Nehemia 8:9-11 “Naye Nehemia, ndiye
aliyekuwa Tirshatha, na Ezra kuhani, mwandishi, na Walawi waliowafundisha watu,
wakawaambia watu wote, Siku hii ni takatifu kwa Bwana, Mungu wenu; msiomboleze
wala msilie. Maana watu wote walilia, walipoyasikia maneno ya torati. Kisha
akawaambia, Enendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena
mpelekeeni sehemu yeye asiyewekewa kitu; maana siku hii ni takatifu kwa Bwana
wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu. Hivyo Walawi
wakawatuliza watu wote, wakasema, Nyamazeni, kwa maana siku hii ni takatifu;
wala msihuzunike.”
Utangulizi:
Ni muhimu kujikumbusha wazi
Kwamba Mwanadamu katika maumbile yake ni kiumbe chenye Hisia, “Human being is Emotional being” Na kwa
sababu ya kuumbwa tukiwa na hisia wakati mwingine tunaweza kukutana na kupanda
au kushuka kwa hisia zetu katika maisha ya kila siku, kuna wakati tunaweza
kupenda na kuna wakati tunaweza kuchukia, wakati mwingine tunaweza kuwa na
furaha na wakati mwingine tunaweza kuwa na huzuni, wakati mwingine kujiamini na
wakati mwingine wasiwasi, wakati mwingine ujasiri wakati mwingine hofu, hii ni
hali ya kawaida ya maumbile ya mwanadamu, Hisia zetu zinatusaidia kukabiliana
na mazingira yetu, kama tutakuwa na siku nzuri tunaweza kuwa na furaha na kama
siku hiyo inaweza kuwa mbaya tunaweza kuwa na fadhaa, timu tunazoshabikia
zikipata ushindi tunaitikia kwa kufurahi, timu tunazoshabikia zikishindwa tunaitikiwa
kwa kuwa na huzuni, tunapopata zawadi za kushitukizwa tunafurahi, tunapopata
habari za huzuni, tunahuzunika, ni Muhimu kufahamu kuwa sio mapenzi ya Mungu
kuwahuzunisha watu wake ona
Maombolezo 3:31-33 “Kwa kuwa Bwana
hatamtupa mtu Hata milele. Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya
wingi wa huruma zake. Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala
kuwahuzunisha”
Tutajifunza somo hili FURAHA YA BWANA NI NGUVU ZENU Kwa
kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo:-
·
Maana
ya Neno Furaha
·
Mafundisho
ya Neno la Mungu kuhusu Furaha
·
Furaha ya
Bwana ni nguvu zenu.
Maana ya neno Furaha
Neno Furaha katika Biblia ya
kiingereza linasomeka kama JOY na
tafasiri ya neno JOY katika kamusi
ya kiingereza JOY – “The climax of Great
pleasure and happiness”, or Feeling great pleasure and happiness, Katika
Lugha ya kibiblia inayotumika katika uhusiano na neno hilo, Kwa Kiibrania ni “CHEDVAH” ambalo tafasiri
yake ni Gladness au rejoicing - a state
of well – being, and contentment katika
kiyunani ni “CHARA” ni hali ya kuwa
na furaha, na kuona kuwa mambo yako vizuri na kuridhika kuwa hakuna wasiwasi
hata kama Mazingira hayaonyeshi kuwa hivyo, Ni uwezo wa kushinda mazingira ya
kuhuzunisha na kuonyesha ukomavu hata kama mazingira hayo hayaonyeshi au kutia
moyo kufurahi.
Mafundisho ya neno la Mungu kuhusu Furaha
Kama tulivyoona maana ya neno
furaha hapo juu, Neno la Mungu linatufundisha kuwa furaha hii sio furaha ya
kawaida furaha hii inaitwa furaha ya Bwana
Nehemia 8:10 “Kisha akawaambia, Enendeni zenu, mle kilichonona, na
kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyewekewa kitu; maana siku
hii ni takatifu kwa Bwana wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya Bwana ni
nguvu zenu.”
Ukiifahamu furaha hii
nakuhakikishia kuwa maisha yako hayatakuwa kama yalivyo na hasa kama
tutahakikisha kuwa tunatembea katika furaha hiyo siku zote za maisha yetu!
Furaha hii inatokana na Mungu mwenyewe ona
Wagalatia 5:22 “Lakini tunda la Roho ni
upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,”
Kwa mujibu wa maandiko furaha hii
haitokani na hisia zetu, Furaha hii ni tunda la Roho Mtakatifu katika maisha
yetu ya kila siku, Ni furaha inayotoka kwa Mungu mwenyewe, ni furaha kutoka kwa
Roho Mtakatifu, furaha hii ikiwa ndani ya Mtu huwa haijalishi mazingira yakoje,
Furaha hii inaangalia mbele ya mapingamizi, haikufanyi kuchoka wala haikufanyi uzimie
moyo ona
Waebrania 12:2-3 “tukimtazama Yesu, mwenye
kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa
mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume
wa kiti cha enzi cha Mungu. Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili
mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije
mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu.”
Furaha hii sio inayotokana na
hisia ni furaha inayotokana na karama ya Mungu kwa watu wake inaambatana na
uwezo mkubwa sana wa kuvumilia na kukufanya uwe wa kawaida katika mazingira yoyote
Warumi 5:3-5 “Wala si hivyo tu, ila na
mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi; na
kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini; na
tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika
mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi.”
Kuna utamu Fulani kama utasoma
kifungu hiki katika lugha ya kiingereza kwa wale wanaokifahamu kidogo ona
Romans 5:3-5 “Not only so, but we also
rejoice in our Sufferings, because we know that suffering produces
perseverance, Perseverance character and character hope and hope does not
disappoint us because, God has poured out his love into our hearts by the Holy
Spirit whom he has given us”
Unaona kwa hiyo ni furaha
inayotokana na upendo wa Mungu uliomiminwa kwetu na Roho Mtakatifu, hivyo hata
wakati wa mateso utawezxa kuona bado furaha hiyo inatawala na haiondolewi na
chochote kwa sababu inatazama mbele ya mateso ambako kuna utuklufu mkubwa !
Furaha hiyo sio ya muda, sio ya
hisia haitokanani na hali ya mazingira kwamba leo nimepata au nimekosa wala
haiwi sawa na ya waliovuna mashamba na zabibu
wala ya maadui zetu ambayo hiyo ni ya kitambo tu , Furaha hii inatoka
kwa Bwana na inazidi furaha ya kawaida ona
Zaburi 4:7-8 “Umenitia furaha moyoni
mwangu, Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai. Katika amani nitajilaza na
kupata usingizi mara, Maana Wewe, Bwana, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa
salama.”
Furaha ya Bwana ni Nguvu zetu !
Baada ya kuwa tumeona maana ya
Furaha na jinsi maandiko yanavyoielezea furaha hiyo sasa turudi katika Mistari
ya msingi kwa nini Nehemia anasema furaha ya Bwana ni Nguvu yenu?
Nehemia 8:9-11 “Naye Nehemia, ndiye aliyekuwa Tirshatha, na Ezra kuhani,
mwandishi, na Walawi waliowafundisha watu, wakawaambia watu wote, Siku hii ni
takatifu kwa Bwana, Mungu wenu; msiomboleze wala msilie. Maana watu wote
walilia, walipoyasikia maneno ya torati. Kisha akawaambia, Enendeni zenu, mle
kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyewekewa
kitu; maana siku hii ni takatifu kwa Bwana wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa
furaha ya Bwana ni nguvu zenu. Hivyo Walawi wakawatuliza watu wote, wakasema,
Nyamazeni, kwa maana siku hii ni takatifu; wala msihuzunike.”
Israel walikuwa wamepelekwa katika
utumwa kihistoria na utumwa huo haukuwa mzuri, wanakumbuka historia chungu ya
utumwa wao, na sasa Mungu alikuwa amewapa neema ya kurejea katika nchi yao, na
chini ya Zerubabeli walikuwa wamelijenga tena Hekalu, na chini ya Nehemia
walikuwa wameujenga ukuta wa Yerusalem na
Nehemia akiungana na Ezra, Ezra aliwasomea watu Torati na kuwakumbusha
maneno yote ya Mungu, na hivyo Israel waligundua kuwa walikuwa kinyume na
maagizo ya Mungu walikuwa wamekengeuka walisahau maagizo ya Bwana hivyo
walipoyasikia maneno ya tarati walilia sana na kuhuzunika, walilia machozi,
walijihukumu kuwa huenda wamemkose Mungu na labda walitaka kuomboleza badala ya kulia na kuomboleza Nehemia
aliwaambia hapana hakuna sababu ya kulia na kuomboleza badala yake walitakiwa kufurahia na kuchinja vitu vinono
na kufanya sikukuu unaona :-
Nehemia 8:10-12 “Kisha akawaambia, Enendeni
zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye
asiyewekewa kitu; maana siku hii ni takatifu kwa Bwana wetu; wala msihuzunike;
kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu. Hivyo Walawi wakawatuliza watu wote,
wakasema, Nyamazeni, kwa maana siku hii ni takatifu; wala msihuzunike. Na watu
wote wakaenda zao kula na kunywa, na kuwapelekea watu sehemu, na kufanya furaha
nyingi, kwa sababu walikuwa wameyafahamu maneno yale waliyohubiriwa.”
Kwa kawaida watu wanapokuwa
katika huzuni wanafunga na kuomba, wanalia, wanagalagala kwenye majivu na kuvaa
magunia, hii ndio ilikuwa nia ya watu, walidhani kuwa kila wakati wanapaswa
kuomboleza, unapogundua kuwa umekosea sio kila wakati unapaswa kulia na
kuhuzunika na kuomboleza na kufunga na kuomba, unapopita katika magumu sio kila
wakati unapaswa kutumia njia ileile
wakati mwingine unachohitaji ni kupiga kelele za shangwe ni kufurahi ni
kujisamehe ni kumuachia Mungu atende kazi yake, kile kitendo tu cha kujua kuwa
umekosea ni tayari kazi ya Roho Mtakatifu imefanyika ndani mwako wakati
mwingine nenda kachinje ule ufurahi kafanye sikukuu! Adui yetu shetani anataka
kuona tunalia tu wakati wote anatarajia tuwe katika taharuki tu lakini iko siri
mwamini Mungu ya kuwa atakupa siku yenye furaha kila aunapoamka asubihi
usiitarajie siku yako wiki yako mwezi wako mwaka wako kuwa mbaya wewe mwambie
Mungu aachilie ile karama yake na tunda lake la furaha hilo linatosha sana
kutuweka huru
Zaburi 118:24 “Siku hii ndiyo aliyoifanya
Bwana, Tutashangilia na kuifurahia.”
Nisikilize kama Nehemia aliweza
kugundua katika nyakati za agano la kale kwamba badala ya watu kulia, badala ya
kuhuzunika, badaya ya kufunga na kuomba na kuvaa magunia na kujipaka majivu,
Basi wanaweza kutumia silaha ya kufurahia kula pamoja kugawa vyakula kutoa kwa
niaba kwaajili ya wengine kwa sababu fuaraha ya Bwana itawapa nguvu, Ni furaha
kutioka kwa Roho wake Mtakatifu, kwa hiyo katika changamoto zozote unazozipitia
usiangalie mazingira wewe furahi, Mungu
anatupenda kiasi kwamba alimtoa Yesu kufa msalabani kwa niaba yetu, kwa hiyo
sio mwakati wetu tena kubeba mateso, ni wakati wetu kufurahi, Hakuna wa
kutukwaza,
Hitimisho !
Unawezaje kuwa na furaha ya Bwana katika maisha yako?
-
Hakikisha kuwa unawapoa watu vitu, Matendo 20:35 “Katika
mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia
wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni
heri kutoa kuliko kupokea.” Kutoa kwa kawaida huwa kunaleta furaha,
Ne heri kutoa kuliko kupokea, katika andiko la Msingi Nehemia aliwaambia watu
wakatioe wawape wakle ambao hawana kitu ili watu wafurahie pamoja kumbe katika
kutoa utaweza kuona furaha ya Bwana ndani yako!
-
Kaa katika uwepo wa Mungu 1Nyakati 16:27 “Heshima na adhama ziko
mbele zake; Nguvu na furaha zipo mahali pake.”
-
Jawa na wingi wa shukurani, Msifu Mungu Zaburi
43:4 “Hivyo nitakwenda madhabahuni kwa Mungu, kwa
Mungu aliye furaha yangu na shangwe yangu; Nitakusifu kwa kinubi, Ee MUNGU,
Mungu wangu.”
-
Uwe mtu wa ibada na kumujua Mungu Zaburi 122:1 “Nalifurahi
waliponiambia, Na twende nyumbani kwa Bwana”.
Furaha ya bwana ni Nguvu zetu kwa
sababu inatupa amani ya kweli ambayo huwezi kuipata katika mitandao ya kijamii,
huwezi kuipata kwa fedha, huwezi kuipata kwa marafiki, kwa kwenda pikiniki, kwa
kufanya ngono, kwa kula madawa ya kulevya, kwa kunywa pombe, kwa kucheza disco
hayo yanaweza kukupa furaha ya muda lakini iliyojawa na majuto, Furaha ya kweli
unaweza kuipata ndani ya Yes utu!
Na Rev. Innocent Samuel Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni