Jumatano, 23 Februari 2022

Mafundisho kuhusu Uadilifu!


Andiko la Msingi: Tito 2:11-12 “Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;”


     

Utangulizi:

Leo hii tutachukua Muda kujifunza kwa undani kuhusu Uadilifu, (Ethics). Moja ya maswala ya msingi sana ambayo kila mwanadamu anapaswa kuwa nayo awapo Duniani ni pamoja na kuwa na uadilifu, uadilifu sio agizo la Dini Fulani au mafundisho ya watu Fulani tu lakini somo kuhusu uadilifu linawahusu wanadamu wote, Mungu anapendezwa na uadilifu, na dunia itakuwa mahali salama na pazuri kama watu watajifunza kuishi kwa uadilifu, Uadilifu unafanya kazi katika Nyanja zote na watu wanaozingatia uadilifu wanakuwa na mafanikio makubwa sana na ustawi katika maeneo yote, kwa ujumla jamii yenye uadilifu watu wake wanaishi kwa amani na utulivu na kwa kumpendeza Mungu na watu wote!

Uadilifu ni nini hasa! Neno uadilifu katika lugha ya kiyunani husomeka kama neno “ETHOS” kwa kiingereza ETHICS na kwa kilatini MORES Maana yake CHARACTER au BEHAVIOR au Attitude  ambalo katika Falsafa tunalielezea neno hili kama Mfumo wa kanuni unaotusaidia kujua jema na baya, na kutusaidia namna ya kuendesha maisha yetu. Kwa kikristo tunaita “Moral Theology

Kwa kiingereza Ethos/Ethics are system of Principles that helps our life to determine what is wrong and what right is, what is good and what is Bad.

Uadilifu pia ni kanuni zinazotuelekeza namna na jinsi ya kuenenda na kufanya kazi Fulani! kwa hiyo, walimu wana aina zao za uadilifu, Wauguzi wana aina zao za uadilifu, wanasiasa wana aina zao za uadilifu, Polisi wana aina zao za uadilifu, wachungaji wana aina zao za uadilifu, Lakini wakristo nao wana aina yao ya uadilifu, Kimsingi uadilifu ni kanuni zinazotuongoza kujua neno na tendo na sifa ambazo zinatupa kukubaliika mbele za Mungu na wanadamu!

Wakolosai 1:9-11 “Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni; mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu; mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha;”

Ki msingi wakristo ndio wanapaswa kuwa taa u nuru ya uadilifu kote duniani na watu wengine wote wanapaswa kujifunza na kutuiga,lazima sisi tuwe mstari wa mbele katika swala zima la kuishi kwa uadilifu, kwa sababu tuna Mungu, tuna mwokozi na tuna Mafundisho yaliyo bora zaidiyanayotokana na kiongozi mwadilifu zaidi kuliko wote Yesu Kristo Bwana na Mwokozi wangu!, katika somo hili tutaangalia eneo kubwa kwa sehemu ule umuhimu tu wa mafundisho kuhusu uadilifu!

Umuhimu wa Mafundisho kuhusu Uadilifu!

1.       # Uadilifu unatufanya sisi kumpendeza Mungu na wanadamu  

 

Kwa mujibu wa maadili ya Kikristo, mtu anayekuwa vizuri katika uadilifu atalenga siku zote kumpendeza Mungu na wanadamu, sio wakati wote jambo hili linaweza kuwa jepesi lakini ni amri ya Mungu kumpenda Mungu na kuwapenda jirani zetu kama nafsi zetu kwa msingi huo neno la Mungu linatuamuru tumpendeze Mungu lakini vilevile tuwapendeze na wanadamu ona

 

Mathayo 22:36-40 “Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.”

 

Kwa msingi huo basi kila mwanadamu anayekua katika uadilifu atashuhudiwa kuwa mwema kwa Mungu na wanadamu, Mwanadamu atakayeishi akiwa na madai kuwa ana mpendeza Mungu na huku anawakwaza wanadamu wenzake, hatuwezi kusema kuwa anampenda Mungu pia

 

1Yohana 2:9-11 “Yeye asemaye kwamba yumo nuruni, naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa. Yeye ampendaye ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo. Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.”

 

Kwa hivyo kiuadilifu tunapaswa kuhakikisha kuwa tunakuwa sahihi mbele za Mungu na wanadamu, tunampendeza Mungu na wanadamu na hili ndio moja ya somo kuu sana la kibiblia, hakikisha kuwa unamtendea mema kila mmoja na hakikisha kuwa unakuwa mbali na ubinafsi na kuwa kila unalotaka wewe kutendewa unawatendea na wengine na kile usichotaka wewe kutendewa usiwatendee wengine

 

Mathayo 7:12 “Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.”

 

Ni mafundisho ya Msingi ya kibiblia kuhakikisha kuwa tunakuwa sawa pande zote kwa Mungu na kwa wanadamu, lazima tuwe na amani pande zote

 

Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;”

 

Maisha ya aina hii ndiyo maisha anayopaswa kuishi mtu muadilifu na anayemcha Mungu hatupaswi kuwa sawa upande mmoja tu Kristo Yesu Mwikozi wetu na kiongozi mkuu wa wokovu wetu ametuachia kielelezo cha maisha ya uadilfu kwa sababu katika maisha yake alimpoendeza Mungu na wanadamu ona

 

Luka 2:51-52 “Akashuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii; na mamaye aliyaweka hayo yote moyoni mwake. Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.”   

 

Kwa msingi huo basi tunapojifunza kuhusu somo la Uadilifu maana yake tunajikumbusha namna inavyotupasa kutenda na kueneda mbele za Mungu na wanadamu, na kuwapendeza katika kiwango kinachopaswa ona

 

2Wakoritho 8:20-21 “Tukijiepusha na neno hili, mtu asije akatulaumu kwa habari ya karama hii tunayoitumikia; tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele za Bwana tu, ila na mbele ya wanadamu.”

 

2.       # Uadilifu unatufanya sisi kuishi kwa utaratibu.

 

Kuishi kwa uadilifu vilevile maana yake ni kujifunza kuishi kwa utaratibu, kama Mungu hangetoa maelekezo au sharia na kanuni watu wangeishi bila kufuata utaratibu, moja ya vita kubwa sana iaisyoonekana duniani ni pamoja na vita ya Utaratibu na Machafuko (Order and Chaos)  hii ni vita inayopiganwa kila siku na nadhani utaratibu unamwakilisha Mungu na machafuko yanamwakilisha shetani, watu wenye maadili wanaishi kwa kufuata utaratibu hatuwezi kuacha mambo yaende kama yanavyokwenda  Mungu si Mungu wa machafuko bali ni Mungu wa utaratibu

 

1Wakoritho 14:33 “Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu.”

 

Unaweza kuona sasa basi kama Mungu sio Mungu wa machafuko ni Mungu wa namna gani ni Mungu wa utaratibu na anataka mambo yote yatendeke kwa uzuri na utaratibu

 

1Wakoritho 14:40 “Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu”. Mungu alipokuwa anauumba ulimwengu alikuwa anaumba kwa kufuata utaratibu hakutanka tu kwa ufupi historia ya uumbaji nni historia ya utaratibu kutoka katika machafuko ona Mwanzo 1:1-8 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja. Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji. Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo. Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili.”

 

Mpaka Mungu anakamilisha nuumbaji maana yake alikuwa anakamilisha utaratibu, hakuna nchi au taifa au taasisi inaweza kuendelea ikiwa watu wanaishi vile watakavyo, hakuna nidhamu hakuna utaratibu watu wanaishi hovyo hovyo tu au bila kufuata utaratibu maandiko yanaionyesha kuwa Mungu anataka kila mahali kuwe na utaratibu na watu waadilifu huishi kwa utaratibu na kwa kufuata utaratibu, unaposikia kuhusunutawala wa sharia maana yake ni utawala wa utaratibu, sio mwizi amekamatwa watu wanapiga moto na kiberiti, Mungu anapoweka viongozi maana yake Mungu anawataka wao wahakikishe kuwa wanasimamia utaratibu na kukemea wale wote wasioenedna kwa utaratibu ona 

 

Tito 1:5 “Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuweka wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru;” unaona meneno hayo uyatengeneze yaliyopunguka katika Biblia ya kiingereza KJV  yanasomeka hivi Titus 1:5 “For this Cause left I thee in Crete, that thou shouldest set in order the things that are wanting, and ordain elders in every city as I had appointed theeKwa hiyo Paulo mtume alimpeleka Tito awe askofu katikamkiswa cha crete ili kuweka utaratibu  unaona kwa hiyo kimsingi mtu hawezi kuwa mwadilifu alafu wakati huo akakosa kuwa mtu wa utaratibu mambo haya yanaenda pamoja

 

 1Timotheo 3:1-6Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha; mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?) Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi.”

 

Watu wale waliojiita wakristo na wakashindwa kuishi kwa kufuata kanuni ya kufanya kazi na kujipatia chakula chao wenyewe Paulo mtume aliwakemea na kuwaita watu wasioenenda kwa utaratibu

 

1Wathesalonike 5:14 “Ndugu, twawasihi, waonyeni wale wasiokaa kwa utaratibu; watieni moyo walio dhaifu; watieni nguvu wanyonge; vumilieni na watu wote.”  Watu wasiokaa kwa utaratibu wanaitwa unruly maandiko yanakemea na kuwataka watu wote wawe wenye kuishi kwa utaratibu kwa msingi huo somo la maadili linakazia watu kuishi kwa kufuata utaratibu na kujihami kwa kujichukulia sharia mkononi au kufanya kila tunaloliona wenyewekuwa jema na ili kwamba watu waishi kwa utaratibu na kuepuka machafuko, ulimwengu wa sasa unakwenda mbio mno na watu wanaishi bila kufuata utaratibu hawajali kanuni na utaratibu ambapo Mungu ameuweka          na ndio maana Isaya nabii anaiona kama kitu kinachoharibika haraka kwa sababu utaratibu umetoweka !

 

Isaya 24:19-20“Dunia kuvunjika, inavunjika sana; dunia kupasuka, imepasuka sana; dunia kutikisika, imetikisika sana. Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela; na mzigo wa dhambi zake utailemea; nayo itaanguka, wala haitainuka tena

 

3.       # Uadilifu humfanya mtu aone kuwa watu wote ni sawa au bora             

 

Maandiko yanatufundisha kuwa Mungu hana upendeleo kwa lugha nyingine Mungu hana ubaguzi.

 

Warumi 2:11 “kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu” Kwa msingi huo Mungu humkubali mtu yeyote yule katika kila taifa anayemkubali yeye

 

Matendo 10:34-35 “Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo; bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye.”

 

Hii maana yake kila mwanadamu ana haki sawa kwa Mungu binadamu wote ni sawa Ni kweli Mungualiichagua Israel ili kuleta Baraka kwa mataifa byote na sasa mtu akimkubali Yesu anakuwa na kibali kwa Mungu bila ubaguzi wa aina yoyote katika Kristo kila mtu ni sawa kila mtu ni uzao wa Ibrahimu na mrithi wa ahadi zile ona

 

Wagalatia 3:27-29 “Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu. Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.”

 

Kwa msingi huo kama Mungu hana ubaguzi na tunajifunza kutoka kwake hii maana yake kila mtu anayemcha Mungu hapaswi kuwa na upendeleo wala ubaguzi Swala la ubaguzi limekuwa moja ya tatizo kubwa sana Duniani, mara kadhaa tumeona Africa na Israel ikiwa ni jamii ambayo imeteseka sana duniani, wengi wakionewa wivu, kubaguliwa kuawa na hata kukojolewa waafrika wakati mwingine wamezaniwa kama watu wasio na akili na wasioweza kufanyololote bila kutumikishwa, wengi wametumiwa kwa faida ya weupe, huku watu weupe wakijifikiri kuwa wao ni bora zaidi duniani katika maadili ya kikristo maandiko matakatifu yanatukataza sio tu kuwabagua watu kwa sababu ya rangi zao bali  hata kwa hali zao za kifedha hatupaswi kuwa na upendeleo

 

Yakobo 2:1-4 “Ndugu zangu, imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe nayo kwa kupendelea watu. Maana akiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu na mavazi mazuri; kisha akiingia na maskini, mwenye mavazi mabovu; nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Keti wewe hapa mahali pazuri; na kumwambia yule maskini, Simama wewe pale, au keti miguuni pangu, je! Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu?

 

Ubaguzi ni mwiko katika Tamko la umoja wa mataifa la haki za binadamu lililotolewa huko Paris December 10 mwaka 1948 ambalo linaitwa kwa kiingereza Universal Declaration of Human Rights UDHR tamko lake la kwanza linasema hivi nanukuu  

 

“All human beings are born free and equal in dignity and rights, they are endowed with reason and conscience and should act toward one another in spirit of brotherhood” 

 

“Kwamba watu wote huzaliwa huru wakiwa sawa na katika haki na heshima na wamepewa akili na dhamiri nani juu yao kushirikiana wana na wengine kwa roho ya udugu”

 

Matamko haya pamoja na mengine mengi yanayofuata yalikuwa na lengo la kukomesha hali ya kujiona mabwana na wengine watumwa au hali ya kuwabaguwa wanadamu kwa sababu zozote zile  maandiko yanamtaka kila mmoja amuhesabu mweznie kuwa ni bora kuliko nansi yake ona

 

Wafilipi 2:3 “Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.”

 

Watu wenye uadilifu hawana ubaguzi, hawapokei uso wa mwanadamu kwa mitazamo ya upendeleo, wanawaona wanadamu wote kuwa ni sawa hawana upendeleo wala hawana ubaguzi kama alivyo baba wa Mbinguni ambayo hutoa haki sawa kwa watu wema na wabaya kwa kuwapa jua lake na mvua 

 

Mathayo 5:44-46 “lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?”

 

4.       Uadilifu unatufanya sisi tuwe mfano wa kuigwa.

 

Tunajifunza kuhusu uadilifu katika neno la Mungu ili kwamba tuwe kielelezo au mfano kwa watu wengine hususani watu wa ulimwengu huu wasio na uadilifu, Mungu alipowaokoa wana wa Israel kule Misri aliwafundisha uadilifu kupiti Musa mtumishi wake ili Israel liwe taifa litakalokuwa kielelezo kwa Mataifa yote

 

Kumbukumbu 4:5-8 “Angalieni nimewafundisha amri na hukumu, vile vile kama Bwana, Mungu wangu, alivyoniamuru, ili mzitende katika nchi mwingiayo ili kuimiliki. Zishikeni basi, mkazitende, maana hii ndiyo hekima yenu na akili zenu, machoni pa mataifa watakaozisikia amri hizi zote, nao watasema, Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na akili. Kwa maana liko taifa gani kubwa, lililo na Mungu aliye karibu nao, kama Bwana, Mungu wetu, alivyo, kila tumwitapo? Tena liko taifa gani kubwa, lililo na amri na hukumu zenye haki kama torati hii yote, ninayoiweka mbele yenu leo.”

 

Ni katika hali kama hii Yesu alipokuja ulimwenguni alikuja kama Mwalimu wa kutufundisha mambo mengi sana ili tuweze kuuiga mfano wake yeye ametuachia mifano mingi ya kuiga na kuishi kwa uadilifu ona

 

Yohana 13:15 “Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.”

Unaona Yesu ametuachia kielelezo ili kwamba na sisi tuweze kumfuata na kutenda kama alivyotenda, aidha Paulo mtume pia alipokuwa duniani alijitajitahidi sana kuwa kielelezo na aliwataka watu wamfuate yeye vilevile kama anavyomfuata Kristo ona

 

1Wakoritho 11:1 “Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo.” Makusudi makubwa ya Bwana Yesu ni kuwa tutakapoishi kwa kufuata mfano wake watu wa ulimwengu watajua kuwa sisi ni wanafunzi wa Yesu ona

 

Yohana 13:35 “Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi”, kwaajili ya haya mitume walisisitiza sana wanafunzi wa Yesu wote waishi kwa kufuata kielelezo

 

Wafilipi 3:17 “Ndugu zangu, mnifuate mimi, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliowapa ninyi.”

 

Wafilipi 4:9 “Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia na kuyaona kwangu, yatendeni hayo; na Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.” Tunapoishi kwa uadilifu moja ya faida kubwa sana ni kuwa watu watayaona matendo mema na kumtukuza Mungu, lakini hata wale wenye kulaumu watakosa sababu zenye mashiko kutokana na kuwa waadilifu ona

 

1Petro 2:12 “Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.”

 

Neno la Mungu linatoa maonyo makali sana kwa watu wasiojua kupambanua mema na mabaya na hata wale amabao kwa kusudi wanageuza na kuona kuwa mabaya ndio mema na mema ndio mabaya ona

 

Isaya 5:20-23 “Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; watiao uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu! Ole wao walio wenye hekima katika macho yao wenyewe, na wenye busara katika fikira zao wenyewe! Ole wao walio hodari kunywa kileo chenye nguvu, watu waume wenye nguvu kuchanganya vileo; wampao haki mwenye uovu, ili wapewe ijara, na kumwondolea mwenye haki haki yake!

 

 

 

 

5.       Uadilifu hutusaidia kuepuka Kanuni ya kupanda na kuvuna

 

Wagalatia 6;7-8 “Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.”

 

Kanuni ya kupanda na kuvuna ni moja ya kanuni yenye nguvu nay a ajabu sana Duniani na kanuni hii inafanya kazi, katika dini ya kihindu na Kibudha kanuni hii huitwa Karma –  ambayo maana yake ni mjumuisho wa matendo ya awali yanayoamua matukio yako ya sasa na baadaye, kanuni hii inatisha sana  kwa sababu huwa haidanganyi na infanya kazi mno,  Na ndio maana Paulo mtume anausema mstari huu kwa maonyo makali neno hilo Msidanganyioke kwa kiibrania ni (Planao) ambalo maana yake kuchezea pua ya Mungu au kuugeuza ukweli wa Mungu, au kufanya mzaha na kanuni za Mungu, kwa hiyo Paulo anaonya kuwa tusifanya mzaha na Kanuni za Mungu zinafanya kazi yeye anachokisema amekisema

Mwanzo 3:4-5 “Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.”

 

Hapa Eva alikuwa anajaribiwa achezee kanuni za kiungu na unajua yaliyotukia, Kanuni za kiungu zinafanya kazi na hazina mzaha, Yakobo ni mfano mzuri wa kuigwa katika maandiko alidanganya kuwa yeye ni Esau ona

 

Mwanzo 27:18-22 “Akaja kwa baba yake, akasema, Babangu. Akasema, Mimi hapa, U nani wewe, mwanangu? Yakobo akamwambia babaye, Mimi ni Esau, mzaliwa wako wa kwanza, nimefanya kama ulivyoniambia. Ondoka, tafadhali, ukae kitako, ule mawindo yangu, ili roho yako inibariki.Isaka akamwuliza mwanawe, Imekuwaje umepata upesi namna hii, mwanangu? Akasema, Kwa sababu BWANA, Mungu wako, amenifanikisha. Isaka akamwambia Yakobo, Karibu, tafadhali, ili nikupapase, mwanangu, nione kwamba wewe ndiwe mwanangu Esau, ama siyo. Basi Yakobo akamkaribia Isaka, babaye, naye akampapasa, akasema, Sauti ni sauti ya Yakobo, lakini mikono ni mikono ya Esau.”

 

Baada ya yeye kudanganya alisababisha machozi makubwa sana kwa kaka yake Esau ona Mwanzo 27:34-35 “Esau aliposikia maneno ya babaye, akalia kilio kikubwa cha uchungu sana, akamwambia babaye, Nibariki na mimi, mimi nami, Ee babangu. Akasema, Nduguyo amekuja kwa hila, akauchukua mbaraka wako.” Baada ya wakati mwingi hiki kilikuja kutokea katiika maisha ya Yakobo

 

Mwanzo 29:15-26 “Labani akamwambia Yakobo, Kwa sababu wewe ni ndugu yangu, basi, je! Unitumikie bure? Niambie mshahara wako utakuwa nini? Labani alikuwa na binti wawili, jina la mkubwa ni Lea, na jina la mdogo ni Raheli. Naye Lea macho yake yalikuwa dhaifu, lakini Raheli alikuwa mzuri wa umbo, na mzuri uso.Yakobo akampenda Raheli akasema, Nitakutumikia miaka saba kwa kumpata Raheli, binti yako mdogo. Labani akasema, Afadhali nikupe wewe kuliko mtu mwingine; kaa kwangu. Yakobo akatumika miaka saba kwa kumpata Raheli. Ikawa machoni pake kama siku chache tu kwa vile alivyompenda. Yakobo akamwambia Labani, Nipe mke wangu, maana siku zangu zimetimia; niingie kwake. Labani akakusanya watu wote wa mahali pale, akafanya karamu. Ikawa wakati wa jioni akamtwaa Lea, binti yake, akamletea Yakobo, naye akaingia kwake. Labani akampa Lea mjakazi wake Zilpa, awe mjakazi wake. Ikawa, kulipokuwa asubuhi, kumbe! Ni Lea. Akamwambia Labani, Nini hii uliyonitenda? Sikukutumikia kwa Raheli? Mbona umenidanganya? Labani akasema, Havitendeki hivi kwetu, kumtoa mdogo kabla ya mkubwa

 

Vile vile Yakobo alidanganywa tena na vijana wake kuhusu ndugu yao Yusufu    

Mwanzo 37:31-35 “Wakaitwaa kanzu ya Yusufu, wakachinja mwana-mbuzi, na kuichovya kanzu katika damu. Wakaenda nayo ile kanzu ndefu, wakamletea baba yao, wakasema, Tumeona hii; basi, utambue kama kanzu hii ni ya mwanao, ama siyo. Akaitambua, akasema, Ndiyo kanzu ya mwanangu, mnyama mkali amemla; bila shaka Yusufu ameraruliwa. Yakobo akararua mavazi yake, akajivika gunia viunoni, na kumlilia mwanawe siku nyingi. Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba yake akamlilia.”

 

Unaona huwezi kupanda ubaya kisha uvune mema kanuni hii inafanya kazi kwa watu wote na kabila zote na jamii zote za dunia kwa sababu ni kanuni ya Mungu,  ni kanuni ya uadilifu pakee inayoweza kukulinda na mavuno ndio maana ile sharia ya dhahabu ikatutahadharia kuwa lolote lile ambalo hupendi wewe kutendewa usiwatendee wengine

 

Mathayo 7:12 “Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.”

Kanuni ya kula mke wa mtu, malipizi yake ni kuliwa kwa mkeo Ayubu 31:9-11 “Kama moyo wangu ulishawishwa kwa mwanamke, Nami nimeotea mlangoni pa jirani yangu; Ndipo hapo mke wangu na asage kwa mwingine, Na wengine na wainame juu yake. Kwani hilo lingekuwa kosa kuu; Naam, lingekuwa ni uovu wa kuadhibiwa na waamuzi;”

 

2.Samuel 11:2-4 “Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho. Naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bath-sheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti? Basi Daudi akapeleka wajumbe, akamtwaa; naye akaingia kwake; naye akalala naye; (maana yule mwanamke amekwisha kutakasika unajisi wake); kisha akarudi nyumbani kwake.”

 

Wote tunajua kile Daudi alikifanya na matokeo yake Mungu alimuambiaje? Ona

2samuel 12:1-11 “Ndipo Bwana akamtuma Nathani aende kwa Daudi. Naye akamwendea, akamwambia, Palikuwa na watu wawili katika mji mmoja; mmoja wao alikuwa tajiri, wa pili maskini.Yule tajiri alikuwa na kondoo na ng'ombe wengi sana; bali yule maskini hakuwa na kitu, ila mwana kondoo mmoja, mdogo, ambaye amemnunua na kumlea; naye akakua pamoja naye, na pamoja na wanawe; hula sehemu ya posho lake, na kukinywea kikombe chake, na kulala kifuani mwake, akawa kwake kama binti. Hata msafiri mmoja akamfikilia yule tajiri, naye akaacha kutwaa mmoja wa kondoo zake mwenyewe au mmoja wa ng'ombe zake mwenyewe, ili kumwandalia yule msafiri aliyemfikilia, bali alimnyang'anya yule maskini mwana-kondoo wake, akamwandalia yule mtu aliyemfikilia. Ndipo hasira ya Daudi ikawaka sana juu ya mtu yule; akamwambia Nathani, Aishivyo Bwana, mtu huyo aliyetenda jambo hili, hakika yake astahili kufa; naye atamrudishia yule mwana-kondoo mara nne, kwa sababu ametenda neno hili, na kwa sababu hakuwa na huruma. Basi Nathani akamwambia Daudi, Wewe ndiwe mtu huyo. Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nalikutia mafuta, uwe mfalme juu ya Israeli, nikakuokoa na mkono wa Sauli; nami nikakupa nyumba ya bwana wako, na wake za bwana wako kifuani mwako; nikakupa nyumba ya Israeli na ya Yuda; na kama hayo yangalikuwa machache, ningalikuongezea mambo kadha wa kadha. Kwa nini umelidharau neno la Bwana, na kufanya yaliyo mabaya machoni pake? Umempiga Uria, Mhiti, kwa upanga, nawe umemtwaa mkewe awe mke wako, nawe umemwua huyo kwa upanga wa wana wa Amoni. Basi, sasa upanga hautaondoka nyumbani mwako, kwa sababu umenidharau, ukamtwaa mkewe Uria, Mhiti, kuwa mke wako. Bwana asema hivi, Angalia, nitakuondokeshea uovu katika nyumba yako, nami nitawatwaa wake zako mbele ya macho yako, na kumpa jirani yako, naye atalala na wake zako mbele ya jua hili. Maana wewe ulifanya jambo lile kwa siri; bali mimi nitalifanya jambo hili mbele ya Israeli wote na mbele ya jua.”     

 

Je Daudi alivuna kile alichokipanda ? ona   Samuel 16:20-23 “Kisha Absalomu akamwambia Ahithofeli, Haya, toa shauri lako, tufanyeje. Naye Ahithofeli akamwambia Absalomu, Ingia wewe kwa masuria ya baba yako, hao aliowaacha ili kutunza nyumba; na Israeli wote watasikia ya kuwa umechukizwa kabisa na baba yako; ndipo itatiwa nguvu mikono yao wote walio pamoja nawe. Basi wakamtandikia Absalomu hema juu ya nyumba darini; naye Absalomu akaingia kwa masuria ya babaye machoni pa Israeli wote. Na shauri lake Ahithofeli, alilokuwa akilitoa siku zile, lilikuwa kama mtu aulizapo kwa neno la Mungu; ndivyo yalivyokuwa mashauri yote ya Ahithofeli, kwa Daudi, na kwa Absalomu.”

 

Muda hauwezi kutosha kuangalia kanuni ya kupanda na kuvuna namna inavyofanya kazi lakini kwa ufupi ni kanuni yenye kutisha sana ukipanda mema utavuna mema na ukipanda mabaya utavuna mabaya haijalishi ni katika siasa au kanisani au maisha ya kawaida, hatuna budi kuwa makini na mbegu tunazozipanda. Somo kuhusu uadilifu litatusaidia.

 

6.       Uadilifu unatukumbusha sisi Kutunza Heshima ya wazazi

               

Uadilifu ni pamoja na kutunza heshima ya wazazi Tangu mwanzo Mungu alikusudia wazazi wapewe heshima kubwa nay a kipekee sana sharia za uadilifu zilikuwa zinakataza vikali kuwavunjia heshima wazazi na hata wakati mwingine zilitoa maelekezo makali kwa mtu aliyevunja heshima kwa wazazi ikiwezekana hata kuuawa ona Kutoka 20:12 neno la Mungu linasema

 

Kutoka 20:12 12. Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.

 

 Wakolosai 3:20 “Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana

 

Waefeso 6:1-3 Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.”

               

Kwanini neno la Mungu linakazia kuwaheshimu baba na mama kuna watu walijiletea laana kwa kutokuwaheshimu wazazi wao, Biblia inaonyesha kuwa kuwadharau wazazi kuna madhara makubwa na athari kubwa katika maisha yetu ona

 

Mwanzo 9:20-26 “Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu; akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake. Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea.Akasema, Na alaaniwe Kaanani; Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.Akasema, Na atukuzwe BWANA, Mungu wa Shemu; Na Kaanani awe mtumwa wake.”             

 

Hamu alijiletea laana na kukosa Baraka za uzaliwa wa kwanza kwa sababu hakuufunika uchi wa baba yake, utupu wa baba yako usiufunue, ni wazi kuwa wazazi wetu wanapaswa kuheshimiwa sana ona pia

 

Mwanzo 39:3-4 “Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza, Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu.Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu, Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu.”

 

Kimaadili maswala haya hayakubaliki nani utovumkubwa sana wa kinidhamu na uadilifu kuna maswala ambayo kiuadilifu yakifanyika yanaweza kuwashangaza hata wapagani hasa kama yatafanywa na waaminio

 

1Wakoritho 5:1-5 “Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye. Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo. Kwa maana kweli, nisipokuwapo kwa mwili, lakini nikiwapo kwa roho, mimi mwenyewe nimekwisha kumhukumu yeye aliyetenda jambo hilo, kana kwamba nikiwapo. Katika jina la Bwana wetu Yesu, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na uweza wa Bwana wetu Yesu; kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu        

 

Maandiko yanaonya vikali kutokuwatendea wazazi mambo ya kijinga na ndio maana katika amri za uadilifu swala la kuwaheshimu wazazi limewekwa katika amri za Mungu za kutunza mahusiano, maandiko hayaruhusu hata kuwalaani wazazi Mafanikio hayawezi kumjia mtu anayemlaani baba yake na mama yake Mithali 20:20 “Amlaaniye babaye au mamaye, Taa yake itazimika katika giza kuu.” Maandiko pia yansisitiza wasikilizwe na wasidharauliwe ona Mithali 23:22 “Msikilize baba yako aliyekuzaa, Wala usimdharau mama yako akiwa mzeeMaandiko yanaonyesha wanaowadharau wazazi wanaweza kufa kifo kibaya Mithali 30:17 “Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling'oa, Na vifaranga vya tai watalila.”

 

Mtu anayejaribu kuwalaani au kuwasumbua alipaswa auawe ona Walawi 20:9 Kwa maana kila mtu amlaaniye baba yake au mama yake hakika atauawa, amemlaani baba yake na mama yake; damu yake itakuwa juu yake.             

 

Torati 21:18-21 “Mtu akiwa na mwana mkaidi, mshupavu, asiyetii sauti ya baba yake, wala sauti ya mama yake, nao wajapomwadhibu hawasikizi, ndipo babaye na mamaye na wamkamate, na kumpeleka kwa wazee wa mji wake, katika lango la mahali pake; wawaambie wazee wa mji wake, Huyu mwana wetu ni mkaidi, mshupavu, hasikizi sauti yetu; ni mwasherati, tena ni mlevi.Waume wote wa mji wake na wamtupie mawe, afe; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako; na Israeli wote watasikia na kuogopa.”

 

Kimsingi sio kuwa maandiko yanafurahia kuuawa kwa watoto, wote tunajua kuwa ni jambo gumu sana kuacha mwanao auawe lakini mpango wa Mungu ni usimamizi mahiri kuhusu wazazi waheshimike kwa msingi huo basi neno la Mungu linatutaka tuwaheshimu wazazi tena sio wet utu hata na wa wengine, tuwasalimie kwa heshima zote, tuwapokee, tusiwapite tuwasaidie kazi mbalimbali na kuwatii na ikuwasikiliza katika mahusia yao na maagizo yao hususani ambaye hayako kinyume na mapenzi ya Mungu.

 

7.       Uadilifu unatukumbusha sisi Kutunza Heshima ya Mungu:

 

Somo kuhusu maadili pia linamtaka kila mwanadamu duniani kutambua uwepo wa Mungu na kumpa heshima yake katika amri za maadili amri kama tatu za mwanzoni ziko kwaajili ya kuhakikisha kuwa heshima ya Mungu inatunzwa

 

Kutoka 20:1-7 “Mungu akanena maneno haya yote akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu. Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.”  

 

Kwa kawaida neno la Mungu linamuhesabia mtu yeyote asiyeamini katika kuwepo kwa Mungu kuwa ni mpumbavu na kamwe maandiko hayana Muda wa kufanya kazi ya kutibitisha kuwa Mungu yupo Lakini neno la Mungu lilianza kwa kusema hapo mwanzo Mungu kwa hiyo kila anayewaza hata moyoni mwake kuwa hakuna Mungu anaitwa mpumbavu ona

 

Zaburi 53:1-3 “Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza, Hakuna atendaye mema. Toka mbinguni MUNGU aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu.Kila mtu amepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja.”

 

Mungu anawajali wanadamu na kuwapenda katika kiwango kikubwa sana na cha hali ya juu, lakini kwa muda mrefu wanadamu wengo na mataifa mengi yamepuuza sana maswala mbalimbali kuhusu Mungu na watu wengi wameshindwa kumuheshimu, unapoangalia sera za kijamaa ni ukweli ulio wazi kuwa ni sera nzuri sana ukilinganisha na za kibepari, hata hivyo tatizo kubwa la sera ya kijamaa ilitaka kuishi kwa ujamaa bila kujali mambo ya Mungu, na hatimaye ujamaa ulianguka, Ujamaa wa kwanza ulifanyika huko Babeli.

 

Mwanzo 10: 1-8. “Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja. Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko. Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. BWANA akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu. BWANA akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao. Basi BWANA akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji

 

Mungu huwa anasikitishwa mno pale wanadamu wanapomdharau na kumsahau, kwa ujumla tunapojifunza kuhusu uadilifu Mungu ndio mwalimu mkuu wa somo hilo hivyo ni wazi kuwa uadilifu unatoka kwa Mungu,

 

Isaya 1: 3-5 “Ng'ombe amjua bwana wake, Na punda ajua kibanda cha bwana wake; Bali Israeli hajui, watu wangu hawafikiri. Ole wake, taifa lenye dhambi, watu wanaochukua mzigo wa uovu, wazao wa watenda mabaya, watoto wanaoharibu; wamemwacha Bwana, wamemdharau yeye aliye Mtakatifu wa Israeli, wamefarakana naye na kurudi nyuma. Mbona mnataka kupigwa hata sasa, hata mkazidi kuasi? Kichwa chote ni kigonjwa, moyo wote umezimia.”

 

Ukweli kuhusu Mungu umedhihirishwa tangu mwanzo, lakini wanadamu kwa kujifikiri kuwa wana akili walijipumbazika na kumvunjia Mungu heshima kwa kuendelea kuishi bila uadilifu

 

Warumi 1:21-25  Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia. Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru; kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;  wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo. Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao.Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina.”

 

Kwa msingi huo sasa unaweza kuona mwenye uumbaji wake anataka aheshimiwe na anakasirishwa sana na watu wanapoacha kujali na kupuuzia kuwa hakuna Mungu au kuzitegemea akili zao wenyewe, watu wengi wanashindwa

 

Mithali 3:5-7 “Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako. Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche Bwana, ukajiepushe na uovu.”

 

Mmiliki wa Meli ya Tutanic ambayo kihistoria ilikuwa meli kubwa sana ya kifahari iliyokuwa na viwanja vya michezo, makasino, na hoteli na uwezo wa kubeba watu 1,500 alipoulizwa kuhusu uimara wa maeli hiyo alisema HATA MUNGU HAWEZI KUIZAMISHA, lakini habari mbaya ilipatikama siku moja mara baada ya kuanza safari kwa meli hiyo kutoka uingereza kuelekea Marekani Tarehe April 14-15, 1912 meli hii kubwa ilipata ajali na kuzama baada ya kugonga mwamba wa barafu na kuzama na watu wengi sana walikufa  kwa nini bila shaka kwa sababu ya kumdharau Mungu.

 

Mathayo 22;37-38 “Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.”

 

Maandiko yanatuamrisha kumpenda Mungu, hatuwezi kwa namna yoyote kuwa waadilifu kama hatumpi Mungu nafasi ya kwanza, Mungu anapaswa kuheshimiwa kwa moyo, na kwa matendo yetu na kwa mali zetu, na kwa ujumla   lakini sio hivyo tu hata mafanikio yetu yanapaswa kuonyesha kuwa yanatokana na Mungu, vyeo na nafasi mbali mbali zinatokana na Mungu

 

Daniel 4: 29-37Baada ya miezi kumi na miwili, alikuwa akitembea ndani ya jumba la kifalme katika Babeli. Mfalme akanena, akasema, Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe kao langu la kifalme, kwa uwezo wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu? Hata neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema, Ee mfalme Nebukadreza, maneno haya unaambiwa wewe; Ufalme huu umeondoka kwako. Nawe utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni; utalishwa majani kama ng'ombe, na nyakati saba zitapita juu yako, hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, awaye yote. Saa iyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadreza; alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng'ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege.Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadreza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi; na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe? Basi wakati uo huo fahamu zangu zikanirudia, na kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu, enzi yangu na fahari yangu zikanirudia; na mawaziri wangu, na madiwani wangu, wakaja kunitafuta; nami nikathibitika katika ufalme wangu, nikaongezewa enzi kupita kiasi. Basi mimi, Nebukadreza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili.”

 

Mungu anawaheshimu wale wanaomuheshimu 1Samuel 2:30 Kwa sababu hiyo, Bwana, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; lakini sasa Bwana asema, Jambo hili na liwe mbali nami; kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu.” Kwa msingi huo katikanuadilifu wetu ni muhimu kwetu kukumbuka kuliheshimu jina la Mungu wetu uadilifu ni pamoja na kumtanguliza Mungu katika maisha yetu yote!

 

8.       Uadilifu unatusaidia sisi Kufikiri kwa undani kila aina ya tendo.

 

Tunapojifunza kuhusu uadlifu katika ukristo haimaanishi tu kujua mema na mabaya bali pia kuangalia mambo ambayo kibnadamu yanaweza kuleta utata mkubwa katika maisha ya kila siku na hata kutufarakanisha na Mungu, kwa hiyo tunapijifunza kuhusu uadilifu hatuangalii tu tendo lenyewe bali pia mtazamo wa mtu kuhusu hilo tendo, nia ya mtu kuhusu hilo tendon a matokeo ya mtu kuhusu hilo tendo, kwa mfano wote tunafahamu kuwa kutoa mimba ni dhambi, lakini wakati mwingine mahospitalini linaweza likatokea jambo lenye utata na kutaka kuamua kama mama afe ili mtoto aishi au mtoto aishi ili mama afe, au mimba imetunga katika eneo lisilo sahihi na hivyo inahatarisha maisha ya mama mjamzito, mguu ukatwe ili kuokoa maisha ya mtu na kadhalika kwa hiyo yako mazingira ambayo unaweza kujikuta katika mazingira magumu na ukashindwa ni jambo gani la kuamua,

 

Kutoka 1:15-17 “Kisha mfalme wa Misri akasema na wazalisha wa Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua; akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi. Lakini wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, wasifanye kama walivyoamriwa na huyo mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale wanaume.”

 

Shifra na Puah wazalisha wa waebrania walikuwa na wakati Mgumu wa kuamua kutii amri ya kifalme na Mungu kwa kutikuwaua watoto, waliamua kumtii Mungu na kuwaacha hai watoto, kuna matukio mengine yanaweza kutokea na yakakupa wakati mgumu sana kujua uadilifu wake unatakaje

 

Hesabu 15:32-36 “Kisha wakati huo wana wa Israeli walipokuwako jangwani, wakamwona mtu mmoja akikusanya kuni siku ya Sabato. Hao waliomwona akikusanya kuni wakamleta kwa Musa na Haruni, na kwa mkutano wote. Nao wakamweka kifungoni, maana, lilikuwa halijasemwa atakalotendwa.  Bwana akamwambia Musa, Mtu huyo lazima atauawa; mkutano wote watampiga kwa mawe huko nje ya marago. Basi mkutano wote wakampeleka nje ya marago, nao wakampiga kwa mawe, akafa; kama Bwana alivyomwagiza Musa

Yako maswala mengine yanahitaji sana kujua mapenzi ya Mungu ili kuweza kujua undani wake na maamuzi ambayo tunaweza kuyachukua katika kuyatafuta mapenzi ya Mungu tunahitaji wakati mwingine kuwa na Muda wa kutafakari, wakati wa kutafakari hatuna budi kufikiri

1.       Neno la Mungu linasema nini

2.       Ufahamu kuhusu ukweli na hali halisi

3.       Ufahamu wetu wenyewe

4.       Ushauri wa wengine

5.       Mabadiliko ya mazingira

6.       Mioyo yetu na dhamiri zetu

7.       Roho yetu na nafsi zetu kama wanadamu

8.       Uongozi wa Roho Mtakatifu

Baada ya kuyafikiri hayo kwa undani Hekima ya kiungu inatuongoza katika kujua jambo Fulani ni dhambi au la.

9.       Uadilifu unatuweka katika nafasi ya kupokea  Baraka mbalimbali.

 

Kuishi kwa uadilifu ni kuishi kwa kumtii Mungu na Baraka zote asili yake ni utii, maandiko yanatuthibitishia ya kuwa Tunapokea Baraka kubwa sana kwa kumtii Mungu ona

 

Mwanzo 12:1-3 “BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa”.       

Baraka za Mungu zitamiminika kwetu ikiwa tutaishi sawa na maagizo yake ya uadilifu, lakini laana kubwa zitatupata ikiwa hatutafuata au kuishi sawa na maagizo yake ya uadilifu

 

Kumbukumbu la Torati 28:1-6 Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo.”

 

Maandiko pia yameidhinisha wazi kuwa kama hatutatii maagizo ya Mungu kuna laana chungu nzima zitaambatana nasi katika maisha yetu Kumbukumbu la Torati 28:15-21 “Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata. Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani. Litalaaniwa kapu lako na chombo chako cha kukandia. Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na utokapo, Bwana atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo.Bwana atakuambatanisha na tauni, hata atakapokwisha kukuondoa katika nchi uingiayo kwa kuimiliki.”

 

Isaya 1:18-20 “Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha Bwana kimenena haya

 

Agano jipya linatufundisha kuwa kuna Baraka mbalimbali za kila namna zinazowajia watu wanaoishi maisha ya utii yaani maisha ya uadilifu moja ya Baraka hiyo ni furaha Yohana 15:10-11 “Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe.”

 

Lakini sio hivyo tu kunakuwa na furaha kubwa sana ya kumtii na kumpendeza Mungu kwa sababu kuna hukumu pia mbele za Mungu 2Wakoritho 5:9-10 “Kwa hiyo, tena, ikiwa tupo hapa, au ikiwa hatupo hapa, twajitahidi kumpendeza yeye. Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.” na Wakolosai 1;10 “mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu;”

Na ndio maana maandiko hayawataki wakristo waishi chini ya kiwango wala kufuatisha viwango vya dunia hii, sisi tunapaswa kuwa mstari wa mbele Warumi 12:2 “Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.”

 

Kuishi kwa uadilifu kunatupa kumpendeza Mungu na kunaleta Baraka nyingi sana katika maisha yetu.

 

10.   Uadilifu unatufunza jinsi ya kuwa na tabia za uungu.

 

Wanadamu wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu Mwanzo 1:27 “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba”.

 

Kuumbwa kwa mfano wa Mungu ni kuumbwa katika uadilifu na sifa kama za Mungu, baada ya anguko uadilifu wa mwanadamu uliathiriwa, hata hivyo Mungu ametufunza mfano wake ili tuufuate, Mungu anabaki pake yake mwema na asiyebadilika na wa milele, kiwango chake cha uadilifu anachokidai kwa wanadamu ni kile ambacho yeye mwenyewe anacho na kwa sababu hiyo anahaki ya kukidai kutoka kwa wanadamu wote wa tamaduni yoyote ile na historia. Matakwa haya haya yako kwa wingi katika neno lake ingawaje vilevile ziko amri nyingine amezidai kwa watu maalumu na kwa wakati maalumu, Mungu ni Pendo na hivyo anawataka watu wote kuwa na upendo

 

 1Yohana 4:19-21 “Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza. Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona. Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.”

 

Mungu ni mtakatifu na kwa sababu hiyo anayo haki ya kutudai kuwa watakatifu katika mwenedno wetu wote

 

1Peter 1:15 -16 “bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;    kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.” Hali kadhalika Mungu ni mwingi wa rehema hivyo nasi tunaagizwa kuwa na rehema, Luka 6:36 “Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.” Yeye ni mwaminifu na hivyo ni haki yake kutuagiza nasi kuwa waaminifu na kutokutoa ushuhuda wa uongo Tito 1:2 katika tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema uongo aliuahidi tangu milele; Kutoka 20:16 “Usimshuhudie jirani yako uongo”. Mungu ni mwadilifu kwa msingi huo anaagiza sisi tuwe waadilifu kama yeye alivyo anachokiagiza sio kigumu kwetu Mungu anajua kuwa tunaweza kwa sababu alituumba tuwe waadilifu, mwanadamu wa kwanza alikuwa mwadilifu ni mpaka Shetani alipoharibu sifa za uadilifu kwa msingi huo ni madai sahihi ya Mungu kwetu kutuagiza kuishi kwa uadilifu na kuudai uadilifu.

Hitimisho!

Uadilifu ndio asili kamili ya uanadamu, kila mwanadamu aliumbwa awe mwema kwa asili, tabia mbaya na mambo yasiyopendeza yalikuwa ni matokeo ya dhambi, na ndio maana sio msingi wa kuokolewa kwetu lakini ni msingi wa ubinadamu wetu, hivyo uwe umeokolewa au la kila mmoja anapaswa kuishi kwa uadilifu hili ni jukumu la dunia nzima bila kujali unaamini nini

Waefeso 2:1-10 “Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine. Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu; ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu. Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;  wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.”

Na mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Rev. Innocent Kamote.

Hakuna maoni: