Kila mtu anamikasa yake ambayo
amewahi kukutana nayo na mingine inaweza kukufedhehesha, mimi nimeshawahi
kufedheheka mara nyingi lakini zilikuwa fedheha ndogondogo, lakini hii ya mwaka
juzi ilikuwa sio fedheha bali ni jifehdeha unajua ilikuwaje? Nilikuwa ndiyo nimehitimu
kwenye chuo cha ustawi wa jamii huko Tengeru Arusha. Nilitoka Arusha na kurejea
Dar ambapo ndipo wazazi wangu waliko, Nilipofika Dar nilibahatika kupata
kibarua kwenye taasisi moja ya watoto.
Nilianza kazi pale kama mtu wa
kujitolea ili kupata uzoefu kama wenyewe walivyoniambia, ningeweza kupata ajira
pia baadaye kama ningeonyesha uwezo mkubwa na Ufahamu wa shughuli za kuishi na
watoto yatima, Hapo kwenye kituo kulikuwa na na mama ambaye ndiye aliyekuwa
naibu mkuu wa kituo, mama huyu alikuwa mcheshi na mwelewa sana, alikuwa na
upendo wa kweli kabisa ambao mtu angeweza kuuhisi hata kutokea mbali sana.
samahani kwa Picha hii kama itakusumbua Masomo haya yanawalenga jamii mbalimbali hasa vijana kwa kusudi la kuwajenga hivyo usifadhaishwe
Mimi kama kijana ambaye sikuzoea
upendo mwingine ila ule wa ngono tu, nilianza kuutafasiri vibaya upendo ule wa
ngono, nilijua kuwa Yule mama alikuwa ananitaka, nilijua anataka vijana,
Nilijiambia kuwa hiyo ni kweli kwani hata wakati ninafanyiwa usaili alionekana
kunitetea sana , nilijua nikimpata tu na ajira nimepata, Lakini pia alikuwa
anatamanisha! Niliamua kumfanyia kampeni ili kumnasa nilianza harakati hizo kwa
kumzoea na kumtania kidogo, kwa utani niliona bila shaka asingepata ujumbe
maana alikuwa mtu wa utani na kila mtu , mtu mcheshi na mwenye kuelewana na
kila mtu, Basi siku hiyo asubuhi kwenye saa tatu nikampatia nafasi, nilimkuta
yuko kwenye chumba kimoja akiwa peke
yake, nilimsalimia na kumwambia kwamba nina ujumbe wake, aliniuliza kimzaha ni
ujumbe gani asubihi ile , ule mzaha ulinifanya niamini kwamba ameshaelewa na
amefurahia ninachotaka kusema, Nilituma
ombi langu ni kiwa na matumaini ya dhati kubwa sana. Alistuka lakini
alijikaza na kusema huo siyo utani mzuri sana, wakati huu tayari ibilisi Alisha
nipanda hivyo nilimwambia sikutanii niko
siriasi ninakupenda tangu siku ile ya kwanza, usione aibu usijisikie vibaya kwa
sababu unanizidi kidogo umri najua wewe una ….’
Yule mama alinikatisha kwa
kunipungia mkono, Nilishusha maruhani yangu, sikiliza najua kama binadamu
unaweza kweli kunipenda kwa njia hiyo,
lakini huoni kuna hatari, mimi ni mke wa mtu tunatarajia kufanya kazi pamoja na umri wako ni mdogo kwangu haipendezi sana
Ulikuwa ni ukweli mtupu, lakini
kufikiri vibaya ambapo huwa tuna kuita ibilisi, kulikuwa kumejenga kibanda
akilini mwangu, sikuliona hilo, hivyo niliendelea kubwabwanya, Najua ni kweli
lakini ninavyokupenda huwezi kuniambia kitu nikubali kwa kweli nihurumie
nakuomba…’ Nilimfuata polepole pale alipokuwa amekaa na kupeleka mkono wangu
shavuni mwake alinyamaza akiniangalia, nadhani kwakuwa hakuamini kuwa ninafanya
upumbavu ule, mimi mawazoni mwangu niliona kwamba kumbe ni rahisi Nilijithibitishia
kwamba alikuwa akinipenda sana, nilishusha mkono wangu na kuufikisha shingoni
na ibilisi wa kujipachika aliupeleka mkono wangu hadi kwenye matiti, Yule mama
alisimama na kutimua mbio hadi nje na dakika kumi baadaye nikiwa najaribu
kujiuliza nimekosea wapi wakati kila kitu kilikuwa kinaenda vizuri niliona
walinzi wawili wa kituo wakiingia mle ndani, waliniomba niende nao ofisini
nilianza kubabaika kwa kuwauliza kulikoni, walisema hakuna jambo isipokuwa
wameambiwa wanipeleke ofisini kwa mkuu wa kituo, nilijua labda yangekuwa ni maswala
ya kazi.
Nilipoingia ofisini nilishangaa
kukuta wafanya kazi wote wa kituo pamoja na Yule mama, bado nilikuwa najua
yalikuwa ni maswala ya kikazi, au kuna dharula Fulani ofisini , ukiendekeza
mwili kweli unakuwa bwege sana niliwasalimia wale wafanyakazi na wengi
hawakuniitikia. Mkuu wa kituo hakuzungumza sana kwani baada ya kusalimia tu
alisema ni jambo la kuhuzunisha sana kukutana asubuhi ile kujadilisuala ambalo
halina maana sana Alisema kuna mwenzetu mmoja asubuhi hii ameonyesha utovu wa
nidhamu ambao haujawahi kuonyeshwa na mtumishi yeyote hapa kituoni, mwenzetu
huyu amemtongoza mama na kujaribu hata kumbaka, napengine sio kujaribu bali kwa
sheria za inchi hivi sasa tunaweza kusema kuwa alimbaka, watumishi wote
walisema ayahaa! Si unajua upambe tena Nilijua kabisa kuwa nilikuwa muhanga,
nilijaribu kujipa moyo kwamba labda angekuwa ni mtumishi mwengine lakini
kutajwa jina Yule mama kulinifanya niache kuendelea kujidanganya.
Mama amewahi kutoa taarifa hii na
tulikuwa tunafikiri kulifikisha Polisi jambo hili lakini tumeona tutaharibu
sifa ya kituo hivyo tunamwomba (alitaja jina langu) amwombe radhi mama … kwa
kile kilichotokea asubuhi ya leo, nilikuwa natetemeka na mimacho ya watumishi
wote ilikuwa kwangu, nilitamani kukanusha, kutukana, na kusema ondoeni upuuzi
wenu lakini nilishindwa nilijikuta
nasema naomba radhi Mama… kwa yote niliyoyatenda Halafu nilinyamaza.
Tunashukuru kwa hilo kuanzia hivi sasa hutakiwi kuonekana katika maeneo haya na
ukionekana itakuwa ni kwa hasara yako mkuu wa kituo alisema.
Unataka kujua mambo yaliendaje
baada ya pale? Nenda kawaulize pale kituoni na uwaambie wewe ndiye Yule
mwakilishi mkuu wa wambeya wa jimbo lenu.