa na mara kadhaa agizo la kuupinga uchawi na
ushirikina liliambatana na kifo!
Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia
vipengele vitatu vifuatavyo:-
1. Msimamo
wa agano la kale kuhusu wachwi
2. Msimamo
wa Agano jipya kuhusu Wachwi
3. Wito
na ushauri wa kimungu kwa wachawi na washirikina
Msimamo wa agano la kale kuhusu wachawi.
·
Walawi
19:31 “Msiwaendee
wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi
BWANA, Mungu wenu”
·
Walawi
20:6 “Na mtu
yule atakayewaendea wenye pepo, na wachawi, ili kuzini pamoja nao, nitakaza uso
wangu juu ya mtu yule, nitamtenga na watu wake”.
·
Walawi
20:27 “ Tena mtu mume au mtu mke aliye na pepo, au
aliye mchawi, hakika atauawa; watawapiga kwa mawe; damu yao itakuwa juu yao.”
·
Kumbukumbu
18:10-14 “Asionekane
kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu
atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala
msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala
mchawi, wala mtu awaombaye wafu. Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa
Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.
Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako. Maana mataifa haya utakaowamiliki
huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na kutazama bao; bali wewe, Bwana, Mungu
wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo.”
·
1Nyakati
10:13 tunaelezwa wazi kuwa sababu za kifo cha mfalme wa kwanza wa Israel
ilikuwa ni kwa sababu alikwenda kuuliza kwa wachwi “Basi Sauli alikufa kwa sababu ya kosa lake
alilomkosa Bwana, kwa sababu ya neno la Bwana, asilolishika; na tena kwa kutaka
shauri kwa mwenye pepo wa utambuzi, aulize kwake, asiulize kwa Bwana; kwa hiyo
akamwua, na ufalme akamgeuzia Daudi, mwana wa Yese.”
·
Hasira ya Bwana Mungu huwaka kwa mtu
anayejishughulisha na maswala ya ushirikina
2Nyakati 33:6 “Tena akawapitisha wanawe motoni katika
bonde la mwana wa Hinomu; akatazama bao, akabashiri, akafanya uganga,
akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya
mengi machoni pa Bwana, hata kumkasirisha.”
Msimamo wa agano jipya kuhusu wachawi.
·
Katika matendo ya mwili yanayotajwa katika agano
jipya ya watu ambao hawataurithi ufalme wa Mungu na wachawi nao wamo Wagalatia 5:19-21 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada
ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda,
ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama
nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo
hawataurithi ufalme wa Mungu.”
·
Agano jipya pia linaeleza wazi kuwa wachawi
sehemu yao itakuwa ni katika lile ziwa la Moto Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na
wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na
waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii
ndiyo mauti ya pili. “
·
Hakuna lugha ya upole kwa wachawi Biblia
inaonyesha wazi kuwa mitume hawajawi kuzungumza na wachawi kwa lugha ya
kubembeleza wakati wote wachawi walikemewa na kuitwa katika toba ili waamini
vinginevyoa adhabu kali ilikuwa ikiambatana nao ona kwa mfano Matendo 8:9-22 “Na
mtu mmoja, jina lake Simoni, hapo kwanza alikuwa akifanya uchawi katika mji
ule, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu
mkubwa. Wote wakamsikiliza tangu mdogo hata mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni uweza
wa Mungu, ule Mkuu. Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mwingi kwa
uchawi wake.Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa
Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.Na yeye
Simoni mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; akashangaa
alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka. Na mitume waliokuwako
Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu,
wakawapelekea Petro na Yohana; ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho
Mtakatifu; kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa
jina lake Bwana Yesu. Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho
Mtakatifu. Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa
kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema,Nipeni na mimi uwezo
huu, ili kila mtu nitakayemweka mikono yangu, apokee Roho Mtakatifu. Lakini
Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania
ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali. Huna fungu wala huna sehemu katika
jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu. Basi, tubia uovu wako
huu, ukamwombe Bwana, ili kama yamkini, usamehewe fikira hii ya moyo wako”
Mungu ni mwingi wa Rehema na upendo lakini nataka nikueleze wazi kuwa hana
huruma na wachawi hata kidogo, kila mtumishi wa Mungu mwenye mamlaka ya kimungu
ameruhusiwa kuwafanya lolote wachawi kusema nao kwa ukali na kuwaamuru kuavcha
hila zao mbaya maan wao ni wana wa ibilisi
Matendo ya Mitume 13:8-11 “.Lakini Elima, yule mchawi
(maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali
moyo wa kuiacha ile imani. Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho
Mtakatifu, akamkazia macho, akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana
wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? Basi,
angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda.
Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa
kumshika mkono na kumwongoza.” Wachawi huzipotosha njia za Bwana
zilizonyooka Paulo anamuadhibu vikali Mchawi kwa sababu anajua kuwa Mungu yuko
kiyuma nao na kuwa wachwi wakati wote hupinga na shauri la Mungu, wako kinyume
na Mapenzi ya Mungu, Mungu alipokuwa anataka kuwaokoa wana wa Israel kutoka
Misri wachawi waliweza kuigiza miujiza ya Mungu vilevile na walichangia kwa
kiasi nkikubwa ugumu wa mowyo wa farao kwa sababu farao aliona hakuna jipa angalia Kutoka 7:22 “Lakini
waganga wa Misri wakafanya mfano wa hayo kwa uganga wao; na moyo wake Farao
ukawa mgumu, wala hakuwasikiza, kama BWANA alivyonena”. Unaona
Biblia ya habari njema BHN inasomeka vizuri katika Kutoka 7:22 inasema “Lakini wachwi wa Misri kwa kutumia uchawi waowakafanyoa vivyo
hivyo,Kwa hiyo moyo wa farao ukabaki kuwa mgumu naye hakuwasikiliza Mose na Aroni
kama mwenyezi Mungu alivyokua amesema” Wachawi hawa ni wapinzani wa
mipango ya Mungu, na wakati mwingine kwa mtu mwenye moyo kama wa Farao ni
vigumu kupambanua na kujua katika ya mtu wa Mungu na Mchawi, farao alifikiri
Musa yuko sawa na wachawi wake tu Mpaka pale Mungu alipodhihirisha uwezo wake
ndipo wachawi wa farao wakamueleza wazi kuwa hiki ni chanda cha Mungu Kutoka
8:19 “Ndipo wale waganga wakamwambia Farao, Jambo hili
ni chanda cha Mungu; na moyo wake Farao ukawa mgumu asiwasikize; vile vile kama
BWANA alivyonena.” Hakuna
popote katika Biblia mchawi au mganga ameonyeshwa kuwa ni mtumishi wa Mungu
hakuna. Wote wanahukumiwa na Mungu kwa
ukali na dhabu kuwa ni kifo au watubu na kumgeukia Mungu, Kazi kubwa ya wachawi
ni kupinga na Mungu na makusudi yake, popote pale mtu wa Mungu unapofanya jambo
na kuona kuwa kuna ushindani, kuna upinzani kuna ugumu usiokuwa wa kawaida,
hakuna mtiririko unaokusudiwa funguka na kukemea nguvu za upinzani shetani ujue
yupo au watumishi wake na wanafanya yao hivyo butua shughulika na Yane na
Yambre ambao ndio hufanya hayo wanayoyafanya yaani wanapingana na imani 2Timotheo 3:8 “Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na
Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili
zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.”
Wito na ushauri wa kimungu kwa wachawi na washirikina
Biblia ina wito
mmoja tu kwa wachawi, watubu ili yamkini Mungu awasamehe fikira yao mbaya,
waache kuzipotoa njia za Bwana zilizonyooka na watubu na kugeuka na kuchomelea
mbali vitabu vyao na mikoba yao na vifaa vyao vya uchawi Matendo ya Mitume 19:19 “Na
watu wengi katika wale waliotumia mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao,
wakavichoma moto mbele ya watu wote; wakafanya hesabu ya thamani yake, wakaona
ya kwamba yapata fedha hamsini elfu.” Biblia inaonyesha kuwa wachawi
kule Efeso walitubu na kuziharibu kabisa kazi mabaya za gharama kubwa hawakuwa
na aibu waliviharibu na kuviteketeza vyote bila kujalia gharama vifaa vyote vya
uchawi walivichoma moto wito wa kibiblia ni kila mtu mbaya aache njia yake
mbaya na amgeukie Mungu naye Mungu atamsamehe Isaya 55:6-7 “Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu
karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na
amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe
kabisa.”
Biblia inaonya
kwa ukali sana kuhusu kujihusisha na ushirikina ukweli ni kuwa hakuna neno la
Huruma kwa wachawi awe mwanaume au awe mwanamke adhabu ya wachawi ni kifo tu,
Katika agano jipya trehema tunayoweza kuiona ni wao kuacha uchawi na kumuamini
Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yao, Neno la Mungu linaposema usimuache
mwanamke mchawi kuishi, liko wazi kuwa hukumu ya wachawi ni kifo tu, kama
unajihusiha na ushirikiana nakuonya kwa jina la Mwenyeji Mungu acha mara moja
Mgeukie Yesu, mwambie akusamehe na kama unajihusisha na uganga acha acha mara
moja na ili uweze kuwa salama Mgeukie Mungu acha kuwadanganya watu, acha
kutumia pepo wa utambuzi, achana na mapepo ya uuguzi, acha kutumiwa na maimuna,
subian, makata na vinyamkera na aina yoyote ya majini na mapepo yanayokutokea
ua kukuotesha ndoto acha nakuonya, na kama unakwenda kwa waganga tubu na
usirudie tena. Vinginevyo kifo cha kimwili na kiroho kinakuhusu.
Rev. Innocent
Kamote
Mkuu wa wajenzi
mwenye Hekima!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni