Hesabu 14: 1- 4 “Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia; watu
wakatoka machozi usiku ule. 2. Kisha wana wa Israeli wote wakamnung'unikia Musa
na Haruni; mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi
ya Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili. 3. Mbona Bwana
anatuleta mpaka nchi hii ili tuanguke kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu
watakuwa mateka; je! Si afadhali turudi Misri?
4. Wakaambiana, Na tumweke mtu mmoja awe akida, TUKARUDI MISRI.
Katika
moja ya Matukio yasiyoweza kusahaulika Katika Historia ya Israel ni pamoja na
tukio hili linalotajwa kutokea katika Mistari hii tuliyoisoma! Haya ni moja ya
maneno yaliyotamkwa na watu waliokata tamaa, Hakuna jambo baya sana Duniani
kama Kukata tama, watu wanapokata tamaa huweza kufanya lolote na kutamka lolote
hiki ndicho kilichotokea hapa!
·
Misri lilikuwa
ndio taifa la kwanza lenye jamii yenye maendeleo makubwa sana “Civilization”
·
Kihistoria jamii
ya wamisri ilikusanyika kwa wingi kutokana na kukua kwa jangwa la sahara kati
ya mwaka wa 7000 mpaka wa 5000 (K.K.)kabla ya Kristo
·
Jamii ya watu
waliokusanyika waliweza kuwa na maendeleo makubwa sana kutokana na matumizi ya
maji ya mto Nile kwa kilimo na umwagiliaji
·
Bonde la mto
nile lilikuwa na rutuba ya kutosha kutokana na kutiririka kwa mbolea toka
Ethiopia na maeneo mengine yenye asili ya mto nile
·
Kutoakana na
kuwepo kwa rutuba hii kuliwafanya watu wengi kufanya makazi ya kudumu pale
Misri na kukawa na maendeleo makubwa katika sekta ya kilimo
·
Misri ilianza
kuwa taifa kamili kutokana na kuweko kwa jamii mbalimbali na falme ndogondogo
zilizoungana na baadaye kuwa na mataifa makubwa mawili yaani Upper Egypt na
Lower Egypt au Delta Nile maendeleo haya yalitokea karne nne kabla ya Kristo,
mwaka wa 3200 baadaye falme hizi mbili ziliungana na kuwa ufalme mmoja chini ya
watawala waliojulikana kama farao
·
Kutokana na
ugunduzi wa chuma uliokuweko miaka mingi wamisri waliweza kuendeleza teknolojia
ya vifaa mbalimbali kwa kilimo huku wakiwa na kiu ya ujuzi na maarifa na sanaa
na taaluma mbalimbali, Misri ilipata neema ya kuwa na watu wengi, Uongozi imara
na kukua kwa maarifa, wamisriwalikuwa na maarifa makubwa ambayo mengina
yanatumika na ulimwengu huu wa leo tulio nao:-
Kulikuwa na
ujuzi wa kuandika katika magombo ya karatasi ziitwazo “papyrus”
Walikuwa ndio
watu wa kwanza kugundua na kutumia kalenda yenye siku 365
Walikuwa na
ujuzi wa maswala ya nyota na unajimu
Uwezo mkubwa wa
uhandisi na ujenzi kwa kutumia Mawe na ujuzi wa kutumia shaba na dhahabu,
walikuwa na ujuzi wa Mathematics na Geometric
Wamisri walikuwa
hodari katika maswala ya upasuaji na utabibu na hata kutunza maiti isiozekwa
muda mrefu
Tawala za
kisiasa zenye nguvu za kifarao ambazo zimedumu kwa zaidi ya miaka 3000
inasemakena ya kuwa Misri ndio taifa lililojiunda katika mfumo wa taifa na
maendeleo kwa muda mrefu zaidi kuliko yote duniani
Kutokana na
utaalamu huo waliweza kuwa na Jeshi kali lenye silaha na ujuzi wa kutumia
farasi na wanyama wengineo
Utawala wa farao
inaaminika kuwa ulidumu kwa miaka 3200 KK mpaka 352KK, kabla ya Kristo.
Hata hivyo
kiroho Misri waliabudu miungu mingi sana miungu mikuu ilikuwa karibu kumi na
Pharao mwenyewe na ukoo wake alihezabika kama uzao uliotoka kwa Mungu hivyo
farao alikuwa Mungu
Pamoja
na nguvu kubwa waliyokuwa nayo taifa Hili Mungu alilipigilia mbali na kuwaokoa
watu wake, lakini katika namna ya kushangaza sana Israel wanagoma kuingia
kanaani baada ya muda fupi tu kwa sababu ya habari za kukata tamaa
walizozisikia toka kwa wapelelezi 12 Hesabu 12:26-31. Israel wanavunjika
moyo na Mungu anakasirishwa sana na jambo hili na hivyo iliwachukua miaka 40
sasa kuimaliza safari kwa kuzungushwa Jangwani!
Kwa
nini Mungu alikasirishwa sana
1.
Walimfanya Mungu
aliyewaahidi kuwa atawapa inchi ile kuwa ni Muongo
2.
Walishindwa
kukumbuka Fadhili na utendaji wa Mungu jinsi alivyowafanyia mambo makubwa sana
3.
Waliangalia
taarifa ya wengi wakasahau taarifa ya wachache Mungu sio Mwanademokrasia
utawala wake unaitwa “THEOCRASY”
4.
Waliona kuwa
tatizo lililoko mbeleyao ni kubwa Kuliko Mungu
5.
Walisahau kuwa
uko uwepo wa Mungu pamoja nao na kuwa Mungu hakuwaacha
6.
Walishindwa
kumuamini Mungu na kuogopa kile kilichokuwa kinawaogopa
Yoshua 2:1-3, 8-11
Siku
zote unapotaka kusonga Mbele kamwe usikae na watu waliakata tamaa, fanya lako
ambalo unajua Mungu amekusudia ulifanye!
Mwamini
Mungu!, angalia historia ya yale ambayo Mungu alikufanyia
Acha
kuangalia mazingira Magumu au ukubwa wa changamoto zako bali angalia Ukubwa wa
Mungu wako!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni