Matendo 9:22 “Sauli akazidi kuwa hodari, akawatia fadhaa
Wayahudi waliokaa Dameski, akithibitisha ya kuwa huyu ndiye Kristo”
Utangulizi:
Tunasoma Katika maandiko ya
kwamba watu wengi wanaotajwa kama mashujaa wa Imani katika biblia, kwamba
walikuwa hodari ona katika
Waebrania 11:32-34 “Nami
niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka
na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii; ambao kwa imani
walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa
vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa
nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya
wageni.”
Kwa msingi huo ni kama
kusema watu wote wenye mafanikio na wanaondelea kufanikiwa katika ulimwengu
walikuwa na uhodari ndani mwao na huu uhodari pia unaweza kuzidi zaidi na
zaidi, maandiko yanatueleza kuwa Sauli akazidi kuwa hodari hii maana yake ni
kuwa alikuwa hodari na akaendelea kuwa hodari, kuwa hodari na hata kujilinda na
kuendelea katika uhodari huo sio jambo jepesi, kuna mambo ambayo ukiyafanya
utazidi kuwa hodari katika maisha yako, kabla ya kuzungumiza jinsi ya kuzidi
kuwa hodari, ni muhimu kwetu tukajifunza somo hili jinsi ya kuzidi kuwa Hodari
kwa kuzingatia vipengele viwili vifuatavyo:-
·
Maana ya neno Hodari
·
Jinsi ya kuzidi kuwa Hodari
Maana ya Neno
Uhodari:-
Neno hodari limetajwa mara
kadhaa katika maandiko, Kila mtu anayetajwa katika maandiko anatajwa vilevile
kuwa alikuwa na uhodari hususani wale wote ambao walikuwa maarufu na ambao
Mungu aliwatumia kwa viwango vya juu katika maandiko kwa mfano tunasoma katika
Matendo 7:22 “Musa
akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa hodari wa maneno na matendo.”
Unaona tunasoma kuwa Musa
alifundishwa Hekima yote ya Wamisri, akawa Hodari wa maneno na matendo, kwa
msingi huo basi ili tuweze kufanikiwa katika maisha yetu na tusiweze
kuharibikiwa hatuna budi kuhakikisha ya kwamba katika kila Nyanja ya maisha yetu tunapaswa kuwa na
uhodari, na kuzidi.
Matendo 18:24-26
“Basi
Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzalia wa Iskanderia, mtu wa elimu, akafika
Efeso; naye alikuwa hodari katika maandiko. Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia
ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha
kwa usahihi habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohana tu. Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi;
hata Prisila na Akila walipomsikia wakamchukua kwao, wakamweleza njia ya Bwana
kwa usahihi zaidi.”
Kwa hiyo utaona hivyo tena
na tena katika maandiko kila wakati neno uhodari likijirudia tena na tena kwa
watu waliokuwa na kitu cha ziada kwa msingi huo ni muhimu kwetu kuwa na ufahamu
wa kutosha ili tuweze kujua ni nini maana ya neno hodari au na kwanini agizo la
Mungu katika maandiko linatutaka kuwa hodari ona
Joshua 1:6-7 “Uwe
hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii
niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa. Uwe hodari tu na ushujaa mwingi,
uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu;
usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila
uendako.”:-
Sasa basi ni nini maana ya
kuwa Hodari? Manoneo yanayotumika katika maandiko kuelezea maana ya kuwa hodari
katika lugha ya kiingereza ni pamoja na:-
Be strong and Courageous Be
powerful ambalo maneno mengine yanayorumika sambaba na neno hili ni Capable,
Forceful, Mighty, Potent, powerful, Fit na kadhalika, Hata hivyo neno hilo
katika lugha ya kivita waebrania wanatumia neno “MARSHAL” ambalo mara
nyingi au chache hutumika kwa maofisa wa jeshi wa ngazi ya juu kabisa wenye
weledi wa kufanya mambo ya kupita kawaida, au kufanya mambo zaidi ya jinsi
ulivyofundishwa katika Nyanja ya kijeshi ni Fidel Marshal – is the most senior
military rank, or ordinary senior to the General officer ranks, usually it is
the highest rank ina an army, and such few persons are appointed to it Kwa hiyo tunapozungumzia mtu Hodari ni yule
anayefanya mambo kwa weledi, au kwa ubora zaidi ya jinsi alivyoelekezwa na
kufundishwa ! kwa hiyo maandiko
yanapozungumzia wale mashujaa wa imani kuwa walikuwa hodari maana yake walikuwa
na rank za juu zaidi za kijeshi, walifanya mambo kwa weledi kwa viwango vya juu
zaidi ya jinsi ya walivyofundishwa
Waebrania 11:32-34 “Nami
niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka
na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii; ambao kwa imani
walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa
vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa
nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya
wageni.”
Kwa msingi huo sasa Mungu anatutaka na sisi
tuwe hodari, lakini kama ni mahodari sasa tuzidi kuwa hodari unaona sasa basi
ni kwa jinsi gani tunaweza kuzidi kuwa Hodari?
1.
Uwe mtu wa Haki
A man of integrity he is or she is a person who is
value what is honest, true, noble, trustworthy, kind and right ahead of
Personal gain yaani ni mtu mwenye kupenda kweli, mwenye kustahi, mwenye kutenda
haki, msafi asiye na lawama, mwema na mwenye sifa njema
Waefeso 4:8 “Hatimaye,
ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote
yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye
sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.”
Mtu wa haki anatembea na uwepo wa Mungu, au Mungu
hufanya masikani yake au atadumu katika vizazi vyake atadumu katika uwepo wa
Mungu atakaa katika masikani za Mungu atafanikiwa
Zaburi
15:1-3 “Bwana, ni nani atakayekaa Katika hema yako? Ni nani
atakayefanya maskani yake Katika kilima chako kitakatifu? Ni mtu aendaye kwa
ukamilifu, Na kutenda haki. Asemaye kweli kwa moyo wake, Asiyesingizia kwa
ulimi wake. Wala hakumtenda mwenziwe mabaya, Wala hakumsengenya jirani yake.”
Unapochunguza maisha ya watu Hodari utaweza kuona
moja ya sifa wanayotajwa kuwa nayo ni kutenda haki, hawakuwa na hila ndani yao
andiko lile katika Waebrania linasisitiza kuwa mashujaa wa imani walitenda haki
sasa basi ikiwa tutaishi maisha ya haki tutazidi kuwa hodari kwa sababu Mungu
atatubariki ona
Zaburi
119:1 -3 “Heri walio kamili
njia zao, Waendao katika sheria ya Bwana. Heri wazitiio shuhuda zake,
Wamtafutao kwa moyo wote. Naam, hawakutenda ubatili, Wamekwenda katika njia
zake.”
2.
Uwe na dhamiri Njema
Ni muhimu kufahamu kuwa watu Hodari vilevile ni watu
wanaokuwa na dhamiri njema, kila unalilifanya unalifanya bila unafiki, Maandiko
yanawataka wakristo kuwa na dhamiri njema ni muhimu kukumbuka kuwa Mungu
hatahukumu matendo ya nje Mungu anaangalia ndani ya moyo na kupima dhamiri
yetu, Neno dhamiri katila lugha ya kiyunani ni SUNOIDA Neno hili
limetajwa mara 34 katika agano jipya mara nne katika injli na kitabu cha
matendo ya mitume lakini mara 30 katika nyaraka ka Mtume Paulo wakati wote
akisisitiza watu kuwa na dhamiri njema, kutokufanya jambo kwaajili ya
unafiki, ona
1Timotheo
1:5-6 “Walakini mwisho wa agizo hilo ni upendo utokao
katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki. Wengine
wakiyakosa hayo wamegeukia maneno ya ubatili”
1Timotheo
1:18-20 “Mwanangu Timotheo, nakukabidhi agizo hilo liwe
akiba, kwa ajili ya maneno ya unabii yaliyotangulia juu yako, ili katika hayo
uvipige vile vita vizuri; uwe mwenye imani na dhamiri njema, ambayo wengine
wameisukumia mbali, wakaangamia kwa habari ya Imani. Katika hao wamo Himenayo na Iskanda, ambao
nimempa Shetani watu hao, ili wafundishwe wasimtukane Mungu.”
Matendo
23:1 ”Paulo akawakazia macho watu wa baraza, akasema, Ndugu zangu,
mimi kwa dhamiri safi kabisa nimeishi mbele za Mungu hata leo hivi.”
Matendo
24:16 “Nami ninajizoeza katika neno hili niwe na dhamiri
isiyo na hatia mbele za Mungu na mbele ya watu siku zote”
1Timotheo
3:8-10 “Vivyo hivyo mashemasi na wawe wastahivu; si wenye
kauli mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana, si watu wanaotamani fedha ya
aibu.wakiishika siri ya imani katika dhamiri safi. Hawa pia na wajaribiwe
kwanza; baadaye waitende kazi ya shemasi, wakiisha kuonekana kuwa hawana hatia.”
Muda usingeweza kutosha kuona namna maandiko
yanavyokazia tena na tena swala la kuwa na Dhamiri njema SUNOIDA kumfikiri
Mungu na wanadamu 2Wakoritho 8:20-21 “Tukijiepusha na neno
hili, mtu asije akatulaumu kwa habari ya karama hii tunayoitumikia;
tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele za Bwana tu, ila na mbele ya
wanadamu.”
3.
Endelea kujisomea siku zote
Ni muhimu kufahamu kuwa watu waliokuwa hodari
vilevile na wanaozidi kuwa Hodari huwa wanasoma na wanajiendeleza katika
maarifa, maandiko yanaonyesha kuwa kadiri mtu anavyosoma ndivyo anavyoongeza ufahamu
wake zaidi ona
Mathayo
24:15 “Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile
lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na
afahamu),”
Kusoma kunaleta ugunduzi wa siri nyingi sana za
kimaandiko Nabii Daniel aligundua kuwa siku za kukaa kwao utumwani zilitabiriwa
kuwa ni miaka 70 na hivyo kwa kusoma vitabu alighundua kuwa wakati huo umefika
na akaanza kumuomba Mungu ona
Daniel
9:1-3 “Katika mwaka wa kwanza wa Dario, mwana wa Ahasuero,
wa uzao wa Wamedi, aliyetawazwa kuwa mfalme juu ya milki ya Wakaldayo; katika
mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu,
nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya
kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini. Nikamwelekezea Bwana Mungu
uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za
magunia na majivu.”
Unaona kumbe Nabii Daniel aligundua baadhi ya mambo
kwa kusoma na akaingiza kumuomba Mungu, ziko siri nyingi zimefichwa katika
vitabu, hivyo watu wanaozigundua ni wale wanaosoma asomaye na afahamu, watu
wengi huwa wanashangazwa sana na hekima kubwa aliyokuwa nayo Paulo Mtume lakini
ukichunguza kwa undani utagundua kuwa mpaka anakuwa mzee alikuwa ni mtu mwenye
tabia ya kupenda kujisomea, hakufikiri kuwa amekwisha kufika lakini mara kwa
mara alitaka kujiendeleza na alikuwa na tabia ya kujisomea ona,
2Timotheo
4:13 “Lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa, ujapo ulilete, na
vile vitabu, hasa vile vya ngozi.”
Je wewe unajisomea? Unaongeza maarifa kwa kupenda
kujisomea? Kusoma kunaongeza maarifa na maarifa yanaongeza ujuzi na ujuzi
unaleta weledi na kukufanya wewe kuwa Hodari.
4. Fanya maamuzi
sahihi
Moja ya mambo ambayo yanawaletea watu wengi sana majuto katika maisha yao
ni pamoja na swala zima la kufanya uamuzi, wako watu wengi sana ambao wanajutia
maamuzi waliyoyafanya na wanahitaji second chance, lakini imeshindikana kwa
sababu ya maamuzi yao! Mashujaa wa imani kila walipotaka kufanya jambo
hawakutumia akili zao, waliuliza kutoka kwa Bwana
1Samuel
23:1-3 “Kisha wakamwambia Daudi, kusema, Angalia,
Wafilisti wanapigana vita juu ya Keila na kuiba nafaka sakafuni mwa kupuria.
Basi Daudi akamwuliza Bwana, kusema, Je! Niende nikawapige hao Wafilisti? Naye
Bwana akamwambia Daudi, Nenda ukawapige Wafilisti, na kuuokoa Keila. Ila watu
wake Daudi wakamwambia, Tazama, sisi tunaogopa hapa katika Yuda; je! Si zaidi
tukienda Keila juu ya majeshi ya Wafilisti? Basi Daudi akamwuliza Bwana tena,
Naye Bwana akamjibu, akasema, Ondoka, ukashukie Keila; kwa kuwa nitawatia hao
Wafilisti mikononi mwako.”
1Samuel
23:9-13 “Naye Daudi alifahamu ya kuwa Sauli
amemkusudia mabaya; akamwambia Abiathari, kuhani, Lete hapa hiyo naivera. Ndipo
Daudi akasema, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, mimi mtumwa wako nimesikia hakika ya
kuwa Sauli anataka kuja huku Keila, ili kuuharibu mji kwa ajili yangu. Je! Watu
wa Keila watanitoa, nitiwe mkononi mwake? Je! Sauli atashuka, kama mtumwa wako
alivyosikia? Ee Bwana, Mungu wa Israeli, nakusihi, umwambie mtumwa wako. Naye
Bwana akamjibu, Atashuka. Ndipo Daudi akasema, Je! Watu wa Keila watanitia mimi
na watu wangu mkononi mwake Sauli? Bwana akasema, Watakutia. Basi Daudi na watu
wake, ambao wapata kama mia sita, wakaondoka na kutoka Keila, wakaenda po pote
walipoweza kwenda. Kisha Sauli akaambiwa ya kwamba Daudi amekimbia toka Keila;
akaacha kutoka nje"
1Samuel
30:8-9 “Daudi akauliza kwa Bwana, akasema, Je!
Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika
utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote. Basi Daudi akaenda, yeye na wale watu
mia sita waliokuwa pamoja naye, nao wakakifikilia kijito Besori, ambapo wale
walioachwa nyuma walikaa.”
Unaona Daudi kila alipokuwa anataka kufanya jambo aliuliza kutoka kwa
Bwana, kwanini alikuwa anafanya hivi ni ili aweze kufanya maamuzi sahihi bila
kutumia au kutegemea akili zake yeye mwenyewe maandiko yanasema hivi katika
Mithali3:5-6 “Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote,
Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye
atayanyosha mapito yako. Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche Bwana,
ukajiepushe na uovu.”
5. Hakikisha
unakuwa mnyenyekevu.
Wengi wetu tunatabia ya kupuuzia hali ya kuwa kujinyenyekeza, Mungu
anapotuinua tunainuka na kiburi, na kwa sababu hiyo inakuwa ngumu kwetu
kufundishika na hata kuonyeka, hasa pale tunapofikiri kuwa labda tuna akili
kuliko wengine, au tunaweza kujidhani kuwa sisi ni kitu maandiko yanaonya sana tabia ya kujiinua na
kujikweza na yanatufundisha kuwa wanyenyekevu, unyenyekevu huwa unalipa, Yesu
Kristo Bwana wetu aklifanikiwa sana kwa sababu alikuwa mnyenyekevu na Mungu
akamuadhimisha mno
Wafilipi 2:3-11 “Msitende neno
lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na
amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake
mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo
ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya
Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;
bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa
wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa
mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha
mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti
lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila
ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.”
Kanuni ya Mungu ya kumpeleka mtu juu ni mtu huyo kujishusha,
kujinyenyekeza, Yesu mwenyewe alisema hivi katika Luka 14:8-11 “Ukialikwa na mtu arusini, usiketi katika kiti cha mbele;
isiwe kwamba amealikwa mtu mwenye kustahiwa kuliko wewe, akaja yule
aliyewaalika wewe na yeye, na kukuambia, Mpishe huyu! Ndipo utakapoanza kwa
haya kushika mahali pa nyuma. Bali ukialikwa, nenda ukaketi mahali pa nyuma,
ili ajapo yule aliyekualika akuambie, Rafiki yangu, njoo huku mbele zaidi;
ndipo utakapokuwa na utukufu mbele ya wote walioketi pamoja nawe. Kwa maana
kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.”
Watu wengi sana duniani wanabadilika mno wanapopata madaraka au kibali,
au pale Mungu anapokuwa amekusudia kuwapeleka kwenye ngazi nyingine, wanapokuwa
wamefanikiwa hujisahau na kuwa na kiburi kiasi cha kutokytaka kuwasikiliza
wengine, hata watu wa Mungu huonekana kuwa wajinga na hawawezi kusikilizwa
katika nafasi yao
2Mambo ya
Nyakati 26:16-20 “Lakini alipokuwa na nguvu, moyo
wake ulitukuka, hata akafanya maovu, akamwasi Bwana, Mungu wake; kwani aliingia
hekaluni mwa Bwana, ili afukize uvumba juu ya madhabahu ya kufukizia. Azaria kuhani
akaingia nyuma yake, na pamoja naye makuhani themanini wa Bwana, mashujaa;
wakamzuia Uzia mfalme, wakamwambia, Si haki yako, Uzia, kumfukizia Bwana
uvumba, ila ni haki ya makuhani wana wa Haruni, waliofanywa wakfu, ili wafukize
uvumba; toka katika patakatifu; kwa kuwa umekosa; wala haitakuwa kwa heshima
yako kutoka kwa Bwana, Mungu. Akaghadhibika Uzia; naye alikuwa na chetezo
mkononi cha kufukizia uvumba; naye hapo alipowaghadhibikia makuhani, ukamtokea
ukoma katika paji la uso wake mbele ya makuhani nyumbani mwa Bwana karibu na
madhabahu ya kufukizia. Azaria kuhani mkuu na makuhani wote wakamtazama, na
angalia, alikuwa na ukoma pajini mwa uso, wakamtoa humo upesi; hata na yeye
mwenyewe akafanya haraka kutoka, kwa sababu Bwana amempiga.”
Unaona hii ni kanuni kubwa sana ya mafanikio kwa mashujaa wa imani, wengi
walifanikiwa kwa sababu walifahamu umuhimu wa kuwa wanyenyekevu, na wengine
tunawasoma kuwa kwa sababu ya kiburi waliasi na kupatwa na mabaya kanuni za
Mungu hazidanganyi kuwa kijapo kiburi ndipo ijapo aibu Mithali 11:2 “Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na
wanyenyekevu.” Ni kwaajili ya
haya sasa Ndipo Mungu anatutaka katika neno lake tuwe wanyenyekevu,
ukijinyenyekeza neema ya Mungu inakuwa kubwa sana, lakini kama hatutajua kanuni
ya kujinyenyekeza Mungu atapinga anasi yeye mwenyewe kwani ukiwa na kiburi
unashughulikiwa na Mungu 1Petro 5:5 “Vivyo hivyo
ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate
kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa
wanyenyekevu neema.”
6.
Uwe mwaminifu.
Hakuna jambo Muhimu katika maisha ya mwanadamu kama
uaminifu, kila mtu duniani anapenda mtu mwaminifu, hata mume mzinzi au mke mzinzi
bado anataka apatiwe uaminifu kutoka kwa mwenziwe, Maandiko yanatutaka tuwe
waaminifu, tena tuwe waaminifu hta kufa
Ufunuo
2:10 “Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa
baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe
mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.”
Kuwa
mwaminifu ni kujidhabihu, ni kujitoa, commitment- kiyunani DESMEFSI ambalo kwa tafasiri ya kiingereza ni
imprisonment - kujifunga au kufanya maamuzi magumu mfano hutafanya jambo Fulani
mapaka jambo Fulani limefanikiwa:-
1Samuel 6:9-11 “Ndipo
Yese akampitisha Shama. Naye akasema, wala Bwana hakumchagua huyu. Yese
akawapitisha wanawe saba mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, Bwana
hakuwachagua hawa. Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa?
Naye akasema, Amesalia mdogo wao, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli
akamwambia Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja
huku.”
Matendo 23:12 “Kulipopambauka,
Wayahudi wakafanya mapatano, wakajifunga kwa kiapo kwamba hawatakula wala
hawatakunywa hata wamwue Paulo.”
Esta 4:15-16 “Basi
Esta akawatuma ili wamjibu Mordekai, Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo
hapa Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu,
usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia
kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie.”
Kwa msingi
huo kuwa mwaminifu kuna maana ya kujifunga, lakini pia kusimamia kitu mpaka
kifanikiwe kwamba iwe ni jambo kubwa au kwamba ni jambo dogo, kwa mujibu wa
mafundisho ya Yesu Kristo yeye alisisitiza kuwa uaminifu pia unapimwa katika
kuanzia na mambo madogo madogo sana Yesu anaamini kuwa mtu akiwa muaminifu
katika jambo lililo dogo anaweza kuwa mwaminifu katika jambo lililo kubwa zaidi
Luka 16:10-12
“Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa
mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa
dhalimu katika lililo kubwa pia. Basi, kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali
ya udhalimu, ni nani atakayewapa amana mali ya kweli? Na kama hamkuwa waaminifu
katika mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe? ”
Watu wengi sana wameshindwa kuwa hodari
katia nafasi walizo nazo na vipawa walivyo navyo kwa sababu tu wameshindwa kuwa
waaminifu, Mungu anahitaji watu ambao ni waaminifu Uaminifu ni tabia ya Mungu
ili sisi nasi tuwe kama baba wa Mbinguni hatuna budi kuwa na tabia hii ya uungu
kwa kuwa waaminifu na Mungu atatufanikisha
Zaburi 145:17
“Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote, Na
mwenye fadhili juu ya kazi zake zote.”
Kwa msingi huo Mungu anatutaka sisi nasi tuwe waaminifu kwa kuingia
katika ushirika wa mwanawe ona
1Wakoritho
1:9 “Mungu ni mwaminifu ambaye mliitwa na yeye
mwingie katika ushirika wa Mwanawe, Yesu Kristo Bwana wetu.”
7. Lazima uwe na
uvumilivu
Watu hodari vilevile ni wavumilivu, au wenye subira ni vigumu sana kuwa
na mafanikio kwa njia rahisi rahisi, mafanikio yanawakuta watu wenye uwezo
mkubwa katika uvumilivu, tunaambiwa kuwa manqabii wote walikuwa wavumilivu sana
lakini vilevile tunaambiwa kuwa Ayubu alikuwa mvumilivu, Mungu anapoona
uvumilivu wetu hatimaye anatukumbuka na kutufadhili ona
Yakobo 5:
10-11 “Ndugu, watwaeni manabii walionena kwa jina
la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu. Angalieni,
twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona
mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.”
Hakuna mafanikio ya kufumba na kufumbua, wala mafanikio hayaji kwa usiku
mmoja, watu wote waliofanikiwa duniani walikuwa na tabia ya uvumilivu,
kujifunza kuwa wavumilivu kutatuletea hali ya kuzaa matunda, ukitaka kuwa na
afya imara lazima ufanye mazoezi, mazoezi sio kitu kitamu, utakimbia, utabeba
vitu vizito, utatembea na kufanya hili ama lile mambo ambayo yanahitaji
nidhambu ya hali ya juu, kwa ufupi uvumilivu ni nidhamu ya hali ya juu, kila
jambo litahitaji uvumilivu Yesu katika mfano wake ule wa mbegu alionyesha wazi
kuwa hata zile zinazozaa matunda huwa hazizai bila uvumilivu ona
Luka 8:11-15
“Na huo mfano, maana yake ni hii; Mbegu ni neno la
Mungu. Wale wa karibu na njia ndio wasikiao, kisha huja Ibilisi akaliondoa hilo
neno mioyoni mwao, wasije wakaamini na kuokoka. Na wale penye mwamba ndio wale
ambao wasikiapo hulipokea lile neno kwa furaha; nao hawana mizizi, huamini
kitambo kidogo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga. Na zilizoanguka penye miiba
ni wale waliosikia, na katika kuenenda kwao husongwa na shughuli na mali, na
anasa za maisha haya, wasiivishe lo lote. Na zile penye udongo mzuri, ndio wale
ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa
matunda kwa kuvumilia.”
Yakobo anatoa mfano wa Mkulima anavyovumilia mpaka kupata mazao, hakuna
kazi ngumu sana duniani kama kulima hasa kama ni kilimo kile cha kutumia mikono
lakini ukifuatilia maisha ya wakulima utaweza kuona na kujifunza kuwa ni watu
wenye imani na subira wanasubiri mpaka wakati wa Mavuno ufike, sisi nasi hatuna
budi kuwa wavumilivu na waaminifu na kufanya majukumu yetu ambayo Mungu ametupa
na kwa uvumilivu mkubwa tutafikia malengo na mafanikio na kuzidi kuwa hodari.
Yakobo 5:7 “Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama,
mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata
yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho.”
Unaona kwa msingi huo kila kitu kinahitaji uvumilivu, malezi yanahitaji
uvumilivu, uanafunzi unahitaji uvumilivu, ualimu unahitaji uvumilivu, uongozi
unahitaji uvumilivu, na kila tukifanyacho kinahitaji uvumilivu, kwa msingi huo
ili tuwezer kufanikiwa katika kila eneo la maisha yetu hatuna budi kuwa na
uvumilivu, na tunapovumilia tutaendelea kuwa hodari zaidi na zaidi.
8.
Jenga mazingira ya kuhitajika.
Maandiko yanasema hivi katika kitabu cha Mithali
14:4 “Zizi ni safi ambapo hapana ng'ombe; Bali nguvu za ng'ombe zaleta
faida nyingi.”
Maandiko yanatufundisha kuwa Ngombe wana faida kuwa
sana japo wakiwepo zizizni inaweza kuonekana kuwa wanachafua, na wakiwa hawapo
yaweza kuonekana kuwa zizi ni safi, lakini ni afadhali kuwa nao kwa sababu wana
faida kubwa sana , wao hulima na kusababisha mazao, tutupa nyama, hutupa
maziwa, hutupa ngozi na kadhalika, kimsingi tunajifunza umuhimu wa watu wenye
bidii, Mungu anataka ufanye kazi kwa bidii na kuwa mwenye faida ili ikiwezekana
watu wakuhitaji, watu maarufu katika Biblia waliitwa watu ambao ulimwengu
haukustahili kuwa nao
Waebrania
11:32-38 “Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha
kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na
za manabii; ambao kwa imani
walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa
vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa
nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya
wageni. Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa. Lakini wengine waliumizwa
vibaya hata kuuawa, wasikubali ukombozi, ili wapate ufufuo ulio bora; wengine
walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani;
walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga;
walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa
wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya; (watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa
nao), walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika na katika milima na katika
mapango na katika mashimo ya nchi.”
Popote ulipo jitume kwa bidii ili watu waone umuhimu
wako, uwe na ubunifu, na uwezo wa kujenga mpango utakaofanya wewe uhitajike na
uonekane umuhimu wako katika jamiii ona
Mwanzo 41:33-38 “Basi,
Farao na ajitafutie mtu wa akili na hekima amweke juu ya nchi ya Misri. Farao
na afanye hivi, tena akaweke wasimamizi juu ya nchi, na kutwaa sehemu ya tano
katika nchi ya Misri, katika miaka hii saba ya kushiba. Na wakusanye chakula
chote cha miaka hii myema ijayo, wakaweke akiba ya nafaka mkononi mwa Farao
wakakilinde kuwa chakula katika miji. Na hicho chakula kitakuwa akiba ya nchi
kwa ajili ya miaka hiyo saba ya njaa, itakayokuwa katika nchi ya Misri, nchi
isiharibike kwa njaa. Neno hilo likawa jema machoni pa Farao, na machoni pa
watumwa wake wote. Farao akawaambia
watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake?”
9.
Usiogope
Hofu ni mojawapo ya kifungo kikubwa sana, Mungu
hafurahii watu wanaoogopa, mtu anayeogopa
na siyejaribu ni kizuizi kikubwa sana na ndio maana mara kwa mara
utaweza kuona Mungu akiwataka watu wake wasiogope Yoshua 1:5-9 “Hapatakuwa
mtu ye yote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama
nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia
wala sitakuacha. Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha
watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa. Uwe hodari tu na
ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa
mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate
kufanikiwa sana kila uendako. Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako,
bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa
na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako,
kisha ndipo utakapositawi sana. Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo
wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja
nawe kila uendako.”
Kwa nini Mungu alimsisitiza Yoshua asiogope
kwa sababu woga uliwkosesha Israel Inchi ya kanaani kwa miaka mingi sana
walikosa urithi wao, watu wengin wanaotaka mtu asijaribu au mtu asifanikiwe
hujaribu kutumia hofu kama njia ya kukuwekea utisho ili uogope na usifanya
majaribio, katika wapelelezi wale walioipepeleza ichi ya kanaani kumi kati yao
walileta habari ya hofu na kuwatisha watu kiasi cha watu kuogopa na kujikosesha
nchi ya maziwa na asali
Hesabu
14:1-9 “Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia; watu
wakatoka machozi usiku ule. Kisha wana wa Israeli wote wakamnung'unikia Musa na
Haruni; mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya
Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili. Mbona Bwana
anatuleta mpaka nchi hii ili tuanguke kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu
watakuwa mateka; je! Si afadhali turudi Misri? Wakaambiana, Na tumweke mtu
mmoja awe akida, tukarudi Misri. Ndipo Musa na Haruni wakaanguka kifudifudi
mbele ya mkutano wa kusanyiko la wana wa Israeli. Na Yoshua mwana wa Nuni, na
Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua
nguo zao; wakanena na mkutano wote wa wana wa Israeli wakasema, Nchi ile
tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi njema mno ya ajabu. Ikiwa Bwana
anatufurahia, atatuingiza katika nchi hii atupe iwe yetu, nayo ni nchi yenye
wingi wa maziwa na asali. Lakini msimwasi Bwana, wala msiwaogope wale wenyeji
wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa, naye
Bwana yu pamoja nasi; msiwaogope.”
Unaona Wana wa Israel walishaogopa mno wakati wao
wanaogopa kumbe wakanaani nao walikuwa wamewaogopa muda mrefu sana na hakuna
ujasiri uliokuwa umesalia ndani yao, wakati mwingine tunajikosesha Baraka za
Mungu kwetu kwa sababu ya hofu ona
Joshua
2:1-11 “Yoshua, mwana wa Nuni, akawatuma watu wawili kutoka
Shitimu kwa siri, ili kupeleleza, akawaambia, Enendeni mkaitazame nchi hii, na
Yeriko. Wakaenda wakafika nyumbani kwa kahaba mmoja jina lake aliitwa Rahabu,
wakalala huko. Mfalme wa Yeriko akaambiwa, kusema, Tazama, watu wawili wa wana
wa Israeli wameingia humu leo usiku, ili kuipeleleza nchi. Mfalme wa Yeriko
akatuma watu kwa Rahabu, akasema, Watoe watu wale waliokuja kwako, walioingia
ndani ya nyumba yako, maana wamekuja ili kuipeleleza nchi. Yule mwanamke
akawatwaa wale watu wawili, akawaficha, akasema, Naam, wale watu walikuja kwangu,
lakini sikujua walikotoka; ikawa kama wakati wa kufungwa lango la mji,
kulipokuwa giza, watu wale wakatoka, wala sijui walikokwenda; wafuateni upesi,
maana mtawapata. Lakini yeye alikuwa amewapandisha darini, akawaficha kwa mabua
ya kitani, aliyokuwa ameyatandika juu ya dari. Basi hao watu wakawafuata kwa
njia iendayo Yordani mpaka vivukoni; na mara wale watu waliowafuatia
walipokwisha kutoka, wakalifunga lango.Tena kabla hawajalala akawaendea juu
darini, akawaambia wale wanaume, Mimi najua ya kuwa Bwana amewapa ninyi nchi
hii, na ya kuwa hofu imetuangukia mbele yenu, na ya kuwa wenyeji wote wa nchi
wanayeyuka mbele yenu. Maana tumesikia jinsi Bwana alivyoyakausha maji ya
bahari ya Shamu mbele yenu, hapo mlipotoka Misri, tena mambo hayo mliyowatendea
wafalme wawili wa Waamori waliokuwa huko ng'ambo ya Yordani, yaani, Sihoni na
Ogu, mliowaangamiza kabisa. Na mara tuliposikia hayo mioyo yetu iliyeyuka, wala
haukusalia ujasiri wo wote katika mtu awaye yote, kwa sababu yenu; kwa kuwa
Bwana, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu, katika mbingu juu na katika nchi chini.”
Hebu jaribu kuwaza wakati Israel wakiwaogopa wanaowaogopa!
Wakanaani walishashikwa na hofu tangu waliposikia matendo makuu ya Mungu lakini
warithi wa ile Inchi nyaani waisrael wenyewe walikuwa wanaogopa na iliwachukua
miaka 40 kuingia katika inchi ya kaanaani lakini tatioz kubwa likichangiwa na
kutokuamini kwao! Kila mtu anayetaka kuwa hodari zaidi inampasa kujifunza
kutokuogopa!
10. Futa
msamiati haiwezekani.
Watu wote waliofanikiwa katika maandiko ni wale
waliokuwa hawana msamiati wa haiwezekani, msamiati huu sio msamiati wa kiungu
hata siku moja Mungu hajawahi kuzungumza kokote kuwa kuna kitu kisichowezekana
hususani kama utamshirikisha na yeye
Mathayo
19:26 “Yesu akawakazia macho, akawaambia, Kwa wanadamu hilo
haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.”
Mwanzo
18:9-14 “Wakamwambia, Yu wapi Sara mkeo? Akasema, Yumo
hemani. Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara
mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma
yake. Basi Ibrahimu na Sara walikuwa wazee, na umri wao mkubwa, na Sara alikuwa
amekoma katika desturi ya wanawake. Kwa hiyo Sara akacheka moyoni mwake,
akisema, Niwapo mkongwe, nitapata furaha, na bwana wangu mzee? BWANA akamwambia
Ibrahimu, Mbona Sara amecheka akisema, Mimi kweli nitazaa mwana, nami ni mzee?
Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda BWANA? Kwa muhula wake nitakurudia,
wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume.”
Yeremia
32:27 “Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili;
je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza? ”
Kwa msingi huo tunachopaswa sisi ni kujiungamanisha
na Mungu ili tuweze kutenda mambo makubwa sana Zaburi 60:12 “Kwa
msaada wa Mungu tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.”
Zaburi
108:13 “Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, Maana Yeye
atawakanyaga watesi wetu.”
11. Kumbuka kuukomboa wakati.
Kulitumikia kusudi lolote la Mungu hapa Duniani
kumbuka limewekwa katika muda, kwa msingi huo Maandiko yanatutaka vilevile kuwa
na hekima ya jinsi na namna ya kuukomboa wakati, kumbuka kuwa kila mwanadamu
anayeishi ulimwenguni ana masaa 24 kwa siku, ana siku saba kwa wiki siku
30 kwa mwezi na Miezi 12 kwa mwaka sawa na siku 365, lakini
moja ya tatizo kubwa tulilonalo wanadamu ni kutokuujua wakati na kutokujua
namna ya kuzitumia nyakati
Luka 19:41-44 “Alipofika
karibu aliuona mji, akaulilia, akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku
hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako. Kwa kuwa siku
zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na
kukuhusuru pande zote; watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako,
wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako.”
Yesu aliulilia mji wa Yerusalem ambao ulibomolewa
vibaya mwaka wa 70 baada ya Kristo yaani kama miaka 27 baadaye na
sababu kubwa ya kubomolewa kwao ni ka sababu hawakujua majira yaani Muda wa
kutembelewa na Mungu walipuuza waklimkataa Yesu walimsulubisha na wakati
ulifika walijuta lakini wakati huo muda ulikuwa umekwisha kwenda, kila mtu
anayetaka kuwa mhodari katika maisha yake lazima ajue kuukomboa wakati, mtu
anayeukomboa wakati katika maandiko anaitwa mtu mwenye hekima ona Waefeso
5:15-17 “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu
wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani
hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo
mapenzi ya Bwana.” Biblia ya kingereza na
NIV inafananisha Muda na nafasi ya bahati OPPORTUNITY – Kwa KIYUNANI Efkairia maana yake –
a time or set of circumstances that makes it possible to do something, yaani ni
muda au wakati ambapo unapata mazingira ya kuweza kufanya jambo, kwahiyo
matumizi ya muda na matumizi ya nafasi za kipekee ambazo ulipaswa kuzitumia
vema, kwa hiyo tiofauti yatu na watu wengine ni sio kwa sababu wao wana muda
mwingi zaidi bali kwa sababu wao wana ujuzi wa kutumia nafasi
Muhubiri 3:1-8
“Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini
ya mbingu. Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati
wa kung'oa yaliyopandwa; Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa
kubomoa, na wakati wa kujenga; Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa
kuomboleza, na wakati wa kucheza; Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya
mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia; Wakati wa kutafuta, na
wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa; Wakati wa kurarua,
na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena; Wakati wa
kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani.”
Kwa msingi huo kujua nyakati kunaweza
kutusaidia kujua nini litupasalo kufanya wana wa Israel walifanikiwa sana hasa
nyakati za utawala la Daudi kwa vile lilikuweko kabila la wana wa isakari ambao
walikuwa na ujuzi wa nyakati na nini kiwapasacho watu kufanya kwa wakati huo
ona
1Nyakati 12:32 “Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua
nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia
mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.”
Kwa msingi huo kila mtu anayetaka
mafanikio ni lazima aelewe na ajue namna na jinsi ya kuutmia wakati ni hekima
kuutumia wakati vizuri! Na ujinga kupoteza muda na kutokujua namna na jinsi ya
kuutumia wakati, Bwana na ampe neema kila mmoja wetu ajue jinsi
anavyopaswa kuutumia wakati ili tusijute baadaye katika jina la Yesu amen.
12. Fanya
kazi kwa bidii.
Unapofuatilia maisha ya watu waliofanikiwa katika
maandiko, utagundua pia kuwa watu hao walikuwa wachapa kazi, hawakuwa wavivu,
wote tunafahamu kuwa kazi ya kwanza aliyopewa Adamu haikuwa kuabudu, Mungu
alimuweka Mwanadamu katika bustani ya edeni ili afanye kazi ona Mwanzo 2:15
“BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni,
ailime na kuitunza.”, kulima na kutunza sio kazi
nyepesi, kwa msingi huo utaweza kugundua kuwa Mungu alimtaka mwanadamu afanye
kazi, hata maumbile ya kiulimwengu yanaonyesha mkazo wa kufanya kazi katika
siku saba ambazo Mungu ametupa utaweza kuona ametoa siku sita za kufanya kazi
na siku moja utamkumbuka bwana Mungu wako ona
Kutoka
35:1-2 “Musa akakutanisha mkutano wote wa wana wa Israeli,
na kuwaambia, Maneno aliyoyausia BWANA ni haya, kwamba myafanye. Fanyeni kazi
siku sita, lakini siku ya saba itakuwa siku takatifu kwenu; ni Sabato ya
kustarehe kabisa kwa BWANA; mtu awaye yote atakayefanya kazi yo yote katika
siku hiyo atauawa”
kwa hiyo utaweza kuona ni kama kwa kiwango Fulani
hivi neno la Mungu linatutaka tufanye kazi kanuni hii ya kufanya kazi
imewafanya watu wa mataifa ya Asia kubarikiwa na kufanikiwa kwa haraka sana,
nilipotembelea Marekani nilikuta jamii kubwa ya wakazi wa marekani katika jimbo
la Viginia ni wakorea na wanapendwa sana na wamarekani kwa sababu ni wachapa
kazi, hata nchi yao imeendelea sana kwa sababu wako aggressive ni wenye juhudi
katika kufanya kazi Maandiko yako kinyume na uvivu na yanamtaka kila mmoja
afanye kazi kwa bidii na mkazo huu umedhihirika hata kwa mkazo ulio wazi kuwa
asiyefanya kazi kula na asile ona
2Wathesalonike
3:10-12 “Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu
tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile
chakula.Maana twasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu, hawana
shughuli zao wenyewe, lakini wanajishughulisha na mambo ya wengine. Basi
twawaagiza hao, na kuwaonya katika Bwana Yesu Kristo, watende kazi kwa utulivu
na kula chakula chao wenyewe.”
Unaona kwa msingi huo kutokufanya kazi ni dhambi,
Mungu anataka watu wafanye kazi zao, kila mmoja awe na shughuli yake mwenyewe
ya kufanya, na kuhakikisha kuwa anajituma, maandiko yanaionyesha kuwa kuna
mafanikio makubwa kama watu watafanya kazi kwa bidii, iko wazi kuwa kila mtu
anayefanya kazi kwa bidii na kwa kujitoa anafanikiwa, tunafahamu yako mapito na
pia kuwa wakati mwingine haiku wazi kwa sababu wako watu wanafanya kazi kwa
bidii nab ado hayaonekani mafanikio, nii ni sehemu ndogo ya matokeo ya kimaisha
lakini Biblia inatuongoza kwamba bado ni agizo la Mungu kufanya kazi kwa bidii,
tunapofanya kazi kwa bidii bila kujali imani zetu na kabila zetu na rangi zetu
ni wazi kuwa Mungu anasimama karibu nasi, kwa hiyo fanya kazi hata kama hujui
Mungu yuko kwenye hatua gani kukutokea
Mithali
12:24 “Mkono wa mwenye bidii utatawala; Bali mvivu
atalipishwa kodi.” Neno la Mungu linatutaka
tufanye kazi na kutunza familia zetu na jama zetu kama mtu anashindwa hata
kuitunza familia yake maandiko yanasema ni mbaya kuliko asiye na imani ona
1Timotheo
5:8 “Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa
nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini” Paulo mtume pamoja na kuwa Muhubiri wa injili
alihakikisha kuwa wakati mwingine anafanya kazi kwa bidii ili kujipatia
mahitaji yake yeye alijua wazi kuwa ni heri kutoa kuliko kupokea
Matendo
20:33-35 “Sikutamani fedha wala dhahabu, wala mavazi ya mtu.
Ninyi wenyewe mnajua ya kuwa mikono yangu hii imetumika kwa mahitaji yangu na
ya wale waliokuwa pamoja nami. Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa
kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana
Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea” Lakini maandiko pia yanataka tujifunze kutoka kwa
chungu au mchwa kwamba wanafanya kazi ka bidii na wanajiwekea akiba hata kwa
wakati wa kiangazi au nukame ona
Mithali
6:6-11 “Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake
ukapate hekima. Kwa maana yeye hana akida, Wala msimamizi, wala mkuu, Lakini
hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa
mavuno. Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako? Bado
kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! Hivyo
umaskini wako huja kama mnyang'anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha”hatuna budi kuhakikisha kuwa kila tulifanyalo
tunalifanya kwa bidii na tunashuhudia mafanikio makubwa sana katika utendaji
wetu wa kazi na maisha yetu.
13. Usiache
kumtegemea Mungu
Maandiko yanaonyesha kudumu kwetu na kuendelea
kusimama kwetu ni kwa kumtegemea Mungu na kumtumaini mtu anayemtegemea Mungu
anafananishwa na mlima sayuni hatatikisika milele
Zaburi
152: 1-5 “Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao
hautatikisika, wakaa milele. Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo
Bwana anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele. Kwa maana fimbo ya
udhalimu Haitakaa juu ya fungu la wenye haki; Wenye haki wasije wakainyosha
Mikono yao kwenye upotovu. Ee Bwana, uwatendee mema walio wema, Nao walio
wanyofu wa moyo. Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka, Bwana atawaondoa
pamoja na watenda maovu. Amani ikae na Israeli.”
Mashujaa wote wa imani walioendelea kuwa
hodari zaidi walimtegemea Mungu na kamwe hawakuwategemea wanadamu, mara unapo
mfanya mwanadamu kuwa kinga yako na kumdaharau Bwana ukweli ni kuwa unajiweka
katika laana na hautafanikiwa
Yeremia
17:5-7 “Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye
mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana.
Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa
jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. Amebarikiwa
mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake. Maana atakuwa kama
mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu
wakati wa hari ujapo”
Kwa msingi huo pamoja na mambo mengine yote hatuna
budi kuhakikisha kuwa tunamtegemea Mungu katika njia zetu zote na maandiko
yanatuasa kwamba wala tusizitegemee akili zetu wenyewe
Mithali 3:5-6 “Mtumaini
Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia
zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.”
Mambo yanapokuwa magumu neno la Mungu
linatuagiza kuomba na kumtwika yeye fadhaa zetu zote ona
1Petro 5:6-7 “Basi
nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana
yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu” hakuna sababu ya kufadhaika
Wafilipi
4:6 “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali
na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu
Ni imani yangu kuwa kanuni hizi zitamsaidia kila mtu
anayetaka kuwa hodari zaidi katika Nyanja mbalimbali ukiyajua hayo heri wewe
ukiyatenda
Yohana 13:17 “Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda”
Rev.
Innocent Kamote
Mkuu
wa wajenzi mwenye Hekima!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni