Mathayo 3:11-12 “Kweli mimi nawabatiza kwa
maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala
sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na
kwa moto. Ambaye pepeto lake li mkononi
mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani,
bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.”
Utangulizi:
Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni
uzoefu wa kiroho unaotokea kwa mtu aliyeokoka kumuwezesha mtu huyo kupokea
uwepo wa Roho Mtakatifu unaoambatana na nguvu za Mungu na ujasiri unaomuwezesha
mtu huyo kuzungumza neno la Mungu kwa ujasiri, huku akithibitishwa na kunena
kwa lugha pamoja na kupokea vipawa na karama nyinginezo, Ubatizo wa Roho
Mtakatifu umetajwa kwa mara ya kwanza na Yohana mbatizaji katika vitabu vya
injili.
Mathayo 3:11-12 “Kweli mimi nawabatiza kwa
maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala
sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na
kwa moto. Ambaye pepeto lake li mkononi
mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani,
bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.”
Marko 1:7-8 “Akahubiri akisema, Yuaja nyuma
yangu aliye na nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuinama na kuilegeza
gidamu ya viatu vyake. Mimi niliwabatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa
Roho Mtakatifu.”
Luka 3:16-17 “Yohana alijibu akawaambia
wote, Kweli mimi nawabatiza kwa maji; lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko
mimi, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya viatu vyake; yeye atawabatiza
kwa Roho Mtakatifu na kwa moto; ambaye pepeo lake li mkononi mwake, naye
atausafisha sana uwanda wake, na kuikusanya ngano ghalani mwake, bali makapi
atayateketeza kwa moto usiozimika.”
Madhehebu mbalimbali ya Kikristo
yanatafasiri ubatizo wa Roho Mtakatifu katika mitazamo tofauti tofauti
kulingana na elimu zao za kitheolojia (Experimental
Theology)
1. Wapentekoste
na wanacharismatic - kuwa ubatizo huu unatokea kwa mtu aliyeokoka yaani aliyemuamini
Bwana Yesu na kumkubali kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake na, kufuatiwa na
kupokea uwepo na nguvu za Roho Mtakatifu ambazo kimsingi zinathibitishwa na
kunena kwa lugha mpya hii ndio alama ya kwanza inayothibitisha uwepo wa Roho wa
Mungu ndani ya mtu na umuhimu wa kuishi maisha yenye nguvu za Roho Mtakatifu na
kupelekea kuwa bora katika nia zetu za kuabudu na kumtumukia Mungu.
2. Madhehebu
ya kiinjili na kiprotestant - wao
wanaamini kuwa ubatizo huu unatokea mara tu mtu anapokuwa amempokea Yesu, mara
mtu anapompokea Yesu, wanaamini kuwa ni kazi ya Roho Mtakatifu kusababisha
kuzaliwa upya kwa mtu huyo na hivyo anakaa ndani yake na hawaamini kuwa wokovu
na uwepo wa Roho au Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni vitu vinaweza kutenganishwa.
3. Wakatoliki
na waanglikana wa High Church wanaamini
kumpokea Roho Mtakatifu tu ni tukio la kisakrament (Kipaimara), wao wanaona
kuwa uwepo wa Roho Mtakatifu ni tukio endelevu la maisha ya kila siku na tukio la
kukua na kukomaa katika utakatifu na huduma.
Kibiblia ubatizo huu wa Roho
Mtakatifu ni moja ya ahadi Muhimu sana aliyoiahidi Mungu baba na Bwana wetu
Yesu Kristo, ambapo wanafunzi wa Yesu Kristo walipaswa kusubiri kwanza pale
Yerusalem mpaka wavikwe uwezo huu kutoka mbinguni.
Luka 24:49 “Na tazama, nawaletea juu yenu
ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.”
Matendo 1:4-5, 8 “Hata alipokuwa amekutana
nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo
mlisikia habari zake kwangu; ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi
mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache.8 Lakini mtapokea
nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu
katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”
Kwa hiyo unaweza kuona kuwa ni
ubatizo wa ahadi kimaandiko na ni tukio ambalo Yesu aliwaelekeza wanafunzi wake
kulisubiria na Yesu alilitofautisha na wokovu pamoja na ubatizo wa maji, na wanafunzi wa Yesu walisubiria ahadi hii na walijazwa au walibatizwa kwa Roho Mtakatifu na kuanza kusema kwa lugha
nyingine.
Matendo 2:1-4 “Hata ilipotimia siku ya
Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi
kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa
wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia
kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha
nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.”
Haikuishia hapo tu kwani baadaye
tunawaona wanafunzi wakiwa na mabadiliko makubwa sana wakiwa pia na karama na
vipawa mbalimbali na wakimtumikia Mungu kwa nguvu na ujasiri mwingi pia wakiwa
moto sana kuanzia Matendo 3 na kuendelea, jambo lililopelekea watu wengi
kuokoka na kukua kwa kanisa na uhai wa kanisa unaoendelea mpaka leo.
Kwa msingi huo basi leo
tutachukua Muda kujifunza kwa kina na mapana na marefu kuhusu Ubatizo wa Roho
Mtakatifu kwa kuzingatia vipengele muhimu vitatu vifuatavyo:-
·
Maana ya ubatizo wa Roho Mtakatifu.
·
Mtu aliyebatizwa kwa Roho Mtakatifu.
·
Jinsi ya kupokea Ubatizo wa Roho Mtakatifu.
Maana ya ubatizo wa Roho Mtakatifu;
Maandiko yanatufundisha ya kuwa
kila mtu aliyeokolewa anakuwa na Roho Mtakatifu ndani yake, hii ni kwa sababu
tukio zima la mtu kumkiri Yesu na kumpokea kama bwana na mwokozi kupitia kazi
aliyoifanya Msalabani ni tukio linalosababishwa na Roho Mtakatifu, kwa hiyo
kuzaliwa mara ya pili ni kuzaliwa kwa roho na kuungwa katika mwili wa Kristo,
kwa Msingi huo basi ni muhimu kufahamu kuwa, Ndani ya kila mtu aliyeokolewa
Roho wa Mungu yupo na hivyo kila aaminiye amefanyika kuwa mali ya Mungu.
Yohana 16:7-11 “Lakini mimi nawaambia iliyo
kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi
hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. Naye akiisha kuja,
huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu. Kwa
habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi; kwa habari ya haki, kwa sababu
mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena; kwa habari ya hukumu, kwa sababu
yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.”
Warumi 8:9 “Lakini ikiwa Roho wa Mungu
anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu
awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.”
Wagalatia 4:5-6 “Na kwa kuwa ninyi mmekuwa
wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba.
Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u
mrithi kwa Mungu.”
Wakati huu Roho Mtakatifu
atafanya kazi na mwamini katika kiwango tofauti tofauti kwa kadiri ya neema ya
Mungu ndani ya waamini, viwango hivi ni sawa na ngazi za ujazo wa maji kutoka
kiwango kimoja hadi kiwango kingine, viwango hivyo vinachangiwa na utii,
kujitoa, maombi, kufunga na maisha kwa ujumla ambapo kila mmoja anakuwa na
kiwango chake viwango hivi tunaweza kuelezea vizuri kwa kutumia maono ya mfano
wa nabii Ezekiel.
Ezekiel 47:1-5 “Baadaye akanileta tena
mpaka lango la nyumba; na tazama, maji yalitoka chini ya kizingiti cha nyumba,
kwa njia ya mashariki, maana upande wa mbele wa nyumba ulielekea upande wa
mashariki; nayo maji yakashuka toka chini ya upande wa kuume wa nyumba, upande
wa kusini wa madhabahu. Ndipo akanileta nje kwa njia ya lango upande wa
kaskazini, akanizungusha kwa njia ya nje mpaka lango la nje, kwa njia yake
iliyoelekea mashariki; na tazama, maji yalitoka upande wa kuume. Na alipotoka
mtu yule, mwenye uzi wa kupimia mkononi mwake, kwenda masharikini, akapima
dhiraa elfu, akanivusha maji yale; maji yakafika mpaka viweko vya miguu. Kisha
akapima dhiraa elfu, akanivusha maji yale, maji yakafika mpaka magoti. Kisha
akapima dhiraa elfu, akanivusha, maji yakafika mpaka viuno. Kisha akapima
dhiraa elfu, yakawa mto nisioweza kuuvuka; maana maji yamezidi, maji ya
kuogelea, mto usiovukika.”
Ezekiel Katika maono haya
anajaribu kuelezea kiwango au viwango mbalimbali vya ujazo wa Roho Mtakatifu
kutofautisha na ubatizo wa Roho Mtakatifu, viwango hivyo vinategemeana na
ukuaji wa kila mwamini kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine, na kila mwamini
anaweza kuongezea kiwango chake yeye mwenyewe kwa kujitoa kwa Mungu kwa hiyo
uko uhusiano wa ukuaji wa kiroho na ujazo wa Roho Mtakatifu, mfano ni kutoka
maji ya kiwango cha viwiko vya miguu, kisha maji ya magotini, kisha maji ya
kiunoni, kisha mto usioweza kuvukika
Ezekiel alikuwa anazungumzia ukuaji wa kiroho wa muumini na uhusiano
wake na ujazo wa Roho Mtakatifu, kwa hiyo mtu anaweza kuwa na Roho Mtakatifu
tangu alipookoka kwa sehemu, lakini akawa hajajazwa au hajabatizwa katika
kiwango cha kufurika ambacho ndio kinaitwa Ubatizo. Mtu anayebatizwa kwa Roho
Mtakatifu ni mtu mwingine ni mtu wa tofauti sana ni mtu wa viwango vya juu sana
, ni mtu ambaye uungu unakaa ndani yake kama tutakavyoona.
Wanafunzi wa Yesu walikuwa na
kiwango cha uwepo wa Roho Mtakatifu wakati wakiwa na Yesu Kristo, kwa hiyo yako
mambo waliweza kuyafanya, lakini katika kiwango cha chini na cha kawaida mfano
kutoa Pepo, kufunuliwa kumjua Yesu, kusikiliza mafundisho yake na kadhalika
walimpokea Roho Mtakatifu kwa sehemu, kwa hiyo walifanya kazi mbalimbali za
Mungu kwa kiwango hicho.
Yohana 20:21-22 “Basi Yesu akawaambia tena,
Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. Naye
akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.”
Luka 9:1-2 “Akawaita wale Thenashara,
akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi. Akawatuma
wautangaze ufalme wa Mungu, na kupoza wagonjwa.”
Luka 10:1,17-19 “1.Basi, baada ya hayo
Bwana aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda
kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe.” 17-19 “Ndipo wale sabini
waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako.
Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme. Tazama,
nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala
hakuna kitu kitakachowadhuru.”
Mathayo 16:15-17 “Akawaambia, Nanyi
mwaninena mimi kuwa ni nani? Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo,
Mwana wa Mungu aliye hai. Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona;
kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni”
Kwa hiyo utaweza kuona kuwa
wanafunzi wa Yesu walipokea Roho Mtakatifu wakati wakiwa na Yesu, walitumwa
kuhubiri, walitoa pepo, walitetemesha utawala wa shetani, waliweza pia kupokea
mafunuo mbalimbali kwa sababu walikuwa na Roho wa Mungu ndani yao, na Yesu aliwatumia
lakini ilikuwa katika kiwango cha chini sana, kiwango cha kawaida na ni
wanafunzi hao hao Yesu anawagiza wasianze kuifanya kazi hiyo mpaka wamepokea
uwezo kutoka juu, mpaka wamejiliwa na Roho Mtakatifu, mpaka wamebatizwa kwa
Roho Mtakatifu ona
Luka 24:49 “Na tazama, nawaletea juu yenu
ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.”
Matendo 1:4-5, 8 “4-5,Hata alipokuwa
amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba,
ambayo mlisikia habari zake kwangu; ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali
ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache.” 8 “Lakini
mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa
mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata
mwisho wa nchi.”
Kwa hiyo ubatizo wa Roho
Mtakatifu ni zaidi ya ujazo, ni zaidi ya kuvikwa, ni zaidi ya kupokea, ujazo
una viwango vya viwiko, magoti, kiuno, lakini ubatizo unahusisha maji
yasiyovukika ni aidha uzame na ufie humo uzikwe humo, mtu anapobatizwa kwa maji
huwa anazamishwa analowekwa kila kitu chake mwili wake, nafsi yake, roho yake
na mpaka nguo zake analowa chapa chapa, anafia kwenye maji anazikwa kwenye
maji, anazamishwa, kwa hiyo ubatizo wa Roho Mtakatifu maana yake ni nini Neno ubatizo linatusaidia kwa sehemu kujua
kinachozungumzwa hapo katika lugha ya kibiblia !
Neno ubatizo limetokana na neno
la kiingereza Baptism ambalo kwa
asili limetokana na neno la Kiyunani cha zamani Baptizein ambalo maana yake kuzamisha to immerse, dip in water,
kuzamisha katika maji, kwa hiyo neno hilo ubatizo wa Roho Mtakatifu maana yake
ni kuzamishwa katika Roho Mtakatifu!, aidha nguo za kitani nyeupe zilipokuwa
zikilowekwa ili zipate rangi ya zambarau au nyekundu, zilizamishwa katika maji
yaliyochemka na rangi hiyo na kutoka nguo hiyo ikiwa imebadilika rangi, yaani
nguo ya kitani ingepoteza rangi yake nyeupe na kuwa na rangi ambayo nguo hiyo
imechovya, kitendo hicho pia kinaitwa ubatizo, sasa maana ile ile inayotumika
katika ubatizo wa maji sasa ndio inatumika katika ubatizo wa Roho Mtakatifu,
kwa hiyo nawashauri walimu wa neno la Mungu kutumia neno ubatizo zaidi kuliko
ujazo, au kuvikwa au kupokea nguvu au kujaa Roho Mtakatifu, japokuwa maneno
hayo yote Ujazo na kuvikwa na kupokea yana maana moja lakini msamiati ulio bora
zaidi utumike kubatizwa.
Kwa hiyo Neno ubatizo linapotumika
pamoja na Roho Mtakatifu maana yake ni ile ile kuzamishwa katika Roho kwa hiyo
kila kitu cha mtu anayebatizwa katika Roho Mtakatifu kina uwepo wa Mungu mtu
analowa Roho Mtakatifu kwenye kila kitu mwili wake, nasfi yake, mavazi yake,
mawazo yake, sauti yake, kivuli chake, jasho lake kila kitu, anafia ndani ya
Roho Mtakatifu anabobea analowa maana yake mpaka mifupa ya mtu mwenye Roho wa
Mungu ina jaa uwepo wa Mungu ndio maana Elisha alipokufa watu, walitupia mwili
katika kaburi lake na ule mwili ulipogusa mifupa ya Elisha ukafufuka angalia:-
2Wafalme 13:20-21 “Elisha akafa, nao
wakamzika. Basi vikosi vya Wamoabi wakaingia katika nchi mwanzo wa mwaka.
Ikawa, walipokuwa wakimzika mtu, angalia, waliona kikosi; wakamtupa yule mtu
kaburini mwa Elisha; mara yule maiti alipoigusa mifupa ya Elisha, alifufuka,
akasimama kwa miguu.”
Kwa hiyo mtu aliyebatizwa kwa
Roho Mtakatifu sio mtu wa kawaida, hawi wa kawaida, anaweza kupigwa mawe na
akavumilia, hawi yeye anayeishi, anaweza kupaa kwenda mji mwingine, anaweza
hata kivuli chake kikasababisha miujiza kwa sababu kila kitu kimelowa uwepo wa
Mungu, wakati mwingine hata mazingira ya mtu aliyebatizwa kwa Roho Mtakatifu
huwa na uwepo wa Roho Mtakatifu, Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni kiwango cha maji
yasiyovukika, unazama, unalowa, unapoteza uhai unapotea huwi wa ulimwengu huu
hata kidogo watu wanaweza kudhani miungu imewashukia kwa jinsi ya kibinadamu
sijui unanielewa?
Matendo 14:8-15 “Na huko Listra palikuwa na
mtu mmoja, dhaifu wa miguu, kiwete tangu tumboni mwa mamaye, ambaye hajaenda
kabisa. Mtu huyo alimsikia Paulo alipokuwa akinena; ambaye akamkazia macho na
kuona ya kuwa ana imani ya kuponywa, akasema kwa sauti kuu, Simama kwa miguu
yako sawasawa. Akasimama upesi akaenda. Na makutano walipoona aliyoyafanya
Paulo wakapaza sauti zao, wakisema kwa Kilikaonia, Miungu wametushukia kwa
mifano ya wanadamu. Wakamwita Barnaba, Zeu, na Paulo, Herme, kwa sababu ndiye aliyekuwa
mnenaji. Kuhani wa Zeu ambaye hekalu lake lilikuwa mbele ya mji, akaleta
ng'ombe na taji za maua hata malangoni, akitaka kutoa dhabihu pamoja na
makutano. Walakini mitume Barnaba na Paulo, walipopata habari, wakararua nguo
zao, wakaenda mbio wakaingia katika makutano, wakipiga kelele, wakisema, Akina
bwana, mbona mnafanya haya? Sisi nasi tu wanadamu hali moja na ninyi;
twawahubiri habari njema, ili mgeuke na kuyaacha mambo haya ya ubatili na
kumwelekea Mungu aliye hai, aliyeumba mbingu na nchi na bahari na vitu vyote
vilivyomo;”
Kwa hiyo watu waliobatizwa kwa
Roho Mtakatifu wana kitu cha ziada na
ndio maana hata lugha inaweza kubadilika na wakaanza kusema kwa lugha mpya kwa
nini uwepo wa Mungu unashuka katika kile eneo la mtu aliyebatizwa kwa Roho
Mtakatifu, hiyo ndio maana ya ubatizo wa Roho Mtakatifu. Kama ukichukua chupa
iliyojaa maji unakitumia kama kielelezo cha ujazo wa Roho Mtakatifu maana yake
ujazo wa chupa hautoshi kuelezea ubatizo wa Roho Mtakatifu maana yake ni nini
maana yake Roho anakuwepo mpaka kwenye chupa yenyewe na kifuniko chake !
Mtu aliyebatizwa kwa Roho Mtakatifu:
1.
Anakuwa
na uhusiano wa ndani sana na Mungu – Kwa kawaida mtu ambaye amebatizwa kwa
Roho Mtakatifu anaumbiwa kiu na hamu na shauku ya kuwa na uhusiano wa ndani
sana na Mungu na kiu yake ya kumtafuta Mungu inakuwa kubwa anaweza kujisikia
kuendelea kuutafuta uso wa Mungu hata kama ibada ya kawaida imeisha, wao
watataka kuongea na Mungu watatafakari, wanakuwa kama hawana kiasi katika swala
la kuutafuta uso wa Mungu wanakaa muda mrefu sana kwenye maombi, kiu yao ni
uwepo wa Mungu.Roho wa Mungu ndani yao anawapa neema ya kuomba kwa kuugua kama
waombolezaji.
a. Yoshua Mwana wa Nuni: Kutoka 33:10-11 “Watu wote wakaiona nguzo ya wingu ikisimama penye mlango
wa hema; watu wote wakaondoka wakasujudu, kila mtu mlangoni pa hema yake.Naye
BWANA akasema na Musa uso kwa uso, kama vile mtu asemavyo na rafiki yake. Kisha
akageuka akarejea hata maragoni; bali mtumishi wake Yoshua, mwana wa Nuni, naye
ni kijana, hakutoka mle hemani.”
b. Daudi – Zaburi 27:1-6 “Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani?
Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani? Watenda mabaya waliponikaribia,
Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka. Jeshi
lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata
hapo nitatumaini. Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta,
Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana,
Na kutafakari hekaluni mwake.”
c. Daniel: Daniel 6:4-11 “Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za
kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona
sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala
hatia ndani yake. Ndipo wale watu wakasema, Hatutapata sababu ya kumshitaki
Danieli huyo, tusipoipata katika mambo ya sheria ya Mungu wake. Basi wale
mawaziri na maamiri wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia hivi,
Mfalme Dario, uishi milele. Mawaziri
wote wa ufalme, na manaibu, na maamiri, na madiwani, na maliwali wamefanya
shauri pamoja ili kuweka amri ya kifalme; na kupiga marufuku, ya kwamba mtu ye
yote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda
wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme atatupwa katika tundu la simba. Sasa,
Ee mfalme, piga marufuku, ukatie sahihi maandiko haya, yasibadilike, kama
ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi, isiyoweza kubadilika. Basi mfalme Dario
akayatia sahihi maandiko yale, na ile marufuku. Hata Danieli, alipojua ya kuwa
yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha
katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu ;) akapiga
magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama
alivyokuwa akifanya tokea hapo. Basi watu hao wakakusanyika pamoja, wakamwona
Danieli akiomba dua, na kusihi mbele za Mungu wake.”
d. Paulo mtume na timu yake ya umisheni:
Matendo 16:12-16 “na kutoka hapo tukafika Filipi,
mji wa Makedonia, mji ulio mkuu katika jimbo lile, mahali walipohamia Warumi;
tukawa katika mji huu, tukikaa siku kadha wa kadha. Hata siku ya sabato
tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana
mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale. Mwanamke
mmoja, jina lake Lidia, mwenye kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji wa Thiatira,
mcha Mungu, akatusikiliza, ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze
maneno yaliyonenwa na Paulo. Hata alipokwisha kubatizwa, yeye na nyumba yake,
akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani
mwangu mkakae. Akatushurutisha.Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali,
kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake
faida nyingi kwa kuagua.”
e. Watu
wa Mungu - Zekaria 12:10 “Nami nitawamwagia watu wa
nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao
watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu
amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile
mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.”
2.
Wanasumbuliwa
sana kueneza injili: - Mtu aliyebatizwa kwa Roho Mtakatifu ndani yake
kunakuwa na kiu ya kutaka kuieneza injili, kwa wengine hawahisi utulivu mioyoni
mwao wanawiwa kwa hiyo wanasukumwa kushuhudia, wanasukumwa kulisema neno la
Mungu na hawawezi kukaa kimya
a. Matendo 17:14-17 “Mara
hiyo wale ndugu wakampeleka Paulo aende zake mpaka pwani; bali Sila na Timotheo
wakasalia huko. Lakini wale waliomsindikiza Paulo wakampeleka mpaka Athene; nao
wakiisha kupokea maagizo kuwapelekea Sila na Timotheo, ya kwamba wasikawie
kumfuata, wakaenda zao. Paulo alipokuwa akiwangojea huko Athene na kuona jinsi
mji ule ulivyojaa sanamu, roho yake ilichukizwa sana ndani yake. Basi katika
sinagogi akahojiana na Wayahudi na waliomcha Mungu, na wale waliokutana naye
sokoni kila siku.”
b. Apolo Matendo 18:24-26 “Basi Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzalia wa
Iskanderia, mtu wa elimu, akafika Efeso; naye alikuwa hodari katika maandiko.
Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa
ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi habari za Yesu; naye alijua
ubatizo wa Yohana tu. Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Prisila
na Akila walipomsikia wakamchukua kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi
zaidi.”
3.
Wanakuwa
na uwezo mkubwa sana wa kukabiliana na changamoto – Mtu aliyebatizwa kwa
Roho Mtakatifu anakuwa na uwezo mkubwa sana wa kukabiliana na changamoto yoyote
inayokuja mbele zake na haogopi kitu na wako tayari hata kufa kwaajili ya
injili
a. Matendo 21:10-13 “Basi
tulipokuwa tukikaa huko siku nyingi, nabii mmoja jina lake Agabo akashuka
kutoka Uyahudi. Alipotufikia akautwaa mshipi wa Paulo, akajifunga miguu na
mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu
watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa Mataifa.
Basi tuliposikia haya, sisi na watu wa mahali pale, tukamsihi asipande kwenda
Yerusalemu. Ndipo Paulo alipojibu, Mnafanya nini, kulia na kunivunja moyo? Kwa
maana mimi, licha ya kufungwa, ni tayari hata kuuawa katika Yerusalemu kwa
ajili ya jina lake Bwana Yesu.”
b. Matendo 4:18-20 “Wakawaita,
wakawaamuru wasiseme kabisa wala kufundisha kwa jina la Yesu.Petro na Yohana
wakawajibu wakawaambia, Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko
Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo
tuliyoyaona na kuyasikia.”
4.
Wanafanya
mambo makubwa ya kushangaza na kupita kawaida – watu waliobatizwa kwa Roho
Mtakatifu wanakuwa na karama na vipawa na uweza wa kiungu unaowawezesha kufanya
mambo ya kutisha na kushangaza katika viwango vikubwa sana
a. Matendo 5:12-15 “Na
kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu; nao wote
walikuwako kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani; na katika wote wengine
hapana hata mmoja aliyethubutu kuambatana nao; ila watu waliwaadhimisha;
walioamini wakazidi kuongezeka kwa Bwana, wengi, wanaume na wanawake; hata
ikawa katika njia kuu hutoa nje wagonjwa, na kuwaweka juu ya majamvi na
magodoro, ili Petro akija, ngawa kivuli chake kimwangukie mmojawapo wao.”
b. Matendo 6:8-10 “Na
Stefano, akijaa neema na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika
watu.Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la
Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na
kujadiliana na Stefano; lakini hawakuweza kushindana na hiyo hekima na huyo
Roho aliyesema naye.”
c. Matendo 19:11-12 “Mungu
akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida; hata wagonjwa
wakaletewa leso na nguo zilizotoka mwilini mwake, magonjwa yao yakawaondokea,
pepo wachafu wakawatoka.”
d. Paulo na Barnaba – Matendo 17:2-6 “Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle
walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu, akiyafunua na
kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya
kwamba, Yesu huyu ninayewapasha ninyi habari zake ndiye Kristo. Wengine
miongoni mwao wakaamini, wakashikamana na Paulo na Sila; na Wayunani waliomcha
Mungu, wengi sana, na wanawake wenye cheo si wachache. Na Wayahudi wakaona
wivu, wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio na sifa njema,
nao wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba
ya Yasoni, wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji; na walipowakosa,
wakamkokota Yasoni na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele,
wakisema, Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika huku nako,”
5.
Watu
waliobatizwa kwa Roho Mtakatifu wanakuwa na ukarimu na uwezo wa kujitoa kwa
hali ya juu, wanauwezo wa kutoa mali zao kwaajili ya injili, hutumii nguvu
wala ushawishi kuwataka watoe, wanajua kujitoa, ukiona ni mpaka upige sarakasi
ndio watu wajitoe ujue watu hao bado maji yao ni ya kisigino bado hayajajaa
a. Matendo 4:31-37 “Hata
walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote
wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri. Na jamii ya watu
walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya
kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu
vyote shirika. Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu
nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote. Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni
mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba
waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa, wakaiweka miguuni pa
mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadiri ya alivyohitaji.Na Yusufu, aliyeitwa na
mitume Barnaba, (maana yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa
Kipro, alikuwa na shamba akaliuza, akaileta fedha, akaiweka miguuni pa mitume.”
b. Wafilipi 4:15-19 “Nanyi
pia, ninyi wenyewe mnajua, enyi Wafilipi, ya kuwa katika mwanzo wa Injili,
nilipotoka Makedonia, hakuna kanisa lingine lililoshirikiana nami katika habari
hii ya kutoa na kupokea, ila ninyi peke yenu. Kwa kuwa hata huko Thesalonike
mliniletea msaada kwa mahitaji yangu, wala si mara moja. Si kwamba nakitamani
kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu.
Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa
Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye
kibali, impendezayo Mungu. Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa
kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.”
6.
Hawasumbuliwi
na wachawi na badala yake wao ndio huwa
juu ya wachawi
a. Wagalatia 5:18-21 “Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya
sheria. Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu,
ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka,
uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo
nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo
ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.”
b. Matendo 8:5-13 “Filipo
akatelemka akaingia mji wa Samaria, akawahubiri Kristo. Na makutano kwa nia
moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona
ishara alizokuwa akizifanya. Kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi
waliopagawa nao, wakilia kwa sauti kuu; na watu wengi waliopooza, na viwete,
wakaponywa. Ikawa furaha kubwa katika mji ule. Na mtu mmoja, jina lake Simoni,
hapo kwanza alikuwa akifanya uchawi katika mji ule, akiwashangaza watu wa taifa
la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa. Wote wakamsikiliza tangu
mdogo hata mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni uweza wa Mungu, ule Mkuu.
Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mwingi kwa uchawi wake. Lakini
walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake
Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake. Na yeye Simoni mwenyewe aliamini
akabatizwa, akashikamana na Filipo; akashangaa alipoziona ishara na miujiza
mikubwa inayotendeka.”
c. Matendo 19:17-21 “Habari
hii ikajulikana na Wayahudi wote na Wayunani waliokaa Efeso, hofu ikawaingia
wote, na jina la Bwana Yesu likatukuzwa. Na wengi wa wale walioamini wakaja
wakaungama, wakidhihirisha matendo yao. Na watu wengi katika wale waliotumia
mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma moto mbele ya watu wote;
wakafanya hesabu ya thamani yake, wakaona ya kwamba yapata fedha hamsini elfu. Hivyo
ndivyo neno la Bwana lilivyozidi na kushinda kwa nguvu. Mambo hayo yalipokwisha
kumalizika, Paulo akaazimu rohoni mwake, akiisha kupita katika Makedonia na
Akaya, aende Yerusalemu, akisema, Baada ya kuwako huko, yanipasa kuuona na Rumi
pia.”
Jinsi ya kupokea Ubatizo wa Roho
Mtakatifu.
1. Fahamu
ya kuwa anayebatiza kwa Roho Mtakatifu Ni Bwana Yesu mwenyewe, Na ubatizo huu
ni mpango wa Mungu, ni ahadi ya Mungu kwa waaminio kwa hiyo kila mmoja
anastahili kupokea kwa Imani na kufungua moyo wake kuhakikisha kuwa maisha yake
yanajaa na kufunikwa na uwepo wa Mungu Roho Mtakatifu sawa na neno lake
lisemavyo:-
a. Mathayo 3:11 “Kweli
mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana
nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza
kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.”
b. Ubatizo huu ni ahadi ya Mungu mwenyewe kwa
kila mtu amwaminiye
Yoel 2:28 “Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho
yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee
wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;”
Luka 24:49 “Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini
kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.”
Matendo 2:38-39
“Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa
jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha
Roho Mtakatifu. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na
kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.”
c. Lazima uwe na nia ya kutumika – Ubatizo
wa Roho Mtakatifu ni kwaajili ya utumishi, Roho wa Mungu anatabia ya
kutaharakisha watu kwaajili ya utumishi, Pale tunapokuwa tayari kwa huduma na
kukubali kutumika huku na huko Roho Mtakatifu atakuwa radhi nasi, Ubatizo huu
hauwafai watu ambao wakataa tu, unawafaa watu ambao wako tayari kwa kazi kwa
sababu Roho Hatakupa kutulia
Waamuzi
13:24-25 “Basi yule mwanamke akamzaa mtoto
mwanamume akamwita jina lake Samsoni, mtoto huyu akakua, Bwana akambarikia.
Roho ya Bwana ikaanza kumtaharakisha katika Mahane-dani, katikati ya Sora na
Eshtaoli.”
Yeremia 47:6-7
“Ee upanga wa Bwana, Siku ngapi zitapita kabla
hujatulia? Ujitie katika ala yako; Pumzika, utulie. Utawezaje kutulia, Ikiwa
Bwana amekupa agizo? Juu ya Ashkeloni na juu ya pwani, Ndipo alipoyaamuru hayo.”
d. Kwa maombi bila kuchoka
Luka 18:9-13 “Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi
mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa. Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye
atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. Maana ni yupi kwenu aliye baba,
ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au samaki, badala ya samaki atampa
nyoka? Au akimwomba yai, atampa nge? Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa
watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho
Mtakatifu hao wamwombao?”
e. Lazima uwe na imani
Maswala yote ya kiroho yanapokelewa kwa Imani, wakati
wote mt akiwa na mashaka hawezi kupokea kitu kutoka kwa Mungu, kwani pasipo
Imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa hiyo Mtu anayemuhitaji Roho wa Mungu ni
lazima aombe kwa Imani,
Waebrania 11:6
“Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa
maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa
thawabu wale wamtafutao.”
Wagalatia 3:2 “Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho
kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? ”
Kwa hiyo baada ya kujifunza namna hii na kusikia neno
la Mungu kuhusu Ubatizo wa Roho Mtakatifu unapaswa kuamini na kuatendea kazi
yale yote ambayo umeyasikia na ninakuhakikishia hutakuwa ulivyo.
Na Rev. Innocent Samuel Kamote
Mkuu wa wajenzi Mwenye hekima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni