Jumanne, 26 Januari 2016

Chapa za Yesu!



Ujumbe: Chapa za Yesu
Wagalatia 6:17 “ Tangu sasa mtu asinitaabishe; kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu”

Leo nataka tutafakari kwa pamoja mstari huu muhimu sana katika maisha yetu ya utumishi pamoja na kumfuata Yesu, yaani ukristo ni swala la kuchukua chapa za Yesu nini maana yake? Kuchukua chapa za Yesu?

Biblia ya kiingereza ya NIV inasomeka hivi “Finally, let no one cause me trouble, for I bear on my body the marks of Jesus”

Biblia ya kiingereza ya New Anerican Standard Bible inatafasiri msatri huo namna hii
we are arrested by the words “ I bear on my body the brand-marks of Jesus” neon hilo Brand ni kama “label” na Marks  ni “alama” au chapa maana yake hii ni alama ya kudumu katika mwili wa mnyama au mwanadamu aliye mtumwa

Nyakati za Biblia mtu alipokuwa na wanyama aliwaweka alama kwa kupasha chuma chenye moto na kumbadika mnyama huyo ili kuonyesha kuwa ni wake, swala hili pia lilifanywa kwa watumwa, mtu aliponunua watumwa na kuwamiliki watumwa pia waliwekwa alma kwa chuma cha moto katika mwili wao na kovu la kudumu lingebaki mwilini mwa mtumwa huyo kuonyesha uhalali wa kumilikiwa watumwa hao waliitwa Doulos kwa lugha ya kiyunani, hakuwa na uwezo wa kutoroka na anemtumikia bwana wake milele hata kufa

Paulo anazungumzia maisha ya kujitoa kwa Yesu moja kwa moja ya kuwa kila anayeamua kuwa mkristo hapaswa kuingiza mguu nusunusu kila mtu anayemtumikia Yesu anapaswa kutambua kuwa
1.       Yeye ni mtumwa ni lazima akubali kuwekwa alama na Yesu ya kuwa yeye ni bwana na kuwa ni lazima kumtumikia hata kufa 1Wakoritho 6:19-20 na Warumi 1:1
2.       Kila anayeamua kumfuata Kristo ni lazima akubali kuwa amekubali kujiandikisha jeshi yeye ni askari na yuko tayari kutumika akikabiliana na mazingira magumu 2Timotheo 2:3, 2Wakoritho 5:15
3.       Kila anayeamua kufuata Yesu ni lazima ajitoe kumuabudu Wafilipi 1:20, 2Wakoritho 4:5

MUNGU ANAWEZA! YESU ANAWEZA! (GOD IS ABLE!)


Ni usemi ambao tunapenda sana kuutumia sisi wakristo katika kutiana moyo kuwa Mungu anaweza!
Ndio tunajua kuwa Mungu anaweza kufanya mambo yote kwa vile tangu utoto tumeambiwa Yasiyowezekana kwa wanadamu kwa Mungu yote yawezekana! Hata wahubiri wa injili wengi wanakazia hilo katika mikutano ya injili bila shaka ni ili kuchochea na kupandisha imani za wasilizaji wao
Swali moja la msingi linasalia litakalotusaidia kutafakari kwa kina usemi huu Mungu anaweza? Sawa anaweza nini
Hili linahitaji majibu, nikifahamu au ukifahamu na tukifahamu kuwa Mungu anaweza nini bila shaka kila mtu akinisalimu au akikusalimu au tukisalimiana Mungu anaweza tutakuwa na ujuzi wa kutosha anaweza kufanya nini? Bilia inaeleza kuwa Mungu anaweza kufanya mambo yote, lakini pia imetaja mambo mengi ambayo Mungu anaweza ni yepi?
1.       Anaweza kuokoa
Waebrania 7:25 Biblia inasomeka hivi Naye,  “kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee”. Biblia inasema Mungu yaani Yesu anaweza kuwaokoa kabisa wamjiao, kuokoa kunakotajwa hapa, ni kifurushi chenya mahitaji mengi ya kibinadam yoote kwa ujumla ukimuendea Mungu anaweza kukupatia ufumbuzi kwa vile anatuombea Unaona!

2.       Anaweza kutulinda tusijikwae
Yuda 1:24 Biblia inasema hivi “Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu” Yuda hapa alikuwa akizuingumzia na kuwakemea walimu wa uongo wa neno la Mungu, ambao wangewakwaza wengi kwa mafundisho yao na kuwapotosha na kuwaangusha, lakini pamoja na kuweko kwa mafundisho na imani potofu nyingi katika nyakati za leo biblia inatuthibitishia kuwa uko uwezo wa Mungu wa kutulinda na mafundisho potofu na roho zidanganyazo, kama haitoshi pia Yesu ana uwezo wa kutulinda tusianguke mpaka tutakaposimama katika utukufu wake Mbinguni bila lawama  wala mawaa katika furaha kuuu

3.       Anaweza kuwasaidia wanaojaribiwa!
Waebrania 2:18 Biblia inasema hivi “Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.” Unaona msomaji wangu mpezni usiogope! Hakuna jaribu ambalo ni geni kwa Yesu hususani katika swala la mateso, Yesu anajua kipimo cha mateso yako anajua kuwa yanaweza kukufikisha mahali unaweza hata ukamkosea, habari njema ni kuwa anaweza kuwasaidia wanaojaribiwa je umawahi kuhitaji msaada wake akashindwa? Liitie jina lake omba bila kukoma mtegemee tu atakusaidia anaweza kufanya hivyo.

4.       Aweza kuvitiisha vitu vyote chini yake !
Wafilipi 3:20-21 Biblia inatuambia hivi “ Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;  atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake. Ndugu yangu Yesu anauwezo wa kutiiisha kila kitu chini yake nini kimeinuka katika maisha yako? Nini kinakunyima furaha na kukusababishia huzuni? Je unadhani kitaendelea? Hapana Hakitaendelea mtegemee Mungu anaweza kukitiisha kila kilichoinuka chini ya miguu yake

5.       Anauwezo wa kutupa Neema!
2Wakoritho 9:8 Biblia inasema hivi “Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema; Unaona mtume hapa Mkuu wa wajenzi mwenzangu anazungumza neema katika mazingira ya utoaji, kama utakuwa na tabia ya utoaji kama biblia inavyoelekeza kwa ukarimu na sio kwa kutafuta sifa hutapungukiwa Mungu atakupa neema na kukujaza kwa wingi, utakuwa na riziki za kila namna na nutabarikiwa zaidi katika kila tendo jema yaani la utoaji

6.       Anaweza kumsimamisha mtu au mtumishi aliyeanguka
Warumi 14: 4 Biblia inasema haya “Wewe u nani unayemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa bwana wake mwenyewe yeye husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, kwa kuwa Bwana aweza kumsimamisha.” Msomaji wangu unaweza kujionea! Wako watu ambao wanamafundisho potofu kuhusu wema na rehema za Mungu wanafundisha kuwa mtu aliyeanguka hawezi kusimama tena, ni mafundisho ya kijinga ni imani ya kipuuzi, lipi lililo jepesi kumwambia aliyelala amka au aliyekufa fufuka? Ikiwa Mungu anaweza kuwafufua wafu kutoka dhambini anashindwaje kumwamsha mwanaye aliyeanguka! Biblia inasema Usihukumu ni Mungu anayeruhusu kwa utukufu wake na anauwezo wa kuhuisha tena, sitii moyo tabia na mwenendo wa kufanya dhambi mara kwa mara kwa kisingizio kuwa Mungu anasimamisha tena, lakini nakataa kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima wale wanaosema mtu akianguka hawezi kusimama tena Munu anaweza, anaweza kumsimamisha mtumishi wake aliyeanguka na kamtumia tena kwa viwango vya juu zaidi bila kiburi

7.       Anauwezo wa kufanya zaidi ya yale tuyaombayo na tuyawazayo
Waefeso 3:20 “Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; Umeona nataka kukamilisha ujumbe huu kwa Pointi hii ya saba kwa vile namba hii kinabii ni utimilifu wa mambo yote ziko sababu nyingi ambazo Mungu anaweza lakini hii inajumuisha yote, kumbe anaweza kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo na tuyawazayo hii imanimaliza siwezi kuendelea bila shaka msomaji wangu umepata ufunuo mkuu sana hata nisipokuombea leo, anaweza kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo na tuyawazayo imani yangu ni kuwa tangu sasa mtu akikusalimu Mungu anaweza utakuwa na ujuzi anaweza nini
Ubarikiwe na Bwana siku njema

Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote.

Umuhimu wa tiba ya Kukanda mwili ( Massage)




Ni muhimu kuwa na ufahamu kuhusu tiba maalumu ya kuukanda mwili ambayo kwa lugha ya kitaalamu hujulikana kama Massage au Massaging therapy, Jambo hili sio starehe kama wengi wanavyofahamu na wala sio anasa au dhambi, ni kwa sababu watu wengi hawana ufahamu wa kutosha kuhusu swala hili, ama kwa sababu linafanyika katika vilabu, baadhi ya viwanja vya ndege kwenye saloon na kadhalika tena kwa malipo, wengi wamefikiri kuwa hii ni Biashara ya anasa na huenda inafanyiwa watu wenye kupenda raha au starehe na wakati mwingine imedhaniwa kuwa ni dhambi kutokana na mazingira ya wanaotibu na pale watu wanapotibiwa na wale wanaozifanya wakiunganisha na tabia za kishetani za ufuska na sitaki kuunga mkono wafanyao hayo na huko lakini nataka kuweka siri hii wazi ili kuisaidia jamii kama Mkuu wa  wajenzi mwenye hekima


Tiba ya kukanda mwili (Massage) ni nini?
Kwa ujumla kuukanda mwili ni tiba inayohusu, kusugua kubonyeza ngozi pamoja na misuli na viungo kadhaa vya mwili, hii ni tiba yenye faida kubwa sana katika mwili na maisha ya Mwanadamu, shetani ameifanya yak wake ili apate nafasi ya kuiba na kupokonya siri zinazoweza kuwasaidia watu wa Mungu Massage licha ya kuzuia uwezekana wa kupata kansa pia inazuia uwezekano mkubwa wa kupooza au ugonjwa wa kiharusi stroke
Aina za ukandaji (Massage)
1.       Kukanda kwa kiswideen (Swedish Massage) hii ni aina ya kuukanda mwili kwa kuupigapiga kwa nguvu au kutetemesha mfano wa wachezaji wa mpira wanapokuwa wamekamatwa na misuli mtu mwenye ujuzi wa hili anaweza kkupigapiga na kwa kutetema na kuuzunguka mwili mzima na hivyo kuupa nguvu mwili na kuufanya usiwe na maumivu na huondoa uchovu
2.       Ukandaji wa ndani zaidi
Ukandaji huu hufanyika polepole na kwa kundamiza zaidi sehemu zenye misuli na viungo ili kwa kawaida kusaidia misuli isiweze kupata uharibifu
3.       Ukandaji wa kimazoezi (Sports Massage) huu ni ukandaji sawa na ule wa Kisweeden ambao hufanyiwa watu wanaoshiriki michezo kama bondia, Mpira kukimbia nk, kwa kusudi la kuleta utulivu wa misuli na kuipoza kutokana na majeraha ya kimichezo au mazoezi magumu
4.       Trigger point Massage ukandaji maalimu katika eneo maalumu lililojeruhiwa hii hufanyika kama sehemu ya kutibu eneo hilo
Faida za Ukandaji.
Ukandaji ni moja ya tiba muhimu baridi na tiba mbadala na njia ya kuepuka kemikali mwilini pia imekuwa ikitolewa kama tiba kamili pamoja na madawa, imebainika kuwa ni tiba kamili na yenye uwezo mkubwa wa kuondoa Uchovu na migandamizo stress na kuondoa maumivu ya misuli katika mwili na misuli iliyoumizwa wakati utafiti zaidi ukiwa unaendelea kuhusu tiba hii tayari maswala kadhaa ymabainika kutibiwa na tiba hii mbadala
1.       Kuondoa maumivu ya kichwa
2.       Mashaka na hofu au wasiwasi
3.       Kuondoa stress au migandamizo na athari zake
4.       Kuondoa maumivu ya misuli
5.       Kulainisha ngozi na kuzipa mazoezi cell za mwili
6.       Kuondoa uchovu na maumivu kwa mishipa ya fahamu
7.       Kuondoa maumivu yatokanayo na michezo na majerhaha au maumivu ya muda
Huko china tiba hii hufanywa na zaidi kwa wazee kwaajili ya kuwakinga na Kansa na stress lakini pia humpa muda mgonjwa wa kansa na kuongeza muda wa uhai, wajukuu wengi huwakandakanda wazee wao kila wanapokutana nao au nwanapoketi au wakiwa wamerudi kutoka matembezi ili kuondoa stress na kuwafanya wajisikie huru
Tahadhari kuhusu tiba ya kukanda
Pamoja na tiba hii kuwa ni yenye uwezo wa kuwafaa watu wengi sana ni muhimu kufahamu kuwa watu wafuatao haitawafaa
1.       Wenye kutoka damu au wenye kuchuruzikwa na damu bila mpangilio
2.       Wenye vidonda vibichi na vilivyo wazi au majeraha yaliyo wazi
3.       Wenye shida ya mishipa ya vein
4.       Waliotenguka au kupata nyufa katika mifupa
5.       Ukandaji pia haupaswi kuwa wenye kusababisha maumivu au usioleta faraja sema mara moja ikiwa ukandaji huounakusababishia maumivu na haupati kile unachokitarajia ni katika hatua chache wakati mwingine tiba hii huweza kusababisha  umwagikaji damu kwa ndani au kuharibu fahamu kama haitafanyika vema na au allege Nzio kama utatumia mafuta ya kulainisha ambayo hayapatani na anayetibiwa
Onyo:
Massage inaweza kufanyika Nyumbani kwako kama utawaelekeza vizuri wale wanaokuzunguka na wakupendao na kukutakia mema, wale ambao huenda saloon na vilabuni wana matatizo ya kisaikolojia na wanahitaji wokovu! Mada na Mkuu wa Wajenzi mwenye hekima. Rev Innocent Kamote.

SOMO: TUKARUDI MISRI!



Hesabu 14: 1- 4 “Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia; watu wakatoka machozi usiku ule. 2. Kisha wana wa Israeli wote wakamnung'unikia Musa na Haruni; mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili. 3. Mbona Bwana anatuleta mpaka nchi hii ili tuanguke kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watakuwa mateka; je! Si afadhali turudi Misri?  4. Wakaambiana, Na tumweke mtu mmoja awe akida, TUKARUDI MISRI.

Katika moja ya Matukio yasiyoweza kusahaulika Katika Historia ya Israel ni pamoja na tukio hili linalotajwa kutokea katika Mistari hii tuliyoisoma! Haya ni moja ya maneno yaliyotamkwa na watu waliokata tamaa, Hakuna jambo baya sana Duniani kama Kukata tama, watu wanapokata tamaa huweza kufanya lolote na kutamka lolote hiki ndicho kilichotokea hapa!

·        Misri lilikuwa ndio taifa la kwanza lenye jamii yenye maendeleo makubwa sana “Civilization”
·        Kihistoria jamii ya wamisri ilikusanyika kwa wingi kutokana na kukua kwa jangwa la sahara kati ya mwaka wa 7000 mpaka wa 5000 (K.K.)kabla ya Kristo
·        Jamii ya watu waliokusanyika waliweza kuwa na maendeleo makubwa sana kutokana na matumizi ya maji ya mto Nile kwa kilimo na umwagiliaji
·        Bonde la mto nile lilikuwa na rutuba ya kutosha kutokana na kutiririka kwa mbolea toka Ethiopia na maeneo mengine yenye asili ya mto nile

·        Kutoakana na kuwepo kwa rutuba hii kuliwafanya watu wengi kufanya makazi ya kudumu pale Misri na kukawa na maendeleo makubwa katika sekta ya kilimo
·        Misri ilianza kuwa taifa kamili kutokana na kuweko kwa jamii mbalimbali na falme ndogondogo zilizoungana na baadaye kuwa na mataifa makubwa mawili yaani Upper Egypt na Lower Egypt au Delta Nile maendeleo haya yalitokea karne nne kabla ya Kristo, mwaka wa 3200 baadaye falme hizi mbili ziliungana na kuwa ufalme mmoja chini ya watawala waliojulikana kama farao
·        Kutokana na ugunduzi wa chuma uliokuweko miaka mingi wamisri waliweza kuendeleza teknolojia ya vifaa mbalimbali kwa kilimo huku wakiwa na kiu ya ujuzi na maarifa na sanaa na taaluma mbalimbali, Misri ilipata neema ya kuwa na watu wengi, Uongozi imara na kukua kwa maarifa, wamisriwalikuwa na maarifa makubwa ambayo mengina yanatumika na ulimwengu huu wa leo tulio nao:-
*      Kulikuwa na ujuzi wa kuandika katika magombo ya karatasi ziitwazo “papyrus”
*      Walikuwa ndio watu wa kwanza kugundua na kutumia kalenda yenye siku 365
*      Walikuwa na ujuzi wa maswala ya nyota na unajimu
*      Uwezo mkubwa wa uhandisi na ujenzi kwa kutumia Mawe na ujuzi wa kutumia shaba na dhahabu, walikuwa na ujuzi wa Mathematics na Geometric
*      Wamisri walikuwa hodari katika maswala ya upasuaji na utabibu na hata kutunza maiti isiozekwa muda mrefu
*      Tawala za kisiasa zenye nguvu za kifarao ambazo zimedumu kwa zaidi ya miaka 3000 inasemakena ya kuwa Misri ndio taifa lililojiunda katika mfumo wa taifa na maendeleo kwa muda mrefu zaidi kuliko yote duniani
*      Kutokana na utaalamu huo waliweza kuwa na Jeshi kali lenye silaha na ujuzi wa kutumia farasi na wanyama wengineo
*      Utawala wa farao inaaminika kuwa ulidumu kwa miaka 3200 KK mpaka 352KK, kabla ya Kristo.
*      Hata hivyo kiroho Misri waliabudu miungu mingi sana miungu mikuu ilikuwa karibu kumi na Pharao mwenyewe na ukoo wake alihezabika kama uzao uliotoka kwa Mungu hivyo farao alikuwa Mungu
Pamoja na nguvu kubwa waliyokuwa nayo taifa Hili Mungu alilipigilia mbali na kuwaokoa watu wake, lakini katika namna ya kushangaza sana Israel wanagoma kuingia kanaani baada ya muda fupi tu kwa sababu ya habari za kukata tamaa walizozisikia toka kwa wapelelezi 12  Hesabu 12:26-31. Israel wanavunjika moyo na Mungu anakasirishwa sana na jambo hili na hivyo iliwachukua miaka 40 sasa kuimaliza safari kwa kuzungushwa Jangwani!
Kwa nini Mungu alikasirishwa sana
1.      Walimfanya Mungu aliyewaahidi kuwa atawapa inchi ile kuwa ni Muongo
2.      Walishindwa kukumbuka Fadhili na utendaji wa Mungu jinsi alivyowafanyia mambo makubwa sana
3.      Waliangalia taarifa ya wengi wakasahau taarifa ya wachache Mungu sio Mwanademokrasia utawala wake unaitwa “THEOCRASY”
4.      Waliona kuwa tatizo lililoko mbeleyao ni kubwa Kuliko Mungu
5.      Walisahau kuwa uko uwepo wa Mungu pamoja nao na kuwa Mungu hakuwaacha
6.      Walishindwa kumuamini Mungu na kuogopa kile kilichokuwa kinawaogopa
Yoshua 2:1-3, 8-11
Siku zote unapotaka kusonga Mbele kamwe usikae na watu waliakata tamaa, fanya lako ambalo unajua Mungu amekusudia ulifanye!
Mwamini Mungu!, angalia historia ya yale ambayo Mungu alikufanyia
Acha kuangalia mazingira Magumu au ukubwa wa changamoto zako bali angalia Ukubwa wa Mungu wako!