Mwaka 1997 nilipokuwa nimemaliza
masomo yangu ya shahada ya kwanza pale chuo kikuu cha Dar es Salaam, nilikuwa
nimefanyiwa mpango wa ajira na jamaa yangu mmoja kwenye kampuni moja jijini Dar
na nikawa nimefanikiwa, Baada ya mipango ya hapa na pale na kunifagilia sana kama wanavyosema watu wa
mjini nilifanikiwa kupata barua ya ajira
kama afisa uhusiano kwenye kampuni moja ambayo haikuwa kubwa sana wakati ule ingawa sasa hivi imeshakuwa,
Nilipata barua iliyonitaka kuanza kazi wiki inayofuata kwa kweli nilifurahi
sana , lakini kitu kibaya kwangu ni kuwa sikuwa na adabu na kile kiburi cha
watoto wa kidato cha pili siyo cha mtu
aliyemaliza chuo kikuu bado kilikuwa
kinayawala kwangu.
Siku ya kuripoti kazini iliwadia
ambapo niliamka mapema sana na kujiandaa. Nilikuwa naishi mabibo External kwa
wazazi wangu wakati huo, Niliondoka nyumbani saa 12 asubuhi nikiwa na uhakika
kuwa nitafika mjini Posta kabla ya saa
mbili asubuhi muda wa kuripoti ofisini, Nilipanda basi hadi ambapo nilipanda basi linguine , tulisafiri
hadi pale Shekilango ambapo gari Fulani ilipoteza muelekeo likataka kuivaa
daladala niliyokuwemo, ilibidi mwenye gari lile linguine kusimama na daladala
yetu pia ilisimama, Abiria wa daladala walishuka na wa lile gari linguine aina
ya Prado nao walishuka , mimi nikawa wa kwanza, kuwaendea wale wenye gari
nyingine ambao walikuwa watatu, mmoja wao mwembamba kiasi na mwenginemfupi
mweusi sana aliyekuwa ndiye msemaji, Hakuwa anasema chochote zaidi ya kuomba
radhi kwa unyenyekevu kuwa gari lao lilikuwa limepata tatizo la usukani. Mimi
nilipandisha sana huku nikitumia maneno
ya kingereza kuwaambia kwamba hawajastaarabika , nilimwambia Yule aliyekuwa
msemaji wao kwamba ndio maana amekuwa
mweusi na kafupi sana kwa sababu ya ujeuri, Yule jamaa alisema ni sawa
ninavyonena, hata hivyo dereva wa daladala yetu alikuwa mstaarabu aliwaunga
mkono jamaa wale akisema anaelewa aina
hozo za tatizo na akaomba abiria tupande garini
na kuondoka niliwageukia wale
jamaa na kuwaambia “You are just luck guys” nikimaanisha kwamba wana bahati
sana
Ndani ya basi nikazidi kusema
kama kinanda , baadhi ya abiria wenye tabia kama mimi wakaniunga mkno , abiria
wengine hawakuniunga mkno, ingawa hawakusema
hivyo, bali ile tazama yao niliijua tu sikujali. Nilifika Posta mapema na
kwenda moja kwa moja kwenye ofisi ambayo nilitakiwa kuanza kazi, iliandikwa
kwenye barua kwamba nimuone mkurugenzi mkuu kabla sijaenda kwa menenja kupangiwa majukumu yangu ya awali. Ilipotimu
saa mbili niliomba kuingia kwa mkurugenzi ambapo niliruhusiwa, niliingia
nikijua kuwa nitapokea zinga la sifa kwa kuchaguliwa kwangu kujiunga na kampuni
ile , haikuwa hivyo ndugu yangu, pale mbele ya kiti alikuweko bwana mmoja
unaweza kuhisi ni nani ? alikuwa ni mtu mfupi mweusi sana. Sikuwa na akili ya
samli kwani nilimtambua mara moja kuwa , Naye hakuwa boga kwani aliponitazama
tu alitabasamu Halafu alisema karibu afisa uhusiano kasha alinyoosha mkono
wake kutaka tusalimiane, nilikuwa
natetemeka naye alijua dhahiri, karibu kaa alisema bila shaka unajua shughuli
za kampuni yetu, kila saa na kila siku utakuwa unapambana na wateja wakorofi
unadhani utaweza kuwavumilia? Aliuliza nilijua alikuwa ananisanifu tu nilisema
ndiyo nitaweza
Halafu aliniuliza je ukiwa kazini
akatokea mtu mwenye gari alafu akjataka kukugonga kwa bahatri mbaya.. no tuseme
ukiwa kwenye daladala likatokea gari linguine likataka kuigonga ile daladala
utafanyaje? Nilinyamaza kwa muda kisha Nitamwacha dereva azungumze na mwenzake
wajue watakavyomalizana wenyewe’ kwa nini hiyo ilikushinda leo asubuhi? Badala
ya kuwa abiria ukawa dereva?
Nilitamani kuona jambo Fulani
linatokea ili mahojiano yale yaishe ni kweli jambo lile lilitokea Yule mkurugenzi ambaye ni Yule bwana
niliyemkashifu pale shekilango aliniomba ile barua ya ajira, aliichukua na
kuichanachana, halafgu aliniambia potea
nisikuone hapa ofisini hata mara moja, nilitaka kufanya jambo Fulani kama
kupambana naye ili nimfunze adabu jamaa
naona alijua aliinua simu kuita mlinzi nilitoka kwa haraka nikiwa nimeshukwa uso,”kweli aushikaye upanga
ataangamia kwa upanga” leo hii ndio nasema habari hizi kwani hata ndugu zangu
sikuwaambia sababu za kukosa kibarua kile
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni