Matendo ya Mitume 28:17-22 “Ikawa baada ya siku tatu akawaita wakuu wa Wayahudi
wakutane, hata walipokutanika akawaambia, Ndugu zangu, ningawa sikufanya neno
kinyume cha watu wetu wala neno lililopingamana na desturi za baba zetu,
nalitiwa katika mikono ya Warumi, hali nimefungwa, tokea Yerusalemu. Na hao
walipokwisha kuniuliza-uliza walitaka kunifungua, kwa maana hapakuwa na sababu
yo yote kwangu ya kuuawa. Lakini Wayahudi walipotoa hoja juu ya shauri hili
nalishurutishwa kutaka rufani kwa Kaisari. Si kwamba nalikuwa na neno la
kuwashitaki watu wa taifa langu. Basi kwa ajili ya hayo, nimewaita mje
kunitazama na kusema nami; kwa maana nimefungwa kwa mnyororo huu kwa ajili ya
tumaini la Israeli. Wale wakamwambia, Sisi hatukupata nyaraka zenye habari zako
kutoka Uyahudi, wala hapana ndugu hata mmoja aliyefika hapa na kutupasha habari,
au kunena neno baya juu yako. Lakini tunataka kusikia kwako uonavyo wewe; kwa
maana katika habari za madhehebu hiyo imejulikana kwetu kwamba inanenwa vibaya
kila mahali.”
Utangulizi:
Ni muhimu kufahamu kuwa Paulo
mtume alitamani sana Kufika Rumi kwa miaka mingi, Mji wa Rumi ndio ulikuwa
makao makuu ya Utawala wa waroma wakati wa ufalme mkubwa wa Kaisari, watu wengi
sana waliishi katika mji mkuu wa Rumi, na wayahudi wengi sana, hivyo Paulo
alitamani kuwa katika safari zake za injili vilevile aweze kufika Rumi, na
alimuomba Mungu ili aweze kufika huko nako, unaweza kuona katika
Warumi 1:9-12 “Kwa maana Mungu, nimwabuduye kwa roho yangu katika Injili
ya Mwana wake, ni shahidi wangu jinsi niwatajavyo pasipo kukoma, siku zote
katika sala zangu, nikiomba nije kwenu hivi karibu, Mungu akipenda kuifanikisha
safari yangu. Kwa maana ninatamani sana kuwaona, nipate kuwapa karama ya
rohoni, ili mfanywe imara; yaani, tufarijiane mimi na ninyi, kila mtu kwa imani
ya mwenzake, yenu na yangu.”
Unaweza kuona kwa hiyo kuwa kiu
kubwa ya Mtume Paulo ilikuwa siku moja aweze kuonana na wayahudi walioko Rumi
ili aweze kuonana nao, iliposhindikana kufika Rumi kwa wakati aliotamani aliwaandikia
waraka, Paulo aliamua kuwaandikia waraka huu ili kuweka mafundisho Muhimu sana kuhusu
Wokovu na ukombozi wa Bwana wetu Yesu Kristo, lakini vilevile kanisa la Rumi na
wayahudi walioko huko na wale walioamini wapate kujua injili aliyokuwa
akiihubiri, Rumi ndio ulikuwa mji mkuu wa ulimwengu wa wakati ule na ulikuwa ni
mji wenye watu wengi sana wakiwepo wayahudi, Paulo aliutamani mji huu kwa kuwa
ulikuwa ni hazina ambayo baadaye ilikuja kutumika kueneza injili ya Kristo
Duniani kwa kujua ubora wa mji huu na umuhimu wa huduma ya Paulo Mtume kwa watu
wa Rumi, Shetani alijaribu kwa kila hila kuzuia injili kupitia Paulo mtume na kupingana naye kwa namna na mazingira
Magumu sana asifike katika mji wa Rumi na hivyo kulikuwa na mazingira magumu
sana
Matendo 27:1-44 “Tukapanda katika merikebu
ya Adramitio iliyokuwa tayari kusafiri mpaka miji ya pwani za Asia, tukatweka;
Aristarko, Mmakedonia wa Thesalonike, akiwa pamoja nasi. Siku ya pili
tukawasili Sidoni; Yulio akamfadhili sana Paulo akampa ruhusa kwenda kwa rafiki
zake, apate kutunzwa. Kutoka huko tukatweka, tukasafiri chini ya Kipro ili
kuukinga upepo, kwa maana pepo zilikuwa za mbisho. Tulipopita bahari ya upande
wa Kilikia na Pamfilia, tukafika Mira, mji wa Likia. Na huko yule akida akakuta
merikebu ya Iskanderia, tayari kusafiri kwenda Italia, akatupandisha humo. Tukasafiri
polepole kwa muda wa siku nyingi, tukafika mpaka Nido kwa shida; na kwa sababu
upepo ulikuwa ukituzuia tukapita chini ya Krete, tukaikabili Salmone.Tukaipita
kwa shida, pwani kwa pwani, tukafika mahali paitwapo Bandari Nzuri. Karibu na
hapo pana mji uitwao Lasea. Na wakati mwingi ulipokwisha kupita, na safari
ikiwa ina hatari sasa, kwa sababu siku za kufunga zilikuwa zimekwisha kupita,
Paulo akawaonya, akawaambia, Wanaume, naona kwamba safari hii itakuwa na
madhara na hasara nyingi, si ya shehena na merikebu tu, ila na ya maisha yetu
pia. Lakini yule akida akawasikiliza nahodha na mwenye merikebu zaidi ya yale aliyoyasema
Paulo.Na kwa sababu bandari ile ilikuwa haifai kukaa wakati wa baridi, wengi
wao wakatoa shauri la kutweka kutoka huko ili wapate kufika Foinike, kama
ikiwezekana, na kukaa huko wakati wa baridi; nayo ni bandari ya Krete,
inaelekea kaskazini-mashariki na kusini-mashariki. Na upepo wa kusi ulipoanza
kuvuma kidogo, wakidhani ya kuwa wamepata waliyoazimu kupata, wakang'oa nanga,
wakasafiri karibu na Krete pwani kwa pwani. Baada ya muda mchache ukavuma upepo
wa nguvu wa namna ya tufani, uitwao Eurakilo, merikebu iliposhikwa, na kutoweza
kushindana na upepo, tukaiacha tukachukuliwa. Na tukipita upesi karibu na
kisiwa kidogo kiitwacho Kauda tukadiriki kuikweza mashua; lakini kwa shida. Walipokwisha
kuikweza wakatumia misaada, wakaikaza merikebu kwa kupitisha kamba chini yake,
nao wakiogopa wasije wakakwama katika fungu liitwalo Sirti, wakatua matanga
wakachukuliwa vivi hivi. Na kwa maana tulikuwa tukipigwa sana na ile tufani,
siku ya pili yake wakaanza kuitupa shehena baharini. Siku ya tatu wakatupa
vyombo vya merikebu kwa mikono yao wenyewe. Jua wala nyota hazikuonekana kwa
muda wa siku nyingi, na tufani kuu ikatushika, basi tukakata tamaa ya kuokoka. Na
walipokuwa wamekaa wakati mwingi bila kula chakula, Paulo akasimama katikati
yao, akasema, Wanaume, iliwapasa kunisikiliza mimi na kutokung'oa nanga huko
Krete, na kupata madhara haya na hasara hii. Sasa nawapeni shauri, iweni na
moyo mkuu, kwa maana hapana hata nafsi mmoja miongoni mwenu atakayepotea, ila
merikebu tu. Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni
wake, naye ndiye nimwabuduye, alisimama karibu nami, akaniambia, Usiogope,
Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote
wanaosafiri pamoja nawe. Basi, wanaume, changamkeni; kwa sababu namwamini
Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa. Lakini hatuna budi kupwelewa
katika kisiwa kimoja. Hata usiku wa kumi
na nne ulipofika, tulipokuwa tukichukuliwa huko na huko katika bahari ya Adria,
kama usiku wa manane baharia wakadhani ya kuwa wanaikaribia nchi kavu. Wakatupa
bildi wakapata pima ishirini, wakaendelea kidogo wakatupa bildi tena, wakapata
pima kumi na tano. Wakachelea tusije tukapwelewa mahali penye miamba, wakatupa
nanga nne za tezi, wakaomba kuche. Na baharia walipotaka kukimbia na kuiacha
merikebu, wakiishusha mashua baharini kana kwamba wanataka kutupa nanga za omo,
Paulo akawaambia akida na askari, Hawa wasipokaa ndani ya merikebu hamtaweza
kuokoka. Basi askari wakazikata kamba za mashua, wakaiacha ianguke. Na
kulipokuwa kukipambauka Paulo akawasihi wote wale chakula, akisema, Leo ni siku
ya kumi na nne kungoja na kufunga, hamkula kitu cho chote. Basi nawasihi mle
chakula, maana itakuwa kwa wokovu wenu; kwa maana hapana hata unywele wa kichwa
cha mmoja wenu utakaopotea. Alipokwisha kusema hayo akatwaa mkate, akamshukuru
Mungu mbele yao wote akaumega akaanza kula. Ndipo wakachangamka wote, wakala
chakula wenyewe. Na sisi tuliokuwa ndani ya merikebu tulipata watu mia mbili na
sabini na sita. Walipokwisha kushiba wakaipunguza shehena ya merikebu,
wakiitupa ngano baharini. Kulipokucha hawakuitambua ile nchi, ila waliona hori
yenye ufuo, wakashauriana kuiegesha merikebu huko, kama ikiwezekana. Wakazitupilia
mbali zile nanga, na kuziacha baharini, pamoja na kuzilegeza kamba za sukani,
wakalitweka tanga dogo ili liushike upepo, wakauendea ule ufuo. Lakini
wakafikia mahali palipokutana bahari mbili, wakaiegesha merikebu, omo ikakwama
ikakaa isitikiswe, bali tezi ilikuwa imefumuliwa kwa nguvu za mawimbi. Shauri la askari lilikuwa kuwaua wafungwa, mtu
asiogelee na kukimbia. Bali akida, akitaka kumponya Paulo, akawazuia, wasifanye
kama walivyokusudia, akawaamuru wale wawezao kuogelea wajitupe kwanza baharini,
wafike nchi kavu; nao waliosalia, hawa juu ya mbao na hawa juu ya vitu vingine
vya merikebu. Na hivyo watu wote wakapata kuifikilia nchi”
Hatimaye Paulo mtume alifika
katika mji huu wa Rumi akiwa mfungwa lakini vilevile kwa shida kubwa sana
wakinusurika kifo kwa njia zote dhoruba njaa na majanga makubwa sana mwishoe
Paulo aliingia Rumi akiwa mfungwa wan je katika nyumba mojawapo chini ya ulinzi
wa akida aliyeitwa Julius, akiwa katika vifungo vya minyororo. Na ndipo wazee wa kiyahudi walipokuja
na kumsalimu lakini wakitaka kujua kwanini dhehebu hili linanenwa vibaya!
Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vikuu viwili vifuatavyo:-
·
Katika
habari ya Madhehebu hiyo inanenwa vibaya!
·
Kwa nini
Dhehebu hili linanenwa vibaya!
Katika habari ya
Madhehebu hiyo inanenwa vibaya!
Kwa bahati njema kama tulivyoona
katika utangulizi wazee na viongozi wakuu wa wayahudi waliokaa Rumi walikuja
kumtembelea na kumjulia hali, na kukutana naye katika nyumba aliyokuwa
amefungwa, Naye aliwaelezea mkasa mzima wa namna alivyo singiziwa maneno ya
uongo na jinsi alivyotaka kuuawa na akaamua kuyaokoa maisha yake kwa kukata
rufaa kuja Rumi kwa kaisari hata hivyo wazee wa kiyahudi kule Rumi hawakuwa na
taarifa yoyote kuhusu kesi yake na kile kilichokuwa kimeendelea juu yake
Matendo 28:17-21 “Ikawa baada ya siku tatu
akawaita wakuu wa Wayahudi wakutane, hata walipokutanika akawaambia, Ndugu
zangu, ningawa sikufanya neno kinyume cha watu wetu wala neno lililopingamana
na desturi za baba zetu, nalitiwa katika mikono ya Warumi, hali nimefungwa,
tokea Yerusalemu. Na hao walipokwisha kuniuliza-uliza walitaka kunifungua, kwa
maana hapakuwa na sababu yo yote kwangu ya kuuawa. Lakini Wayahudi walipotoa
hoja juu ya shauri hili nalishurutishwa kutaka rufani kwa Kaisari. Si kwamba
nalikuwa na neno la kuwashitaki watu wa taifa langu. Basi kwa ajili ya hayo,
nimewaita mje kunitazama na kusema nami; kwa maana nimefungwa kwa mnyororo huu
kwa ajili ya tumaini la Israeli. Wale wakamwambia, Sisi hatukupata nyaraka
zenye habari zako kutoka Uyahudi, wala hapana ndugu hata mmoja aliyefika hapa
na kutupasha habari, au kunena neno baya juu yako.”
Wazee wa kitahudi pale Rumi
hawakuwa na neno lolote kuhusu Paulo Mtume na walikiri kuwa hawakuwahi kupata
hata barua kuhusu Paulo mtume zilizotoka uyahudi, na hawa wayahudi waliosafiri
kutoka Israel hawakuwahi kmzungumzia Paulo Mtume lakini jambo moja tu walitaka
kujua habari ya dhehebu, kitu walichotaka kukisikia kutoka kwa Paulo na kutaka
uhakika kutoka kwake ni habari ya dhehebu lake kuwa linanenwa vibaya kila
mahali
Matendo 28:22 “Lakini tunataka kusikia
kwako uonavyo wewe; kwa maana katika habari za madhehebu hiyo imejulikana kwetu
kwamba inanenwa vibaya kila mahali.”
Wazee wa kiyahudi walikuwa
wamechoshwa kusikia kuwa kuna mamdhehebu mengi yametokea miongoni mwa wayahudi
na yanajulikana kila mahali lakini katika habari ya Madhehebu hii habari
imetukfikia kuwa inanenwa vibaya kila mahali, Wazee walimuuliza Paulo mtume
swali hili kwa sababu yeye hakuwa maarufu na watu walimchukia kiasi cha
kutokutaka kuzungumza habari zake, yeye alikuwa ni mtu aliyechukiwa na Wayahudi
wote kila mahali hata huko Asia uturuki ya leo, kila mahali alikokwenda sio
yeye tu watu wote waliomuhubiri Kristo walichukiwa na kuuawa wayahudi
walifikiri kuwa ukristo unaondoa taratibu zao na desturi zao
Matendo 6:8-14 8. “Na Stefano, akijaa neema
na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu. Lakini baadhi
ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la
Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na
Stefano; lakini hawakuweza kushindana na hiyo hekima na huyo Roho aliyesema
naye. Hata wakashawishi watu waliosema, Tumemsikia mtu huyu akinena maneno ya
kumtukana Musa na Mungu. Wakawataharakisha watu na wazee na waandishi,
wakamwendea, wakamkamata, wakampeleka mbele ya baraza. Wakasimamisha mashahidi
wa uongo waliosema, Mtu huyu haachi kusema maneno ya kufuru juu ya mahali hapa
patakatifu na juu ya torati; maana tumemsikia akisema kwamba Yesu huyo
Mnazareti atapaharibu mahali hapa, na kuzibadili desturi tulizopewa na Musa.”
Wayahudi walimuua Stefano kwa
sababu alimuhubiri Kristo akiyatumia maandiko kuthibitisha kuwa Yesu ni Masihi,
wayahudi walimshitaki Paulomtume pia kuwa ameingiza watu wa mataifa Hekaluni
Matendo 21:27-29 “Basi zile siku saba
zilipokuwa karibu kutimia, Wayahudi waliotoka Asia wakamwona ndani ya hekalu,
wakawataharakisha watu wote, wakamkamata,wakapiga kelele, na kusema, Enyi
wanaume wa Israeli, tusaidieni. Huyu ndiye mtu yule afundishaye watu wote kila
mahali kinyume cha taifa letu na torati na mahali hapa. Tena, zaidi ya haya,
amewaingiza Wayunani katika hekalu, akapatia unajisi mahali hapa patakatifu.
Kwa maana walikuwa wamemwona Trofimo, Mwefeso, pamoja naye mjini, ambaye
walidhania ya kuwa Paulo amemwingiza katika hekalu.”
Pia unaweza kuona kuwa wayahudi
kutoma Asia walimfanyia fujo kubwa Paulo mtume kule Thesalonike Wakati Paulo
mtume na Sila walipoihubiri injili, wayahudi walijaa wivu kuiona mafanikio ya
injili na wakawafuatia kwa ukaribu na kufanya ghasia kubwa sana ona
Matendo 17:1-14 “Wakiisha kupita kati ya
Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalonike, ambapo palikuwa na sinagogi la
Wayahudi. Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo,
akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu, akiyafunua na kuwaeleza ya
kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu
huyu ninayewapasha ninyi habari zake ndiye Kristo. Wengine miongoni mwao
wakaamini, wakashikamana na Paulo na Sila; na Wayunani waliomcha Mungu, wengi
sana, na wanawake wenye cheo si wachache. Na Wayahudi wakaona wivu,
wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio na sifa njema, nao
wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya
Yasoni, wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji; na walipowakosa, wakamkokota
Yasoni na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema,
Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika huku nako, na Yasoni amewakaribisha;
na hawa wote wanatenda mambo yaliyo kinyume cha amri za Kaisari, wakisema na
kwamba yupo mfalme mwingine, aitwaye Yesu. Wakafadhaisha ule mkutano na wakubwa
wa mji walipoyasikia hayo. Nao walipokwisha kumtoza dhamana Yasoni na wenziwe
wakawaacha waende zao. Mara hao ndugu wakawapeleka Paulo na Sila usiku hata
Beroya. Nao walipofika huko wakaingia katika sinagogi la Wayahudi. Watu hawa
walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa
uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo
ndivyo yalivyo. Basi watu wengi miongoni mwao wakaamini, na wanawake wa
Kiyunani wenye cheo, na wanaume si wachache. Lakini Wayahudi wa Thesalonike
walipopata habari ya kwamba neno la Mungu linahubiriwa na Paulo hata katika
Beroya, wakaenda huko nako wakawachafua na kuwafadhaisha makutano. Mara hiyo
wale ndugu wakampeleka Paulo aende zake mpaka pwani; bali Sila na Timotheo
wakasalia huko.”
Ukristo na wahubiri wa kweli
hawakuweza kukubalika kirahisi, Paulo mtume na washirika wake walipingwa kila
mahali, nyakati za kanisa la kwanza injili haikuwa rahisi, ibilisi aliwatumia
wayahudi kuhakikisha kuwa wanafanya fujo na kuharibu kabisa mpango wa Mungu
hata kwa kukodi, watu wasio na sifa
njema ili mradi tu kuharibu haklinya hewa, na kuuahribu Ukristo, Wayahudi kutoa
sehemu mbalimbali duniani walikuwa wamekwenda Yerusalem mara kadhaa katika siku
kuu mbalimbali na inawezekana walikutana
na Wayahudi kutoa Asia ambao waliwatahadharisha kuhusu Ukristo kuwa ni
madhehebu yasiyofaa kuna wakati ambapo hata Kaisari aliwafukuza wakristo
waondoke Rumi kwa sababu ilifikiriwa kuwa wana imani tofauti mwaka wa 49AD
Baada ya Kristo ona
Matendo 18:1-2 “Baada ya mambo hayo, Paulo
akatoka Athene akafika Korintho. Akamwona Myahudi mmoja, jina lake Akila,
mzalia wa Ponto; naye amekuja kutoka nchi ya Italia siku za karibu, pamoja na
Prisila mkewe, kwa sababu Klaudio amewaamuru Wayahudi wote watoke Rumi, naye akafikilia
kwao;”
Hata hivyo habari njema ni kuwa
Wayahudi wa Rumi na hawakumpokea Paulo kwa fujo na hivyo walimsikiliza na
hawakumshutumu kwa lolote lakini walitaka kusikia kutoka kwake, kuwa hawa watu
wayahudi wanaomuhubiri Yesu kuwa ni masihi awathibitishie maana kila mahali
hawa wanaomuhubiri Kristo kwa dhati wananenwa vibaya kila mahali hu ni uzushi
au ni ukweli, huyu Masihi mnayemuhubiri ni kweli au ni uzushi? Hivyo walitaka
kusikia Kutoka kwa Paulo Mtume kwamba hiki sasa ndio chanzo cha ukweli wa habari
zote ambazo tumekuwa tukizisikia tunataka kusikia kutoka kwako hii ikoje katika
habari ya madhehebu hii inanenwa vibaya
Kwa
nini Dhehebu hili linanenwa vibaya!
1.
Walimuhubiri
Christo.
Kristo
Yesu, mateso yake kufa kwake na kufufuka kwake ilikuwa ndio kiini kiku cha
ujumbe wa wahubiri wa nyakati za kanisa la kwanza, Nyakati za kanisa la kwanza
wahubiri waliwaelekeza watu kwa Yesu, wakliwathibitishia wayahudi kwa wayunani
kuwa Kristo ni Bwana, mahubiri yenye nguvu kupita yote ni yale ambayo kiini cha
ujumbe wake ni Yesu, waelekeze watu kwa Yesu, sio dhebu lako, sio kwa mchungaji
wako, waimarishe watu wasimame imara katika imani wakimtegemea Yesu, Paulo
mtume na timu yake ya umisheni na uinjilisti hawakupeleka khadithi kwa watu
walipeleka neno la Mungu, hawakupeleka hekima za wanadamu, walilihubiri neno
lililothibitishwa kwa ishara na miujiza ya jina la Yesu jambo hili liliwafanya kunenwa vibaya kila
mahali. Ona;-
1Wakoritho 1:22-24 “Kwa
sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta HEKIMA; BALI SISI
TUNAMHUBIRI KRISTO, ALIYESULIBIWA; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni
upuzi; bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na
hekima ya Mungu”
Dhehebu au
mtu awaye yote anayemuhubiri Kristo hawezi kufurahiwa, shetani hawezi kufurahi
watu wamuhubiri Kristo shetani anataka mahubiri ya aina nyingine anataka watu
wahubiri uponyaji na wa mwilini ambao ni wa kitambo na mafanikio ya mwilini ambayo pia ni ya kitambo,
lakini ile injili ya kweli ya kuwaelekeza watu kwa Yesu, na kubadilisha desturi
za watu waache tabia mbaya, waishi maisha matakatifu, waache uchawi, waache
ushirikina, wabadilike biashara ya uaguzi iharibike kamwe shetani haitaki
injili ya aina hiyo wala hawezi kuikubali, unapomuhubiri Kirsto Kuzimu hakuwezi
kufurahia na ndio maana nyakati za Kanisa la kwanza waliigundua siri kwamba
nguvu ya kweli iko katika kumuhubiri Kristo, hivyo kila Muhubiri wa nyakati za
kanisa la kwanza alipohubiri Kristo ndio ilikuwa kiini cha somo lake na matokeo yalikuwa makubwa sana nay a
kushangaza ona
Matendo 5:42 “Na
kila siku, ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kuhubiri
habari njema za YESU KWAMBA NI KRISTO.”
Matendo 8:4-5 “Lakini
wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno. Filipo akatelemka
akaingia mji wa Samaria, AKAWAHUBIRI KRISTO.”
Matendo 4:18-20 “Wakawaita,
wakawaamuru wasiseme kabisa wala kufundisha KWA JINA LA YESU. Petro na Yohana
wakawajibu wakawaambia, Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko
Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo
tuliyoyaona na kuyasikia.”
Mahali
popote au dhehebu lolote au taasisi yoyote ambapo Yesu anatajwa na kuelezewa
vema, shetani hawezi kukubali mahali hapo panenwe vizuri, Jina la Yesu lina
nguvu uwezo na mamlaka ya kuokoa na kuwaelimisha watu na kuwastaarabisha na
kuwaponya na kuwaleta katika kiwango kikinge, kwa sababu hiyo kila mahali
ambapo Kirtso anahubiriwa kwa dhati mahali hapo hapawezi kunenwa vema! Wapanene
vema kwa lipi ilihali biashara zao zinaharibiwa, biashara ya tabia mbaya na
ukahaba, na wizi, na ulevi na mapinduzi makubwa yanatokea watafurahishwa vipi,
ni kwaajili ya haya katika habari ya madhehebu hiyo inanenwa vema!
2.
Walikazia
kuwa viwango visivyo vya ulimwengu huu.
Kanisa au
dhehebu tamu ni lile ambalo wahubiri wake wanakazia viwango, wanawaelekeza watu
kuishi kwa viwango vya juu zaidi vya kibiblia, hawalichuji neno la Mungu wala
kulighoshi wanakaza, injili za kina Paulo mtume zilikaza wazi wazi wala
msiifuatishe namna ya dunia hii ona
Warumi 12:2 “Wala
msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate
kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.”
Watu au
wakristo wanaoishi kwa viwango vya juu anavyovitaka Kristo na wahubiri
wakikazia viwango anacvyovotaka Kristo shetani hawezi kufurahia, dunia haiwezi
kukuinena vema, utasikia wanajifanya watakatifu sana sio wanajifanya maandiko
yanatuita sisi ni watakatifu, hatupaswi kuishi chini ya kiwango sisi sio wa ulimwengu huu na hivyo usufikiri
kuwa dunia itakukubali, ikukubali kwa lipi, ikuunge mkono kwa lipi lazima
unenwe vibaya
Yohana 15:18 -19 “Iwapo
ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia
ninyi. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa
kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu
hiyo ulimwengu huwachukia.”
Sisi
tumechaguliwa na Yesu, na sisi sio wa ulimwengu huu, hatuwezi kukubaliwa na
ulimwengu, Mkristowa kweli ukiona unakubalika tu kila mahali lazima ujihoji,
sisi sio wa kawaida Yesu ametuambia lazima ulimwengu utuchukie na kama
utatuchukia utatunena vizuri kwa lipi ? sisi ni ukuhani mteule, taifa takatifu
watu wa miliki ya Mungu, tumeitwa kutoka gizani sisi ni nuru giza hakliwezi
kuwa na furaha na sisi hata kidogo, hivyo kama wanasengenya wasengenye sana,
kama wanaroga waroge sana, kama wanakosoa wakosoe sana katika habari ya
madhehebu hii inanenwa vibaya hii
1Petro 2:9 -10 “Bali
ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya
Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie
katika nuru yake ya ajabu; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa
la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.”
Unaona
kumbe kama dhehebu au kanisa au wahubiri na waamini wataishi maisha ya kiwango
kile Mungu alichotuitia ulimwengu hauwezi kufurahia hata kidogo, watufurahie
kwa lipi kama hatuna urafiki na dunia
Yakobo 4:4 “Enyi
wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila
atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.”
Unaona
nyakati za kanisa la kwanza watu walikuwa serious hawakuwa na mchezo walivunja
urafiki na dunia, hawakuwa na mahusiano ya kijinga na watu wasioamini, unadhani
dunia ingewakubalije, unadhani wangesifiwa unadhani wangenenwa vema?
2Wakoritho 6:14-18 “Msifungiwe
nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki
gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena
pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani
pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na
sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya
kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao
watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana,
Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi
mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike”
Yesu
alieleza wazi kuwa kwa kumfuata yeye na kumuamini hali haiwezi kuwa nzuri kwa
dunia lazima watatuchukia, watatutesa, watatuua, na tunaweza kuchukiwa na
mataifa yote kwaajili ya Kristo,
Mathayo 24:9 “Wakati
huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa
kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu.”
Moyo wangu
unalibeba jina la Yesu unamuamini Yesu, nimejitenga na dunia, nimevunja urafiki
na watu waovu, naishi maisha ya mfano nakazaia utakatifu naonyesha namna
tunavyotakiwa kuvaa kwa nidhamu, naonyesha namna inavyotupasa kuabudu
kumuheshimu Mungu naelekeza watu kwa Yesu, naishi maisha ya kiwango kisha
unatarajia dunia inipende inipende kwa lipi? Katika habari ya madhehebu hii imejulikana kwetu
kuwa inanenwa vibaya kila mahali!
3.
Waliihubiri
kweli!
Wanadamu
huwa wanachukia ukweli, watu wengi hawapendi kuambiwa ukweli, ukitaka kuchukiwa
wewe uwe tu msema kweli, utaona, watu wana mambo yao na wanataka wasiambiwe,
ukiwaambia tu tayari unakosana nao kwa sababu watu wanapenda uongo na wanataka
kudanganywa na ndio maana utaina imani za ajabu ajabu zenye usanii mwingi
zinakubalika na kujaza watu wengi, wewe nyoosha maelezo utaona kimsingi
tunapomuhubiri Yesu tunahubiri ukweli yeye ndio njia na kweli na uzima Yohana 14:6 “Yesu
akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa
njia ya mimi.” Tunapolihubiri neno la Mungu na kulitumia kwa halali
tunaihubiri kweli Yohana 17:17 “Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.” Kwa
msingi huo unapotaka kuwa na uadui na watu na ukitaka watu wakuchukie wewe uwe
msema kweli, moja ya sababu ya Ndugu zake Yusufu kumchukia na hata kutaka
kumuua ukiacha ndoto zake ni kwa sababu Yusufu alikuwa mkweli alipopeleka
ripoti ya mambo yao kwa baba yake
aliipeleka kama ilivyo
Mwanzo 37:2-4 “Hivi
ndivyo vizazi vya Yakobo. Yusufu, aliyekuwa mwenye miaka kumi na saba, alikuwa
akichunga kondoo pamoja na ndugu zake; naye alikuwa kijana pamoja na wana wa
Bilha, na wana wa Zilpa, wake wa baba yake. Yusufu akamletea baba yao habari
zao mbaya. Basi Israeli akampenda Yusufu kuliko wanawe wote, maana ni mwana wa
uzee wake, akamfanyia kanzu ndefu. Ndugu zake wakaona ya kuwa baba yao
anampenda kuliko ndugu zake wote, wakamchukia, wala hawakuweza kusema naye kwa
amani.”
Nyakati za
Kanisa la kwanza wahubiri hawakuwapaka watu mafuta kwa mgongo wa chupa
walipeleka injili kavukavu na ukweli wake wote bila kuichuja jambo hili
liliwafanya waonekane kuwa maadui ona Wagalatia
4:16 “Je! Nimekuwa adui wenu kwa sababu nawaambia
yaliyo kweli?” watu katika
ulimwengu huu wana mambo yao na yana faida klatika akili zao na hivyo sio
rahisi kukubali mabadiliko anapotokea mtu kuwaambia ukweli wanachukia, dunia ya
leo inahitaji kuhubiriwa kweli, mitume walihubniri ukweli, manabii walisema
ukweli, wengine waliuawa kwa sababu ya kusema ukweli madhahebu haya yalinenwa
vibaya kila mahali kwa sababu watu hawataki kuambiwa ukweli ona
Warumi 1:16-22 “Kwa
maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa
kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia. Kwa maana haki ya Mungu
inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye
haki ataishi kwa imani. Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka
mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu. Kwa
kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu
aliwadhihirishia. Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu
yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu
wake; hata wasiwe na udhuru; kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama
ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao
yenye ujinga ikatiwa giza. Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;” Pale
stefano alipowaambia watu ukweli walimsagia meno na wakamuua kwanini basi
dhehebu linalohubiri kweli lisinenwe vibaya kila mahali.
4.
Shetani amepofusha fikra zao:
Kuna mambo
mengi sana yanayowafanya watu wawe vipofu wa kiroho, wakati mwingine shetani,
wakati mwingine kiburi, wakati mwingine ujinga, wakati mwingine kupuuzia,
wakati mwingine kuongozwa na viongozi vipofu, wakati mwingine kufuata mkumbo,
wakati mwingine kurithi na kadhalika, au kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu
huu, unapkuwa kipofu kwa sababu yoyote
ile kati ya hizo huwezi kuona Yesu katika ubora wake kwa sababu maarifa yako na
ujuzi wako unapigwa upofu ili usihifahamu kweli ambayo inatabia ya kukuweka
huru
Yohana 8:31-32 “Basi
Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu,
mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli
itawaweka huru.” Kazi mojawapo kubwa anayoifanya shetani pamoja
na nyenzo zake nyingine ni kupofusha fikra na hivyo kuwafanya watu wawe wagumu
na wawe vipofu ili wasimjue Yesu na nuru ya injili isiwazukie
2Wakoritho 4:3-4 “Lakini
ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao
mungu wa dunia hii AMEPOFUSHA FIKIRA ZAO wasioamini, isiwazukie nuru ya injili
ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.” Unaona watu ambao fikra zao zimepofushwa
na ibilisi hawawezi kuona utamu wa injili ya Bwana Yesu wao wataipinga tu wao
ni vipofu hawawezi kuona ni watu wa dunia hii wanafuata kawaida ya ulimwengu
huu wako chini ya mkuu wa anga hili ambaye anatenda kazi kwa wana wa kuasi waefeso 2:1-2 “Nanyi
mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa
kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga,
roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi;” unaona kwa
msingi huo hawawezi kamwe kuisifia kazi ya injili na badala yake itanenwa
vibaya kila mahali, wengine kwa sababu ya kiburi na wengine kwa sababu ya kukaa
chini ya viongozi wasioifahamu kweli na kupata mafundisho potofu Mathayo 15:14 “Waacheni;
hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake,
watatumbukia shimoni wote wawili.” Kwa msingi huo wakati mwingine
sio rahisi mtu wa kawaida kujua maswala haya ya muhimu ya kiroho ni kwaajili ya
haya utaweza kuona katika habari ya madhehebu hii inanenwa vibaya kila mahali.
5.
Kwa sababu
ya tabia ya mwilini .
Kristo
Yesu amekuja kuwakomboa watu kwa jinsi ya Rohoni, ukiisha kusamehewa dhambi pia
unaponywa kwa msingi huo asili ya ukombozi wetu inaanzia rohoni, neno
linapohubiriwa ni mpaka mtu wa rohoni asikie ndipo na wa kawaida anaweza
kuelewa kwa msingi huo mtu wa mwilini hawezi kuyatambua mambo ya Roho wa Mungu
1Wakoritho 2:13-15 “Nayo
twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali
yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.
Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake
huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya
rohoni. Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu.”
Injili ni
swala la kiroho, hivyo uwezo wa kufasiri maswala ya rohoni unamuhitaji Mungu
ambaye ni Roho unahitaji msaada wa Roho Mtakatifu, ni vigumu kwa ulimwengu
kuitambua haya nan i vigumu kwa watu wa mwilini kuyatambua haya, ulimwengu
haujui kuwa Mungu Roho Mtakatifu yupo, haujui kuwa Roho Mtakatifu yuko kazini,
haujui kuwa yeye ni roho wa kweli, na hawawezi kumpokea maana hawamuoni
Yohana 14:16-20 “Nami
nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala
haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu. Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni
tena; bali ninyi mnaniona. Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai.
Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani
yangu, nami ndani yenu.”
Kuifahamu
injili, na kumfahamu Yesu kristo hakuji kwa akili za kibinadamu ni hekima
inayotoka kwa Mungu hivyo wanadamu wa kawaida huona kuwa ni ujinga na upuuzi
swala zima la injili na kwa sababu hiyo hawawezi kuzungumza jema kuhusu Ukristo
sahihi
1Wakoritho 1:18-20 “ Kwa sababu neno la msalaba kwao
wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. Kwa kuwa
imeandikwa, Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, Na akili zao wenye akili
nitazikataa. Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mlete hoja wa
zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu? ”
6.
Dunia
inamchukia Mungu
Kwa kawaida
dunia iko kinyume na Mungu na inamchukia Mungu, Nyakati za kanisa la kwanza
waliwaelekeza watu kwa Mungu na kulitangaza jina la Mungu, Dunia haimtaki Yesu
na inamchukia Yesu na inachukia jina lake nyakati za kanisa la kwanza
walimtangaza Yesu na walitii agizo lake la kuipeleka injili, Yesu alikwisha
kuonya kuwa wale waifanyao kazi hiyo kwa dhati na kwa moyo watachukiwa
udhihirisho wa chuki hiyo ni pamoja na kunenwa vibaya Mathayo 10:22 “Nanyi mtakuwa mkichukiwa na
watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye
atakayeokoka,” unaona ni wazi kuwa Yesu alijua kuwa wanafunzi wake
wa kweli watachukiwa na watachukiwa
kwaajili ya jina lake ni wazi kabisa kuwa Yesu anajua kuwa kwa chuki hizo watu
hawawezi kulinenea vizuri kanisa la kweli nah ii ni kwa sababu ulimwengu
unamchukia Mungu na hivyo sio ajabu kuchukia mali yake
Yohana 15:18 -19 “Iwapo
ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia
ninyi. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa
kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu
hiyo ulimwengu huwachukia”
Maandiko
yako wazi kuwa watu wa ulimwengu huu ni waovu, wenye tama, wenye chuki, wenye
wivu, wauaji, wagomvi, wadanganyifu, matapeli, wachawi, wasengenyaji, wambeya,
wenye kumchukia Mungu, wenye kiburi na majivuno, wenye kujisifu, wasiotii
wazazi wao, wenye nia mbaya wenye ujuzi wa kutenda maovu kuliko mema, wenye
kuvunja mapatano, wasio na huruma wenye mioyo mibovu wasiotii wazazi unategemea
watu kama hawa watalipenda kanisa ambalo liko kinyume na njia zao, linakemea uovu na kuonyesha njia ya
haki sio rahisi
Warumi 1:28-30 “Na
kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate
akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa. Wamejawa na udhalimu wa kila
namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na
hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya,wenye kusingizia, wenye kumchukia
Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya,
wasiowatii wazazi wao, wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda
jamaa zao, wasio na rehema; ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya
kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu,
bali wanakubaliana nao wayatendao”
na maandiko yanaonyesha wazi kuwa pia huenda wako watu wengi wanaomchukia Mungu pasipo
sababuna pia wanaowachukia watu wa Mungu pasipo sababu ni wengi Daudi
alichukiwa pasipo sababu alikuwa na maadui wengi ijapokuwa hakuwa mtenda maovu
ona
Zaburi 69:4 “Wanaonichukia bure ni wengi
Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari, Adui
zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nalilipishwa kwa nguvu Vitu
nisivyovichukua”. Dunia inamchukia Mungu na neno lake kwa sababu
linawashuhudia kuwa ni waovu Yohana 7:7
“Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi; bali
hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu”
unaona kanisa la kwanza hawakukubali kukalia kimya uovu waliukemea
waliushuhudia kuwa haukuwa sahihi waliwaonyesha njia, hali kadhalika kazi hii
ndio aliyoifanya Yesu alikema unafiki wa kidini, alionya na kuelekeza ibada
sahihi na namna sahihi ya kumuabudu Mungu je unatarajia kama kanisa au dhebu
litayatenda haya au mimi na wewe tutayafanya haya je tutanenwa vizuri kila
mahali? Katika habari ya madhehebu hiyo imejulikana kwetu kuwa inanenwa vibaya.
7.
Kumfuata
Yesu sio rahisi.
Nyakati za
kanisa la kwanza mafundishi kuhusu dhiki nha udhia yalikuwa ni mojawapo ya
nguzio muhimu sana ya Ukristo, wakristio waliteseka kwa namna na kwa njia mbali
mbali ilikuwa kama kuchagua injili ni kuchagua njia ya mateso na mitume
waliweka wazi hili kama msingi wa mafundisho yao na ya Kristo
Matendo 14:21-22 “Hata
walipokwisha kuihubiri Injili katika mji ule, na kupata wanafunzi wengi,
wakarejea mpaka Listra na Ikonio na Antiokia, wakifanya imara roho za wanafunzi
na kuwaonya wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika
ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi.”
1Petro 1:6 -7 “Mnafurahi
sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima,
mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali; ili kwamba kujaribiwa kwa imani
yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa
kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa
kwake Yesu Kristo”.
Unaona
tangu mwanzo Yesu alikuwa amekwisha kuonya kuwa kufuata yeye sio lele mama
nyakati za leo injili zilizojaa mitaani ni za mafanikio na vitu vya duniani,
injili za nyakati zetu mkazo ulikuwa ni
huu hapa IMETUPASA KUINGIA KATIKA UFALME
WA MUNGU KWA NJIA YA DHIKI NYINGI, injili
za leo ni kutesa duiniani na mbinguni ahaaaa tunapoteza muelekeo sio
kuwa naunga mkono mateso hakuna mtu anapenda mateso lakini sisi ambao tumepata
rata commitment zetu ni tofauti sana na zile wanazopata watu wanaopitia shida kwa
ukweli Yesu hakuonyesha kuwa kazi ya injili ni lele,mama Luka 14:26-27 “Kama mtu akija kwangu naye
hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume
na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Mtu
ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi
wangu”. Lakini watu wengi
sana leo wanajihurumia na wanapoutazama Ukristo wa kweli na kuona msimamo wa
aina hii ni wazi kabisa kuwa hawawezi kuzungumza mazuri kwa kuona watu ambao
wana misimamo mikali na wanasonga mbele bila kujali kuwa wanapitia changamoto
gani watu ambao wako tayari kuzipoteza nafsi zao kuliko kuziokoa Mathayo 16:24-26 “Wakati
huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane
mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi
yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.
Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi
yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? ”
Misimamo
hii na misingi hii ndio ilikuwa misimamo ya Paulo mtuma na ilikuwa ni misimamo
ya injili waliyoihubiri na ilikuwa misimamo ya kanisa la nyakati za kanisa la
kwanza ni kwaajili ya haya watu wa ulimwengu ule walichukizwa na misimamo yao
na kuona kuwa watu hawa wanaupindua ulimwengu na kubadili desturi za kilimwengu
na kuuleta umayi kwa Yesu hivyo shetani alitumia silaya ya kuinena vibaya
lakini wazee wa kirumi waliomfuata Paulo wao walikuwa waungwana na wenye hekima
hawakutaka kusikia tu walimuuliza Paulo mtume mwenyewe wakitaka kusikia kutoka
kwake kwanini katika habari ya madhehebu hii inannenwa vibaya ?
Bwana
atupe neema kanisa la leo ili tusinenwe vibaya kwa ubaya badala yake tunanene
vibaya kwa sababu ya viwango vya kujitoa kwetu kwa Mungu kuwa vya hakli ya njuu
kiasi cha kuuchanganya ulimwengu, ni maombi yangu kuwa tutasimama imara na
kuendelea kuipeleka injili mpaka Yesu afurahi barikiwa!
Na mkuu wa
wajenzi mwenye Hekima
Rev.
Innocent Kamote