Jumanne, 19 Machi 2024

Kanisa kubwa !


Luka 14:21-23 “Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete. Mtumwa akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa ingaliko nafasi. Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa.”



Lakewood Church ni Kanisa linaloongozwa na Mchungaji Joel Osteen, jijini Houston Texas Nchini Marekani  ni kanisa kubwa lenye washirika wapatao 45,000, Kanisa hili lina uwezo wa kuketisha watu 16,800 kwa wakati wa ibada moja na wana ibada nne za kiingereza na ibada mbili za Kihispania kwa wiki, hii ni moja ya mfano wa Kanisa kubwa

 

Utangulizi:

Ni muhimu kufahamu kwamba mara nyingi sana tunajifunza jinsi ya kupanda makanisa, na aina ya makanisa tunayopaswa kupanda, Lakini vile vile tunajifunza kuhusu uamsho, kukua kiroho na maswala yanayofanana na hayo, tukihimiza kuhusu uinjilisti umisheni na mengineyo, Hata hivyo wazo la kuwa na kanisa kubwa mara nyingi limeachwa kuzungumziwa, kimsingi maswala yote ni muhimu kama kupanda makanisa, kufanya uinjilisti, kutuma wamishionari, na uamsho mkubwa kutokea haya yote yanaweza kufanyika kwa wepesi sana kama washirika wa makanisa na Watumishi wa Mungu wataingiziwa wazo la kuwa na kanisa kubwa (Mega Church) Roho wa Bwana tangu mwanzo katika mpango wake anaonyesha kuwa anapendezwa na uwepo wa kanisa kubwa (Mega Church)

Kanisa kubwa kwa kawaida ni kanisa lenye washirika wengi sana ambao hawapungui washirika 2,000 wanaohudhuria ibada ya mahali pamoja na kushiriki katika maswala mbalimbali ya kielimu na kijamii kila wiki, Mungu anapokuwa amekuamini anakupa kuchunga zaidi ya watu 2000 na kuendelea mpaka kufikia maelfu kwa maelfu, Yesu Kristo wakati mwingine alikuwa na ibada zenye makusanyiko yenye watu wengi sana na wakati Fulani maelfu kwa maelfu mpaka wakakanyagana

Luka 12:1a “Wakati huo, makutano walipokutanika elfu elfu, hata wakakanyagana,” unaona elfu elfu maana yake ni Elfu mara Elfu ni idadikubwa sana ya watu waliokusanyika wakihitaji huduma ya kiroho kutoka kwa Yesu Kristo, Mungu anataka kila mchungaji akue kiroho na abadilishe mtazamo na kuanza kufikiri mikakati ya kuwa na Kanisa kubwa, lenye watu wengi sana kuanzia na kundi hilo dogo ambalo Mungu amekupa, mpaka kufikia kuwa wengi sana

Ayubu 8:5 -7 “Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii, Na kumsihi huyo Mwenyezi; Ukiwa wewe u safi na mwelekevu; Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako, Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa. Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, Lakini mwisho wako ungeongezeka sana.”

Unaona kimsingi Mungu anataka kumfanikisha kila mchungaji na kila kanisa kuwa na maelfu ya watu, ni mapenzi ya Mungu kila kanisa liwe na washirika wengi sana, idadi ya watu wanaookolewa na idadi ya watu wanaopotea ikilinganishwa utaweza kuona kuwa wanaopotea ni wengi sana kuliko wanaookolewa

Mathayo 7:13-14 “Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.”

Yesu aliposema maneno haya hakuwa na maana kuwa wakristo wawe wachache, au wanaookolewa wawe wachache, wala hakutukataza kanisa kuridhika na watu wachache, kusudi lake ni kuonyesha tu kuwa njia ya uzima haipendwi sana na sio rahisi kwa watu kuichagua kutokana na ugumu wake, lakini linapokuja swala la kuokoa Roho Mtakatifu ameonyesha kuwa ana uwezo wa kuokoa maelfu ya watu na kumfanya kila mchungaji kuwa na kanisa kubwa sana, kuna faida kubwa san asana za kuwa na kanisa kubwa nitazizungumza baadaye lakini nataka uelewe kwanza uelewe  kuwa ni mapenzi ya Mungu kuwa na kanisa kubwa na ni jambo ambalo linawezekana na ni jambo la Baraka sana!  Mungu anataka tuwe na makanisa makubwa sana yajae watu mpaka wamwagike, ndio maana Mungu hajakupa mji Fulani pekee wala nchi Fulani Mungu alitupa ulimwengu mzima  endendeni ulimwenguni kote Mungu anataka utukufu wake na habari za mwanae Yesu Kristo zienezwe kila mahali mijini na vijijini kila mahali hata mwisho wa nchi, hii maana yake nini kila unayemuona ni wako, kila unayemuona anastahili kuwa mshirika wako, kila unayemuona fanya mkakati awe wako,  Roho Mtakatifu ni Bwana wa Mavuno na Hashindwi kuokoa maelefu kwa maelfu

Matendo 2:40-47 “Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali. Kila mtu akaingiwa na hofu; ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mitume. Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika, wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja. Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe, wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.”

Kwa hiyo utaweza kuona kuwa ni mapenzi ya Mungu kuwa na kundi kubwa la washirika katika kanisa moja, Shetani amefanikiwa sana kuwapa moyo wa kuridhika wachungaji wetu wengi, wengi wetu tukishafanikiwa kumiliki Prado, kama Fulani, na kulipwa vizuri, na kujenga nyumba nzuri na kuwa na uwezo wa kubadilisha mboga, basi watu wanaanza kuridhika, na kufikiri kuwa wamekwisha kuvuka na wamefika, Ni jambo zuri watmishi wa Mungu kuwa na unafuu wa maisha lakini tusikubali kabisa kuisikiliza sauti ya shetani ikitunong’oneza “You have made it” ushatoboa na kuwa kila kitu kwako kiko vizuri, shetani akifanikiwa kukunongoneza na hayo tayari amekwisha kupiga upofu usitazame mbele, Yeye anataka ubaki na kijikanisa kidogo na usahau kabisa kuwa kuna maelfu kwa maelfu ya watu wanaenda jehanamu kila iitwapo leo, Idadi ya washirika wako ni kipimo kidogo sana cha watu unaowapunguza wasiende motoni, Mungu anataka uwe na macho mapana na yanayoona mbali, Maandiko hayaonyeshi kuwa ni lazima uwe na idadi Fulani ya watu, lakini pia hayakatai wewe kuwa na idadi kubwa sana ya watu, na Mungu akikuamini unaweza kuwa na kanisa kubwa hapa nikimaanisha kanisa lenye idadi kubwa sana ya watu wanaookolewa!

Historia ya kanisa inathibitisha tu kwa mfano kanisa lililokuwako Antiokia lililochungwa na Barnaba na Paulo na wenzao lilikuwa na washirika wapatao laki tano wanaoabudu mahali pamoja,  Na kule Korea ya kusini Kanisa alilokuwa akichunga David Yong Choi  linauwezo wa kuketisha watu wapatao laki saba 700,000 katika ibada moja, mchungaji huyu aliaminiwa na Mungu kiasi cha kuwa na washirika zaidi ya milioni mbili, kwa hiyo wazo la kuwa na kanisa kubwa linawezekana na sasa tunapozungumzia uamsho na mikazo ya kupanda makanisa tusisahau kupanua mawazo ya watumishi wa Mungu kuwa na maeneo makubwa, majengo makubwa, na maono makubwa ya kuhakikisha kuwa tunawafikia watu wengi sana na kuwaleta kwa Yesu, jambo ambalo litaleta uamsho mkubwa zaidi. Uamsho ni ajenda yetu! Tutajifunza somo hili Kanisa kubwa kwa kuzingatia maswala ya msingi yafuatayo:-

 

·         Misingi ya kuwa na Kanisa kubwa

·         Faida za kuwa na kanisa kubwa

·         Jinsi ya kuwa na kanisa kubwa

 

Misingi ya kuwa na kanisa kubwa

Tumeona kuwa kuwa na kanisa kubwa ni mapenzi ya Mungu, lakini hata hivyo ni muhimu kufahamu kuwa ili Mungu aweze kulikuza kanisa kwanza inapaswa kuwa ndoto ya kila mchungaji kiongozi wa kanisa la mahali pamoja, Kila mchungaji aanze kufikiri na kuwaza kuwa na MEGA CHURCH kuwa na Kanisa kubwa, Kwa sababu Mungu ametupa shamba kubwa la mavuno kama Shamba letu la mavuno lingekuwa dogo tungevuna kidogo lakini Shamba ambalo tumepewa ni ulimwengu mzima

Mathayo 28:18-20 “Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.”

Shamba alilotupa Mungu sio pale kilosa, tu wala sio Liwale tu, wala sio kiomboi, wala tambukareli, wala misozwe, wala kule mndemo, sio nyegezi, wala Isanga, wala kilindoni, wala mafia pekee Mungu ametupa ulimwengu mzima, Mungu ametupa mataifa yote, kumbuka basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, kwa hiyo ni agizo la kibiblia kufanya wanafunzi wengi maandiko sio tu yametupa uwanja mpana, lakini vile vile tyunaelezwa kuwa mavuno ni mengi sana

Mathayo 9:36-38 “Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji. Ndipo alipowaambia wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake.”

Unaona? mavuno ni mengi tunaaambiwa na Mwalimu, na tena Bwana wa Mavuno Roho Mtakatifu yupo, na nadhani uliona kasi yake ya mavuno kuanzia siku ya Pentekoste, kwa hiyo hatuna udhuru, tunahitaji kwanza kuwa na ndoto, tunahitaji tu kuwa na maono, tunahitaji tu kufanya maandalizi yanayolingana ili Mungu aweze kutuamini na kutupa watu wengi sana, washirika wakiwa wengi sana maelfu kwa maelfu kuna mambo mengi sana yatarahisishwa na kunakuwa na faida kubwa sana ambazo nitazielezea baadaye, lakini wote lazima tukubaliene kuwa tumepokea kiasi, na bado tunataka Mungu apanue mipaka yetu ili aweze kutujaza, lazima upanue hozi, yako ili Mungu akuongeze

Zaburi 81:10 “Mimi ndimi Bwana, Mungu wako, Niliyekupandisha toka nchi ya Misri; Fumbua sana kinywa chako nami nitakijaza.”

Zaburi 2:7-8. “Nitaihubiri amri; Bwana aliniambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa. Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, Na miisho ya dunia kuwa milki yako.”

1Nyakati 4:9-10 “Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni. Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.”

Unaona! Mungu yuko tayari kutubariki, lakini sisi nasi tunasehemu yetu ya kufanya, ukifumbua sana kinywa Mungu atakijaza, ukimuomba Bwana atakupa mpaka miisho ya dunia kuwa milki yako, na ukiomba akuzidishie hozi (territory, a boundary, a land mark, a state  kwa kiibrania Gebul Gebul) Mungu atazidisha, sasa maono haya hayawezi kuanzia chini yanapaswa kuwa malengo ya kichwa cha kanisa n ahata ukiwa nayo moyoni tu, athari zake zitaanza kuonekana kwa jamii ya kanisa la mahali pamoja, sasa basi licha ya kuwa na ndoto hii yako mambo ya msingi ya kuyafanyia kazi ili tuweze kuona matokeo yanayokusudiwa yakifumuka !

a.       Maombi – Ni muhimu kufahamu kuwa hakuna mahali kokote ambako jambo lolote linalohusiana na uamsho lilitokea bila maombi, wote tunajua kuwa Israel waliokolewa kutoka utumwani baada ya kuuugua sana, walipolia na kuugua kwaajili ya utumwa ule mzito Ndipo Mungu akashuka ili awaokoe, uamsho nyakati za kanisa la kwanza yalikuwa ni matokeo ya watu kuomba kwa siku kumi walipokuwa wakiomba siku ya Pentekoste Roho Mtakatifu alishuka na siku hiyo hiyo watu wapatao 3000 waliokoka na kanisa lilikuwa na kuongezeka kwa kasi 

 

Matendo 1:12-14 “Kisha wakarudi kwenda Yerusalemu kutoka mlima ulioitwa wa Mizeituni, ulio karibu na Yerusalemu, wapata mwendo wa sabato. Hata walipoingia, wakapanda orofani, walipokuwa wakikaa; Petro, na Yohana, na Yakobo, na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartholomayo na Mathayo, Yakobo wa Alfayo, na Simoni Zelote, na Yuda wa Yakobo. Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake.”

 

Unaona tunasoma kwamba baada ya Yesu kupaa, jamaa walirudi katika chumba kilichokuwepo Oriofani na kwa moyo mmoja walianza kuomba, maombi haya yakiwemo ya mama yake Yesu na wanafunzi wengine na wengine waliokuwepo ndiyo yaliyokuwa sababu ya kuandaa utayari wa Roho Mtakatifu kufanya kazi na wao, ni maombi ndiyo Daniel ndiyo yaliyoleta matokeo ya uamshi wa Israel kurudi kwao baada ya miaka 70, ni Maombi ya Mordekai na esta yaliyosababisha wayahudi waliohukumiwa kuuawa, kuwa na nguvu dhidi ya adui zao, ni maombi ya Nehemia ndiyo yaliyoleta uamsho wa ujenzi wa ukuta Yerusalem na maombi ya ezra yaliteta uamsho wa kiroho na kuwafanya watu kutubu na kuanza kumcha bwana, hakunamkinaweza kutokea bkla maombi ya dhati ya kuutaka uamsho, maombi ndio yanayosababisha kanisa kutuma wainjilisti, manabii na mitume katika kazi zinazokusudiwa

 

Matendo 13:1-3 “Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli. Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.”

 

Matendo 4:24-33 “Nao waliposikia, wakampazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, Mola, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo; nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha babaetu Daudi, mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na makabila wametafakari ubatili? Wafalme wa dunia wamejipanga, Na wakuu wamefanya shauri pamoja Juu ya Bwana na juu ya Kristo wake. Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta, ili wafanye yote ambayo mkono wako na mashauri yako yamekusudia tangu zamani yatokee. Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu. Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri. Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika. Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote.”

 

Maombi yana matokeo makubwa sana katika historia ya uamsho kokote pale utaweza kuona kuwa uamsho huo ulisababishwa na maombi, kwa hiyo baada ya kuwa na ndoto au maono ya kanisa kubwa mzigo mkubwa lazima uelekezwe katika kuomba maombi maombi maombi na Roho Mtakatifu atashuka na kuanza kutimiza kiu na kutoa nguvu ya kutimiza maono na mzigo ambao kimsingi ni wake kupitia sisi

 

b.      Ukuaji wa ndani – Ukuaji wa Kanisa kiidadi utakuwa na maana sana kama utaanza na ukuaji mkbwa wa ndani, Hapa nazungumzia ukuaji wa kiroho, Mungu hawezi kukupa washirika wengi  na ukawa na kanisa kubwa kama kwanza bado hujahakikisha wale wachache wanakomaa kiroho, achana na haya makusanyiko ya watu wanaohitaji mazingaombwe tu, wanaohitaji kuponywa tu, wanaomfuata Yesu kwa sababu walikula mikate wakashiba, wale washirima wachache tulionao lazima waandaliwe kuwa nguzo itakayokuwa na uwezo wa kubeba kanisa kubwa, kwa msingi huo ni lazima waandaliwe kuwa viongozi, Yesu alikuwa na wanafunzi wa aina nyingi, alikuwa na watatu muhimu, alikuwa na wote 12, thenashara, alikuwa na wale 70 na alikuwa na wale 120, kisha walikuwepo 500 na pia alikuwa na umati mkubwa sana  wa wanafunzi, Muhimu sana ni wale 12, hawa waliandaliwa kwa muda mrefu zaidi kuliko wale wengine hii ni kwa sababu wao walikuwa ni Msingi wa kanisa, ni nguzo,

 

Marko 3:13-19 “Akapanda mlimani, akawaita aliowataka mwenyewe; wakamwendea. Akaweka watu kumi na wawili, wapate kuwa pamoja naye, na kwamba awatume kuhubiri, tena wawe na amri ya kutoa pepo. Akawaweka wale Thenashara; na Simoni akampa jina la Petro; na Yakobo, mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye Yakobo, akawapa jina la Boanerge, maana yake, wana wa ngurumo; na Andrea, na Filipo, na Bartholomayo, na Mathayo, na Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Thadayo, na Simoni Mkananayo, na Yuda Iskariote, ndiye aliyemsaliti. Kisha akaingia nyumbani.”

 

Luka 10:1-12 “Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe. Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake. Enendeni, angalieni, nawatuma kama wana kondoo kati ya mbwa-mwitu. Msichukue mfuko, wala mkoba, wala viatu; wala msimwamkie mtu njiani. Na nyumba yo yote mtakayoingia, semeni kwanza, Amani iwemo nyumbani humu; na akiwamo mwana wa amani, amani yenu itamkalia; la, hayumo, amani yenu itarudi kwenu. Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii. Na mji wo wote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu; waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni, Ufalme wa Mungu umewakaribia. Na mji wo wote mtakaouingia, nao hawawakaribishi, tokeni humo, nanyi mkipita katika njia zake semeni, Hata mavumbi ya mji wenu yaliyogandamana na miguu yetu tunayakung'uta juu yenu. Lakini jueni hili, ya kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia. Nawaambia ya kwamba siku ile itakuwa rahisi zaidi Sodoma kuistahimili adhabu yake kuliko mji huo.”

 

Muda hauwezi kutosheleza kuinyesha aina zote za wanafunzi Yesu aliokuwa nao, lakini jambo kubwa la Msingi ni kuwa wanafunzi wake walitofautiana viwango vya maandalizi kwa makusudi mbalimbali, nafurahia sana kuwa makanisa mengi yana madarasa ya jumapili ambapo watu hujifunza maandiko, lakini changamoto kubwa au dosari kubwa ni kuwa hakuna madarasa ya biblia ya kuwatofautisha wanafunzi hao, katika shule nyingi za jumapili makanisani mtu aluyeokoka miaka 20 iliyopita anakuwa darasa moja tu na mtu aliyeokoma juzi, ndani ya kanisa kwa kawaida ukiacha watoto ambao huwa na madarasa yao , na laba vijana ambao huwa na madarasa yao, kunapaswa kuwepo na makundi kama manne kama sio matano ya watu tofauti kwa mafundisho tofauti, mfano darasa la kwanza wanaweza kuwa watu wanaojifunza masomo ya Mwanzo ya wokovu, kisha ubatizo, na meza ya bwana na kadhalika, dara sa la pili wakawa ni watu wanaojifunza namna ya kuhubiri injili, kushuhudia, kulea wanaookolewa na kadhalika, darasa la tatu likawa ni jamii ya watu wanaojifunza kuhudumia wengine yaani watendakazi, hawa wanakuwa na uwezo wa kuchaguliwa kuma wazee, mashemasi, na kusimamia makanisa ya nyumbani na kufanya huduma hata za maziko na kadhalika, na kundi la nne likawa ni jamii ya watu ambao wanaweza kuhudumu pamoja na Mchungaji, wanaweza kutumwa kufungua makanisa, wanaweza kwenda kwenye shule za kupanda makanisa, n ahata kupelekwa chuo cha Biblia kwa maandalizi ya utumishi wa juu zaidi, kisaikolojia ukiweka watu wote darasa moja huwezi kupata ukuaji wa kiroho unaolingana na wengine watachoshwa kujifunza mambo yale yale kwa miaka mingi, waumbie kiu ya kutamani kuja darasa la juu kila wakati, tengeneza miundo itakayosaidia watu kukua kiroho, kitabia na upendo, watu wakiandaliwa katika mtindo huo tutapata watu wenye sifa kuwa ni nguzo, ambao watabeba mzigo mkubwa wa usimamizi wa kanisa, na mchungaji utatoka kwenye ngazi ya kuchunga kundi dogo kwa fimbo na makubazi na utakwenda kwenye kiwango cha kuchunga ukiwa juu ya farasi na mabuti na kofia cowboy unayechunga ranch, Mungu akufunulie, yako makanisa unakuta mchungaji ameita watu mbele anaombea watu wanaanguka na hakuna wahudumu, mapepo yanafumuka watu mapaja yanaonekana hakuna hata watu wa kuwafunika, mapepo yanapiga ngumi, hakuna mtu wa kuwabana, katika hali kama Hiyo Mungu katika hekima yake atakuacha usubiri sana, huna watu, huna viongozi, huna wahudumu, bado Imani yako iko kwenye kuwekea mikono tu, ukipewa watu elfu utawekea mikono wangapi, kuna kiwango Mungu anataka ukifikie ukue na kanisa likue kazi ya huduma itendeke, ukuaji wa watu ni muhimu sana, ukuaji wa kiroho wa Mchungaji na wazee wa kanisa unatupa nafasi kubwa ya kukua kwa kanisa

 

Waefeso 4:11-15 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo.”

 

Wagalatia 2:6-9 “Lakini wale wenye sifa ya kuwa wana cheo; (walivyokuwa vyo vyote ni mamoja kwangu; Mungu hapokei uso wa mwanadamu); nasema, hao wenye sifa hawakuniongezea kitu; bali, kinyume cha hayo, walipoona ya kuwa nimekabidhiwa injili ya wasiotahiriwa, kama vile Petro ya waliotahiriwa; (maana yeye aliyemwezesha Petro kuwa mtume wa waliotahiriwa ndiye aliyeniwezesha mimi kwenda kwa Mataifa); tena walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa; Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;”

 

c.       Ukuaji wa Hekima – Luka 2:52 “Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.” Hakuna jambo la msingi na la Muhimu kama kukua katika Hekima! wote tunafahamu umuhimu wa Hekima, nimewahi kusikia watu wakimsifia mchungaji mmoja kwamba ana misimamo mizuri, anafundisha vizuri lakini hana Hekima washirika walikuwa wakimteta Mtumishi huyo Mzuri wa Mungu, na nilipokuwa nikitafakari na kujiuliza nilikuja kusikia kuwa alikuwa alikuwa mkali na wakati mwingine alikuwa akiwashushua washirika mbele ya watu na kuwafanya wajisikie kuaibishwa, anafokea mafundi mitambo sauti inapokuwa haijakaa vizuri, anafokea mashemasi wake ambao hajawafundisha vena kujua wajibu wao, ni wat utu wameambiwa wewe ni shemasi kuanzia leo, lakini hawana mafunzo, tayari watu mia tatu tu wanamtoa jasho, mzigo umemuelemea yeye, hajawafunza watu wabebe mzigo pamoja naye anabeba peke yake anaelemewa na akiwa katika mifungo hasira na stresses zinamuelemea zaidi, na katika kanisa lake ana majukumu mengine ya uangalizi wa makanisa mengine tayari hajaandaliwa kuwa nguzo lakini amebebeshwa mzigo mkubwa kuliko uwezo wake na hekima inakosekana,  tunapojiandaa kuongoza umati mkubwa sana wa watu basi Hekima ni ya muhimu sana Mfalme sulemani alipotawazwa kuwa mfalme na kugundua kuwa anaongoza watu wengi sana alihitaji hekima kukua katika hekima ni jambo la Muhimu sana! Ona

 

2Nyakati 1:7-12 “Usiku ule Mungu akamtokea Sulemani, akamwambia, Omba utakalo nikupe. Sulemani akamwambia Mungu, Umemfanyia baba yangu Daudi fadhili kuu, nawe umenimilikisha mimi badala yake. Basi sasa, Ee Bwana Mungu, na limyakinie baba yangu Daudi neno lako; maana umenitawaza niwe mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya nchi. Basi sasa nipe hekima na maarifa, nijue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa; kwa kuwa ni nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi? Naye Mungu akamwambia Sulemani, Kwa sababu neno hili lilikuwamo moyoni mwako, wala hukujitakia mali, wala utajiri, wala utukufu, wala maisha za wakuchukiao, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; bali umejitakia hekima na maarifa, upate kuwahukumu watu wangu, niliokutawaza juu yao; basi hekima na maarifa umepewa; nami nitakupa mali, na utajiri, na utukufu, kupita walivyokuwa navyo wafalme wote waliokuwa kabla yako, wala baada yako hapatakuwa na mtu atakayekuwa navyo.”   

 

Kusimamia watu walio wengi kunahitaji hekima, na maarifa, lazima uwe na neema kubwa ya kukusaidia katika mazingira hayo, Kusimamia kanisa kubwa kama alivyo @Bishop Barnabas Mtokambali, au @Bishop Zachary Kakobe, na wengineo rafiki zangu ambao sijawataja hapo kunahitaji uwe na ukomavu mkubwa sana wa kiroho, lakini zaidi sana hekima, watu haw ahata kama unaabudu katika kanisa lake hata kama hakujua lakini upendo wake unakuguza moja kwa moja wanaongoza taasisi kubwa sana lakini wanauwezo wa kumfikia kwa upendo mtu mmoja mmoja na kumgusa binafsi bila hata ya kujali wana heshima kiasi gani, ili uongoze kanisa kubwa lazima tuombe hekima

 

Yakobo 1:5-6 “Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.”

 

Hekima itakusaidia katika mifumo yote ya

 

i.                     Kuweka maono na mipango mkakati ya kanisa na ku9nyesha muongozo huku ukiwasaidia washirika kuelewa wanakokwenda

ii.                   Kuwashirikisha washirika katika maswala mazima ya huduma na kukusaidia kuongoza makundi madogo madogo kwa hiyari na kubeba mzigo wa kanisa pamoja nawe

iii.                  Kuhakikisha kuwa wanaifikia jamii, kwa kunda matukio mbalimbali, kukutana na mahitaji yao, na kujihusisha na maswala ya kijamii

iv.                 Kufanya mawasiliano yenye tija na washirika na watu wanaoizunguka taasisi, matumizi mazuri ya emails,mitandao ya kijamii

v.                   Mpangilio mzuri na wenye kuvutia wa ibada, wenye maana na unaotosheleza mahitaji ya kundi kwa watu wanaohudhuria kila siku n ahata wageni, kuna kanisa moja alikwenda mgeni mmoja akakuta mchungaji anafoka sana kiasi ambacho mgeni alijihisi anafokewa yeye na hakurudi tena, mawasiliano mabaya

vi.                 Jinsi na namna ya kuendeleza viongozi, mipangilio ya kundi la maombi, kundi la kuabudu, kundi la kwaya, maombi na ibada zinazotoa ukuaji wa kiroho wa binafsi na kuwaletea ahueni ya maisha wanaohudhuria, watu wanakuja na mizigo yao kanisani na hivyo wanahitaji kutuliwa wanapokuja kanisani

vii.               Kusimamia kweli za misingi ya kiroho za kanisa lako, lakini vilevile kwenda na mabadiliko yaliyioko duniani, mfano nyakati za leo madhabahu nyingi zinapambwa kwa mvuto wa kipekee wa mifumo ya jipsum na taa za kuvutia, na kadhalika, wewe miaka yote uko namipazia ya mirangi rangi kama mganaga wa kienyeji, be flexible badilika kutokana na ukisasa ulioko, weka Priojectors au monitor za television zinazoonyesha nyimbo, matangazo, na mahubiri ili wanaoandika waweze kufuatilia kwa kwa ukaribu bila kupitwa na kitu, Mafundi mitambo wako wakipata semina nzuri kutoka kwa watu wenye ujuzi sahihi wa vyombo vya music, wapigaji na kadhalika tutakuwa na ibada zenye utulivu na kila kitu kitaenda vema na hekima yako itadhihirika katika utaratibu mzima unaouweka.                              

 

Faida za kuwa na kanisa kubwa

1.       Huduma mbalimbali – mojawapo ya faida ya kanisa kubwa ni pamoja na kuwa na huduma mbalimbali, unakuwa na washirika wenye vipawa vyote, na karama nyingi sana, ujuzi mwingi, elimu kubwa, wataalamu mbalimbali ambao kimsingi wanaweza kutumia vipawa vyao katika kulisaidia kanisa, Kanisa la Full Gospel nilikokuwako zamani kwa Askofu kakobe kwa mfano Engineer Mbwambo, aliyekuwa moja ya viongozi wa kanisa hilo aliweza kutumia ujuzi wake huo katika kusimamia ujenzi wa Kanisa, Fundi Mvungi kule Tanga Full Gospel, aliweza kusimamia ujenzi wa kanisa la Nguvumali pale tanga, Profesa Kimeme katika kanisa la TAG anasaidia sana katika ustawi wa shule za kanisa, idadi kubwa ya watu wanaokuwako kanisani inasaidia kuwa na idadi kubwa ya watu wanaolifanya kanisa kuwa imara kama wakishirikishwa, chukulia tu una walimu waliookoka wa sekondari na msingi wako kanisani wameokoka umewafundisha Imani vizuri je huwezi kufurahia kipawa hicho hicho kiktumiwa katika madarasa ya biblia jumapili?, kanisa kubwa lenye idadi kubwa ya watu linaruhusu kuwa na watu wengi na huduma nyingi na zikipangiliwa vizuri, huwezi kukosa watu wa kuratibu mambio mbalimbali na kuifanya huduma kuwa na mvuto, uimbaji, utakuwa na waimbaji wa kutosha, wapiga vyombo, mafundi mitambo, waandaaji wa matangazo, wanasheria wa kanisa, na wataalamu wa kila aina.

 

2.       Nguvu kubwa ya maombi -  kanisa lenye watu wengi linakuwa na nguvu kubwa sana ya maombi, mnaweza hata kuwa na mfumo wa maombi ya mnyororo ambapo kila saa linaweza kuwa na watu wanaooomba kwa uaminifu na kumnyima pumzi shetani, hata hivyo katika hali ya kawaida tu watu wanapokuwa wengi na mkafanya maombi ya pamoja kunakuwa na nguvu kubwa sana ya uwepo wa Mungu kwa kanuni za kibiblia

 

Mathayo 18:19-20 “Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.”

 

Maandiko yanasema wawili au watatu wakipatana katika jambo lolote watakaloliomba watafanyiwa sasa unapokuwa umati mkubwa sana wa watu maana yake nguvu ya maombi ya umoja inakuwa kubwa kuliko maelezo. Mkuu wa anaga katiika eneo hilo anapigwa na kusambaratishwa na kuleta mpenyo kwa haraka, kwa hiyo kadiri kanisa linavyokuwa kiroho na kiidadi linajiweka katika nafasi kubwa ya ushindi kutokana na muungano wetu na umoja wetu

 

Kumbukumbu 30:29-30 “Laiti wangekuwa na akili, hata wakafahamu haya, Ili watafakari mwisho wao. Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi, Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama Bwana asingaliwatoa?

 

Andiko laonyesha nguvu ya mtu mmoja ni 1000 na nguvu ya watu wawili ni 10,000 je wakiwa 1000? Tunapokuwa wengi tunakuwa na nguvu kuibwa sana ya kiroho kuliko kawaida na ndio maana shetani katika hekima yake hatataka kanisa lolote la mahali pamoja liwe kubwa n ahata mawazo ya kuwa na kanisa kubwa kwa wachungaji haiwezi kupangwa kwa urahisi.

 

3.       Umati huvutia umati – Kwa kawaida unapokuwa na umati mkubwa sana wa watu, umati huo unatabia ya kuvuta umati, mfano unapokuwa na kanisa lenye watu mia tano nadhani huwezi kukosa wageni 25 kwa kiwango cha chini sana kwa mwezi, lakini sio hivyo tu matarajio ya watu huwa ni makubwa na Imani hupanda sana, Imani ya kila mmoja inakuwa kwa kasi sana na kupaa juu, kuliko Imani ya mtu mmoja, kuna kanuni hii ya kuwa Mungu pia hujitukuza kwenye umati mkubwa sana wa watu, thamani ya muhubiri inapanda kila mtu mwenye shida yake anataka kukufikia na kuutumia muda mfupi sana ulionao  kukutana na mahitaji yao

 

Luka 5:18-24 “Na tazama, wakaja watu wanamchukua kitandani mtu mwenye kupooza; wakataka kumpeleka ndani na kumweka mbele yake. Hata walipokosa nafasi ya kumpeleka ndani kwa ajili ya lile kundi la watu, walipanda juu ya dari wakampisha katika matofali ya juu, wakamshusha yeye na kitanda chake katikati mbele ya Yesu. Naye alipoiona imani yao, alimwambia, Ee rafiki, umesamehewa dhambi zako. Basi, wale waandishi na Mafarisayo wakaanza kuhojiana wakisema, Ni nani huyu asemaye maneno ya kukufuru? N'nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?Na Yesu alijua hoja zao, akajibu akawaambia, Mnahojiana nini mioyoni mwenu? Lililo jepesi ni lipi? Kusema, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, uende? Lakini, mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (alimwambia yule mwenye kupooza). Nakuambia, Ondoka, ujitwike kitanda chako, ukaende zako nyumbani kwako.”

 

Yesu alikuwa amezingirwa na umati mkubwa sana kiasi ambacho ilikuwa ni ngumu kufikia mijamaa ikaamua kutoboa dari kumshusha mgonjwa wao pale alipo Yesu Imani yao ikiwa kubwa sana, mahali popote ambapo watu wanakusanyika kwa wingi hii inamaanisha pana kitu, watu wanasaidika hapo na hivyo watu hujaa, sana Peto ulifikia wakati hata muda wa kugusa watu hana watu wakabuni kulaza wagonjwa ili kivuli chake tu kikipita kiwaguse unaona hii maana yake nini Thamani ya Muhubiri inapanda, Imani ya muhubiri inakuwa na huduma yako inakuwa Mungu hataruhusu tena uwekee watu mikono utachoka sasa Mungu ataruhusu hata kivuli chako kisaidie watu

 

Matendo 5:12-16 “Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu; nao wote walikuwako kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani; na katika wote wengine hapana hata mmoja aliyethubutu kuambatana nao; ila watu waliwaadhimisha; walioamini wakazidi kuongezeka kwa Bwana, wengi, wanaume na wanawake; hata ikawa katika njia kuu hutoa nje wagonjwa, na kuwaweka juu ya majamvi na magodoro, ili Petro akija, ngawa kivuli chake kimwangukie mmojawapo wao. Nayo makutano ya watu wa miji iliyoko kandokando ya Yerusalemu wakakutanika, wakileta wagonjwa, nao walioudhiwa na pepo wachafu; nao wote wakaponywa.”

 

Kumbuka ni Petro huyu huyu ambeye sura ya tatu alimsika mtu aliyepooza mikono na kumuombea asimame kwa jina la Yesu, sasa wahitaji wamekuwa wengi hawezi kugusa watu wote sasa watu wanahitaji japo kivuli chake tu, umati unasababisha Imani za watu zikue na huduma yako inakuwa unatoka katika hali ya kuchunga vikondoo vichache unakwenda kuchunga ranchi, toka kwenye makubazi na fimbo, chunga juu ya farasi ukiwa na viatu mchingoko na kofia ya kuziia jua Rancher, hiki ndio kiwangi Mungu anataka ukifikie sijui mnanielewa?  Neno lile ILA WATU WALIWAADHIMISHA katika kiyunani linatumika neno MEGALUNO ambalo kwa kiingereza ni MAGNIFY  Yaani waliwakuza, waliwaona sio watu wa kawaida waliwahehimu sana, unapoadhimia kuwa na kanisa Kubwa Mungu atafanya mambo makubwa na wewe atakukuza pia, hali ya heaa ya kiroho kwenye kanisa dogo na hali ya hewa kwenye kanisa kubwa ni vitu viwili tofauti kama utakuwa umewahi kuhubiri,

 

4.       Kanisa kubwa kazi kubwa – unapokuwa katika kanisa kubwa Utendaji wa Mungu kimiujiza unakuwa mkubwa na matarajio ya watu kupokea yanakuwa na kazi inayofanyika inakuwa kubwa, hii haimaanishi Mungu hafanyi kwenye kanisa dogo anafanya lakini kuna tofauti kubwa sana, linapokuja swala la watu wengi sana Imani inakuwa kubwa sana , matarajio ni makubwa sana, nguvu ya Mungu inakuwa kubwa sana miujiza inakuwa mikubwa sana  shuhuda zinakuwa nyingi sana, Mungu anatukuzwa kikubwa sana, Baraka za Mungu zinakuwa nyingi sana, Michango inakuwa mingi sana, uchumi unatrahisishwa sana, mtafanya uinjilisti kirahisi sana, mnaweza kushuhudia nyumba kwa nyumba kwa nyumba nyingi sana, mnaweza kupeleka chuo cha biblia wachungaji wengi sana,mnaweza kupanda makanisa mengi sana, mnaweza kuhudumia watu wengi sana, kanuni ya wingi inatumiwa sana na hawa jamaa wanaokusanya watu wengi, ukifanikiwa kukusanyha watu wengi sana mahali pamoja Mungu hujitukuzwa kwa kiwango kikubwa sana, hawa watu wenye makusanyiko makubwa hakuna chochote walichokuzidi isipikuwa watu wengi, nah ii ni kwa sababu walikuwa na maono hayo, na hawakuridhika, wana matangazo kwenye redio wana vituo vya televisheni, na kupitia umati walionao wanavutia umati mkubwa sana angalia @Bishop Dickson Kaganga pale Zanzibar he is coming, angalia hekima yake, ndugu tunapozungumzia uamsho natuwezi kuacha kuzungumzia kuwa na makanisa makubwa Maga church Hebu na tumuamini Mungu sasa kwaajili ya kanisa kubwa, usiridhike tu kwa sababu jnabadili mboga, una prado, una kigorofa wenzako wana mpaka personal jet  Mungu akutoe hapo ulipo wewe na mimi na tuanze kufikiri mambo makubwa  “Attempt Great things for God”  alisema Missionary William Carey   na Mungu anapokufanikisheni kiuchumi endelea kuutumia uchumi huo kwa kuendeleza kazi ya Mungu cha kujilimbikizia mali, hatukuja na kitu duniani wala hatutaondoka na kitu, tunapowaza kanisa kubwa mwenye kanisa anakuona anakuchunguza unachowaza kanisa kubwa ni uchumi mkubwa uchumi huu sio wa Mchungaji ni uchumi wa kazi ya Mungu, tutajali mpaka yatima, tutasomesha yatima tutajali wajene, tutajali wenye ulemavu tutafanya mambo mengi na mfano mzuri ni Marehemu @TB Joshua hakuwa na choyo, Mungu akipombariki taifa zima lilibarikiwa  na ulimwengu mzima, Kanisa linaweza kutuma wamishionari kila mahali na tukawalipa mshahara

 

5.       Kanisa kubwa watendakazi wengi – Kanisa inapokuwa kubwa kunakuwa na wafanyakazi wengi sana wa serikalini na watu wenye ajira, lakini pia  wafanya biashara na watu mbali mbali kwa msingi huo kanisa linakuwa na kipato kikubwa zaidi, uchumi mkubwa katika kanisa unapelekea kufanikisha kazi nyingi za Mungu, hata hivyo watakuwepo wengine kama watazamaji, na wengine , lakini mwisho wa siku kundi kubwa la watenda kazi pia litapatikana watu ambao watayatoa maisha yao pamoja na kazi nyingine kumtumikia Mungu, hawa ni watu wa maana bila kupuuzia wale wengine umuhmu wao unakuja kuwa wanaweza kujihusisha na kazi ya Mungu moja kwa moj a na kusaidia ukuaji wa kanisa zaidi, na Mchungaji kiongozi atakuwa na nafasi kubwa ya kutuma watendakazi katika shamba la Mungu

 

Mattayo 9:37-38 “Ndipo alipowaambia wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache.Basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake.”

 

Wahudumu katika maeneo mbalimbali ya ukuaji wa kanisa watapatikana, jambo ambalo sio rahisi kuwapata kwenye kanisa dogo, kumbuka hapa ninapozungumzia kanisa kubwa na dogo nazungumzia ukubwa kiidadi na namaanisha wingi wa watu, Kanisa litaweza kuwa na nguvu hata ya kuwahudumia masikini na kusababisha Baraka kubwa sana

 

Zaburi 41:1-2 “Heri amkumbukaye mnyonge; Bwana atamwokoa siku ya taabu. Bwana atamlinda na kumhifadhi hai, Naye atafanikiwa katika nchi; Wala usimtie katika hali wamtakiayo adui zake. Bwana atamtegemeza alipo mgonjwa kitandani. Katika ugonjwa wake umemtandikia.”

 

Kanisa litakuwa na baraka kubwa kama wataweza kufanya huduma kwa watu wenye mahitaji muhmu na maalumu, na fedha hazitakuwa tatizo kutokana na wingi wa watu kile kidogo anachojitoa kila mtu kama mkiwa wengi kinakuwa kitu kikubwa ! wenye vipindi vua televisheni wataweza kufadhili uwepo wa hewani, na redioni na matangazo ya injili na kwenye magazeti, na huduma nyinginezo za maedeleo ya kanisa

 

6.       Kanisa kubwa mamlaka kubwa -  Kanisa kubwa linakuwa na nguvu kubwa sana katika jamii, na sio hivyo tu linakuwa na mamlaka kubwa sana na linakuwa taifa lenye nguvu, wanasiasa hupapatikia sana Kanisa kubwa, mchungaji mwenye kanisa kubwa huwa na mamlaka kubwa na thamani yako haitaruhusu kugombea uaskofu, zaiti ya kujitiisha katika ushirika wa kanisa lako na skofu wako huku ukifanya huduma zako, kila Mchungaji akikusudia kuwa na kanisa mkubwa anakuwa mkubwa katika jumuia ya kanisa lake la mahali pamoja, na hivyo ni ngumu sana kwa mtu aliye busy kuanza kuwania ngazi za kisiasa za kanisa namaanisha uongozi wa kikanisa hapa, Serikali huanza kuwa na hofu kwa kanisa lenye watu wengi, Mchungaji mwenye kanisa kubwa huwa kama serikali, washirika wenye taaluma mbalimbali hata za usalama wa taifa, ni nadra kumficha Mchungaji wao kitu, unaweza kualikwa kwenye matukio makubwa sana na hata kukaribishwa ikulu, Mchungaji mwenye kanisa kubwa la mahali pamoja anakubwa mtu mkubwa sana, wanasiasa wanajua kuwa kanisa kubwa maana yake ni umati mkubwa wa watu, maana yake kura nyingi za watu, lakini kikanisa kidogo, kinadharaulika, wanasiasa wanajua kuwa neno lako na maelekezo yako yanaweza kuwapa kura au kuwanyima kura na watakuwa wakikujia kusalimu au kwa maombi na kadhalika, wanasiasa huogopa sana na hawawezi kwa namna yoyote kupuuzia ushawishi wa Mtu anayeaminiwa kama wewe,

 

Luka 13:31-33 “Saa ile ile Mafarisayo kadha wa kadha walimwendea, wakamwambia, Toka hapa, uende mahali pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua. Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika. Pamoja na hayo imenipasa kushika njia yangu leo na kesho na kesho kutwa; kwa kuwa haimkini nabii aangamie nje ya Yerusalemu.”  

 

Marko 6:17-20 “Kwa maana Herode mwenyewe alikuwa ametuma watu, akamkamata Yohana, akamfunga gerezani, kwa ajili ya Herodia, mkewe Filipo ndugu yake, kwa kuwa amemwoa; kwa sababu Yohana alimwambia Herode, Si halali kwako kuwa na mke wa nduguyo. Naye yule Herodia akawa akimvizia, akataka kumwua, asipate.Maana Herode alimwogopa Yohana; akimjua kuwa ni mtu wa haki, mtakatifu, akamlinda; na alipokwisha kumsikiliza alifadhaika sana; naye alikuwa akimsikiliza kwa furaha.”

 

Mtumishi wa Mungu mwenye watu wengi anaogopewa na mfalme na mfalme huwatendea haki na kuwachukualia kwa uzito mkubwa watu hawa wenye ushawishi mkubwa katika jamii, Yesu hakuwahi kumuogopa kabisa herode wala Pilato, hali kadhalika Yohana Mbatizaji na ushawishi wako unajulikana

 

7.       Kanisa kubwa jamii kubwa – Kanisa linapokuwa kubwa watu wanakuwa jamii kubwa, ni rahisi kupata mchumba na kuolewa, makanisa makubwa hufunga ndoa nyingi mpaka ndoa sitini kwa wakati mmoja, kunapatikana muunganiko wa kupata kazi, na uhusiano mkubwa na watu wa jamii mbalimbali, mambo mengi duniani yanafanikishwa na kujuana amini usiamini, watu wanapenda kukaa mahali ambapo wanahisi usalama Amani na baraka, na mnapokuwa katika kanisa moja na imani moja ni rahisi kuinuana na kufikia malengo ya kimaisha kwa namna nyepesi sana tunaweza tisiwe kama kanisa la Kwanza kwa kuuza kila tulicho nacho na kushiriki pamoja, lakini tunaweza kushirikiana katika maswala ya msingi, ikiwa ni pamoja na ushirika kikazi, kibiashara, makampuni na kadhalika na kama wakristo hawa wakipata maelekezo mazuri na malezi mazuri hakuna mtu atajuitia kuajiri wapendwa katika kampuni yake

               

Jinsi ya kuwa na kanisa kubwa

1.       Watu wawe watendaji -  Mchungaji yeyote anayetaka kuwa na kanisa kubwa hatakubali kuwaacha washirika wawe ni watu wanaoketi na kusikiliza neno kila siku na badala yake atasababisha kazi ya huduma itendeke, yaani kila mtu ndani ya kanisa awe na jambo la kufanya katika huduma, au afanye kivitendo, ukuaji wa kiroho wa wakristo hauko katika kuwapatia tu maarifa lakini maarifa ya namna ya kutumika, hivyo kila mtu ahusike katika utumishi, kila mtu amtumikie Mungu kivitendo, Yesu hakuwa tu Mwalimu lakini alikuwa mtendaji, Maandiko yanahamashisha utendaji zaidi ona

 

Matendo 1:1 “Kitabu kile cha kwanza nalikiandika, Theofilo, katika habari ya mambo yote aliyoanza Yesu kufanya na kufundisha,”

 

Waefeso 4:11-12 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;”

 

Yakobo 1:22-25 “Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo. Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.”

 

Neno la Mungu linasisitiza sana katika kutenda, mwanafunzi halisi wa Yesu sio yule anayesikia tu ni yule anayetenda, kama watu watajifunza kuomba, kisha hawaombi, au kushuhudia kisha hawashuhudii, au kufanya umisheni kisha hawaendi, utoaji kisha hawatoi, ukarimu kisha hawafanyi, Imani bila matendo imekufa, Kanisa lenye malengo ya kuzaa matunda linapaswa kuwa kanisa la watu wanaolitendea kazi neno la Mungu, watu wanasikia sana lakini wanaotenda ni wachache, Mungu anapendezwa na watu wanaotenda. Tukiwa wasikiaji tu na sio watendaji swala la kuwa kanisa kubwa litasalia kuwa ndoto, mwanafunzi halisi wa Yesu ambaye ana hekima ni yule anayelitendea kazi neno la Mungu

 

Mathayo 7:24-27 “Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.”

 

Kanisa ambalo watu wake wanalitendea kazi neno la Mungu kivitendo, linaweza kutimiza mapenzi ya Mungu na kufanikiwa sana katika matokeo ya wazi yatakayolipeleka katika ngazi nyingine ikiwepo kuyatimiza mapenzi ya Mungu na kuwa Kanisa kubwa!

 

2.       Lisha kondoo wa Bwana – Wajibu mkubwa wa mtumishi wa Mungu aliyeaminiwa na Bwana ni kuwalisha kondoo wake Yohana 21:15-17 “Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia , Naam ,Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana-kondoo wangu. Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo zangu. Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo zangu.”

 

Hutatoa hesabu kwa programu nyingine zaidi ya Programu ya kulisha kundi na kulichunga kundi, Mchungaji anayelenga kuwa na kanisa kubwa atahakikisha anatoa muda wake mwingi kwa kanisa la mahali pamoja, hata kuliko kanisa la kitaifa, watu wengi sana wanatafuta umaarufu wakifikiri kuwa wanaweza kuwa maarufu kwa kuwa waangalizi, au maaskofu wa kanda au maaskofu wakuu, kuwa askofu ni wito mwingine mkubwa na mgumu zaidi, hakuna sababu ya kuwasumbua waangalizi wako, wala maaskofu wako, wala cheo chochote, wewe lenga tu kuwa na kanisa kubwa, ukiwa na kanisa kubwa watu wote watakujua  Pale Kenya Yuko mtu mmoja wa Mungu simfahamu sana lakini anajulikana sana kama @Evangelist Ezekiel mtu huyu hajiiti askofu, tena wala hajiiti mchungaji, anajiita Mwinjilisti Ezekiel, ni maarufu  sana huyu mtu, mimi simjui kwa undani sana lakini nimejikuta namjua sio kwa sababu ni askofu la hasha bali kwa sababu ana kanisa kubwa, @Joel Osteen kule Marekani tunamjua sio kwa sababu ni askofu bali kwa sababu ana kanisa kubwa, ukiwa na kanisa kubwa san ahata askofu wako atakujua unaona,  uwe mwaminifu kwa kanisa lako, tii taratibu za kitaifa na za kikatiba za kanisa lako lakini moyo wako uweke kwenye kukuza kanisa lako la mahali pamoja na Huduma yako kubwa itakuwa na kuwafikia watu wengi na hutahitaji kujiita jina kubwa bali, utakuwa maarufu tu kwa sababu Baba mwenyewe atakuheshimu, waheshimu sana wale unaowahudumia wajali, walishe wasaidie, wainue wakuze na utabarikiwa sana.

 

3.       Tufanye kazi kwa bidii – Maono ya kuwa na kanisa kubwa hayawezi kutokea kwa mtu mvivu, lazima kazi kubwa ifanyike , viongozi na watumishi wa Mungu wote duniani wanaofanya kazi sana utaweza kugundua kuwa walikuwa na bidi sana Mchungaji Zachary Tenee aliyekuwa na kanisa kubwa sana kule Younde Cameroon alikuwa ni mchapa kazi, yeye na washirika wake walikuwa na bidi, siku aliyokufa Zachary Tenee mkewe alisema maneno haya kaburini, “Mungu wangu ulinipokonya mume wangu alipokuwa akali hai, wakati wote alifanya kazi zako na sasa kama haitoshi umeamua kunipokonya kabisa hata nisimuone” hii maana yake ni nini alikuwa anachapa kazi, maandiko hayaungi mkono uvivu,

 

Mithali 12:24 “Mkono wa mwenye bidii utatawala; Bali mvivu atalipishwa kodi.”

 

Yeremia 48:10. “Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya Bwana kwa ulegevu; na alaaniwe auzuiaye upanga wake usimwage damu.”          

 

Warumi 12:11- “kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;”

 

4.       Maombi - Kanisa halikui kwa sababu tu ya maono bali kwa mbinu za kibiblia, kuna mambo mengi ya kimikakati naweza kuyaweka hapa lakini yanaweza yasikusaidie, napenda sana njia za kibiblia ambazo zikitumiwa zinaweza kuleta matokeo, na moja ya njia ya ajabu sana ni Maombi, unapoomba Mungu mwenyewe atatoa njia ya kufanya atakupa na mbinu za kufanya ili kanisa liwe kubwa lakini maombi maombi maombi, Lazima umuamini Mungu kwaajili ya kanisa kubwa na maombi ni moja ya njia muhimu.  

 

Isaya 56:5-8. “Nitawapa hawa nyumbani mwangu, na ndani ya kuta zangu, kumbukumbu na jina, lililo jema kuliko kuwa na wana na binti; nitawapa jina lidumulo milele, lisilokatiliwa mbali. Na wageni, walioandamana na Bwana ili wamhudumu, na kulipenda jina la Bwana, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu; Nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote. Bwana MUNGU, akusanyaye waliofukuzwa katika Israeli asema, Pamoja na hayo nitamkusanyia na wengine, zaidi ya hao walio wake waliokusanywa.”      

 

Ili Mungu akukusanyie watu mbalimbali na kuwaleta katika kuta za nyumba yake lazima nyumba hiyo iwe nyumba ya sala yaani uwekezaji mkubwa uwe ni maombi, maombi hurahisisha kazi na wakati watu wanaomba Mungu mwenyewe atasema ni namna gani mnaweza kuifanya kazi yake na atakupa mwelekeo

 

Matendo 13:1-3 “Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli. Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.”

 

Matendo 16:6-10 “Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia. Walipofika kukabili Misia wakajaribu kuenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa, wakapita Misia wakatelemkia Troa. Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie. Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema.”

 

Nyakati za kanisa la Kwanza wao waliomba na kumtii Mungu na wakaweka neno la Mungu na agizo la krist kivitendo, Roho wa Mungu aliwaongoza aliwajulisha wapi pa kwenda na pale ambapo hakutaka waende aliwakataza, maombi yataleta kila kitu mbinu na njia za kufanya kwa kadiri ya kutaka kwetu kuyatimiza mapenzi ya Mungu, Kwa hiyo mchungaji anayetaka kanisa kubwa asipuuzie kamwe swala la maombi.            

 

Na. Rev Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

0718990796



Hakuna maoni: