Ni muhimu kuwa na ufahamu kuhusu
tiba maalumu ya kuukanda mwili ambayo kwa lugha ya kitaalamu hujulikana kama
Massage au Massaging therapy, Jambo hili sio starehe kama wengi wanavyofahamu
na wala sio anasa au dhambi, ni kwa sababu watu wengi hawana ufahamu wa kutosha
kuhusu swala hili, ama kwa sababu linafanyika katika vilabu, baadhi ya viwanja
vya ndege kwenye saloon na kadhalika tena kwa malipo, wengi wamefikiri kuwa hii
ni Biashara ya anasa na huenda inafanyiwa watu wenye kupenda raha au starehe na
wakati mwingine imedhaniwa kuwa ni dhambi kutokana na mazingira ya wanaotibu na
pale watu wanapotibiwa na wale wanaozifanya wakiunganisha na tabia za kishetani
za ufuska na sitaki kuunga mkono wafanyao hayo na huko lakini nataka kuweka
siri hii wazi ili kuisaidia jamii kama Mkuu wa
wajenzi mwenye hekima
Tiba ya kukanda mwili (Massage) ni nini?
Kwa ujumla kuukanda mwili ni tiba
inayohusu, kusugua kubonyeza ngozi pamoja na misuli na viungo kadhaa vya mwili,
hii ni tiba yenye faida kubwa sana katika mwili na maisha ya Mwanadamu, shetani
ameifanya yak wake ili apate nafasi ya kuiba na kupokonya siri zinazoweza
kuwasaidia watu wa Mungu Massage licha ya kuzuia uwezekana wa kupata kansa pia
inazuia uwezekano mkubwa wa kupooza au ugonjwa wa kiharusi stroke
Aina za ukandaji (Massage)
1. Kukanda
kwa kiswideen (Swedish Massage) hii ni aina ya kuukanda mwili kwa kuupigapiga
kwa nguvu au kutetemesha mfano wa wachezaji wa mpira wanapokuwa wamekamatwa na
misuli mtu mwenye ujuzi wa hili anaweza kkupigapiga na kwa kutetema na
kuuzunguka mwili mzima na hivyo kuupa nguvu mwili na kuufanya usiwe na maumivu
na huondoa uchovu
2. Ukandaji
wa ndani zaidi
Ukandaji huu
hufanyika polepole na kwa kundamiza zaidi sehemu zenye misuli na viungo ili kwa
kawaida kusaidia misuli isiweze kupata uharibifu
3. Ukandaji
wa kimazoezi (Sports Massage) huu ni ukandaji sawa na ule wa Kisweeden ambao
hufanyiwa watu wanaoshiriki michezo kama bondia, Mpira kukimbia nk, kwa kusudi
la kuleta utulivu wa misuli na kuipoza kutokana na majeraha ya kimichezo au
mazoezi magumu
4. Trigger
point Massage ukandaji maalimu katika eneo maalumu lililojeruhiwa hii hufanyika
kama sehemu ya kutibu eneo hilo
Faida za Ukandaji.
Ukandaji ni moja ya tiba muhimu
baridi na tiba mbadala na njia ya kuepuka kemikali mwilini pia imekuwa
ikitolewa kama tiba kamili pamoja na madawa, imebainika kuwa ni tiba kamili na
yenye uwezo mkubwa wa kuondoa Uchovu na migandamizo stress na kuondoa maumivu
ya misuli katika mwili na misuli iliyoumizwa wakati utafiti zaidi ukiwa
unaendelea kuhusu tiba hii tayari maswala kadhaa ymabainika kutibiwa na tiba
hii mbadala
1. Kuondoa
maumivu ya kichwa
2. Mashaka
na hofu au wasiwasi
3. Kuondoa
stress au migandamizo na athari zake
4. Kuondoa
maumivu ya misuli
5. Kulainisha
ngozi na kuzipa mazoezi cell za mwili
6. Kuondoa
uchovu na maumivu kwa mishipa ya fahamu
7. Kuondoa
maumivu yatokanayo na michezo na majerhaha au maumivu ya muda
Huko china tiba
hii hufanywa na zaidi kwa wazee kwaajili ya kuwakinga na Kansa na stress lakini
pia humpa muda mgonjwa wa kansa na kuongeza muda wa uhai, wajukuu wengi
huwakandakanda wazee wao kila wanapokutana nao au nwanapoketi au wakiwa
wamerudi kutoka matembezi ili kuondoa stress na kuwafanya wajisikie huru
Tahadhari kuhusu tiba ya kukanda
Pamoja na tiba
hii kuwa ni yenye uwezo wa kuwafaa watu wengi sana ni muhimu kufahamu kuwa watu
wafuatao haitawafaa
1. Wenye
kutoka damu au wenye kuchuruzikwa na damu bila mpangilio
2. Wenye
vidonda vibichi na vilivyo wazi au majeraha yaliyo wazi
3. Wenye
shida ya mishipa ya vein
4. Waliotenguka
au kupata nyufa katika mifupa
5. Ukandaji
pia haupaswi kuwa wenye kusababisha maumivu au usioleta faraja sema mara moja
ikiwa ukandaji huounakusababishia maumivu na haupati kile unachokitarajia ni
katika hatua chache wakati mwingine tiba hii huweza kusababisha umwagikaji damu kwa ndani au kuharibu fahamu
kama haitafanyika vema na au allege Nzio kama utatumia mafuta ya kulainisha
ambayo hayapatani na anayetibiwa
Onyo:
Massage inaweza
kufanyika Nyumbani kwako kama utawaelekeza vizuri wale wanaokuzunguka na
wakupendao na kukutakia mema, wale ambao huenda saloon na vilabuni wana
matatizo ya kisaikolojia na wanahitaji wokovu! Mada na Mkuu wa Wajenzi mwenye
hekima. Rev Innocent Kamote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni