Jumatatu, 18 Machi 2024

Ukuaji wa Kanisa


Matendo 2:46-47 “Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe, wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.”            



Lakewood Church ni Kanisa linaloongozwa na Mchungaji Joel Osteen, jijini Houston Texas Nchini Marekani  ni kanisa kubwa lenye washirika wapatao 45,000, Kanisa hili lina uwezo wa kuketisha watu 16,800 kwa wakati wa ibada moja na wana ibada nne za kiingereza na ibada mbili za Kihispania kwa wiki, hii ni moja ya mfano wa Kanisa kubwa


Utangulizi:

Somo hili linazungumzia kuhusu ukuaji wa Kanisa, kitu chochote chenye uhai kinakuwa, Kanisa lililo hai linakuwa na kuongezeka, kwa kawaida kanisa linakuwa, kiroho, kiidadi na kijiografia, yaani watu wake wanakua kiroho wanakomaa, wanakuwa na uzoefu wa kutosha katika kuukulia wokovu, lakini pia wanaongezeka kwa idadi ya watu waoookolewa kila siku, lakini pia linatawanyika kuyafikia maeneo mengine ambayo hayajafikiwa Matendo 8:4 “Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno.” Ili kanisa liweze kukua katika mazingira hayo makubwa matatu, kuna mbinu za ukuaji wa kanisa, mbinu hizo ndizo ambazo tunakwenda kuzizungumzia kwa undani, kwa kina na mapana namarefu katika somo hili Muhimu:-

Katika somo hili yako maswala mbalimbali kadhaa ambayo tutakenda kujifunza kwa undani kwa kuzingatia maswala kadaa wa kadhaa:-

Maana ya Mbinu za ukuaji wa kanisa (the Strategy For church Growth)

Mithali 24:5-6 “Mtu mwenye hekima ana nguvu; Naam, mtu wa maarifa huongeza uwezo; Maana kwa mashauri ya akili utafanya vita; Na kwa wingi wa washauri huja wokovu.”  Biblia ya kiingereza ya MSG inasomeaka hivi Proverbs 24:5-6 “It’s better to be wise than strong; intelligence outranks muscle any day. Strategic planning is the key to warfare to win; you need a lot of good counsel.” Neno Mbinu au Strategy linamaanisha ni kampeni za kijeshi, au Mbinu inayotumiwa na wewe au adui yako ili upoate au apate ushindi

·         Neno mbinu au Stategy Linatokana na neno la kiasili la kiyunani  Strategos  Strategy  ambalo maana yake ni kuongoza Jeshi kwa hivyo kimsingi linatokana na maswala ya uongozi wa kijeshi  (General) lakini linaweza kutumiika pia katika kampeni za mambo mengine na mikakati ya aina yoyote

 

·         Yesu alisema Nitalijenga kanisa langu juu ya mwamba wala malango ya kuzimu hayataliweza ni tamko la mikakati ya kijeshi kwani shetani amejaribu kuliharibu kanisa, kulidhoofisha na kulisambaratisha na kulitoa katika malengo yake makuu na kulifanya lisiendelee lakini wewe kama kiongozi wa kiroho katika eneo lako unapaswa uwe na mbinu na mikakati ya kuhakikisha kuwa kazi hii inaendelea na ushindi dhidi ya upinzani wa adui unapatikana na kazi inaendelea Mathayo 16:18 “Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.”

 

·         Uongozi hapa unajumuisha  kuwasaidia watu kufuata vema mpango mkakati na kushinda vikwazo na kufikia malengo yaliyokusudiwa katika staili ya kijeshi hii ndio mbinu, Kwa hiyo Mtumishi wa Mungu wa Kanisa la mahali pamoja ni mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa Kanisa ambaye anapaswa kuwa na fikra au mikakati ya kuhakikisha kanisa linakuwa na kusonga mbele kwa gharama ya dhamu ya Yesu kristo iliyomwagika pale msalabani

Neno kukua kwa kanisa lina maanisha kuwa kanisa ni

·         Kanisa ni zaidi ya dhehebu au shirika, ni kitu chenye uhai, na kitu chochote chenya uhai, kinakua, kinasegea, kinaweza kwenda mbele au kurudi nyuma, kusimama au kukaa au kutembea lakini la msingi Zaidi kadiri siku zinavyokwenda linapaswa kukua.

·         Ni kama mwili ulio hai wenye uwezo wa kukua na kujizalisha wenyewe, hii ina maana ya kuwa kila kanisa la mahali pamoja lina uwezo wa kukua na kujizalisha lenyewe na kupanda makanisa mengine hivyo kama kanisa lina uhai basi ni muhimu kanisa likaelewa jambo hili la msingi Yesu mwenyewe alitoa msingi wa ukuaji wa kanisa wenye nguvu ambapo kanisa linapaswa kukua kiroho, kiidadi na kijiografia.

 

·         Waefeso 4:11-14 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.”

 

·          Matendo 2:46-47 “Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe, wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.”

 

·         Matendo 1:8 “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”        

 

·         Maandiko yote hapo juu yanazungumzia ukuaji wa Kanisa kiroho, kiidadi na kijiografia na  hii ina maana ya kuwa kanisa linaweza kupandwa mahali kokote na katika jamii yoyote  na likaongezeka kutoka katika jamii hiyo na lika sambaa kuelekea katika jamii nyingine  na kuweza kufika hata sehemu nyingine ulimwenguni au mwisho wa nchi, huku watu wakibadilishwa katika tabia na mwenendo ili wamfananie Kristo, huu ndio msingi wa kimungu kwa hivyo mtu awaye yote asiogope kupanda kanisa au kuanzisha kanisa  huu ndio ulikuwa mkakati wa Yesu Kristo kuhusu kanisa lake  na ahadi yake ni kuwa pamoja nasi hata ukamilifu wa Dahari.

Kwanini tunasoma Mbinu za ukuaji wa kanisa?

·         Somo hili litatusaidia jinsi ya kushughulikia na maswala ya kiroho,tamaduni na nguvu ya jamii husika katika upandaji au ukuaji wa kanisa na litakufundisha  asili na ukuaji wa kanisa



·         Litasaidia kukuonyesha wewe na jamii ya watu unaowahudumia umuhimu na ulazima wa agizo kuu katika Mathayo 28:18-20 “Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.”  hii itakusaidia kuweza kuwa mfuatiliaji wa karibu wa kujua kuwa kanisa linakua au la kwa kutumia grafu au utafiti wa kawaida wa Ugunduzi kuhusu ukuaji wa kanisa,litakufundisha namna ya kuanzisha na kuendeleza kanisa.

 

·         Somo litakupa mifano mbalimbali ya ukuaji wa makanisa katika maeneo mbalimbali Duniani na kukuonyesha faida na uzuri au utamu wa kukua kwa kanisa pia katika eneo lako utajifunza tamaduni na muundo wa jamii unayoihudumia  na kuchagua njia inayofaa kwa ajili ya kujenga kanisa lenye nguvu litakalojieneza na kujiendesha na kijitegemea lenyewe indigenous church.

 

·         Kujifunza jinsi na namna ya kupanga mikakati ya kushambulia kwa injili miji na pamoja na kufikia kila jamii kwa injili, kupanda makanisa na kufanya kazi na watu na makundi yao katika namna mbalimbali, kutumia mbinu za kifundi kugundua ni maeneo gani yanapokea injili kwa haraka  na kuchukua hatua za haraka kupanda kanisa hapo, pia kupanga mipango au kuweka malengo ya baadaye katika eneo unalo lihudumia au uatakalolihudumia

 

·         Kuwa na uelewa kuwa nguvu ya ukuaji wa kanisa inategemeana na uhusiano wetu na Roho Mtakatifu kwako na kwa watu unaowahudumia  ili kuweza kuubeba agizo lile kuu na kanuni hizi zinazotolewa zinaweza kufanya kazi katika eneo lolote iwe mijini, kijijini kwa kanisa kubwa au kanisa lililo dogo.

 

Mbinu za ukuaji wa Kanisa:-

FANYA KAZI SAWA NA KANUNI ZA KIBIBLIA ZA UKUAJI WA KANISA

Mtu awaye yote ambaye anataka kanisa lake liweze kukua au anataka kupanda kanisa ni muhimu kwanza akafanya kazi au akakubaliana na kanuni za ukuaji wa kanisa zinazotolewa na Biblia hii ndio kanuni ya msingi ya upandaji na ukuaji wa kanisa katika sura hii tunashughulikia msingi huu wa Kibiblia na kitheolojia wa ukuaji wa kanisa katika msingi huu basi tutajifunza kwa kuzingatia maeneo manne

·         Lazima ujue kuwa unajenga kanisa lenye msingi wa Agano jipya

·         Lazima ukubali kuwa mwaminifu katika majukumu ya Shughuli hii

·         Lazima uweke au utoe kipaumbele kwa kile ambacho Mungu anakipa kipaumbele

·         Lazima ujue kufanya kazi na Mungu katika Uamsho

LAZIMA UJUE KUWA UNAJENGA KANISA LENYE MSINGI WA AGANO JIPYA

Biblia ni neno la Mungu na ndio msingi mkuu wa kwanza unaotuongoza katika mbinu yoyote ya ukuaji na upandaji wa kanisa, Biblia inafunua kuwa ni aina gani ya kanisa Mungu anataka  na ni namna gani anataka kanisa likue kwa msingi huo mbinu yoyote mbadala ya ukuaji au upandaji wa kanisa ni lazima itokane na misingi inayopatikana katika Biblia, Unapopanda kanisa kinyume na msingi ule unaowekwa na Biblia tunaouona katika agano jipya Basi ukuaji wa kanisa hilo utaingia matatani kama tunataka makanisa yetu yakuwe basi lazima tujenge msingi wa kanisa linalokuwa kwa mujibu wa makanisa ya agano jipya kumbuka kuwa mjenzi mkuu wa kanisa ni Yesu Kristo na ndiye aliyetualika sisi nasi kujenga pamoja naye Mathayo 16:18 “Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.”kwa msingi huo ili kanisa liweze kukua linatakiwa kuzingatia maswala ya msingi makuu matatu yafuatayo

a.       Lazima ujenge kanisa kwa msingi wa kibiblia

b.      Lazima ujenge kanisa ambalo Yesu Kristo ndiye kiini kikuu

c.       Lazima ujenge kanisa ambalo Roho Mtakatifu anapewa kipaumbele.

Lazima ujenge kanisa kwa msingi wa kibiblia

Ni muhimu kabla ya kuangalia kanisa kwa msingi wa kibiblia tuchukue Muda kujifunza neno kanisa kwanza lina maana gani:-

1.       Neno kanisa kwa kiingereza Church limetokana na neno la kiyunani Kuriake yaani mali ya Bwana

 

2.       Neno linalotumika katika agano jipya kuhusu kanisa ni neno la kiyunani Ekklesia ekklesia ambalo maana yake ni kusanyiko  ambalo neno lake la msingi ni Ekkleo yaani “walioitwa watoke miongoni mwa

 

3.       Kwa msingi huo Yesu alipokuwa anazungumzia habari za kujenga kanisa hakuwa anamaanisha kuwa atajenga Hekalu zuri juu ya mawe, alikuwa akizungumzia watu ambao angewaita watoke miongoni mwa udunia na kuwa awakusanye pamoja wawe wake kwa Makusudi yake ya milele

 

4.       Hata hivyo Biblia inapotumia neno kanisa hususani agano jipya ambalo hutueleza jinsi kanisa lilivyoanza na kukua na kuenea tunaweza kusema neno kanisa pia lina maana kuu nne zifuatazo

·         Ni kanisa la mahali pamoja (the Local church) Warumi 16:4-5 “Basi walipokuwa wakipita kati ya miji ile, wakawapa zile amri zilizoamriwa na mitume na wazee walioko Yerusalemu, ili wazishike. Makanisa yakatiwa nguvu katika ile Imani, hesabu yao ikaongezeka kila siku.”  Kwa hiyo hapa kanisa yaani ni kundi la watu waliookoka wanaokusanyika pamoja kila wakati kwa Makusudi ya kuabudu katika miji mbalimbali, au kijiji, au nchi sehemu Fulani fulani

 

·         Ni wakristo (The society of People) ni jamii ya watu Matendo 11:20-26 “Lakini baadhi ya hao walikuwa watu wa Kipro na Kirene, nao walipofika Antiokia wakasema na Wayahudi wa Kiyunani, wakihubiri habari njema za Bwana Yesu. Mkono wa Bwana ukawa pamoja nao, watu wengi wakaamini, wakamwelekea Bwana. Habari hizo za watu hao zikafika masikioni mwa kanisa lililokuwako katika Yerusalemu; wakamtuma Barnaba, aende hata Antiokia. Naye, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo. Maana alikuwa mtu mwema amejaa Roho Mtakatifu na imani; watu wengi wakaongezeka upande wa Bwana. Kisha akatoka akaenda Tarso kumtafuta Sauli; hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia.” Kanisa ni jamii ya watu wanaofundishwa ili waishi maisha yanayofanana na Kristo, na ndio kusudi hasa na maana ya jina wakristo

 

·         Mkutano au jamii ya watu walioko mahali Fulani wote wakiwa na Imani moja Mwili wa Kristo (The body of Jesus) Waefeso 1:22-23 “akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.”

 

·         Ni kila mwamini wa kweli katika Kristo waliopita, walioko na watakaokuja walio duniani au mbinguni kokote ambao majina yao yameandikwa mbinguni ni kanisa  Waebrania 12:23. “mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,”

               

5.       Maana nyingine za kanisa ni pamoja na

·         Jengo mahali  au nyumba ambapo wakristo hukutana kwa ajili ya kufanya ibada

·         Dhehebu, huu ni ushirika wowote wa Kikristo wenye mafundisho fulani sahii na namna fulani ya ibada za Kikristo na namna zinavyoendeshwa

Kwa msingi huo kuhitimisha maana ya kanisa tunaweza kusema kuwa kanisa ni kundi la watu wanapokutana pamoja kuabudu, kujifunza, na kuhudumiana na wanaomkubali Yesu kuwa Bwana na mwokozi wakifuata mafundisho yake na kumtumikia.

Kanisa lenye msingi wa kibiblia

·         Nyakati za kanisa la kwanza walitambua na kulikubali neno la Mungu kuwa limevuviwa na kuwa kanisa limetokana na Neno la Mungu, Kwa Msingi huo kanisa lazima litokane na kuhubiriwa kwa neno la Mungu na wale wanaolisikia kuliamini Matendo 4:4 “Lakini wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini; na hesabu ya watu waume ikawa kama elfu tano.”             

·         Waliamini katika ahadi za kibiblia na mafundisho ya mitume

·         Walikubali kuongozwa na neno la Mungu na kuwa ndio mamlaka ya mwisho lenye kuongoza kimaadili na kiimani

·         Walikuwa na imani yenye nguvu iliyojengwa katika msingi wa neno la Mungu

·         Walikataa kila aina ya fundisho lisilikubaliana na neno la Mungu au lenye msingi wa mila na tamaduni za kimapokeo

·         Walikubali kuteseka na walipotawanyika walieneza injili, walikubali kufa kwa ajili ya imani na walihubiri kotekote

·         Mafundisho yao yalikuwa yenye msingi wa kibiblia sawa na Mafundisho ya Bwana wetu Yesu

Kwa msingi huo mtu awaye yote akipanda kanisa kulingana na msingi wa neno la Mungu kanisa hilo litakua na kuendelea mbele na kamwe halite tikiswa, kwa sababu litakuwa sawa na kanisa alilolikusudia Kristo, watu wanalisikia neno, wanaliamini, wanalitii, wanaungana na mitume, wanajifunza, wanabatizwa, wanakuwa kiroho, wanakuwa waombaji, wanakuwa na misimamo, wanaichukia Dunia, wanaishi maisha yanayomuakisi Kristo, wanafundisho la mitume, wanaamini katika nguvu ya ujazo wa Roho Mtakatifu, wanamsikiliza, anawaongoza, wanafunga, wanatoa, wanatoa pepo, wana dalili zote za kanisa tunalolisoma katika kitabu cha matendo ya Mitume  

Kanisa lenye msingi wa kibiblia

Lilizaliwa kutimiza andiko

Matendo 2;1-21

Imani yeke katika Kristo ilitokana na maandiko

Matendo 17;2-4, 18;28

Mafundisho yalitokana na maandiko

Matendo 17;11-12

Washirika walifundishwa neno

Warumi 15;4,Matendo 18;11

Matumaini na kujitia moyo sawa na maandiko

Warumi 15;4

Maadili sawa na maandiko

1Koritho 10;5-11,1Timotheo 3;15-16

Mafundisho ni Neno la Mungu

Matendo 6;2-4,18;11

Imani na nguvu yao ni neno la Mungu

Efeso 6;13-17

Kukua kwake kulitegemea Neno la Mungu

2Petro 2;2

Kutawanyika kwao kulitegemea Neno la Mungu

Matendo 6;7,8;4,12;24.13;49

 

Lazima ujenge kanisa ambalo Yesu Kristo ndiye kiini kikuu

Kanisa lolote lile haliwezi kukua kama Kristo sio kiini kikuu cha kanisa hilo, Lazima tujenge kanisa lenye uhusiano na Kristo aliye mizabibu wa kweli Yohana 15;1-8 na sisi tu matawi ndani yake na ya kuwa hatuwezi kufanya neno lolote pasipo yeye hii ndio kanuni  ya nyakati za kanisa la kwanza walizingatia swala zima la kumpa Kristo kipaumbele Yohana 15:1-8 “Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa. Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.  Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea.Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.”

·         Kanisa lilikuwa kwa sababu lilikuwa na uhusiano mzuri na Kristo, watu walibaki ndani ya Kristo.

·         Kristo alihesabiwa kuwa kichwa na kanisa ni mwili wake walimtii walitumia mamlaka yake na jina lake  waliamini kuwa yeye ndiye anayetoa maelekezo anayelitunza na kulilisha kanisa

 

Wakolosai 1:9-19 “Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni; mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu; mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha; mkimshukuru Baba, aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru. Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi; naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.  Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.  Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye. Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote. Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae;”

 

Waefeso 1:16-19 “Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye. Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae;”

 

1Wakoritho 12:26-27 “Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho. Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake.”

 

·         Kristo alihesabiwa kama Mume na kanisa kama bibi harusi  kwa hivyo Yesu alilipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake analisafisha  na kulitunza na kanisa kama bibi harusi linajitoa kwa Kristo linampenda na kumtii linajitunza katika usafi  na uzuri 2Koritho 11;2-3,Warumi 7;2-4,Efeso 5;23-30,Ufunuo 19;7-8,21;2

 

·         Kristo anahesabiwa kama Mjenzi au jiwe kuu la Pembeni ndiye mjenzi mkuu na mbunifu wa swala zima la kanisa na kanisa ni Jengo la Mungu kwa msingi huu walifuata mpango wake walikuwa na umoja kwa ajili yake walijifanya kuwa nyumba halisi ya Mungu, Kwa msingi huo basi kanisa linalohitaji kukua ni lazima lijenge msingi wake katika kumuweka Kristo kama kiini kikuu cha maswala yote ya kikanisa.

Lazima ujenge kanisa ambalo Roho Mtakatifu anapewa kipaumbele

Kabla ya kuondoka kwake kwenda mbinguni Yesu aliwaambia wanafunzi wake waziwazi kwamba wanapaswa kusubiri nguvu za Roho Mtakatifu kabla ya kuanza kujaribu chochote katika agizo kuu Luka 24:44-49 “Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi. Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.  Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya. Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.”   

Matendo 1;1-8 “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”  kwa msingi huo Matendo yote ya kanisa tunayo yasoma katika kitabu cha Matendo ya mitume ni matokeo ya Nguvu hizo au agizo katika Matendo 1;8 Roho Mtakatifu ndiye anayetoa nguvu ya huduma na kusababisha kanisa kubeba kazi ya Mungu kwa ufasaha kwa msingi huo kanisa likizingatia hili na washirika wakiwa ni waliojaa Roho Mtakatifu na Viongozi litafanikiwa katika kila walifanyalo na walitendalo kwa ajili ya ujenzi wa ufalme wa Mungu .

Kwanini Roho Mtakatifu apewe kipaumbele katika Shughuli za upandaji na ukuaji wa kanisa?

·         Kwa ajili ya kushuhudia na kueneza injili Matendo 1;8

·         Kwa ajili ya kumtukuza Mungu na kuelezea kazi zake Matendo 2;1-11

·         Kwa ajili ya kuhubiri na kufundisha Matendo 2;14-47

·         Kwa ajili ya kutumia nafasi kuhudumu na kushuhudia Matendo 3;1-26

·         Kwa ajili ya ujasiri wakati wa upinzani Matendo 4;5-20

·         Kwa ajili ya kutiwanguvu upya kueneza neno Matendo4;23-31

·         Kwa ajili ya kuelewa na kutambua unafiki Matendo 5;14-16

·         Kwa ajili ya uponyaji na mijadala Matendo 5;28-29

·         Kwa ajili ya furaha wakati wa majaribu Matendo 5;40-42

·         Kwa ajili ya kumhudumia watu kwa haki Matendo 6;1-7

·         Kwa ajili ya uaminifu hata kufa Matendo 7;1-60

·         Kwa ajili ya kuhubiri kila mahali Matendo 8;1-13

·         Kwa ajili ya kupambana na nguvu za upinzani Matendo 8;9-13,Matendo 13;6-11.

·         Kwa ajili ya kusaidia wengine kuipokea Roho Mtakatifu Matendo 9;14-17

·         Kwa ajili ya kazi maalumu alizotuitia Matendo 9;10-20

·         Kwa ajili ya kuvuka mipaka ya kitamaduni Matendo 10;1-48

·         Kwa ajili ya kuwapelekea injili watu wasio wa utamaduni wetu Matendo11;1-26

·         Kwa ajili ya kufikia mahitaji ya wale wenye kuhitaji Matendo11;27-30

·         Kwa ajili ya kutuokoa kimuujiza wakati wa hatari Matendo12;1-17

·         Kwa ajili ya uongozi wake katika safari za umisheni Matendo 13;1-52

Lazima uweke msingi sio wa kumpa kipaumbele Roho Mtakatifu tu bali nafasi ya kuliongoza kanisa katika Nyanja zote, Nyakati za Kanisa la kwanza walifanikiwa sana kuupindua ulimwengu wa nyakati zao kwa sababu walimpa kipaumbele Roho Mtakatifu, Kumpokea Roho Mtakatifu lilikuwa ni swala nyeti kwa wakristo na mitume waliwauliza wakristo kama wamempokea Roho Mtakatifu sawa na kama walivyouliza watu wasiookoka je mmeokoka? Je mlipomkea Roho Mtakatifu pale mlipoamini?  Kwa nini walifanya hivi kwa sababu Roho Mtakatifu alikuwa wa Muhimu sana katika maisha ya muamini na ukuaji wa kanisa na huduma zake.

Matendo 19:1-6 “Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko; akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana. Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu. Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.”

LAZIMA UKUBALI KUWA MWAMINIFU KATIKA MAJUKUMU YA SHUGHULI HII

Ukuaji na upandaji wa kanisa ni somo gumu kueleweka kivitendo kutokana na mfumo wa kanisa na njia mbalimbali za ukuaji wake hii maana yake ni kuwa Shughuli hii inahitaji uaminifu kwa majukumu yoyote ambayo Mungu anakupa hata kama wakati mwingine mambo yaweza kuwa kinyume na matarajio hata kinyume na yale tunayokuwa tumemuomba Mungu kuyafanya pamoja nasi

Utata katika ukuaji wa makanisa

1.       Yesu alisema nitalijenga kanisa langu juu ya Mwamba na malengo ya kuzimu hayataliweza Mathayo 16;18 kwa msingi huo jambo la muhimu ni kutimiza kusudi lake na kwa kweli kanisa linakua kwa kasi ulimwenguni

·         Kanisa la Presbyterian huko Korea ya kusini lilikuwa kwa kasi na kuongezeka mara mbili katika miaka ya 1950 hata leo

·         Huko Ethiopia waongofu wapatao 120,000 walibatizwa

·         Watu 80,000 wa nyanda za juu walimfuata Yesu huko Formosa

Huu ni ushahidi ulio wazi kuwa kanisa linakua lakini wakati mwingine ni vigumu kujua kuwa kanisa linakua kwa sababu kadhaa zifuatazo

·         Mlipuko wa ukuaji au kuongezeka kwa idadi ya watu na hivyo kuongezeka kwa idadi ya watu wasiofikiwa

·         Kiburi cha udhehebu na matatizo ya kugawanyika kwa makanisa

·     Matukio yanayozuia ukuaji wa kasi wa kanisa kama vita, upinzani wa injili, ukimbizi n.k.

·   Kukosekana kwa taarifa za ukuaji wa makanisa duniani, kutokutunzwa kwa Kumbukumbu za ukuaji wa kanisa na kushindwa kutoa kipaumbele kwa maswala ya kuwafikia wale wasiofikiwa na injili

·         Kuwafikia wasiofikiwa na injili leo limekuwa si swala la muhimu katika makanisa, Makanisa yanayotuma wamishionari na Fedha za kusaidia kazi za umisheni wako gizani hawajui yanayoendelea huko, Matukio yanayozuia ukuaji wa kanisa hayabadilishwi na hubakia hivyo hivyo

Je Kanisa linaweza kukua kwa kasi kwa njia gani?

1.       Weka msingi wa ukuaji wa kanisa mapema wakati watu wanapoanza kuokoka

a.       Ukuaji wa kanisa ni jambo ambalo linatakiwa kupandwa mapema ndani ya watu wanaookolewa katika kanisa lako njia hii ilitumiwa na kanisa la Yoido Full Gospel Church (Assemblies of God) huko Seoul, Korea na kupata mafanikio makubwa sana

Ø  Mwaka 1973 Washirika walifikia 20,000 na kabala ya mwaka 1979 kanisa lilifikia idadi ya washirika 100,000.

Ø  Mwaka 1994 kanisa lilikuwa na washirika 700,000 watu wazima, Na sasa kanisa hilo lina watu washirika wapatao milioni mbili 2,000,000

2.       Zingatia umuhimu wa kuwa na makanisa ya nyumbani

Ø  Moja ya njia nyingine iliyotumika Korea ni kutawanya makanisa ya nyumbani, Mungu alimuongoza Mchungaji David Yonggicho na kumpa uwezo wa kukabidhi madaraka au kugawa majukumu kwa washirika kuhudumiana katika makanisa ya nyumbani

Ø  Washirika walikubali majukumu hayo na kuanza kufungua makanisa ya nyumbani ya kujifunza Biblia na maombi

Ø  Majirani walianza kukubali wokovu na matokeo yake idadi ya kanisa iliongezeka  na mwishoni mwa mwaka 1979 kulikuwa na makanisa ya nyumbani yapatayo 7,000 waliokuwa wakikutana kila wiki kwa ajili ya kuabudu pamoja wakijifunza maandiko na kuomba na kuabudu

Ø  Ilipofika Mwaka 1994 kulikuwa na makanisa ya nyumbani  yapatayo 21,800

3.       Zingatia umuhimu wa kuligawa kanisa linapokuwa limeongezeka

Ø  Mpango huu ndio mpango wa ukuaji wa kanisa unaouma lakini unasaidia sana katika ukuaji wa kanisa au ni mojawapo ya njia ya ukuaji wa kanisa kwani wakati mwingine inashauriwa kutumika kwa njia hii maadamu tu Mchungaji asiwe na roho ya ubinafsi

Ø  Njia hii inaweza kuleta uchungu na kuzuia ukuaji wa kanisa  wengi wameiacha imani kutokana na tabia zisizo za Kikristo na kukosekana kwa upendo  kunakotokana na mafarakano

Ø  Wakati mwingine kundi moja linapoondoka lile linalobaki huona wanazidiwa katika kukabiliana ana majukumu yaliyokuwa mbele yao mgawanyo huu unaweza kusababisha kutokuweko kwa umoja katika kanisa katika mwili wa Kristo vyovyote iwavyo Historia ya kanisa inaonyesha ya kuwa Mungu huitumia njia hii wakati mwingine ili kusababisha ukuaji wa kanisa, Baadhi ya madhehebu pia yamezaliwa kutokana na kuchangiwa na tabia za kutokupokelewa vema katika makanisa yao ya awali

 






                                  Moja ya njia za ukuaji wa kanisa wakati mwingine ni kugawanyika.

 

Mambo ya kufanya njia hii inapotokea

 

Kanisa linapogawanyika hata kama ni kwa mafarakano au kwa Ridhaa ya Mchungaji wa kanisa mama ni muhimu kufahamu kuwa unawajibika kufanya mambo ya msingi yafuatayo

·         Kumbuka kuwa ni mpango wa Mungu Kanisa kukua hata kama njia inaweza kuwa sio sahii lakini wakati mwingine Mungu kwake ni sahii

·         Omba kwamba Bwana awabariki wale walioondoka na kuwa Mungu awatumie kuwa Baraka na kufanya kazi ya injili na kuieneza katika eneo lao

·         Waonyeshe upendo wale walioondoka na shirikiana nao kwa njia yoyote iwezekanayo ambayo haiko kinyume na Biblia

·         Hakikisha kuwa unalifanyia kazi swala la kusamehe na kutokuwaona wapendwa katika Bwana kuwa maadui zako na elewa kuwa ni njia ya lazima katika kuzalisha ukuaji wa kanisa

4.       Zingatia umuhimu wa kanisa mama kuzaa kanisa jipya

Maswala ya kuzaa makanisa mengine ni lazima yawekewe msingi katika makanisa mama au wachungaji husika, mara nyingi kunakuwa na visingizio vingi lakini kama tupo kwa ajili ya Mungu mpango huu ni wa lazima

Ø  Unaweza kupunguza idadi ya washirika wanaotokea upande fulani au familia zinazotokea upande fulani kisha kisha ukazaa kanisa jipya

Ø  Au unaweza kuweka mpango wa aina nyingine kutoka kanisa mama kuzaa kanisa

Ø  Au unaweza kuweka mpango wa kufundisha watenda kazi au kuandaa watumishi ndani ya kanisa lako kisha ukawatuma katika eneo jipya na kuzaa makanisa kanisa lililo hai huzaa na kuongezeka lenyewe

5.       Kumbuka kuwa njia kubwa ya mafanikio ni ile ya makanisa ya nyumbani

Ø  Njia hii ndio njia nzuri zaidi kwani watenda kazi walioandaliwa kumhudumia makanisa ya Nyumbani makanisa hayo yanapokuwa katika mitaa yao baadaye yanaweza kugawanywa na kuwa makanisa kamili  hii imefanikiwa kule Korea

6.       Njia nyingine za upandaji au ukuaji wa makanisa ni pamoja na

Ø  Kushuhudia nyumba kwa nyumba katika maeneo ya kanisa

Ø  Kulenga kuyafikia maeneo yaliyo mbali na kanisa, kuwafikia walioko magerezani,kufanya mikutano ya injili, kugawa tracts na kuwazuia Biblia kwa bei nafuu

Ø  Kuongezeka kwa kuzaliana

Ø  Kuwatumia washirika wanaohamishwa katika maeneo yasiyofikiwa kuanzisha makanisa

Ø  Kujaribu kuwarejesha wale waliorudi nyuma

Ø  Kutumia vyombo vya habari, kama televisheni, radio na magazetu pamoja na huduma za jamii

Ø  Kuanzisha vyuo vya Biblia kwa wale wanaopenda kujifunza Biblia kwa mitindo hii kanisa litaweza kukua



Kanisa kukua ni swala la uaminifu kwa Mungu

Uaminifu kwa Mungu katika kuhakikisha kuwa kanisa lake linakuwa hujumuisha swala zima la

1.       Kuhubiri injili lakini kuhubiri injili bila kufanya wanafunzi au kufanya ufuatiliaji ni tabia isiyo ya uaminifu kwa kanisa, kama kanisa halijajipanga kuhakikisha wanaookolewa wanasimama ni bora kutokufanya mikutano

2.       Kuhubiri injili kisha kutokufanya ufuatiliaji wa kiuanafunzi kwa waongofu wapya ni kutimiza au kuwa mwaminifu kwa sehemu tu ya lile agizo kuu

3.       Ni kushindwa kuliko wazi kwa kutafuta waliopotea ambao wameweza kuitikia vema ujumbe wa injili

4.       Ni kushindwa kuona umuhimu wa nini kifanyike baada ya kushuhudia au Kuhubiriwa kwa injili na watu kuokolewa hili ndilo tatizo la makanisa mengi leo

5.       Kanisa la kwanza hawakuwa hodari katika kuhubiri pekee bali katika kuhakikisha wale waliohubiriwa wanakaa katika Imani ona Matendo 15:36 “Baada ya siku kadha wa kadha Paulo akamwambia Barnaba, Haya! Mrejee sasa tukawaangalie hao ndugu katika kila mji tulipolihubiri neno la Bwana, wa hali gani.”

Kuna njia Tano muhimu za kuonyesha uaminifu wetu kwa Mungu sambamba na ukuaji wa makanisa

1.       Kutoa zaka  na matoleo mengineyo kwa uaminifu kama utii kwa neno la Mungu ili Fedha itumike kwa Makusudi ya injili

2.       Kumtangaza Kristo kama mwokozi, kila mahali na kila wakati

3.       Kuweka mikakati na kuwafikia waliopotea kwa njia na namna mbalimbali

4.       Kuhakikisha kuwa waongofu hao wapya wanafuatiliwa na kulishwa neno la Mungu

5.       Kueneza kanisa lililojaa Neno na nguvu za Roho Mtakatifu

6.       Kutunza Kumbukumbu ya watu wanaookolewa na idadi yao

7.       Kuhakikisha walioamini wanakuwa wanafunzi kwa kupanga madarasa ya kibiblia

Uaminifu kwa Mungu ni swala gumu na wala sio swala rahisi kama tunavyofikiri

Historia inaonyesha kuwa ukuaji wa kanisa unatofautiana katika kila eneo kutokana na hali zinazochangiwa na eneo husika au na watu husika na ziko sababu mbalimbali zinazochangia hali kuwa rahisi au kuwa ngumu sababu hizi zinaweza kuwa ni kanisa lenyewe husika au jamii au siasa au uchumi au hali ya tamaduni na maswala mengineyo yanaweza kuchangia katika ukuaji au kutokukua kwa kanisa  na wakati mwingine sababu zinaweza kuwa za kipekee sana kiasi cha kuweza kusababisha hali iliyotumika mahali fulani isifanye kazi katika mazingira mengine

Uamsho huko Philippines.

Nchini Ufilipino (Philippines) kumewahi Kuweko na Uamsho mkubwa sana kwa sababu ya Mafundisho kushuhudia na makanisa mengi yalipandwa na kustawi lakini ni hali gani zilichangia Filipino Kuweko na Uamsho huu

a.       Wakati wa vita vya pili vya dunia wafilipino wengi waliamua kuishi milimani mbali sana

b.      Mchungaji mmoja aliyeitwa Dia na mkewe waliamua kukataa kushirikiana na maadui na kwenda kuhubiri huko ndani milimani na Mungu aliwaongoza kuifikia miji mitatu midogo, huko walipata washirika ingawa Mchungaji wao alikuwa dikteta Kanisa lilikuwa licha ya Historia hiyo ya kukatisha tamaa, kuzunguka nakutawaliwa na maadui mazingira ambayo sehemu nyingine huweza kufanya kanisa lisikue, kuzungukwa kwa hatari kwa Mchungaji Dia na nchi ya milima kulimfanya kutopuuzia kuyafikia makundi ambayo Mungu alitaka aweze kuyafikia na kuleta Uamsho

 

c.       Mambo yaliyochangia kukua kwa kanisa huko Ufilipino ni pamoja na mialiko,uwezo wa kuwafuata watu ndani sana, Mafundisho na mahubiri mazuri Uamsho wa wakristo, ushuhudiaji wa nyumba kwa nyumba, ufuatiliaji na kustawisha makanisa yaliyozaliwa hali hii ilipelekea kuwako kwa Uamsho mkubwa nchini Filipino

Maeneo mapya ya kinjili

India

·         Mpaka mnamo nusu ya Karne ya 19 na mwanzoni  mwa karne ya 20 Tatizo kuu nchini India lilikuwa ni ubaguzi wa wenyewe ka wenyewe ujulikanao kama Caste system mpaka nyakati za hivi karibuni bado jamii ya kihindu wanafuata ubaguzi huu wa kijamii kwa sheria iitwayo Manu jamii ya kihindu imegawanyika katika makundi manne ya jamii

·         1 Brahmins hii ni jamii ya makuhani na wasomi

·         2 Kshatriya  hii ni jamii ya mashujaa wanajeshi

·         3 vaishyas hii ni jamii ya wasanii,wafanya biashara na wakulima

·         4 Sudras hii ni jamii ya vibarua na walala hoi

·         5. Outcastes hii ni jamii ya watu wenye hali ngumu nay a chini sana na wanaodhaniwa kuwa waliolaaniwa




  

    Brahimas           Kshatriyas                  Vaishyas                        shudras                outcastes

 Jamii ya madaraja ya ubaguzi ya kihindu Kama yanavyoonekana katika michoro Picha na maelezo kwa hisani ya Library ya Mwalimu wa somo Mchungaji Innocent Mkombozi Kamote

 

·         Katika madaraja hayo manne ya watu huko India kuna madaraja ambayo  yanaingilika na kuna madaraja ambayo hayaingiliki kwa maswala ya kuwapelekea injili au hata mawasiliano ya kawaida

·         Mahatma Gandhi wakati fulani aliwahi kufunga siku 21 na kuhatarisha maisha yake ili kuwapandisha watu hao daraja  na alifanya kila jitihada kuwainua  na walijulikana kama Harijan ambalo ni jina maalumu kuwa watu wa Mungu hili ni jina walilopewa na Mahatma Gandhi

·         Jamii hii ya watu wa daraja la chini ni rahisi kuipokea injili huko india ukilinganisha na madaraja mengine

 

Zambia

·         Zambia injili iliingizwa kwa kupandikizwa shule wamishionari wengi waliopanda makanisa kusini mwa jangwa la sahara walitumia shule na hivyo ilisaidia watoto wa wapagani waliokuja kusoma kuingiziwa injili na kuikubali

·         Kwa msingi huo njia ya kuingiza injili katika eneo fulani inategemea kuwa mazingira hayo yakoje na Mungu anakupa namna gani ya kupenda kanisa au kupeleka injili kulingana na eneo husika

Iceland

·         Injili ilipandwa kupitia kuongoka kwa familia nzima nzima mpaka mwaka wa 1000 baada ya Kristo kisiwa chote kilikuwa kimeukubali ukristo

Amerika ya kusini Latin America

·         Injili iliwafikia kupitia Vyombo vya habari Redio, Television na magazeti yalitumika kuwafikishia ujumbe wa injili  vilitumika aidha kwa ajili ya kutangazia semina za kuandaa Viongozi, kampeni za maombi, watenda kazi na mikutano mikubwa ya injili iliyokuwa na nguvu za Roho na uponyaji vilizifanya nchi za Brazil na America ya kusini na kati kufikiwa kwa injili

·         Waliompokea Kristo walifanyiwa ufuatiliaji, walipewa Biblia na madarasa ya waongofu wapya yalianzishwa, makanisa ya nyumbani na shule za Biblia kwa njia ya Posta

Kwa msingi huo ni muhimu kufahamu kuwa ukuaji wa kanisa unatofautiana kati ya udongo na udongo au kati ya sehemu na sehemu na nivigumu wakati mwingine kutumia kanuni iliyotumika sehemu fulani ikafanya kazi sehemu nyingine na kama tulivyoona maeneo mengine Fedha inahitajika sana katika kuwafikishia injili

LAZIMA UWEKE AU UTOE KIPAUMBELE KWA KILE AMBACHO MUNGU ANAKIPA KIPAUMBELE

Jambo kubwa la msingi kabla ya kuangalia kanuni zozote za ukuaji wa kanisa ni kukubali kutoa kipaumbele kwa kile ambacho Mungu anakipa kipaumbele yaani kusudi lake la kuwafikia watu wote duniani ni la Muhimu sana ukiisha kuwa na moto ambao Mungu anao ndipo sasa yeye atakupa njia na msaada wa kukujulisha wapi uweke nguvu kubwa, wapi utoe Muda wa kutosha, wapi utapata Fedha kwa ajili ya kutimiza huduma aliyokuitia ni kitu gani ambacho Mungu anakipa kipaumbele?

·         Ni mpango mzima wa Mungu kwa wanadamu

·         Kila kinachofanywa sawa na maagizo ya Yesu ni mpango wa Mungu na Mungu amekipa kipaumbele  mfano, Kutoa chakula kwa wenye njaa, kuonyesha upendo na kuipeleka injili kwa kila jamii au kushughulikia na yatima na wajane n.k.

·         Kubwa zaidi ni kuipeleka injili na kutimiza agizo kuu kusudi kuu la Mungu ni kutafuta waliopotea ni kuwarudishia watu uhusiano wake na Mungu Yohana 20:21 “Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi.” 2Wakoritho 5:18 “Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho;”

·         Kanisa ndilo lenye wajibu huu na kila mwamini anao wajibu huu pamoja na kutimiza Mathayo 5:16 “Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.”

Kusudi la Mungu ni kutafuta kile kilichopotea

1.       Luka 15 ina mafundisho yanayohusu Jinsi Mungu anavyotoa kipaumbele katika kutafuta kile kilichopotea kuna mifano kadhaa inayotolewa katika sura hii kama vile

·         Mchungaji kutafuta mwana kondoo aliyepotea

·         Mwanamke kutafuta shilingi iliyopotea

·         Baba kumpokea mwana mpotevu

·         Mifano yote hiyo inaishia na kuonyesha furaha na ushindi wa kukipata kile klilichokuwa kimepotea

·         Mungu ni lazima atafute kile kilicho chake kilichopotea ni haki yake kwa sababu ni uumbaji wake  kwa msingi huo kusudi la Mungu ni kuokoa na kuhakikisha wale waliopotea wanarudi kwake na sio kupotelea huko

·         Kutafuta ni muhimu na kwa sababu hiyo kusudi kuu la Mungu au kile ambacho Mungu anakipa kipaumbele ni kuhakikisha kuwa waliopotea wanakuja nyumbani.

·         Kusudi la Mungu na huruma zake limefunuliwa katika Luka 15 aidha tunaona katika sehemu nyingine pia za Biblia zikiunga mkono kusudi hili la Mungu kwa mfano

*      Maombi ya Bwana Yesu kwa wanafunzi wake Mathayo 9;37-38

*      Agizo la Bwana Yesu kwa wanafunzi wake Mathayo 28;19-20

*      Mifano hiyo ya Bwana yesu kuhusu vilivyopotea Luka 15

*      Kusudi Yesu alilolitoa kwa ajili ya kuja kwake Luka 19;10

*      Msukumo wa Mungu kumtoa mwana wake wa pekee Yohana 3;16

*      Kazi ya mitume katika kutimiza agizo kuu Matendo 2;37-38

*      Ujumbe kwetu kama mabalozi wa Kristo 2Koritho 5;18-20

·         Kwa msingi huu basi Mungu anataka kila kanisa la mahali pamoja kuweka kipaumbele katika maswala ambayo yeye ameyapa kipaumbele na tukafanya hivyo makanisa yatakua na kuwafikia wengi waliopotea duniani.

 

2.       Fuata maelekezo ya Mungu katika huduma

a.       Biblia inatoa maelekezo ya namna ya kutimiliza huduma tulizo nazo katika kuwafikia wasio fikiwa kwa msingi huo kila muumini katika kanisa ni lazima atumie nafasi uwezo na kipato alicho nacho katika kuhakikisha kuwa wanavitumia vile Mungu alivyowapa katika kazi yake.

*      Kila mshirika atiwe moyo kutumia kile alichopewa na Mungu kwa faida ya ufalme wa Mungu

*      Kumbuka ule mfano wa talanta Mathayo 25:14-30 unatupa ujumbe gani

*      Unatoa onyo kwa wale wasiotumia kile walicho nacho hata kama ni kidogo

*      Kanisa litakuwa na kuongezeka kama kila mshirika atatumia kwa makini au kufuata kwa makini maelekezo ya Mungu  na kutumia njia na uwezo aliopewa na Mungu kwa namna yoyote ile kuwafikia wengine

*      Kwa msingi huo kila mmoja anahitaji maelekezo Binafsi ya Mungu ili kushiriki au ashiriki namna gani katika kulitimiza Jukumu lililoko mbele yetu

b.      Wajibu wetu Kibiblia sasa ni lazima kuweka kipaumbele katika mambo yale ambayo Mungu anayapa kipaumbele tukikumbuka kuwa watu Bilioni tatu hivi duniani hawajafikiwa wala kuisoma Biblia hata ile ya agano jipya Jukumu hili si la watu fulani ni Jukumu la kila mtu  kwa hiyo watu wafanye nini sasa ili kutimiza majukumu yao?

*      Kila mtu anawajibu wa Kushuhudia watu nyumba kwa nyumba au mtu kwa mtu

*      Kuwezesha  vipindi katika vyombo vya habari

*      Kufanya mikutano ya mitaani

*      Kutembelea wagonjwa mahospitalini na magereza

*      Huduma kwa wanafunzi mashuleni na vyuoni

*      Na kuwafikia wasiofikiwa kwa kubuni mbinu ambazo zitaleta matunda

*      Kuonyesha upendo kivitendo.

*      Kufanya kazi hii na Roho Mtakatifu.

LAZIMA UJUE KUFANYA KAZI NA MUNGU KATIKA UAMSHO

Uamsho ni nini?

Hakuna malezo ya kutosheleza katika msemo mmoja juu ya Uamsho lakini kuna semi nyingi zinazoweza kutumika kuelezea Uamsho

1.       Ni nguvu kubwa ya kiinjilisti iliyoamka inayowaleta watu katika mguso wa Roho wa Mungu

2.       Ni kazi ya Roho Mtakatifu ya kupandikiza maisha mapya na nguvu za Ukristo na kanisa

3.       Ni Kuamka kwa hali ya kujirudia ndani ya waamini ili kuwafikia wasio fikiwa au wenye dhambi

4.       Ni Ufufuo au hali ya kurudisha uhai tena , ni kuamsha hali za kulipuka kwa utendaji mkuu wa kimungu katika kanisa

5.       Ni nguvu kubwa ya kupanda makanisa na kuhakikisha yanasitawi kila mahali ambako injili haijafika

6.       Ni kiu ya kuona maelfu kwa maelfu wanakuja kwa Yesu, makanisa yanaongezeka kiroho, kiidadi na kijografia

7.       Kiu ya watu kujazwa Roho Mtakatifu, kuwepo kwa Karama na utendaji mkubwa wa Roho Mtakatifu, kiu kubwa ya maombi na kufunga bila watu kusukubwa, kiu ya kujifunza na kusoma neno la Mungu, kiu ya kuhudhuria ibada na kuwa tayari kujifunza na kuyatendea kazi yale watu waliyojifunza

Mambo sita yanayo saidia kuleta Uamsho

1.       Kusudia kuwa na uhitaji wa Uamsho

Lazima kama unahitaji Uamsho katika kanisa lako basi kiwe ni kitu kilicho maanishwa kabisa hii ni kwa sababu kuna wakati mwingine hutokea washirika wengine hawahitaji Uamsho kwa sababu kadhaa zifuatazo

*      Wako washirika wanaogopa Uamsho

*      Wanahofia kuwa kutatokea mitikisiko mikubwa  na maswala mengine yatafumuka

*      Wanahofia kutokea kwa migawanyiko kwani baadhi watakuwa wanakiu ya kumtafuta Mungu kwa undani sana na wengine hawata mtafuta Mungu

*      Hivyo ni lazima kama unataka Uamsho ukusudie kweli kweli na washirika pia, washirika wakongwe wasiwavunje moyo wachanga na badala yake wawaonyeshe upendo na kuwatia moyo ili wakue

2.       Kubaliana na Hali za Kipentekoste

*      Kumbuka kuwa ile hali ya wakati  wa pentekoste  itashuka katika kanisa

*      Mabadiliko ya waamini binsfi na kundi lazima yatokee

3.       Kubaliana na Mfumuko wa maombi

*      Watu wataungana kwa pamoja katika kuomba sawa na Matendo 4:24-31

*      Ujasiri wa kushuhudia na kuhubiri Matendo 28:30-31

*      Kuokoka kwa wenye dhambi Matendo 9:3-5

*      Huduma za uponyaji na miujiza Matedno 19:11-12

*      Mapepo kufumuka na kutolewa Matendo 19:11-12

*      Kusamehe maadui na kuwaombea maadui Matendo 7:54-60

*      Kutokea kwa mateso na majaribu makali na watu kukubali hata kufa Matendo 20:9-12

*      Matukio ya kupita kawaida wakati wa ibada  na wakati wa kuabudu Matendo 19:11

4.       Soma kwa undani kitabu cha Matendo ya mitume

*      Wengi wa watu waliofanikiwa kupata Uamsho wanashuhudia kuwa walipata nguvu hiyo kutokana na usomaji wa kitabu cha Matendo ya mitume na kutamani kuyaona waliyoyasoma

*      Uamsho mara nyingi huwajia watu wanaouhitaji na kuuomba kwa bidii na hivyo lazima kuukaribisha na kusoma kitabu cha Matendo ya mitume ni maandalizi ya Uamsho na namna ya kuukaribisha  Uamsho kwa kawaida unaturejesha katika kile kilichofanyika katika nyakati za kanisa la kwanza na hivyo tunahitaji kujua nini kilitokea ili kujiandaa

*      Soma historia za uamsho kwa mfano uamsho wa (Azusa Street Rivival) ambapo umasho mkubwa ulitokea kati ya Tarehe 9 mwezi April mwaka 1906 na kuendelea mpaka 1915, ambapo uamsho huu ulianza na Muhubiri Mmarekani mweusi William Seymour ambaye alialikwa huko Los Angels ambaye alikuwa akisisitiza sana kuhusu mjadala uliokuweko kuhusu Ujazo wa Roho Mtakatifu ambapo alipokuwa anahubiri watu kadhaa walijazwa Roho Mtakatifu na kuanza kunena kwa Lugha, wakipiga kelele huku wakimtukuza Mungu jambo lililoshitua watu na kusababisha watu kuja kushangaa na huko wagonjwa waliponywa na watu wakajazwa Roho na ndio ukawa Mwanzo wa uamsho wa kipentekoste ulioenea kote duniani hata leo

5.       Omba kwa ajili ya Uamsho

*      Hakuna mahali ambapo Uamsho ulitokea Bila maombi ya bidii kila mahali katika historia za Uamsho watu walianza kuomba sana kwa bidii wakati mwingine kwa kuendelea kwa majuma na miezi bila kukoma

*      Huko Korea mwaka 1907 waamini walianza kuomba kila saa 11 alfajiri  na jambo hilo lilichangia katika kukua kwa kanisa (Maombi ya Alfajiri)

*      Amerika Mwaka 1858 watu walihudhuria maombi kwa viwango vikubwa sana  mpaka ikashindikana namna ya kupata mahali pa kuwaweka miguu, muungano wa madhehebu katika maombi ulichangia sana katika kukua kwa kanisa

*      Huko Scotland 1859 walianzisha maombi ya jioni kila siku jioni  kwa muda wa mwaka mzima na Uamsho mkubwa ulitokea

*      Swala la kuomba na Uamsho linaonekana kwa wale 120 walioamua kusubiri kwa maombi kusubiri nguvu waliyoahidiwa na Kristo

*      Uamsho uliotuletea makanisa ya Kipentekoste ya karne hii ya 20 ulianza na maombi kulikuwa na vikundi vya waombaji kutoka makanisa mbalimbali kama Lutheren, Methodist, Presbyterian, catholics na washirika wa makanisa mengine

*      Ni muhimu kuimba, kuhubiri na kufundisha kuhusu Uamsho pangeni Muda manaokubaliana kikanisa kwa ajili ya maombi ya Uamsho

*      Mahubiri kuhusu Uamsho yatawahamasisha kuwa na hamu na shauku kwa ajili ya Mungu na kupandisha imani na kutaka Uamsho huo

*      Mwisho fanyia kazi yale yote unayoayaombea kwani Imani bila Matendo imekufa Yakobo 2;20.

*      Ombea watu ujazo wa Roho Mtakatifu, hubiri, panda makanisa, ombeni, anza kiri Uamsho.

 

Vikwazo Vikuu vya Uamsho katika makanisa

Mambo yanayosaidia kukua kwa kanisa

Vikwazo vinavyozuia kukua kwa kanisa

 

Mazingira

1.       Watu wanaopokea Injili kirahisi

2.       Mazingira ya watu wakarimu na wakaribishaji

3.       Watu wanaoingilika

 

 

Mazingira

1.       Watu wasiopokea injili kwa urahisi

2.       Mazingira ya  wasio wakarimu na wakaribishaji

3.       Watu wasioingilika wagumu kuwafikia

 

 

Watu wa Ndani ya Kanisa

1.       Watu wanaobadilishwa na Kristo, waliokomaa

2.       Kuishi kwa furaha na Amani, Mchungaji na watu wake

3.       Wakristo wepesi washuhudiaji

4.       Mchungaji na washirika waliojaa Roho Mtakatifu

5.       Mvuto wenye nguvu katika maisha

6.       Maono, Imani na maombi

7.       Imani katika Neno la Mungu

 

Watu wa Ndani ya Kanisa

1.       Watu ambao ni , vuguvugu, na waliodumaa

2.       Watu wasio na Amani, wenye mafarakano, na migongano

3.       Watu wasiojua wajibu wao kazi ya injili ameachiwa Mchungaji tu

4.       Wachungaji na washirika waliopoa wasio na Roho Mtakatifu

5.       Maisha yasiyo na ushuhuda

6.       Hakuna maono, Imani wala maombi

7.       Hakuna Imani katika neno la Mungu

 

 

Programu za ndani ya Kanisa

1.       Ibada zenye mpangilio na mvuto mzuri

2.       Roho wa Mungu kupewa nafasi   

3.       Kanisa linye lengo la kufikia wengine 

4.       Mafunzo kwa washirika wote 

5.       Kanisa linalojali mshirika mmojammoja 

6.       Wote wanashiriki huduma kikamilifu 

7.        Watenda kazi wazuri wanafungua kazi                                                               

 

Program za ndani ya Kanisa

1.       Ibada zisizo na mpangilio unaoeleweka

2.       Ibada zisizo na mwelekeo

3.       Kanisa lenye kujiangalia lenyewe pale pale lilipo

4.       Mafunzo kwa baadhi ya washirika tu

5.       Kanisa ambalo Mshirika anapotelea humo hajaliwi

6.       Huduma inaachiwa wale wanaolipwa tu

7.       Watenda kazi wazuri wanapewa uongozi

 

 

Njia zinazotumiwa na Kanisa husika

1.       Kuhubiri na kuifundisha Biblia

2.       Watoto wa washirika wanaokoka

3.       Wanayafikia maeneo yasiyofikiwa

4.       Mikutabo ya injili mara kwa mara

5.       Kutembelaa na kushuhudia

6.       Kutumia vyombo vya habari

7.       Mafunzo ya Biblia kwa njia mbalimbali

8.       Maombezi, miujiza na uponyaji

9.       Washirika wanaojitoa kwa 100%

10.   Wenye mipango ya kuongezeka

 

Njia zinazotumiwa na Kanisa husika

1.       Mafundisho na mahubiri duni

2.       Watoto wa washirika wanasahaulika

3.       Wanahubiriana ndani tu

4.       Ibada za kawaida tu zinaendelea

5.       Hakuna kutembelea wala kushuhudia

6.       Hakuna matumizi ya vyombo vya habari

7.       Hakuna mafunzo ya Biblia kwa njia nyionginezo

8.       Hakuna, maombezi miujiza wala uponyaji

9.       Washirika hawajitoi kwa dhati ni unafiki tu

10.   Hakuna mipango ya namna ya kuongezeka

 

 


UPANDAJI WA MAKANISA NI MOJA YA NJIA YA KUKUA KWA KANISA.

Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa ukuaji wa kanisa umegawanyika katika makundi makuu  matatu yaani Kiroho, Kiidadi na kijiografia kukua kiroho ni hali ya kutoka katika uchanga kuelekea katika hali ya kukomaa, kiidadi ni kuongezeka kwa idadi ya watu wanaookolewa katika kanisa la mahali Pamoja, na kijiografia ni kutwawanyika kutoka mahali pamoja na kupeleka injili na amakanisa katika maeneo mengine

·         Waefeso 4:11-14 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.”

 

·          Matendo 2:46-47 “Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe, wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.”

 

·         Matendo 1:8 “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”

 

·         Matendo 8:4 “Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno.”

KUKUA KIROHO

Kukua Kiroho ndio msingi wa kukua kwa namna nyinginezo zinazobakia, njia  ya ukuaji wa kiroho ambayo Bwana Yesu ametuachia ni pamoja na Roho Mtakatifu na watumishi wenye wito maalumu ambao wanaoitwa na Bwana kwa kusudi la kulikamilisha kanisa Matendo 1;8,Efeso 4;1-16 kwa msingi huo Kujumuika na wengine pia ni njia ya kukua Kiroho. Washirika wasokua kiroho ni tatizo kubwa sana katika kusababisha uamsho utokee, lazima kila mmoja aiskubali kudumaa akubali kukua kiroho kufikia hatua ambayo Mungu ameikusudia,

Waebrania 5:11-14 “Ambaye tuna maneno mengi ya kunena katika habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa kusikia. Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu. Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga. Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.”

KUKUA KIIDADI

Kukua kiidadi ni moja ya njia ya kuonyesha uhai wa kanisa hata hivyo yako mambo yawezayo kuchangia ukuaji wa kanisa hasa unapoangalia hali halisi ya ukuaji wakati wa Kanisa la kwanza Kanisa lilikuwa kwa namna ya kupita kawaida lakini moja au baadhi ya mambo yaliyochangia ukuaji ni pamoja na Miujiza na Ushirika Biblia inatoa mwanga unaochangia katika ukuaji wa kanisa kuwa ni pamoja na Kuhubiriwa kwa injili, kumruhusu Bwana afanye kazi pamoja nao na kuthibitishwa kwa neno kupitia Ishara na miujiza Marko 16:20, “Kisha wanafunzi Wake wakatoka, wakahubiri kila mahali, naye Bwana akatenda kazi pamoja nao na kulithibitisha neno Lake kwa ishara zilizofuatana nalo.” Mambo mengine yaliyochangia katika ukuaji wa kanisa yako wazi katika kitabu cha matendo ya mitume kiidadi.

 

MATENDO

TUKIO AU MATUKIO

MATOKEO

2:1-41

Pentecoste, Kujazwa Roho, Kunena kwa lugha, Mahubiri.

a

2:42-47

Mafundisho, Ushirika, maombi, Miujiza, Umoja, Kuabudu,  Kuwapendeza watu wote

b

4:4

Kuponywa kwa mtu aliyepooza na mahubiri

c

5:12-16

miujiza, *kumbuka inawavuta wengi wasioamini na ni chambo chambo

d

5:42-6:1-7

Mafundisho na kushuhudia Hekaluni na nyumba kwa nyumba.

e

9:31

Wakati wa amani, Kuishi kwa ajili ya Kristo na kutiwa moyo kwa Roho Mtakatifu

f

14:1

Kuhubiri kwa ujasiri katika masinagogi

g

16:4-5

Kukataa mafundisho ya sheria,kutembelea makanisa na kutoa msaada Kiroho

h

17:10-12

Kuhubiri huko Beroya na kuyachunguza maandiko

i

19:8-20

Kuhubiri na kufundisha na miujiza ya kila siku

j

 

Kwa hiyo utaweza kuona kuwa kanisa la kwanza lilianza na idadi ya watu 120 na likakua na kuongezeka toka siku ya Pentekoste kwa kufikia 3000 na baadaye 5000 na baadaye watu waliendelea kuongezeka kiasi ambacho Mwandishi wa kitabu cha matendo yaani Luka  anaeleza kuwa idadi ya watu wanaume kwa wanawake wakaongezeka kwa Bwana Matendo 5;14 inasema “Lakini walioamini wengi wakaongezeka kwa Bwana, idadi kubwa ya wanaume na wanawake” Kwa msingi huo kuongezeka kiidadi ni mpango wa Mungu na tunapaswa kuuwaza na kuufanyia kazi aidha ni muhimu kuweka Rekodi ya idadi ya watu kanisa la kwanza walijuaje kuwa kanisa linaongezeka hii iko wazi kuwa walikuwa wakiwahesabu kila wakati chukua idadi ya washirika wanaohudhuria. Kwa msingi huo katika kanisa atakuwepo mtunza takwimu mwenye kuangalia kama idadi ya washirika inakuwa au kupungua na kutunza kumbukumbu hizo.

KUKUA KIJIOGRAFIA

Huku ni kukua kutoka eneo moja kuelekea eneo lingine Ni muhimu kufahamu kuwa kanisa la kwanza pia walikuwa kijiografia ingawa kutawanyika kwao mwanzoni ilikuwa kwa ajili ya mateso lakini waamini waliotawanyika walikuwa kama mbegu zilizokufa na kuzaa matunda, aidha agizo kuu pia liko kijiografia Matendo 28; 18-28 Marko 16; 15 Matendo 1; 8 Kwa hiyo Yesu alikuwa na mpango wa kijiografia wa kuifikisha injili ulimwenguni kuanzia Yesrusalem, Uyahudi, Samaria, na hata mwisho wa nchi

Umuhimu wa kukua kijiografia

Kukua kijiografia ndio kiini cha somo hili kwa ufupi ndio kupanda makanisa, kupanda makanisa ni njia nzuri ya Kufanya uinjilisti iliyo bora zaidi kuliko zote Mchungaji ukiona kanisa lililo komaa lina kusumbua unaweza kulikabidhi kwa wachungaji wengine na ukaamua kupanda kanisa jipya utajisikia Raha ya ajabu sana na utafurahia aina hii ya uinjilisti kuna usemi usemao “NI RAHISI KUWA NA MTOTO KULIKO KUFUFUA MFU” hapa simaanishi kuwa kanisa lililo kwisha anzishwa ni mfu hapana lakini hapa nazungumzia kushughulikia na kanisa lililo na udumavu wa kiroho ni kazi ngumu kuliko kuanzisha kanisa jipya

Kwa nini ni muhimu kupanda makanisa

1.       Kupanda kanisa ni mpango wa Mungu wa Kibiblia na ni mpango wa Mungu sawa na Matendo 1;8

2.       Kupanda kanisa ni njia ya kuzalisha Viongozi wapya wa kanisa

3.       Kupanda makanisa ni njia ya kuleta Uamsho kwa makanisa ya zamani mara nyingi tunajua kuwa makanisa yaliyotangulia huwa na tabia ya kujisahau na hivyo linapoanzishwa kanisa jipya tayari hofu huwapata wale waliotangulia na hivyo Mungu hufurahia sana huko mbinguni kwani ni changamoto kwa kazi na ufalme wa Mungu unajengeka

4.       Kupanda kanisa ni kuzuri kwani kunakusaidia kulifikia eneo jipya ambalo halijafikiwa na injili Paulo mtume alisema hamu yake na shauku ni kuipeleka injili kule ambako Kristo hajasikika Warumi 15:20kadhalika nikijitahidi kuihubiri Injili, nisihubiri hapo ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine;”       

5.       Kupanda makanisa kunaimarisha Dhehebu lako si kwamba kupanda kanisa kwa kweli kwa undani kunaimarisha mwili wa Kristo tu lakini dhehebu lako unalofanya kazi pamoja nalo linaimarika kwa kueneza injili na kufikia maeneo yasiyo fikiwa.

Maadui wakuu wa upandaji wa makanisa

a.       Wakristo wa mwilini

Tunapozungumzia wakristo wa mwilini tunazungumzia jamii ya watu ambao aidha walimwamini Yesu na kuipokea badiliko la kiroho na kuwa na uwezo wa kushinda dhambi lakini baadaye wakapoa na wakabaki na jina tu kuwa ni wakristo lakini wamekufa

 

Ufunuo 3;1“Haya ndiyo maneno Yake Yeye aliye na zile Roho saba za Mungu na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, kwamba una sifa ya kuwa hai, lakini umekufa.” Pia ni jamii ya wakristo wanaoishi maisha vuguvugu

 

Ufunuo 4;14-16 “Haya ndiyo maneno Yake Yeye aliye Amen, shahidi mwaminifu na wa kweli, mtawala wa uumbaji wote wa Mungu. Nayajua matendo yako, ya kwamba wewe si baridi wala si moto. Afadhali ungelikuwa baridi au moto. Hivyo kwa kuwa u uvuguvugu, kwamba wewe si baridi wala si moto, nitakutapika utoke kinywani Mwangu.”

 

Hawa ni wakristo wa majina tu na sio wakristo halisi pia wanaweza kuwa wakristo waliozaliwa katika dini za Kikristo na hivyo wanaishi maisha ya kawaida sana hawa wanakuwa kizuizi katika kupanda makanisa kwa vipi?

 

*      Hawawezi kuubeba injili na kuwapelekea wale ambao bado hawajafikiwa na injili Warumi 10;14-15  Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!”      

 

*      Kanisa linakuwa na Jeshi dhaifu wakati Ufalme wa Mungu unatekwa na wenye nguvu yaani watu wenye wivu wa kimapinduzi kwa ajili ya Mungu Mathayo 11:12 “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.”

 

*      Kanisa linakuwa na watu wasioweza kuzaa matunda kwani wako nje ya mizabibu Yohana 15;5Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.”     

 

*      Kanisa linaweza kuwa na watumishi wasio na wito au kuwapa uongozi watu wasio wakristo, ndoa zisizoeleweka, na kuweza kupata makanisa mbali sana  na watu kukosa sehemu za kuabudu

 

*      Wakristo wanaogombana wenyewe kwa wenyewe 1Wakorintho 3:1-3 “Lakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo. Naliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula; kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi, kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?

       

b.      Chanzo cha wakristo wa mwilini Kuweko

·         Kukosekana kwa maombi

·         Kuanza kuchukuliana na dunia

·         Ubinafsi katika kutoa

·         Kuhubiri dini zaidi kuliko injili

·         Kushindwa kuwafikia wanafunzi kuanzia shule za msingi mpaka vyuo vya Biblia

·         Kukosa Viongozi wazuri wa kiroho

·         Wakristo wasio na matunda ya Roho Mtakatifu, wamedumaa, wanamafarakano, washabiki wa wahubiri, hawatambui uwepo wa kara tofauti tofauti.

 

c.       Uongozi Mbaya

 

Ni muhimu kufahamu kuwa aina za Viongozi tunaowaandaa inaweza kuleta mafanikio makubwa au kutofanikiwa kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa kanisa na upandaji wa makanisa,Yesu alichukua Muda wa kutosha kuandaa Viongozi, mwanzoni hakulenga tu kujikusanyia maelfu ya watu lakini alikaa na wachache ili kuwapandikizia kusudi la Baba yake  na kisha kupitia wao kanisa lilikuwa na kuongezeka Viongozi hufananishwa na Nguzo Wagalatia 2:6-9. “Lakini wale wenye sifa ya kuwa wana cheo; (walivyokuwa vyo vyote ni mamoja kwangu; Mungu hapokei uso wa mwanadamu); nasema, hao wenye sifa hawakuniongezea kitu; bali, kinyume cha hayo, walipoona ya kuwa nimekabidhiwa injili ya wasiotahiriwa, kama vile Petro ya waliotahiriwa; (maana yeye aliyemwezesha Petro kuwa mtume wa waliotahiriwa ndiye aliyeniwezesha mimi kwenda kwa Mataifa); tena walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa; Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;”  utafiti unaonyesha kuwa moja ya matatizo makubwa ya kutokukua kwa makanisa mengi ni Viongozi, viongozi wasio na utii, viongozi wanaotaka kusikilizwa wao, viongozi ambao hawana maono, hawashirikiani na Mchungaji, wanaompiga vita mchungaji na kuwacha kuangalia ni nini mapenzi ya Mungu kwa watu wake na kanisa lake na wajibu wa kanisa duniani,

 

d.      Kukosa majibu ya matatizo ya watu na mahitaji yao

 

Kanisa linalokua ni lile ambalo matatizo ya watu hupata ufumbuzi,kama kanisa haliwezi kukutana na mahitaji ya watu basi halitimizi wito wake kwa ukamilifu chunguza duniani ukaone Popote duniani mahali kanisa limekua ni pale ambapo watu hupokea majibu ya mahitaji yao hii ndio huchangia wakati mwingine kuwa hata imani potofu zenye majibu ya matatizo ya watu watu hujikusanya huko ni muhimu kuwa na kanisa ambalo Mwenye dhambi anapokea Msamaha, wenye kiu wanakunywa, wenye njaa ya roho wanajazwa, wenye magonjwa wanapona, walioteswa na ibilisi wanafunguliwa asiye na matumaini anapokea matumaini watu wanatiwa moyo na wanautazamia uzima wa milele.

 

e.      Kukosekana kwa maombi endelevu

Maombi endelevu yanapokuweko katika kanisa ni lazima kanisa litakua na kufunikwa na furaha ya kimungu watu wanapokusanyika kwa ajili ya Mungu na kuomba Mungu huwa katikati yao na Mungu humwaga Roho ya furaha kwa kujibu maombi na kushughulikia na mahitaji ya watu na watu wanapotoka na furaha  watu huvutiwa kuwako mahali penye furaha, shetani hakimbii watu wanapohubiri au wanaposhiriki meza ya bwana yeye hukimbia watu wanapoomba maombi yana nguvu kubwa ya kulifanya kanisa kusimamia na kukua na kuongezeka

 

f.         Kushindwa kuwaachilia watu wa kawaida kwenda kuanzisha kazi mpya

 

Kama watumishi Viongozi wa makanisa wanataka makanisa yao yakuwe ni lazima wakubali kuwaachia watu wa kawaida kutoka na kuanzisha kazi mpya lakini ni muhimu pia kanisa likiwaandaa kwa kazi hizo kama kanisa halina muundo unaoruhusu watu kumtumikia Mungu basi hata kama kuna watu wenye kiu ya kufanya hivyo hawawezi kufanya hivyo wachungaji wanao wajibu wa kuwafundisha na kuwatia moyo watu wa kawaida na kuwatuma katika huduma hata kama wakati mwingine watu hao ni muhimu katika kanisa mama unapoacha ubinafsi na kujaribu kulifanyia kazi hili kanisa litakua kwanini kanisa lisikue kwa mtu wa aina hii.

 

g.       Kukosekana kwa maono  

 

Makanisa mengi yasiyokuwa ni yale yenye Viongozi wabinafsi na wasio na maono ya kiulimwengu wao hujitazama wenyewe tu jambo hili linaweza kupelekea watu kujichokea kanisa lazima liwe na maono ya kupeleka injili kila mahali kusikofikiwa, lazima liwaombee watu hao na kuwawezesha kanisa linapofanya haya haliwezi kuzeeka bali linakuwa kijana,zuri na lenye nguvu kinyume cha hapo linakomaa na mazoea huchukua nafasi na kunakua hakuna jipya

 

h.      Kukosa kiongozi mwenye uwezo mkubwa wa kimaongozi

 

Mchungaji anatakiwa kuwa mtu mwenye maono makubwa imani na uwezo mkubwa wa kuongoza akiwa amejaa maombi, asiyekata tamaa, mwenye uwezo wa kupokea maono toka kwa Mungu na kuongoza watu, Kama katika kanisa lako hakuna mtu anaweza kufanya lolote mpaka kwa ruhusa ya Mchungaji fahamu kabisa kanisa hilo haliwezi kukua lakini lazima Kuweko na umoja yanapokuja maono kama ni kwa Mchungaji Viongozi wakiyaunga mkono kwa kauli moja  kunakuwa na nguvu kubwa na kazi itafanikiwa, Kama uongozi wa Mchungaji ni dhaifu kanisa lote linakuwa dhaifu Mchungaji akiwa na uwezo mkubwa wa kuubeba maono basi washirika watayapokea kwa nguvu na kumuunga mkono na kumtia moyo,makanisa mengi hayakui kwa sababu tu hayana Viongozi wenye uwezo wa kubeba Jukumu kubwa la kimaongozi

SIFA ZA MTU MWENYE KUANZISHA KANISA                                                       

Kanisa linaweza kuanzishwa na mtu Yeyote 

Kanisa linaweza kuanzishwa na mtu wa aina yoyote anaweza kuwa Mmisheni, Mwinjilisti, Mchungaji, mtume au nabii au mtu yeyote wa kawaida ambaye katika mpango wa Mungu amepata nafasi ya kufanya hivyo lengo likiwa ni kumpanda Kristo katika jamii ya watu wasiomfahamu na kuanzisha ushirika wa mahali pamoja kwa msingi huo kupenda kanisa hakuhitaji mtu fulani maalumu sana au mwenye sifa ambazo ni za hali ya juu sana Nyakati za kanisa la kwanza makanisa mengine mengi yalianzishwa na watu wa kawaida tu Matendo 8;4 “Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno  kwa msingi huo hatupaswi kuogopa kuanzisha makanisa unahitaji imani tu  je unafikiri mtu anayepaswa kuanzisha kanisa anatakiwa kuwa wa namna gani?

·         Hakuna sifa maalumu za mtu anayepaswa kuanzisha kanisa Mungu hutumia watu wa kawaida tu

·         Mtu anaye anzisha kanisa anapaswa tu kuwa mtu anayekubalika na watu wale anaotaka kuwafikia katika jamii na Elimu yao

·         Awe ni mtu mwenye haiba ya kuingiliana na watu wapya na kuwavutia kwa muda mfupi tu na kuweza kuzungumza na watu wa kila aina na kila ngazi, Mtu anayejificha, na kujitenga na watu na kutokusikia raha kuhusu watu hasa wageni hawezi kufanikiwa katika kuifanya kazi hii

·         Awe  ni mtu anayejali sana watu na kuwajibika kwa ndani sana kuhusu matatizo yao  ya binafsi watu na jamii

·         Lazima awe mtu wa Mungu yaani aliyeokolewa ingawa si lazima awe na ujuzi sana au aliyeenda chuo.

·         Lazima awe anasukumwa na upendo wa ndani sana wa kimungu kwa ajili ya watu wanaopotea  sawa na Mchungaji anayetafuta kondoo aliyepotea Luka 15;3-7

·         Awe mtu wa maombi Wakolosai 1;9-11,2;1-3,Efeso 3;14-19 1Wathesalonike 1;2-3 Mathayo 9;39 Yesu alisema Ombeni ili Bwana wa mavuno atume watenda kazi katika shamba lake

·         Anatakiwa kuwa mtu wa maono na mbunifu huku akiwa na mvumilivu na mtu asiyeweza kukata tamaa akiwa mtu wa imani kwamba anachokifanya ni mpango wa Mungu na kuwa Mungu amemtuma kuifanya kazi hii.

Jinsi ya kuanzisha kanisa

Ni muhimu kufahamu kuwa hakuna njia maalumu ya kuanzisha kanisa uongozi wote wa namna ya kuanzisha kanisa unaachwa kwa Roho Mtakatifu, njia iliyotumika eneo fulani inaweza isifanya kazi katika eneo lingine kwa msingi huo tunaweza kujifunza tu kutoka katika uzoefu wa namna watu wengine walivyotumiwa na Mungu katika kuanza makanisa na mafanikio waliyoyapata kutokana na njia walizozitumia wakawapata watu waliookolewa na makanisa yakakua, tunajua kuwa kuna shuhuda nyingi sana kuwa kuanzisha kanisa ni kazi ngumu lakini kumbuka kuwa Roho wa Mungu ndiye anayefanya kazi na mtu anaye anzisha kanisa njia hizi hutumika katika kuanzishwa kwa makanisa.

·         Kuanzishwa kanisa kupitia Mikutano ya injili na baadaye kuwa na mpango wa namna ya kuwatunza wale waliookolewa na kuwalisha Neno, Kumbuka kuwa kuhubiri pakee hakutoshi ni lazima kuhubiri injili kuambatane na Kuweko kwa mipango ya malezi ya watu wanaookolewa

·         Kuanzishwa kupitia ushuhudiaji wa mtu kwa mtu  hii ni njia yenye matokeo makubwa sana kuliko hata mkutano wa injili katika maeneo mengine na imeleta matokeo mazuri na mahusiano mazuri yanayoweza kufungua njia ya kufanya ufuatiliaji kwa waongofu wapya

·         Kanisa mama kugawa watu na kuanzisha tawi lingine kwa amani hii nayo ni njia inayoweza kutumika katika kuanzisha kanisa jipya na kuyafikia maeneo yasiyofikiwa inawezekana tu kwa wachungaji wasiojali maslahi yao Binafsi.

·         Kuna njia nyingine yoyote inayoweza kufaa katika uanzishaji wa kanisa basi inaweza kutumiwa katika kuanzisha kanisa

Mambo ya kuzingatia wakati wa kupanda kanisa

1.       Hakikisha unafanya uchunguzi wa eneo unalotaka kuanzisha kanisa (Survey).

Kufanya survey ni jambo la msingi sana na la kibiblia kabisa wote tunakumbuka kuwa wakati Mungu alipokuwa anataka kuwarithisha wana wa israel nchi ya kanaani alimwamuru Musa kuwatuma watu 12 wapelelezi ili kuipeleleza nchi maana yake ni kufanya uchunguzi kuwa nchi ile ni ya namna gani

 

Hesabu 13; 1-21.BWANA akamwambia Musa, Watume baadhi ya watu wakaipeleleze nchi ya Kanaani,ambayo ninawapa Waisraeli. Kutoka katika kila kabila la baba zao tuma mmoja wa viongozi wao.’’ Hivyo kwa agizo la BWANA Musa akawatuma kutoka Jangwa la Parani. Wote walikuwa viongozi wa Waisraeli. Haya ndiyo majinayao: Kutoka kabila la Reubeni, Shamua mwana wa Zakuri, kutoka kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori, kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune, kutoka kabila la Isakari, Igali mwana wa Yosefu, kutoka kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni, kutoka kabila la Benyamini, Palti mwana wa Rafu, kutoka kabila la Zabuloni, Gadieli mwana wa Sodi, kutoka kabila la Manase (kabila la Yosefu), Gadi mwana wa Susi, kutoka kabila la Dani, Amieli mwana wa Gemali, kutoka kabila la Asheri, Sethuri mwana wa Mikaeli, kutoka kabila la Naftali, Nabi mwana wa Wofsi, kutoka kabila la Gadi, Geueli mwana wa Maki. Haya ndiyo majina ya watu ambao Musa aliwatuma kuipeleleza nchi. Mose akampa Hoshea mwana wa Nuni jina la Yoshua.”

Musa alipowatuma wakaipeleleze Kanaani, alisema, ‘‘Pandeni kupitia Negebu, mwende mpaka nchi ya vilima. Mwuone nchi ni ya namna gani na kama watu waishio humo wana nguvu au dhaifu, iwapo ni wachache au wengi. Kwamba wanaishi katika nchi ya namna gani? Je, ni nzuri au mbaya? Wanaishi katika miji ya namna gani? Je, haina kuta au ngome? Ardhi ikoje? Ina rutuba au la? Je, kuna miti ndani yake au la? Jitahidini kadri mwezavyo kuleta baadhi ya matunda ya nchi.’’ (Ulikuwa msimu wa kuiva zabibu za kwanza.) Hivyo wakapanda na kuipeleleza nchi kutoka Jangwa la Sini hadi Rehobu, kuelekea Lebo Hamathi”.

 Maswala ya kuyachunguza katika jamii unayokwenda kupanda kanisa

·         Peleleza mfumo wa jamii yao jinsi ulivyo

·         Chunguza vikwazo vya kiroho vilivyoko katika eneo husika

·         Chunguza sheria zao na mila na tamaduni zao

·         Mahusiano ya kifamilia katika jamii

·         Dini na madhehebu yaliyoko hapo

·         Viwango vyao vya maadili aina ya watu, uchumi wao Lugha zao,tamaduni zao


2.       Hakikisha unaanza na eneo ambalo linapokea injili kwa urahisi (Receptive Areas)

 

Jambo la msingi katika kupenda makanisa baada ya kuwa umefanya Survey chunguza ni wapi mavuno yako tayari kisha anzia huko ndege kubwa huanguka na kuvunjika kunapokuwa na wing uzito au ukungu unaomfanya Pilot asione vizuri na wakati mwingine ndege inaweza kupata ugumu wa kutua na kugonga milima  kwa sababu ya kutokuona vizuri  hii ni kwa sababu ya kushindwa kuona vizuri, hali kama hii huweza kutokea wakati wa kupenda kanisa  Mungu anapokutuima katika eneo fulani  atakuongoza kule ambako kuna upenyo wa watu kuipokea injili wakati mwingine atakuongoza kwa Roho wake  na wakati mwingine atakuongoza kupitia kutazama vema Matendo 10;1-23 Yohana 4;30-35 kwa msingi huo ni muhimu kugundua maeneo ambayo injili inapokelwa kwa uarahisi na kuyafikia kwanza  ili utaligundua kwa upokeaji wao wa injili na mwitiko mkubwa wanaoonyesha kwa ujumbe wa injili

 

3.       Hakikisha kuwa unayafikia makundi yote

 

Mpango wa Mungu ni kuwafikia watu wote  kwani kwa Mungu watu wote ni sawa ,Yeye hushughulika na watu wote na mahitaji yao na matatizo yao kwa viwango vyovyote walivyo navyo awe masikini au tajiri,msomi au mjinga  kwea msingi huo Mungu hana upendeleo kwa hiyo zingatia kuyafikia makundi yote kosa moja lifanywalo na watumishi wengi sana ni kulenga kundi fulani na kuacha kundi jingine huu sio mpango wa Mungu fikia Masikini, wafanya biashara, matajiri, wanasiasa,Viongozi, vibarua ,wasio na kazi usipendelee kundi fulani kwa ajili ya mafungu Ubaguzi ni dhambi Yakobo 2;1-9

 

4.       Panda kanisa linalojitegemea (the Indigenous churches)

 

Moja ya matatizo yanayoyapata makanisa mengi na kuathiri ukuaji wa makanisa hayo ni kutegemea msaada hii ni sumu mbaya sana mchungaji au mpandaji wa kanisa lazima ahakikishe kuwa kwa kadiri inavyowezekana anapanda kanisa linalojitegemea na kujiendesha  na kujiongoza na kujieneza  na kujitafasiria Maandiko sawa na mazingira yake kanisa la namna hii lipande kila mahali ambako injili hupokelewa kirahisi, sio dhambi kutegemezwa kwa sababu ni mpango wa Mungu pia lakini msingi mzuri ni kutokutegemea watu bali kumtegemea Mungu jambo la namna hii litakusaidia katika kuhakikisha unakuwa na kanisa lenye ufahamu wa kutosha na linaloweza kuwa na faida kubwa katika ufalme wa Mungu kwa kazi za baadaye




 

 


Ufunguo wa kanisa linalotaka kukua lazima uwe Kanisa linalojitegemea Self suppoting church, kanisa linalojiongoza Self governing, Kanisa linalojieneza self propagating linalojaa roho na kujitafasiria Maandiko kulingana na mazingira yake.

 

5.       Hakikisha kuwa unaweka msingi mzito wa muhimu kwa kanisa jipya

 

Mtu anayeanzisha kanisa anapaswa kuahakikisha kuwa anajenga msingi imara kwa kanisa analolianzisha  msingi huo ni mafundisho mazuri na sahii kwa, Mwanzilishi wa kanisa ni kama mjenzi na kwa msingi huo anapashwa kujenga msingi imara katika kanisa analolianzisha kwa faida ya umaliziaji wa baadaye  na ili kanisa liweze kuwa na msingi wa kukua lazima lifundishwe majukumu ya kila mkristo na Baraka za kutimiza majukumu hayo na waelekeze kazi na wajibu wa kanisa kwa Mungu kwa kanisa lenyewe na kwa jamii inayolizunguka kanisa yaani kuabudu, ushirika na kuwafgikia wasiofikiwa.

 

6.       Hakikisha kuwa unapanda kanisa lenye nidhamu

 

Kanisa linalopandwa lazima liwe kanisa linaloweka msingi wa nidhamu mbele na pia kutowaaacha wale walioanguka katika neema ya Mungu bila kuwarejesha katika ushirika na utumishi, Mungu anachukizwa na wachungaji wasiojali kondoo Soma Ezekieli 34, Wagalatia 6;1-2 Mithali 24;16, Mika 7;8 1Thesalonike 5;14 Isaya 35;3 na Waebrania 12;13 Lengo likiwa kurekebisha, kurudisha kutunza ushuhuda na kuwaonya wengine Mungu atakupa Hekima ya kushughulikia na matatizo hayo kwa njia mbalimbali. Aidha tujihadhari kutenga watu kwa jazba na chuki, hakikisha unamsaidia mtu mpaka kwenye kilele cha ubora wa ugfuatiliaji usikubali kupoteza mtu kirahisi, Yesu hakupoteza hata mmoja aliwalinda wote wale ambao amepewa na Mungu, Yohana 17:12 “Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.”

 

Na. Rev Innocent Samuel Kamote

 

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Hakuna maoni: