Wakati wa kufanya agano la chumvi.
- Mizimu, mapepo, shetani na wachawi na waganga au
makuhani wa kichawi huwaathiri watu katika maisha yao na kusababisha
msongo wa mawazo, kwa kutumia nguvu za giza, kwa kutumia nguvu hizo za
giza na za kichawi wanawasababishia watu kupoteza mwelekeom kuwa na
bumbuwazi, kuteseka, kuelemewa, kuwa na uzito na kupata changamoto za
kifedha na kiuchumi na changamoto nyinginezo nyingi.
Uchawi ni silaha ya giza inayotumiwa
na wachawi kwa kusudi la kuharibu maisha ya watu wanaofanikiwa na
kufanikiwa katika mazingira mbalimbali,
silaha hiyo ya giza ni silaha ya kiroho lakini matokoe yake hutokea katika hali
halisi.kuteseka kwa watu waliorogwa au kuchawiwa kunategemeana na nguvu
iliyotumika katika kunuiziwa nguvu za mashambulizi
Pepo watatafasiri uchawi na manuizo
na kuyawasilisha kwa watu waliolengwa na kuwashambulia na matokeo yanaweza
kutokea katika ulimwengu wa miili yao, mambo magumu na matukio ya ajabu huanza
kutiokea katika maisha yao na njia pakee ya kuimarisha na kuleta ukombozi ni
agano la chumvi
Ukombozi kupitia gano la chumvi ni
rahisi sana kwa muonekano lakini una nguvu kubwa za ajabu sana, ukombozi huu
una nguvu ya kuondoa kabisa maedhara ya nguvu zisizoonekana za kichawi na
kuukausha au kuuondoa kabisa na kuondoa hali ya kushindwa kwa sababu zozote
zile, kwa kufanya hivyo haimaanishi oia mkuwa tutaacha kabisa kuschughulikia
nguvu za giza kwa namna za kawaida, lakini tutaendelea ili kuhakikisha kuwa
tunaendelea kukua kiroho.
- Unafanya gano
la Chumvi wakati gani?
Tunafanya agano la chumvi wakati
tunapohisi kuwa kuna matukio ya vita za kiroho zilizohusisha nguvu za giza, ni
kweli kwamba mtu aliyeokoka hawezi kushambuliwa na nguvu za giza kwa sababu
imeandikwa hakuna ugaga wala uchawi juu ya Yakobo Hesabu 23:23 “Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga
juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani
aliyoyatenda Mungu!”
Lakini kumbuka tuna mashambulizi
kutoka kwa mamadui, tuko vitani, majeshi ya pepo yanatumwa kwetu kwa mauizo na
sadaka za iana mbalimbali na kwa maelekezo ya aina mbalimbali kwa hiyi kuna
kiwango cha mashambulizi ambayo tunakutana nayo wakati mwingine kwa asilimia 30
au 60 au 90 kwa hiyo wote kwa kiwango Fulani tunashambuliwa na nguvu za giza
kulingana na kiwango za kuzaa kwetu matunda kumbuka mfano wa zile mbegu
zilizoangukia kwenye udongo mzuri Marko
4:8 “Nyingine zikaanguka penye udongo ulio mzuri,
zikazaa matunda, zikimea na kukua, na kuzaa, moja thelathini, moja sitini, na
moja mia.” Kama ukuaji wetu wa kiroho unaweza kuzaa matunda kwa
asilimia hizo zilizotajwa ni dhahiri na mashambulizia yanaweza kuwepo kutokana
na kiwango kwa hiyo niia nyepesi ya kuondoa kiwango hicho cha mashambulizi ya
nguvu za giza ni kwa kutumia ganano la chumvi
na ukifanya mara kwa mara unaziondoa kabisa katika mwili wako tunaweza
kujitibu kwa agano la chumvi mara unapohisi au kusikia changamoto hizi:-
-
Uchovu wa
kimwili na kiroho
-
Kupoteza hamasa
-
Kupoteza uwezo
wa kufikiri
-
Kuelemewa na
mawazo
-
Hasira za kupita
kawaida
-
Mgandamizo wa
mawazo stresses
-
Aina yoyote ya
ugonjwa na wakati wowote unapokuwa unahisi kuwa kuna uvamizi na hali isiyo ya
kawaida katika mwili wako, uchumi wako, kazi yako, huduma yako na roho yako.
-
Lakini pia
udhaifu wowowte wa kimwili, kiroho na kihisia ujue kuna mashambulizi ya mizimu,
mapepo, wachawi na kadhalika basi unahitaji tiba ya agano la chumvi.
- Mambo
unayohitaji kwaajili ya kutekeleza agano la chumvi
-
Utahitaji ndoo
au beiseni
-
Utalijaza maji
safi kwa asilimia 50% yaani nusu
-
Utahitaji
chumvi yam awe kwa kiwango chochote kana huna ya mawe unaweza kutumia ya mezani
lakini ya mezani uwezo wake utapungua kwa asilimia 30% ukilinganisha na ile ya
mawe
-
Taulo la
kujikaushia
-
Na sehemu ya
kukanyajia
-
- Jinsi ya
kufanya ibada ya agano la chumvi.
1.
Weka maji
kwenye ndoo yajae kwa asilimia 50% yaani nusu yake kwa kiwango tu cha kufunika
enka za miguu
2.
Weka vijiko
vidogo viwili vya chumvi ya mawe
3.
Omba kwa
kumaanisha na kwa imani kwamba Mungu akuondolee nguvu zote za giza, pia omba maalumu
kwaajili ya kuziharibu kabisa na kuzibomboa nguvu zote za mizimu, pepo, waganga
na wachawi na kila manuizo yaliyofanywa kinyume nawe na kukuletea athari, omba
maombi ni muhimu sana na yana uwezo mkubwa sana yanapofanyika sambaba na ibada
hii ya ukombozi.
4.
Hakikisha
umekaa sawa sawa na miguu yako hususani enka ziwe zimezama katika maji, miguu
yako isigusane bali iwe mbalimbali kati ya sentimita 2-3 hii inasaidia kuodoa
uchawi wote uliorogwa kwa nguvu za giza, kama miguu yako itagusana itakuwa
kikwazo kwa ibada hii,
5.
Hakikisha miguu
inakaa kati ya dakika 10-15 na usizidishe zaidi ya dakika 15, ukizidisha nguvu
za giza zinazotoka kwa njia ya miguu zinaweza kuingia mwilini mwako
6.
Wakati miguu
yako inapokuwa katika maji yenye chumvi anza kuomba au kunuiza kwa jina la
Yesu Mungu au kuimba maombi
7.
Wote wenye
pumzi wote waishio duniani wote wampendao
(Wamchao) Mungu na waseme fadhili zake ni za milele
8.
Wote wanaoeneza
habari zake watangazao habari njema duniani kote na waseme fadhili zake ni za
milele.
Kwa ufupi utaimba zaburi 118:1-14
1. Haleluya. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa
maana fadhili zake ni za milele.
2. Israeli na aseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za
milele.
3. Mlango wa Haruni na waseme sasa, Ya kwamba fadhili
zake ni za milele.
4. Wamchao Bwana na waseme sasa, Ya kwamba fadhili
zake ni za milele.
5. Katika shida yangu nalimwita Bwana; Bwana akanijibu
akaniweka panapo nafasi.
6. Bwana yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu
atanitenda nini?
7. Bwana yuko upande wangu, msaidizi wangu, Kwa hiyo
nitawaona wanaonichukia wameshindwa.
8. Ni heri kumkimbilia Bwana Kuliko kuwatumainia
wanadamu.
9. Ni heri kumkimbilia Bwana. Kuliko kuwatumainia
wakuu.
10. Mataifa yote walinizunguka; Kwa jina la Bwana
naliwakatilia mbali.
11. Walinizunguka, naam, walinizunguka; Kwa jina la
Bwana naliwakatilia mbali.
12. Walinizunguka kama nyuki, Walizimika kama moto wa
miibani; Kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.
13. Ulinisukuma sana ili nianguke; Lakini Bwana
akanisaidia.
14. Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu, Naye amekuwa
wokovu wangu.
Hitimisho:
Baada ya kumaliza maombi haya ya ukombozi kulinga nan
a mahitaji yako unaweza kuanza kumshukuru Mungu kwa ulinzi wake anaokupa na
namna anavyokuzunguka
Utayamwaga maji yake chooni na kisha utasafisha ndoo
na maji safi. Utakausha miguu yako vema kwa taulo na kisha utajipaka mafuta ya
mzeituni na kuomba Mungu akupeleke kwenye kiwango kingine cha maswala
mbalimbali uyatakayo. Ibada inaweza kufanyika pia kwa makusudi mbalimbali
ambayo mengine hayajaainishwa katika somo hili mfano kuweka wakfu, kiongozi,
kujilinda na cheo chako na kadhalika
Mwisho wa ibada hii.
Matokeo:
- Athari zote za nguvu za Giza na mashambulizi ya
wachwi, waganga na mapepo na shetani zinaondoka
- Maji ya agano la chumvi yana nguvu kubwa sana
yenyewe tu kunyonya nguvu zote za giza
- Nguvu za giza na magonjwa yote yanayoambatana na
nguvu hizo yanaondoka na wakati mwingine maji yanaweza kuwa na rangi
nyeusi kama ishara ya kuondoka kwa nguvu hizo, au yanaweza kuwa na
uvuguvugu au yakawa na harufu mbaya hii ni shara ya vitu vibaya kuondoka
mwilini mwako
KUMBUKA: Somo hili lina uhusiano na huduma za kinabii,
sio vizuri kufundisha au kulifanyia kazi kanisani ikiwa huamini katika huduma
za kinabii
Na Rev. Innocent Samuel Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye hekima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni