Marko 14:27-31 “Yesu akawaambia, Mtakunguwazwa ninyi nyote kwa ajili yangu usiku huu; kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji, na kondoo watatawanyika. Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya. Petro akamwambia, Hata wajapokunguwazwa wote, lakini siyo mimi. Yesu akamwambia, Amin, nakuambia wewe, Leo, usiku huu, kabla ya kuwika jogoo mara mbili, utanikana mara tatu. Naye akazidi sana kusema, Ijaponipasa kufa nawe, hata hivyo sitakukana kamwe. Na wote wakasema vile vile.”
Utangulizi:
Tunakaribia kabisa katika juma
muhimu la Pasaka, na jumbe mbalimbali zitakuwa zinahubiriwa katika majira haya
na msimu huu kuelekea katika wakati wa Pasaka, mimi nami nimetia mkono wangu
nipate kuzungumza lile ambalo Mungu anataka kusema na watu wake katika majira
haya ya Pasaka, Katika majira haya ya pasaka nataka tujikumbushe kwamba uko
umuhimu wa kujishusha, tunapokumbuka na kuadhimisha pasaka tunakumbuka tu sio
ukombozi wa Mwanadamu pekee bali na umuhimu wa kuchukua nafasi ya chini kwa
kujinyenyekeza na kuacha kabisa kujiona Bora kuliko wengine
Wafilipi 2:3-8 “Msitende neno lo lote kwa
kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu
mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe,
bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu
ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna
namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana
nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana
mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza
akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.”
Unaona tunajifunza kwamba Pasaka
ni unyenyekevu, Kitendo cha Yesu Kristo kuubeba Msalaba na kukibali mateso ili
hali alikuwa Mungu, katika msimu huu wa Pasaka kinatukumbusha kuwa wakati wote
tunapaswa kuufuata mfano wake, na kuacha kujitutumua au kujiweka katika nafasi
ambayo sisi wenywewe tunadhani kuwa ni wa muhimu kuliko wengine, kila mmoja
amuhesabu mwenzake kuwa ni bora kuliko nafsi yake! Tutajifunza somo hili Hata wajapokunguwazwa wote, lakini siyo
mimi! Kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo:-
·
Maana ya neno Kunguwazwa
·
Hata wajapokunguwazwa wote lakini sio mimi
·
Mambo muhimu ya kujifunza
Maana ya neno Kungunguwazwa
Marko 14:27-31 “Yesu akawaambia, MTAKUNGUWAZWA
ninyi nyote kwa ajili yangu usiku huu; kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga
mchungaji, na kondoo watatawanyika. Lakini baada ya kufufuka kwangu,
nitawatangulia kwenda Galilaya. Petro akamwambia, Hata wajapokunguwazwa wote,
lakini siyo mimi. Yesu akamwambia, Amin, nakuambia wewe, Leo, usiku huu, kabla
ya kuwika jogoo mara mbili, utanikana mara tatu. Naye akazidi sana kusema,
Ijaponipasa kufa nawe, hata hivyo sitakukana kamwe. Na wote wakasema vile vile.”
Ni muhimu kufahamu kuwa lugha ya
Kiswahili inayotumika mahali hapo kama Kunguwazwa ni lugha ya Kiswahili cha
kizamani, Neno Mtakungwaza katika Biblia ya kiingereza ya KJV mstari wa 27
unasomeka hivi And Jesus saith unto them
All Ye shall be OFFENDED because of me this night” kwa hiyo neno
kukunguwazwa katika kiingereza ni Offended ambalo kwa kiyunani ni SKANDALIZO Ambalo maana yake ni
kuingia mtegoni, au kukwazwa au kukoseshwa, au kuchukizwa kama linavyotumiwa na
waandishi wengine
Mathayo 26:31-35 “Ndipo Yesu akawaambia,
Ninyi nyote MTACHUKIZWA kwa ajili yangu usiku huu kwa kuwa imeandikwa,
Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi watatawanyika. Lakini baada ya kufufuka
kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya. Petro akajibu, akamwambia,
Wajapochukizwa wote kwa ajili yako, mimi sitachukizwa kamwe. Yesu akamwambia,
Amin, nakuambia wewe, usiku huu kabla ya kuwika jogoo, utanikana mara tatu.
Petro akamwambia, Ijaponipasa kufa nawe, sitakukana kamwe. Na wanafunzi wote
wakasema vivyo hivyo.”
Kukunguwazwa huku au kuchukizwa
kuna uhusiano wa kumkana au kumkimbia Yesu, usiku wa kukamatwa kwa Yesu,
ulikuwa ni usiku wa kujaribiwa kwa wanafunzi wake, na shetani alikuwa
ameruhusiwa ili awapepete kama ngano, kwaaajili ya kuonyesha kuwa bado walikuwa
hawako imara kumtetea au hata kuwa pamoja na Yesu wakati ule
Luka 22:31-34 “Akasema, Simoni, Simoni,
tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano; lakini
nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu
zako. Akamwambia, Bwana, niwapo pamoja nawe, mimi ni tayari kwenda gerezani au
hata kifoni. Akasema, Nakuambia, Petro, jogoo hatawika leo, kabla wewe
hujanikana mara tatu ya kuwa hunijui.”
Yesu Kristo alikuwa amejua kuwa
usiku ule atakaokamatwa, utakuwa ni usiku wa majaribu makubwa kwa wanafunzi
wake, aliwataka waombe kule bustanini ili wasiingie majaribuni, ulikuwa ni
usiku wa kutosha, Imani ya kila mwanafunzi na uaminifu wa kila mwanafunzi
ungepimwa wakati wa kukamatwa kwa Yesu, wote wangekimbia maana yake wangemkana
Yesu kivitendo na kutokukubali kufa naye, Japo walimuahidi, Lakini katika namna
ya kushangaza Petro ndiye ambaye aliharibu zaidi siku ile kuliko wanafunzi wote
nan die aliyeombewa na Bwana, na alielezwa wazi kuwa yeye angamkana Yesu mara
tatu, kwa sababu alijiamini mno kuliko wengine akidhani kuwa wengine ni
wadhaifu kuliko yeye
Hata wajapokunguwazwa wote
lakini sio mimi
Wakati Yesu akiahidi kuwa usiku
ule kila mmoja atakungwazwa kwaajili yake kama tusomavyo katika andiko la
Msingi Marko 14:27-31 “Yesu akawaambia, MTAKUNGUWAZWA ninyi nyote kwa ajili
yangu usiku huu; kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji, na kondoo
watatawanyika. Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya.
Petro akamwambia, Hata wajapokunguwazwa wote, lakini siyo mimi. Yesu
akamwambia, Amin, nakuambia wewe, Leo, usiku huu, kabla ya kuwika jogoo mara
mbili, utanikana mara tatu. Naye akazidi sana kusema, Ijaponipasa kufa nawe,
hata hivyo sitakukana kamwe. Na wote wakasema vile vile.”
Petro yeye alijiamini kupita
kawaida, na kutaka kumthibitishia Yesu kuwa yeye hatakunguwazwa, na
akamhakikishia Yesu kuwa yuko tayari kufa naye n ahata kwenda gerezani pamoja
naye Petro alimwambia Bwana Hata wajapokunguwazwa wote lakini sio mimi, Petro
alikuwa na uhakika kuwa hawezi kukomsea Yesu hata siku Moja, wengine wanaweza
kumkosea Yesu lakini sio mtu kama yeye, Petro alikuwa na ujasiri mkubwa sana,
wote tunajua jnsi Petro alivyikuwa mwanafunzi muhimu katika wanafunzi wa Yesu,
yeye anatajwa kuwa ni nguzo za kanisa
-
Wagalatia
2:9 “tena walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa;
Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba
mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu
wa tohara;”
Nyakati za
Kanisa la Kwanza Petro au Kefa alijulikana kuwa ni Nguzo, katika madarasa ya
uanafunzi ya Yesu Kristo, Petro Yakobo na Yohana, walikuwa dara sa la juu zaidi
kuliko wanafunzi wenguine wote, walishuhudia mambo makubwa sana, na walijua
siri ambazo wanafunzi wengine hawakujua
-
Mathayo
17:3-9 “Na baada ya siku sita Yesu akawatwaa Petro,
na Yakobo, na Yohana nduguye, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani; akageuka
sura yake mbele yao; uso wake ukang'aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama
nuru. Na tazama, wakatokewa na Musa na Eliya, wakizungumza naye. Petro akajibu
akamwambia Yesu, Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa; ukitaka, nitafanya hapa
vibanda vitatu, kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya.
Alipokuwa katika kusema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti
ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu,
ninayependezwa naye; msikieni yeye. Na wale wanafunzi waliposikia, walianguka
kifulifuli, wakaogopa sana. Yesu akaja, akawagusa, akasema, Inukeni, wala
msiogope. Wakainua macho yao, wasione mtu ila Yesu peke yake. Na walipokuwa
wakishuka mlimani, Yesu aliwaagiza, akasema, Msimwambie mtu ye yote habari ya
maono hayo, hata Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu.”
Unaona Petro
alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi wachache waliokwenda pamoja na Yesu katika
mlima mrefu faraghani na kuona maono mazito na walielezwa wasimwambie mtu awaye
yote kwa hiyo unaweza kuona uimara wa Petro, unaweza kujua kuwa alimjua Yesu
kwa viwango vikubwa na vya juu zaidi alikuwa shahidi wa Yesu Kristo mwenye
ujuzi mkubwa na wa juu zaidi hata wa kuelezea Yesu ni nani, Yeye mwenyewe
alikiri kuwa ni miongoni mwa watu waliouona utukufu wake
-
1Petro
1:16-18 “Maana hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa
werevu, tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake;
bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake. Maana alipata kwa Mungu Baba heshima
na utukufu, hapo alipoletewa sauti iliyotoka katika utukufu mkuu, Huyu ni
Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye. Na sauti hiyo sisi tuliisikia
ikitoka mbinguni tulipokuwa pamoja naye katika mlima ule mtakatifu.”
Petro alikuwa
miongoni mwa wanafunzi wa yesu waliowahi kuisikia sauti ya Mungu baba ikisema
huyu ndiye Mwanangu mpendwa ninayependezwa naye, na kama haitoshi miongoni mwa
wanafunzi wa Yesu aliyeweza kujibu swala la Yesu kwa ufasaha zaidi ya wanafunzi
wengine na kusifiwa kuwa alikuwa amefunuliwa na baba wa Mbinguni Petro alikuwa
ni wa kwanza
-
Mathayo
16:13-17 “Basi Yesu akaenda pande za
Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu
kuwa ni nani? Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya,
wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa
ni nani? Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye
hai. Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na
damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.”
Petro alikuwa ni
Mwanafunzi wa kipekee, alimjua Yesu Vizuri na alikuwa tayari kumfuata alifuzu
mitihani yote ya Bwana Yesu, alijaribu mambo mengi kuliko wengine ja unajua ya
kuwa ni yeye ndiye mwanafunzi pekee aliyejaribu kutembea juu ya maji?
-
Mathayo
14:25-30 “Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu
akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari. Wanafunzi walipomwona akienda juu
ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu. Mara Yesu
alinena, akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope. Petro akamjibu, akasema,
Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji. Akasema, Njoo. Petro
akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu. Lakini
alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe.”
Petro alikuwa
miongoni mwa wanafunzi wa Yesu ambao, walipata mafunzi mazui nay a kina nay a
ndani zaidi hususani wakati Yesu anafufua wafu
-
Marko
5:37-43 “Wala hakumruhusu mtu afuatane naye, ila
Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye Yakobo. Wakafika nyumbani kwa yule mkuu wa
sinagogi, akaona ghasia, na watu wakilia, wakifanya maombolezo makuu.
Alipokwisha kuingia, akawaambia, Mbona mnafanya ghasia na kulia? Kijana hakufa,
bali amelala tu. Wakamcheka sana. Naye alipokwisha kuwatoa nje wote, akamtwaa
babaye yule kijana na mamaye, na wale walio pamoja naye, akaingia ndani
alimokuwamo yule kijana. Akamshika mkono kijana, akamwambia, Talitha, kumi;
tafsiri yake, Msichana, nakuambia, Inuka. Mara akasimama yule kijana, akaenda;
maana alikuwa amepata umri wa miaka kumi na miwili. Mara wakashangaa mshangao
mkuu. Akawaonya sana, mtu asijue habari ile; akaamuru apewe chakula ”
Hata muda
mchache kidogo kabla ya kukamatwa kwa Yesu, Petro, Yakobo na Yohana
walichukuliwa hatua moja zaidi na Bwana kwaajili ya kuwataka waombe kwa kukesha
pamoja naye
Marko 14:33-35 “Akamtwaa
Petro na Yakobo na Yohana pamoja naye, akaanza kufadhaika sana na kuhangaika.
Akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa mkeshe.
Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akiomba ya kuwa, ikiwezekana,
saa hiyo imwepuke.”
Unaweza kuona maswala kadhaa
kuhusu Petro kwamba alikuwa ni mtu wa namna gani, na alikuwa na nafasi ya namna
gani katika moyo wa Yesu, na sasa bwana anaposema wote watakunguzwazwa usiku
ule kwaajili yake unaweza kupata picha ya mtu anayezungumzwa kwa kujiamini kuwa HATA WAJAPOKUNGUWAZWA WOTE LAKINI SIO MIMI,
yaani Petro alikuwa ana uhakika ambao haukuwa na shaka ndani yake kuwa yeye
anaweza kuwa tayari kwenda na Yesu gerezani, yeye anaweza kumtetea Yesu, yuko
tayari hata kufa naye, na hata kama wanafunzi wengine wote watamkimbia Yesu na
kumkana jambo kama hilo sio rahisi kwake Petro alizungumza kwa kujiamini sana,
huku akiwa na ujasiri uliopitiliza, akijiona yeye ana kitu cha ziada na wengine
ni wadhaifu, alijitumaini nafsi yake na akili zake, Watu wanaojifikiria kuwa
wao ni wajanja na wenye akili na ujuzi kuliko wengine mara nyingi ndio ambao
wakati mwingine hawafai kwa lolote high self-esteem was also linked to a
higher frequency of violent and aggressive behaviours , Watu wanaojiamini
kupita kawaida wakati mwingine ndio hujiweka katika nafasi kubwa ya kukosea na
kuharibu kabisa, na wakati mwingine
inaongoza katika uharibifu muwa wa mahusiano ya kila aina, kujiamini sio kitu
kibaya kwani wakati mwingine kinaongoza katika aina Fulani ya mafanikio, lakini
katika mazingira mengine kujiamini kupita kawaida kunatuletea udanganyifu wa
moyo, unaweza kujikuta unajikweza kupita kawaida, au unaahidi kitu ambacho
hauna uwezo nacho au uwezo wa kukitekeleza,
na Yesu alikuwa anamuelewa Petro alipojipambanua kuwa HATA WAJAPOKUNGUWAZWA WOTE LAKINI SIO MIMI
Yesu alikuwa anamuona kuwa usiku ule hata kabla ya kuwika jogoo jamaa
atamkana Yesu mara tatu
Luka 22:33-34.” Akamwambia, Bwana, niwapo
pamoja nawe, mimi ni tayari kwenda gerezani au hata kifoni. Akasema, Nakuambia,
Petro, jogoo hatawika leo, kabla wewe hujanikana mara tatu ya kuwa hunijui.”
Mambo muhimu ya kujifunza
Ni makossa makubwa sana kufikiri
au kuamini kuwa njia yako ya kufikiri na kutenda iko juu sana kuliko wengine,
au kufikiri kuwa wewe ndiye uko sahihi wakati wote, watu wengi wamefunga mlango
wa kupokea mawazo yaw engine na kunufaika na ushauri wa watu wengine kwa sababu wamefikiri kuwa wao ni bora kuliko
wengine na wamedhani wengine ni dhaifu, kufikiri hivyo ni kuona maluwe luwe tu kama Petro maluluwe luwe haya yanaweza
kukufikirisha kuwa wewe huwezi kukosea na hutakuja kukosea huku ni kujiamini
kuliko pitiliza, Petro alikuwa akimthibitishia Yesu kuwa yeye atakuwa pamoja
naye kwa gharama yoyote ile, hakuwa amejua kuwa Yesu ni Mungu na kuwa Mungu
anamuona,
Wako watu wa namna kama ya Petro
ambao wanajiamini kupita kawaida, wanafikiri kuwa wanamjua yesu kwa ukaribu
kuliko yeyote, wanamjua Mungu kuliko wengine, wana mafundisho sahihi kuliko
wengine , wana dhehebu zuri kuliko wengine, wana uzoefu na Mungu kuliko
wengine, wana ni hadari, ni waombaji, ni watoaji, wako mstari wa mbele katika
utumishi, wanaomba sana, wanafunza sana, wamefanikiwa sana na pengine hawana
dhambi au hawawezi hata kuanguka, wao wamenyooka kuliko wengine, wao wana nidhamu
kuliko wengine, wao waaakili kuliko wengine, Mtazamo wa aina hii hauwezi
kukubalika na Yesu, maandiko yanaonya
wazi wazi kila ajidhaniae ya kuwa amesimama na aangalie asianguke
-
1Wakorintho
10:11-12 “Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi
ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.
Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.”
Onyo linatolewa
kwa kila Mkrito na mafunzo yanaelekezwa kwetu kwamba wakati wote tusijifikiri
kuwa sisi ni bora kuliko wengine, Waandishi wa habari nchini Marekani waliwahi
kumuuliza Billy Gharamu kwamba ana maoni gani kuhusu anguko la Muhubiri
mwenzake aitwaye Jimmy Swaggat Grahamu alijibu kama swaggart ameanguka mimi
naweza kuanguka zaidi yake, Usifikiri wale wanao anguka kuwa hawampendi Mungu
kama wewe, Mungu hapadezwi kabisa na kiburi, kiburi na majivuno na kujihesabia
haki paee ni anguko tosha ndio maana
maandiko yanatuonya kuwahesabu wengine kuwa ni bora kuliko sisi
-
Wafilipi
2:3 “Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa
majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko
nafsi yake.”
Maandiko
yanataka wakati wote tujicheki wenyewe kwanza kabla ya kuacha kuwacheki wengine
-
Luka
6:41-42 “Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho
ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe
huiangalii? Au, utawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu yangu, niache nikitoe
kibanzi kilicho ndani ya jicho lako, nawe huiangalii boriti iliyo ndani ya
jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako
mwenyewe, ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi kilichomo katika jicho la
ndugu yako.”
Mungu atasimama
hukumuni na kila mtu anayejifikiri kuwa ana haki inayotokana na juhudi zake,
kiufupi maandiko yanaonyesha kukataliwa n ahata kukemewa kwa watu wanaojifikiri
kuwa wana ubora Fulani kuliko wengine
-
Luka
18:9-14 “Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya
kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote. Watu wawili walipanda kwenda
hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru. Yule Farisayo akasimama
akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu
wengine, wanyang'anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi
nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote. Lakini yule
mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni,
bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.
Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule;
kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.”
-
Isaya
65:5 “watu wasemao, Simama peke yako, usinikaribie
mimi, kwa maana mimi ni mtakatifu kuliko wewe; watu hao ni moshi puani mwangu,
moto uwakao mchana kutwa.”
Wako watu
duniani ambao kwa vipimo vyao vya kibinadamu hufikiri kuwa wana haki kuliko
wengine kwa sababu ya juhudi zao, na
hivyo wanashindwa kuona asili yao ya dhambi,
na kutokustahili kwao, hawajui kwamba bila msaada wa Mungu hatuwezi
lolote, na kuwa wakati wote tunahitaji rehema za Mungu, neema na msaada wake,
kwa sababu ya matendo yao ya nje na wema wa kinafiki wa kujionyesha na
kukandamiza wengine wakiwashutumu kuwa ni wenye dhambi na wao ni watakatifu, ni
dhaifu na waio ni wenye nguvu, hawana msimamo na wao ndio wanaostahili, ni
dhana ya aina hii ndio ilitompoza Petro akidhani ya kuwa yeye ni mwenye nguvu
na sio dhaifu kama wanafunzi wengine hili ndio tatizo kuwa la watu wengi wa
Mungu, kudhani kuwa wao ndio wao.
Nabii Eliya
aliwahi kujiamini na kujifikiri kua katika Israel Nzima watu wote wameabudu
sanamu na kusujudia mabaali alifikiri amebaki yeye peke yake na kwa kiburi
chake alijieleza mbele za Mungu kuwa amesalia yeye peke yake, ona
1Wafalme 19:9-10. “Akafika
kunako pango, akalala ndani yake. Na tazama, neno la Bwana likamjia, naye
akamwambia, Unafanya nini hapa, Eliya? Akasema, Nimeona wivu mwingi kwa ajili
ya Bwana Mungu wa majeshi; kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, na
kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua manabii wako kwa upanga; nami nimesalia,
mimi peke yangu; nao wanitafuta roho yangu, waiondoe.”
Warumi 11:2-4 “Mungu
hakuwasukumia mbali watu wake aliowajua tokea awali. Au hamjui yale yaliyonenwa
na maandiko juu ya Eliya? Jinsi anavyowashitaki Waisraeli mbele za Mungu,
Bwana, wamewaua manabii wako, wamezibomoa madhabahu zako, nami nimesalia peke
yangu, nao wananitafuta roho yangu. Lakini ile jawabu ya Mungu yamwambiaje?
Nimejisazia watu elfu saba wasiopiga goti mbele ya Baali.”
Mungu alitaka
kushughulika na kiburi cha Eliya aliwashitaki watu wa Mungu kana kwamba wote
wameasi na wote hakuna aliyesalia ila yeye peke yake, watu wa Mungu
hawashitakiwi, Mungu alimjibu kuwa anao wengine elfu saba wala hawajapiga goti
lao kwa baaali, unapokuwa na kiburi unajiona uko katika ulimwengu wa pake yako,
unauona umashuhuri wako wewe mwenyewe lakini Mungu anaiona mioyo, tuache
kujiamini kupitiliza, na badala yake wakati wote tuombe Mungu atupe
unyenyekevu, ujumbe mkubwa katika pasaka hii ni kutembea kwa unyenyekevu, Petro
alijiamini aliona kuwa yeye hawezi kukosea Lakini Yesu alimwambia hata kabla ya
kuwika jogoo utanikana mara tatu!
Ni Petro tena
yule yule aliyehitaji kufundishwa tena kuhusu kuwahubiri mataifa, kitendo chake
cha kuwa myahudi alifikiri hana kibali cha kuwahubiri mataifa, akijiamini tena
kupita kawaida kwamba Wayahudi ni safi na mataifa ni najisi, na katika moyo
wake aliwaita mataifa najisi Ni Mungu tena alimkemea Petro kuwa kilichotakaswa
na Mungu usikiite wewe najisi
Matendo 11:8-9. “Nikasema,
Hasha, Bwana, kwa maana kitu kilicho kichafu au kilicho najisi hakijaingia
kabisa kinywani mwangu. Sauti ikanijibu mara ya pili kutoka mbinguni,
Alivyovitakasa Mungu, usivinene wewe najisi.”
Wakati wote lazima
tukumbuke kuwa chochote ambacho Mungu ametujaalia ni kwa neema yake na sio
vinginevyo, juhudi zetu na jitihada binafsi hazina kitu cha ziada cha
kutusaidia, tutembee kwa unyenyekevu mbele za Mungu na kuacha kiburi na
majivuno na kila tunapozungumza tuweke akiba ya maneno kumbuka Mungu huwapinga
wajikwezao bali huwapa wanyenyekevu neema alisema Petro
1Petro 5:5 “Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee.
Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu
huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.”
Yakobo 4:6 “Lakini
hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao,
bali huwapa neema wanyenyekevu.”
“Hata wajapokunguwaa wote lakini sio Mimi
alisema petro kwa kujiamini kumbe atamkana Yesu mara tatu tena kwa kuapia”
Na Rev. Innocent Samuel Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni